Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neno-la-mungu-45. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo neno-la-mungu-45. Onyesha machapisho yote

10.23.2019

Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe.

10.22.2019

Kazi ya Roho Mtakatifu ni nini? Kazi ya Roho Mtakatifu hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu.

10.15.2019

Kiongozi wa uongo au mchungaji wa uongo ni nini? Je, kiongozi wa uongo au mchungaji wa uwongo anaweza kutambuliwaje?



Maneno Husika ya Mungu:
Wale ambao wanaweza kufuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu, na ambao wanaweza kuzifuata nyayo za Mungu, kiasi kwamba wamfuate Mungu popote Awaongozapo—hawa ni watu ambao wamebarikiwa na Mungu. Wale wasiofuata kazi ya sasa ya Roho Mtakatifu hawajaingia katika kazi ya maneno ya Mungu, na haijalishi wanafanya kazi kiasi gani, au mateso yao ni makubwa vipi, au wanakimbia hapa na pale kiasi gani, hakuna linalomaanisha chochote kwa Mungu kati ya hayo, na Yeye hatawasifu.

10.13.2019

Mpinga Kristo ni nini? Mpinga Kristo anaweza kutambuliwaje?


Maneno Husika ya Mungu:
Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa upinzani kwa Mungu wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu.