Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja upendo wa Mungu. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja upendo wa Mungu. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote

12.31.2019

Tuna Bahati Kukutana na Kuja kwa Mungu


Latest Swahili Praise and Worship Song | "Tuna Bahati Kukutana na Kuja kwa Mungu" | Tenzi ya Rohoni


Tuna bahati kukutana na kuja kwa mungu, twaisikia sauti Yake.
Tuna bahati kukutana na kuja kwa mungu, tunahudhuria sikukuu ya Mwanakondoo.
Tunamjua Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaona matendo Yake ya ajabu.
Tunaelewa siri ya maisha ya mwanadamu, maneno ya Mwenyezi Mungu ni ya thamani zaidi.

12.26.2019

Watu wa Mungu ni nini? Watendaji huduma ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:


Mabikira watano wenye busara wanawakilisha wana Wangu na watu Wangu kati ya wanadamu ambao Niliumba. Kuwaita[a] “mabikira” ni kwa sababu ingawa wamezaliwa duniani, bado wanapatwa na Mimi; mtu anaweza kusema kwamba wamekuwa watakatifu, kwa hivyo wanaitwa “mabikira.” “Watano” liliotajwa awali linawakilisha idadi ya wana Wangu na watu Wangu ambao Nimewajaalia. “Mabikira watano wapumbavu” linarejelea watendaji huduma. Wananifanyia huduma bila kuweka kiwango kidogo zaidi cha umuhimu kwa maisha, wakifuatilia mambo ya nje pekee (kwa sababu hawana sifa Yangu, bila kujali kile wanachokifanya ni jambo la nje), na hawawezi kuwa wasaidizi Wangu wenye uwezo, kwa hiyo wanaitwa “mabikira wapumbavu.” “Watano” lililotajwa awali linamwakilisha Shetani, na wao kuitwa[b] “mabikira” kunamaanisha kwamba wameshindwa na Mimi na wanaweza kunifanyia huduma, lakini mtu wa aina hii si mtakatifu, kwa hivyo wanaitwa watendaji huduma.

12.19.2019

Tuna Bahati Kukutana na Kuja kwa Mungu

Latest Swahili Praise and Worship Song | "Tuna Bahati Kukutana na Kuja kwa Mungu" | Tenzi ya Rohoni

Tuna bahati kukutana na kuja kwa mungu, twaisikia sauti Yake.
Tuna bahati kukutana na kuja kwa mungu, tunahudhuria sikukuu ya Mwanakondoo.
Tunamjua Mwenyezi Mungu mwenye mwili, tunaona matendo Yake ya ajabu.

12.18.2019

Mungu huwaokoa watu gani? Yeye huwaondosha watu gani?

Maneno Husika ya Mungu:


Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa.

12.14.2019

Matendo maovu ni yapi? Maonyesho ya matendo maovu ni yapi?

Maneno Husika ya Mungu:


Ni kiwango kipi ambacho kulingana nacho matendo ya mtu yanatathminiwa kuwa mema au mabaya? Inategemea na iwapo katika fikira, maonyesho, na matendo yako, una ushuhuda wa kutia ukweli katika vitendo na wa kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli au la. Ikiwa huna uhalisi huu au huishi kwa kudhihirisha hili, basi bila shaka wewe ni mtenda maovu.

12.09.2019

Matendo mema ni nini? Maonyesho ya matendo mema ni yapi?

Maneno Husika ya Mungu:


Ukimiliki ukweli, unaweza kumfuata Mungu. Kama unaishi kwa kudhihirisha, unaweza kuwa onyesho la neno la Mungu. Kama unao uzima, unaweza kufurahia baraka ya Mungu. Ni wale tu walio na ukweli wanaweza kufurahia baraka ya Mungu. Mungu huhakikisha kwamba anawafidia wale wote wanaompenda kwa moyo wao wote pamoja na pia wanaovumilia magumu na mateso, na wala si kwa wale wanaojipenda tu na wamejipata kwenye mtego wa uwongo wa Shetani.

12.04.2019

Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu

Neno la Mungu | "Unapaswa Kuishi kwa Ajili ya Ukweli kwa Maana Unamwamini Mungu"

Mwenyezi Mungu anasema, "Kumwamini Mungu si rahisi jinsi mwanadamu anaweza kuona. Mungu anavyoona, ukiwa tu na ufahamu lakini huna neno Lake kama uhai; ikiwa wewe unazingatia tu maarifa yako mwenyewe lakini huwezi kutenda ukweli au kuishi kwa kudhihirisha neno la Mungu, basi hii ni dhihirisho kwamba huna moyo wa upendo kwa Mungu, na inaonyesha kwamba moyo wako si mali ya Mungu.

11.30.2019

Kuna tofauti zipi kati ya mabadiliko ya tabia na tabia nzuri?

Maneno Husika ya Mungu:

Mabadiliko katika tabia hasa huhusu mabadiliko katika asili ya watu. Mambo ya asili ya mtu hayawezi kuonekana kutoka kwa mienendo ya nje; yanahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuwepo kwao. Yanahusisha moja kwa moja maadili ya mtu katika maisha, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi yake, na kiini chake.

11.28.2019

Mabadiliko ya tabia hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:

Ikiwa tabia yako inaweza kubadilika au la inategemea na ikiwa unaweza kuendelea na maneno halisi ya Roho Mtakatifu au la na una ufahamu wa kweli. Hili ni tofauti na kile mlichoelewa awali. Kile ulichoelewa kuhusu mabadiliko katika tabia awali kilikuwa kwamba wewe, ambaye ni rahisi kuhukumu, kupitia kwa kufundishwa nidhamu na Mungu huzungumzi ovyo ovyo tena. Lakini hii ni hali moja tu ya mabadiliko, na hivi sasa suala muhimu zaidi ni kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu.

11.24.2019

Maskani Yangu Yako Wapi



Wazazi wa Wenya walitengana alipokuwa na umri wa miaka miwili, na baada ya hapo aliishi na baba yake na mama wa kambo. Mamake wa kambo hakuweza kumvumilia na daima alikuwa akibishana na baba yake.

11.09.2019

Kwa Ajili ya Nani Mtu Aishi



Kwa Ajili ya Nani Mtu Aishi

I
Haikuwa wazi ni kwa ajili ya nani mtu anapaswa kuishi. Sasa nina jibu kwa hilo.
Nilikuwa naishi tu kwa ajili yangu mwenyewe, kutafuta hadhi tu na umaarufu.
Maombi kwa Mungu yaliyojaa maneno mema, lakini nikishikilia njia zangu mwenyewe katika maisha halisi.
Imani juu ya msingi wa kesho na majaliwa, sina ukweli au uhalisi.
Mila na sheria, zikifungia imani yangu; sikubaki na kitu ila utupu.
Kushindwa kuishi kama binadamu, sistahili upendo wa Mungu kwa ajili yangu.

11.06.2019

Mwana wa Adamu Ameonekana



Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma


Kutoka Mashariki ya ulimwengu (Mashariki ... Mashariki ...),

mwale wa mwanga unatokea (mwanga ... mwanga ...),

ukiangaza njia yote kwenda magharibi.

Mwana wa Adamu ameshuka duniani.

11.01.2019

Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme



Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu


Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.

Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.

Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.

Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.

Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.

10.30.2019

Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu



I

Mwenyezi Mungu mwenye mwili

Anaonekana katika siku za mwisho Mashariki,

kama tu vile jua la haki likichomoza;

mwanadamu ameona mwanga wa kweli ukionekana.

Mungu wa haki na mwenye uadhama, mwenye upendo na huruma

Anajificha kwa unyenyekevu miongoni mwa wanadamu,

Akitoa ukweli, kuzungumza na kufanya kazi.

10.28.2019

Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu



 Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV

Mandhari iliyochorwa katika Biblia “Amri ya Mungu kwa Adamu”
ni ya kugusa na yenye kutia moyo.
Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,
uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao.

10.25.2019

Kuna tofauti zipi kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya pepo wabaya?

Maneno Husika ya Mungu:
Lazima uelewe ni mambo yapi yanatokana na Mungu ni mambo yapi yanatokana na Shetani. Mambo yanayotokana na Mungu hukusababisha kuwa wazi zaidi kuhusu maono, na hukusababisha kusogea karibu na karibu zaidi na Mungu, ukishiriki upendo na ndugu kwa bidii; unakuwa na uwezo wa kutilia maanani mzigo wa Mungu, na moyo wako umpendao Mungu haupungui; kuna njia mbele yako kuitembea.

10.24.2019

Kazi ya pepo wabaya ni nini? Kazi ya pepo wabaya hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia katindani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuwa na hali za kawaida mbele ya Mungu. Ambayo ni kusema, punde tu kuna kazi ya Shetani ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba.

10.22.2019

Kazi ya Roho Mtakatifu ni nini? Kazi ya Roho Mtakatifu hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu.

10.21.2019

Kuna tofauti ipi kati ya mtumishi mwema na mtumishi muovu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu.

10.20.2019

Kuna tofauti ipi kati ya ngano na magugu?


Maneno Husika ya Mungu:
Kama Nilivyosema, Shetani amewatuma wale ambao wananifanyia huduma kuukatiza usimamizi Wangu; hawa watendaji huduma ni magugu, lakini ngano hairejelei wazaliwa wa kwanza, lakini badala yake wana wote na watu ambao si wazaliwa wa kwanza. Siku zote ngano itakuwa ngano, siku zote magugu yatakuwa magugu; hii ina maana kwamba asili ya wale wa Shetni haiwezi kubadilika kamwe. Kwa hiyo, kwa ufupi, wao wanabaki kama Shetani. Ngano inamaanisha wana na watu, kwa sababu kabla ya kuumbwa ulimwengu Niliwaongezea watu hawa sifa Yangu.