1.27.2018

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Mwenyezi Mungu

Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VI

Utakatifu wa Mungu (III)

Mwenyezi Mungu alisema, Mnahisi vipi baada ya kusema sala zenu? (Tunafurahia na kuguswa sana.) Wacha tuanze ushirika wetu. Tulishiriki mada ipi wakati uliopita? (Utakatifu wa Mungu.) Na ni kipengele kipi cha Mungu Mwenyewe kinahusisha utakatifu wa Mungu? Je, kinahusisha kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo ni nini hasa mada inayohusiana na kiini cha Mungu? Je, ni utakatifu wa Mungu? (Ndiyo.) Utakatifu wa Mungu: hiki ni kiini cha kipekee cha Mungu. Ni nini ilikuwa dhamira kuu tuliyoshiriki wakati uliopita? (Kutambua uovu wa Shetani.) Na ni yapi tuliyoyashiriki wakati uliopita kuhusu uovu wa Shetani? Mnaweza kukumbuka? (Jinsi Shetani anampotosha mwanadamu. Anatumia maarifa, sayansi, desturi ya kitamaduni, ushirikina, na mienendo ya kijamii kutupotosha.) Sahihi, hii ndiyo ilikuwa mada kuu tuliyojadili wakati uliopita. Shetani hutumia maarifa, sayansi, ushirikina, desturi ya kitamaduni, na mienendo ya kijamii kumpotosha mwanadamu; hizi ndizo njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu. Hizi ni njia ngapi kwa jumla? (Tano.) Ni njia zipi tano? (Sayansi, maarifa, desturi ya kitamaduni, ushirikina, na mienendo ya kijamii.) Mnafikiri Shetani anatumia nini zaidi kumpotosha mwanadamu, kitu ambacho kinampotosha kwa kina zaidi? (Desturi ya kitamaduni.) Kaka na dada wengine wanadhani kwamba ni desturi ya kitamaduni. Kuna nyingine? (Maarifa.) Inaonekana kwamba mna kiwango cha juu cha maarifa. Kuna mengine zaidi? (Maarifa.) Mnashiriki mtazamo sawa. Kaka na dada waliosema desturi ya kitamaduni, mnaweza kutueleza mbona mnafikiri hivi? Je, mna uelewa wowote wa jambo hili? Je, hamtaki kueleza uelewa wenu? (Filosofia za Shetani na mafundisho ya Confucius na Mencius zimetopea sana katika akili zetu, kwa hivyo tunahisi kwamba haya yanatupotosha sana.) Wale wanaofikiria kwamba ni maarifa, mnaweza kueleza mbona? Semeni sababu zenu. (Maarifa hayawezi kuturuhusu kumwabudu Mungu. Yanapinga kuwepo kwa Mungu, na yanapinga kanuni ya Mungu. Yaani, maarifa yanatuambia tusome kuanzia umri mdogo, na kwamba ni kupitia tu kusoma na kupata maarifa ndipo siku zetu za baadaye na kudura zetu zinahakikishwa. Kwa njia hii yanatupotosha.) Kwa hivyo Shetani anatumia maarifa kudhibiti siku zako za baadaye na kudura yako, kisha anakuongoza kuendelea kupitia pua lako; hivi ndivyo unavyofikiria Shetani anampotosha mwanadamu kwa kina zaidi. Kwa hivyo wengi wenu wanafikiri Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu kwa kina. Kuna mengine zaidi? Je, sayansi na mienendo ya kjamii, kwa mfano? Kuna yeyote anayekubaliana na haya? (Ndiyo.) Leo Nitashiriki tena kuhusu njia tano ambazo Shetani anampotosha mwanadamu, na, baada ya Mimi kumaliza, Nitawauliza baadhi ya maswali ili kuona ni katika kipengele kipi hasa Shetani anampotosha mwanadamu kwa kina zaidi. Mnaelewa mada hii, siyo?
Upotovu wa Shetani wa mwanadamu unadhihirika kimsingi katika vipengele vitano; hivi vipengele vitano ni njia tano ambazo Shetani anampotosha mwanadamu. Ya kwanza kati ya njia hizi tano tulizotaja ni maarifa, kwa hivyo wacha kwanza tuchukue maarifa kama mada ya kushiriki. Shetani hutumia maarifa kama chambo. Sikiza kwa makini: Ni aina tu ya chambo. Watu wanavutiwa “kusoma kwa bidii na kuboreka kila siku,” kujihami kwa maarifa, kama silaha, kisha kutumia maarifa kufungua njia ya sayansi; kwa maneno mengine, kadri unapopata maarifa zaidi, ndivyo utavyoelewa zaidi. Shetani huwaambia watu haya yote. Shetani huwaambia watu kuwa na fikira za juu pia, kwa wakati sawa wanaposoma maarifa, akiwaambia kuwa na matarajio na maadili. Bila kujua kwa watu, Shetani anasambaza ujumbe mwingi kama huu, na kuwafanya watu kuhisi bila kujua kwamba vitu hivi ni sahihi, ama ni vya manufaa. Bila kujua, watu wanatembea njia ya aina hii, bila kujua wanaongozwa mbele na matarajio na maadili yao. Hatua kwa hatua, watu bila kujua wanajifunza kutoka kwa maarifa waliyopewa na Shetani kufikiria kwa watu wakubwa ama maarufu, na kukubali fikira hizi. Wanajifunza pia jambo moja baada ya lingine kutoka kwa matendo ya wengine ambao watu wanachukulia kuwa “mashujaa.” Mnaweza kujua baadhi ya yale ambayo Shetani anatetea kwa mwanadamu katika matendo ya hawa “mashujaa,” ama kile anachotaka kuingiza kwa mwanadamu. Ni kipi ambacho Shetani anaingiza kwa mwanadamu? Mwanadamu lazima awe mzalendo, awe na uadilifu wa kitaifa, na awe shujaa. Ni yapi ambayo mwanadamu anajifunza kutoka kwa baadhi ya hadithi za kihistoria ama kutoka kwa wasifu wa mashujaa? Kuwa na hisia ya uaminifu wa kibinafsi, ama kufanya lolote kwa ajili ya rafiki ya mtu ama kwa rafiki. Miongoni mwa maarifa haya ya Shetani, mwanadamu bila kujua anajifunza mambo mengi, na anajifunza mambo mengi hasi. Katikati ya kutojua huku, mbegu zilizotayarishwa kwa ajili yao na Shetani zinapandwa katika akili zao zisizokomaa. Mbegu hizi zinawafanya kuhisi kwamba wanapaswa kuwa watu wakubwa, wanapaswa kuwa maarufu, wanapaswa kuwa mashujaa, kuwa wazalendo, kuwa watu wanaopenda familia zao, ama kuwa watu wanaoweza kufanya chochote kwa ajili ya rafiki na kuwa na hisia za uaminifu wa kibinafsi. Baada ya kushawishiwa na Shetani, bila kujua wanatembea njia ambayo amewatayarishia. Wanapotembea njia hii, wanalazimika kukubali kanuni za Shetani za kuishi. Bila kujua na bila wao kuwa na uelewa kabisa, wanakuwa na kanuni zao za kuishi, wakati hizi si chochote ila kanuni za Shetani ambazo zimeingizwa kwao kwa nguvu. Wakati wa mchakato wa kujifunza, Shetani anawasababisha kukuza malengo yao wenyewe, kuamua malengo yao ya maisha wenyewe, kanuni za kuishi, na mwelekeo wa maisha, wakati huo wote anawaingizia mambo ya Shetani, kwa kutumia hadithi, kwa kutumia wasifu, kwa kutumia mbinu zote zinazowezekana kuwapata watu, kuchukua chambo polepole. Kwa njia hii, watu wanakuwa na mambo yao ya kupitisha muda na shughuli katika mkondo wa kujifunza kwao: Wengine wanakuja kupenda fasihi, wengine uchumi, wengine unajimu ama jiografia. Kisha kuna wengine wanaokuja kupenda siasa, wengine wanaopenda fizikia, wengine kemia, na hata wengine wanaopenda theolojia. Haya yote ni sehemu ya maarifa na nyote mmepatana nayo. Katika mioyo yenu, kila mmoja wenu anajua yalivyo na mambo haya, kila mmoja amepatana nayo awali. Kuhusiana na maarifa ya aina hii, yeyote anaweza kuzungumza bila kikomo kuhusu moja yao fulani. Na hivyo ni wazi jinsi maarifa haya yameingia kwa kina katika akili ya mwanadamu, inaonyesha nafasi iliyochukuliwa na maarifa haya katika akili ya mwanadamu na jinsi yalivyo na athari ya kina kwa mwanadamu. Punde tu mtu anapenda sehemu ya maarifa, wakati katika moyo wake mtu amependa kwa dhati mojawapo, basi bila kujua anaendeleza maadili: Watu wengine wanataka kuwa watunzi, wengine wanataka kuwa waandishi, wengine wanataka kuwa na kazi kutokana na siasa, na wengine wanataka kushiriki katika uchumi na kuwa wanabiashara. Kisha kuna kundi la watu ambao wanataka kuwa mashujaa, kuwa wakubwa ama maarufu. Bila kujali mtu anataka kuwa mtu wa aina gani, lengo lake ni kuchukua mbinu hii ya kujifunza maarifa na kuitumia kwa ajili yake, kufikia matamanio yake, maadili yake mwenyewe. Haijalishi inasikika kuwa nzuri namna gani—anataka kufikia ndoto yake, asiishi katika maisha haya bure, ama anataka kushiriki katika kazi—anakuza haya maadili na matarajio ya juu lakini, kimsingi, yote ni ya nini? Je, mmeyafikiria haya awali? Mbona Shetani anataka kufanya hivi? Madhumuni ya Shetani ni yapi, kuyaweka mambo haya kwa mwanadamu? Mioyo yenu lazima ielewe vizuri swali hili.
Sasa wacha tuzungumze kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu. Kutokana na yale tuliyoyazungumzia hadi sasa, mmeanza kutambua malengo husuda ya Shetani? (Kidogo.) Mbona Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu? Anataka kufanya nini kwa mwanadamu kutumia maarifa? Kumwongoza mwanadamu kufuata njia ya aina ipi? (Kumpinga Mungu.) Bila shaka ni kumpinga Mungu. Hii ni athari unayoweza kuona kwa watu wanaojifunza maarifa, na matokeo unayoyaona baada ya kujifunza kwa maarifa—kumpinga Mungu. Hivyo ni nini malengo husuda ya Shetani? Hujayaelewa, sio? Katika mchakato wa mwanadamu kujifunza maarifa, Shetani atatumia mbinu zozote ili watu waridhishe tamaa yao wenyewe na kutambua maadili yao. Je, uko wazi kuhusu njia hasa anayotaka Shetani kukuongoza? Bila kutia chumvi, watu wanafikiri kwamba hakuna chochote kibaya na kujifunza maarifa, kwamba ni mkondo wa kiasili. Wanafikiri kwamba kukuzaa maadili ya juu ama kuwa na matarajio kunaitwa tu kuwa na hamu ya kupata, na kwamba hii inapaswa kuwa njia sawa ya watu kufuata katika maisha. Iwapo watu wanaweza kupata maadili yao wenyewe, ama kuwa na kazi maishani—je, si ni adhimu zaidi kuishi namna hii? Sio tu kuheshimu babu za mtu kwa njia hiyo bali pia kuacha alama yako katika historia—hili si jambo zuri? Hili ni jambo zuri na linalofaa katika macho ya watu wa kidunia. Je, Shetani, hata hivyo, na malengo yake husuda, anawapeleka watu kwa njia ya aina hii na kisha kuamua amemaliza? Bila shaka la. Kwa kweli, haijalishi jinsi yalivyo juu maadili ya mwanadamu, haijalishi matamanio ya mwanadamu ni ya uhalisi jinsi gani ama jinsi yote yanaweza kuwa ya kufaa, yote ambayo mwanadamu anataka kufikia, yote ambayo mwanadamu anatafuta yameunganishwa bila kuchangulika na maneno mawili. Haya maneno mawili ni muhimu sana kwa maisha ya kila mtu, na haya ni mambo ambayo Shetani ananuia kuingiza ndani ya mwanadamu. Maneno haya mawili ni yapi? Moja ni “umaarufu” na nyingine ni “faida”: Ni umaarufu na faida. Shetani anatumia njia ya hila sana, njia ambayo iko pamoja sana na dhana za watu; si aina ya njia kali. Katikati ya kutoelewa, watu wanakuja kukubali njia ya Shetani ya kuishi, kanuni zake za kuishi, kuanzisha malengo ya maisha na mwelekeo wao katika maisha, na kwa kufanya hivyo wanakuja pia bila kujua kuwa na maadili katika maisha. Haijalishi maadili haya yanaonekana kusikika kuwa ya juu kiasi gani katika maisha, ni kisingizio tu ambacho kinahusiana kwa kutochangulika kwa umaarufu na faida. Mtu yeyote aliye mkubwa ama maarufu, watu wote kwa hakika, chochote wanachofuata maishani kinahusiana tu na haya maneno mawili: “umaarufu” na “faida.” Sivyo? (Ndiyo.) Watu hufikiri kwamba punde tu wanapata umaarufu na faida, wanaweza basi kuyatumia kwa faida yao kufurahia hadhi ya juu na utajiri mwingi, na kufurahia maisha. Baada ya wao kuwa na umaarufu na faida, wanaweza basi kuyatumia kwa faida yao katika kutafuta kwao raha na kufurahia kwao kwa fidhuli mwili. Watu kwa hiari, lakini bila kujua, wanachukua miili na akili zao na vyote walivyonavyo, siku zao za baadaye, na kudura zao na kuzikabidhi zote kwa Shetani ili kupata umaarufu na faida wanayotaka. Watu hufanya hivi kamwe bila kusita kwa muda, kamwe bila kujua haja ya kupata tena yote. Je, watu bado wanaweza kujidhibiti baada ya wao kwenda upande wa Shetani kwa njia hii na kuwa mwaminifu kwake? Bila shaka, la. Wanadhibitiwa na Shetani kikamilifu na kabisa. Hawawezi kikamilifu na kabisa kujinusuru kutoka kwa bwawa ambamo wamezama ndani. Baada ya mtu kukwama katika umaarufu na faida, hatafuti tena kile kilichong’aa, kile chenye haki ama yale mambo ambayo ni mazuri na mema. Hii ni kwa sababu nguvu za ushawishi ambazo umaarufu na faida yanayo juu ya watu ni kubwa mno, na vinakuwa vitu vya watu kutafuta katika maisha yao yote na pia milele bila kikomo. Hili silo ukweli? Watu wengine watasema kwamba kujifunza maarifa si chochote zaidi ya kusoma vitabu ama kujifunza mambo kadhaa ambayo hawajui tayari, wakisema kwamba wanafanya hivi ili wasiwe nyuma ya nyakati ama wasiwachwe nyuma na dunia. Watasema kwamba maarifa yanafunzwa tu ili waweke chakula mezani, kwa sababu ya siku zao za baadaye ama kwa sababu ya mahitaji ya kimsingi. Sasa unaweza kuniambia iwapo kuna mtu yeyote ambaye atastahimili mwongo wa kusoma kwa bidii kwa mahitaji ya kimsingi tu, ili kutatua swala la chakula tu? (La, hakuna.) Hakuna watu kama hawa! Kwa hivyo ni nini anatesekea matatizo haya na kutesekea miaka hii yote? Ni kwa sababu ya umaarufu na faida: Umaarufu na faida yanamgoja mbele, yanamwita, na anaamini tu kwa kupitia bidii yake mwenyewe, matatizo na mapambano ndiyo anaweza kufuata ile njia na hivyo kupata umaarufu na faida. Lazima ateseke matatizo haya kwa sababu ya njia yake ya siku za baadaye, kwa sababu ya raha yake ya siku za baadaye na kwa sababu ya maisha bora. Mnaweza kuniambia haya yanayoitwa maarifa kwa hakika ni nini? Si kanuni za kuishi na njia ya kupitia maisha iliyoingizwa kwa watu na Shetani, iliyofundishwa kwao na Shetani katika kujifunza kwao maarifa? Je, si maadili ya juu ya maisha yaliyoingizwa kwa mwanadamu na Shetani? Chukua, kwa mfano, mawazo ya watu wakubwa, uadilifu wa watu maarufu ama roho jasiri ya watu mashujaa, ama chukua uungwana na wema wa nguli na wenye panga katika riwaya za kareti; mawazo haya yanashawishi kizazi kimoja baada ya kingine, na watu wa kila kizazi wanaletwa kuyakubali mawazo haya, kuishi kwa sababu ya mawazo haya na kuyafuata bila kikomo. Hii ndiyo njia, mbinu, ambayo Shetani anatumia maarifa kumpotosha mwanadamu. Kwa hivyo baada ya Shetani kuwaongoza watu kwa njia ya umaarufu na faida, inawezekana wao kumwamini Mungu bado, kumwabudu Yeye? (La, haiwezekani.) Je, maarifa na kanuni za kuishi zilizoingizwa kwa mwanadamu na Shetani zina fikira yoyote ya kumwabudu Mungu? Zina fikira yoyote ya ukweli? (La, hazina.) Je, zina uhalisi wowote wa kumcha Mungu na kuepuka uovu. (La, hazina.) Mnaonekana kuongea kwa uhakika kidogo, lakini haijalishi. Tafuteni ukweli kwa mambo yote na mtapata majibu sahihi; ni kwa majibu sahihi tu mnaweza basi kutembea njia sahihi.
Wacha turejelee tena kwa ufupi: Shetani hutumia nini kuendelea kumfungia mwanadamu na kumdhibiti? (Umaarufu na faida.) Kwa hivyo Shetani hutumia umaarufu na faida kudhibiti fikira za mwanadamu hadi anachofikiria tu ni umaarifa na faida. Wanapambana kwa sababu ya umaarufu na faida, wanateseka matatizo kwa sababu ya umaarufu na faida, wanastahimili udhalilishaji kwa sababu ya umaarufu na faida, wanatoa kila kitu walichonacho kwa sababu ya umaarufu na faida, na watafanya maoni au uamuzi wowote kudumisha na kupata umaarufu na faida. Kwa njia hii, Shetani humfunga mwanadamu kwa pingu zisizoonekana. Pingu hizi zinabebwa katika miili ya watu, na hawana nguvu ama ujasiri wa kuzirusha mbali. Kwa hivyo watu kamwe wanatembea kwenda mbele kwa ugumu mkubwa, wakibeba pingu hizi bila kujua. Kwa ajili ya umaarufu na faida, binadamu hutenganishwa na Mungu na anamsaliti. Kwa kupita kwa kila kizazi, binadamu anakuwa mwovu zaidi na zaidi, mweusi wa moyo zaidi na zaidi, na hivyo kwa njia hii kizazi kimoja baada ya kingine kinaharibiwa katika umaarufu na faida ya Shetani. Tukiangalia sasa vitendo vya Shetani, ni nini hasa nia zake husuda? Ni wazi sasa, sivyo? Shetani si wa kuchukiza? (Ndiyo!) Pengine leo bado hamwezi kuona kupitia nia husuda za Shetani kwa sababu mnafikiri hakuna maisha bila umaarufu na faida. Mnafikri kwamba, iwapo watu wataacha umaarufu na faida nyuma, basi hawataweza tena kuona njia mbele, hawataweza tena kuona malengo yao, siku zao za baadaye zawa giza, zilizofifia na za ghamu. Lakini, polepole, nyote siku moja mtatambua kwamba umaarufu na faida ni pingu za ajabu ambazo Shetani hutumia kumfunga mwanadamu. Hadi ile siku utakuja kutambua hili, utapinga kabisa udhibiti wa Shetani na utapinga kabisa pingu anazoleta Shetani kukufunga. Wakati utakapofika wa wewe kutaka kutupilia mbali vitu vyote ambavyo Shetani ameingiza ndani yako, utakuwa basi umejiondoa kwa Shetani na pia utachukia kwa kweli vyote ambavyo Shetani amekuletea. Hapo tu ndipo utakuwa na upendo na shauku ya kweli kwa Mungu; hapo tu ndipo utaweza kutembea njia sahihi ya uhai katika ufuataji wa ukweli.
Tumetoka tu kuongea kuhusu jinsi Shetani hutumia maarifa kumpotosha mwanadamu, basi kinachofuata wacha tushiriki kuhusu jinsi Shetani hutumia sayansi kumpotosha mwanadamu. Kwanza, kwa kutumia sayansi kumpotosha mwanadamu, Shetani hutumia jina la sayansi kuridhisha kutaka kujua kwa mwanadamu, kuridhisha hamu ya mwanadamu [a]kutafiti sayansi na kuchunguza siri. Pia, katika jina la sayansi, Shetani huridhisha haja ya mwili na mahitaji ya mwanadmu kuendelea kuinua ubora wao wa maisha. Shetani hivyo, katika jina hili, hutumia njia ya sayansi kumpotosha mwanadamu. Je, ni kufikiria tu kwa mwanadamu ama akili za mwanadamu ambazo Shetani anapotosha kwa kutumia njia hii ya sayansi? Miongoni mwa watu na mambo katika mazingira yetu ambayo tunaweza kuona na ambayo tunakutana nayo, ni yapi mengine ambayo Shetani anatumia sayansi kupotosha? (Mazingira ya kiasili.) Mko sahihi. Inaonekana kwamba mmedhuriwa sana na hili, na pia mmeathirika sana na yeye. Mbali na kutumia sayansi kumdanganya mwanadamu, kutumia matokeo yote ya utafiti na mahitimisho mbalimbali ya sayansi kumdanganya mwanadamu, Shetani pia hutumia sayansi kama mbinu ya kutekeleza uangamizi na unyonyaji tele wa mazingira ya kuishi aliyopewa mwanadamu na Mungu. Anafanya hivi chini ya kisingizio kwamba iwapo mwanadamu anatekeleza utafiti wa kisayansi, basi mazingira ya kuishi ya mwanadamu yatakuwa bora na bora zaidi na viwango vya kuishi vya mwanadamu daima vitaboreka, na zaidi ya hayo kwamba maendeleo ya kisayansi yanafanywa ili kuhudumia mahitaji ya mwili ya mwanadamu yanayozidi kila siku na haja ya daima ya kuinua ubora wao wa maisha. Kama sio kwa sababu ya sababu hizi, basi huuliza kile unachofanya hata kuendeleza sayansi. Huu ni msingi wa kidhahania wa maendeleo ya Shetani ya sayansi. Sayansi, hata hivyo, ina matokeo yapi kwa binadamu? Mazingira yetu ya karibu kabisa yana nini? Si hewa ambayo binadamu hupumua imechafuliwa? Maji tunayoyanywa kweli bado ni safi? (La.) Basi, je, chakula tunachokula, kingi chake ni cha kiasili? (La.) Basi ni nini tena? Kinakuzwa kwa kutumia mbolea na kupaliliwa kwa kutumia vinasaba, na pia kuna mabadiliko yanayozalishwa kwa kutumia mbinu mbalimbali za sayansi, ili kwamba hata mboga na matunda tunayoyala sio ya kiasili tena. Si rahisi sasa kwa watu kupata mazao ya vyakula ambavyo havijabadilishwa kula. Hata mayai hayaonji yalivyokuwa yakionja awali, baada ya kusindikwa na inayoitwa sayansi na Shetani. Kwa kuangalia taswira kubwa, anga nzima imeharibika na kuchafuliwa; milima, maziwa, misitu, mito, bahari, na kila kitu juu na chini ya ardhi vyote vimeharibiwa na inayoitwa mafanikio ya kisayansi. Kwa maneno mengine, ikolojia nzima, mazingira yote ya kuishi yaliyopewa mwanadamu na Mungu yamechafuliwa na kuharibiwa na iitwayo sayansi. Ingawa kuna watu wengi waliopata walichotarajia katika suala la ubora wa maisha wanaotafuta, kuridhisha tamaa na miili yao, mazingira ambayo mwanadamu anaishi kimsingi yameharibiwa na kuangamizwa na “mafanikio” mbalimbali yaliyoletwa na sayansi. Hata nje ama katika nyumba zetu hatuna tena haki ya kupumua pumzi moja ya hewa safi. Wewe niambie, hii ni huzuni ya mwanadamu? Bado kuna furaha yoyote ya kuzungumzia kwa mwanadamu kuishi katika nafasi hii ya kuishi? Mwanadamu anaishi katika nafasi hii ya kuishi na, kutoka mwanzoni, haya mazingira ya kuishi yaliumbwa na Mungu kwa ajili ya mwanadamu. Maji ambayo watu hunywa, hewa ambayo watu hupumua, chakula ambacho watu hula, mimea, miti, na bahari—haya mazingira ya kuishi yote yalipewa mwanadamu na Mungu; ni asili, na hutekeleza kulingana na amri asili iliyotolewa na Mungu. Kama hakungekuwa na sayansi, na watu wangefurahia alichopewa mwanadamu kulingana na njia ya Mungu, wangekuwa na furaha na wangefurahia kila kitu kikiwa cha asili kabisa. Sasa, hata hivyo, haya yote yameangamizwa na kuharibiwa na Shetani; nafasi ya kimsingi ya kuishi ya mwanadamu haipo tena katika hali yake asili zaidi. Lakini hakuna anayeweza kutambua kilichosababisha matokeo ya aina hii ama jinsi haya yalikuja kuwa, na zaidi ya hapo hata watu zaidi wanaelewa na kukaribia sayansi kwa kutumia mawazo waliyoingiziwa na Shetani, na kwa kutazama sayansi kwa macho ya dunia. Je, hii si ya kuchukiza sana na ya kusikitisha? Kwa kuwa Shetani sasa amechukua nafasi ambamo wanadamu wapo na mazingira yao ya kuishi na kuwapotosha kuwa katika hali hii, na kwa kuwa wanadamu wanaendelea kwa njia hii, kuna haja yoyote ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu hawa duniani ambao wamepotoshwa sana na ambao wamekuwa maadui Wake? Kuna haja ya mkono wa Mungu kuwaangamiza wanadamu? (La.) Iwapo wanadamu watazidi kuendelea kwa njia hii, watachukua mwelekeo upi? (Uharibifu.) Wanadamu wataharibiwa vipi? Zaidi ya mwanadamu kutafuta kwa tamaa umaarufu na faida, daima anaendelea kutekeleza uchunguzi wa sayansi na utafiti wa kina, kisha bila kikomo huridhisha mahitaji yake ya mwili na tamaa; yapi tena ni matokeo ya mwanadamu? Kwanza kabisa hakuna tena usawa wa ikolojia na, pamoja na hili, miili ya wanadamu yote imetiwa doa na kuharibiwa na mazingira ya hali hii, na magonjwa mbalimbali ya kuambukiza, mapigo, na ukungu uliosambaa kila mahali. Hii ni hali ambayo mwanadamu sasa hawezi kudhibiti, sivyo? Sasa kwa sababu mnaelewa hili, iwapo wanadamu hawamfuati Mungu, lakini daima wanamfuata Shetani kwa njia hii—kutumia maarifa daima kujitajirisha, kutumia sayansi kuchunguza bila kikomo siku za baadaye za maisha ya binadamu, kutumia mbinu ya aina hii kuendelea kuishi—mnaweza kutambua hitimisho ya asili ya wanadamu itakuwa vipi? Matokeo ya mwisho asilia yatakuwa yapi? (Uharibifu.) Itakuwa uharibifu: kukaribia uharibifu hatua moja kwa wakati. Kukaribia uharibifu kwa hatua moja kwa wakati! Inaonekana sasa kama sayansi ni aina ya ushombwe ama sumu inayofanya kazi polepole ambayo Shetani amemwandalia mwanadamu, ili wakati mnapojaribu kupambanua mambo mnafanya hivyo katika hali ya ukungu; haijalishi mnaangalia kwa ugumu aje, hamwezi kuona mambo kwa wazi, na haijalishi mnajaribu sana vipi, hamwezi kuyatambua. Shetani, hata hivyo, bado anatumia jina la sayansi kuzidisha hamu yako na kukuongoza kwa pua, mguu mmoja mbele ya mwingine, kuelekea shimo na kuelekea kifo. Sivyo? (Ndiyo.) Hii ndiyo njia ya pili.
Suala la jinsi Shetani hutumia desturi ya kitamaduni kumpotosha mwanadamu pia linahitaji maelezo. Kuna usawa mwingi kati ya desturi ya kitamaduni na ushirikina, ni tu kuwa desturi ya kitamaduni ina hadithi fulani, vidokezo, na vyanzo fulani. Shetani ametunga na kuunda ngano ama hadithi nyingi katika vitabu vya historia, na kuacha watu na hisia za kina za desturi ya kitamaduni ama watu wa kishirikina. Chukua kwa mfano Watu Wanane Wasiokufa Wanaovuka Bahari, Safari ya kwenda Magharibi, Mfalme Mkuu Jade, Nezha Anamshinda Joka Mfalme, na Uchunguzi wa Miungu, zote za Uchina. Haya hayajakita mizizi katika akili za mwanadamu? Hata iwapo watu wengine hawajui maelezo yote, bado wanajua hadithi za jumla, na yaliyomo kwa jumla ndiyo yanayokwama katika moyo wako na yanakwama katika akili yako, na huwezi kuyasahau. Haya ni mambo ambayo Shetani alimwekea mwanadamu kitambo sana, baada ya kusambaza katika nyakati tofauti mawazo yake na filosofia zake mbalimbali za maisha. Haya mambo yanadhuru moja kwa moja na kumomonyoa nafsi za watu na kuweka watu chini ya fingo moja baada ya jingine. Hiyo ni kusema kwamba baada ya wewe kukubali mambo haya yanayotoka kwa desturi ya kitamaduni, hadithi ama ushirikina, baada ya mambo haya kuwekwa kwa akili yako, baada ya hayo kukwama katika moyo wako, ni kama tu apizo—unakamatwa na kushawishika na hizi tamaduni, haya mawazo na hadithi za kitamaduni. Yanashawishi maisha yako, mtazamo wako wa maisha na pia yanashawishi maoni yako ya mambo. Hata zaidi yanashawishi ufuataji wako wa njia sahihi ya maisha: Hii bila shaka ni apizo! Unajaribu lakini huwezi kuyatupilia mbali; unayakatakata lakini huwezi kuyakata chini; unayapiga lakini huwezi kuyapiga chini. Sivyo? (Ndiyo.) Zaidi ya hayo, baada ya mwanadamu bila kujua kuwekwa chini ya aina hii ya apizo, bila kujua, anaanza kumwabudu Shetani, kukuza taswira ya Shetani katika moyo wake. Kwa maneno mengine, anamweka Shetani kama sanamu, kifaa cha yeye kuabudu na kutazamia, hata kwenda mbali zaidi na kuichukulia kwa njia sawa ambayo wangemchukulia Mungu. Bila kujua, mambo haya yako katika mioyo ya watu yakidhibiti maneno na matendo yao. Bila kujua unakubali kuwepo kwa hadithi hizi, kuzitengenezea sanamu halisi, kuzibadili kuwa mambo halisi yaliyopo. Katika kutojua, unapokea haya mawazo bila kufahamu na kuwepo kwa vitu hivi. Pia unapokea bila kufahamu mashetani, Shetani na sanamu ndani ya nyumba yako na ndani ya moyo wako—hii bila shaka ni apizo. Je, mnahisi sawa? (Ndiyo.) Kuna yeyote miongoni mwenu ambao wamechoma ubani na kuabudu Budhaa? (Ndiyo.) Kwa hivyo madhumuni ya kuchoma ubani na kumwabudu Budhaa yalikuwa yapi? (Kuombea amani.) Je ni ujinga kuombea amani kutoka kwa Shetani? Shetani analeta amani? (La.) Kuifikiria sasa, mlikuwa wajinga hapo nyuma? (Ndiyo.) Namna ya aina hiyo ni ya upuuzi, jinga na nyofu, siyo? Shetani hawezi kukupa amani. Mbona? Shetani anafikiria tu jinsi ya kukupotosha na hawezi kukupa amani; anaweza tu kukupa nafasi ya kupumua ya muda mfupi. Lakini lazima uchukue kiapo na ukivunja ahadi yako ama ukivunja kiapo ulichofanya, basi utaona jinsi anavyokuadhibu. Kwa kukufanya uchukue kiapo, kwa kweli anataka kukudhibiti, sivyo? Wakati mlipoombea amani, mlipata amani? (La.) Hamkupata amani, lakini kinyume na hayo alileta bahati mbaya, majanga yasiyoisha na majanga mengi—kweli bahari isiyo na mipaka ya uchungu. Amani haiko miongoni mwa miliki ya Shetani, na hili ni ukweli. Haya ndiyo matokeo kwa wanadamu ya ushirikina wa kikabila na desturi ya kitamaduni.
Suala la Shetani kutumia kwa manufaa yake mienendo ya kijamii kumpotosha mwanadamu pia linahitaji maelezo maalum. Hii mienendo ya kijamii ina mambo mengi. Watu wengine husema: “Je, ni kuhusu nguo tunazovaa? Je, ni kuhusu mtindo wa karibuni, vipodozi, kutengeneza nywele na chakula cha kidomo? Je, ni kuhusu mambo haya? Hii ni sehemu ya mienendo, lakini hatutaki kuzungumzia haya hapa. Tunataka tu kuzungumza kuhusu mawazo ambayo mienendo ya kijamii inaleta kwa watu, jinsi inasababisha watu kutenda duniani, malengo ya maisha na mtazamo ambao inaleta kwa watu. Hii ni muhimu sana: inaweza kudhibiti na kushawishi hali ya akili ya mwanadamu. Moja baada ya nyingine, hii mienendo yote inabeba ushawishi mwovu unaoendelea kumpotosha mwanadamu, unaoshukisha maadili yao na ubora wao wa tabia zaidi na zaidi, hadi kwa kiwango ambamo tunaweza hata kusema wengi wa watu sasa hawana uadilifu, hawana ubinadamu, wala hawana dhamiri yoyote, wala akili yoyote. Hivyo mienendo hii ni ipi? Huwezi kuona mienendo hii kwa macho. Wakati upepo wa mwenendo unavuma, pengine ni idadi ndogo ya watu tu watakuwa waanzisha mitindo. Wanaanza kwa kufanya jambo la aina hii, kukubali wazo la aina hii ama mtazamo wa aina hii. Wengi wa watu, hata hivyo, katikati ya kutojua kwao, bado watazidi kuambukizwa, kufanywa wenyeji na kuvutia aina hii ya mwenendo, hadi wote bila kujua na bila kujitolea wanamkubali, na wote wanazama na kudhibitiwa na yeye. Kwa mwanadamu ambaye si wa mwili na akili timamu, ambaye kamwe hajui ukweli, ambaye hawezi kusema tofauti kati ya vitu vyema na hasi, mienendo ya aina hii moja baada ya nyingine inawafanya wote wawe radhi kukubali mienendo hii, mtazamo wa maisha, filosofia za maisha na maadili yatokayo kwa Shetani. Wanakubali anachowaambia Shetani juu ya jinsi ya kukaribia maisha na jinsi ya kuishi ambayo Shetani amewapa. Hawana nguvu, wala hawana uwezo, wala ufahamu wa kupinga. Kwa hivyo hii mienendo hasa ni nini? Nimechukua mfano rahisi ambao mnaweza kuja kuelewa. Kwa mfano, watu wa kale waliendesha biashara zao kwa njia ambayo haikudanganya wazee wala vijana, na ambayo iliuza bidhaa kwa bei sawa bila kujali aliyekuwa akinunua. Je, dokezo la dhamiri na ubinadamu haliwasilishwi hapa? Wakati watu walitumia aina hii ya imani walipokuwa wakifanya biashara zao, tunaweza kusema kwamba bado walikuwa na baadhi ya dhamiri, baadhi ya ubinadamu wakati huo? (Ndiyo.) Lakini na mahitaji ya mwanadamu ya kiasi kinachopanda daima cha pesa, watu bila kujua walikuja kupenda pesa, hupenda faida na hupenda raha zaidi na zaidi. Kwa hivyo watu walikuja kuona pesa kuwa muhimu zaidi? Wakati watu wanaona pesa kuwa muhimu zaidi, bila kujua wanapuuza sifa, umashuhuri wao, ufahari, na uadilifu wao; wanapuuza mambo haya yote, sivyo? Unapojihusisha katika biashara, unaona mtu mwengine akichukua mbinu tofauti na kutumia njia mbalimbali kuibia watu na kuwa tajiri. Ingawa pesa iliyopatwa ni faida iliyopatwa vibaya, wanakuwa tajiri zaidi na zaidi. Familia yao yote inajihusisha na biashara sawa na wewe, lakini wanafurahia maisha kukuliko, na unahisi vibaya, ukisema: “Mbona siwezi kufanya hivyo? Mbona siwezi kupata kama wapatavyo? Ni lazima nifikirie njia ya kupata pesa zaidi, kufanya biashara yangu kufanikiwa.” Kisha unafikiria hili. Kulingana na mbinu ya kawaida ya kutengeneza pesa, kutodanganya wazee wala vijana na kuuza vitu kwa bei sawa kwa wote, pesa unayotengeneza ni kwa dhamiri nzuri, lakini haiwezi kukufanya kuwa tajiri haraka. Hata hivyo, chini ya tamaa ya kutengeneza faida, kufikiria kwako kunapitia mabadiliko taratibu. Katika mabadiliko haya, kanuni zako za tabia pia zinaanza kubadilika. Wakati unamdanganya mtu kwa mara ya kwanza, unapomlaghai mtu kwa mara ya kwanza, una mashaka, ukisema “Hii ni mara ya mwisho namdanganya mtu na sitafanya hivyo tena. Siwezi kudanganya watu. Kudanganya watu kutapata tu adhabu na kutaleta majanga kwangu! Hii ni mara ya mwisho namdanganya mtu na sitafanya hivyo tena.” Unapomdanganya mtu kwa mara ya kwanza, moyo wako una aibu kiasi; hii ndiyo kazi ya dhamiri ya mwanadamu—kuwa na aibu na kukushutumu, ili ihisi kuwa siyo asili wakati unamdanganya mtu. Lakini baada ya wewe kufanikiwa kumdanganya mtu unaona kwamba sasa una pesa zaidi kuliko awali, na unafikiria mbinu hii inaweza kuwa ya manufaa sana kwako. Licha ya maumivu madogo ndani ya moyo wako, bado unahisi kujipongeza kwa “mafanikio” yako, na unahisi kuridhishwa kidogo na wewe mwenyewe. Kwa mara ya kwanza, unakubali tabia yako mwenyewe na unakubali uwongo wako mwenyewe. Baadaye, wakati mwanadamu amechafuliwa na kudanganya huku, ni sawa na mtu ambaye anahusika na kamari na kisha anakuwa mchezaji kamari. Katika kutoelewa, anapenda tabia yake ya kudanganya na anaikubali. Katika kutoelewa, anachukua kudanganya kuwa tabia halali ya kibiashara, na anachukua kudanganya kuwa mbinu ya manufaa zaidi ya kusalimika kwake na maisha yake; anafikiria kwamba kwa kufanya hivi anaweza kuwa tajiri haraka. Mwanzoni mwa mchakato huu watu hawawezi kukubali tabia ya aina hii, wanadharau tabia hii na njia hii ya kufanya mambo, hadi wanapoijaribu na kuijaribu kwa njia yao wenyewe, kibinafsi na moja kwa moja, na kisha mioyo yao inaanza kubadilika polepole. Kwa hivyo mabadiliko haya ni yapi? Ni kukubali na kukiri mwenendo huu, kukiri na kukubali wazo la aina hii lililoingizwa kwako na mwenendo wa jamii. Katika kutoelewa, unahisi kwamba usipodanganya katika biashara basi utapata hasara, kwamba usipodanganya basi utakuwa umepoteza kitu. Bila kujua, kudanganya huku kunakuwa nafsi yako, tegemeo kuu lako, na pia kunakuwa aina ya tabia ambayo ni kanuni isiyoweza kutupiliwa mbali katika maisha yako. Baada ya mwanadamu kukubali tabia hii na kufikiria huku, je, moyo wa mwanadamu unapitia mabadiliko? Moyo wako umebadilika, basi uadilifu wako umebadilika? Ubinadamu wako umebadilika? (Ndiyo.) Basi dhamiri yako imebadilika? (Ndiyo.) Uwepo wote wa mwanadamu unapitia mabadiliko bora, kutoka kwa mioyo yao hadi kwa mawazo yao, hadi kwa kiwango ambapo wanabadilika kutoka ndani hadi nje. Mabadiliko haya yanakuweka mbali na mbali zaidi kutoka kwa Mungu, na unakuwa na uafikiano zaidi na zaidi na Shetani, unakuwa sawa zaidi na zaidi na yeye.
Sasa mienendo hii ya kijamii ni rahisi kwako kuelewa. Nilichagua tu mfano rahisi, mfano unaoonekana kawaida ambao watu watakuwa wanajua. Hii mienendo ya kijamii ina ushawishi mkubwa kwa watu? (Ndiyo!) Kwa hivyo hii mienendo ya kijamii ina athari inayodhuru kwa kina kwa watu? (Ndiyo!) Athari ya kudhuru kwa kina kwa watu. Shetani hutumia moja ya mienendo hii ya kijamii baada ya nyingine kupotosha nini ya mwanadamu? (Dhamiri, akili, ubinadamu, maadili.) Nini tena? (Mtazamo wa mwanadamu wa maisha.) Je, inasababisha kuzorota polepole ndani ya watu? (Ndiyo.) Shetani hutumia hii mienendo ya kijamii kuvuta watu hatua moja baada ya nyingine hadi katika kiota cha mashetani, ili watu walionaswa katika mienendo ya kijamii bila kujua wanatetea pesa na tamaa za mwili, na pia kutetea uovu na ukatili. Punde mambo haya yameingia moyoni mwa mwanadamu, ni nini basi mwanadamu anakuwa? Mwanadamu anakuwa ibilisi Shetani! Hii ni kwa sababu ya mwelekeo kisaikolojia upi katika moyo wa mwanadamu? Ni kipi ambacho mwanadamu anatetea? Mwanadamu huanza kupenda uwovu na ukatili. Hawapendi uzuri ama wema, wala hata amani. Watu hawako radhi kuishi maisha rahisi ya ubinadamu wa kawaida, lakini badala yake wanataka kufurahia hadhi ya juu na utajiri mkubwa, kufurahia raha za mwili, na kutumia juhudi zote kuridhisha miili yao, bila vizuizi, hakuna vifungo vya kuwashikilia nyuma, kwa maneno mengine kufanya chochote wanachotaka. Hivyo wakati mwanadamu ametumbukizwa katika mienendo ya aina hii, maarifa ambayo wamefunzwa yanaweza kuwasaidia kuwa huru? Je, desturi ya kitamaduni na ushirikina wanayojua yanaweza kuwasaidia kutupilia mbali hii hatari ya kutisha? Je, maadili ya desturi na sherehe za desturi ambazo mwanadamu huelewa zinaweza kumsaidia kujizuia? Chukua Fasihi Bora ya Herufi Tatu, kwa mfano. Inaweza kusaidia watu kutoa miguu yao katika mchanga unaomeza wa mienendo hii?[b] (La, haiwezi.) Kwa njia hii, mwanadamu anakuwa nini zaidi na zaidi? Zaidi na zaidi mwovu, mwenye kiburi, mwenye kushusha hadhi, mwenye ubinafsi, na mwenye kijicho. Hakuna tena upendo kati ya watu, hakuna tena upendo wowote kati ya wanafamilia, hakuna tena uelewa wowote kati ya jamaa na marafiki; mahusiano ya binadamu yamejawa udanganyifu, yamejawa ukatili. Kila mtu anataka kutumia njia za udanganyifu na mbinu katili kuishi miongoni mwa wanadamu wenzake; wanadanganya, wanalaghai, na kuwa wakatili ili kukamata riziki zao; wanashinda vyeo vyao na kupata faida zao wenyewe kwa kutumia ukatili na wanafanya chochote watakacho kwa kutumia njia mbovu na katili. Si ubinadamu huu unatisha? (Ndiyo.) Baada ya kunisikia Nikiongea kuhusu vitu hivi sasa, hamfikiri kwamba inatisha kuishi miongoni mwa aina hii ya umati, katika dunia hii na katika mazingira haya ambayo Shetani amepotosha? (Ndiyo.) Kwa hivyo mmewahi kujihisi kuwa wenye kusikitisha? Lazima mnaihisi kiasi sasa. (Ndiyo.) Kwa kusikiza sauti zenu, inaonekana kana kwamba mnafikiria “Shetani hutumia njia nyingi mbalimbali kumpotosha mwanadamu. Anakamata kila fursa na yupo kila mahali tunageukia. Mwanadamu bado anaweza kuokolewa? Bado kuna matumaini kwa wanadamu? Wanadamu wanaweza kujiokoa? (La.) Je, Mfalme Mkuu wa Jade anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Confucius anaweza kumwokoa mwanadamu? Je, Guanyin Bodhisattva anaweza kumwokoa mwanadamu? (La.) Kwa hivyo ni nani anayeweza kumwokoa mwanadamu? (Mungu.) Watu wengine, hata hivyo, wataibua katika mioyo yao maswali kama: “Shetani anatudhuru kwa kiasi kikubwa sana, kwa hasira sana basi hatuna matumaini ya kuishi, wala imani katika kuishi. Sote tunaishi miongoni mwa upotovu na kila mtu anampinga Mungu hata hivyo, ili mioyo yetu sasa yote imekuwa baridi kabisa. Kwa hivyo wakati Shetani anatupotosha, Mungu yuko wapi? Mungu anafanya nini? Chochote Mungu anatufanyia kamwe hatukihisi!” Watu wengine wanapata hasara bila kuepukika, na bila kuepukika wanahisi kuvunjika moyo kiasi. Kwenu, kichocheo hiki, hisia hii ni ya kina sana kwa sababu vyote ambavyo Nimekuwa nikisema vimekuwa kuwafanya watu kuja kuelewa polepole, kuhisi zaidi na zaidi kwamba hawana matumaini, kuhisi zaidi na zaidi kwamba wameachwa na Mungu. Lakini usijali. Mada yetu ya kushiriki leo, “uovu wa Shetani,” siyo dhamira yetu ya kweli. Kuongea kuhusu kiini cha utakatifu wa Mungu, hata hivyo, lazima kwanza tuongee kuhusu jinsi Shetani anampotosha mwanadamu na uovu wa Shetani ili kuifanya kuwa wazi zaidi kwa watu, mwanadamu sasa yuko katika hali ya aina gani na ni kwa kiwango kipi hasa mwanadamu amepotoshwa. Lengo moja la kuongea juu ya hili ni kuruhusu watu kujua uovu wa Shetani, ilhali jingine ni kuwaruhusu watu kuelewa kwa kina zaidi utakatifu ni nini. Mnaelewa sasa, sivyo?
Je, haya mambo ambayo Nimeongea kuhusu hivi karibuni ni ya kina zaidi kuliko ya wakati uliopita? (Ndiyo.) Hivyo uelewa wenu sasa basi ni wa kina zaidi? (Ndiyo.) Najua kwamba sasa watu wengi wananitarajia kusema ni nini hasa utakatifu wa Mungu, lakini Ninapozungumza kuhusu utakatifu wa Mungu Nitaongea kwanza kuhusu matendo ambayo Mungu anafanya. Nyinyi nyote mnapaswa kusikiza kwa makini, kisha nitawauliza utakatifu wa Mungu ni nini hasa. Sitawaeleza moja kwa moja, lakini badala yake nitawaacha mjaribu kuutambua, kuwapa nafasi ya kuutambua. Mnafikiri nini kuhusu mbinu hii? (Ni nzuri.) Kwa hivyo sikizeni kwa makini.
Wakati wowote Shetani anampotosha mwanadamu ama anashughulika na madhara yasiyodhibitiwa, Mungu hasimami bila kazi, wala haweki kando ama kupuuza wale ambao amechagua. Yote ambayo Shetani anafanya ni wazi kabisa na yanaeleweka na Mungu. Haijalishi anachofanya Shetani, haijalishi mwenendo anaosababisha kuibuka, Mungu anajua yote ambayo Shetani anajaribu kufanya, na Mungu hawawachi wale ambao amechagua. Badala yake, bila kuvuta macho hata kidogo, kwa siri, kwa ukimya, Mungu anafanya yote yanayohitajika. Anapoanza kufanya kazi kwa mtu, wakati amemchagua mtu, Haambii yeyote, wala Hamwambii Shetani, wala hata kufanya maonyesho makubwa. Anafanya tu kwa ukimya, kwa asili kile ambacho kinahitajika. Kwanza, Anakuchagulia familia; usuli ambao hiyo familia inao, wazazi wako ni nani, mababu zako ni nani—haya yote tayari yaliamuliwa na Mungu. Kwa maneno mengine, haya hayakuwa uamuzi wa mvuto wa ghafla yaliyofanywa na Yeye, lakini badala yake hii ilikuwa kazi iliyoanza kitambo. Baada ya Mungu kukuchagulia familia, pia Anachagua tarehe ambayo utazaliwa. Kwa sasa, Mungu anaangalia unapozaliwa katika dunia hii ukilia, Anatazama kuzaliwa kwako, Anatazama unapotamka maneno yako ya kwanza, Anatazama unapoanguka na kutembea hatua zako za kwanza, ukijifunza kutembea. Kwanza unachukua hatua moja na kisha unachukua nyingine… sasa unaweza kukimbia, sasa unaweza kuruka, sasa unaweza kuongea, sasa unaweza kuonyesha hisia zako. Wakati huu, unapokua, macho ya Shetani yamewekwa kwa kila mmoja wenu, kama chui mkubwa mwenye milia anavyomwangalia nyara wake. Lakini kwa kufanya kazi Yake, Mungu hajawahi kuteseka mapungufu yoyote ya watu, matukio ama mambo, ya nafasi ama wakati; Anafanya kile anachopaswa kufanya na Anafanya kile Anacholazimika kufanya. Katika mchakato wa kukua, unaweza kukutana na mambo mengi ambayo hupendi, kukutana na magonjwa na kuvunjika moyo. Lakini unapotembea njia hii, maisha yako na bahati zako ziko chini ya ulinzi wa Mungu kabisa. Mungu anakupa hakikisho halisi litakalodumu maisha yako yote, kwani Yeye yuko kando yako, anakulinda na kukutunza. Bila kujua haya, unakua. Unaanza kukutana na mambo mapya na unaanza kujua dunia hii na wanadamu hawa. Kila kitu ni kipya kwako. Unapenda kufanya mambo yako na unapenda kufanya kile unachopenda. Unaishi katika ubinadamu wako mwenyewe, unaishi katika nafasi yako ya kuishi na huna hata kiasi kidogo cha mtazamo kuhusu kuwepo kwa Mungu. Lakini Mungu anakulinda katika kila hatua ya njia unapokua, na Anakutazama unapoweka kila hatua mbele. Hata unapojifunza maarifa, ama kusoma sayansi, Mungu hajawahi toka upande wako kwa hatua hata moja. Wewe ni sawa na watu wengine kwamba, katika harakati za kuja kujua na kukutana na dunia, umeanzisha maadili yako mwenyewe, una mambo yako mwenyewe ya kupitisha muda, mambo unayopenda mwenyewe, na pia unayo matamanio ya juu. Wakati mwingi unafikiria siku zako za baadaye, wakati mwingi ukichora muhtasari wa jinsi siku zako za baadaye zinapaswa kuwa. Lakini haijalishi kitakachofanyika njiani, Mungu anaona vyote na macho wazi. Labda wewe mwenyewe umesahau siku zako za nyuma, lakini kwa Mungu, hakuna anayeweza kukuelewa bora kumliko Yeye. Unaishi chini ya macho ya Mungu, unakua, unapevuka. Wakati huu, jukumu muhimu la Mungu ni kitu ambacho hakuna yeyote kamwe hufahamu, kitu ambacho hakuna yeyote anajua. Mungu hakika hakuambii kukihusu. Kwa hivyo hiki kitu muhimu ni nini? Je, mnajua? (Kuleta watu mbele Yake.) Kwa hivyo Mungu anafanya nini kuleta watu mbele Yake? Analeta watu mbele Yake wakati upi? Je, mnajua? Hii ni kazi muhimu zaidi ya Mungu? Hiki ni kitu muhimu zaidi ambacho Mungu anafanya? Tunaweza kusema kwamba ni hakikisho kwamba Mungu atamwokoa mtu. Hii inamaanisha kwamba Mungu anataka kumwokoa mtu huyu, kwa hivyo lazima Afanye hivi, na kazi hii ni muhimu sana kwa mwanadamu na Mungu. Je, mnajua hili? Inaonekana kwamba hamna hisia yoyote kuhusu hili, ama dhana yoyote kuhusu hili, kwa hivyo nitawaambia. Kutoka ulipozaliwa hadi sasa, Mungu amefanya kazi nyingi sana kwako, lakini Hakukwambia kila wakati Alifanya kitu. Haikuwa ujue, kwa hivyo hukuambiwa, sivyo? (Ndiyo.) Kwa mwanadamu, kila kitu anachofanya Mungu ni muhimu. Kwa Mungu, ni kitu ambacho lazima Afanye. Lakini katika moyo wake kuna kitu muhimu Anapaswa kufanya ambacho kinazidi yoyote ya mambo haya. Ni nini hicho? Yaani, kutoka ulipozaliwa hadi sasa, Mungu lazima ahakikishe usalama wa kila mmoja wenu. Mnaweza kuhisi kana kwamba hamwelewi kikamilifu, kusema “usalama huu ni muhimu sana?” Kwa hivyo ni nini maana halisi ya “usalama”? Labda mnauelewa kumaanisha amani ama pengine mnauelewa kumaanisha kutopitia maafa ama msiba wowote, kuishi vyema, kuishi maisha ya kawaida. Lakini katika mioyo yenu lazima mjue kwamba si rahisi hivyo. Kwa hivyo ni nini hasa kitu hiki ambacho Nimekuwa nikizungumzia, ambacho Mungu anapaswa kufanya? Kinamaanisha nini kwa Mungu? Kuna hakikisho lolote la usalama wenu? Kama sasa hivi? La. Kwa hivyo ni nini hiki ambacho Mungu anafanya? Usalama huu unamaanisha humezwi na Shetani. Je, jambo hili ni muhimu? Wewe humezwi na Shetani, kwa hivyo hili linahusisha usalama wako, au la? Hili linahusisha usalama wako binafsi, na hakuwezi kuwa na lolote muhimu zaidi. Baada ya wewe kumezwa na Shetani, nafsi yako wala mwili wako si vya Mungu tena. Mungu hatakuokoa tena. Mungu huacha nafsi kama hiyo na huacha watu kama hao. Kwa hivyo Nasema kitu muhimu sana ambacho Mungu anapaswa kufanya ni kuhakikishia usalama wako, kuhakikisha kwamba hutamezwa na Shetani. Hili ni muhimu kiasi, silo? Kwa hivyo mbona hamwezi kujibu? Inaonekana kwamba hamwezi kuhisi wema mkubwa wa Mungu!
Mungu anafanya mengi kando na kuhakikisha usalama wa watu, kuhakikisha kwamba hawatamezwa na Shetani; pia hufanya kazi nyingi sana kwa kutayarisha kumchagua mtu na kumwokoa. Kwanza, una tabia gani, utazaliwa kwa familia ya aina gani, wazazi wako ni nani, una kaka na dada wangapi, hali na hadhi ya kiuchumi ya familia yako ni gani, hali ya familia yako ni gani—haya yote yanapangiwa wewe kwa uangalifu na Mungu. Je, unajua ni familia ya aina gani watu waliochaguliwa na Mungu wanazaliwa ndani mara nyingi, kama inavyohusu watu wengi? Ni familia mashuhuri? Kunaweza kuwa na nyingine. Hatuwezi sema kwa uhakika hakuna yoyote, lakini kuna chache sana. Ni familia za utajiru wa kupindukia, kama yenye mabilioni ama yenye mamilioni nyingi? Mara nyingi huwa si aina hii ya familia. Kwa hivyo Mungu anapangia watu familia za aina gani zaidi? (Familia za kawaida.) Kwa hivyo familia za kawaida ni zipi? Sanasana ni familia zinazofanya kazi na familia za ukulima. Wafanyakazi wanategemea mishahara yao kuishi na wanaweza kumudu mahitaji ya kimsingi. Hawatakuruhusu kwenda njaa wakati wowote, lakini huwezi kutarajia mahitaji yote ya mwili kutoshelezwa. Wakulima wanategemea kupanda mazao kwa chakula yao, na wana nafaka za kula, na kwa vyovyote vile, hutakuwa na njaa, lakini huwezi kuwa na nguo nzuri sana. Tena kuna familia zingine ambazo zinashughulika katika biashara ama zinazoendesha biashara ndogondogo, na zingine ambazo wazazi ni wenye akili, na hizi zinaweza kuhesabika kama familia za kawaida. Kuna baadhi ya wazazi ambao ni wafanyakazi wa ofisi ama maafisa wadogo wa serikali kwa kiwango zaidi, ambazo haziwezi kuhesabika kama familia mashuhuri pia. Watu wengi zaidi wanazaliwa katika familia za kawaida, na haya yote yanapangiliwa na Mungu. Kusema kwamba, kwanza kabisa mazingira haya unayoishi si familia ya uwezo mkubwa ambayo unaweza kufikiria, lakini badala yake ni familia uliyoamuliwa na Mungu, na watu wengi wataishi katika mipaka ya aina hii ya familia; hatutazungumza mambo ya pekee hapa. Kwa hivyo je, hadhi ya kijamii? Hali ya uchumi ya wengi wa wazazi ni wastani na hawana hadhi ya juu ya kijamii—kwao ni vizuri tu kuwa na kazi. Kuna wowote walio magavana? Kuna wowote walio maraisi? (La.) Kwa zaidi ni watu kama mameneja wa biashara ndogo ama wakubwa wa muda mfupi, wote wakiwa na hadhi wastani ya kijamii, wote wakiishi katika hali wastani ya uchumi. Sababu nyingine ni mazingira ya kuishi ya familia. Kwanza kabisa, hakuna wazazi ambao wanaweza kushawishi kwa wazi watoto wao kutembea njia ya uaguzi na kupiga ramli; hawa pia ni wachache. Wazazi wengi ni wa kawaida kiasi na ni wa hali moja na nyinyi. Mungu anaweka mazingira ya aina hii kwa ajili ya watu wakati sawa na kuwachagua, na ni kwa manufaa sana ya kazi Yake ya kuokoa watu. Kwa nje, inaonekana kwamba Mungu hajafanya chochote kuu kwa mwanadamu; Anafanya kila kitu kwa siri tu, kwa unyenykevu na kwa kimya. Lakini kwa hakika, vyote ambavyo Mungu anafanya vinafanywa kuweka msingi wa wokovu wako, kuandaa njia mbeleni na kuandaa hali zote muhimu za wokovu wako. Mara moja wakati maalum wa kila mtu, Mungu anawarudisha mbele Yake—wakati unapofika kwako kusikia sauti ya Mungu, huo ndio wakati unapokuja mbele Yake. Wakati hili linafanyika, watu wengine wamekuwa wazazi tayari wenyewe, ilhali wengine ni watoto wa mtu tu. Kwa maneno mengine, watu wengine wameoa na kupata watoto ilhali wengine bado hawajaoa, na hawajaanza bado familia zao. Lakini licha ya hali za watu, Mungu tayari ameweka nyakati utakapochaguliwa na injili na maneno Yake yatakapokufikia. Mungu ameweka hali, ameamulia mtu fulani ama muktadha fulani ambamo injili itapitishwa kwako, ili uweze kusikia maneno ya Mungu. Mungu tayari amekuandalia hali zote muhimu ili, bila kujua, unakuja mbele Yake na unarudishwa kwa familia ya Mungu. Pia, bila kujua, unafuata Mungu na kuingia katika kazi Yake ya hatua kwa hatua, kuingia katika njia ya Mungu ya kazi ambayo, hatua kwa hatua amekuandalia. Mungu angalau anafanya na anampa mwanadamu wakati huu kwanza na kabisa utunzaji na ulinzi ambayo mwanadamu anafurahia, na hii bila shaka ni kweli. Kwa hivyo Mungu anatumia njia za aina gani? Mungu anaweka watu na vitu mbalimbali ili mwanadamu aweze kuona kuwepo Kwake na matendo Yake miongoni mwao. Kwa mfano, kuna watu wengine wanaomwamini Mungu kwa sababu mtu katika familia yao ni mgonjwa, na wanasema “Mmoja wa familia yangu ni mgonjwa, nitafanya nini? Watu wengine kisha wanasema “Mwamini Yesu!” Kwa hivyo wanaanza kumwamini Mungu, na imani hii kwa Mungu imekuja kwa sababu ya hali hii. Kwa hivyo ni nani aliyepangilia hali hii? (Mungu.) Kwa njia ya hali hii wanamwendea Mungu. Kuna familia zingine kama hii ambamo wote ni waumini, vijana na wazee, ilhali kuna zingine ambamo imani ni ya kibinafsi. Kwa hivyo Niambie, ni nini muumini anapata kutoka kwa Mungu? Inavyoonekana, ugonjwa unakuja, lakini kwa hakika ni hali aliyopewa yeye ili aje mbele ya Mungu—huu ni wema wa Mungu. Kwa sababu maisha ya familia ya watu wengine ni magumu na hawawezi kupata amani yoyote, fursa ya bahati inakuja ambapo mtu atapitisha injili na kusema “Familia yako ina magumu. Mwamini Yesu. Mwamini Yesu na utakuwa na amani.” Bila fahamu, mtu huyu basi anakuja kumwamini Mungu katika hali asili, kwa hivyo hii si aina ya hali? (Ndiyo.) Na je, familia yake kuwa na amani si neema aliyopewa na Mungu? (Ndiyo.) Kisha kuna wengine wanaokuja kumwamini Mungu kwa sababu zingine, lakini licha ya sababu inakuleta kumwamini Yeye, yote hakika yamepangwa na kuongozwa na Mungu, bila shaka.
Mwanzoni, Mungu alitumia njia mbalimbali kukuchagua na kukuleta katika familia Yake. Hili ni jambo la kwanza Anafanya na ni neema anampa kila mtu. Sasa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, Hampi tena mwanadamu neema na baraka tu kama Alivyofanya mwanzoni, wala halazimishi watu kwenda mbele—hii ni kwa sababu ya msingi wa kazi katika enzi ya Neema. Wakati wa kazi ya siku hizi za mwisho, ni nini mwanadamu ameona kutoka kwa vipengele hivi vyote vya kazi ya Mungu ambavyo wamepitia? Hawajaona tu upendo wa Mungu, lakini pia hukumu na kuadibu kwa Mungu. Kwa wakati huu, Mungu zaidi ya hayo, anamtegemeza, tia nuru, na kumwongoza mwanadamu, ili aje kujua nia Zake polepole, kujua maneno Anayozungumza na ukweli Anaompa mwanadamu. Wakati mwanadamu ni mnyonge, wakati amevunjika roho, wakati hana popote pa kugeukia, Mungu atatumia maneno Yake kufariji, kushauri na kuwatia moyo, ili mwanadamu wa kimo ndogo aweze kupata nguvu polepole, kuinuka kwa wema na kuwa radhi kushirikiana na Mungu. Lakini wakati mwanadamu hamtii Mungu ama anampinga Yeye, ama anapofichua upotovu wake na kumpinga Mungu, Mungu hataonyesha huruma kumrudi yeye na kumfundisha nidhamu. Kwa ujinga, kutojua, unyonge, na uchanga wa mwanadamu, hata hivyo, Mungu ataonyesha uvumilivu na ustahimilivu. Kwa njia hii, kupitia kazi yote Mungu anamfanyia mwanadamu, mwanadamu anapevuka, anakua na anakuja kujua nia za Mungu polepole, kujua baadhi ya ukweli, kujua ni nini mambo mema na ni nini mambo hasi, kujua uovu ni nini na kujua giza ni nini. Mungu hamrudi na kumfundisha nidhamu mwanadamu siku zote wala Haonyeshi uvumilivu na ustahimilivu siku zote. Badala yake anampa kila mtu kwa njia tofauti, katika hatua zao tofauti na kulingana na kimo na ubora wa tabia yao tofauti. Anamfanyia mwanadamu mambo mengi na kwa gharama kubwa; mwanadamu hafahamu lolote la gharama hii ama mambo haya Mungu anafanya, ilhali yote ambayo anafanya kwa kweli inafanywa kwa kila mtu. Upendo wa Mungu ni wa kweli: Kupitia neema ya Mungu mwanadamu anaepuka janga moja baada ya jingine, ilhali kwa unyonge wa mwanadamu, Mungu anaonyesha ustahimili wake muda baada ya muda. Hukumu na kuadibu kwa Mungu yanaruhusu watu kuja kutambua upotovu wa wanadamu polepole na kiini chao potovu cha kishetani. Kile ambacho Mungu anapeana, kutia nuru Kwake kwa mwanadamu na uongozi Wake yote yanawaruhusu wanadamu kujua zaidi na zaidi kiini cha ukweli, na kujua zaidi kile ambacho watu wanahitaji, njia wanayopaswa kuchukua, kile wanachoishia, thamani na maana ya maisha yao, na jinsi ya kutembea njia iliyo mbele. Haya mambo yote ambayo Mungu anafanya hayatengwi na lengo Lake la awali. Ni nini, basi lengo hili? Je, mnajua? Mbona Mungu anatumia njia hizi kufanya kazi Yake kwa mwanadamu? Anataka kutimiza matokeo gani? Kwa maneno mengine, ni nini ambacho anataka kuona kwa mwanadamu na kupata kutoka kwake? Kile ambacho Mungu anataka kuona ni kwamba moyo wa mwanadamu unaweza kufufuliwa. Kwa maneno mengine, njia hizi ambazo anatumia kufanya kazi kwa mwanadamu ni za kuamsha bila kikomo moyo wa mwanadamu, kuamsha roho ya mwanadamu, kumwacha mtu kujua alipotoka, ni nani anayemwongoza, kumsaidia, kumkimu, na ni nani ambaye amemruhusu mwanadamu kuishi hadi sasa; ni ya kuwacha mwanadamu kujua ni nani Muumbaji, ni nani wanapaswa kuabudu, ni njia gani wanapaswa kutembelea, na mwanadamu anapaswa kuja mbele ya Mungu kwa njia gani; yanatumika kufufua moyo wa mwanadamu polepole, ili mwanadamu ajue moyo wa Mungu, aelewe moyo wa Mungu, na aelewe utunzaji mkuu na wazo nyuma ya kazi Yake kumwokoa mwanadamu. Wakati moyo wa mwanadamu umefufuliwa, hataki tena kuishi maisha ya msherati, tabia potovu, lakini badala yake kutaka kutafuta ukweli kwa kuridhishwa kwa Mungu. Wakati moyo wa mwanadamu umeamshwa, anaweza basi kujinusuru kutoka kwa Shetani, kutoathiriwa tena na Shetani, kutodhibitiwa na kudanganywa na yeye. Badala yake, mwanadamu anaweza kushiriki katika kazi ya Mungu na katika maneno Yake kwa njia njema kuridhisha moyo wa Mungu, na hivyo kupata kumcha Mungu na kuepukana na uovu. Hili ndilo lengo la awali la kazi ya Mungu.
Kuzungumza kuhusu uovu wa Shetani hivi sasa kulimfanya kila mtu kuhisi kana kwamba watu huishi kwa huzuni sana na kwamba maisha ya mwanadamu yamejaa bahati mbaya. Lakini mnahisi vipi sasa kwani Nimezungumza kuhusu utakatifu wa Mungu na kazi ambayo anafanya kwa mwanadamu? (Furaha sana.) Tunaweza kuona sasa kwamba kila kitu Mungu anafanya, kila kitu ambacho anapanga kwa uangalifu kwa mwanadamu ni safi kabisa. Kila kitu anachofanya Mungu ni bila kasoro, kumaanisha ni bila dosari, hakihitaji yeyote kukosoa, kutoa mawaidha ama kufanya mabadiliko yoyote. Kila kitu ambacho Mungu anafanya kwa kila mtu hakina shaka; Anaongoza kila mtu kwa mkono, Anakuchunga kwa kila muda na Hajawahi kuondoka upande wako. Watu wanapokua katika mazingira haya na kukua na usuli wa aina hii, tunaweza kusema kwamba watu kwa kweli wanakua katika kiganja cha mkono wa Mungu? (Ndiyo.) Kwa hivyo sasa bado mnahisi hisia za hasara? (La.) Je, kuna yeyote anayehisi kuvunjika moyo bado? (La.) Kwa hivyo kuna yeyote anayehisi kwamba Mungu amewaacha wanadamu? (La.) Kwa hivyo ni nini hasa Mungu amefanya? (Anawahifadhi wanadamu.) Wazo na utunzaji mkuu nyuma ya kila anachofanya Mungu hayapingwi. Hata zaidi, wakati Mungu anapofanya kazi Yake, hajawahi kuweka sharti ama mahitaji yoyote kwa yeyote kujua gharama anayomlipia, kwa hivyo huhisi shukrani kwake kwa kina. Je, Mungu amewahi kufanya chochote kama hiki kabla? (La.) Katika miaka yenu mirefu yote, kimsingi kila mtu amekutana na hali nyingi hatari na kupitia majaribu mengi. Hii ni kwa sababu Shetani yupo kando yako, macho yake yakikutazama kila wakati. Anapenda janga linapokupata, wakati maafa yanakupata, wakati hakuna chochote kinaenda sawa kwako, na anapendelea unaponaswa na wavu wa Shetani. Kuhusu Mungu, anakulinda kila wakati, kukuweka mbali na bahati moja mbaya baada ya nyingine na kutokana na janga moja baada ya jingine. Hii ndiyo maana Nasema kwamba kila kitu ambacho mwanadamu anacho—amani na furaha, baraka na usalama wa kibinafsi—yote hakika yanadhibitiwa na Mungu, na Anaongoza na kuamua maisha na hatima ya kila mtu. Lakini, je, Mungu ana dhana iliyovimbishwa ya cheo chake, kama wanavyosema watu wengine? Kukuambia “Mimi ni mkuu kabisa wa wote, ni Mimi ninayechukua watamu wenu, lazima nyote mniombe huruma na kutotii kutaadhibiwa na kifo.” Je, Mungu amewahi kutishia wanadamu kwa njia hii? (La.) Ashawahi kusema “Wanadamu ni wapotovu kwa hivyo haijalishi Ninavyowashughulikia, utendeaji wowote holela utatosha; Sihitaji kupanga mambo vizuri sana kwa sababu yao.” Je, Mungu anafikiria kwa njia hii? (La.) Kwa hivyo Mungu ametenda kwa njia hii? (La.) Kinyume na haya, utendeaji wa Mungu wa kila mtu ni wenye ari na ambao umewajibika, umewajibika zaidi hata kuliko vile ulivyo kwa wewe mwenyewe. Sivyo hivi? Mungu haongei bure, wala hasimami juu akijifanya kuwa muhimu wala hadanganyi watu. Badala yake, Anafanya vitu ambavyo Yeye Mwenyewe anapaswa kufanya kwa uaminifu na kwa ukimya. Mambo haya yanaleta baraka, amani na furaha kwa mwanadamu, yanamleta mwanadamu kwa amani na kwa furaha mbele ya macho ya Mungu na ndani ya familia Yake na yanamletea mwanadamu akili sahihi, kufikiria sahihi, maoni sahihi na akili timamu wanapaswa kuwa nayo kuja mbele ya Mungu na kupokea wokovu wa Mungu. Kwa hivyo Mungu amewahi kuwa mdanganyifu kwa mwanadamu katika kazi Yake? (La.) Ashawahi kuonyesha maonyesho ya uongo ya ukarimu, Akimtuliza mwanadamu na mazungumzo ya kufurahisha, kisha kumgeukia mwanadamu? (La.) Je, Mungu ashawahi kusema kitu kimoja na kisha kufanya kingine? (La.) Je, Mungu ashawahi kupeana ahadi tupu na kujigamba, Akikuambia kwamba Anaweza kukufanyia hili ama kukusaidia kufanya lile, na kisha kutoweka? (La.) Hakuna ujanja ndani ya Mungu, hakuna uongo. Mungu ni mwaminifu na kila kitu Anachofanya ni cha ukweli na halisi. Yeye ndiye wa pekee ambaye watu wanaweza kutegemea na wa pekee ambaye watu wanaweza kuaminia maisha yao na yote wanayo Kwake. Kwa vile hakuna ujanja ndani ya Mungu, tunaweza kusema kwamba Mungu ndiye wa kweli zaidi? (Ndiyo.) Bila shaka tunaweza, siyo? Ingawa, kuzungumza kuhusu maneno haya sasa, likitumika kwa Mungu ni dhaifu sana, cha ubinadamu sana, hakuna lolote tunaloweza kufanya kulihusu kwa vile hii ni mipaka ya lugha ya binadamu. Si sahihi sana hapa kumwita Mungu wa kweli, lakini tutatumia neno hili kwa sasa. Mungu ni mwaminifu na wa kweli, sivyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo tunamaanisha nini kwa kuongea kuhusu vipengele hivi? Je, tunamaanisha tofauti kati ya Mungu na mwanadamu na tofauti kati ya Mungu na Shetani? Tunaweza kusema hivi kwa sababu mwanadamu hawezi kuona chembe cha tabia potovu ya Shetani kwa Mungu. Je, Niko sahihi kusema hivi? Ninaweza kupata Amina kwa sababu ya hili? (Amina!) Hatuoni uovu wowote wa Shetani ukifichuliwa kwa Mungu. Yote ambayo Mungu hufanya na kufichua ni muhimu sana na ya msaada sana kwa mwanadamu, yanafanywa kumkimu mwanadamu kabisa, yamejaa uhai na yanampa mwanadamu njia ya kufuata na mwelekeo wa kuchukua. Mungu hajapotoka, na zaidi ya hayo, kuangalia sasa kila kitu Mungu hufanya, tunaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu? (Ndiyo.) Kwa sababu Mungu hana upotovu wowote wa mwanadamu na hana chochote hata kidogo kama tabia potovu ya mwanadamu ama kiini cha Shetani, kutoka mtazamo huu tunaweza kusema kwamba Mungu ni mtakatifu. Mungu hafichui upotovu wowote, na ufunuo wa kiini Chake katika kazi Yake yote ni thibitisho tunalohitaji kwamba Mungu Mwenyewe ni mtakatifu. Je, mnaona hili sasa? Kusema kwamba, kuitambua asili takatifu ya Mungu, kwa sasa wacha tuangalie hivi vipengele viwili: 1) Hakuna tabia potovu ndani ya Mungu; 2) kiini cha kazi ya Mungu kwa mwanadamu kinamruhusu mwanadamu kuona kiini cha Mungu mwenyewe na kiini hiki ni kizuri kabisa na halisi kabisa. Kwa kuwa ni vitu vipi ambavyo kila namna ya kazi ya Mungu inamletea mwanadamu? Vyote ni vitu vizuri, vyote ni upendo, vyote ni ukweli na vyote ni halisi. Kwanza, Mungu anamhitaji mwanadamu kuwa mwaminifu—hili si zuri? Mungu anampa mwanadamu maarifa—hili si zuri? Mungu anamfanya mwanadamu aweze kutambua kati ya mema na maovu—hili si zuri? Anamruhusu mwanadamu kuelewa maana na thamani ya maisha ya binadamu—hili si zuri? Anamruhusu mwanadamu kuona ndani ya kiini cha watu na mambo kulingana na ukweli—hili si zuri? (Ndiyo.) Na matokeo ya haya yote ni kwamba mwanadamu hadanganywi tena na Shetani, haendelei kudhuriwa na Shetani ama kudhibitiwa na yeye. Kwa maneno mengine, yanawaruhusu watu kujinusurisha kabisa kutoka upotovu wa Shetani, na hivyo kutembea polepole njia ya kumcha Mungu na kuepuka maovu. Mmetembea umbali ngani tayari katika njia hii sasa? Ni vigumu kusema, sivyo? Lakini angalau sasa mna uelewa wa mwanzo wa jinsi Shetani anampotosha mwanadamu, vitu vipi ni ovu na vitu vipi ni hasi? (Ndiyo.) Kwa uelewa huu wa mwanzo, angalau mnatembea sasa njia sahihi, mmeanza kujua ukweli, kuona mwanga wa maisha, na hivyo imani yenu kwa Mungu ni kubwa zaidi.
Tutamaliza sasa kuzungumzia kuhusu utakatifu wa Mungu, kwa hivyo nani miongoni mwenu, kutoka yote ambayo mmesikia na kupokea, anaweza kusema utakatifu wa Mungu ni nini? Utakatifu wa Mungu ninaozungumzia unarejelea nini? Lifikirie kidogo. Utakatifu wa Mungu ni nini? Je, utakatifu wa Mungu ni ukweli Wake? (Ndiyo.) Je, utakatifu wa Mungu ni uaminifu Wake? (Ndiyo.) Je, utakatifu wa Mungu ni kutokuwa na ubinafsi Wake? (Ndiyo.) Je, utakatifu wa Mungu ni unyenyekevu Wake? (Ndiyo.) Je, utakatifu wa Mungu upo ndani ya upendo Wake kwa mwanadamu? (Ndiyo.) Je, utakatifu wa Mungu upo katika Yeye kumpa mwanadamu ukweli na uhai bure? (Ndiyo.) Haya yote ambayo Mungu anafichua ni ya kipekee; hayapo katika ubinadamu potovu, wala hayawezi kuonekana hapo. Hakuna hata chembe ya hayo yanaweza kuonekana katika mchakato wa upotovu wa Shetani wa mwanadamu, wala katika tabia potovu ya Shetani wala katika kiini ama asili ya Shetani. Kwa hivyo chote ambacho Mungu Anacho na Alicho ni ya kipekee na Mungu tu Mwenyewe anayo kiini cha aina hii, ni Mungu Mwenyewe tu anamiliki kiini cha aina hii. Baada ya kuzungumza hili hadi sasa, kuna yeyote kati yenu ambaye ameona yeyote mtakatifu hivi miongoni mwa wanadamu? (La.) Kwa hivyo, kuna yeyote mtakatifu hivi miongoni mwa watu maarufu, watu wakuu na mashuhuri mnaoabudu katika ubinadamu? (La.) Hakuna yeyote kabisa ambaye anaweza kuitwa mtakatifu! Wanaoitwa “watakatifu” wa wasioamini wote ni wanafiki walaghai na ndio wajanja zaidi, ibilisi Shetani anayedhuru kwa siri zaidi. Hili si lolote isipokuwa ukweli. Tunaweza kusema tu kwamba Mungu pekee ni mtakatifu kweli, kwamba utakatifu wa Mungu ni wa kipekee na Yeye tu anaweza kujumuisha hili kwa jina na pia kwa kweli. Zaidi ya hayo, kuna pia sehemu yake ya utendaji. Je, kuna tofauti zozote kati ya utakatifu ninaozungumzia sasa na utakatifu ambao mlifikiria na kudhania awali? (Ndiyo.) Kwa hivyo tofauti hii ni kubwa kiasi gani? (Kubwa sana!) Kwa kutumia maneno yenu, watu wanamaanisha nini sanasana wanapoongea kuhusu utakatifu huu? (Baadhi ya tabia ya nje.) Tabia ama wanapoeleza kitu, wanasema kwamba ni kitakatifu. Kwa hivyo maelezo haya ya “utakatifu” ni dhahania? Ni kitu tu kinachoonekana kuwa safi na kizuri, kitu kinachoonekana ama kusikika kuwa kizuri kwa watu, si chochote cha asili yoyote halisi ya utakatifu. Hakuna chochote halisi kuhusu kile watu wanadhania utakatifu kuwa. Kando ya hili, “utakatifu” ambao watu wanafikiria unarejelea nini hasa? Je, ni kile wanachokifikiria ama kudhania kuwa? Kwa mfano, Wanabudhaa wengine hufariki wakati wanatia vitendoni, wanaaga wakiwa wamekaa pale wakilala. Watu wengine husema kwamba wao ni watakatifu na wameruka mbinguni. Hii pia ni aina ya ubunifu. Pia kuna wengine ambao wanafikiria kwamba kichimbakazi anayeelea chini kutoka mbinguni ni mtakatifu. Pia kuna wengine ambao wanafikiri kwamba kutooa kamwe, kula na kuvaa vibaya na kuteseka maisha yote ya mtu ni takatifu. Kwa kweli, wazo la watu la neno “takatifu” limekuwa tu kama fikira tupu na dhahania ambayo kimsingi haina kiini, na zaidi ya hayo haina chochote kuhusu kiini cha utakatifu. Kiini cha utakatifu ni upendo wa kweli, lakini hata zaidi ya hili ni kiini cha ukweli, cha haki na mwanga. Neno “takatifu” linafaa tu linapotumika kwa Mungu; hakuna chochote katika uumbaji kinachostahiki kuitwa takatifu. Mwanadamu lazima aelewe hilo. Kutotambua utakatifu wa kweli ni nini ni kutotambua Mungu. Mungu pekee ni mtakatifu, na huu ni ukweli usiokanika.
Hebu turudi kuzungumza kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu. Tumeongea karibuni kuhusu mbinu mbalimbali ambazo Mungu anafanya kazi kwa mwanadamu ambazo kila mmoja wenu mnaweza kupitia nyinyi wenyewe, kwa hivyo sitatoa maelezo zaidi. Lakini katika mioyo yenu pengine mmechanganyikiwa kuhusu mbinu ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu, ama kwa kiwango cha chini zaidi ana upungufu wa maelezo, kwa hivyo itawafaidi kumzungumzia. Je, mnataka kumwelewa? (Ndiyo.) Pengine wengine wenu watauliza: “Mbona tuzungumze kuhusu Shetani tena? Tumeona tayari kwamba Shetani ni mwovu na tunachukia Shetani tayari, kwa hivyo Shetani bado anaweza kutupotosha? Kwa kweli, ingawa mnaweza kumchukia Shetani, hamwelewi kabisa. Kuna mambo mengine ambayo bado mnahitaji kukabili, kama sivyo hamwezi kweli kuepukana na ushawishi wa Shetani.
Tumezungumza hapo awali njia tano ambazo Shetani anatumia kumpotosha mwanadamu, sivyo? Ndani ya hizi njia tano kuna mbinu anazotumia, ambazo mwanadamu anapaswa kutambua. Njia ambazo Shetani anampotosha mwanadamu ni aina ya kifuniko tu; ya kudhuru kwa siri zaidi ni mbinu zinazojificha nyuma ya sura hii ya kinafiki na anataka kutumia mbinu hizi kufikia malengo yake. Mbinu hizi ni zipi? Nipeni muhtasari. (Anadanganya, anashawishi na anatishia.) Kadri mnavyoendelea kutaja ndivyo mnavyokaribia. Inaonekana kana kwamba mmedhuriwa kwa kina na yeye na mna hisia kali kuhusu mada hii. (Anatumia pia maneno matamu na uongo, anashawishi, anadanganya, na anamiliki kwa nguvu.) Anamiliki kwa nguvu—hii inatoa fikra ya kina, sivyo? Watu wanaogopa umiliki wa nguvu wa Shetani. Kuna mengine? (Huwadhuru watu kikatili, hutumia vitisho na vivutio, na hudanganya.) Uongo ni kiini cha matendo yake na hudanganya ili kukulaghai. Ni nini asili ya kudanganya? Je, kudanganya si sawa na kulaghai? Lengo la kusema uongo kwa kweli ni kukudanganya. Mengine zaidi? Zungumzeni. Niambieni yote mnayoyajua. (Hushawishi, hudhuru, hupofusha na hudanganya.) Wengi wenu mnahisi sawa kuhusu uongo huu, sivyo? (Hujipendekeza, humdhibiti mwanadamu, humkamata mwanadamu, humtishia sana mwanadamu na humzuia mwanadamu kumwamini Mungu.) Ninajua vizuri kiasi mnachomaanisha na yote ni mazuri pia. Nyote mnajua kitu kuhusu hili, kwa hivyo wacha sasa tufanye muhtasari.
Kuna njia sita za msingi ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu.
Ya kwanza ni kudhibiti na kulazimisha. Yaani, Shetani atafanya vyovyote vile kudhibiti moyo wako. “Kulazimisha” kunamaanisha nini? (Kunamaanisha shurutisho.) Hukutishia na kukulazimisha kumtii, kukufanya kufikiria matokeo usipomtii. Unaogopa na huthubutu kumpinga, basi huna chaguo ila kuwa chini ya ushawishi wake.
Ya pili ni kudanganya na kulaghai. “Kudanganya na kulaghai” yanahusisha nini? Shetani hutunga baadhi ya hadithi na uongo, kukulaghai wewe kuziamini. Hakwambii kamwe kwamba mwanadamu aliumbwa na Mungu, wala hasemi pia moja kwa moja kwamba hukuumbwa na Mungu. Hatumii jina “Mungu” kabisa, lakini badala yake hutumia kitu kingine mbadala, akitumia kitu hiki kukudanganya ili kimsingi usiwe na wazo la kuwepo kwa Mungu, na kamwe hakuwachi kujua Mungu kwa kweli ni nani. Huu ulaghai bila shaka unahusisha vipengele vingi, sio tu hiki kimoja.
Ya tatu ni kufunza kwa nguvu. Je, kuna kufunza kwa nguvu? (Ndiyo.) Kufunza nini kwa nguvu? Je, kufunzwa kwa nguvu kunafanywa kwa hiari ya mwanadamu mwenyewe? Je, kunafanywa na idhini ya mwanadamu? (La.) Haijalishi kama hukuidhinisha. Katika kutojua kwako, humwaga ndani yako, kuweka ndani yako kufikiria kwa Shetani, kanuni zake za maisha na kiini chake ovu, Hakika, vyote anavyokuingizia Shetani ni uongo, uwongo wa kudanganya na hakika ni uzushi na uwongo ambayo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu. Hizi sumu za kishetani zinapandwa katika bongo za watu na katika akili zao, na hii kweli inatia kasumba watu. Wakati tu mtu amekubali hizi sumu za kishetani, anakuwa sio mwanadamu wala pepo, bila ubinadamu wowote.
Ya nne ni vitisho na vivutio. Yaani, Shetani hutumia mbinu mbalimbali ili umkubali, umfuate, ufanye kazi katika Huduma yake; hujaribu kufikia malengo yake kwa vyovyote vile. Saa zingine hukupa fadhili ndogo lakini bado hukushawishi kufanya dhambi. Usipomfuata, atakufanya uteseke na kukuadhibu na atatumia njia mbalimbali kukushambulia na kukutega.
Ya tano ni uongo na kiharusi. “Uongo na kiharusi” ni kwamba Shetani hutunga kauli na mawazo yanayosikika kuwa matamu ambayo yako pamoja na dhana za watu kufanya ionekane kwamba anatilia maanani miili ya watu ama anafikiria kuhusu maisha yao na siku zao za baadaye, wakati hakika anakudanganya tu. Kisha anakupooza ili usijue kile kilicho sahihi na kile kilicho makosa, ili ufuate njia yake kwa kutojua na hivyo kuja chini ya udhibiti wake.
Ya sita ni uangamizi wa mwili na akili. Shetani huharibu kipi cha mwanadamu? (Akili yao, nafsi yao yote.) Shetani huharibu akili yako, kukufanya kutokuwa na nguvu za kupinga, kumaanisha kuwa polepole sana moyo wako unageuka kwa Shetani licha ya wewe mwenyewe. Huingiza mambo haya ndani yako kila siku, kila siku akitumia mawazo na utamaduni huu kukushawishi na kukuelimisha, polepole akiharibu utashi wako, kukufanya kutotaka kuwa mtu mzuri tena, kukufanya kutotaka tena kustahimili kushikilia kile unachoita cha haki. Bila kujua, huna tena utashi wa kuogelea kinyume na mkondo dhidi ya bamvua, lakini badala yake kububujika chini pamoja nayo. “Uangamizi” unamaanisha kwamba Shetani hutesa watu sana hadi wanakuwa sio kama wanadamu wala pepo, kisha anachukua fursa ya kuwameza.
Kila ya hizi njia zote Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu inaweza kumfanya mwanadamu kutokuwa na nguvu ya kupinga; yoyote inaweza kuwa ya kufisha kwa watu na kuwaacha bila nafasi ya kupinga kabisa. Kwa maneno mengine, chochote anachofanya Shetani na njia yoyote anayotumia inaweza kukufanya kupotoka, inaweza kukuleta chini ya udhibiti wa Shetani na inaweza kukuzamisha katika bwawa la uovu ili usiweze kutoroka. Hizi ndizo njia Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu na ni katili, za kijicho, za kudhuru kwa siri na zenye kustahili dharau sana. Kila mtu ameonja uchungu wa njia hizi kibinafsi, kwa hivyo moyo wa mwanadamu unaweza basi kumchukia Shetani kwa uchungu na kuamua kuasi dhidi ya huyu ibilisi mwovu.
Tunaweza kusema Shetani ni mwovu, lakini ili kuthibitisha hili ni lazima tuangalie matokeo ya upotovu wa Shetani wa mwanadamu ni yapi na ni tabia gani na viini vipi anamletea mwanadamu. Nyote mnajua baadhi ya haya, kwa hivyo ongeeni kuyahusu. Baada ya Shetani kumpotosha mwanadamu, ni tabia gani za kishetani anaonyesha ama kufichua? (Zenye kiburi na zenye maringo, zenye ubinafsi na zenye kustahili dharau, zisizo aminifu, zenye ujanja, zenye kudhuru kwa siri na zenye kijicho, na zisizo na ubinadamu.) Kwa ujumla, tunaweza kusema hazina ubinadamu, siyo? Wacha kaka na dada wengine wazungumze. (Zenye kiburi, zenye ujanja, zenye kijicho, zenye ubinafsi, zenye tamaa, za juujuu, za uwongo.) Usiseme kinachofichuliwa na baadhi ya tabia ya kipengele; Lazima useme ni nini kiini cha kipengele hicho. Unaelewa? (Punde mwanadamu anapopotoshwa na Shetani, wakati mwingi hasa huwa mwenye kiburi na mwenye makuu, wa majivuno na mwenye maringo, mwenye tamaa na mwenye ubinafsi. Haya ndiyo mazito sana.) (Baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, anatenda yasiyo na maadili kimwili na kiroho. Kisha anakua mkatili kwa Mungu, anampinga Mungu, hamtii Mungu, na anapoteza dhamiri yake na akili ambayo mwanadamu anapaswa kuwa nayo.) Yale ambayo mmesema yote kimsingi ni sawa na yana tofauti kidogo tu, na wengine wenu wanajali zaidi maelezo madogo. Kwa muhtasari, “mwenye kiburi” limekuwa jina ambalo limetajwa sana—mwenye kiburi, mwenye ujanja, mwenye kijicho na mwenye ubinafsi. Lakini nyote mmepuuza kitu sawa. Watu wasio na dhamiri, ambao wamepoteza akili zao na ambao hawana ubinadamu—bado kuna kitu muhimu pia ambacho hakuna yeyote kati yenu amesema. Kwa hivyo ni kipi? (Kusaliti.) Sahihi! Hakuna yeyote ambaye amesema “kusaliti.” Matokeo ya mwisho ya tabia hizi ambazo zipo kwa mwanadamu yeyote baada ya kupotoshwa na Shetani ni kusaliti kwao Mungu na kutomtambua tena. Licha ya kile Mungu anamwambia mwanadamu ama licha ya kazi anayomfanyia, hakubali kile ambacho anajua kuwa ukweli, na inaweza kuonekana kwamba hamtambui Mungu tena na anamsaliti: Haya ndiyo matokeo ya upotovu wa Shetani wa mwanadamu na ni sawa kwa tabia zote potovu za mwanadamu. Miongoni mwa njia ambazo Shetani hutumia kumpotosha mwanadamu—maarifa ambayo mwanadamu hujifunza, sayansi anayojua, ushirikina, utamaduni wa jadi, na mienendo ya kijamii anayoelewa—kuna yoyote ambayo mwanadamu anaweza kutumia kusema kile kilicho haki na kile kisicho haki? Kuna viwango vyovyote vya kufanya kazi kutoka hapa? (La.) Kuna chochote kinachoweza kumsaidia mwanadamu kujua kilicho takatifu na kilicho ovu? (La.) Hakuna viwango na hakuna msingi ambao unaweza kumsaidia mwanadamu. Hata kama watu wanajua neno “takatifu,” hakuna yeyote anayejua kweli kile kilicho takatifu. Kwa hivyo mambo haya ambayo Shetani anamletea mwanadamu yanaweza kumruhusu kujua ukweli? Hayawezi kumruhusu mwanadamu kujua ukweli. Je, yanaweza kumruhusu mwanadamu kuishi na ubinadamu unaoongezeka? Je, yanaweza kumruhusu mwanadamu kuishi katika uelewa unaoongezeka wa jinsi ya kumwabudu Mungu kwa kweli? (La.) Ni dhahiri kwamba hayawezi kumruhusu mwanadamu kumwabudu Mungu, wala hayawezi kumruhusu mwanadamu kujua utakatifu na uovu ni nini. Kinyume chake, mwanadamu anakuwa zaidi na zaidi msherati, mbali na mbali zaidi na Mungu, zaidi na zaidi mwovu, zaidi na zaidi mpotovu. Hii ndiyo sababu kuu ya mbona tunasema Shetani ni mwovu. Baada ya kuchangua asili ovu nyingi za Shetani, je, mmeona Shetani kuwa na dalili yoyote ya utakatifu katika asili zake ama katika uelewa wenu wa kiini chake? (La.) Hiyo ni ya hakika, sivyo? Kwa hivyo mmeona kiini chochote cha Shetani ambacho kinashiriki usawa wowote na Mungu? (La.) Je, kuna maonyesho ya Shetani ambayo yanashiriki usawa na Mungu? (La.) Kwa hivyo sasa Nataka kuwauliza, kwa kutumia maneno yenu, utakatifu wa Mungu ni nini hasa? Kwanza kabisa, utakatifu wa Mungu unasemwa kwa uhusiano na nini? Je, unasemwa kwa uhusiano na kiini cha Mungu? Ama unasemwa kwa uhusiano na vipengele fulani vya tabia Yake? (Unasemwa kwa uhusiano na kiini cha Mungu.) Lazima tupate kidato wazi katika mada yetu tunayopenda. Unasemwa kwa uhusiano wa kiini cha Mungu. Kwanza kabisa, tumetumia uovu wa Shetani kama foili ya[c] kiini cha Mungu, kwa hivyo umeona kiini chochote cha Shetani katika Mungu? (La.) Je, kiini chochote cha mwanadamu? (La.) Mtu aniambie. (Utakatifu wa Mungu ni wa kipekee, ni mwaminifu, wa dhati na hakuna tabia potovu ndani ya Mungu. Mungu ni mwema kabisa, kama vile vitu vyote Yeye huletea binadamu.) (Kiini chote cha Mungu ni chema, yote anayofichua ni kwa ajili ya wokovu wa mwanadamu na kwa mwanadamu kuishi kwa kudhihirisha usawa wa kawaida wa binadamu. Ni ili Aweze kweli kulinda mtu na ili mwanadamu aweze kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida.) Je, ni tu kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida? (Ni ili mwanadamu aweze kweli kujua ukweli; Utakatifu Wake ni upendo Wake wa kweli na wokovu wa wanadamu.) (Yote ambayo yamefichuliwa na kiini cha Mungu ni mema. Ukweli wa Mungu, uaminifu Wake, kutokuwa na ubinafsi Kwake, unyenyekevu Wake na upendo Wake kwa wanadamu yote yanaonyesha kiini cha utakatifu wa Mungu.) (Mungu si mwenye kiburi, hana ubinafsi na hasaliti, na katika kipengele hiki kiini takatifu cha Mungu pia kinaonekana kufichuliwa.) Mm. Kunayo mengine ya kuongeza? (Mungu hana dalili za tabia potovu ya Shetani. Chochote Shetani anacho ni hasi kabisa, wakati kile ambacho Mungu anacho ni kizuri. Tunaweza kuona kwamba Mungu yuko upande wetu daima. Kutoka tulipokuwa wachanga hadi sasa, hasa nyakati zile tulipotea njia, Alikuwa nasi, Akitutazama na kutuweka salama. Hamna ujanja ndani ya Mungu, hamna udanganyifu. Yeye hunena kwa udhahiri na uwazi, na hii pia ni asili ya kweli ya Mungu.) Vizuri sana! (Hatuwezi kuona tabia yoyote potovu ya Shetani katika kazi ya Mungu, hamna udanganyifu, hamna kujisifu, hamna ahadi tupu na hamna ujanja. Mungu ni wa pekee ambaye mwanadamu anaweza kuamini na kazi ya Mungu ni ya uaminifu na kweli. Kutoka kwa kazi ya Mungu tunaweza kuona Mungu akiwaambia watu wawe waaminifu, wawe na hekima, wawe na uwezo wa kung’amua kati ya mema na mabaya na kuwa na utambuzi. Kwa haya tunaweza kuona utakatifu wa Mungu.) Kuna mengine yoyote ya kuongeza? Je, mmemaliza? (Ndiyo.) Je, mmeridhika na mliyoyasema? Hasa ni kiasi gani cha uelewa kwa kweli upo mioyoni mwenu? Na mnaelewa kiasi kipi utakatifu wa Mungu? Najua kwamba kila mmoja kati yenu katika moyo wake ana baadhi ya kiwango cha ufahamu wa utambuzi, kwa sababu kila mtu anaweza kuhisi kazi ya Mungu kwao na, katika viwango tofauti, wao hupata vitu vingi kutoka kwa Mungu; wao hupata neema na baraka, wao hutiwa nuru na kuangaziwa, na wao hupokea hukumu na kuadibu kwa Mungu ili kwamba mwanadamu aweze kuwa na uelewa rahisi wa kiini cha Mungu. 
Ingawa "utakatifu wa Mungu" tunaojadili leo unaweza kuonekana geni kwa watu wengi, bila kujali jinsi unaweza kuonekana tumeanza mada hii, na mtakuwa na ufahamu zaidi mnapotembea katika njia yenu kwenda mbele. Itawalazimu kuja kuhisi na kuelewa kutoka kwa uzoefu wenu wenyewe kwa utaratibu. Sasa uelewa wenu wa utambuzi kuhusu kiini cha Mungu bado unahitaji kipindi cha muda mrefu kujifunza, kuthibitisha, kuhisi na kuipitia, hadi siku moja mtatambua utakatifu wa Mungu kutoka katikati ya moyo wenu kuwa kiini cha Mungu ambacho hakina dosari, upendo wa Mungu usio na ubinafsi, ambao ni upendo usio na ubinafsi zaidi ambao Mungu humpa mwanadamu, na mtakuja kutambua ya kwamba utakatifu wa Mungu hauna dosari wala haushutumiki. Hivi viini vya Mungu si maneno tu ambayo Yeye hutumia kuonyesha utambulisho Wake, bali Mungu hutumia kiini Chake kwa kimya na kwa dhati kushughulika na kila mtu. Kwa maneno mengine, kiini cha Mungu si tupu, wala si cha nadharia au mafundisho ya dini na hakika si aina ya maarifa. Si aina ya elimu kwa mwanadamu, lakini badala yake ni ufunuo wa kweli wa matendo ya Mungu mwenyewe na ni kiini ambacho kimefichuliwa cha kile Mungu anacho na alicho. Binadamu anapaswa kutambua kiini hiki na kukifahamu, kwa kuwa kila kitu Mungu hufanya na kila neno Yeye husema ni la thamani kubwa na umuhimu mkubwa kwa kila mtu. Unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kumwamini Mungu; unapokuja kuelewa utakatifu wa Mungu, basi unaweza kweli kutambua maana halisi ya maneno haya "Mungu Mwenyewe, wa Kipekee." Hutafikiria tena kwamba unaweza kuchagua kutembea njia zingine, na hutakuwa tena radhi kusaliti kila kitu ambacho Mungu amekupangia. Kwa sababu kiini cha Mungu ni takatifu, hiyo ina maana kwamba kupitia tu Mungu ndipo unaweza kutembea njia yenye kung’aa na sahihi katika maisha; ni kupitia tu Mungu unaweza kujua maana ya maisha, ni tu kupitia Mungu unaweza kuishi kwa kudhihirisha maisha halisi, kumiliki ukweli, kujua ukweli, na ni kupitia tu Mungu unaweza kupata maisha kutoka kwa kweli. Ni Mungu Mwenyewe tu anaweza kukusaidia kuepuka maovu na kukuokoa kutoka kwa madhara na udhibiti wa Shetani. Kando na Mungu, hakuna mtu au kitu kinaweza kukuokoa kutoka kwa bahari ya mateso, ili usiteseke tena: Hili linaamuliwa na kiini cha Mungu. Ni Mungu Mwenyewe tu hukuokoa bila ubinafsi wowote, ni Mungu pekee anayehusika na maisha yako ya baadaye, na hatima yako na maisha yako, na Yeye anapanga mambo yote kwa ajili yako. Hili ni jambo ambalo hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kinaweza kutimiza. Kwa sababu hakuna kitu ambacho kimeumbwa au hakijaumbwa kina kiini cha Mungu kama hiki, hakuna mtu au kitu kina uwezo wa kukuokoa au kukuongoza wewe. Huu ndio umuhimu wa kiini cha Mungu kwa mwanadamu. Labda mnahisi kuwa maneno haya Niliyoyasema yanaweza kweli kusaidia kimsingi katika kanuni. Lakini kama wewe unatafuta ukweli, kama wewe unapenda ukweli, katika uzoefu wako wa baada ya hapa maneno haya hayataleta tu mabadiliko katika hatima yako, lakini zaidi ya hayo yatakuleta kwa njia sahihi katika maisha. Je, unafahamu hili, siyo? (Ndiyo.) Kwa hivyo sasa mna moyo wa kupenda katika kutambua kiini cha Mungu? (Ndiyo.) Ni vizuri kuwa na moyo wa kupenda. Tutamalizia hapa kujadili mada yetu ya leo juu ya kutambua utakatifu wa Mungu.
Ningependa kuwazungumzia kuhusu kitu mlichofanya kilichonishangaza mwanzoni mwa mkusanyiko wetu leo. Wengine wenu pengine mlikuwa na hisia za shukrani hivi karibuni, ama kuhisi shukrani, na hivyo mlitaka kuonyesha kimwili kile mlichokuwa nacho akilini mwenu. Hili si la kushutumiwa, na si sahihi wala makosa. Lakini ni nini ambacho Ningetaka kuwaambia? Kile mlichofanya si makosa na sina tamaa ya kuwashutumu kwa njia yoyote. Ningependa muelewe kitu. Ni nini hiki? Kwanza Ningetaka kuwauliza kuhusu mlichokifanya hivi sasa. Je, kulikuwa ni kusujudu ama kupiga magoti kuabudu? Kuna yeyote anayeweza kuniambia? (Tunaamini ilikuwa kusujudu. Tunasujudu kwa njia hii.) Mnaamini kulikuwa kusujudu, kwa hivyo ni nini maana ya kusujudu? (Kuabudu.) Kwa hivyo ni nini kupiga magoti kuabudu basi? Sikutaja hili haraka kabisa kwa sababu mada yetu ya ushiriki leo ni muhimu sana na Sikutaka kuathiri hali ya mioyo yenu. Je, mnasujudu katika mikusanyiko yenu ya kawaida? (La.) Je, mnasujudu mnaposema sala zenu? (Ndiyo.) Je, mnasujudu kila wakati mnaposema sala zenu, hali zinaporuhusu? (Ndiyo.) Hivyo ni vizuri sana. Lakini ni nini Ningependa nyinyi muelewe leo? Ni aina mbili za watu ambao kupiga magoti kwao kunakubaliwa na Mungu. Hatuhitaji kutafuta maoni katika Biblia ama tabia za watu wa kiroho, na Nitawaambia kitu kweli hapa na sasa. Kwanza, kusujudu na kupiga magoti kuabudu si kitu sawa. Mbona Mungu anakubali kupiga magoti kwa wale wanaosujudu wenyewe? Ni kwa sababu Mungu humwita mtu Kwake na humwita mtu huyu kukubali agizo la Mungu, kwa hivyo anasujudu mwenyewe mbele ya Mungu. Huyu ni mtu wa aina ya kwanza. Aina ya pili ni kupiga magoti kuabudu kwa mtu anayemcha Mungu na kuepukana na maovu. Kuna watu hawa wa aina mbili tu. Kwa hivyo mko katika aina gani? Mnaweza kusema? Huu ni ukweli kabisa, ingawa unaweza kuumiza hisia zenu kidogo. Hakuna kitu cha kusema kuhusu kupiga magoti kwa watu wakati wa sala—hii ni sahihi na ndivyo inavyopaswa kuwa, kwa sababu wakati watu wanasali wakati mwingi ni kuombea kitu, kufungua mioyo yao kwa Mungu na kukutana Naye uso kwa uso. Ni mawasiliano na mazungumzo, moyo kwa moyo na Mungu. Lakini ninapokutana nanyi katika ushirika, sijawauliza msujudu wenyewe. Simaanishi kuwashutumu kwa yale ambayo mmefanya leo. Mnajua kwamba nataka tu kuweka wazi kwenu ili muelewe kanuni hii, mnajua? (Tunajua.) Ili msiendelee kufanya hili. Je, watu basi wana fursa yoyote ya kusujudu na kupiga magoti mbele ya uso wa Mungu? Daima kutakuwa na fursa. Hatimaye siku itakuja lakini wakati sio sasa. Mnaona? (Ndiyo.) Je, hili linawafanya kuhisi vibaya? (La.) Hivyo ni vizuri. Labda maneno haya yatawatia moyo ama kuwashawishi ili muweze kujua katika mioyo yenu taabu ya sasa kati ya Mungu na mwanadamu na aina ya uhusiano uliopo sasa kati yao. Ingawa tumeongea na kuzungumza sana hivi karibuni, uelewa wa mwanadamu kuhusu Mungu bado uko mbali na kutosha. Mwanadamu bado ana umbali mrefu wa kwenda katika njia hii ya kutafuta kumwelewa Mungu. Si nia yangu kuwafanya mfanye hivi kwa dharura, ama kuwaharakisha kuonyesha matamanio na hisia za aina hizi. Yale mliyofanya leo yanaweza kufichua na kuonyesha hisia zenu za kweli, na Naliyafahamu. Kwa hivyo wakati mlipokuwa mkiyafanya, nilitaka tu kusimama na kuwatakia mema, kwa sababu Nataka nyote muwe wazima. Kwa hivyo katika maneno na vitendo vyangu vyote ninafanya yote ninayoweza kuwasaidia, kuwaongoza, ili muwe na uelewa sahihi na mtazamo sahihi wa mambo yote. Mnaweza kuelewa haya, sivyo? (Ndiyo.) Hivyo ni vizuri sana. Ingawa watu wana baadhi ya uelewa wa tabia mbalimbali za Mungu, kipengele cha kile anacho Mungu na alicho na kazi Mungu anafanya, wingi wa uelewa huu hauendi mbali na kusoma maneno kwenye ukurasa, ama kuyaelewa katika kanuni, ama tu kuyafikiria. Yale wanayoyakosa sana watu ni uelewa na mtazamo wa kweli unaotoka kwa uzoefu halisi. Ingawa Mungu hutumia njia mbalimbali kuamsha mioyo ya wanadamu, bado kuna njia ndefu ya kutembea kabla mioyo ya wanadamu iamshwe kikamilifu. Sitaki kumwona yeyote akihisi kana kwamba Mungu amemwacha nje kwa baridi, kwamba Mungu amemwacha ama amempuuza. Ningetaka tu kuona kila mtu katika njia ya kutafuta ukweli na kutafuta kumwelewa Mungu, akiendelea mbele kwa ujasiri na utashi usiosita, bila wasiwasi, bila kubeba mizigo. Haijalishi umefanya makosa gani, haijalishi umepotoka aje ama vile ulivyotenda dhambi, usiwache haya yawe mizigo ama vikorokoro ziada kubeba katika ufuataji wako wa kumwelewa Mungu: Endelea kutembea mbele. Haijalishi itafanyika lini, moyo wa Mungu ambao ni wokovu wa mwanadamu haubadiliki: Hii ni sehemu ya thamani sana ya kiini cha Mungu. Mnahisi vizuri kiasi sasa? (Ndiyo.) Ninatumai kwamba mnaweza kuchukua mtazamo sahihi katika mambo yote na maneno ambayo Nimezungumza. Wacha tukomeshe ushirika wetu hapa, basi. Kwaheri kila mtu! (Kwaheri!)
Januari 11, 2014
kutoka kwa Mwendelezo wa Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni