XIX. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Ukweli wa ni Kwa Nini Njia ya Kweli Imepitia Usumbufu Tangu Nyakati za Kale
Kwa nini serikali ya Kikomunisti ya China hutesa kwa ukali, kukandamiza na kuchukulia hatua Mwenyezi Mungu na Kanisa la Mwenyezi Mungu?
“Hiki ni kizazi kibaya” (Luka 11:29).
“Ulimwengu mzima uko ndani ya maovu” (1 Yohana 5:19).
“Namna ambavyo umeanguka toka mbinguni, Ewe Luciferi, mwana wa asubuhi! Namna ambavyo umeangushwa chini, wewe uliyedhoofisha mataifa! Kwani umesema moyoni mwako, Nitapaa hadi mbinguni, Nitakiinua kiti changu cha enzi juu ya nyota za Mungu: Pia nitakaa juu ya mlima wa mkusanyiko, kwa pande za kaskazini: Nitapaa juu ya mawingu; Nitakuwa kama Aliye Juu Zaidi” (Isaya 14:12-14).
“Na kulikuwa na vita huko mbinguni: Mikaeli na malaika wake walipigana dhidi ya lile joka; na lile joka likapigana na malaika wake, na wakashindwa; na hapakuwa na mahali pao mbinguni tena. Na hilo joka kubwa likarushwa nje, yule nyoka mzee, anayeitwa Ibilisi, na Shetani, ambaye analaghai dunia nzima: alirushwa nje hadi duniani, nao malaika wake wakarushwa nje pamoja na yeye. ... Na wakati joka liliona kwamba lilirushwa duniani, lilimtesa yule mwanamke ambaye alimzaa mtoto mwanaume” (Ufunuo 12: 7-9, 13).
Maneno Husika ya Mungu:
Huu ndio ukweli: Wakati dunia haikuwepo bado, malaika mkuu ndiye aliyekuwa malaika mkuu zaidi mbinguni. Alikuwa na mamlaka juu ya malaika wote kule mbinguni; haya ndiyo yaliyokuwa mamlaka ambayo Mungu alimpa. Kando na Mungu, yeye ndiye aliyekuwa malaika mkubwa zaidi mbinguni. Wakati Mungu alipouumba binadamu baadaye, malaika mkuu alitekeleza usaliti mkuu zaidi dhidi ya Mungu duniani. Nasema kwamba alimsaliti Mungu kwa sababu alitaka kuwasimamia binadamu na kuzidi mamlaka ya Mungu. Ni malaika mkuu ambaye alimjaribu Hawa hadi akatenda dhambi; alifanya hivyo kwa sababu alipenda kuanzisha ufalme wake duniani na kuwafanya binadamu wamsaliti Mungu na kumtii yeye badala yake. Aliona kwamba kulikuwa na vitu vingi ambavyo vilimtii; malaika walimtii sawa na vile ambavyo watu wa dunia walivyomtii. Ndege na wanyama, miti, misitu, milima, mito na vitu vyote vilivyo duniani vilikuwa chini ya utunzaji wa binadamu—yaani, Adamu na Hawa—huku nao Adamu na Hawa wakimtii. Malaika mkuu hivyo basi alitamani kuzidi mamlaka ya Mungu na kumsaliti Mungu. Baadaye aliwaongoza malaika wengi kumsaliti Mungu, ambao baadaye walikuja kuwa pepo wachafu mbalimbali. Je, maendeleo ya binadamu hadi siku ya leo hayajasababishwa na upotovu wa malaika mkuu? Binadamu wako tu namna walivyo leo kwa sababu malaika mkuu alimsaliti Mungu na kuwapotosha binadamu.
kutoka katika “Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili
Pigano linapiganwa kwa njia hii katika ulimwengu wa roho: Ni tumaini lisilofanikiwa la Shetani kuwapotosha wanadamu kwa kiwango fulani, kuufanya ulimwengu kuwa mbaya na mwovu, na hivyo kumvuta mwanadamu ndani ya matope na kuuharibu mpango wa Mungu.
kutoka katika “Sura ya 5” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati huu wote Shetani amekuwa akimfinyanga mwanadamu, akiwa na matumaini yasiyofaa ya kuwameza binadamu na kisha kusababisha Mungu kuuharibu ulimwengu na kupoteza ushahidi Wake.
kutoka katika “Sura ya 6” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu anafanya kazi, Mungu anamtunza mtu, anamwangalia mtu, na Shetani anafuata hatua Yake yote. Yeyote anayefadhiliwa na Mungu, Shetani pia anatazama, akifuata nyuma. Iwapo Mungu anamtaka mtu huyu, Shetani atafanya kila kitu kwa uwezo wake kumzuia Mungu, akitumia mbinu mbalimbali mbovu kujaribu, kusumbua na kuharibu kazi anayofanya Mungu ili kufikia lengo lake lililofichwa. Lengo lake ni nini? Hataki Mungu awe na mtu yeyote; anataka wale wote ambao Mungu anataka, kuwamiliki, kuwatawala, kuwaelekeza ili wamwabudu, ili watende maovu pamoja naye. Je, hii siyo nia ya husuda ya Shetani? … Shetani yuko vitani na Mungu, akifuata nyuma Yake. Lengo lake ni kubomoa kazi yote ambayo Mungu anataka Kufanya, kuwamiliki na kudhibiti wale wote ambao Mungu anawataka, kuwafisha kabisa wale ambao Mungu anataka. Kama hawajafishwa, basi wanakuja kwa milki ya Shetani kutumiwa naye—hili ndilo lengo lake.
kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee IV” katika Neno Laonekana katika Mwili
Udhihirisho wa joka kuu jekundu ni upinzani Kwangu, ukosefu wa ufahamu na utambuzi wa maana ya maneno Yangu, mateso ya mara kwa mara Kwangu, na kutafuta kutumia njama ili kuzuia usimamizi Wangu. … Joka kuu jekundu Ninayezungumzia si joka kuu jekundu lolote fulani; badala yake ni pepo mbaya anayenipinga Mimi, ambaye kwaye “joka kuu jekundu” ni kisawe.
kutoka katika “Sura ya 96” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Maarifa ya utamaduni wa kale kwa taratibu yamemwondoa mwanadamu kutoka katika uwepo wa Mungu na kumweka mwanadamu kwa mfalme wa mashetani na wana wake. Vitabu Vinne na Maandiko ya Kale ya Kiyunani Matano vimepeleka fikra na mawazo ya mwanadamu katika enzi nyingine ya uasi, na kumfanya mwanadamu kuendelea kuwaabudu wale walioandika Vitabu hivyo na Maandiko ya Kiyunani, wakikuza zaidi mitazamo yao juu ya Mungu. Mfalme wa mashetani bila huruma alimtupa Mungu nje kutoka katika moyo wa mwanadamu bila wao kujua, huku akifurahia kuuchukua moyo wa mwanadamu. Baada ya hapo na kuendelea mwanadamu akawa na roho mbaya na ya uovu akiwa na sura ya mfalme wa mashetani. Chuki juu ya Mungu ilijaza kifua chao na sumu ya mfalme wa mashetani ikasambaa ndani ya mwanadamu hadi alipomalizwa kabisa. Mwanadamu hakuwa na uhuru tena na hakuweza kuvunja vifungo vya mfalme wa mashetani. Kwa hiyo, mwanadamu angeweza kuendelea kukaa pale tu na kufungwa, kujisalimisha kwake na kujitiisha kwake. Amepanda zamani sana mbegu ya kutoamini kuwa kuna Mungu ndani ya moyo mchanga wa mwanadamu, akimfundisha mwanadamu dhana za uongo kama vile, “kujifunza sayansi na teknolojia, kutambua Vipengele Vinne vya Usasa, hakuna Mungu duniani.” Si hivyo tu, ametangaza kwa kurudiarudia, “Hebu tujenge makazi mazuri sana kwa kufanya kazi kwa bidii,” akiwaomba wote kujiandaa toka wakiwa watoto kutumikia nchi yao. Mwanadamu amepelekwa mbele yake bila kujitambua, na bila kusita akajichukulia sifa (akimrejelea Mungu akiwa Ameshikilia binadamu mzima katika mikono Yake). Hajawahi kuhisi aibu au kuwa na hisia yoyote ya aibu. Aidha, bila aibu amewanyakua watu wa Mungu na kuwaweka katika nyumba yake, wakati akirukaruka kama panya mezani na kumfanya mwanadamu amwabudu kama Mungu. Ni ujahili kabisa huu Anaropoka tuhuma hizo za kushtua, “Hakuna Mungu duniani. Upepo upo kwa ajili ya sheria za asili; mvua ni unyevunyevu unaoganda na kudondoka chini kama matone; tetemeko la ardhi ni mtikisiko wa uso wa ardhi kwa sababu ya mabadiliko ya jiolojia; ukame ni kwa sababu ya ukavu hewani kwa mwingiliano wa kinyuklia katika uso wa jua. Haya ni matukio ya asili. Ni sehemu gani ambayo ni tendo la Mungu?” Hata anaropoka[a]kauli kama hizi zisizo na aibu: “Mwanadamu alitokana na sokwe wa zamani, na dunia leo imeendelea kutoka katika jamii ya kale ya takribani miaka bilioni moja iliyopita. Ama nchi inaendelea au inaanguka inaamuliwa na mikono ya watu wake.” Mwanadamu amemning’iniza ukutani miguu juu kichwa chini na kumweka mezani ili kutunzwa vizuri na kuabudiwa. Anapokuwa anapiga kelele kwamba “Hakuna Mungu,” anajichukulia mwenyewe kuwa ni Mungu, na kumsukumia mbali Mungu nje ya mipaka ya dunia bila huruma. Anasimama katika sehemu ya Mungu na kutenda kama mfalme wa mashetani. Ni upuuzi mkubwa kiasi gani! Anamsababisha mtu kuteketezwa na chuki yenye sumu. Inaonekana kwamba Mungu ni adui wake mkubwa na Mungu Hapatani naye kabisa. Anafanya hila zake za kumfukuza Mungu wakati anabakia huru na hajapatikana.[1] Huyo kweli ni mfalme wa mashetani! Tunawezaje kuvumilia uwepo wake? Hatapumzika hadi awe ameisumbua kazi ya Mungu na kuiacha katika matambara na kuwa katika hali ya shaghalabaghala kabisa,[2] kana kwamba anataka kumpinga Mungu hadi mwisho, hadi mmoja kati yao awe ameangamia. Anampinga Mungu kwa makusudi na kusogea karibu zaidi. Sura yake ya kuchukiza imefunuliwa toka zamani na sasa imevilia damu na kugongwagongwa,[3] ipo katika hali mbaya sana, lakini bado hapunguzi hasira zake kwa Mungu, kana kwamba anatamani kummeza Mungu kabisa kwa mara moja ili kutuliza hasira moyoni mwake.
kutoka katika “Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kutoka juu hadi chini na kuanzia mwanzo hadi mwisho, amekuwa akisumbua kazi ya Mungu na kutenda kinyume Chake. Mazungumzo yote ya “urithi wa utamaduni wa kale,” “maarifa ya thamani ya utamaduni wa kale,” “mafundisho ya imani ya Tao na imani ya Confucius,” na “maandiko ya kale ya Confucius na ibada ya kishirikina” vimempeleka mwanadamu kuzimu. Sayansi na teknolojia ya kisasa, vilevile maendeleo ya viwanda, kilimo, na biashara havionekeni popote. Badala yake, anasisitiza ibada za kishirikina zilizoenezwa na “masokwe” wa kale kwa makusudi kabisa kuingilia, kupinga na kuharibu kazi ya Mungu. Sio tu amemtesa mwanadamu hadi leo hii, bali anataka kummaliza[4] mwanadamu kabisa. Mafundisho ya maadili ya kishirikina na kurithisha maarifa ya utamaduni wa kale vimemwambukiza mwanadamu kwa muda mrefu na kumbadilisha mwanadamu kuwa mashetani wakubwa na wadogo. Kuna wachache sana ambao wapo tayari kumpokea Mungu na kukaribisha kwa furaha ujio wa Mungu. Uso wa mwanadamu umejawa na mauaji, na katika sehemu zote, kifo kipo hewani. Wanatafuta kumwondoa Mungu katika nchi hii; wakiwa na visu na mapanga mikononi, wanajipanga katika pambano kumwangamiza Mungu. Sanamu zimetapakaa nchi nzima ya shetani ambapo mwanadamu anafundishwa kuwa hakuna Mungu. Juu ya nchi hii kunatoka harufu mbaya sana ya karatasi linaloungua na ubani, ni harufu nzito sana inayomaliza hewa. Inaonekana kuwa ni harufu ya uchafu unaopeperuka wakati joka anapojisogeza na kujizungusha, na ni harufu ambayo mwanadamu hawezi kuvumilia bali kutapika tu. Licha ya hiyo, kunaweza kusikika pepo waovu wakikariri maandiko. Sauti inaonekana kutoka mbali kuzimu, na mwanadamu hawezi kujizua kusikia baridi ikiteremka chini ya uti wake. Katika nchi hii sanamu zimetapakaa, zikiwa na rangi zote za upinde wa mvua, ambazo zinaibadilisha nchi kuwa ulimwengu unaometameta, na mfalme wa mashetani amekenua, kana kwamba njama zake ovu zimefanikiwa. Wakati huo mwanadamu hana habari naye, wala mwanadamu hajui kwamba shetani amekwishamharibu kwa kiwango ambacho amekuwa hawezi kuhisi na ameshindwa. Anatamani kumfutilia mbali Mungu mara moja, na kumtukana na kumwangamiza, na kujaribu kuchana na kuvuruga kazi Yake. Anawezaje kumruhusu Mungu kuwa wa hadhi sawa? Anawezaje kumvumilia Mungu “akiingilia” kazi miongoni mwa wanadamu? Anawezaje kumruhusu Mungu kufichua uso wake wa chuki? Anawezaje kumruhusu Mungu kuingilia kazi yake? Inawezekanaje Shetani huyu anayevimba kwa ghadhabu, amruhusu Mungu kutawala nguvu yake duniani? Anawezaje kukubali kushindwa kwa urahisi? Sura yake ya chuki imefunuliwa wazi, hivyo mtu anajikuta hajui kama acheke au alie, na ni vigumu sana kuzungumzia hili. Hii si asili yake?
kutoka katika “Kazi na Kuingia (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kwa maelfu ya miaka hii imekuwa ni nchi ya uchafu, ni chafu sana, shida zimejaa, mizimu wanazunguka kila kona, wakihadaa na kudanganya, wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi,[5] wakiwa katili na waovu, wakikandamiza mji huu ulio mahame na kuuacha ukiwa umetapakaa maiti; harufu ya uozo inaijaza nchi na kuenea hewani, na inalindwa isivyo kawaida.[6] Nani awezaye kuuona ulimwengu kupita anga? Ibilisi anaufunga mwili wote wa mwanadamu, anafumba macho yake yote, na kufunga kinywa chake kwa nguvu. Mfalme wa pepo amefanya ghasia kwa maelfu kadhaa ya miaka, hadi leo hii, wakati bado anaangalia kwa karibu mji ulio mahame kana kwamba ulikuwa kasiri la pepo lisilopenyeka; kundi hili la walinzi, wakati uo huo, wakiangalia kwa macho yanayong’aa, wakiogopa sana kwamba Mungu atawakamata bila wao kujua na kuwafutilia wote mbali, Akiwaacha wakiwa hawana sehemu ya amani na furaha. Inawezekanaje watu wa mji wa mahame kama huu wawe wamewahi kumwona Mungu? Je, wamekwishawahi kufurahia uzuri na upendo wa Mungu? Wanathamini vipi masuala ya ulimwengu wa kibinadamu? Ni nani miongoni mwao anayeweza kuelewa matakwa ya kina ya Mungu? Haishangazi, basi, kwamba Mungu mwenye mwili abaki kuendelea kuwa Amefichwa: Katika jamii ya giza kama hii, ambapo pepo hawana huruma na ni katili, inawezekanaje mfalme wa pepo anayeua watu kwa kufumba na kufumbua, avumilie uwepo wa Mungu ambaye ni mwenye upendo, mpole, na mtakatifu? Anawezaje kushangilia na kufurahia ujio wa Mungu? Vikaragosi hawa! Wanalipa upole kwa chuki, wanamtweza Mungu kwa muda mrefu, wanamtukana Mungu, ni washenzi kupita kiasi, hawamjali Mungu hata kidogo, wanapora na kuteka nyara, wamepoteza dhamiri yote, na hawana hata chembe ya wema, na wanawajaribu watu wasiokuwa na hatia kuwa watu wasiokuwa na uwezo wa kuhisi. Wazazi wa kale? Viongozi Wapendwa? Wote wanampinga Mungu! Udukuzi wao umeacha wote walio chini ya mbingu katika hali ya giza na machafuko! Uhuru wa dini? Haki halali na matakwa ya wananchi? Zote hizo ni njama za kufunika dhambi! Nani ambaye ameikumbatia kazi ya Mungu? Nani ametoa maisha yake au kumwaga damu kwa ajili ya kazi ya Mungu? Kwa kizazi baada ya kizazi, kutoka kwa wazazi hadi watoto, mwanadamu aliyepo katika utumwa bila heshima amemfanya Mungu mtumwa—hii inawezaje kukosa kuamsha hasira? … Kwa nini kuweka kikwazo hicho kisichopenyeka katika kazi ya Mungu? Kwa nini utumie hila mbalimbali kuwadanganya watu wa Mungu? Uhuru wa kweli na haki na matakwa halali vipo wapi? Usawa uko wapi? Faraja iko wapi? Wema upo wapi? Kwa nini kutumia mbinu za hila kuwadanganya watu wa Mungu? Kwa nini kutumia nguvu kukandamiza ujio wa Mungu? Kwa nini asimruhusu Mungu kuzunguka katika dunia ambayo Ameiumba? Kwa nini kumbana Mungu hadi Anakosa sehemu ya kupumzisha kichwa Chake? Wema upo wapi miongoni mwa wanadamu? Ukarimu upo wapi miongoni mwa wanadamu? Kwa nini kusababisha matamanio makubwa kiasi hicho kwa Mungu? Kwa nini kumfanya Mungu kuita tena na tena? Kwa nini kumlazimisha Mungu kumhofia Mwana Wake mpendwa? Kwa nini jamii hii ya giza na mbwa wao walinzi wasimruhusu Mungu kuja bila kizuizi na kuzunguka dunia ambayo Aliiumba?
kutoka katika “Kazi na Kuingia (8)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Shetani hupata umaarufu wake kupitia kwa kuudanganya umma. Mara nyingi hujiweka kama kiongozi na kuchukua wajibu wa kielelezo cha haki. Akisingizia kuwa anasalimisha haki, anaishia kumdhuru binadamu, kudanganya nafsi zao, na kutumia mbinu zote ili kuweza kuteka nyara hisia na fikira za binadamu, kumdanganya na kumchochea. Shabaha yake ni kumfanya binadamu kuidhinisha na kuufuata mwenendo wake wa maovu, kumfanya binadamu kujiunga naye katika kupinga mamlaka na ukuu wa Mungu. Hata hivyo, wakati mtu anapokuwa mwerevu na kutambua njama zake, mipango na sifa zake hizo na hataki kuendelea kudhalilishwa na kudanganywa naye hivyo au kuendelea kuwa mtumwa wa Shetani, au kuadhibiwa na kuangamizwa pamoja na Shetani, Shetani naye hubadilisha sifa zake za awali za utakatifu na kuondoa baraka yake bandia ili kufichua uso wake wa kweli wenye maovu, ubaya, sura mbaya na wa kikatili. Shetani hawezi kupenda jambo lolote isipokuwa kumaliza wale wote wanaokataa kumfuata yeye na wale wanaopinga nguvu zake za giza. Wakati huu Shetani hawezi tena kuvaa sura ya uaminifu, na utulivu; badala yake, sifa zake za kweli za sura mbaya na za kishetani zilizokuwa zimefichwa kwenye mavazi ya kondoo zinafichuliwa. Mara tu njama za Shetani zinapomulikwa, na sifa zake za kweli kufichuliwa, yeye huingia kwenye hisia za hasira kali na kuonyesha ushenzi wake; tamanio lake la kudhuru na kudanganya watu ndipo litazidi zaidi. Hii ni kwa sababu anapandwa na hasira kali kwa kuzindukana kwa binadamu; anataka kuwa na kisasi kingi dhidi ya binadamu kwa maazimio yake ya kutamani kuwa na uhuru na nuru na kutokuwa mateka wa jela yake. Hasira yake kali inanuiwa kutetea maovu yake, na pia ni ufunuo wa kweli wa asili yake ya kishenzi.
… Sababu inayomfanya Shetani kukereka na kuwa mkali ni: Kwa sababu njama zake zisizotamkika zimefichuliwa; mipango yake haikwepeki kwa urahisi; malengo yake yasiyo na mipaka na tamanio la kubadilisha Mungu na kujifanya kuwa Mungu, vyote vimekwama na kuzuiliwa; shabaha yake ya kudhibiti binadamu wote imeishia patupu na haiwezi tena kutimizwa.
kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee II” katika Neno Laonekana katika Mwili
Tanbihi:
1. “Huru na hajapatikana” inaonyesha kwamba shetani anapagawa na kucharuka.
2. “Hali ya shaghalabaghala kabisa” inahusu jinsi tabia ya shetani ya ukatili haivumiliki kuona.
3. “Imevilia damu na kugongwagongwa” inahusu sura mbaya ya kutisha ya mfalme wa pepo.
4. “Kummaliza” inahusu tabia ya kidhalimu ya mfalme wa pepo, ambaye huwaangamiza watu wote.
5. “Wakitoa tuhuma zisizokuwa na msingi” inahusu mbinu ambazo ibilisi hutumia huwadhuru watu.
6. “Inalindwa isivyo kawaida” inaonyesha kuwa mbinu ambazo ibilisi hutumia huwatesa watu ni mbovu hasa, na kuwadhibiti watu sana kiasi kwamba hawana nafasi ya kusogea.
a. Maandishi ya asili yanasoma “Baadhi hata hupiga kelele.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni