Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo dutu-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo dutu-ya-Mungu. Onyesha machapisho yote

10.22.2019

Kazi ya Roho Mtakatifu ni nini? Kazi ya Roho Mtakatifu hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu.

10.19.2019

Kumfuata mtu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa huchukuliwa kama wenye dharau. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni.

10.17.2019

Asiyeamini ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:

      Kwa sababu unamwamini Mungu, basi lazima uweke imani ndani ya maneno yote ya Mungu na ndani ya kazi Yake yote. Hii ni kusema kwamba, kwa sababu unamwamini Mungu, ni lazima umtii. Kama huwezi kufanya hivi, basi haijalishi iwapo unamwamini Mungu. Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini.

10.16.2019

Unafiki ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Ufafanuzi wa neno “Mfarisayo” ni upi? Ni mtu ambaye ni mnafiki, ambaye ni bandia na anajifanya katika kila kitu anachofanya, akijifanya kuwa mwema, mwenye fadhila, na mzuri. Je, hivyo ndivyo alivyo kwa kweli? Yeye ni mnafiki, na hivyo kila kitu kinachodhihirika na kufichuliwa ndani yake ni cha uongo, yote ni kujifanya—sio hali yake ya kweli. Hali yake ya kweli imefichwa ndani ya moyo wake; haionekani. Watu wasipofuatilia ukweli, kama hawaelewi ukweli, basi maarifa yao ya kidini na nadharia ambazo wamepata zinakuwa nini? Je, zinakuwa maneno ya mafundisho ambayo watu huzungumzia mara nyingi? Watu hutumia haya yanayodaiwa kuwa mafundisho sahihi kujifanya na kujionyesha kuwa wazuri.

10.12.2019

Kwa nini makanisa yanaweza kupotoka na kuwa dini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya. Ikiwa imesimama juu ya msingi wake asili, kazi ya Roho Mtakatifu imepiga hatua kadhaa kwa kina.

10.08.2019

Kuna tofauti ipi kati ya mtu kutekeleza wajibu wake na kutoa huduma?

Maneno Husika ya Mungu:
Hakuna uhusiano kati ya wajibu wa mwanadamu na endapo amebarikiwa au amelaaniwa. Wajibu ni kile ambacho mwanadamu anapaswa kutimiza; ni wajibu wake na hautegemei fidia, masharti, au sababu. Hapo tu ndipo huko kutakuwa kufanya wajibu wake. Mwanadamu aliyebarikiwa hufurahia wema baada ya kufanywa mkamilifu baada ya hukumu. Mwanadamu aliyelaaniwa hupokea adhabu tabia yake isipobadilika hata baada ya kutiwa adabu na kuhukumiwa, yaani, hajakamilishwa. Kama kiumbe, mwanadamu anapaswa kutimiza wajibu wake, afanye anachopaswa kufanya, na afanye anachoweza kufanya, bila kujali kama atabarikiwa au kulaaniwa. Hili ndilo sharti la msingi kwa mwanadamu, kama anayemtafuta Mungu.

10.03.2019

Mtu mwaminifu ni nani? Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu?

Mtu mwaminifu ni nani? Kwa nini Mungu huwapenda watu waaminifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Uaminifu unamaanisha kumpa Mungu moyo wako; kutomdanganya katu katika kitu chochote; kuwa wazi Kwake katika mambo yote, kutowahi kuficha ukweli; kutowahi kufanya kile kinachowadanganya wale walio juu na kuwafumba macho wale walio chini; na kutowahi kufanya kile ambacho kinakupendekeza kwa Mungu. Kwa ufupi, kuwa waaminifu ni kujizuia dhidi ya uchafu katika matendo na maneno yenu, na kutomdanganya Mungu wala binadamu.

10.01.2019

Inamaanisha nini kuomba kwa kweli?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi

Maneno Husika ya Mungu:
Ni nini maana ya kuomba kwa kweli? Ina maana ya kuzungumza maneno yaliyo ndani ya moyo wako kwa Mungu, na kuwasiliana na Mungu baada ya kufahamu mapenzi Yake na kutegemea maneno Yake; ina maana ya kuhisi kuwa karibu na Mungu hasa, kuhisi kwamba Yeye yuko mbele yako, na kwamba una kitu cha kumwambia; na inamaanisha kuwa mwangavu hasa ndani ya moyo wako, na kuhisi kwamba Mungu ni wa kupendeza hasa. Utajisikia kutiwa moyo sana, na baada ya kusikia maneno yako ndugu zako watajisikia kufurahishwa, watahisi kwamba maneno unayosema ni maneno yaliyo ndani ya mioyo yao, maneno ambayo wangependa kusema, na kwamba kile unachosema kinawakilisha kile wanachotaka kusema.

9.28.2019

Hukumu ni nini?

Hukumu ni nini?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu.

9.23.2019

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hushikilia mamlaka katika ulimwengu wa kidini na watu wengi huwatii na kuwafuata—huu ni ukweli. Unasema kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hawaukubali ukweli wa Mungu kuwa amekuwa mwili, kwamba hawaamini ukweli ulioonyeshwa na Mungu mwenye mwili na kwamba wanaitembea njia ya Mafarisayo, na tunakubaliana na jambo hili. Lakini kwa nini unasema kuwa wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote ni Mafarisayo wanafiki, kuwa wote ni wapinga Kristo waliofichuliwa na kazi ya Mungu katika siku za mwisho, na kwamba wataingia katika maangamizo mwishoni? Hatuwezi kukubali jambo hili kwa wakati huu. Tafadhali shiriki unachotegemeza dai hili, kwamba watu hawa hawawezi kuokolewa na kwamba ni lazima wote waingie katika maangamizo.

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

Jibu:
Asili ya jinsi watu katika jamii ya kidini wanavyomkana Mungu zinaweza tu kufichuliwa na kuchanguliwa baada ya kuja kwa Kristo mwenye mwili. Hakuna wanadamu wapotovu wanaoweza kuutambua ukweli na asili ya jamii ya kidini ya kumkana Mungu, kwa sababu wanadamu wapotovu hawana ukweli. Wanaweza tu kudhibitiwa, kuchanganywa, na kuchezewa na wachungaji wa uwongo na pepo wapinga Kristo ili kujiunga nao katika kufanya uovu, na kuwa watumishi na washiriki wa Shetani katika kumkana Mungu. Hili ni jambo la kawaida. … Hebu tuone jinsi, wakati wa Enzi ya Neema, Bwana Yesu alivyoufichua ukweli na asili ya jinsi pepo wabaya wapinga Kristo katika jamii ya kidini walivyomuasi Mungu daima:

9.20.2019

Wakati huo, wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, Mafarisayo Wayahudi walimkana na kumhukumu Yeye vikali na kumtundika msalabani. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anapokuja kufanya kazi Yake, wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa pia wanamkana Yeye vikali na kumhukumu Yeye, wakimtundika Mungu msalabani tena. Kwa nini Mafarisayo Wayahudi na wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa huuchukia ukweli hivyo na kumpinga vikali Kristo kwa njia hii? Ni nini hasa kiini chao cha asili?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

Wakati huo, wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, Mafarisayo Wayahudi walimkana na kumhukumu Yeye vikali na kumtundika msalabani. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anapokuja kufanya kazi Yake, wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa pia wanamkana Yeye vikali na kumhukumu Yeye, wakimtundika Mungu msalabani tena. Kwa nini Mafarisayo Wayahudi na wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa huuchukia ukweli hivyo na kumpinga vikali Kristo kwa njia hii? Ni nini hasa kiini chao cha asili?

Jibu:
Kila mtu anayeamini katika Bwana anajua Mafarisayo waliompinga Bwana Yesu, lakini mzizi, asili ya kweli ya upinzani wao ilikuwa nini? Unaweza kusema kwamba katika historia ya dini ya miaka 2,000, hakuna mtu aliyeelewa jibu la swali hili. Ingawa kulaani kwa Bwana Yesu kwa Mafarisayo kuliandikwa katika Agano Jipya, hakuna mtu ambaye ameweza kumaizi asili ya Mafarisayo. Mwenyezi Mungu anapowasili katika siku za mwisho, Anafichua jibu la kweli kwa swali hili. Hebu tusome maneno ya Mwenyezi Mungu, “Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima.

9.16.2019

Kwa miaka elfu mbili, imani ya mwanadamu katika Bwana imekuwa imetegemezwa Biblia, na kuja kwa Bwana Yesu hakukuikanusha Biblia ya Agano la Kale. Baada ya Mwenyezi Mungu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, kila mtu anayemkubali Mwenyezi Mungu atalenga kula na kunywa maneno ya Mwenyezi Mungu na aitasoma Biblia mara chache tena. Kile ninachopenda kufuatilia ni, baada ya mtu kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, ni mtazamo gani sahihi hasa mtu anafaa kuwa nao kwa Biblia, na mtu anafaa kuitumia kwa jinsi gani? Imani ya mtu katika Mungu inafaa itegemezwe nini ili mtu aitembee njia ya imani katika Mungu na kupata wokovu wa Mungu?

Biblia ni kumbukumbu halisi ya hatua za kwanza mbili za kazi ya Mungu. Kwa maneno mengine, ni ushuhuda wa hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu, ambazo zinahitimisha uongozi na ukombozi wa wanadamu baada ya kuumbwa kwa mbingu na dunia na vitu vyote, pamoja na wanadamu. Kutokana na kuisoma Biblia, kila mmoja anaweza kuona jinsi Mungu aliwaongoza wanadamu wakati wa Enzi ya Sheria na kuwafundisha kuishi mbele Zake na kumwabudu Yeye. Tunaweza kuona pia jinsi Mungu aliwakomboa wanadamu wakati wa Enzi ya Neema na kuwasamehe dhambi zao zote zilizopita huku akiwapa amani, furaha, na kila aina ya neema. Watu hawawezi tu kuona kwamba Mungu alikuwa amewaumba wanadamu, bali pia kwamba Yeye alikuwa amewaongoza kwa uthabiti na halafu akawakomboa.

9.06.2019

Unashuhudia kuwa katika siku za mwisho Mungu hufanya kazi Yake ya hukumu ili kumtakasa na kumwokoa mwanadamu kabisa, lakini baada ya kusoma maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu, ninaona kwamba baadhi yayo humhukumu na kumlaani mwanadamu. Kama Mungu humhukumu na kumlaani mwanadamu, si basi mwanadamu atapatwa na adhabu? Na unawezaje kusema kwamba aina hii ya hukumu huwatakasa na kuwaokoa wanadamu?

Katika siku za mwisho, Mungu huonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu ili kuunda kikundi cha washindi, kundi la wale ambao ni wenye moyo mmoja na akili moja na Mungu. Hii iliamuliwa na Mungu alipoumba ulimwengu. Unaweza kusema kuwa tayari Mungu amelifanya kundi la washindi, kwamba wote wamefanyika kupitia hukumu na kuadibu kwa Mungu, na kwamba wametoka katika taabu za mateso ya kikatili ya Chama Cha Kikomunisti cha China. Ni ukweli kwamba tayari Mungu amefanya jambo hili; hakuna mtu anayeweza kulipinga. Kuna watu wengine ambao wanaona kwamba baadhi ya maneno ya Mungu yana shutuma na laana ya watu na wao hukuza mawazo. Huu ni upumbavu. Hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni kiti cheupe cha enzi cha hukumu kilichotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo.

9.05.2019

Unashuhudia kwamba Bwana amerudi katika mwili ili kuonyesha ukweli na kufanya kazi ya hukumu na utakaso wa mwanadamu katika siku za mwisho, lakini wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanaamini kwamba Bwana atarudi na mawingu, na kwamba wale wote wanaoamini katika Bwana watabadilika umbo mara moja na watanyakuliwa katika mawingu kukutana na Bwana, kama tu alivyosema Paulo: “Kwani maongezi yetu yako mbinguni; ambako pia tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo: Atakayeubadilisha mwili wetu wa uovu, ili uweze kuwa kwa kadri ya mwili wake wenye utukufu, kulingana na kufanyika ambapo ataweza kuvitiisha vitu vyote kwake” (Wafilipi 3:20-21). Bwana ni mwenye uweza na hakuna kitu ambacho Hawezi kufanya. Mungu atatubadilisha na kututakasa, akifanikisha hili kwa neno moja tu. Hivyo kwa nini bado Anahitaji kupata mwili ili kuonyesha ukweli na kufanya hatua ya kazi ya hukumu na utakaso wa mwanadamu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,siku za mwisho

Kazi ya Mungu kila wakati ni isiyoweza kueleweka. Hakuna yeyote anayeweza kueleza unabii wa Mungu. Mwanadamu anaweza tu kuelewa unabii unapotimizwa. Hii inamaanisha nini? Inamaanisha kuwa hakuna mtu anaweza kuelewa busara na kudura ya Mungu. Wakati Bwana Yesu Alionekana kufanya kazi katika Enzi ya Neema, hakuna mtu angeweza kuielewa. Wakati Mwenyezi Mungu Atafanya kazi ya hukumu ya siku za mwisho katika Enzi ya Ufalme, hakuna mtu anaweza kuijua mapema pia.

9.01.2019

Bibilia inasema: “Kwani mwanadamu husadiki moyoni ili kupata haki; na kwa mdomo hukubali hadi apate wokovu” (Warumi 10:10). Tunaamini kwamba Bwana Yesu alitusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wenye haki kupitia imani. Aidha, tunaamini kwamba mtu akiokolewa mara moja, basi ameokolewa milele, na Bwana atakaporudi tutanyakuliwa na tutaingia katika katika ufalme wa mbinguni. Hivyo kwa nini unashuhudia kuwa tunapaswa kukubali kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho kabla ya kuweza kuokolewa na kuletwa katika ufalme wa mbinguni?

Waumini wote katika Bwana hufikiria: Bwana Yesu alitukomboa Alipokufa msalabani, hivyo tayari tumeondolewa dhambi zote. Bwana hatuoni tena kama wenye dhambi. Tumekuwa wenye haki kupitia kwa imani yetu. Mradi tuvumilie hadi mwisho, tutaokolewa. Bwana atakaporudi tutanyakuliwa moja kwa moja kuingia katika ufalme wa mbinguni. Naam, huo ndio ukweli? Je, Mungu aliwahi kamwe kutoa ushahidi katika maneno Yake wa kuunga mkono madai haya? Kama mtazamo huu hauambatani na ukweli, matokeo yatakuwa ni yapi? Sisi ambao tunamwamini Bwana tunapaswa kutumia maneno Yake mwenyewe kama msingi wa mambo yote.

8.24.2019

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa mara nyingi huwahubiria waumini kwamba mahubiri yoyote yanayosema kwamba Bwana amekuja katika mwili ni uongo. Wao hutegemeza hili aya za Biblia: “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazameni, Kristo yuko huku, au yuko pale; msiamini hili. Kwa kuwa wataibuka Makristo wasio wa kweli, na manabii wasio wa kweli, nao wataonyesha ishara kubwa na vioja; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi” (Mathayo 24: 23-24). Sasa hatuna habari tunavyofaa kumtambua Kristo wa kweli kutoka kwa wale wa uongo, hivyo tafadhali jibu swali hili.

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

Bwana Yesu kweli alitabiri kwamba kungekuwa na Kristo wa uongo na manabii wa uongo katika siku za mwisho. Huu ni ukweli. Lakini Bwana Yesu pia alitabiri wazi mara nyingi kwamba Atarudi. Hakika tunaamini hivyo? Wakati wa kuchunguza unabii wa Bwana Yesu kurudi, watu wengi huupa kipaumbele wasiwasi wao wa Kristo wa uongo na manabii wa uongo. na kutotilia maanani jinsi ya kukaribisha kuwasili kwa bwana harusi, na jinsi ya kusikia sauti ya bwana harusi. Suala ni lipi hapa? Je, si hili ni jambo la kula kwa hofu ya kusongwa, ya kuwa mwenye busara katika umaskini na kuwa mjinga utajirini?

8.17.2019

Kwa nini serikali ya Kikomunisti ya China hutesa kwa ukali, kukandamiza na kuchukulia hatua Mwenyezi Mungu na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

XIX. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Ukweli wa ni Kwa Nini Njia ya Kweli Imepitia Usumbufu Tangu Nyakati za Kale

Kwa nini serikali ya Kikomunisti ya China hutesa kwa ukali, kukandamiza na kuchukulia hatua Mwenyezi Mungu na Kanisa la Mwenyezi Mungu?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Hiki ni kizazi kibaya” (Luka 11:29).
Ulimwengu mzima uko ndani ya maovu” (1 Yohana 5:19).
“Namna ambavyo umeanguka toka mbinguni, Ewe Luciferi, mwana wa asubuhi! Namna ambavyo umeangushwa chini, wewe uliyedhoofisha mataifa! Kwani umesema moyoni mwako, Nitapaa hadi mbinguni, Nitakiinua kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu: Pia nitakaa juu ya mlima wa mkusanyiko, kwa pande za kaskazini: Nitapaa juu ya mawingu; Nitakuwa kama Aliye Juu Zaidi” (Isaya 14:12-14).

8.11.2019

Ukweli ni nini? Maarifa ya Biblia na mafundisho ni nini?

XVII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Kati ya Uhalisi wa Ukweli na Maarifa ya Biblia na Mafundisho

Ukweli ni nini? Maarifa ya Biblia na mafundisho ni nini?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana1:1).
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).
Mimi ndiye njia, ukweli na uhai” (Yohana 14:6).
Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli” (Yohana 17:17).

8.05.2019

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote kweli wamewekwa na Mungu? Kukubali na utii kwa wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa kunawakilisha utii wa mtu kwa Mungu na kumfuata Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki

XV. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Asili ya Mafarisayo na ya Ulimwengu wa kidini ambao Humkana Mungu

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wote kweli wamewekwa na Mungu? Kukubali na utii kwa wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa kunawakilisha utii wa mtu kwa Mungu na kumfuata Mungu?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa hivyo basi, tazama, nimefikiwa na kilio chao wana wa Israeli: na mimi pia nimeona ukandamizaji ambao Wamisri wanatumia kuwakandamiza. Kwa hivyo njoo sasa, nami nitakutuma kwake Farao, ili uwalete watu wangu, wana wa Israeli, kutoka Misri” (Kutoka 3:9-10).
“Yesu akasema kwa Simoni Petro, Simoni, mwana wa Yohana, je, unanipenda Mimi kuliko hawa? … Akasema kwake, Walishe wanakondoo Wangu. Akasema kwake tena mara ya pili, Simioni, mwana wa Yona, unanipenda Mimi? … Akasema kwake, Walishe kondoo Wangu” (Yohana 21:15-16).

8.02.2019

Kwa nini Bwana Yesu aliwalaani Mafarisayo? Ni nini hasa asili ya Mafarisayo?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

XV. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Asili ya Mafarisayo na ya Ulimwengu wa kidini ambao Humkana Mungu

Kwa nini Bwana Yesu aliwalaani Mafarisayo? Ni nini hasa asili ya Mafarisayo?

Aya za Biblia za Kurejelea:
Kwa nini nyinyi pia mnavunja amri ya Mungu kwa utamaduni wenu? Kwani Mungu aliamuru, Akisema, Mwonyeshe babako na mamako heshima: na, Yule anayemlaani baba au mama yake, na afe hicho kifo. Lakini mnasema, Yeyote ambaye atamwambia baba au mama yake, ni zawadi, chochote ambacho ungefaidi kupitia mimi; Na asimwonyeshe baba yake au mama yake heshima, atakuwa huru. Hivyo hamjaibatilisha amri ya Mungu kwa utamaduni wenu. Nyinyi wanafiki, Isaya alitabiri vyema kuwahusu, akisema, Watu hawa wananikaribia kwa vinywa vyao, na wananiheshimu kwa midomo yao; lakini moyo wao uko mbali nami. Lakini wananiabudu bure, wakifunza mafundisho ya dini ambayo ni amri za wanadamu” (Mathayo 15:3-9).