10.23.2019

Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe. Hasa katika enzi ya mwisho ambapo mwanadamu atakamilishwa, Mungu atafanya kazi mpya hata haraka zaidi. Hivyo, bila utii moyoni mwake, mwanadamu ataona vigumu kufuata nyayo za Mungu. Mungu hafuati kanuni zozote, wala hachukulii hatua yoyote ya kazi Yake kama isiyobadilika. Badala yake, kazi Anayofanya daima ni mpya zaidi na daima ni juu zaidi. Kazi Yake inazidi kuwa ya utendaji kwa kila hatua, sambamba zaidi na matendo halisi ya mwanadamu. Baada tu ya mwanadamu kuwa na uzoefu wa aina hii ya kazi ndipo anaweza kufikia mabadiliko ya mwisho ya tabia yake. Maarifa ya mwanadamu ya maisha yanakua hata juu zaidi, na vivyo hivyo kazi ya Mungu pia inakuwa juu zaidi. Mwanadamu anaweza kufikia ukamilifu kwa njia hii tu na kufaa kwa matumizi ya Mungu. Kwa upande mmoja, Mungu anafanya kazi hivi ili kupinga na kubadilisha fikira za mwanadamu, na kwa upande mwingine, kumwongoza mwanadamu katika hali ya juu zaidi na kweli zaidi, hadi katika ulimwengu wa juu zaidi wa imani katika Mungu, ili mwishowe, mapenzi ya Mungu yaweze kufanyika. Wote walio na asili isiyotii wanaopinga kwa kusudi wataachwa nyuma na hatua hii ya kazi ya Mungu ya haraka na yenye kusonga mbele kwa nguvu; wale tu walio na moyo mtiifu na wako tayari kuwa wanyonge wataendelea hadi mwisho wa njia. Katika kazi kama hii, nyote mnapaswa kujua jinsi ya kutii na kuweka kando fikira zenu. Mnapaswa kuwa waangalifu katika kila hatua mnayochukua. Kama wewe ni mzembe, hakika utakuwa mmoja wa wale wanaochukiwa na kukataliwa na Roho Mtakatifu na yule anayemkatiza Mungu katika kazi Yake. … Kazi inayofanywa na Mungu ni tofauti kutoka kipindi kimoja hadi kingine. Ukionyesha utii mkubwa katika awamu moja, lakini katika awamu ifuatayo uonyeshe utii mdogo ama usionyeshe wowote, basi Mungu atakuacha. Ukienda sambamba na Mungu anapopaa hatua hii, basi lazima uendelee kuwa sambamba Anapopaa ifuatayo. Ni hapo tu ndipo utakuwa mtu ambaye ni mtiifu kwa Roho Mtakatifu. Kwa sababu unamwamini Mungu, lazima ubakie daima katika utii wako. Huwezi tu kutii unapotaka na kutotii usipotaka. Namna hii ya utii haikubaliki na Mungu. Kama huwezi kwenda sambamba na kazi mpya Ninayoshiriki na uendelee kuyashikilia maneno ya zamani, basi kutakuaje na ukuaji katika maisha yako? Kazi ya Mungu ni kukuruzuku kupitia neno Lake. Unapotii na kulikubali neno Lake, basi Roho Mtakatifu hakika atafanya kazi ndani yako. Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa njia Ninayozungumza kabisa. Fanya Nilivyosema, na Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako mara moja. Natoa mwangaza mpya ili muweze kuona na kuwaleta kwa mwangaza wa wakati wa sasa. Unapotembea katika mwangaza huu, Roho Mtakatifu ataanza kazi ndani yako mara moja.
kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Hivi sasa, njia ambayo Roho Mtakatifu hutembea ni maneno halisi ya Mungu. Kwa hiyo, kwa mtu kuitembea, ni lazima atii, na kula na kunywa maneno halisi ya Mungu mwenye mwili. Anafanya kazi ya neno, na kila kitu kinaanza kutoka kwa neno Lake, na kila kitu kinaanzishwa juu ya neno Lake, neno Lake la sasa. Kama ni kuwa bila shaka yoyote kabisa kuhusu Mungu kuwa mwili au kumjua Yeye, mtu anapaswa kuweka bidii zaidi katika maneno Yake. Vinginevyo, hawezi kutimiza chochote kamwe, na ataachwa bila chochote. Ni kwa kuja kumjua Mungu tu na kumridhisha kwa msingi wa kula na kunywa maneno Yake ndipo mtu anaweza kuanzisha polepole uhusiano unaofaa na Yeye. Kula na kunywa maneno Yake na kuyaweka katika matendo ni ushirikiano bora zaidi na Mungu, na ni kitendo kinachotoa ushuhuda vizuri zaidi kama mmoja wa watu Wake. Mtu akielewa na aweze kutii kiini cha maneno halisi ya Mungu, anaishi katika njia inayoongozwa na Roho Mtakatifu na ameingia katika njia sahihi ya Mungu kumkamilisha mwanadamu.
kutoka katika “Wale Ambao Tabia Yao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kiwango cha chini zaidi ambacho Mungu anahitaji kwa watu ni kwamba waweze kufungua mioyo yao Kwake. Ikiwa mwanadamu atautoa moyo wake wa kweli kwa Mungu na kusema kile kilicho ndani ya moyo wake kwa Mungu, basi Mungu yuko tayari kufanya kazi ndani ya mwanadamu; Mungu hataki moyo wa mwanadamu uliopotoka, lakini moyo wake ulio safi na mwaminifu. Ikiwa mwanadamu hasemi yaliyo moyoni mwake kwa Mungu kwa kweli, basi Mungu haugusi moyo wa mwanadamu, au kufanya kazi ndani yake.
kutoka katika “Kuhusu Desturi ya Sala” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima kwanza uutoe moyo wako kwa Mungu, na uuweke moyo wako uwe mtulivu mbele za Mungu. Baada tu ya kuutoa moyo wako mzima katika Mungu ndipo utaweza kuwa na maisha ya kawaida ya kiroho hatua kwa hatua. Kama, kwa imani yao katika Mungu, watu hawautoi moyo wao kwa Mungu, ikiwa moyo wao hauko katika Mungu, na wala hawauchukulii mzigo wa Mungu kama wao wenyewe, basi kila kitu wanachofanya ni kumdanganya Mungu, nayo ni matendo ya watu wa kidini, wasioweza kuipokea sifa ya Mungu. Mungu hawezi kupata kitu chochote kutoka kwa aina hii ya mtu; aina hii ya mtu anaweza tu kutumika kama foili[a] kwa kazi ya Mungu, kama pambo katika nyumba ya Mungu, kuchukua nafasi, naye hana manufaa—Mungu hamtumii aina hii ya mtu. Katika mtu kama huyo, sio tu kwamba hakuna nafasi kwa ajili ya kazi ya Roho Mtakatifu, hata zaidi hakuna thamani ya ukamilifu; aina hii ya mtu ni “mfu atembeaye” halisi—hana sehemu ambazo zinaweza kutumika na Roho Mtakatifu—wao wote wametwaliwa na Shetani, kupotoshwa kwa kiwango kilichokithiri na Shetani, ambao ni chombo cha kuondolewa na Mungu. Kwa sasa Roho Mtakatifu hawatumii tu watu kwa kuyaweka maadili yao katika matumizi, lakini pia kuwakamilisha na kubadilisha dosari zao. Kama moyo wako unaweza kumiminwa ndani ya Mungu, na kukaa kimya mbele za Mungu, basi utakuwa na nafasi na sifa za kuhitimu ili kutumiwa na Roho Mtakatifu, kupokea nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na hata zaidi, utakuwa na nafasi kwa Roho Mtakatifu kufidia dosari zako. Unapoutoa moyo wako kwa Mungu, unaweza kuingia kwa undani zaidi kwenye upande mzuri na kuwa kwenye kiwango cha juu zaidi cha uelewaji; katika upande hasi, utakuwa na uelewa zaidi wa makosa na dosari zako mwenyewe, utakuwa na hamu zaidi ya kutafuta kuyakidhi mapenzi ya Mungu, na hutakuwa katika hali ya kukaa tu, utaingia ndani kwa utendaji. Hii itamaanisha kuwa wewe ni mtu sahihi.
kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kufaa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Roho Mtakatifu anafanya kazi kwa kanuni hii: kupitia ushirikiano na watu, kupitia kwa wao kuomba kimatendo, kumtafuta na kusonga karibu na Mungu, matokeo yanaweza kupatikana na wanaweza kupata nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu. Si kwamba Roho Mtakatifu anafanya kazi kivyake, au mwanadamu anafanya kazi kivyake. Wote ni wa muhimu, na jinsi wanadamu wanavyoshiriki zaidi na jinsi wanavyotaka zaidi kufikia viwango vya mahitaji ya Mungu, ndivyo kazi ya Roho Mtakatifu inaimarika. Ni ushirikiano halisi tu wa wanadamu, kupitia kazi ya Roho Mtakatifu, ndivyo vinaweza kutoa matukio halisi na ufahamu wa kweli wa kazi ya Mungu. Hatua kwa hatua, kupitia kwa mazoea kwa njia hii, mwanadamu mkamilifu hatimaye huzalishwa. Mungu hafanyi vitu vya miujiza; katika dhana za mwanadamu, Mungu ni mwenye uweza, na kila kitu kinafanywa na Mungu—na hutokea kwamba watu wanasubiri tu bila kufanya chochote, hawasomi maneno ya Mungu au kuomba, na wanasubiri tu kuguswa na Roho Mtakatifu. Walio na ufahamu sahihi, hata hivyo, wanaamini hili: matendo ya Mungu yanaweza kufikia pale ambapo ushirikiano wangu umefikia, na athari ya kazi ya Mungu kwangu inategemea namna ninavyoshirikiana. Mungu anenapo, ninapaswa kufanya lolote niwezalo na kuyaelekea maneno ya Mungu; hili ndilo ninapaswa kufanikisha.
kutoka katika “Jinsi ya Kujua Uhalisi” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika uzoefu wako unaona kuwa moja ya masuala muhimu zaidi ni kuutuliza moyo wako mbele ya Mungu. Ni suala ambalo linahusu maisha ya kiroho ya watu, na kuendelea kwa maisha yao. Ni kama tu moyo wako uko na amani mbele za Mungu ndio kutafuta kwako ukweli na mabadiliko katika tabia yako kutazaa matunda. Kwa sababu unakuja ukiwa na mizigo mbele za Mungu na huwa unahisi kila mara kuwa unapungukiwa kiasi kikubwa, kwamba kuna ukweli mwingi ambao unahitaji kujua, uhalisi mwingi unaohitaji kupitia, na kwamba unapaswa kujali kikamilifu kuhusu mapenzi ya Mungu—mambo haya kila mara huwa mawazoni mwako, ni kana kwamba yamekufinyia chini sana kiasi kwamba huwezi kupumua, na hivyo unahisi mzito wa moyo (lakini sio kwa hali hasi). Ni watu wa aina hii pekee ndio wanastahili kukubali kupata nuru ya maneno ya Mungu na kuguswa na Roho wa Mungu. Ni kwa sababu ya mzigo wao, kwa sababu ni wenye moyo mzito, na, inaweza kusemwa, kwa sababu ya gharama ambayo wamelipa na mateso ambayo wamepitia mbele ya Mungu ndio wanapata nuru na mwangaza wa Mungu, kwa kuwa Mungu hamtendei yeyote kwa upendeleo. Yeye huwa mwenye haki kila mara katika kuwatendea watu, lakini Yeye sio holela katika kuwakimu watu, na hawapi bila masharti. Huu ni upande mmoja wa tabia Yake yenye haki. Katika maisha halisi, watu wengi bado hawajaufikia ulimwengu wa aina hii. Kwa kiwango cha chini zaidi, mioyo yao bado haijamgeukia Mungu kikamilifu, na hivyo bado hakujakuwa na mabadiliko yoyote makubwa katika tabia ya maisha yao. Hii ni kwa sababu wanaishi tu kati ya neema ya Mungu, na bado hawajapata kazi ya Roho Mtakatifu. Vigezo vya Mungu kuwatumia watu ni kama ifuatavyo: Mioyo yao inamgeukia Mungu, wanasumbuliwa na maneno ya Mungu, wanakuwa na mioyo ya kutamani, na wako na azimio la kutafuta ukweli. Ni watu wa aina hii tu ndio wanaoweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu na mara kwa mara wapate nuru na mwangaza.
kutoka katika “Ni Muhimu Sana Kuanzisha Uhusiano wa Kufaa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuna sharti moja kwa kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya watu. Bora wako tayari kutafuta na hawasitisiti ama kuwa na shaka kuhusu matendo ya Mungu, nao wanaweza kushikilia wajibu wao kila wakati, hivi tu ndivyo wanaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Katika kila hatua ya kazi ya Mungu, kinachohitajika kwa wanadamu ni imani kuu na kutafuta mbele za Mungu—kupitia tu kwa mazoea ndipo watu wataweza kugundua jinsi Mungu Anavyopendeka na jinsi Roho Mtakatifu Anavyofanya kazi ndani ya watu. Usipopata uzoefu, usipoihisi njia yako kupitia hayo, usipotafuta, hutapata chochote. Lazima uhisi njia yako kupitia mazoea yako, na kwa kupitia mazoea yako tu ndipo utaona matendo ya Mungu, na kugundua maajabu Yake na mambo Yake yasiyoeleweka.
kutoka katika “Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuna kanuni kwa kukamilishwa kwa watu na Mungu, ambayo ni kwamba Yeye hukupa nuru kwa kutumia sehemu yako inayofaa ili uwe na njia ya kutenda na unaweza kujitenga na hali zote hasi, ikisaidia roho yako kupata uhuru, na ikikufanya uweze kumpenda zaidi. Kwa njia hii, unaweza kuiacha tabia potovu ya Shetani. Wewe huna hila na uko wazi, ukiwa tayari kujijua, na ukiwa tayari kutia ukweli katika vitendo. Mungu huona kwamba uko tayari kujijua na uko tayari kutia ukweli katika vitendo, kwa hiyo unapokuwa dhaifu na hasi, Yeye hukupa nuru maradufu, Akikusaidia kujijua zaidi, kuwa tayari kujitubia, na kuweza zaidi kutenda mambo ambayo unapaswa kuyatenda. Ni kwa njia hii tu ambapo moyo wako unahisi amani na utulivu. Mtu ambaye kwa kawaida huzingatia kumjua Mungu, ambaye huzingatia kujijua, ambaye huzingatia vitendo vyake mwenyewe ataweza kupokea kazi ya Mungu mara kwa mara, mara kwa mara kupokea mwongozo na nuru kutoka kwa Mungu. Hata ingawa yuko katika hali hasi, anaweza kugeuka mara moja, iwe ni kwa sababu ya matendo ya dhamiri au kwa sababu ya nuru kutoka kwa neno la Mungu.
kutoka katika “Ni Wale Wanaolenga Kutenda tu Ndio Wanaweza Kukamilishwa” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika maisha yako ya kila siku, unapaswa kuyaelewa maneno hayo uyasemayo na mambo hayo uyafanyayo ambayo yatasababisha uhusiano wako na Mungu kuwa usio wa kawaida, halafu ujirekebishe na kuingia katika tabia sahihi. Yachunguze maneno yako, vitendo vyako, kila mwenendo wako, na fikra zako na mawazo wakati wote. Ielewe hali yako ya kweli na ingia katika njia ya kazi ya Roho Mtakatifu. Ni kwa njia hii tu ndipo unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu. Kwa kupima iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kurekebisha makusudi yako, kuielewa asili ya mwanadamu, na kujielewa mwenyewe; kupitia hili, utaweza kuingia katika uzoefu halisi, na kujinyima kwa kweli, na kupata utiifu wa makusudi. Katika masuala hayo kama unapokuwa unapitia iwapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, utaweza kupata fursa za kukamilishwa na Mungu, utaweza kuelewa hali nyingi, ambazo kwazo Roho Mtakatifu Anafanya kazi, na utaweza kubaini mengi ya udanganyifu na njama za Shetani. Ni kupitia njia hii tu ndipo unaweza kukamilishwa na Mungu. Unaweka uhusiano wako na Mungu sawa ili kwamba ujisalimishe mwenyewe mipangilio yote ya Mungu. Ni ili utaingia kwa kina zaidi katika uzoefu halisi, na kupata kazi zaidi ya Roho Mtakatifu. …
… Kwa kila tamshi la Mungu, baada ya kulisoma na kupata ufahamu, utaliweka katika vitendo. Bila kujali ulivyokuwa ukitenda kabla—pengine huko nyuma mwili wako ulikuwa dhaifu, ulikuwa muasi, na ulipinga—hili silo jambo kubwa, na haliwezi kuzuia maisha yako yasikue leo. Ilimradi unaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na Mungu leo, basi kuna tumaini. Ikiwa kwa kila wakati unaposoma maneno ya Mungu, unakuwa na mbadiliko na kuruhusu watu wengine kuona kwamba maisha yako yamebadilika kuwa mazuri, inaonyesha kwamba una uhusiano wa kawaida na Mungu na kwamba umewekwa sawa. Mungu hashughulikii watu kulingana na dhambi zao. Ilimradi unaweza kutoasi tena na hupingi tena baada ya wewe kuelewa na kufahamu, basi Mungu atakuwa bado Ana huruma na wewe. Unapokuwa na ufahamu huu na nia ya kutafuta kukamilishwa na Mungu, basi hali yako katika uwepo wa Mungu itakuwa ya kawaida. Bila kujali unachofanya, zingatia: Mungu atafikiri nini ikiwa nitafanya hiki? Kitawaathiri vipi ndugu? Chunguza makusudi yako katika maombi, ushirika, usemi, kazi na kuhusiana na watu, na chunguza endapo uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida au si wa kawaida. Ikiwa huwezi kutofautisha makusudi yako na fikra zako, basi huna ubaguzi, kitu ambacho kinathibitisha kwamba unaelewa kidogo sana kuhusu ukweli. Kuwa na ufahamu ulio wazi wa kila kitu ambacho Mungu hufanya, vitazame vitu kulingana na neno la Mungu na vitazame vitu kwa kusimama katika upande wa Mungu. Kwa njia hii mitazamo yako itakuwa sahihi. Kwa hiyo, kujenga uhusiano mzuri na Mungu ni kipaumbele cha juu kwa mtu yeyote anayemwamini Mungu; kila mtu anapaswa kuichukulia kama kazi muhimu na kama tukio lao kubwa la maisha. Kila kitu unachofanya kinapaswa kipimwe dhidi ya iwapo una uhusiano wa kawaida na Mungu au la. Ikiwa uhusianao wako na Mungu ni wa kawaida na makusudi yako ni sahihi, basi kifanye. Ili kudumisha uhusiano wa kawaida na Mungu, hupaswi kuogopa kupoteza maslahi binafsi, hupaswi kumruhusu Shetani kushinda, hupaswi kumruhusu Shetani kupata kitu dhidi yako, na hupaswi kumruhusu Shetani kukufanya uwe kichekesho. Kusudi kama hili ni udhihirisho kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Si kwa ajili ya mwili, badala yake ni kwa ajili ya amani ya roho, ni kwa ajili ya kupata kazi ya Roho Mtakatifu na kwa ajili ya kuyaridhisha mapenzi ya Mungu. Ili kuingia katika hali sahihi, unapaswa kujenga uhusiano mzuri na Mungu, unapaswa kuweka sawa mtazamo wako wa imani kwa Mungu. Ni kumruhusu Mungu kukupata, kumruhusu Mungu kufichua matunda ya maneno Yake kwako na kukuangazia na kukupatia nuru zaidi. Kwa namna hii utaingia katika tabia nzuri.
kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anafanya kazi ndani ya wale wanaotafuta na kulithamini neno la Mungu. Kadri unavyolithamini neno la Mungu, ndivyo Roho wa Mungu atakavyofanya kazi zaidi ndani mwako. Kadri mtu anavyolithaminineno la Mungu, ndivyo nafasi yake ya kukamilishwa na Mungu inavyokuwakubwa. Mungu anawakamilisha wale ambao wanampenda Yeye kwa kweli. Anawakamilisha wale ambao mioyo yao iko katika amani mbele Yake. Ukiithamini kazi yote ya Mungu, ukiuthamini mwanga wa Mungu, ukiuthamini uwepo wa Mungu, ukithamini kujali na kuwekwa kwa Mungu, ukithamini jinsi neno la Mungu linakuwa ukweli wako na utoaji wa maisha, unafuata zaidi moyo wa Mungu. Ukiithamini kazi ya Mungu, ukiithamini kazi yote ambayo Mungu Amefanya juu yako, Mungu Atakubariki na kufanya kila kitu kilicho chako kuongezeka.
kutoka katika “Mungu Anakamilisha Wale Wanaoufuata Moyo Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Roho Mtakatifu hufanya kazi kulingana na maneno ya Kristo, na hufanya kazi pia kulingana na watu kukubali na kumtii Kristo. Ni ikiwa tu watu watamkubali Kristo na kumtii Kristo ndipo wanaweza kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ikiwa watu humpinga Kristo au kuasi dhidi ya Kristo, basi hawatakuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Kama imani ya mtu kwa Mungu inaweza kuwaletea wokovu inaamuliwa na kama anaweza kweli kumkubali na kumtii Kristo au la. Kazi ya Roho Mtakatifu imejitegemeza kikamilifu kwa mtu kukubali na kumtii Kristo. Katika Enzi ya Neema, kazi ya Roho Mtakatifu ilifanywa kulingana na watu kukubali Bwana Yesu, kumtii Yeye, na kumwabudu Yeye. Katika Enzi ya Ufalme, kazi ya Roho Mtakatifu inafanywa kulingana na watu kukubali Mwenyezi Mungu, kumtii Mwenyezi Mungu, na kumwabudu Mwenyezi Mungu. Katika siku za mwisho, Roho Mtakatifu hufanya kazi kulingana na maneno ya Mwenyezi Mungu, ili kuwaleta waumini katika uhalisi wa maneno ya Mungu na kuwafanya wafikie wokovu na ukamilifu. Huu ni msingi na kanuni ya kazi ya Roho Mtakatifu. Viongozi wengi wa dini wamekufa kama adhabu ya kumpinga au kumlaumu Kristo. Watu wengi wa kidini wamepoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kuanguka katika giza kupitia kukataa kwao kumkubali Kristo wa siku za mwisho. Katika nyumba ya Mungu, maisha ya watu wengi yamechakaa na wamekata tamaa kwa sababu ya fikra zao za kudumu juu ya Kristo, na bado wengi wengine wametengwa na kazi ya Roho Mtakatifu kwa kumwamini tu Roho wa Mungu na si Kristo. Mambo haya yote yamesababishwa na watu kutomkubali na kumtii Kristo. Iwapo muumini ana kazi ya Roho Mtakatifu au la huamuliwa kikamilifu na mtazamo wake kwa Kristo. Ikiwa mtu anamwamini tu Mungu wa mbinguni, na hamtii Kristo, hatapokea kazi ya Roho Mtakatifu kamwe. Kwa sasa, bado kuna watu wengi katika makanisa mbalimbali ambao humwamini tu Roho Mtakatifu lakini hawamwamini Kristo, na hivyo hupoteza kazi ya Roho Mtakatifu. Kuna wengi ambao huamini tu maneno ya Kristo, lakini hawamtii Kristo, na kwa hivyo wanachukiwa na Mungu. Kwa hivyo, kumkubali Kristo na kumtii Kristo ni muhimu katika kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu. Ni iwapo tu mtu humkubali Kristo na kumtii Kristo ndipo atapata wokovu na kukamilishwa. Inaweza kuonekana basi kwamba kazi ya Roho Mtakatifu katika kila enzi ina misingi na kanuni yake. Watu wengi sana bado hawaoni umuhimu wa kumtii Kristo. Roho Mtakatifu hufanya kazi kulingana na maneno ya Kristo kabisa. Ikiwa watu hawawezi kuyakubali maneno ya Kristo, na wanaendelea kushikilia fikra kuhusu na wakayapinga maneno ya Mungu, basi hawawezi kabisa kupokea kazi ya Roho Mtakatifu. Watu wengi huomba tu katika jina la Mwenyezi Mungu, lakini hawatii kazi ya Kristo, na hawakubali kabisa maneno ya Kristo. Watu kama hawa ni wapinga Kristo, na hawawezi kabisa kuipokea kazi ya Roho Mtakatifu.
kutoka katika “Matokeo Ambayo Yanaweza Kufanikishwa na Ufahamu Halisi wa Ukweli” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha
Almuradi unatafuta kujijua mwenyewe na kuutafuta ukweli, Roho Mtakatifu atafanya kazi ndani yako. Ingawa huhisi jinsi Roho Mtakatifu anavyofanya kazi, lakini utakuwa na ufahamu zaidi wa ukweli na wako mwenyewe kwa msingi wa neno la Mungu, naam, hili ndilo hufanya kazi ya Roho Mtakatifu kuwa ya ajabu sana. Si ya kimwujiza kabisa kwa njia inavyokusaidia kujielewa mwenyewe na kuuelewa ukweli. Je, huoni kwamba Mungu ni mwenyezi? Je, si Mungu ni wa ajabu? Hivi ndivyo kazi ya Roho Mtakatifu ilivyo ya ajabu. Kwa nje, hujui jinsi Roho Mtakatifu anavyofanya kazi Yake. Ikiwa umepata uzoefu kwa muda mfupi, kimsingi huelewi. Hata hivyo, baada ya kuipitia kwa muda mrefu zaidi, utajiona ukibadilika. Mtazamo wako juu ya mambo utabadilika. Ujuzi wako wa neno la Mungu utabadilika na kuendelea. Utakuwa na ukuaji na kuingia inapokuja kwa ukweli. Maarifa yako kuhusu upotovu wako yatakuwa na maendeleo ya kina zaidi na karibu sana na kiini. Haya ni matunda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Kazi ya Roho Mtakatifu hasa ni kuwaongoza watu kuingia katika neno la Mungu na kuuelewa ukweli. Ni vipengele vipi kuingia katika neno la Mungu kunavihusisha? Kuingia katika neno la Mungu hakumaanishi kwamba mtu anasoma sentensi moja mahsusi ya Mungu, anaizingatia kidogo na kisha ana uelewa kidogo. Huku si sawa na kuingia katika neno la Mungu. Hakuko namna hii. Jambo muhimu zaidi ni kuingia katika neno la Mungu kupitia uzoefu. “Uzoefu” huu unahusisha tajriba anuwai. Uzoefu wa mwanadamu sio kipengele kimoja tu cha uzoefu, lakini una sehemu nyingi. Kutimiza wajibu wa mtu ni kupitia neno la Mungu. Kuweka ukweli katika matendo pia ni kupitia neno la Mungu. Hasa, kupitia aina mbalimbali za majaribu na usafishwaji hata zaidi sana ni kupitia neno la Mungu. Almuradi unapitia neno la Mungu, bila kujali mazingira au tukio, utaweza kupata kazi ya Roho Mtakatifu. Kwa mfano, tunapokabiliwa na majaribu, sisi humwomba Mungu na tunajaribu kuelewa mapenzi ya Mungu. Matokeo yake, Roho Mtakatifu hutupa nuru na kutuwezesha kuyaelewa mapenzi ya Mungu. Hivi ndivyo kwa sababu inahusiana na kuingia katika neno la Mungu.
kutoka katika “Kujua Kazi ya Roho Mtakatifu Kuna Umuhimu Mkubwa kwa Wokovu wa Mwanadamu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha II


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni