10.24.2019

Kazi ya pepo wabaya ni nini? Kazi ya pepo wabaya hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia katindani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuwa na hali za kawaida mbele ya Mungu. Ambayo ni kusema, punde tu kuna kazi ya Shetani ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba. Kazi ya roho waovu huharibu uhusiano wa kawaida kati ya mwanadamu na Mungu, na huvuruga maono ya awali ya watu na njia ambayo maisha yao yameingia, katika mioyo yao hawawezi kamwe kumkaribia Mungu, daima mambo hufanyika ambayo huwasababishia vurugu na kuwatia pingu, na mioyo yao haiwezi kupata amani, kuacha upendo wao wa Mungu bila nguvu, na kuwafanya kusononeka. Hayo ndiyo maonyesho ya kazi ya Shetani. Kazi ya Shetani inadhihirishwa katika yafuatayo: kutoweza kushikilia msimamo na kuwa na ushuhuda, kukusababisha kuwa mtu ambaye ana makosa mbele ya Mungu, na ambaye hana uaminifu kwa Mungu. Kwa kuingilia kwa Shetani, unapoteza upendo na uaminifu kwa Mungu ndani yako, unaondolewa uhusiano wa kawaida na Mungu, hufuatilii ukweli, ama kujiendeleza, unarudi nyuma, na kuwa baridi, unajipendeza, unaachia uenezaji wa dhambi, na huchukii dhambi; zaidi ya hayo, kuingilia kwa Shetani kunakufanya mpotovu, kunasababisha mguso wa Mungu kutoweka ndani yako, na kunakufanya kulalamika kuhusu Mungu na kumpinga Yeye, kukufanya uwe na shaka na Mungu, na hata kuna hatari ya wewe kumwacha Mungu. Hii yote ni kazi ya Shetani.
kutoka katika “Kazi ya Roho Mtakatifu na Kazi ya Shetani” katika Neno Laonekana katika Mwili
leo kunao baadhi ya pepo wabaya wanaofanya kazi kupitia kwa mambo yasiyo ya ulimwenguni humu ili kumpotosha mwanadamu; hilo si chochote bali ni uigaji kwa upande wao, kumpotosha mwanadamu kupitia kwa kazi ambayo kwa sasa haifanywi na Roho Mtakatifu. Pepo wengi wabaya huiga ufanyaji wa miujiza na uponyaji wa magonjwa; si chochote ila kazi ya pepo wabaya, kwani Roho Mtakatifu hafanyi tena kazi kama hiyo leo. Wale wote wanaokuja baadaye na wanaoiga kazi ya Roho Mtakatifu—ni pepo wabaya. Kazi yote iliyotekelezwa Israeli wakati huo ilikuwa ile ya rohoni. Hata hivyo, Roho Mtakatifu sasa hafanyi kazi kwa njia hiyo, na kazi yoyote kama hiyo inayofuata ni shughuli na usumbufu wa Shetani na wa pepo waovu. Lakini huwezi kusema kwamba mambo yote ya rohoni ni shughuli ya pepo waovu. Hili linategemea enzi ya kazi ya Mungu.
kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi.
kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili
Shetani bado yuko katika udhibiti wa udhaifu ndani ya mwanadamu, na bado anaweza kumfanya ateseke. Pepo wabaya bado wanaweza kufanya kazi ndani ya watu kuwaingilia, kuwasababisha wawe katika hali ya kuchanganyikiwa kimawazo, kupoteza ufahamu wao, kutokuwa watulivu kiakili na kupata upinzani katika kila jambo. Bado kuna mambo fulani ya kimawazo ndani ya binadamu au roho ambayo yanaweza kudhibitiwa na kutawaliwa na Shetani. Hii ndiyo maana haiwezekani kwako kuwa na magonjwa, matatizo na kuhisi mwenye kutaka kujitia kitanzi na wakati mwingine pia kuhisi huzuni ya dunia, au kwamba maisha hayana maana. Hiyo ni kusema, kuteseka huku bado kuko chini ya uongozi wa Shetani—huu ni udhaifu wa kusababisha mauti kwa mwanadamu. Shetani bado ana uwezo wa kutumia vile vitu ambavyo amevipotosha na kuvikanyagia chini—ni vitu ambavyo Shetani anaweza kutumia dhidi ya mwanadamu. … kuwa pepo wabaya bado wanaweza kutumia nafasi na wakufanyie mchezo na bado wanaweza kukutumia. Hii ni kwa sababu binadamu ni mpumbavu sana kiasi kwamba, wakati mwingine, hawezi kuelewa tofauti kati ya kuguswa na Roho Mtakatifu na kuingiliwa na pepo wabaya. Je, huu si udhaifu wenye kusababisha mauti? Roho wabaya ni wenye kujitakia mema wenyewe. Wanaweza kuzungumza kutoka ndani yako au kunong’oneza ndani ya sikio lako, au la sivyo wanaweza kuyachanganya mawazo na akili yako, na wanaweza kukandamiza kuguswa kwa Roho Mtakatifu ili usiweze kulihisi. Baada ya hapo wanaanza kukuingilia, kuzikanganya fikira zako na kuvuruga akili yako, kukufanya usiyekuwa na utulivu na usiye thabiti. Hivyo ndivyo ilivyo kazi ya roho wabaya.
kutoka katika “Maana ya Mungu Kuupitia Uchungu wa Dunia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Ikiwa wanasema kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao kila mara, kwamba wanapata nuru kutoka kwa Mungu na kuguswa na Roho Mtakatifu kila wakati, na wanapata ufahamu mpya kila wakati, basi hili si la kawaida. Ni la rohoni kabisa! Bila tashwishi yoyote, watu kama hao ni pepo wabaya! Hata wakati ambapo Roho wa Mungu huja ndani ya mwili, kuna nyakati ambapo lazima Ale, na lazima Apumzike—sembuse mwanadamu. Wale ambao wamemilikiwa na pepo wabaya huonekana kutokuwa na hisia na udhaifu wa mwili. Wanaweza kutelekeza na kuacha kila kitu, wao ni wenye uwezo wa kustahimili mateso na hawahisi uchovu hata kidogo sana, kana kwamba wamevuka mipaka ya mwili. Je, hili silo la rohoni kabisa? Kazi ya pepo mwovu ni ya rohoni, na mambo haya ni yasiyofikiwa na mwanadamu. Wale wasioweza kutofautisha huwa na wivu wanapoona watu kama hao, na husema kwamba imani yao katika Mungu ni thabiti sana, na wana imani kubwa, na kwamba wao huwa si wadhaifu kamwe. Kwa kweli, hili ni dhihirisho la kazi ya pepo mwovu. Hiyo ni kwa sababu watu wa kawaida huwa na udhaifu wa binadamu usioepukika; hii ni hali ya kawaida ya wale walio na kuwepo kwa Roho Mtakatifu.
kutoka katika “Utendaji (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Sifa ya wazi zaidi ya kazi ya pepo waba ya ni kwamba ni ya mwujiza, kwamba maneno ambayo pepo wabaya huyanena au huwauliza watu kufanya siyo ya kawaida, siyo ya mantiki, na hata huyasaliti maadili ya msingi ya ubinadamu wa kawaida na uhusiano wa kibinadamu, na kwamba yanakusudiwa kutofanya chochote ila kuwadanganya watu, kuwavuruga watu, na kuwapotosha watu. Pepo wabaya wanapowapagawa watu, baadhi yao huhisi hofu kubwa, wengine huingia katika hali isiyo ya kawaida, huku wengine wakichanganyikiwa, na wengine bado hujikuta wakiwa na wasiwasi wa ajabu na hawawezi kutulia tuli. Kwa vyovyote vile, pepo wabaya wanapowapagawa watu, watu hubadilika, kuwa kitu ambacho si binadamu wala pepo mbaya, na wao hupoteza ubinadamu wao wa kawaida. Hili linatosha kuthibitisha kuwa asili ya pepo wabaya ni mbaya na mbovu, ambayo kwa usahihi ndiyo asili ya Shetani. Pepo wabaya huwafanya watu kuwachukia kabisa na kuwadharau, na bila shaka hawana faida yoyote au msaada kwa watu. Mambo ya pekee ambayo Shetani na kila aina ya pepo wabaya wana uwezo wa kufanya ni kuwapotosha, kuwadhuru, na kuwameza watu.
Maonyesho makuu ya wale ambao wana kazi ya pepo wabaya (wale waliopagawa na pepo wabaya) ni:
Aina ya kwanza ni kwamba pepo wabaya huwaambia watu kufanya hili na lile, au kumwambia mtu kitu fulani, au kuwaelekeza watu kunena unabii wa uongo.
Aina ya pili ni kwamba watu mara nyingi hunena kile kinachodaiwa kuwa “lugha” katika sala ambazo hakuna anayezielewa, na hata wasemaji wenyewe hawaelewi. Baadhi ya wanenaji wanaweza hata “kuifasiri lugha” wenyewe.
Aina ya tatu ni kwamba mtu mara nyingi hupokea ufunuo, kwa marudio mengi, wakati huu akielekezwa kwa njia hii na pepo wabaya, wakati ufuatao akielekezwa kwenye njia ile, katika hali ya daima ya wasiwasi.
Aina ya nne ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya wanataka kufanya hili ama lile kwa haraka, wakikosa subira mno kiasi cha kutongoja, huwa hawafikirii kama hali zinaruhusu, hata hukimbia nje usiku wa manane na tabia yao hasa si ya kawaida.
Aina ya tano ni kwamba watu wenye kazi ya pepo wabaya huwa na kiburi ovyo ovyo, hawana mantiki, na usemi wao wote ni wa kujionyesha kuwa bora na huwa unakuja kutoka kwa nafasi ya kuamuru. Wao huwakanganya watu, na kama pepo wabaya, huwalazimisha watu kufanya mambo.
Aina ya sita ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya hawawezi kushiriki kuhusu ukweli, sembuse kuzingatia kazi ya Mungu, na wao ni waasi kwa Mungu na hutenda kiholela, wakifanya vitendo viovu vya ukatili vya kila aina ili kuharibu utaratibu wa kawaida wa kanisa.
Aina ya saba ni kwamba mtu ambaye ana kazi ya pepo wabaya hujifanya kuwa mtu mwingine bila sababu yoyote, au hudai kwamba alitumwa na mtu fulani na kwamba watu wanafaa kumsikiliza. Hakuna mtu anayeweza kuelewa alikotoka.
Aina ya nane ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya aghalabu hawana hisi ya kawaida, wala hawaelewi ukweli wowote; hawana uwezo wowote wa kupokea na pia hawajapatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na kile ambacho watu huona ni kwamba katika kupokea mambo hawa watu ni wapuuzi visivyo kawaida na si sahihi hata kidogo.
Aina ya tisa ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya huzingatia hasa kuwakemea wengine wakati wa kazi, daima wao hutenda ovyo ovyo na daima husababisha vurugu na usumbufu; kila kitu wanachokifanya na kusema huwashambulia, kuwafunga na kuwapotosha watu wengine, na wao hufikia kiwango cha kuwavunjia watu azma zao na kuwafanya kuwa hasi ili wasiweze kufanikiwa upya baada ya hali ngumu. Wao ni mashetani, kwa kweli kabisa, ambao huwadhuru wengine, hucheza na wengine na kuwala, nao hufurahi kwa siri wanapofanya wapendavyo. Hili ndilo lengo kuu la kazi ya pepo wabaya.
Aina ya kumi ni kwamba watu ambao wana kazi ya pepo wabaya huishi maisha yasiyo ya kawaida kabisa. Macho yao hutoa kimulimuli cha kiuaji, na maneno wanyozungumza ni ya kuogofya kabisa, kana kwamba pepo mbaya alikuwa ameshuka ulimwenguni. Hakuna utaratibu wa maisha kwa mtu wa aina hii, ni vigeugeu sana, na ni watu wasiobashirika kama mnyama wa mwitu ambaye hajafunzwa. Wao ni wa kuwakirihi na kuwachukiza wengine sana. Hivyo ndivyo hasa mtu ambaye pepo wabaya wamemfunga anavyoonekana.
Aina kumi zilizo hapo juu ndizo maonyesho makuu ya kazi ya pepo wabaya. Mtu yeyote ambaye huonyesha mojawapo ya maonyesho haya bila shaka atakuwa na kazi ya pepo wabaya. Ili kuwa dhahiri, wote ambao huonyesha maonyesho yaliyo hapo juu ya kazi ya pepo wabaya, bila kujali ni aina gani wanamiliki, ni watu ambao wana kazi ya pepo wabaya. Watu ambao wamepagawa na pepo wabaya mara nyingi hasa wanakuwa wenye chuki na kujitenga na wale ambao Roho Mtakatifu anafanya kazi ndani yao na wanaoweza kuuongea ukweli. Ndivyo inavyokuwa mara nyingi kwamba watu wanapokuwa bora zaidi, ndipo wanapotaka kuwashambulia na kuwashutumu, ilhali watu wanapokosa mwelekeo na kuchanganyikiwa zaidi, ndipo wanapofanya kadri wanachoweza kuwalaghai na kuwavisha kilemba cha ukoka, na hasa wao kuwa radhi kujihusisha nao. Kazi ya pepo wabaya hugeuza nyeusi ikawa nyeupe, na kuyafanya mazuri kuwa mabaya na mabaya kuwa mazuri. Hayo ndiyo matendo ya pepo wabaya.
kutoka katika “12 Matatizo Ambayo Makanisa Yote Yanahitaji Kutatua Kwa haraka” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Roho yoyote ambayo kazi yake inajionyesha katika hali isiyo ya ulimwenguni humu ni pepo mbaya, na kazi na matamko ya roho yoyote inayotekeleza kazi isiyo ya ulimwenguni humu ndani ya watu ni kazi ya pepo mbaya; mbinu hizi zote ndizo ambazo pepo wabaya hufanya kazi na si za kawaida na za humu ulimwenguni, na zinaonyeshwa kimsingi kwa njia sita zifuatazo:
1. Udhibiti wa moja kwa moja wa uneni wa watu, jambo ambalo linaonyesha waziwazi kwamba pepo mbaya anazungumza, na wala si watu wenyewe wanaozungumza kwa kawaida;
2. Hisia kwamba pepo mbaya anawaelekeza watu na kuwaamuru kufanya hiki na kile;
3. Watu ambao, wakati wakiwa kwenye chumba, wanaweza kujua wakati mtu yuko karibu kuingia ndani;
4. Watu ambao mara nyingi wanazisikia sauti zikiwazungumzia na ambazo wengine hawawezi kuzisikia;
5. Watu ambao wanaweza kuona na kusikia mambo ambayo wengine hawawezi;
6. Watu ambao siku zote wanafadhaishwa, na wanajizungumzia wenyewe, na hawawezi kuwa katika mazungumzo ya kawaida au utangamano na watu.
Wale wote ambao pepo mbaya anafanya kazi ndani yao bila kuepukika wanayo maonyesho haya sita. Wao hawana urazini, siku zote wako katika hali ya taharuki, hawawezi kutangamana na watu kwa njia ya kawaida, ni kana kwamba wao hawashawishiki kwa lolote lile, na kuna jambo lililojitenga na lisilo lao. Watu kama hao wamepagawa na pepo mbaya au wanaye pepo mbaya anayefanya kazi ndani yao, na kazi yote ya pepo wabaya inajionyesha na si ya ulimwenguni humu. Hii ndiyo kazi inayotambulika kwa haraka zaidi kuhusu pepo wabaya. Wakati pepo mbaya anapompagaa mtu, anacheza nao kiasi cha kwamba wanaathirika kabisa. Wanakosa urazini, kama zuzu, hali ambayo inathibitisha kwamba kiini cha mambo ni kuwa, pepo wabaya ni pepo waovu wanaopotosha na kuteketeza watu. Matamko ya pepo wabaya ni rahisi kuyatambua: Matamko yao yanaonyesha kikamilifu kiini chao cha uovu, yapo palepale, yamevurugika, na yananuka, yanarishai harufu ya kifo. Kwa watu walio na uhodari mzuri, maneno ya pepo wabaya huwafanya kuhisi utupu na kutovutiwa, yasiyorekebisha maadili, yasiyo na chochote ila uongo na maneno yasiyo na maana, wanahisi wakiwa wamevurugika na wanaona ugumu kuelewa yote haya, kama zigo la upuuzi. Huu ni baadhi ya upuuzi unaotambulika kwa haraka zaidi kuhusu pepo wabaya. Kuwaroga watu, baadhi ya wale pepo wabaya wa “kiwango cha juu” hujifanya kuwa Mungu au Kristo wanapoongea, huku wengine wakijifanya kuwa malaika au watu maarufu. Wanapoongea, pepo hawa wabaya ni stadi katika kuiga maneno au kauli fulani za Mungu, au sauti ya Mungu, na watu wasiouelewa ukweli wanadanganywa kwa urahisi na pepo kama hawa wabaya wa “kiwango cha juu.” Watu wa Mungu waliochaguliwa lazima wawe wazi kwamba, kiini cha mambo ni kwamba, pepo wabaya ni waovu na wasio na aibu, na hata kama wao ni pepo wabaya wa “kiwango cha juu,” wao hawana ukweli kabisa. Pepo wabaya, zaidi ya yote, ni pepo wabaya, kiini cha pepo wabaya ni uovu, na wenye sampuli moja na Shetani.
kutoka katika “Jinsi ya Kutambua Hotuba ya Kishetani na Uongo wa Roho Wabaya, Makristo wa Uongo na Wapinga Kristo” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni