Kwa miaka elfu mbili, dunia nzima ya kidini imeamini kwamba Mungu ni Utatu, na Utatu ni nadharia bora zaidi ya mafundisho yote ya Kikristo. Hivyo, tafsiri ya “Utatu” inashikilia kweli? Utatu una uwepo kweli? Kwa nini unasema kwamba Utatu ni uwongo mkuu mno wa ulimwengu wa kidini?
Jibu:
Nyote mnategemeza uthibitisho wenu kwamba Bwana Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu kwa kile kilichorekodiwa katika Biblia, na kisha mnapomwona Bwana Yesu akimwomba Mungu Baba, hili linadhibitisha zaidi kwenu kwamba Bwana Yesu na Mungu wana uhusiano wa Baba na Mwana. Ongezea kwa hilo ushuhuda wa Roho Mtakatifu na ushuhuda na uwekeaji mipaka wa mitume, na basi mna hakika kwamba Mungu ni Utatu. Kwa miaka elfu mbili, dunia ya dini imekuwa na hakika kwamba Mungu mmoja wa kweli aliyeziumba mbingu na dunia na vitu vyote ni Utatu, hasa kwa sababu Mungu alipata mwili ili Aifanye kazi ya ukombozi, na pia kwa sababu ya suitafahamu zilizoibuka kutokana na watu kukosa kuuelewa ukweli wa kupata mwili.