10.25.2019

Kuna tofauti zipi kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya pepo wabaya?

Maneno Husika ya Mungu:
Lazima uelewe ni mambo yapi yanatokana na Mungu ni mambo yapi yanatokana na Shetani. Mambo yanayotokana na Mungu hukusababisha kuwa wazi zaidi kuhusu maono, na hukusababisha kusogea karibu na karibu zaidi na Mungu, ukishiriki upendo na ndugu kwa bidii; unakuwa na uwezo wa kutilia maanani mzigo wa Mungu, na moyo wako umpendao Mungu haupungui; kuna njia mbele yako kuitembea. Mambo ambayo hutokana na Shetani hukusababisha kupoteza maono na vyote ulivyokuwa navyo awali vimetoweka; unajitenga na Mungu, huna upendo kwa ndugu nawe una moyo wa chuki. Unakuwa mwenye kukata tamaa, hutaki tena kuishi maisha ya kanisa, na moyo wako umpendao Mungu hauko tena. Hii ni kazi ya Shetani na pia ni matokeo ambayo yameletwa na kazi ya roho mbaya.
kutoka katika “Sura ya 22” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu harudii kazi Yake, Hafanyi kazi ambayo si halisi, Hamtaki mwanadamu afanye mambo zaidi ya uwezo wake, na Hafanyi kazi ambayo inazidi akili ya mwanadamu. Kazi yote Anayofanya ipo ndani ya mawanda ya akili ya kawaida ya mwanadamu, na haizidi ufahamu wa ubinadamu wa kawaida, na kazi Yake ni kulingana na mahitaji ya kawaida ya mwanadamu. Ikiwa ni kazi ya Roho Mtakatifu, mwanadamu anakuwa wa kawaida zaidi, na ubinadamu wake unakuwa wa kawaida kabisa. Mwanadamu ana maarifa mengi ya tabia yake ya kishetani na iliyopotoka, na asili ya mwanadamu, na ana shauku kubwa ya kuuelewa ukweli. Hiyo ni kusema, maisha ya mwanadamu yanakua zaidi na zaidi, na tabia upotovu ya mwanadamu inakuwa na uwezo wa mabadiliko zaidi na zaidi—yote hiyo ni maana ya Mungu kuwa maisha ya mwanadamu. Kama njia haiwezi kufunua vitu hivyo ambavyo ni asili ya mwanadamu, haiwezi kubadilisha tabia ya mwanadamu, na, zaidi ya hayo, hauwezi kumleta mbele ya Mungu au kumpa ufahamu wa kweli juu ya Mungu, na hata kufanya ubinadamu wake kuwa duni zaidi na hisia zake kuwa si za kawaida zaidi, basi njia hii itakuwa si njia ya kweli, na inaweza kuwa ni kazi ya roho mchafu, au njia ya zamani. Kwa ufupi, haiwezi kuwa kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu.
kutoka katika “Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuhusu kuwasaidia watu kupata faida; ni kuwaadilisha watu; hakuna kazi ambayo haiwanufaishi watu. Haijalishi kama ukweli ni wa kina au usio wa kina, na haijalishi tabia ya wale wanaopokea ukweli huo ilivyo, chochote ambacho Roho Mtakatifu anafanya, yote hayo huwanufaisha watu.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu. Wakati watu wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndani yao ni watakatifu hasa. Wale ambao wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu huishi kwa kudhihirisha upendo wa Mungu, upendo wa kaka na dada zao, na kufurahia vitu ambavyo Mungu hufurahia na kuchukia vitu ambavyo Mungu huchukia. Watu ambao wanaguswa na kazi ya Roho Mtakatifu wana ubinadamu wa kawaida, na wanamiliki ubinadamu na daima hufuatilia ukweli. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani ya watu, hali zao huwa nzuri zaidi na zaidi, na ubinadamu wao unakuwa wa kawaida zaidi na zaidi, na ingawa ushirikiano wao mwingine unaweza kuwa mpumbavu, motisha zao ziko sahihi, kuingia kwao ni kwa hali nzuri, hawajaribu kukatiza, na hakuna nia mbaya ndani yao. Kazi ya Roho Mtakatifu ni ya kawaida na ya kweli, Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa mwanadamu kulingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na Yeye huwapa nuru na kuongoza watu kulingana na ufuatiliaji halisi wa watu wa kawaida. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi kwa watu, Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kulingana na mahitaji ya watu wa kawaida, Anawakimu kwa msingi wa mahitaji yao, na Yeye huwaongoza na kuwapa nuru kwa hali nzuri kwa msingi wa kile ambacho wanakosa, na kwa upungufu wao; wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, kazi hii inalingana na amri za maisha ya kawaida ya mwanadamu, na ni katika maisha halisi pekee ndio watu wanaweza kuona kazi ya Roho Mtakatifu. Iwapo, katika maisha yao ya kila siku, watu wako katika hali nzuri na wana maisha ya kawaida ya kiroho, basi wanamiliki kazi ya Roho Mtakatifu. Katika hali kama hiyo, wakati wanakula na kunywa maneno ya Mungu wana imani, wakati wanaomba wanatiwa moyo, wakati kitu kinawafanyikia wao si baridi, na wakati kinawafanyikia wanaweza kuona masomo ambayo Mungu anawahitaji kujifunza, na hawako baridi, ama dhaifu, na ingawa wana ugumu wa kweli, wako tayari kukubali mipango yote ya Mungu.
…………
Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia katindani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuwa na hali za kawaida mbele ya Mungu. Ambayo ni kusema, punde tu kuna kazi ya Shetani ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba. Kazi ya roho waovu huharibu uhusiano wa kawaida kati ya mwanadamu na Mungu, na huvuruga maono ya awali ya watu na njia ambayo maisha yao yameingia, katika mioyo yao hawawezi kamwe kumkaribia Mungu, daima mambo hufanyika ambayo huwasababishia vurugu na kuwatia pingu, na mioyo yao haiwezi kupata amani, kuacha upendo wao wa Mungu bila nguvu, na kuwafanya kusononeka. Hayo ndiyo maonyesho ya kazi ya Shetani. Kazi ya Shetani inadhihirishwa katika yafuatayo: kutoweza kushikilia msimamo na kuwa na ushuhuda, kukusababisha kuwa mtu ambaye ana makosa mbele ya Mungu, na ambaye hana uaminifu kwa Mungu. Kwa kuingilia kwa Shetani, unapoteza upendo na uaminifu kwa Mungu ndani yako, unaondolewa uhusiano wa kawaida na Mungu, hufuatilii ukweli, ama kujiendeleza, unarudi nyuma, na kuwa baridi, unajipendeza, unaachia uenezaji wa dhambi, na huchukii dhambi; zaidi ya hayo, kuingilia kwa Shetani kunakufanya mpotovu, kunasababisha mguso wa Mungu kutoweka ndani yako, na kunakufanya kulalamika kuhusu Mungu na kumpinga Yeye, kukufanya uwe na shaka na Mungu, na hata kuna hatari ya wewe kumwacha Mungu. Hii yote ni kazi ya Shetani.
kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anafanya kazi kwa njia ya upole, upendo, laini na ya kujali, kwa njia hasa iliyopimwa na ni sahihi. Njia Yake haikufanyi kuhisi hisia kali kama vile, “Mungu lazima aniache nifanye hivi” ama “Lazima Mungu aniache nifanye vile.” Mungu kamwe hakupi mawazo makali ya aina hiyo ama hisia kali zinazofanya mambo kutovumilika. Sivyo? Hata unapoyakubali maneno ya Mungu ya hukumu na kuadibu, unahisi vipi basi? Unapohisi mamlaka ya Mungu na nguvu ya Mungu, unahisi vipi basi? Unahisi kwamba Mungu ni mtakatifu na asiyekosewa? (Ndiyo.) Unahisi ukiwa mbali na Mungu nyakati hizi? Unahisi unamwogopa Mungu? (La.) La, badala yake, unahisi heshima inayomcha Mungu. Je, watu wanahisi haya mambo yote kwa sababu tu ya kazi ya Mungu? …
… Inapokuja kwa kazi ya Shetani kwa mwanadamu, hapa Nina maneno mawili yanayoweza kuelezea vizuri asili yenye nia mbaya na ovu ya Shetani, yanayoweza kuwaruhusu kujua chuki ya Shetani: Katika mtazamo wa Shetani kwa mwanadamu, daima anataka kumiliki na kumtawala kwa nguvu, kila mmoja wao, ili aweze kufika mahali ambapo anaweza kumdhibiti mwanadamu kabisa, kumdhuru mwanadamu, ili aweze kutimiza lengo hili na tamaa isiyowezekana. “Umiliki wa nguvu” unamaanisha nini? Unafanyika na kibali chako, ama bila kibali chako? Unafanyika na kujua kwako, ama bila kujua kwako? Ni bila kujua kwako kabisa! Katika hali ambazo huna ufahamu, pengine wakati hajasema chochote ama pengine wakati hajafanya chochote, wakati hakuna kauli kigezo, hakuna muktadha, yuko hapo karibu nawe, akikuzunguka. Anatafuta fursa ya kukunyonya, kisha anakumiliki kwa nguvu, anakutawala, akitimiza lengo lake la kukudhibiti kikamilifu na kukudhuru. Hii ni nia na tabia ya kawaida zaidi katika mapambano ya Shetani dhidi ya Mungu kwa ajili ya mwanadamu.
kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine husema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao nyakati zote. Hili haliwezekani. Ikiwa wangesema kwamba Roho Mtakatifu yuko nao kila mara, hilo lingekuwa la kweli. Ikiwa wangesema kwamba fikira na hisi zao ni za kawaida nyakati zote, hilo pia lingekuwa la kweli, na lingeonyesha kwamba Roho Mtakatifu yuko nao. Ikiwa wanasema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao kila mara, kwamba wanapata nuru kutoka kwa Mungu na kuguswa na Roho Mtakatifu kila wakati, na wanapata ufahamu mpya kila wakati, basi hili si la kawaida. Ni la rohoni kabisa! Bila tashwishi yoyote, watu kama hao ni pepo wabaya! Hata wakati ambapo Roho wa Mungu huja ndani ya mwili, kuna nyakati ambapo lazima Ale, na lazima Apumzike—sembuse mwanadamu. Wale ambao wamemilikiwa na pepo wabaya huonekana kutokuwa na hisia na udhaifu wa mwili. Wanaweza kutelekeza na kuacha kila kitu, wao ni wenye uwezo wa kustahimili mateso na hawahisi uchovu hata kidogo sana, kana kwamba wamevuka mipaka ya mwili. Je, hili silo la rohoni kabisa? Kazi ya pepo mwovu ni ya rohoni, na mambo haya ni yasiyofikiwa na mwanadamu. Wale wasioweza kutofautisha huwa na wivu wanapoona watu kama hao, na husema kwamba imani yao katika Mungu ni thabiti sana, na wana imani kubwa, na kwamba wao huwa si wadhaifu kamwe. Kwa kweli, hili ni dhihirisho la kazi ya pepo mwovu. Hiyo ni kwa sababu watu wa kawaida huwa na udhaifu wa binadamu usioepukika; hii ni hali ya kawaida ya wale walio na kuwepo kwa Roho Mtakatifu.
kutoka katika “Utendaji (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Baadhi ya utofauti mwingine waziwazi kati ya kazi mbalimbali za pepo wabaya na kazi ya Roho Mtakatifu, na namna ambavyo zinaonyeshwa kwa njia mahususi. Roho Mtakatifu huwachagua watu wanaofuatilia ukweli, na walio na dhamiri na mwelekeo, na wanaomiliki uadilifu. Hawa ndio aina ya watu ambao Roho Mtakatifu hufanya kazi ndani yao. Pepo wabaya huchagua watu ambao ni wajanja na wa kipuuzi, wasiopenda ukweli, na wasio na dhamiri wala mwelekeo. Watu kama hao ndio pepo wabaya hufanya kazi ndani yao. Ni nini tunachoona tunapolinganisha wale waliochaguliwa kwa kazi ya Roho Mtakatifu, na wale waliochaguliwa kwa kazi ile ya pepo wabaya? Tunaweza kuona kwamba Mungu ni mtakatifu, na mwenye haki, kwamba wale wanaochaguliwa na Mungu huutafuta ukweli, na wanayo dhamiri na mwelekeo, kwamba wanao uadilifu na wanapenda kile ambacho ni haki. Wale wanaochaguliwa na pepo wabaya ni wajanja, ni wachoyo na wenye dharau, hawaupendi ukweli, hawana dhamiri na mwelekeo, na hawautafuti ukweli. Pepo wabaya huchagua tu mambo mabaya na wale watu ambao si wa kweli, ambapo tunaona ya kwamba pepo wabaya wanapenda uovu na giza, kwamba wanawakimbia wale wanaoutafuta ukweli, na ni wepesi wa kuwamiliki wale ambao wako kombo na ni wajanja, wale ambao wanavutiwa na udhalimu, na wanaorogwa kwa urahisi. Wale ambao pepo wabaya huchagua kufanyia kazi ndani yao hawawezi kuokolewa, na wanaondolewa na Mungu. Ni lini, na ni katika mazingira gani, ndipo pepo wabaya hufanya kazi? Wao hufanya kazi wakati watu wamesonga mbali na Mungu na kuasi dhidi ya Mungu. Kazi ya pepo wabaya huwaroga watu, na hufanya hivyo kwa kuchukua fursa ile wanapotenda dhambi. Wakati watu wako katika hali yao dhaifu zaidi, hasa wanapokuwa katika maumivu makuu ndani ya mioyo yao, wakati wanapohisi vibaya na wakiwa wamechanganyikiwa, pepo mbaya huchukua fursa hii kujiingiza ndani polepole ili kuwaroga na kuwapotosha, kuleta kutoelewana kati yao na Mungu. Kunao wakati wa kazi ya Roho Mtakatifu: Wakati watu wanapomwita Mungu, wakati mioyo yao inapomgeukia Mungu, wanapomhitaji Mungu, wanapotubu kwa Mungu, na wanapoutafuta ukweli, basi ndipo Roho Mtakatifu huanza kufanya kazi ndani yao. Tazama namna ambavyo kila dhana ya kazi ya Roho Mtakatifu ilivyo ili kumwokoa mwanadamu, namna Anavyotafuta fursa za kumwokoa mwanadamu, ilhali pepo wabaya hutafuta fursa za kuwapotosha na kuwalaghai watu. Pepo wabaya wanayo dharau na ni waovu, ni wenye kudhuru kwa siri na wabaya, kila kitu wanachofanya kinalenga katika kumteketeza na kumpotosha mwanadamu, na kile tu ambacho Roho Mtakatifu hufanya ni kwa upendo na wokovu wa mwanadamu. Athari ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuwatakasa watu, kuwaokoa dhidi ya kupotoka kwao, kuwaruhusu kujijua na kumjua Shetani, kuweza kuasi dhidi ya Shetani, kuweza kuufuatilia ukweli, na hatimaye kuishi kwa kudhihirisha mfanano wa mwanadamu. Pepo wabaya hupotosha, hutia najisi, na kuwafunga watu, huwaweka ndani zaidi ya dhambi, na kuwasababishia maumivu makubwa zaidi katika maisha yao, na hivyo wakati pepo wabaya wanapofanya kazi ndani ya watu, watu hao wamo hatarini; hatimaye, wanateketezwa na Shetani, jambo ambalo ni matokeo ya kazi ya pepo wabaya. Athari ya kazi ya Roho Mtakatifu ni kuweza hatimaye kuwaokoa watu, kuwafanya kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kuwa huru na kukombolewa kabisa, na kupokea baraka za Mungu. Pepo wabaya humweka mwanadamu katika giza, humpeleka kwenye shimo la kuzimu; Roho Mtakatifu humchukua mwanadamu kutoka kwenye giza, na kumpeleka kwenye mwangaza, na hadi kwenye uhuru. Kazi ya Roho Mtakatifu huwapa watu nuru na kuwaongoza watu, Huwapa fursa mbalimbali, na wanapokuwa wanyonge na dhambi Yeye huwapa faraja. Huwaruhusu watu kujijua, huwaruhusu kuufuatilia ukweli, na Halazimishi watu kufanya mambo, lakini Huwaacha kujichagulia njia yao wao wenyewe, na hatimaye Huwapeleka kwenye mwangaza. Pepo wabaya huwalazimisha watu kufanya mambo na kuwaamrisha hapa na pale. Kila kitu wanachosema ni uongo na kinawaroga watu, kuwadanganya na kuwafunga; pepo wabaya hawawapatii watu uhuru, hawawaruhusu kuchagua, huwalazimisha kufuata barabara ya maangamio, na hatimaye kuwaingiza ndani ya dhambi zaidi na zaidi, na kuwasababishia kifo.
kutoka katika “Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha II


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni