1.26.2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Biblia

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee V

Utakatifu wa Mungu (II)

Habari za jioni kila mtu! (Habari ya jioni Mwenyezi Mungu!) Leo, kaka na dada, hebu tuimbe wimbo. Tafuta mmoja ambao mnapenda na ambao mmeimba mara nyingi kabla. (Tungependa kuimba wimbo wa neno la Mungu “Upendo Safi Bila dosari.”)
Kiitikio: “Upendo” unarejelea hisia safi bila dosari, ambapo mnatumia mioyo yenu kupenda, kuhisi, na kuwa wa kufikiri. Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, hakuna mpango, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna chaguo na hakuna chochote kichafu.
1. Iwapo mna upendo kama huo, basi hamdanganyi, hamlalamiki, hamsaliti, hamuasi, hamchukui, ama kuuliza kupokea chochote ama idadi fulani. Iwapo mnapenda, basi mnatoa kwa furaha.
2. Iwapo mna upendo kama huo, basi mnavumilia magumu, na kushirikiana na Mungu. Mnaweza kupeana vyote mlivyo navyo kwa sababu ya Mungu: familia zenu, siku zenu za baadaye, ujana wenu, na ndoa zenu. Vinginevyo, upendo wenu si upendo hata kidogo, lakini ni udanganyifu na usaliti!
Huu ulikuwa wimbo mzuri kuchagua. Mnapenda kuimba wimbo huu? (Ndiyo.) Mnahisi nini baada ya kuimba wimbo huu? Mnaweza kuhisi upendo wa aina hii ndani yenu? (Siyo vile bado.) Ni maneno gani kutoka ndani ya wimbo huu yanakugusa kwa kina? (Haya ni: Katika upendo hakuna masharti, hakuna vizuizi, na hakuna umbali. Katika upendo hakuna tuhuma, hakuna udanganyifu, hakuna mpango, na hakuna ujanja. Katika upendo hakuna chaguo na hakuna chochote kichafu. Lakini ndani yangu bado naona uchafu na pia naona wapi najaribu kufanya mipango na Mungu, maeneo niliyo na upungufu, kwa hivyo ninapofikiria kuhusu mimi leo kwa kweli sijafikia aina ya upendo ulio safi na bila dosari. ) Kama hujafikia aina ya upendo ambao ni safi na bila dosari, una upendo wa aina gani? Una kiwango kipi cha upendo ndani yako? (Niko tu katika hatua ambapo niko tayari kutafuta na nina hamu.) Kulingana na kimo chako mwenyewe na kutumia maneno yako mwenyewe kutoka kwa uzoefu wako mwenyewe, umefikia kiwango kipi? Je, una udanganyifu, una malalamiko? (Ndiyo.) Je, una madai ndani ya moyo wako, kuna vitu ambavyo unataka na kutamani kutoka kwa Mungu? (Ndiyo, kuna hivi vitu vilivyo na doa.) Vinajitokeza katika hali gani? (Wakati hali ambayo Mungu amenipangia hailingani na fikira zangu ya vile inapaswa kuwa, ama wakati matakwa yangu hayajatimizwa, nitaonyesha aina hii ya tabia potovu.) Nyinyi huimba wimbo huu mara nyingi? Mnaweza kujadili vile mnaelewa “upendo safi bila dosari”? Na mbona Mungu anafafanua upendo namna hii? (Naupenda wimbo huu sana mimi mwenyewe kwa sababu kwa kweli naweza kuona kwamba upendo huu ni upendo kamili. Hata hivyo, nahisi umbali kiasi na kiwango hicho. Sasa niko tu katika hatua ambapo niko tayari kutoa mambo fulani na kuvumilia baadhi ya gharama katika kufuatilia ukweli, lakini punde tu kitu kinaathiri siku zangu za usoni na kudura yangu, ninahisi kuchanganyikiwa ndani yangu. Naona kwamba ndani yangu nina imani kidogo kwa Mungu.) (Sasa nahisi kwamba bado niko mbali sana kufikia upendo wa kweli, lakini kuna baadhi ya maeneo ambapo nimeweza kuendelea mbele kuufikia, njia moja nafanya hivi ni kupitia nguvu ambayo maneno ya Mungu yananipatia na njia nyingine ni kwamba katika hali hizi nashiriki na Mungu kupitia maombi. Hata hivyo, inapohusiana maoni yangu ya uwepo, nahisi kwamba wakati mwingine siwezi kuyashinda.) Umewahi kufikiria kuhusu vitu ambavyo vinaweza kuwa vinakuzuia nyakati hizo huwezi kuyashinda? Umewahi kuchunguza maswala haya? (Ndiyo, nimekuwa nikichunguza na kwa sehemu kubwa ni kiburi changu na majivuno na pia matarajio yangu ya siku zangu za baadaye na kudura yangu ambavyo ni kizuizi kikubwa.) Wakati matarajio ya siku zako za baadaye na kudura ni kizuizi kikubwa, umewahi kufikiria kuhusu mbona ni kizuizi kikubwa? Ni vipi siku za baadaye na kudura vinaweza kuwa kizuizi? Unataka nini kutoka kwa siku zako za baadaye na kudura yako? (Siko wazi sana katika suala hili, wakati mwingine najipata katika hali ambapo nahisi sina siku za baadaye na kudura ama wakati mwingine nahisi hata kwamba sina hatima kwa kile ambacho Mungu amenifichulia. Katika nyakati hizi nahisi mnyonge sana na nahisi kwamba hii imekuwa kizuizi kikubwa kwa mimi mwenyewe. Hata hivyo, baada ya kipindi cha uzoefu na kupitia maombi, hali inaweza kugeuka, lakini bado nahisi mara nyingi kusumbuliwa na suala hili.) Unarejelea nini kwa kweli unaposema “siku za baadaye na kudura”? (Inamaanisha kwamba wakati Mungu amenipangia baadhi ya hali, nahisi kuwa mbali sana na mahitaji Yake. Wakati mwingine nastaajabu iwapo Mungu ananifichua ama la na nahisi kwamba sina kudura ama hatima, na nahisi mnyonge sana.) Mnarejelea nini mnaposema “siku za baadaye na kudura”? Kuna kitu mnachoweza kuashiria? Ni picha ama kitu mlichofikiria ama ni kitu mnaweza kweli kuona? Ni kitu halisi? (Ni hatima.) Hatima ni nini? Siku zako za baadaye ni nini? Katika kila mioyo yenu mnapaswa kufikiri, wasiwasi mlio nayo katika mioyo yenu kuhusu siku zenu za baadaye na kudura zenu inarejelea nini? (Ni kuokolewa na kusalimika, na matumaini ya kufaa polepole ili kutumiwa na Mungu na kutekeleza wajibu wangu hadi katika kiwango cha juu kupitia njia ya kufanya wajibu wangu. Vitu hivi mara nyingi vinafichuliwa na Mungu, na nahisi kwamba nina upungufu.) Kaka na dada wengine wanapaswa kujadili, unaelewaje “upendo safi bila dosari”? (Hakuna chochote kichafu kutoka kwa mtu binafsi na hadhibitiwi na siku zake za baadaye na kudura zao. Licha ya vile Mungu anamtunza, anaweza kutii kikamilifu kazi ya Mungu, na pia kutii mipango ya Mungu na kumfuata Yeye hadi mwisho kabisa. Upendo wa aina hii tu kwa Mungu ni upendo safi bila dosari. Ni wakati tu ninapojilinganisha na hilo ndipo ninapogundua kwamba katika miaka michache ambayo nimemwamini Mungu, nimeweza, juujuu, kutoa vitu fulani ama kuvumilia baadhi ya gharama, lakini sijawahi kuweza kweli kumpa Mungu moyo wangu. Wakati Mungu ananifichua, nahisi kana kwamba nimeainishwa kama mtu ambaye hawezi kuokolewa, na nakaa katika hali hizo hasi. Najiona nikifanya wajibu wangu, lakini wakati huo huo nikijaribu kutekeleza mipango na Mungu, na kutoweza kumpenda Mungu kwa moyo wangu wote, na kwamba hatima yangu, siku zangu za baadaye, na kudura yangu yote daima yako kwa akili yangu. Nakumbuka ushirika wa mwanadamu ulisema wakati mmoja kwamba tunapaswa kulipisha upendo wa Mungu kwa kutekeleza wajibu wetu, kwamba upendo lazima uonyeshwe kwa kweli, na sio tu maneno matupu. Kwa kulinganisha nahisi mbali sana na upendo huu.)
Inaonekana kwamba mmeimba wimbo huu mara nyingi na mna baadhi ya uelewa kuuhusu na kwamba kuna uhusiano fulani na uzoefu wako halisi. Hata hivyo, karibu kila mtu ana viwango tofauti vya kukubali kila kirai katika wimbo “Upendo Safi bila Dosari.” Watu wengine wako radhi, watu wengine wanatafuta kuweka kando siku zao za baadaye, watu wengine wanatafuta kuweka kando familia zao, watu wengine hawatafuti kupokea chochote. Bado wengine wanajihitaji kuwa bila udanganyifu, bila malalamiko, na kutoasi dhidi ya Mungu. Kwa nini Mungu angetaka kupendekeza aina hii ya upendo na kuhitaji kwamba watu wampende namna hii? Hii ni aina ya upendo ambao watu wanaweza kuufikia? Hiyo ni kusema, watu wanaweza kupenda namna hii? Watu wanaweza kuona kwamba hawawezi, kwa sababu hawamiliki kamwe upendo wa aina hii, na wakati hawaumiliki, na kimsingi hawajui kuhusu upendo, Mungu anazungumza maneno haya, ambayo ni mageni kwao. Kwa sababu watu wanaishi katika dunia hii, wanaishi katika tabia yao potovu, iwapo watu wangekuwa na aina hii ya upendo ama iwapo mtu angeweza kumiliki aina hii ya upendo, bila kuwa na maombi na madai, kuwa radhi kujitoa wenyewe na kuwa radhi kustahimili mateso na kuacha vyote vilivyo vyao, mtu anayemiliki aina hii ya upendo angewezaje kuonekana katika macho ya watu wengine? Si angekuwa mtu kamili? (Ndiyo.) Mtu kamili kama huyo yupo katika dunia hii? Hayupo, yupo? Mtu wa aina hii hayupo kabisa katika dunia hii, ila angeweza kuishi katika utupu, siyo? Hivyo, watu wengine—kupitia uzoefu wao—wanatumia juhudi nyingi kuwa kama kile ambacho maneno haya yalielezea. Wanajishughulikia, wanajizuia, na hata daima wanajitupa: Wanastahimili mateso na wanaacha dhana ambazo si sahihi walizokuwa nazo. Wanaacha njia walivyokuwa wakiasi Mungu, wanaacha tamaa zao na matakwa. Lakini mwishowe bado hawawezi kufikia mahitaji hayo. Kwa nini hayo yanafanyika? Mungu anasema mambo haya ili kupeana kiwango cha watu kufuata, ili watu wajue kiwango wanachodaiwa na Mungu. Lakini Mungu huwahi kusema kwamba watu lazima wafikie hiki mara moja? Je, Mungu huwahi kusema ni katika wakati upi watu wanapaswa kufikia hiki? (La.) Je, Mungu huwahi kusema kwamba watu lazima wampende namna hii? Kifungu hiki kinasema hivi? La, hakisemi hivi. Mungu anawaambia watu tu kuhusu “upendo” Aliokuwa akirejelea. Kuhusiana na watu kuweza kumpenda Mungu namna hii na kumtendea Mungu namna hii, mahitaji ya Mungu ni yapi? Si muhimu kuyafikia mara moja, ama papo hapo kwa sababu watu hawawezi kufanya hivyo. Mmewahi kufikiria kuhusu masharti ambayo watu wanapaswa kutimiza ili kupenda namna hii? Iwapo watu wangeyasoma maneno haya mara nyingi watakuwa na upendo huu polepole? (La.) Masharti ni yapi basi? Kwanza, watu wanawezaje kuwa huru kutokana na tuhuma kumhusu Mungu? (Ni watu waaminifu tu wanaoweza kufikia jambo hilo.) Je, kuwa huru kutokana na udanganyifu? (Pia wanapaswa kuwa watu waaminifu.) Kuwa mmoja asiyetaka kufanya mipango na Mungu? Huyo pia lazima awe mtu mwaminifu, Je, kutokuwa na ujanja? Kunarejelea nini kusema hakuna chaguo katika upendo? Yote yanarejelea kuwa mtu mwaminifu? Kuna maelezo mengi hapo; uwezo wa Mungu kutaja upendo wa aina hii ama uwezo wa Mungu kufafanua aina hii ya upendo, kuisema namna hii, hii inathibitisha nini? Tunaweza kusema kwamba Mungu anamiliki upendo wa aina hii? (Ndiyo.) Mnaona hii wapi? (Kwa upendo Mungu alio nao kwa mwanadamu.) Upendo wa Mungu kwa mwanadamu una sharti? (La.) Kuna vizuizi ama umbali kati ya Mungu na mwanadamu? (La.) Mungu ana tuhuma kumhusu mwanadamu? (La.) Mungu humwangalia mwanadamu, humwelewa mwanadamu, siyo? (Ndiyo.) Mm, kwa kweli anamwelewa mwanadamu. Je, Mungu ni mdanganyifu kwa mwanadamu? (La.) Kwa sababu Mungu anaongea kikamilifu kuhusu upendo huu, moyo Wake ama kiini Chake kinaweza kuwa kamili sana? Watu wamewahi kufafanua upendo kwa njia hii? (La.) Mwanadamu amefafanua upendo katika hali gani? Mwanadamu anazungumza vipi kuhusu upendo? Si ni kupeana ama kutoa? (Ndiyo.) Ufafanuzi wa mwanadamu wa upendo ni rahisi, na hauna kiini.
Ufafanuzi wa Mungu wa upendo na namna Mungu anazungumza kuhusu upendo inahusiana na kipengele cha kiini Chake, lakini kipengele kipi cha kiini Chake? Wakati uliopita Tulishiriki kuhusu mada muhimu sana, ni mada ambayo watu wamezungumzia mara nyingi na kutaja awali, na ni neno ambalo linatajwa mara nyingi katika kipindi cha kumwamini Mungu, lakini ni neno linalojulikana na pia ni geni kwa watu, lakini mbona hivyo? Ni neno linalotoka kwa lugha za mwanadamu, miongoni mwa mwanadamu ufafanuzi wake ni dhahiri na pia ni usio dhahiri, lakini neno hili ni nini? (Utakatifu.) Naam, utakatifu: hiyo ilikuwa mada ya wakati uliopita tuliposhiriki. Tulishiriki kiasi kuhusu mada hii, lakini kushiriki kwetu hakukuwa kamili. Kulingana na sehemu tuliyoshiriki wakati uliopita, kila mtu alipata uelewa mpya kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Mnafikiri uelewa mpya ulikuwa nini? Yaani, nini katika uelewa huo ama maneno hayo yaliwafanya kuhisi kwamba uelewa wenu wa utakatifu wa Mungu ulikuwa tofauti ama uliobadilishwa na kile Nilichoshiriki kuhusu utakatifu wa Mungu? Je, mnakumbuka? Je, uliacha maono? (Mungu anasema Anachohisi katika moyo Wake; ni safi. Hiki ni kipengele kimoja cha utakatifu.) Hii ni sehemu moja yake, kuna chochote kingine cha kuongezea? (Kuna utakatifu wakati Mungu ana ghadhabu kwa mwanadamu, hakuna dosari.) (Naona katika mamlaka ya Mungu ukamilifu Wake, uaminifu Wake, hekima Yake na utawala Wake juu ya vitu vyote. Naelewa mambohaya.) “Utawala juu ya vitu vyote,” ambao ni kuhusu mamlaka ya Mungu, sasa tunazungumza kuhusu utakatifu wa Mungu. (Kuhusu utakatifu wa Mungu, naelewa kwamba kuna ghadhabu ya Mungu na huruma ya Mungu katika tabia Yake ya haki, hili liliacha maono yenye nguvu kwangu. Pia lilileta fikira kwamba tabia ya Mungu ya haki ni ya kipekee, ambayo zamani sikuwa na uelewa kama huo wa ama ufafanuzi kama huo wake. Lakini katika ushirika Wako Ulijadili kwamba ghadhabu ya Mungu ni tofauti na hasira ya mwanadamu. Ni kitu ambacho hakuna kiumbe anamiliki. Ghadhabu ya Mungu ni kitu chema na kina kanuni; inatolewa kwa sababu ya kiini kiasilia cha Mungu. Ni kwa sababu Anaona kitu hasi na hivyo Mungu anaachilia ghadhabu Yake. Katika huruma ya Mungu, pia naona kwamba ni kitu ambacho hakuna kiumbe anamiliki. Ingawa mwanadamu ana matendo mazuri ama vitendo vya haki ambavyo vinachukuliwa kuwa sawa na huruma, ni vichafu na kuna nia nyuma yavyo. Aina zingine zinazoitwa huruma hata ni bandia na tupu. Lakini nimeuona wokovu wa Mungu wakati anaonyesha huruma kwa watu, na huruma hii inamweka mwanadamu moja kwa moja kwa njia ya kuokolewa. Inawaweka watu kwa njia sahihi ya kumwamini Mungu ili wapokee hatima na matumaini yao mazuri. Kwa hivyo huruma ya Mungu inamilikiwa na kiini Chake. Kwa hivyo, hata ingawa Mungu angeharibu mji kwa sababu ya ghadhabu Yake, kwa sababu ana kiini cha huruma, Angeweza kwa wakati wowote ama pahali popote kuonyesha huruma kuwaokoa na kuwalinda watu wa mji huo. Huu ni uelewa wangu.) Una baadhi ya uelewa kuhusu tabia ya haki ya Mungu.
Wakati Niliwauliza baadhi ya maswali sasa hivi, wengi wenu walitambua kwamba upendo wa Mungu ni mkubwa sana na halisi sana, lakini hamna maarifa ya kiini takatifu cha Mungu. Kuhusu mada yetu ya sasa, Nitazungumzia eneo hili, ambalo ni maarifa ya utakatifu wa Mungu. Mara nyingi watu huhusisha tabia ya haki ya Mungu na utakatifu Wake na wote wanajua na wamesikia maelezo fulani kuhusu tabia Yake ya haki. Zaidi, watu wengi mara nyingi wanachanganya utakatifu wa Mungu na tabia ya haki katika ushirika wao, wakisema kwamba tabia ya Mungu ya haki ni takatifu. Kila mtu anajua neno “takatifu” na ni neno linalotumika sana, lakini kuhusiana na kidokezo cha neno hilo, maonyesho gani ya utakatifu wa Mungu ambayo watu wanaweza kuona? Ni nini Mungu amefichua ambacho watu wanaweza kutambua? Ninahofia kwamba hiki ni kitu ambacho hakuna anayejua. Tunasema kwamba tabia ya Mungu ni ya haki, lakini basi ukichukua tabia ya haki ya Mungu na kuisema kuwa takatifu, hiyo inaonekana isiyo dhahiri kiasi, ya kuchanganya kiasi; mbona hivi? Unasema tabia ya Mungu ni ya haki, ama unasema tabia Yake ya haki ni takatifu, hivyo katika mioyo yenu mnauainisha utakatifu wa Mungu vipi? Mnauelewa vipi? Hivyo ni kusema, ni nini Mungu amefichua ama ni nini kuhusu kile Mungu anacho na maana Yake ambacho watu wanaweza kutambua kama takatifu? Umefikiria hili hapo awali? Kile Nilichoona ni kwamba watu mara nyingi husema maneno yanayotumika sana ama wana virai ambavyo vimesemwa mara kwa mara, lakini hawajui wanachosema. Hivi tu ni vile kila mtu anavyosema, na wanasema hivi mara nyingi, hivyo inakuwa kirai kilichowekwa. Hata hivyo, iwapo wangechunguza na kutafiti kwa kina maelezo, wangepata kwamba hawajui maana halisi ni nini ama inachorejelea. Kama tu neno “takatifu,” hakuna anayejua kabisa ni kipengele kipi cha kiini cha Mungu kinarejelewa kuhusiana na utakatifu Wake. Kuhusu kupatanisha neno “takatifu” na Mungu, hakuna anayejua na mioyo ya watu imechanganyikiwa, na ni pana jinsi wanavyotambua Mungu ni mtakatifu. Lakini unapoichunguza, Mungu ni mtakatifu vipi? Kuna anayejua? Nahofia hakuna aliye wazi kabisa kuhusu suala hili. Leo tutashiriki kuhusu mada kupatanisha neno “takatifu” na Mungu ili watu waweze kuona maudhui ya kweli ya kiini cha utakatifu wa Mungu, na hili litazuia watu wengine kulitumia neno hilo kimazoea ovyo ovyo na kusema vitu kwa nasibu wakati hawajui maana yake, ama hata kama wako sawa na sahihi ama la. Watu daima wameisema hivi: umeisema, nimeisema, na imekuwa jinsi ya kuongea na watu hivyo wameliharibu neno “takatifu” bila kusudi.
Kuhusu neno “takatifu,” juujuu linaonekana rahisi sana kuelewa, siyo? Kwa kiwango cha chini kabisa watu wanaamini neno “takatifu” linamaanisha nadhifu, isiyo na doa, tukufu, na safi, kama tu katika wimbo tulioimba karibuni “Upendo Safi Bila dosari,” ambapo “takatifu” na “upendo” yamewekwa pamoja, ambayo ni sahihi; hii ni sehemu yake, upendo wa Mungu ni sehemu ya kiini Chake, lakini si kiini chote. Hata hivyo, katika mitazamo ya watu, wanaona neno na kulishirikisha na vitu ambavyo wao wenyewe wanaviona kuwa nadhifu na safi, ama na vitu ambavyo wao binafsi wanafikiri havina doa wala havina dosari. Kwa mfano, watu wengine husema kwamba ua la yungiyungi ni safi, ni vipi watu walikuja kufafanua ua la yungiyungi kwa njia hii? (“Ua la yungiyungi linamea kwa matope lakini linatoa maua bila dosari.”) Linatoa maua bila dosari kutoka kwa maji machafu, hivyo watu wakaanza kutumia neno “takatifu” kwa ua la yungiyungi. Watu wengine pia walichukulia hadithi za mapenzi zilizobuniwa na wengine na yaliyomo ndani kuwa takatifu, ama wangemchukulia mhusika mkuu anayestahili upaa kuwa mtakatifu. Zaidi, wengine walifikiria watu kutoka kwa Biblia, ama wengine walioandikwa katika vitabu vya kiroho—kama watakatifu, mitume, au wengine ambao walimfuata Mungu awali Alipokuwa akifanya kazi Yake—kama waliokuwa na uzoefu wa kiroho ambao ulikuwa takatifu. Haya yote ni mambo yaliyofikiriwa na watu na hizi ni dhana zinazoshikiliwa na watu. Mbona watu wanashikilia dhana kama hizi? Kuna sababu moja na ni rahisi sana: Ni kwa sababu watu wanaishi miongoni mwa tabia potovu na wanaishi katika dunia ya uovu na uchafu. Kila kitu wanachoona, kila kitu wanachogusa, kila kitu wanachopitia ni uovu wa Shetani na upotovu wa Shetani na pia kufanya mipango, kupigana wenyewe kwa wenyewe, na vita vinavyotokea miongoni mwa watu walio chini ya ushawishi wa Shetani. Kwa hivyo, hata wakati Mungu anafanya kazi Yake kwa watu, ama hata wakati Anazungumza na watu na tabia na kiini Chake vyote vinaonyeshwa kwa watu, hawawezi kuona ama kukubali kile ambacho ni utakatifu. Hata zaidi, hii ndiyo sababu watu mara nyingi husema Mungu ni mtakatifu. Kwa sababu watu wanaishi miongoni mwa uchafu na upotovu na wanamilikiwa na Shetani, hawaoni mwangaza na hawajui masuala ama vitu vyema na zaidi, hawajui ukweli. Kwa hivyo, hakuna anayejua maana ya takatifu. Baada ya kusema hayo, kuna vitu vitakatifu ama watu watakatifu miongoni mwa ubinadamu huu potovu? (La.) Tunaweza kusema kwa uhakika kwamba la, hakuna, kwa sababu kiini cha Mungu tu ndicho kitakatifu. Kuhusu utakatifu wa kiini cha Mungu, wakati uliopita tulishiriki kidogo kuuhusu na huo ulikuwa msukumo wa maarifa ya watu ya utakatifu wa Mungu, lakini hautoshi. Hauwezi kutosha kusaidia watu kujua kikamilifu utakatifu wa Mungu, wala hautoshi kuwasaidia kuelewa kwamba utakatifu wa Mungu ni wa kipekee. Zaidi, hautoshi kuruhusu watu kuelewa kipengele cha maana ya ukweli ya utakatifu kwani imejumuishwa kabisa kwa Mungu. Kwa hivyo, ni muhimu kwamba tuendelee ushirika wetu katika mada hii. Katika kifungu cha tatu ushirika wetu ulijadili mada tatu, kwa hivyo sasa tunapaswa kujadili mada ya nne, na tutaanza kusoma maandiko.
4. Majaribu ya Shetani
(Mat 4:1-4) Kisha Yesu akaongozwa na Roho kwenda nyikani ili ajaribiwe na Ibilisi. Na baada ya kufunga siku arobaini mchana na usiku, mwishowe alihisi njaa. Na mjaribu alipomjia, alimwambia, Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Lakini Yesu akamjibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate peke yake, ila kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu. Haya ndiyo maneno ambayo ibilisi kwanza alijaribu kumjaribu Bwana Yesu. Ni nini maudhui ya aliyoyasema ibilisi? Endelea na uyasome. Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate Ibilisi alisema maneno haya, ambayo yalikuwa rahisi kiasi, lakini kuna shida na maudhui muhimu ya maneno haya? (Ndiyo.) Shida ni nini? Alisema, “Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu” kwa hivyo katika moyo wake, alijua kwamba Bwana Yesu alikuwa Mwana wa Mungu? Alijua kwamba Alikuwa Kristo? (Ndiyo.) Basi kwa nini alisema “ukiwa ndiwe”? (Alikuwa akijaribu kumjaribu Mungu.) Hakika, alikuwa akijaribu kumjaribu Mungu, lakini ni nini madhumuni ya kufanya hivyo? Alisema, “Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu ” Katika moyo wake alijua kwamba Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, haya yalikuwa wazi katika moyo wake, lakini licha ya haya, alinyenyekea Kwake au kumwabudu Yeye? (La.) Alitaka kufanya nini? Alitaka kufanya hivi na kusema maneno haya kumfanya Bwana Yesu kukasirika na kisha kumshawishi kuchukua chambo, na kumdanganya Bwana Yesu kufanya mambo kulingana na njia yake ya kufikiri na kuinuka kwa chango chake. Si alimaanisha hivi? Katika moyo wake alijua wazi kwamba huyu alikuwa Bwana Yesu Kristo, lakini alisema hivi hata hivyo. Hii si asili ya Shetani? Asili ya Shetani ni nini? (Kuwa mjanja, mwovu na kutokuwa na Heshima kwa Mungu.) Hamheshimu Mungu. Ni kitu kipi hasi alichokuwa akifanya hapa? Hakutaka kumshambulia Mungu? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, alisema: “Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate .”); si hii ni nia ovu ya Shetani? (Ndiyo.) Alikuwa anajaribu kufanya nini kweli? Lengo lake ni wazi sana: Alikuwa anajaribu kutumia mbinu hii kukanusha nafasi na utambulisho wa Bwana Yesu Kristo. Alisema, “Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Usipo, basi wewe siwe Mwana wa Mungu na Hufanyi kazi hii.” Ni haya yaliyomaanishwa hapa? Alitaka kutumia mbinu hii kumshambulia Mungu, alitaka kuvunja na kuharibu kazi ya Mungu; huu ndio uovu na ujanja wa Shetani. Uovu wake ni maonyesho ya kiasili ya asili yake. Ingawaje alijua Bwana Yesu Kristo alikuwa Mwana wa Mungu, kupata mwili kwenyewe kwa Mungu Mwenyewe, hangeweza kuwacha kufanya kitu kama hiki, kumfuata Mungu nyuma na kuendelea kumshambulia na kujaribu sana kuvuruga na kuharibu kazi ya Mungu na kumfanya Mungu kuwa adui.
Sasa, hebu tuchambue kirai hiki alichotumia Shetani: “amuru kwamba mawe haya yawe mikate” Kubadili mawe yawe mikate—hili linamaanisha chochote? Halina maana. Iwapo kuna chakula, mbona usile? Mbona ni muhimu kubadili mawe yawe mikate? Kuna maana hapa? (La.) Ingawa alikuwa amefunga wakati huo, kwa hakika Bwana Yesu alikuwa na chakula cha kula? Je, Alikuwa na chakula? (Alikuwa nacho.) Kwa hivyo, hapa, tunaona upuuzi wa matumizi ya Shetani ya kirai hiki. Kwa usaliti na uovu wake wote, tunaona upuuzi na ujinga wake, siyo? Shetani anafanya idadi fulani ya mambo. Unaona asili yake ovu na unaona akiharibu kazi ya Mungu. Ni wa kuchukiza na kuudhi. Lakini kwa upande mwingine, unapata asili ya kitoto na ujinga nyuma ya maneno na vitendo vyake? (Ndiyo.) Huu ni ufunuo kuhusu asili ya Shetani; ana asili ya aina hii na atafanya kitu kama hiki. Kwa wanadamu, kirai hiki ni cha upuuzi na cha kuchekesha. Lakini maneno kama hayo kwa hakika yanaweza kutamkwa na Shetani. Tunaweza kusema kwamba ni asiyejua? Mjinga? Uovu wa Shetani uko kila mahali na daima unafichuliwa. Na Bwana Yesu anamjibu aje? (“Mtu hataishi kwa mkate peke yake, ila kwa kila neno linalotoka katika kinywa cha Mungu ”) Maneno haya yana nguvu yoyote? (Yanayo.) Mbona tunasema kwamba yana nguvu? (Ni ya ukweli.) Sahihi. Maneno haya ni ukweli. Sasa, mtu anaishi kwa mkate tu? Bwana Yesu alifunga kwa siku na usiku 40. Alikufa kwa njaa? (La.) Hakufa kwa njaa, kwa hivyo Shetani alimkaribia, akimwambia abadili mawe yawe chakula kwa kusema kitu kama hiki: Ukiyabadili mawe yawe chakula, Hutakuwa basi na vitu vya kula? Si basi Hutalazimika kufunga, Hutalazimika kuwa na njaa? Lakini Bwana Yesu alisema, Mtu hataishi kwa mkate peke yake inayomaanisha kwamba, ingawa mwanadamu anaishi katika mwili, kile kinachompa uhai, kile kinachouruhusu mwili wake kuishi na kupumua, si chakula, ila maneno yote yaliyotamkwa na kinywa cha Mungu. Katika upande mmoja, mwanadamu anachukulia maneno haya kuwa ukweli. Maneno haya yanampa imani, yanamfanya ahisi kwamba anaweza kumtegemea Mungu, kwamba Mungu ni ukweli. Kwa upande mwingine, kuna kipengele cha vitendo katika maneno haya? (Kunacho.) Mbona? Kwa sababu Bwana Yesu amefunga kwa siku na usiku 40 na bado Anasimama hapo, bado ako hai. Huu ni mfano? Cha maana hapa ni kwamba Hajakula chochote, chakula chochote kwa siku na usiku 40. Bado ako hai. Huu ni ushahidi wa nguvu nyuma ya kirai Chake. Kirai hiki ni rahisi, lakini, kuhusiana na Bwana Yesu, Alifunzwa kirai hiki na mtu mwengine, ama Alikifikiria tu kwa sababu ya kile Shetani alimwambia? Fikiria jambo hili. Mungu ni ukweli. Mungu ni uhai. Je, ukweli na uhai wa Mungu uliongezwa kwa kuchelewa? Ulitokana na uzoefu? (La.) Ni ya asili ndani ya Mungu, kumaanisha kwamba ukweli na uhai vipo ndani ya kiini cha Mungu. Licha ya kile kinachomfanyikia, Anachofichua ni ukweli. Ukweli huu, kirai hiki—iwapo maudhui yake ni ndefu ama fupi—kinaweza kumwacha mwanadamu aishi, kimpe uhai; kinaweza kumwezesha mwanadamu kupata, ndani yake, ukweli, uwazi kuhusu safari ya maisha, na kumwezesha kuwa na imani kwa Mungu. Hiki ndicho chanzo cha matumizi ya Mungu ya kirai hiki. Chanzo ni chema, kwa hivyo kitu hiki chema ni takatifu? (Ndiyo.) Kirai cha Shetani kinatoka kwa asili ya Shetani. Shetani anafichua asili yake ovu, asili yake yenye kijicho, kila mahali, daima. Sasa, ufunuo huu, anaufanya kiasili? (Ndiyo.) Kuna yeyote anayemchochea? Kuna yeyote anayemsaidia? Kuna yeyote anayemshurutisha? (La.) Anautoa kwa hiari yake mwenyewe. Hii ni asili ovu ya Shetani. Licha ya kile Mungu anafanya na jinsi Anavyokifanya, Shetani ako nyuma Yake. Kiini na sura ya ukweli ya vitu hivi ambavyo Shetani anasema na kufanya ni kiini cha Shetani—kiini ovu, kiini cha kuonea kijicho. Sasa, kuendelea kusoma, ni nini tena Shetani anasema? Tuendelee kusoma hapa chini.
(Mat 4:5-6) Kisha Ibilisi akamchukua hadi mji mtakatifu, na kumweka juu ya kinara cha hekalu, Na akamwambia, Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini: kwa maana imeandikwa,
Atawaagiza malaika wake wakuchunge: Na mikononi mwao watakubeba, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe wakati wowote.
Hebu kwanza tuzungumze kuhusu kirai hiki cha Shetani. Alisema “Ukiwa wewe ndiwe Mwana wa Mungu, jitupe chini ,” na kisha akadondoa kutoka kwa maandiko, “Atawaagiza malaika wake wakuchunge: Na mikononi mwao watakubeba, usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe wakati wowote .” Unahisi vipi unaposikia maneno ya Shetani? Si ni ya kitoto sana? Ni ya kitoto, upuuzi na kuchukiza. Mbona Nasema hivi? Daima Shetani hufanya kitu kijinga, anaamini kwamba ni mwerevu sana; na mara nyingi hutaja maandiko—hata neno la Mungu—anajaribu kuyabadili maneno haya dhidi ya Mungu kumshambulia na kumjaribu. Lengo lake la kufanya hivi ni kuharibu mpango wa kazi ya Mungu. Hata hivyo, unaona chochote kwa kile Shetani amesema? (Kuna nia mbaya hapo.) Shetani daima amekuwa mjaribu; haongei kwa njia inayoeleweka rahisi, huongea kwa njia isiyo wazi akitumia majaribu, ulaghai na ushawishi. Shetani anamjaribu Mungu na pia mwanadamu: Anafikiri kwamba Mungu na mwanadamu wote hawajui, ni wajinga, na hawawezi kutofautisha kwa wazi vitu vilivyo. Shetani anafikiri kwamba Mungu na pia mwanadamu hawataona hadi kwa kiini chake na kwamba Mungu na mwanadamu wote hawataona ujanja wake na nia zake mbaya. Si hapa ndipo Shetani anapata ujinga wake? (Ndiyo.) Zaidi, Shetani anataja maandiko wazi; anafikiria kwamba kufanya hivyo kunamfanya kuaminika, na kwamba hutaweza kuona dosari zozote kwa haya ama kuepuka kudanganywa na haya. Si hapa ndipo Shetani anakuwa mjinga na kama mtoto? (Ndiyo.) Hii ni kama wakati watu wengine wanaeneza injili na kuwa na ushuhuda kwa Mungu, si wasioamini watasema kitu kama alichosema Shetani? Umesikia watu wakisema kitu kama hiki? (Ndiyo.) Unahisi kuchukizwa unaposikia vitu kama hivyo? (Ndiyo,) Unapohisi kuchukizwa, pia unahisi kutiwa kinyaa na kukirihishwa? (Ndiyo.) Unapokuwa na hisia hizi unaweza kutambua kwamba Shetani na tabia potovu ambayo Shetani anamfanyia mwanadamu ni ovu? Katika mioyo yenu mmewahi kuwa na utambuzi kama, “Mungu kamwe haongei namna hiyo. Maneno ya Shetani yanaleta mashambulizi na majaribu, maneno yake ni ya ujinga, ya kuchekesha, ya kitoto, na ya kuchukiza. Hata hivyo, katika matamshi ya Mungu na vitendo vya Mungu, Hangetumia mbinu kama hizi kuzungumza ama kufanya kazi Yake, na Hajawahi kufanya hivyo”? Bila shaka, katika hali hii watu wana tu kiasi kidogo cha kuhisi kuendelea na hawana utambuzi wa utakatifu wa Mungu; wanaweza tu kukubali kwamba neno la Mungu ni ukweli, lakini hawajui kwamba ukweli ni utakatifu wenyewe. Na kimo chenu cha sasa, mnahisi tu hivi: “Kila kitu Mungu anasema ni ukweli, ni cha manufaa kwetu, na lazima tukikubali”; bila kujali iwapo unaweza kukubali hili au la, bila ubaguzi unasema kwamba maneno ya Mungu ni ukweli na kwamba Mungu ni ukweli, lakini hujui kwamba ukweli ni utakatifu wenyewe na kwamba Mungu ni mtakatifu. Hivyo, jibu la Yesu kwa maneno ya Shetani lilikuwa lipi?
(Mat 4:7) Yesu akamwambia, Imeandikwa tena, Usimjaribu Bwana Mungu wako.
Kuna ukweli katika kirai hiki ambacho Yesu alisema? (Ndiyo.) Kuna ukweli kwa kirai hicho. Juujuu inaonekana kama amri ya watu kufuata, ni kirai rahisi sana, lakini ni kimoja ambacho mwanadamu na Shetani wamekiuka mara nyingi. Hivyo, Bwana alimwambia, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” kwa sababu hiki ndicho kile Shetani alifanya mara nyingi na alifanya kila juhudi kufanya hivyo, unaweza hata kusema kwamba Shetani alifanya hivyo bila haya. Ni asili ya msingi ya Shetani kutomcha Mungu na kutomheshimu Mungu kwa moyo wake. Hivyo, hata wakati Shetani alikuwa kando ya Mungu na angeweza kumwona, Shetani hakuweza kuacha kumjaribu Mungu. Kwa hivyo, Bwana Yesu alimwambia Shetani, “Usimjaribu Bwana Mungu wako.” Hiki ni kirai ambacho Mungu amemwambia Shetani mara nyingi. Si kutumia kirai hiki kunafaa hata leo? (Ndiyo.) Mbona? (Kwa sababu pia sisi humjaribu Mungu mara nyingi.) Watu mara nyingi humjaribu Mungu, lakini mbona watu hufanya hivyo mara nyingi? Je, ni kwa sababu watu wamejawa na tabia potovu ya kishetani? (Ndiyo.) Kwa hivyo kile Shetani alisema hapa juu ni kitu ambacho watu husema mara nyingi? (Ndiyo.) Katika hali gani? Mtu anaweza kusema kwamba watu wamekuwa wakisema mambo kama haya na kuyafichua kiasili licha ya wakati na mahali. Hii inadhihirisha kwamba tabia ya watu ni sawa kabisa na tabia potovu ya Shetani. Bwana Yesu alisema kirai rahisi, ambacho kinawakilisha ukweli na ambacho watu wanahitaji. Hata hivyo, katika hali hii Bwana Yesu alikuwa akigombana na Shetani? Kulikuwa na chochote cha kukabiliana kwa kile Alisema kwa Shetani? (La.) Bwana Yesu aliyachukulia vipi majaribu ya Shetani kwa moyo Wake? Je, Alihisi kuchukizwa na kutiwa kinyaa? (Ndiyo.) Bwana Yesu alihisi kutiwa kinyaa na kuchukizwa lakini Hakugombana na Shetani, wala hata chini zaidi Hakuzungumza kuhusu kanuni zozote kubwa, sivyo? (Ndiyo.) Mbona hivyo? (Bwana Yesu hakutaka kumkiri Shetani.) Kwa nini Hakutaka kumkiri Shetani? (Kwa sababu Shetani daima ako hivyo, hawezi kubadilika.) Tunaweza kusema kwamba Shetani hana akili? (Ndiyo, tunaweza.) Je, Shetani anaweza kutambua kwamba Mungu ni ukweli? Shetani hatawahi kutambua kwamba Mungu ni ukweli na hatawahi kukubali kwamba Mungu ni ukweli; hii ni asili yake. Zaidi, kuna kitu kingine kuhusu asili ya Shetani kinachotia watu kinyaa, ni nini? Katika majaribio yake ya kumjaribu Bwana Yesu, aliamini nini katika moyo wake? Hata kama alimjaribu Mungu na hangefaulu, ila Shetani alijaribu tu. Hata kama angeadhibiwa, aliifanya tu. Hata kama hangepata chochote chema kutoka kwa kufanya hivyo, aliifanya tu, na kuendelea na kusimama dhidi ya Mungu hadi mwisho kabisa. Hii ni asili ya aina gani? Si huo ni uovu? (Ndiyo.) Yule anayekasirika sana wakati Mungu anatajwa, amemwona Mungu? Yule anayekuwa na hasira wakati Mungu anatajwa, anamjua Mungu? Hajui Mungu ni nani, hamwamini, na Mungu hajamwongelesha. Mungu hajawahi kumsumbua, kwa hivyo mbona akuwe na hasira? Tunaweza kusema kwamba mtu huyu ni mwovu? (Ndiyo.) Huyu anaweza kuwa mtu mwenye asili ovu? Haijalishi ni mienendo gani inafanyika duniani, iwe ya kufurahisha, chakula, watu maarufu, watu wenye sura nzuri, hakuna yoyote haya yanayomsumbua, lakini kutajwa mara moja kwa neno “Mungu” na anakasirika; huu si mfano wa asili ovu? Huu unatumika kama ushahidi wa kuridhisha wa asili ovu ya mwanadamu. Sasa, mkijizungumzia, kuna wakati ambapo ukweli unatajwa, ama wakati majaribio ya Mungu kwa mwanadamu yanatajwa ama wakati maneno ya Mungu ya hukumu dhidi ya mwanadamu yanatajwa, na mnahisi kusumbuliwa, kutiwa kinyaa, na hamtaki kusikia kuyahusu? Mioyo yenu inaweza kufikiri: Huu ni ukweli vipi? Si watu wote walisema kwamba Mungu ni ukweli? Huu si ukweli, haya bila shaka ni maneno ya Mungu ya maonyo kwa mwanadamu! Watu wengine hata wanaweza kuhisi kuchukizwa kwa mioyo yao: Haya yanatajwa kila siku, majaribio Yake kwetu yanatajwa kila siku kama hukumu Yake; haya yote yataisha lini? Tutapokea lini hatima njema? Haijulikani hasira hii isiyo na busara inatoka wapi. Hii ni asili ya aina gani? (Asili ovu.) Inasababishwa na asili ovu ya Shetani. Na kwa Mungu kuhusu asili ovu ya Shetani na tabia potovu ya mwanadamu, Hagombani kamwe wala kubishana na watu, na kamwe Halalamiki wakati watu wanatenda kutokana na ujinga. Hamtamwona Mungu akiwa na mitazamo sawa kuhusu vitu ambavyo watu wanavyo, na zaidi hamtamwona Akitumia maoni ya wanadamu, maarifa yao, sayansi yao ama filosofia yao ama fikira za mwanadamu kushughulikia vitu, Badala yake, kila kitu anachofanya Mungu na kila kitu Anachofichua kinahusiana na ukweli. Yaani, kila neno ambalo amesema na kila kitendo amefanya kinahusiana na ukweli. Ukweli huu sio tu ndoto isiyo na msingi; ukweli huu na maneno haya yanaelezwa na Mungu kwa sababu ya kiini cha Mungu na uhai Wake. Kwa sababu maneno haya na kiini cha kila kitu Mungu amefanya ni ukweli, hivyo tunaweza kusema kwamba kiini cha Mungu ni kitakatifu. Kwa maneno mengine, kila kitu ambacho Mungu anasema na kufanya kinaleta uzima na mwangaza kwa watu, kinawaruhusu watu kuona vitu vyema na uhalisi wa vitu hivi vyema na kuashiria ubinadamu kwa njia ya mwangaza ili waweza kutembea njia njema. Vitu hivi vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha Mungu na vinaamuliwa kwa sababu ya kiini cha utakatifu Wake. Mmekiona, siyo? Tutaendelea kuyasoma maandiko. .
(Mat 4:8-11) Tena, Ibilisi akamchukua hadi kwenye mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na utukufu wao; Na akamwambia, Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu. Kisha Yesu akamwambia, Ondoka uende zako, Shetani; kwa kuwa imeandikwa, Muabudu Bwana Mungu wako, na ni yeye peke yake utakayemtumikia. Basi Ibilisi akamwacha, na, tazama, malaika wakaja na wakamhudumia. Shetani, ibilisi, baada ya kushindwa katika hila zake mbili za awali, alijaribu nyingine tena: Alionyesha falme zote duniani na utukufu wa falme hizi kwa Bwana Yesu na kumwambia amwabudu ibilisi. Unaona nini kuhusu sura za ukweli za ibilisi kutoka kwa hali hii? Si Shetani ibilisi hana haya kabisa? (Ndiyo.) Anaweza kukosa haya namna gani? Kila kitu kiliumbwa na Mungu, lakini Shetani anakigeuza na kumwonyesha Mungu akisema, “Hivi vyote nitakupa, ukianguka chini na kuniabudu.” Je, si hili ni mabadiliko ya jukumu? Si Shetani hana haya? Mungu aliumba kila kitu, lakini kilikuwa cha raha Zake? Mungu alimpa mwanadamu kila kitu, lakini Shetani alitaka kunyakua vyote na baadaye akasema, “Niabudu! Niabudu na ntakupa Wewe haya yote.” Huu ni uso usiopendeza wa Shetani; hana haya kabisa, siyo? Shetani hata hajui maana ya neno “haya,” na huu ni mfano mwingine tu wa uovu wake. Hata hajui “haya” ni nini. Shetani anajua vyema kwamba Mungu aliumba kila kitu na kwamba Anavisimamia na Anavitawala. Kila kitu ni cha Mungu, si cha mwanadamu, sembuse Shetani, lakini Shetani ibilisi bila haya alisema kwamba angempa Mungu kila kitu. Si tena Shetani anafanya kitu cha ujinga na kisicho na aibu? Mungu anamchukia Shetani hata zaidi sasa, siyo? Lakini licha ya kile Shetani alijaribu kufanya, Bwana Yesu alikiamini? (La.) Bwana Yesu alisema nini? (“Muabudu Bwana Mungu wako,.”) Je, kirai hiki kina maana ya utendaji? (Ndiyo.) Maana gani ya utendaji? Tunaona uovu na kutokuwa na aibu kwa Shetani katika matamshi yake. Kwa hivyo iwapo mwanadamu angemwabudu Shetani, hitimisho lingekuwa nini? Angepokea utajiri na utukufu wa falme zote? (La.) Angepokea nini? Je, wanadamu wangekuwa wasio na haya na wa kuchekwa kama tu Shetani? (Ndiyo.) Hawangekuwa tofauti na Shetani basi. Kwa hivyo, Bwana Yesu alisema kirai hiki ambacho ni muhimu kwa kila mtu: “Muabudu Bwana Mungu wako, na ni yeye peke yake utakayemtumikia,” kinachosema kwamba isipokuwa Bwana, isipokuwa Mungu Mwenyewe, ukimhudumia mwengine, ukimwabudu Shetani ibilisi, basi utagaagaa katika uchafu sawa na Shetani. Kisha utashiriki kutokuwa na haya na uovu wa Shetani, na kama tu Shetani ungemjaribu Mungu na kumshambulia Mungu. Na basi mwisho wako ungekuwa upi? Ungechukiwa na Mungu, kufilishwa na Mungu na kuangamizwa na Mungu, sivyo? Baada ya Shetani kumjaribu Bwana Mungu mara kadhaa bila mafanikio, alijaribu tena? Shetani hakujaribu tena na kisha akaondoka. Hii inathibitisha nini? Inathibitisha kwamba asili ovu ya Shetani, kuonea kijicho kwake, na ujinga na upuuzi wake yote hayastahili kutajwa mbele ya Mungu kwa sababu Bwana Yesu alimshinda Shetani kwa sentensi tatu tu, na baadaye akatoroka na mkia wake katikati ya miguu yake, kuaibika sana asiweze kuonyesha uso wake tena, na hakumjaribu Yeye tena. Kwa sababu Bwana Yesu alikuwa amelishinda jaribio hili la Shetani, Angeweza kuendelea kwa urahisi kazi ambayo Alipaswa kufanya na kuanza kazi zilizokuwa mbele Yake. Je, yote aliyoyasema Bwana Yesu na kufanya katika hali hii yanabeba maana kiasi ya vitendo kwa kila mtu yakitumika sasa? (Ndiyo.) Maana ya utendaji ya aina gani? Je, kumshinda Shetani ni kitu rahisi kufanya? (La.) Ingekuwa nini basi? Ni lazima watu wawe na uelewa wazi wa asili ovu ya Shetani? Ni lazima watu wawe na uelewa sahihi wa majaribu ya Shetani? (Ndiyo.) Ukiwahi kupitia majaribu ya Shetani katika maisha yako, na iwapo unaweza kuona hadi kwa asili ovu ya Shetani, utaweza kumshinda? Iwapo unajua kuhusu ujinga na upuuzi wa Shetani, bado unaweza kusimama kando ya Shetani na kumshambulia Mungu? (La, hatungeweza.) Ikiwa unaelewa jinsi kuwa na kijicho na kutokuwa na aibu kwa Shetani vinafichuliwa kupitia kwako—iwapo unatambua wazi na kujua mambo haya—bado ungemshambulia na kumjaribu Mungu kwa njia hii? (La, hatungeweza.) Utafanya nini? (Tutaasi dhidi ya Shetani na kumwacha.) Hili ni jambo rahisi kufanya? (La.) Hili si rahisi, kufanya hivi, watu wanalazimika kuomba mara nyingi, ni lazima wajiweke mbele ya Mungu, na lazima wajichunguze. Lazima watii nidhamu ya Mungu na hukumu Yake na kuadibu Kwake na kwa njia hii tu ndipo watu wataweza kujitoa polepole kutoka kwa utawala na udhibiti wa Shetani.
Tunaweza kuweka pamoja mambo yanayojumuisha kiini cha Shetani kutoka kwa mambo haya ambayo amesema. Kwanza, kiini cha Shetani kwa jumla kinaweza kusemwa kuwa ovu, ambacho ni kinyume na utakatifu wa Mungu. Kwa nini Nasema kiini cha Shetani ni ovu? Mtu anapaswa kuangalia matokeo ya kile Shetani anafanyia watu ili kuona haya. Shetani anapotosha na kudhibiti mwanadamu, na mwanadamu anatenda chini ya tabia potovu ya Shetani, na anaishi katika dunia iliyopotoshwa na Shetani na kuishi miongoni mwa watu potovu. Wengi wanamilikiwa na kusimilishwa na Shetani bila kusudi na mwanadamu hivyo ana asili ovu ya Shetani. Kutoka kwa yote Shetani amesema na kufanya, tunaweza kuona kiburi chake na kuona ujanja na kijicho chake. Kiburi cha Shetani kimsingi kinaonekana vipi? Je, Shetani daima anataka kuchukua nafasi ya Mungu? Shetani daima anataka kuharibu kazi ya Mungu na nafasi ya Mungu na kuyachukua kuwa yake ili watu waunge mkono na kuabudu Shetani; hii ni asili ya kiburi ya Shetani. Lakini wakati Shetani anapotosha watu, anafanya hivyo kwa njia ya ujanja na ya usaliti: Wakati Shetani anafanya kazi yake kwa watu, hawaambii watu moja kwa moja jinsi ya kumkataa na kumpinga Mungu. Wakati Shetani anamjaribu Mungu, hatoki na kusema, “Nakujaribu, nitakushambulia,” hivyo Shetani anatumia mbinu gani? (Ushawishi.) Anashawishi, anajaribu, anashambulia, na anaweka mitego yake, na hata kwa kutaja maandiko, Shetani anazungumza na kutenda kwa njia mbalimbali ili kutimiza nia zake mbaya. Baada ya Shetani kufanya hivi, ni nini kinachoweza kuonekana kutoka kile kilichojitokeza kwa mwanadamu? Je, si watu wana kiburi? Mwanadamu ameteseka kutoka kwa upotovu wa Shetani kwa maelfu ya miaka na hivyo mwanadamu amekuwa mwenye kiburi na mwenye majivuno mengi sana, na amekuwa mjanja, mwenye kijicho, na asiyefikiri, siyo? Haya mambo yote yametokana kwa sababu ya asili ya Shetani. Kwa sababu asili ya Shetani ni ovu, amempa mwanadamu asili hii ovu na kumletea mwanadamu tabia hii potovu. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi chini ya tabia potovu ya kishetani na, kama Shetani, mwanadamu anaenda kinyume na Mungu, anamshambulia Mungu, na kumjaribu Yeye hadi kwa kiwango ambacho mwanadamu hamwabudu Mungu na hamheshimu katika moyo wake, siyo?
Kuhusu utakatifu wa Mungu, hata kama inaweza kuwa mada inayojulikana, katika majadiliano inaweza kuwa dhahania kiasi kwa watu wengine, na maudhui yake yanaweza kuwa ya kina sana. Zamani, watu hawakushughulika sana na mada ya utakatifu wa Mungu, kwa hivyo hawaielewi. Lakini msijali, Nitawasaidia kuelewa maana ya utakatifu wa Mungu. Naona kwamba ni vigumu kidogo kwenu kupokea, wacha tuseme hili kwanza: Iwapo unataka kujua mtu, angalia tu kile anachofanya na matokeo ya vitendo vyake, na utaweza kuona kiini cha mtu huyo. Kwa hivyo hebu tushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu kutoka kwa mtazamo huu kwanza. Tulisema kwamba kiini cha Shetani ni ovu na chenye kijicho, na kwa hivyo vitendo vya Shetani kwa mwanadamu vimekuwa kumpotosha bila kikomo. Shetani ni mwovu, kwa hivyo watu ambao amepotosha hakika ni waovu, siyo? Kuna yeyote anayeweza kusema, “Shetani ni mwovu, pengine mtu aliyepotosha ni mtakatifu”? Ni mzaha, siyo? Je, hata inawezekana? (La.) Kwa hivyo usimfikirie hivyo, wacha tumzungumzie kutoka kwa kipengele hiki: Shetani ni mwovu, hiki ni kiini chake na ni halisi, haya si mazungumzo matupu tu. Hatujaribu kusema uwongo juu ya Shetani; tunashiriki tu kuhusu ukweli na uhalisi na pia kuhusu ukweli unaomzunguka. Hii inaweza kuumiza watu wengine ama sehemu fulani ya watu, lakini hakuna nia mbaya hapa; pengine mtasikia haya leo na kuhisi kutostareheka kiasi, lakini siku fulani hivi punde, wakati mnaweza kumtambua, mtajichukia, na mtahisi kwamba kile tulichozungumzia leo ni cha manufaa kwenu na chenye thamani.
Kiini cha Shetani ni ovu, kwa hivyo matokeo ya vitendo vya Shetani bila shaka ni ovu, ama kwa kiwango cha chini kabisa, yanahusiana na uovu wake, tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Kwa hivyo, je Shetani anampotosha mwanadamu vipi? Kwanza lazima tuangalie hasa—uovu uliofanywa na Shetani duniani na miongoni mwa ubinadamu ambao unaonekana, tunaoweza kuhisi; mmewahi kuyafikiria haya awali? Pengine hamkuyafikiria sana, kwa hivyo wacha Nitaje pointi kadhaa muhimu ili muweze kuona jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Kuna nadharia inayoitwa mageuko; kila mtu anajua kuihusu, siyo? Mageuko na uyakinifu huu, si sehemu ya maarifa yanayosomwa na mwanadamu? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani kwanza anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu, na kisha anatumia sayansi kuamsha mvuto wa wanadamu kwa maarifa, sayansi, na vitu vya ajabu, ama kwa vitu ambavyo watu wanataka kuchunguza; hii ni kusema, Shetani anatumia maarifa ya kisayansi kumpotosha mwanadamu. Vitu vifuatavyo vinavyotumiwa na Shetani kumpotosha mwanadamu ni desturi ya kitamaduni na ushirikina, na baada ya vitu hivyo, anatumia mienendo ya kijamii. Hivi vyote ni vitu ambavyo watu wanapatana navyo katika maisha yao ya kila siku na hivi vyote vinahusiana na vitu vilivyo karibu na watu, vitu wanavyoona, wanavyosikia, wanavyogusa na wanavyopitia. Mtu anaweza kusema kwamba vinazunguka kila mtu, haviwezi kutorokwa na kuepukika. Wanadamu hawana njia ya kuepuka kuathiriwa, kuambukizwa, kudhibitiwa, na kufungwa na vitu hivi; hawana nguvu za kuvisukuma mbali.
Kwanza tutazungumza kuhusu maarifa. Si kila mtu angechukulia maarifa kuwa kitu chema? Ama kwa kiwango cha chini kabisa, watu wanafikiri kwamba kidokezo cha neno “maarifa” ni chema badala ya hasi. Kwa hivyo mbona tunataja hapa kwamba Shetani anatumia maarifa kwanza kumpotosha mwanadamu? Si nadharia ya mageuko ni kipengele cha maarifa? Si sheria za kisayansi za Newton ni sehemu ya maarifa? Si mvuto wa dunia ni sehemu ya maarifa, siyo? (Ndiyo.) Hivyo mbona maarifa yametajwa miongoni mwa maudhui anayoyatumia Shetani kumpotosha mwanadamu? Maoni yenu hapa ni yapi? Je, maarifa yana hata chembe cha ukweli ndani yake? (La.) Kwa hivyo ni nini kiini cha maarifa? (Yanaenda kinyume na ukweli.) Maarifa ambayo mwanadamu anatafiti yanafunzwa kwa msingi upi? Yanalingana na nadharia ya mageuko? Si maarifa ambayo mwanadamu amechunguza, ujumla wake, unatokana na ukanaji Mungu? (Ndiyo.) Hivyo, kuna sehemu yoyote ya maarifa haya ambayo ina uhusiano na Mungu? Je, yanahusiana na kumwabudu Mungu? Yanahusiana na ukweli? (La.) Shetani anatumiaje maarifa kumpotosha mwanadamu? Nimetoka tu kusema kwamba hakuna sehemu yoyote ya maarifa haya inahusiana na kumwabudu Mungu ama na ukweli. Watu wengine wanayafikiria hivi: “Yanaweza kutokuwa na chochote kuhusiana na ukweli, lakini hayawapotoshi watu.” Mnafikiri nini kuhusu haya? Ulifundishwa na maarifa kwamba furaha ya watu ilitegemea kile walichokiumba na mikono yao? Je, maarifa yaliwahi kukufunza kwamba hatima ya mwanadamu ilikuwa mikononi mwake? (Ndiyo.) Haya ni mazungumzo ya aina gani? (Ni upuuzi.) Sahihi! Ni upuuzi! Maarifa yanatatiza kujadili. Unaweza kuiweka kwa urahisi kwamba eneo la maarifa ni maarifa tu. Hili ni eneo la maarifa linalofunzwa kwa msingi wa ukanaji Mungu na kutokuwa na uelewa kwamba Mungu aliumba mambo yote. Watu wanaposoma aina hii ya maarifa, hawaoni Mungu anatawala mambo yote, hawaoni Mungu anaongoza ama anasimamia mambo yote. Badala yake, wanayofanya tu ni kutafiti, kuchunguza, na kutafuta majibu ya kisayansi bila kikomo kwa sehemu hiyo ya maarifa. Hata hivyo, iwapo watu hawamwamini Mungu na badala yake wanatafiti tu, kamwe hawatapata majibu ya kweli, siyo? Maarifa yanakupa tu riziki, yanakupa tu kazi, yanakupa tu mapato ili usiwe na njaa, lakini kamwe hayawezi kukusaidia kumjua Mungu, hayatakusaidia kumwamini Yeye, kumtii Yeye, na maarifa kamwe hayatakuweka mbali na maovu. Kadiri unavyosoma maarifa, ndivyo utatamani zaidi kuasi dhidi ya Mungu, kumtafiti Mungu, kumjaribu Mungu, na kwenda kinyume na Mungu. Hivyo sasa, tunaona yapi ambayo maarifa yanawafunza watu? Yote ni filosofia ya Shetani. Je, filosofia za Shetani na kanuni za kuishi zinazopatikana kwa wanadamu potovu zina uhusiano wowote na ukweli? (La.) Hazina uhusiano wowote na ukweli na, kwa kweli, ni kinyume cha ukweli. Watu mara nyingi husema, “Maisha ni mwendo”; haya ni mazungumzo ya aina gani? (Upuuzi.) Watu pia wanasema, “Mwanadamu ni chuma, mchele ni chuma, mwanadamu huhisi anataabika kwa njaa asipokula mlo”; hii ni nini? (Upuuzi, maneno ya Shetani.) Hata ni uwongo mbaya zaidi na inachukiza kuisikia. Hivyo, maarifa ni kitu ambacho pengine kila mtu anakijua. Kwa yanayoitwa maarifa ya mwanadamu, Shetani amejaza kidogo filosofia yake ya maisha na kufikiria kwake. Na wakati Shetani anafanya haya, Shetani anamruhusu mwanadamu kuomba kufikiria kwake, filosofia, na mtazamo wake ili mwanadamu aweze kukana uwepo wa Mungu, kukana utawala wa Mungu juu ya mambo yote na utawala juu ya hatima ya mwanadamu. Kwa hivyo, masomo ya mwanadamu yanapoendelea, anahisi uwepo wa Mungu kuwa usio yakini anapopata maarifa zaidi, na mwanadamu anaweza hata kuhisi kwamba Mungu hayupo kwa sababu ya mitazamo, dhana, na fikira ambazo Shetani ameongeza kwa akili ya mwanadamu. Shetani anapoweka fikira hizi ndani ya akili ya mwanadamu, si watu wanapotoshwa na mambo haya? (Ndiyo.) Ni nini msingi wa maisha ya mwanadamu sasa? Kweli anategemea maarifa haya? La; msingi wa maisha ya mwanadamu ni fikira, mitazamo na filosofia za Shetani ambazo zimefichwa kwa maarifa haya. Hapa ndipo kiini cha upotovu wa Shetani wa mwanadamu unafanyika, hili ndilo lengo la Shetani na mbinu yake ya kumpotosha mwanadamu.
A. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Maarifa Kumpotosha Mwanadamu
Kwanza tutazungumzia kipengele cha juujuu zaidi cha mada hii. Mlipokuwa mnafunzwa Kiswahili shuleni, je, lugha na maandishi yaliweza kuwapotosha watu? Hayangeweza. Maneno yanaweza kupotosha watu? (La.) Maneno hayapotoshi watu; ni chombo kinachowaruhusu watu kuongea na chombo ambacho watu wanatumia kuwasiliana na Mungu. Zaidi, lugha na maneno ni jinsi ambavyo Mungu anawasiliana na watu sasa, ni vyombo, ni vya umuhimu. Moja ongeza moja ni mbili, haya ni maarifa, siyo? Mbili zidisha kwa mbili ni nne, haya ni maarifa, siyo? Lakini yanaweza kukupotosha? Hii ni akili ya wote na kanuni kwa hivyo haiwezi kupotosha watu. Kwa hivyo ni maarifa gani yanayopotosha watu? Ni maarifa ambayo yamechanganywa mitazamo na fikira za Shetani, Shetani anataka kujaza mitazamo na fikira hizi ndani ya ubinadamu kupitia maarifa. Kwa mfano, katika insha, kuna chochote kibaya na maneno yaliyoandikwa? (La.) Hivyo, shida inaweza kuwa wapi? Mitazamo na nia ya mwandishi alipoandika insha hiyo na pia maudhui ya fikira zake—haya ni mambo ya kiroho—yanaweza kuwapotosha watu. Kwa mfano, iwapo ungekuwa ukitazama kipindi kwa runinga, ni mambo yapi ndani yake yangeweza kubadili mtazamo wako? Je, yale yaliyosemwa na wasanii, maneno yenyewe, yangeweza kuwapotosha watu? (La.) Ni mambo yapi ambayo yangeweza kuwapotosha watu? Ingekuwa fikira na maudhui ya kiini ya kipindi, ambayo yangewakilisha mitazamo ya mwelekezi, na taarifa iliyo kwa mitazamo hii ingeshawishi mioyo na akili za watu. Siyo? (Ndiyo.) Je, mnajua Narejelea nini katika mjadala Wangu wa Shetani kutumia maarifa kuwapotosha watu? (Ndiyo, tunajua.) Hutafahamu vibaya, siyo? Hivyo unaposoma riwaya ama insha tena, unaweza kutathmini iwapo fikira zilizoelezwa katika insha hiyo zinapotosha ama hazipotoshi mwanadamu ama kuchangia kwa ubinadamu? (Tunaweza kufanya hivyo kidogo.) Hiki ni kitu ambacho lazima kisomwe na kupitiwa polepole, si kitu kinachoeleweka kwa urahisi mara moja. Kwa mfano, unapotafiti ama kusoma sehemu ya maarifa, baadhi ya vipengele vyema vya maarifa hayo vinaweza kukusaidia kuelewa baadhi ya akili ya wote kuhusu eneo hilo, na kile ambacho watu wanapaswa kuepukana nacho. Chukua mfano wa “umeme,” hili ni eneo la maarifa, siyo? Ungekuwa mjinga kama hungejua kwamba umeme unaweza kuwatetemesha watu, siyo? Lakini utakapoelewa sehemu hii ya maarifa, hutakuwa na uzembe kuhusu kugusa kitu cha umeme na utajua jinsi ya kutumia umeme. Haya yote ni mambo mema. Unaelewa kile tunachojadili kuhusu jinsi maarifa yanawapotosha watu? (Ndiyo, tunaelewa.) Iwapo unaelewa hatutaendelea kukizungumzia zaidi kwa sababu kuna aina nyingi za maarifa ambazo zinasomwa duniani na lazima mchukue wakati wenu kuzitofautisha wenyewe.
B. Jinsi ambavyo Shetani Anatumia Sayansi Kupotosha Mwanadamu
Sayansi ni nini? Si sayansi imewekwa kwa hadhi ya juu na kuchukuliwa kuwa muhimu katika akili za karibu kila mtu? (Ndiyo, imewekwa kwa hadhi ya juu.) Sayansi inapotajwa, si watu wanahisi, “Hiki ni kitu ambacho watu wa kawaida hawawezi kuelewa, hii ni mada ambayo tu watafiti wa kisayansi ama wataalam wanaweza kugusia. Haina uhusiano wowote na sisi watu wa kawaida”? Je, ina uhusiano lakini? (Ndiyo.) Shetani anatumiaje sayansi kuwapotosha watu? Hatutazungumza kuhusu mambo mengine isipokuwa mambo ambayo watu mara nyingi wanapatana nayo katika maisha yao binafsi. Umesikia kuhusu “jeni,” siyo? (Ndiyo.) Nyote mnalijua neno hili, siyo? Je, jeni ziligunduliwa kupitia sayansi? Jeni zinamaanisha nini hasa kwa watu? Hazifanyi watu kuhisi kwamba mwili ni kitu cha ajabu? Wakati watu wanajulishwa kwa mada hii, si kutakuwa na watu—hasa wenye kutaka kujua—ambao watataka kujua zaidi ama kutaka maelezo zaidi? Hawa watu wanaotaka kujua wataweka nguvu zao zote kwa mada hii na wakati hawana shughuli watatafuta maelezo kwa vitabu na intaneti kujifunza maelezo zaidi kuihusu. Sayansi ni nini? Kuongea waziwazi, sayansi ni fikira na nadharia ya vitu ambavyo mwanadamu anataka kujua, vitu visivyojulikana, na ambavyo hawajaambiwa na Mungu; sayansi ni fikira na nadharia za siri ambazo mwanadamu anataka kuchunguza. Unafikiria wigo wa sayansi ni upi? Unaweza kusema kwamba unajumuisha mambo yote, lakini mwanadamu anafanya vipi kazi ya sayansi? Je, ni kupitia utafiti? Inahusiana na kutafiti maelezo na sheria za vitu hivi na kuweka mbele nadharia zisizoaminika ambazo watu wote wanafikiria, “Wanasayansi hawa ni wakubwa mno! Wanajua mengi na wana maarifa mengi kuelewa mambo haya!” Wanapendezwa sana na watu hao, siyo? Watu wanaotafiti sayansi, wana mitazamo ya aina gani? Hawataki kutafiti ulimwengu, kutafiti mambo ya ajabu ya maeneo ya maslahi yao? Matokeo ya mwisho ya haya ni nini? Baadhi ya sayansi ina watu wanaofikia mahitimisho yao kwa kubahatisha, nyingine ina watu wanaotegemea uzoefu wa binadamu kwa mahitimisho yao na hata eneo lingine la sayansi litakuwa na watu wanaofikia mahitimisho yao kutokana na uzoefu ama uchunguzi wa kihistoria na usuli. Sivyo? (Ndiyo.) Hivyo, sayansi inawafanyia nini watu? Kile sayansi inafanya ni kwamba inawaruhusu tu watu kuona vyombo katika ulimwengu wa maumbile na tu kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu; haimruhusu mwanadamu kuona sheria ambazo Mungu anatumia kutawala mambo yote. Mwanadamu anaonekana kupata majibu kutoka kwa sayansi, lakini majibu hayo yanachanganya na yanaleta tu uradhi wa muda mfupi, uradhi ambao unawekea moyo wa mwanadamu mipaka kwa ulimwengu wa maumbile. Mwanadamu anahisi kwamba tayari amepata majibu kutoka kwa sayansi kwa hivyo licha ya suala litakaloibuka, anaamini kwa dhati mitazamo yao ya kisayansi kulithibitisha ama kulikubali. Moyo wa mwanadamu unamilikiwa na sayansi na kushawishiwa nayo hadi pahali ambapo mwanadamu tena hana akili ya kumjua Mungu, kumwabudu Mungu, na kuamini kwamba mambo yote yanatoka kwa Mungu na mwanadamu anapaswa kumwangalia kupata majibu. Hii si ukweli? Unaweza kuona kwamba kadiri ambavyo mtu anaamini sayansi, anakuwa mjinga zaidi, akiamini kwamba kila kitu kina suluhisho la sayansi, kwamba utafiti unaweza kutatua chochote. Hamtafuti Mungu na haamini kwamba Yupo; hata watu wengine ambao wamemfuata Mungu kwa miaka mingi wataenda na kutafiti vimelea kwa msukumo ama kutafuta baadhi ya maelezo ili kupata majibu. Mtu kama huyo haangalii masuala kwa mtazamo wa ukweli na wakati mwingi anataka kutegemea mitazamo na maarifa ya kisayansi ama majibu ya kisayansi kutatua shida; lakini hamtegemei Mungu na hamtafuti Mungu. Je, watu kama hao wana Mungu katika mioyo yao? (La.) Hata kuna watu wengine wanaotaka kutafiti Mungu kwa njia sawa na vile wanasoma sayansi. Kwa mfano, kuna wataalam wengi wa kidini walioenda mahali safina ilisimama baada ya mafuriko makubwa. Wameiona safina, lakini katika kuonekana kwa safina hawaoni uwepo wa Mungu. Wanaamini tu hadithi na historia na haya ni matokeo ya utafiti wao wa kisayansi na utafiti wa dunia ya maumbile. Ukitafiti vitu yakinifu, viwe mikrobiolojia, falaki, ama jiografia, hutawahi kupata matokeo yanayosema kwamba Mungu yupo ama kwamba anatawala mambo yote, Sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo sayansi inamfanyia nini mwanadamu? Si inamweka mbali na Mungu? Si hii inawaruhusu watu kumtafiti Mungu? Si hii inawafanya watu kuwa na shaka zaidi kuhusu uwepo wa Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo Shetani anataka kutumia vipi sayansi kumpotosha mwanadamu? Si Shetani anataka kutumia mahitimisho ya kisayansi kuwadanganya na kuwanyima watu hisia? Shetani anatumia majibu yenye maana nyingi kushikilia mioyo ya watu ili wasitafute ama kuamini uwepo wa Mungu, na hivyo watakuwa wenye tuhuma kwa Mungu, kumkanusha Mungu na kuwa mbali na Yeye. Hivyo, hii ndiyo sababu tunasema ni njia moja Shetani anawapotosha watu.
C. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Desturi ya Kitamaduni Kumpotosha Mwanadamu
Je, kuna mambo mengi yanayochukuliwa kuwa sehemu ya desturi ya kitamaduni? (Ndiyo.) Hii desturi ya kitamaduni inamaanisha nini? (Inapitishwa kutoka kwa mababu.) Inapitishwa kutoka kwa mababu, hiki ni kipengele kimoja. Familia, vikundi vya makabila, na hata jamii ya binadamu imepitisha njia yao ya maisha kutoka mwanzo, ama imepitisha mila, misemo, na kanuni, ambazo zimeingizwa kwa fikira za watu. Watu wanafikiria nini kuhusu mambo haya? Watu wanayachukulia kuwa yasiyoweza kutengwa na maisha yao. Wanayachukua mambo haya na kuyachukulia kuwa kanuni na uhai wa kutii, na daima hawako tayari kuyabadilisha ama kuyaacha mambo haya kwa sababu yalipitishwa kutoka kwa mababu. Kuna vipengele vingine vya desturi ya kitamaduni, kama kile kilichopitishwa na Confucius ama Mencius, ama mambo waliyofunzwa watu na Udao ama Uconfucius ambayo yamekuwa sehemu ya kila mtu hadi ndani kwa mifupa yao. Sivyo? (Ndiyo.) Desturi ya kitamaduni hii inajumuisha nini? Inajumuisha likizo ambazo watu wanasherehekea? Kwa mfano, hapo juu kuna Tamasha la Majira ya machipuko, Tamasha la Taa, Siku ya Kufagia Kaburi, Tamasha la Mashua ya Joka, na kuna Siku ya Kimataifa ya Leba, Siku ya Watoto, Tamasha ya Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani, na Siku ya Kitaifa. Baadhi za familia hata husherehekea likizo zingine, ama husherehekea wakati wazee wanahitimu umri fulani, ama wakati watoto wanahitimu umri wa mwezi 1 na wakati wako na umri wa siku 100. Hizi zote ni likizo za desturi. Je, si usuli wa likizo hizi unajumuisha desturi ya kitamaduni? Ni nini kiini cha desturi ya kitamaduni? Kina chochote kuhusu kumwabudu Mungu? Kina chochote kuhusu kuwaambia watu kuweka katika vitendo ukweli? (La.) Kuna likizo zozote za watu kutoa sadaka kwa Mungu, kwenda kwa madhabahu ya Mungu na kupokea neno Lake? Kuna likizo kama hizi? (La.) Watu hufanya nini katika likizo hizi zote? (Kumwabudu Shetani. Kula, kunywa na shughuli za burudani.) Katika nyakati za sasa zinaonekana kuwa hafla za kula, kunywa, na kujiburudisha. Basi ni nini chanzo cha desturi ya kitamaduni? Desturi ya kitamaduni imetoka kwa nani? (Shetani.) Imetoka kwa Shetani. Katika usuli wa hizi likizo za desturi, Shetani anaingiza mambo ndani ya mwanadamu, haya ni mambo gani? Kuhakikisha kwamba watu wanakumbuka mababu zao, hili ni mojawapo ya mambo haya? Kwa mfano, wakati wa Tamasha la Kufagia Kaburi watu husafisha makaburi na kutoa sadaka kwa mababu zao. Hivyo watu hawatasahau mababu zao, siyo? Pia, Shetani anahakikisha kwamba watu wanakumbuka kuwa wazalendo, kama katika Tamasha la Mashua ya Joka. Je, Tamasha la Katikati ya Majira ya Kupukutika kwa Majani? (Kupatana kwa familia.) Ni nini usuli wa kupatana kwa familia? Sababu zake ni nini? (Kuweka familia kwanza, na hisia.) Kuwasiliana na kuunganika kihisia, siyo? Bila shaka, iwapo ni kusherehekea Mkesha wa Mwaka Mpya wa Mwezi ama Tamasha la Taa, kuna njia nyingi za kuelezea sababu za usuli. Haijalishi mtu anaelezea sababu iliyo nyuma yazo, kila moja ni njia ya Shetani ya kuingiza filosofia yake na kufikiria kwake kwa watu, ili waweze kupotea kutoka kwa Mungu na wasijue kwamba kuna Mungu, na kwamba watoe sadaka ama kwa mababu zao au Shetani, ama kwamba ni udhuru wa kula, kunywa na kujifurahisha kwa ajili ya matamanio ya mwili. Kila ya likizo hizi inaposherehekewa, fikira na mitazamo ya Shetani yanapandwa kwa kina ndani ya akili za watu na hata hawajui. Wakati watu wanafika umri wa kati ama zaidi, mambo haya, fikira na mitazamo hii ya Shetani tayari yamekita mizizi ndani sana ya mioyo yao. Zaidi, watu wanafanya juhudi zao kabisa kueneza fikira hizi, ziwe sahihi ama si sahihi, kwa kizazi kifuatacho bila wasiwasi. Sivyo? (Ndiyo.) Hivyo desturi hii ya kitamaduni na likizo hizi zinapotosha vipi watu? (Watu wanawekewa mipaka na kufungwa na kanuni za hizi desturi kana kwamba hawana muda ama nguvu kumtafuta Mungu.) Hiki ni kipengele kimoja. Kwa mfano, kila mtu anasherehekea wakati wa Mwaka Mpya wa Mwezi, usingesherehekea, hungehisi huzuni? Hungehisi, “Haiya, sikusherehekea Mwaka Mpya. Siku hii ya Mwaka Mpya wa Mwezi ilikuwa mbaya sana, na haijasherehekewa; mwaka huu wote utakuwa mbaya”? Si ungehisi kutokuwa na utulivu? (Ndiyo.) Na pengine kuogopa kiasi, siyo? Kuna hata watu wengine ambao hawajatoa sadaka kwa mababu zao kwa miaka mingi na ghafla wamekuwa na ndoto ambapo mtu aliyekufa anawaomba pesa, watahisi nini ndani yao? “Inahuzunisha kwamba huyu mtu aliyekufa anahitaji pesa ya kutumia! Nitawachomea baadhi ya pesa ya karatasi, nisipo hiyo hakika haitakuwa sawa. Sisi tunaoishi tunaweza kupatana na shida kidogo nisipochoma baadhi ya pesa ya karatasi, ni nani anayeweza kusema wakati janga litatokea?” Daima watakuwa na wingu hili ndogo la hofu na wasiwasi katika mioyo yao. Hivyo ni nani anayewapa wasiwasi? (Shetani.) Shetani huleta wasiwasi. Si hii ndiyo njia moja ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? Anatumia mbinu na udhuru mbalimbali ili kukudhibiti, kukutishia, kukufunga, hadi kiasi kwamba unachanganyikiwa na kumkubali na kumnyenyekea; hivi ndivyo Shetani anampotosha mwanadamu. Nyakati nyingi ambapo watu ni wanyonge ama hawaelewi vyema hali ilivyo, wanaweza bila kutaka, kufanya kitu kwa njia iliyochanganyikiwa, yaani, wanaanguka chini ya mshiko wa Shetani bila kusudi na wanaweza kufanya kitu bila kusudi na wasijue wanafanya nini. Hii ni njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu. Hata kuna watu wachache sasa ambao wanasita kuachana na desturi za kitamaduni ambazo zimekita mizizi na hawawezi tu kuziacha. Ni hasa wakati ni wanyonge na wasipoonyesha hisia ndipo wanataka kusherehekea likizo za aina hizi na wanataka kukutana na Shetani na kumridhisha Shetani tena, ambako kupitia huko wanaweza pia kujifariji ndani yao. Si mambo yanaenda hivi? (Ndiyo.) Ni nini usuli wa hizi desturi za kitamaduni? Mkono mweusi wa Shetani unavuta nyuzi nyuma ya pazia? Asili ovu ya Shetani inatawala na kudhibiti vitu? Shetani anadhibiti hivi vitu vyote? (Ndiyo.) Wakati watu wanaishi katika desturi ya kitamaduni na kusherehekea likizo za desturi za aina hizi, tunaweza kusema kwamba haya ni mazingira ambapo wanadanganywa na Shetani na kupotoshwa na Shetani? Si wana furaha kupotoshwa na Shetani? Si hivi ndivyo jinsi ilivyo? (Ndiyo.) Hiki ni kitu ambacho sisi wote tunakiri, siyo? Na kitu ambacho sote tunakijua.
D. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Ushirikina Kumpotosha Mwanadamu
Mnalijua neno “ushirikina,” siyo? Katika ushirikina, watu mara nyingi wanakutana na nini? (Miungu ya uongo) Kuna usawa unaopatana na desturi ya kitamaduni hapa, lakini hatutazungumza kuhusu huo leo, badala yake Nitajadili unaokabiliwa mara nyingi: uganga, uaguzi, kuchoma ubani, na kuabudu Buddha. Watu wengine wanafanya uganga, wengine wanaabudu Buddha na kuchoma ubani, ilhali wengine wanabashiriwa ama wanaambiwa bahati zao kwa kumruhusu mtu kusoma vipengele vya uso yao. Wangapi kati yenu wameambiwa bahati zao ama wamesomwa uso? Hiki ni kitu ambacho watu wengi wanataka, siyo? (Ndiyo.) Mbona hivyo? Watu wanapata faida ya aina gani kutoka kwa uaguzi na uganga? Wanapata uradhi wa aina gani kutoka kwa hayo? (Udadisi.) Ni udadisi tu? Haiwezi kuwa udadisi. Ni nini lengo la ubashiri? Mbona ufanyiwe? Si kwa ajili ya kuona siku za baadaye? Watu wengine wanasomwa nyuso zao ili kutabiri siku za baadaye, wengine wanafanya hivyo ili kuona iwapo watakuwa na bahati nzuri au la. Wengine wanafanya hivyo ili kuona vipi ndoa zao zitakuwa, na bado wengine wanafanya hivyo kuona bahati itakayoletwa na mwaka ulio mbele. Watu wengine wanasomwa nyuso zao kuona matarajio ya wana na binti zao yatakuwa vipi na kuona vipengele vyote vya vitu hivi, na wanabiashara wengine wanafanya hivyo kuona watatengeneza pesa ngapi ili waweze kupata mwongozo kwa kile wanachopaswa kufanya. Watu wengine wanataka tu kujua bahati yao itakuwaje na siku za baadaye zitaleta nini. Je, ni kuridhisha udadisi tu? (La.) Wakati watu wanasomwa nyuso zao ama kufanya vitu vya aina hii, ni kwa faida ya siku zao za baadaye binafsi na wanaamini kwamba haya yote yanahusiana kwa karibu na hatima zao. Je, kuna yoyote katika mambo haya yaliyo ya manufaa? (La.) Mbona si ya manufaa? Si kitu kizuri kujua kidogo kuhusu siku za badaye? Hii inakusaidia kujua wakati shida inaweza kutokea, ili uweze kuiepuka kama ulikuwa unajua kuihusu awali, siyo? Kupigiwa ramli kunaweza kukuruhusu kuongozwa kuhusiana nako, ili mwaka ulio mbele uweze kuwa mzuri na unaweza kuwa tajiri ukifanya biashara. Si hii ni ya manufaa? (La.) Iwapo ina manufaa haituhusu, hatutaishiriki leo; mjadala wetu hauhusishi maudhui na mada hii. Shetani anatumiaje ushirikina kumpotosha mwanadamu? Kile ambacho watu wanajua kuhusu vitu kama ubashiri, kusoma uso, na uaguzi ni ili waweza kujua bahati zao zitakuwa vipi katika siku za baadaye na vile njia iliyo mbele inakaa, lakini mwishowe, ni mikono ya nani inadhibiti vitu hivi? (Mikono ya Mungu.) Viko katika mikono ya Mungu. Kuhusiana na Shetani, kwa kutumia mbinu hizi, anataka watu wajue nini? Shetani anataka kutumia kusoma uso na uaguzi ili kuwaambia watu kwamba anajua bahati zao mbeleni, na Shetani anataka kuwaambia watu kwamba anajua vitu hivi na anavidhibiti. Shetani anataka kutumia fursa hii na kutumia mbinu hizi kudhibiti watu, ili kwamba watu wanamwekea imani isiyoweza kutambua na kutii kila neno lake. Kwa mfano, ukisomwa uso, mwaguzi akifunga macho yake na kukwambia kila kitu ambacho kimekufanyikia katika miongo michache iliyopita kwa uwazi kamili, ungehisi vipi ndani yako? Ghafla ungehisi, “Nimependezwa sana na huyu mwaguzi, yuko sahihi sana! Sijawahi mwambia yeyote maisha yangu ya nyuma, alijuaje kuyahusu?” Haitakuwa vigumu sana kwa Shetani kujua maisha yako ya nyuma, siyo? Mungu amekuongoza hadi leo, na Shetani pia amewapotosha watu wakati huo wote na amekufuata. Shetani ni roho ovu; kupita kwa miongo kwako si chochote kwa Shetani na si vigumu kwake kujua vitu hivi. Wakati unajua kwamba alichosema Shetani ni sahihi, si unampa moyo wako? Siku zako za baadaye na bahati yako, si unategemea udhibiti wake? Papo hapo, moyo wako utahisi heshima ama ustahi kwake, na kwa watu wengine, nafsi zao pengine tayari zimenyakuliwa naye. Na utamwuliza mwaguzi mara moja: “Napaswa kufanya nini baada ya hapa? Napaswa kuepukana na nini mwaka ujao? Ni vitu gani ambavyo sipaswi kufanya? Na kisha atasema: “Hupaswi kwenda pale, hupaswi kufanya hili, usivae nguo za rangi fulani, hupaswi kwenda pahali kama hapo na hapo mara nyingi, na unapaswa kufanya mambo fulani zaidi…” Si utatia vyote anavyosema moyoni mara moja? (Ndiyo.) Ungevikariri haraka kuliko neno la Mungu. Mbona ungevikariri haraka hivyo? (Vina faida kwangu.) Kwa sababu ungetaka kumtegemea Shetani kwa sababu ya bahati njema, si hapa ndipo anaunyakua moyo wako? Unapofanya kile anachosema na maneno yake sasa yanakuwa ukweli kama alivyotabiri, hungetaka kurudi nyuma kwake na kujua ni bahati gani mwaka unaokuja utaleta? (Ndiyo.) Utafanya chochote Shetani anakwambia ufanye na utaepukana na vitu anakwambia uepukane navyo, si unatii vyote anasema? Utaletwa chini ya bawa lake haraka sana, kupotoshwa, na kuwekwa chini ya udhibiti wake. Hii inafanyika kwa sababu unaamini anachosema ni ukweli na kwa sababu unaamini kwamba anajua kuhusu maisha yako ya nyuma, maisha yako ya sasa, na vitu ambavyo siku za badaye zitaleta; hii ni mbinu Shetani anatumia kudhibiti watu. Lakini kwa kweli, ni nani aliye katika udhibiti? Ni Mungu Mwenyewe, si Shetani. Shetani anatumia tu hila zake hapa kudanganya watu wajinga, kuwadanganya watu wanaoona tu ulimwengu wa maumbile kumwamini na kumtegemea. Kisha, wataanguka katika mshiko wa Shetani na kutii kila neno lake. Lakini Shetani wakati wowote hupunguza jitihada watu wanapotaka kumwamini na kumfuata Mungu? Shetani hapunguzi jitihada. Katika hali hii, watu kweli wanaanguka katika mshiko wa Shetani? (Ndiyo.) Tunaweza kusema kwamba tabia ya Shetani hapa haina haya hata kidogo? (Ndiyo.) Mbona tungesema hivyo? (Shetani anatumia hila.) Hmm, kwa sababu hila za Shetani ni za ulaghai na zinadanganya. Shetani hana haya na anawadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti kila kitu chao na kuwadanganya watu kufikiria kwamba anadhibiti hatima zao. Hii inawafanya watu wajinga kuja kumtii kabisa na anawadanganya na sentensi moja ama mbili tu na katika kuchanganyika kwao, watu wanasujudu mbele yake. Si hii ni sahihi? (Ndiyo.) Hivyo, Shetani anatumia mbinu za aina gani, anasema nini kukufanya umwamini? Kwa mfano, pengine hujamwambia Shetani idadi ya watu katika familia yako, lakini anaweza kusema kwamba kuna watatu katika familia yako, akiwemo binti ambaye ana miaka 7, na pia umri wa wazazi wako. Iwapo ulikuwa na tuhuma na shaka zako mwanzoni, hutahisi kwamba anaaminika zaidi kidogo baada ya kusikia hayo? (Ndiyo.) Na kisha Shetani anaweza kusema, “Kazi imekuwa ngumu kwako leo, wakubwa wako hawakupi utambuzi unaostahili na daima wanafanya kazi dhidi yako.” Baada ya kuyasikia hayo, ungefikiri, “Hiyo ni sahihi kabisa! Mambo hayajakuwa yakienda vizuri kazini.” Hivyo ungemwamini Shetani zaidi kidogo. Kisha angesema kitu kingine kukudanganya, kukufanya umwamini hata zaidi, na kidogo kidogo, utajipata huwezi kupinga ama kuwa na tuhuma kwake tena. Shetani anatumia tu hila chache zisizo na maana, hata ndogo zisizojalisha, kukufadhaisha. Unapofadhaishwa, hutaweza kupata njia zako, hutajua kile cha kufanya, na utaanza kufuata kile Shetani anasema. Hii ni mbinu ya “ah nzuri sana” anayotumia Shetani kumpotosha mwanadamu pahali unapoingia katika mtego wake bila kusudi na unashawishiwa naye. Unaona, Shetani anakwambia mambo machache ambayo watu wanafikiria kuwa mambo mazuri, na kisha anakwambia kile cha kufanya na kile cha kuepuka na hivyo ndivyo unaanza kufuata njia hiyo bila kusudi. Punde unapoanza kufuata njia hiyo, haitakuwa chochote ila shida kwako; daima utakuwa ukifikiria kile alichosema Shetani na kile alichokwambia ufanye, na bila kujua utamilikiwa naye. Mbona hivi? Ni kwa sababu wanadamu hawana ukweli na hivyo hawawezi kusimama dhidi ya majaribu na ushawishi wa Shetani. Wanapokabiliwa na uovu, ujanja, usaliti, na kijicho cha Shetani, wanadamu ni wajinga sana, wasiojua na wanyonge, siyo? Si hii ni mojawapo ya njia ambayo Shetani anampotosha mwanadamu? (Ndiyo.) Mwanadamu anadanganywa na kulaghaiwa bila kusudi, kidogo kidogo, kupitia mbinu mbalimbali za Shetani, kwa sababu hawana uwezo wa kutofautisha kati ya mema na hasi. Hawana kimo hiki, na uwezo wa kumshinda Shetani.
E. Jinsi Ambavyo Shetani Anatumia Mienendo ya Kijamii Kumpotosha Mwanadamu
Je, mienendo ya kijamii ni kitu kipya? (La.) Hivyo ilianza lini? Mtu anaweza kusema kwamba mienendo ya kijamii ilianza wakati Shetani alipoanza kuwapotosha watu? (Ndiyo.) Mienendo ya kijamii inajumuisha nini? (Mtindo wa mavazi na vipodozi.) Hiki ni kitu ambacho watu mara nyingi wanakutana nacho. Mtindo wa mavazi, mtindo wa kisasa na mienendo, hiki ni kipengele kidogo. Kuna kingine zaidi? Je, misemo maarufu ambayo watu wanapenda kusema inahesabika pia? Je, pia mitindo ya maisha ambayo watu wanataka inahesabika? Je, nyota wa muziki, watu mashuhuri, majarida, na riwaya ambazo watu hupenda zinahesabika? (Ndiyo.) Katika akili zenu, ni kipengele kipi cha mienendo hii kinaweza kumpotosha mwanadamu? Ni mienendo ipi inawavutia sana? Watu wengine husema: “Sisi sote tumefikia umri fulani, tuko katika miaka ya arobaini, hamsini, sitini, sabini ama themanini ambapo hatuwezi kufaa katika mienendo hii na haituvutii tena.” Je, hii ni sahihi? (La.) Wengine husema: “Hatufuati watu mashuhuri, hicho ni kitu ambacho vijana walio katika umri wa ujana na ishirini wanafanya; pia hatuvai nguo za mitindo ya kisasa, hicho ni kitu ambacho watu wanaojali sura wanafanya.” Kwa hivyo ni ipi kati ya hii inaweza kuwapotosha? (Misemo maarufu.) Je, hii misemo maarufu inaweza kuwapotosha watu? Huu ni msemo mmoja, na mnaweza kuona iwapo unawapotosha watu au la, “Pesa inamfanya farasi jike kwenda”; huu ni mwenendo? Si hiki ni kitu kibaya zaidi kulinganishwa na mienendo ya mavazi na chakula mliyotaja? (Ndiyo.) “Pesa inamfanya farasi jike kwenda” ni filosofia ya Shetani na inaenea katika kila jamii ya binadamu. Mnaweza kusema kwamba ni mwenendo kwa sababu umepatiwa kila mtu na sanasana uko katika mioyo yao. Watu walienda kutoka kutoukubali msemo huu hadi kuuzoea ili wanapokutana na maisha halisi, polepole waliukubali kwa kimya, kukiri uwepo wake na hatimaye, waliupa muhuri wao wa idhini. Sivyo? (Ndiyo.) Je, hii si njia ya Shetani kumpotosha mwanadamu? Pengine nyinyi mlioketi hapa hamwelewi msemo huu kwa kiwango sawa, lakini kila mtu ana viwango tofauti vya tafsiri na kukiri kwa msemo huu kutokana na mambo ambayo yamefanyika karibu nao na uzoefu wao binafsi, siyo? Licha ya kiwango cha uzoefu mtu anao na msemo huu, ni nini athari mbaya unaweza kuwa nao katika moyo wa mtu? (Watu wangeweza kufikiri kwamba pesa inaweza kufanya chochote, na wangeheshimu pesa.) Kitu fulani kinafichuliwa kupitia tabia ya binadamu ya watu katika dunia hii, mkiwemo nyinyi mlioketi hapa. Hiki kinafasiriwa vipi? Ni ibada ya pesa. Ni vigumu kutoa hili kwa moyo wa mtu? Ni vigumu sana! Inaonekana kwamba upotovu wa Shetani wa mwanadamu ni kamili kabisa! Tunaweza kusema hivyo? (Ndiyo.) Hivyo baada ya Shetani kutumia mwenendo huu kuwapotosha watu, unaonyeshwa vipi kwao? Hamhisi kwamba hamtaishi siku moja katika dunia hii bila pesa yoyote, kwamba hata siku moja haiwezekani? (Ndiyo.) Hadhi ya watu inatokana na kiasi cha pesa wakonayo na pia heshima yao. Migongo ya maskini imekunjwa kwa aibu, ilhali matajiri wanafurahia hadhi zao za juu. Wanatenda kwa njia ya kujigamba na wana majivuno, wakiongea kwa sauti kubwa na kuishi kwa kiburi. Msemo na mwenendo huu unaleta nini kwa watu? Si watu wengi wanaona kupata pesa kunastahili gharama yoyote? Si watu wengi hutoa Heshima na uadilifu wao wakitafuta pesa zaidi? Si watu wengi hupoteza fursa ya kufanya wajibu wao na kumfuata Mungu kwa sababu ya pesa? Si hii ni hasara kwa watu? (Ndiyo.) Si Shetani ni mbaya kutumia mbinu hii na msemo huu kumpotosha mwanadamu kwa kiwango kama hicho? Si hii ni hila yenye kijicho? Unaposonga kutoka kuukataa huu msemo maarufu hadi mwishowe kuukubali kama ukweli, moyo wako unaanguka kabisa chini ya mshiko wa Shetani, na hivyo unakuja kuishi naye bila kusudi. Msemo huu umekuathiri kwa kiwango kipi? Unaweza kujua njia ya ukweli, unaweza kujua ukweli, lakini huna nguvu ya kuufuatilia. Unaweza kujua kwa hakika neno la Mungu, lakini huko radhi kulipa gharama, huko radhi kuteseka kulipa gharama. Badala yake, kwako, ni afadhali utoe siku zako za baadaye na kudura yako kwenda kinyuma na Mungu hadi mwisho kabisa. Licha ya kile Mungu anasema, licha ya kile Mungu anafanya, licha ya kiasi unagundua kwamba upendo wa Mungu kwako ni wa kina na mkubwa, bado ungeendelea kwa njia hiyo kwa ukaidi na kulipa gharama ya msemo huu. Hii inamaanisha kwamba huu msemo tayari unadhibiti tabia na fikira zako, na unaona afadhali hatima yako idhibitiwe na msemo huu kuliko kuyatoa yote. Watu wanafanya hivi, wanadhibitiwa na msemo huu na kutawaliwa nao. Hii si athari ya Shetani kumpotosha mwanadamu? Hii si filosofia na tabia potovu ya Shetani ikikita mizizi kwa moyo wako? Ukifanya hivyo, si Shetani amefikia lengo lake? (Ndiyo.) Unaona jinsi Shetani amempotosha mwanadamu kwa njia hii? (La.) Hukumwona. Unaweza kumhisi? (La.) Hukuihisi. Je, unaona uovu wa Shetani hapa? (Ndiyo.) Shetani humpotosha mwanadamu wakati wote na pahali pote. Shetani anaifanya isiwezekane kwa mwanadamu kujilinda dhidi ya upotovu huu na anamfanya mwanadamu mnyonge kwake. Shetani anakufanya ukubali fikira zake, mitazamo yake na mambo maovu yanayotoka kwake katika hali ambapo huna kusudi na huna utambuzi wa kile kinachokufanyikia. Watu wanakubali kikamilifu vitu hivi na hawavibagui. Wanapenda sana vitu hivi na kuvishikilia kama hazina, wanaviacha vitu hivi viwatawale na kuwachezea, na hivi ndivyo upotovu wa Shetani wa mwanadamu unakuwa wa kina na kina zaidi.
Mbinu nyingi zilizojadiliwa awali ambazo Shetani hutumia kuwapotosha watu ni dhahiri na kila mtu amezipitia; Shetani huzitumia na haziwezi kuepukika. Mwanadamu ana maarifa na baadhi ya nadharia za kisayansi, mwanadamu anaishi na ushawishi wa desturi ya kitamaduni, na kila mtu anarithi desturi ya kitamaduni. Mwanadamu ataendeleza desturi ya kitamaduni aliyopewa kutoka kwa Shetani na pia kutenda pamoja na mienendo ya kijamii ambayo Shetani anawapa wanadamu. Licha ya kutoweza kutengana na Shetani, kushiriki na kile ambacho Shetani anafanya wakati wote, kukubali ujanja, kiburi, kijicho, na uovu wake—baada ya kumiliki tabia hizi za Shetani—je, mwanadamu ana furaha ama huzuni katika kuishi miongoni mwa wanadamu hawa na katika dunia hii? (Huzuni.) Mbona unasema hivyo? (Amefungwa na vitu hivi na maisha yake ni mapambano machungu.) Hmm. Unaweza kumwona mtu ambaye ana miwani na anaonekana wa hekima; pengine kamwe hapigi kelele, awe daima na lugha ya kushawishi, wa busara, na zaidi ya hayo, kwa sababu ya umri wake mkubwa, pengine amepitia vitu vingi na kuwa na uzoefu mkubwa; pengine anaweza kuzungumza kwa undani kuhusu masuala makubwa na madogo na kuwa na msingi dhabiti wa kile anachosema; pengine pia ana seti ya nadharia ya kutathmini uhalisi na sababu ya vitu; na watu pengine wanaweza kuangalia tabia yake, sura yake, na kuona jinsi anajibeba na kuona uadilifu wake na hulka yake na kutopata dosari kwake. Watu kama hawa hasa wanashughulika na mienendo ya kijamii ya sasa na hawachukuliwi kuwa wa mtindo wa kizamani; badala yake yeye ni mtu anayevumbua na kujaribu mawazo mapya kabisa yasiyokubalika kwa urahisi na ni mtu wa mitindo. Ingawa mtu huyu anaweza kuwa mzee, kamwe hayuko nyuma ya nyakati na kamwe si mzee sana kufunzwa. Juujuu, hakuna anayeweza kupata dosari kwake, lakini ndani amepotoshwa na Shetani kabisa na kikamilifu. Juujuu hakuna chochote kibaya, yeye ni mpole, ni muungwana, anayo maarifa na maadili fulani; ana uadilifu na vitu anavyojua vinalingana na vile wanavyojua vijana. Hata hivyo, kuhusu asili na kiini chake, mtu huyu ni mfano kamili na unaoishi wa Shetani, ana usawa kabisa na Shetani. Hili ni “tunda” la upotovu wa Shetani wa mwanadamu. Kile Nilichosema kinaweza kuwaumiza, lakini chote ni ukweli. Maarifa ambayo mwanadamu anasoma, sayansi anayoelewa, na njia anayochukua kufaa na mienendo ya jamii, bila ubaguzi, ni vyombo vya upotovu wa Shetani. Huu ni ukweli kabisa. Kwa hivyo, mwanadamu anaishi miongoni mwa tabia ambayo imepotoshwa kabisa na Shetani na mwanadamu hana njia ya kujua utakatifu wa Mungu ni nini na kiini cha Mungu ni nini. Hii ni kwa sababu juujuu mtu hawezi kupata dosari kwa njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu; hakuna anayeweza kuamua kutoka kwa tabia ya mtu kwamba kuna chochote kibaya. Kila mtu anaendelea na kazi yake kwa kawaida na kuishi maisha ya kawaida; wanasoma vitabu na magazeti kwa kawaida, wanasoma na kuzungumza kwa kawaida; watu wengine hata wamejifunza kuwa na sura ya kinafiki ya maadili ili waweze kusema salamu zao, kuwa na heshima, kuwa na adabu, kuwaelewa wengine, kuwa na urafiki, kuwasaidia wengine, kuwa wenye hisani, na wataepuka kulalamika kwa wengine na kuepuka kutumia watu kwa manufaa yao. Hata hivyo, tabia yao iliyopotoka ya kishetani imekita mizizi ndani yao; kiini hiki hakiwezi kubadilishwa kwa kutegemea juhudi za nje. Mwanadamu hana uwezo wa kujua utakatifu wa Mungu kwa sababu ya kiini hiki, na licha ya kiini cha utakatifu wa Mungu kuwekwa wazi kwa mwanadamu, mwanadamu hakichukulii kwa umakini. Hii ni kwa sababu Shetani tayari amemiliki kabisa hisia, fikira, mitazamo, na mawazo ya mwanadamu kupitia njia mbalimbali. Huu umiliki na upotovu si ya muda mfupi ama ya mara kwa mara; upo kila mahali na kila wakati. Kwa hivyo, watu wengi ambao wamemwamini Mungu kwa miaka mitatu au minne—hata miaka sita na saba—bado wanashikilia mawazo na mitazamo ambayo Shetani amewaekea kana kwamba wanashikilia hazina. Kwa sababu mwanadamu ameukubali uovu, kiburi, na asili ya kijicho ya Shetani, bila kuepukika kwa mahusiano ya ana kwa ana ya mwanadamu mara nyingi kuna migogoro, mara nyingi kuna magombano na kutokuwa na uwiano, mambo ambayo yameumbwa kwa sababu ya asili ya kiburi ya Shetani. Iwapo Shetani angempa mwanadamu vitu vyema—kwa mfano, iwapo Uconfucius na Udao wa desturi ya kitamaduni ambayo mwanadamu alikubali ilichukuliwa kuwa vitu vizuri—watu wa aina sawa wanapaswa kuweza kupatana na wengine baada ya kukubali vitu hivyo, siyo? Hivyo mbona kuna mgawanyiko mkubwa kati ya watu waliokubali vitu sawa? Mbona hivyo? Ni kwa sababu viti hivi vimetoka kwa Shetani na Shetani husababisha mgawanyiko miongoni mwa watu. Vitu ambavyo Shetani anapatiana, bila kujali jinsi vinavyoonekana kuwa vya heshima na vikubwa juujuu, vinamletea mwanadamu na vinaleta katika maisha ya mwanadamu kiburi pekee, na si chochote ila ujanja wa asili ovu ya Shetani. Sivyo? Mtu ambaye angeweza kujificha, kumiliki maarifa mengi, ama kuwa na malezi mazuri angekuwa na wakati mgumu kusitiri tabia yao potovu ya kishetani. Haijalishi mtu huyu atajificha kwa njia ngapi, kama ulimfikiri kuwa mtakatifu, ama kama ulifikiri ni mkamilifu, ama kama ulifikiri ni malaika, haijalishi ulifikiri ni mtu safi vipi, maisha yake yangekuwaje nyuma ya pazia? Utaona asili ipi katika ufunuo wa tabia yake? Bila shaka ungeona asili ovu ya Shetani. Mtu anaweza kusema hivyo? (Ndiyo.) Kwa mfano, tuseme mnamjua mtu wa karibu nanyi ambaye mnafikiri kuwa mtu mzuri, ama ulimfikiri kuwa mtu mzuri, pengine mtu uliyemwabudu kama Mungu. Kwa kimo chako cha sasa, unawafikiri vipi? Kwanza, unaangalia iwapo mtu wa aina hii ana ama hana ubinadamu, iwapo ni mwaminifu, iwapo ana upendo wa kweli kwa watu, iwapo maneno na vitendo vyao vinafaidi na kusaidia wengine. (La.) Yaitwayo wema, upendo na uzuri unaofichuliwa hapa, ni nini kweli? Yote ni sura ya kinafiki, yote ni uongo. Hii sura ya kinafiki ya nyuma ya pazia ina madhumuni maovu ya chinichini: Ni ya kumfanya mtu huyo apendwe na kuabudiwa kama Mungu. Je, mnaona jambo hili kwa dhahiri? (Ndiyo.)
Mbinu ambazo Shetani anatumia kuwapotosha watu zinaletea nini binadamu? Kuna chochote chema kuzihusu? (La.) Kwanza, mwanadamu anaweza kutofautisha kati ya mema na mabaya? (La.) Unaona, katika dunia hii, awe ni mtu fulani mkubwa ama gazeti fulani, ama kituo fulani cha redio, yote yatasema kwamba hiki ama kile ni chema ama kibaya, si hayo ni barabara? (La.) Si hayo ni sahihi? (La.) Tathmini zao za matukio na watu ni za haki? (La.) Kuna ukweli ndani ya tathmini hizi? (La.) Je, dunia hii ama ubinadamu huu unatathmini vitu vyema na hasi kulingana na kiwango cha ukweli? (La.) Mbona watu hawana uwezo huo? Watu wamesoma maarifa mengi na wanajua mengi kuhusu sayansi, uwezo wao si mkubwa kutosha? Mbona hawawezi kutofautisha kati ya vitu vyema na hasi? Mbona hivi? (Kwa sababu watu hawana ukweli; sayansi na maarifa si ukweli.) Kila kitu Shetani anauletea ubinadamu ni uovu na upotovu na hakina ukweli, uhai, na njia. Na uovu na upotovu ambao Shetani anamletea mwanadamu, unaweza kusema kwamba Shetani ana upendo? Unaweza kusema kwamba mwanadamu ana upendo? Watu wengine wanaweza kusema: “Huko sahihi, kuna watu wengi duniani kote wanaosaidia maskini na watu wasio na makazi. Si hao ni watu wazuri? Pia kuna mashirika ya hisani ambayo yanafanya kazi nzuri, si kazi yote wanayofanya ni ya uzuri?” Kwa hivyo tunasema nini kuhusu hayo? Shetani anatumia mbinu na nadharia mbalimbali kumpotosha mwanadamu; huu upotovu wa mwanadamu ni dhana isiyo dhahiri? La, siyo dhahiri. Shetani pia anafanya vitu vingine vya utendaji, vikiwemo baadhi ya vitu vya uongo vinavyojifanya kuwa vitu vizuri, na pia vitendo vya udanganyifu kabisa, ambavyo Shetani anafanya na nia na madhumuni yake mwenyewe. Watu waliopotoshwa na Shetani ni kitu kimoja; pia wako katika dunia hii na katika jamii wakikuza mtazamo ama nadharia. Katika kila nasaba na katika kila kipindi cha historia wanakuza nadharia na kuingiza baadhi ya fikira ndani ya wanadamu. Fikira na nadharia hizi polepole zinakita mizizi katika mioyo ya watu, na kisha watu wanaanza kuishi kwa nadharia na fikira hizi; si wanakuwa Shetani bila kusudi? Si watu wako kitu kimoja na Shetani? Wakati watu wamekuwa kitu kimoja na Shetani, ni nini mtazamo wao kwa Mungu mwishowe? Si ni mtazamo sawa ambao Shetani anao kwa Mungu? Hakuna anayethubutu kukubali haya, siyo? Ni ya kutisha sana! Watu ni Shetani, na asili yao ni ile asili ya Shetani. Mbona Nasema kwamba asili ya Shetani ni ovu? Hii inaamuliwa na kuchambuliwa kulingana na kile Shetani amefanya na vitu ambavyo Shetani amefichua; si bila ustahili kusema kwamba Shetani ni mwovu. Iwapo Ningesema tu kwamba Shetani ni mwovu, mngefikiri nini? Mngefikiri, “Bila shaka Shetani ni mwovu.” Hivyo nitakuuliza: “Ni kipengele kipi cha Shetani ni ovu?” Ukisema: “Shetani kumpinga Mungu ni uovu,” bado hutakuwa ukizungumza kwa uwazi. Sasa tumesema mambo maalum kwa njia hii; je, mna uelewa kuhusu maudhui maalum ya kiini cha uovu wa Shetani? (Ndiyo.) Sasa kwa kuwa mmekuwa na huu uelewa wa asili ovu ya Shetani, ni kiasi gani mnaelewa kuhusu nyinyi wenyewe? Je, mambo haya yanahusiana? (Ndiyo.) Je, uhusiano huu unawaumiza? (La.) Ni wenye msaada kwenu? (Ndiyo.) Ni wenye msaada vipi? (Msaada mkubwa sana!) Hebu tuzungumzie mambo maalum; Sitasikia maneno yenye maana nyingi. Ni kwa kiasi kipi “mkubwa sana” kinarejelea? (Tunajua vitu ambavyo Mungu anachukia, vitu vipi vinaenda kinyume na Mungu; mioyo yetu inaelewa kiasi kuhusu vitu hivi.) Mm, kuna kitu kingine cha kuongezea? Ninaposhiriki kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, ni muhimu Niwe na ushirika kuhusu kiini ovu cha shetani, ni nini maoni yako? (Ndiyo, ni muhimu.) Mbona? (Uovu wa Shetani unauweka utakatifu wa Mungu katika heshima ya juu.) Je, ndivyo ilivyo? Hii ni sahihi kidogo kwa sababu bila uovu wa Shetani, watu hawatajua kuhusu utakatifu wa Mungu; hii ni sahihi. Hata hivyo, ukisema kwamba utakatifu wa Mungu upo tu kwa sababu ya tofauti yake na uovu wa Shetani, hii ni sahihi? Hii hoja si sahihi. Utakatifu wa Mungu ni kiini kiasilia cha Mungu; hata ingawa Mungu anaufichua ama kutenda, Anayo hiki kiini kiasilia na kinafichuliwa kiasili, ni cha Mungu Mwenyewe na daima kimekuwepo, lakini mwanadamu hawezi kukiona. Mwanadamu anaishi miongoni mwa tabia potovu ya Shetani na miongoni mwa kiini chake potovu, na mwanadamu hajui kuhusu utakatifu ama maudhui maalum ya utakatifu wa Mungu. Si hii ni sahihi? Hivyo, unaona ikiwa muhimu kwamba tushiriki kwanza kuhusu kiini ovu cha Shetani? (Ndiyo, ni muhimu.) Unaona, tumeshiriki kuhusu vipengele vingi vya upekee wa Mungu na hatukutaja kiini cha Shetani, siyo? Watu wengine wanaweza kuonyesha baadhi ya shaka kama, “Unashiriki kuhusu Mungu Mwenyewe, mbona Unazungumza daima kuhusu jinsi Shetani anawapotosha watu na jinsi asili ya Shetani ni ovu?” Umeyaweka mapumzikoni mashaka haya? (Ndiyo.) Uliyawekaje mapumzikoni? (Kupitia ushirika wa Mungu, tulitofautisha kile ambacho ni ovu.) Wakati watu wana utambuzi wa uovu na wakati wana ufafanuzi sahihi wa uovu, wakati watu wanaweza kuona wazi maudhui maalum na udhihirisho wa uovu, chanzo na kiini cha uovu—wakati utakatifu wa Mungu unajadiliwa sasa—watu basi watatambua wazi, ama kuufahamu wazi kama utakatifu wa Mungu, kama utakatifu wa kweli. Nisipojadili uovu wa Shetani, watu wengine wataamini kimakosa kwamba kitu fulani ambacho watu wanafanya katika jamii ama miongoni mwa watu—ama kitu fulani katika dunia hii—kinaweza kuhusiana na utakatifu. Si mtazamo huu ni wa makosa? (Ndiyo.) Hivi, Nimeshiriki kuhusu kiini cha Shetani. Mmefikia uelewa upi wa utakatifu wa Mungu kupitia uzoefu wenu wa miaka ya hivi karibuni, kutokana na nyinyi kuona neno la Mungu na kutokana na kupitia kazi Yake? Endelea, na uuzungumzie. Si lazima utumie maneno yanayofurahisha sikio, zungumza tu kutoka kwa uzoefu wako mwenyewe, utakatifu wa Mungu ni upendo Wake tu? Ni upendo wa Mungu tu tunaoelezea kama utakatifu? Huo utakuwa wa upande mmoja sana, siyo? Si huo utakuwa wa upande mmoja? (Ndiyo.) Hivyo, mbali na upendo wa Mungu, kuna vipengele vingine vya kiini cha Mungu ambavyo mmeona? (Ndiyo.) Mmeona nini? (Mungu anachukia tamasha na likizo, mila, na ushirikina; huu ni utakatifu wa Mungu.) Ulisema tu kwamba Mungu anachukia mambo fulani; Mungu ni mtakatifu kwa hivyo Anachukia vitu, inamaanisha hivyo? (Ndiyo.) Katika mizizi ya hayo, ni nini utakatifu wa Mungu? Utakatifu wa Mungu hauna maudhui makubwa, ni kwamba tu Anachukia vitu? Katila akili zenu mnafikiria, “Kwa sababu Mungu anachukia vitu hivi ovu, hivyo mtu anaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu”? Si huu ni uvumi hapa? Si hii ni aina ya dhana na hukumu? Ni nini mwiko mkubwa zaidi inapokuja kwa kuelewa kiini cha Mungu? (Kuacha ukweli nyuma.) Ni wakati tunaacha ukweli nyuma kuzungumza kuhusu mafundisho ya kidini, huu ni mwiko mkubwa sana kufanya. Kitu kingine? (Uvumi na ubunifu.) Uvumi na ubunifu, huu pia ni mwiko wa nguvu sana. Mbona uvumi na ubunifu si wa manufaa? Vitu unavyobashiri kuhusu na kufikiria vitu ambavyo kweli unaweza kuona? (La.) Ni kiini cha kweli cha Mungu? (La.) Nini tena ni mwiko? Ni mwiko kuhesabu tu kifungu cha maneno yanayosikika kuwa mazuri kuhusu kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Si huku ni kujigamba na upuuzi? Hukumu na uvumi ni upuuzi, kama tu kuchukua maneno yanayosikika kuwa mazuri. Kuna kingine tena? Sifa tupu pia ni upuuzi, siyo? (Ndiyo.) Je, Mungu anafurahia kusikiza watu wakisema upuuzi wa aina hii? (La, hafurahii.) Ni nini kisawe cha “kutofurahia” kitu? (Kuhisi kutostareheka.) Anahisi kutostareheka kusikia huu upuuzi! Mungu anaongoza na kuokoa kundi la watu, na baada ya kundi hili la watu kusikia maneno Yake hawaelewi Anachomaanisha. Mtu anaweza kuuliza: “Mungu ni mwema?” na wangejibu, “Mwema!” “Mwema vipi?” “Mwema sana sana!” “Mungu anampenda mwanadamu?” “Ndiyo!” “Kiasi gani?” “Sana, sana zaidi!” “Unaweza kuelezea upendo wa Mungu?” “Ni wa kina zaidi kuliko bahari, wa juu zaidi kuliko anga!” Si huu ni upuuzi? Si huu upuuzi ni sawa na kile mlichotoka kusema kuhusu, “Mungu anachukia tabia potovu ya Shetani, hivyo Mungu ni mtakatifu”? (Ndiyo.) Si kile mlichotoka kusema ni upuuzi? Mengi ya haya mambo ya upuuzi yanayosemwa yanatoka wapi? (Shetani.) Yanatoka kwa Shetani. Mambo ya upuuzi yanayosemwa kimsingi yanatoka kwa kutowajibika kwa watu na kutomheshimu Mungu. Tunaweza kusema hayo? (Ndiyo.) Hukuwa na uelewa wowote lakini bado uliongea upuuzi, si huku ni kutowajibika? Si ni kutomheshimu Mungu? Umesoma kiasi kidogo cha maarifa, umeelewa kiasi kidogo cha kufikiria, na kiasi kidogo cha mantiki, ambayo umetumia hapa na, zaidi, umefanya hivyo ukimjua Mungu. Unafikiri Mungu anahisi kutostareheka kuyasikia hayo? Mnawezaje kumjua Mungu mkitumia mbinu hizi? Je, si hayo yanasikika kuwa ya kufedhehesha? Kwa hivyo, inapokuja kwa maarifa ya Mungu, mtu lazima awe makini sana; mahali unapojua Mungu, zungumza tu kuhusu hayo. Zungumza kwa uaminifu na kivitendo na usipambe maneno yako na pongezi za kawaida na usitumie sifa isiyostahilika; Mungu haihitaji na kitu kama hiki kinatoka kwa Shetani. Tabia ya Shetani ni ya kiburi na Shetani anapenda kupewa sifa isiyostahilika na kusikia maneno mazuri. Shetani ataridhishwa na kufurahia iwapo watu watataja maneno yote mazuri ambayo wamejifunza na kutumia maneno haya kwa Shetani. Lakini Mungu hahitaji hii; Mungu hahitaji kuvishwa kilemba cha ukoka ama sifa isiyostahilika na Hahitaji kwamba watu wazungumze upuuzi na kumsifu kwa upofu. Mungu anachukizwa sana na hata Hatasikiza sifa ambayo haiko sambamba na ukweli. Hivyo, wakati watu wengine wanamsifu Mungu kwa upofu na kile wanachosema hakilingani na kile kiko katika mioyo yao na wanapofanya viapo kwa upofu na kumwomba ovyo ovyo, Mungu hasikizi hata kidogo. Lazima uwajibike kwa kile unachosema. Ikiwa hujui jambo, sema tu; ikiwa unajua jambo, onyesha hivyo kwa njia ya kitendo. Sasa, kwa maudhui halisi ya utakatifu wa Mungu, mna uelewa maalum kuuhusu? Sasa hamtathubutu kusema vitu vya upuuzi, siyo? Hamwongei upuuzi, lakini hamwezi kuwacha kuongea, kwa hivyo mnapaswa kuwa na uelewa fulani, siyo? Mnafikiria jambo hili? Mnalishughulikia kwa makini, siyo? Unaweza kusema mambo machache sasa. (Nilipofichua uasi, nilipokuwa na makosa, nilipokea hukumu na kuadibu kwa Mungu, na hapo niliona utakatifu wa Mungu. Na nilipoanguka katika hali na mazingira ambayo hayakukubaliana na matarajio yangu, niliomba kuhusu mambo haya na kutafuta nia za Mungu na Mungu aliponipa nuru na kuniongoza na maneno Yake, niliona utakatifu wa Mungu.) Hmm, haya yametoka kwa uzoefu wako mwenyewe, siyo? (Wakati Mungu anawaongoza watu katika njia yote, na sababu anatawala watu, kwa hayo naona utakatifu wa Mungu. Kwa kweli, kwa kile ambacho Mungu ametoka kuzungumzia jinsi Shetani anampotosha mwanadamu na mwanadamu amekuwa akiishi chini ya upotovu na mateso ya Shetani, mwanadamu hana mamlaka juu ya haya, kwa kweli naona utakatifu wa Mungu kupitia kazi ya Mungu kwa mwanadamu.) (Nimeona kwa kile Mungu amezungumzia kwamba mwanadamu amepotoshwa na kudhuriwa na Shetani hivi. Hata hivyo, Mungu ametoa yote kutuokoa na kutoka haya naona utakatifu wa Mungu.) Hii ni njia ya kweli ya kuzungumza na ni maarifa ya kweli. Kuna maoni mengine tofauti na haya? (Sijui iwapo uelewa wangu ni sahihi au la. Katika ushirika ambao Mungu alikuwa na sisi hivi karibuni, naona uovu wa Shetani kwa mambo ambayo Shetani anasema na kufanya. Katika ushirika wa kwanza, alisema kwamba Mungu alimwambia mwanadamu kile alichoweza na asichoweza kula, na kwamba maneno ya Mungu yalifichua usafi na uwazi; kutoka kwa haya naona utakatifu wa Mungu. Hiki ni kile naweza kuongezea.) Mm. Kwa kile mmesikia watu hawa wakisema, mnasema Amina zaidi kwa maneno ya nani? Matamshi ya nani, ushirika wa nani ulikuwa karibu zaidi na ushirika wa mada yetu leo, ya nani ilikuwa ya kweli zaidi? Ushirika wa dada wa mwisho ulikuwa vipi? (Mzuri.) Unasema Amina kwa kile alichosema, ni nini alichosema kilichokuwa sahihi kwa lengo? Unaweza kuwa wazi, sema unachotaka kusema na usijali kuhusu kutokuwa sahihi. (Katika maneno ambayo dada alizungumza hivi karibuni, nilisikia kwamba neno la Mungu linaeleweka kwa urahisi na ni wazi sana, si kama maneno ya Shetani yasiyo ya moja kwa moja. Niliona utakatifu wa Mungu kwa haya.) Hmm, hii ni sehemu ya hayo. Je, nyote mlisikia kilichosemwa hivi karibuni? (Ndiyo.) Kilikuwa sahihi? (Ndiyo.) Hebu tumpigie dada makofi. Vizuri sana. Naona kwamba mmepata kitu katika ushirika hizi mbili za hivi karibuni, lakini lazima nyinyi mwendelee kufanya kazi kwa bidii. Ni lazima mfanye kazi kwa sababu kuelewa kiini cha Mungu ni somo kubwa sana; si kitu ambacho mtu anaweza kuelewa mara moja ama anaweza kuzungumza wazi kwa maneno machache tu.
Kila kipengele cha tabia potovu ya Kishetani ya watu, maarifa, filosofia, fikira na mitazamo ya watu, na vipengele binafsi vinawazuia pakubwa kujua kiini cha Mungu; hivyo mnapozisikia mada hizi, mada zingine zinaweza kuwa mbali kwenu kufikia, mada zingine pengine hamtaelewa, ilhali mada zingine pengine kimsingi hamtalingana nazo na hali halisi. Licha ya hayo, Nimesikia kuhusu uelewa wenu wa utakatifu wa Mungu na Najua kwamba katika mioyo yenu mmeanza kukubali kile Nilichosema na kushiriki kuhusu utakatifu wa Mungu. Najua kwamba katika mioyo yenu hamu yenu ya kuelewa kiini cha utakatifu wa Mungu imeanza kuchipuka. Lakini ni nini kinachonifanya kuwa na furaha zaidi? Ni kwamba wengine wenu tayari wanaweza kutumia maneno rahisi sana kuelezea maarifa yenu ya utakatifu wa Mungu. Ingawa hiki ni kitu rahisi kusema na Nimekisema awali, katika mioyo ya wengi wenu hii bado haijakubaliwa ama kuweka alama. Hata hivyo, wengine wenu wameweka maneno haya moyoni na ni vizuri kabisa na huu ni mwanzo mzuri sana. Natumai kwamba kwa mada ambazo mnafikiri kuwa za maana sana—ama kwa mada ambazo ziko mbali kwenu kufikia—mtaendelea kushiriki katika ushirika, na kufanya ushirika zaidi na zaidi. Kwa yale masuala ambayo yako mbali kwenu kufikia kutakuwa na mtu wa kuwapa mwongozo zaidi. Mkishiriki katika ushirika zaidi kuhusu maeneo ambayo mnaweza kufikia sasa, Roho Mtakatifu atafanya kazi Yake na mtakuwa na uelewa mkubwa zaidi. Kuelewa kiini cha Mungu na kujua kiini cha Mungu kinapeana msaada usioweza kupimika kwa kuingia kwa watu katika maisha. Natumai kwamba hamtapuuza haya ama kuyaona kama mchezo; kwa sababu kumjua Mungu ni msingi muhimu na msingi wa imani ya mwanadamu kwa Mungu na ufuatiliaji wa mwanadamu wa ukweli na wokovu na kitu ambacho hakifai kuachiliwa. Iwapo mwanadamu anamwamini Mungu lakini hamjui Mungu, na iwapo mwanadamu anaishi miongoni mwa baadhi ya barua na mafundisho ya kidini, hutawahi kufikia wokovu hata kama utatenda na kuishi kulingana na maneno ya juujuu ya ukweli. Hiyo ni kusema, iwapo imani yako kwa Mungu haitokani na kumjua, basi imani yako haimaanishi chochote. Unaelewa, sivyo? (Ndiyo, tunaelewa.) Ushirika wetu utaishia hapa kwa leo.
Januari 4, 2014
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni