8.16.2019

Ni nini hasa mtu anayefuata mapenzi ya Mungu? Na ushahidi wa kweli wa imani katika Mungu ni nini?

XVIII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kilicho Kufuata Mapenzi ya Mungu na Kilicho Ushahidi wa Kweli wa Imani katika Mungu

Ni nini hasa mtu anayefuata mapenzi ya Mungu? Na ushahidi wa kweli wa imani katika Mungu ni nini?


Aya za Biblia za Kurejelea:
“Kutoka hapo Ayubu akainuka, na akalipasua joho lake, na akanyoa kichwa chake, na akaanguka chini, na kuabudu, Naye akasema, Nilitoka kwa tumbo la mama yangu nikiwa uchi, na mimi nitarudi huko nikiwa uchi; Yehova alinipa, na Yehova amechukua; jina la Yehova libarikiwe” (Ayubu 1:20-21).
“Naye akasema, Umchukue mwana wako sasa, mwana wako wa pekee Isaka, unayempenda, na uende hadi nchi ya Moria; na huko umtoe kwa sadaka ya kuteketezwa juu ya mojawapo ya milima ambayo nitakuambia.… Na Ibrahimu akanyosha mbele mkono wake, na kukichukua kisu ili amchinje mwana wake” (Mwanzo 22:2, 10).
Hao ndio wale hawakunajisiwa na wanawake; kwani wao ni bikira. Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo. Na vinywani mwao hakukuwa na hila: kwani hawana hatia mbele ya Kiti cha Mungu cha enzi” (Ufunuo 14:4-5).
Maneno Husika ya Mungu:
Yesu aliweza kukamilisha agizo la Mungu—kazi ya ukombozi wa wanadamu wote—kwa sababu alikabidhi kila tatizo kwa mapenzi ya Mungu, bila kufuata mipango na fikira Zake binafsi. Basi pia, Yeye Alikuwa rafiki mwema wa Mungu—Mungu Mwenyewe, jambo ambalo nyote mnalielewa vizuri sana. (Kwa kweli, alikuwa Mungu Mwenyewe aliyetolewa ushahidi na Mungu; Ninataja jambo hili hapa kwa kuutumia ukweli wa Yesu ili kuonyesha mfano wa suala hili.) Aliweza kuuweka mpango wa usimamizi wa Mungu katika kiini cha mambo yote, na kila mara alimwomba Baba wa mbinguni na kuyatafuta mapenzi ya Baba wa mbinguni. Aliomba, na kusema: “Mungu Baba! Timiza kile ambacho ni mapenzi Yako, na usitende kulingana na nia Zangu; ingekuwa heri ukitenda kulingana na mpango Wako. Mwanadamu anaweza kuwa dhaifu, lakini kwa nini unapaswa kumshughulikia? Ni vipi ambavyo mwanadamu aliweza kuwa mhusika wa shughuli Zako, mwanadamu ambaye ni kama chungu mkononi Mwako? Ndani ya moyo Wangu, Ninatamani tu kutimiza mapenzi Yako, na Ninatamani Utende Unachotaka kutenda ndani Yangu kulingana na makusudio Yako mwenyewe.” Alipokuwa njiani kuelekea Yerusalemu, Yesu alihisi maumivu makali, kama kwamba kisu kilikuwa kimedungwa ndani ya moyo Wake, ilhali hakuwa na nia yoyote ya kwenda kinyume cha Neno lake; kila mara kulikuwa na nguvu zenye uwezo mkuu zilizomvutia Yeye kuelekea mahali ambapo Angesulubiwa. Mwishowe, alipigiliwa misumari juu ya msalaba na akawa mfano wa mwili wenye dhambi, akiikamilisha kazi hiyo ya ukombozi wa wanadamu, na kufufuka kutoka kwa pingu za kifo na Kuzimu. Mbele Yake, kifo, jehanamu, na Kuzimu vilipoteza nguvu zao, na vilishindwa Naye. Aliishi miaka thelathini na tatu, na katika miaka hiyo yote daima Alifanya kila Alichoweza kutimiza mapenzi ya Mungu kulingana na kazi ya Mungu wakati huo, bila kuzingatia atakachofaidi au kupoteza Yeye binafsi, na kila mara akiwaza kuhusu mapenzi ya Mungu Baba. Hivyo, baada ya Yeye kubatizwa, Mungu alisema: “Huyu ni Mwana wangu Mpendwa, ambaye Ninapendezwa naye.” Kwa sababu ya huduma Yake mbele ya Mungu, iliyokuwa na upatanifu na mapenzi ya Mungu, Mungu aliuweka mzigo mzito wa kuwakomboa wanadamu wote juu ya mabega yake na akamfanya ajitolee kuutimiza, na Alikuwa na ujuzi na ustahiki wa kuikamilisha kazi hii muhimu.
kutoka katika “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wanaomhudumia Mungu wanapaswa kuwa marafiki wema wa Mungu, wanapaswa kumfurahisha Mungu, na kuwa na uaminifu wa hali ya juu kwa Mungu. Bila kujali iwapo unatenda bila kuonekana na watu, au mbele ya watu, unaweza kupata furaha ya Mungu mbele za Mungu, unaweza kusimama imara mbele za Mungu, na bila kujali jinsi watu wengine wanavyokutendea, wewe huifuata njia yako mwenyewe kila mara, na kuushughulikia kwa makini mzigo wa Mungu. Mtu wa aina hii pekee ndiye rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu wanaweza kumhudumia Yeye moja kwa moja kwa sababu wamepewa agizo kuu la Mungu, na mzigo wa Mungu, wao wanaweza kuuchukulia moyo wa Mungu kama moyo wao wenyewe, na mzigo wa Mungu kama mzigo wao wenyewe, na hawazingatii iwapo watafaidi au watapoteza matarajio: Hata wasipokuwa na matarajio, na hawatafaidi chochote, watamwamini Mungu daima kwa moyo wa upendo. Kwa hivyo, mtu wa aina hii ni rafiki mwema wa Mungu. Marafiki wema wa Mungu ni wasiri Wake pia; ni wasiri wa Mungu pekee ndio wanaoweza kushiriki katika kutotulia Kwake, matamanio Yake, na ingawa mwili wao una uchungu na ni mdhaifu, wanaweza kuvumilia uchungu na kuacha kile wanachokipenda ili kumridhisha Mungu. Mungu huwapa watu wa aina hii mizigo mingi, na kile ambacho Mungu atafanya hudhihirishwa kupitia kwa watu hawa. Yaani, watu hawa wanapendwa na Mungu, wao ni watumishi wa Mungu wanaoupendeza moyo Wake, na ni watu wa aina hii pekee ndio wanaoweza kutawala pamoja na Mungu.
kutoka katika “Jinsi ya Kuhudumu kwa Upatanifu na Mapenzi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mtu ambaye kweli anafanya mapenzi ya Mungu anaweza kutoa sifa kutoka ndani ya kina cha moyo wake katikati ya hukumu ya Mungu, kuadibu, na majaribio, na anaweza kutii Mungu kwa ukamilifu na kujitelekeza mwenyewe, hivyo kumpenda Mungu kwa moyo wa uaminifu, nia moja, na utakatifu; huyo ndiye mtu kamili, na pia ni kazi ambayo Mungu anataka kufanya, na kile ambacho Mungu anataka kutimiza.
kutoka katika “Juu ya Hatua za Kazi ya Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika imani yake kwa Mungu, Petro alitafuta kumridhisha Mungu katika kila kitu, na alitafuta kutii yote yaliyotoka kwa Mungu. Bila malalamiko hata kidogo, aliweza kukubali kuadibu na hukumu, na vile vile usafishaji, dhiki na ukosefu maishani, yote ambayo hayangeweza kubadilisha upendo wake wa Mungu. Je, huu si upendo mkamilifu wa Mungu? Je, hii si ni kutimiza wajibu wa kiumbe wa Mungu? kuadibu, hukumu, dhiki—una uwezo wa kufikia utii hadi kifo, na hili ndilo linafaa kutimizwa na kiumbe wa Mungu, huu ni usafi wa upendo wa Mungu. Kama mwanadamu anaweza kutimiza kiasi hiki, basi yeye ni kiumbe wa Mungu mwenye sifa inayostahili, na hakuna kitu kinachokidhi mapenzi ya Muumba bora zaidi ya hiki.
kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili
Punde tu anapotajwa Petro, kila mtu anajawa na sifa, … Alikuwa makini sana sio tu kula na kunywa maneno Yangu, lakini hata zaidi kufahamu nia Zangu, na daima alikuwa na busara na tahadhari katika mawazo yake, kwa hivyo daima alikuwa mwerevu kwa makini ndani ya roho yake, na hivyo aliweza kuniridhisha kwa vyote alivyofanya. Kwa maisha ya kawaida, alikuwa makini kuunganisha katika maisha[a]masomo ya wale walioshindwa katika siku za nyuma ili kujichochea mwenyewe kufanya juhudi kubwa zaidi, akihofia sana kwamba anaweza kuanguka ndani ya nyavu za ushinde. Alikuwa pia makini kupata imani na upendo wa wote ambao kupitia enzi nyingi walikuwa wamempenda Mungu. Kwa njia hii, aliharakisha maendeleo ya ukuaji wake sio tu kwa masuala hasi, lakini hasa kwa masuala chanya, hadi akawa katika uwepo Wangu mwanadamu pekee aliyenijua bora kabisa. Kwa sababu hii, si vigumu kuwazia jinsi alivyoweza kuweka yote aliyokuwa nayo mikononi Mwangu, kukosa kuwa tena bwana wake mwenyewe hata kwa kula, kuvaa, ama mahali aliishi, lakini alifanya kuniridhisha kwa mambo yote msingi ambao alifurahia fadhila Yangu. Mara nyingi Nilimweka chini ya jaribio, ambalo hakika lilimwacha nusu mfu, lakini hata katikati ya haya mamia ya majaribio, hakupoteza imani Kwangu hata mara moja ama kusikitishwa nami. Hata Niliposema nimemtupa kando, hakufa moyo wala kukata tamaa, lakini aliendelea kama mbeleni akitekeleza kanuni zake ili kunipenda kwa njia ya vitendo. Nilipomwambia kwamba, ingawa alinipenda, Sikumsifu ila Ningemtupa katika mikono ya Shetani mwishowe. Katikati ya majaribio haya, ambayo hayakufikia mwili wake lakini yalikuwa majaribio ya njia ya maneno, bado alisali Kwangu: “Ee, Mungu! Miongoni mwa mbingu na dunia na mambo lukuki, kuna mwanadamu yeyote, kiumbe chochote, ama kitu chochote kisicho mikononi Mwako, Mwenyezi? Unapotaka kunionyesha huruma, moyo wangu unafurahishwa sana na huruma Yako; unapotaka kunihukumu, ingawa sifai, nahisi hata zaidi siri ya kushangaza ya matendo Yako, kwa sababu Umejawa na mamlaka na hekima. Ingawa mwili wangu unaweza kuteseka, natulizwa ndani ya roho yangu. Ningewezaje kutosifu hekima Yako na matendo Yako? Hata kama nitafa baada ya kuja kukujua, kamwe nitakuwa tayari. Ee, Mwenyezi! Hakika si kwamba Wewe kweli hutaki kuniruhusu nikuone? Hakika si kwamba sistahili kweli kupokea hukumu Yako? Inaweza labda kuwa kwamba kuna kitu ndani yangu usichotaka kuona?” Katikati ya majaribu ya aina hizi, hata kama Petro hakuweza kufahamu nia Zangu kwa usahihi, ni wazi kwamba aliliona kuwa suala la fahari na utukufu binafsi kutumiwa na Mimi (iwe tu kupokea hukumu Yangu ili binadamu waweze kuuona ukuu na ghadhabu Yangu), na hakuwa mwenye huzuni kwa ajili ya kuwekwa chini ya jaribio. Kwa sababu ya uaminifu wake mbele Yangu, na kwa sababu ya baraka Zangu juu yake, amekuwa mfano mwema na mfano wa kuigwa kwa mwanadamu kwa maelfu ya miaka.
kutoka katika “Sura ya 6” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati Ayubu alipopitia majaribio yake kwa mara ya kwanza, alinyang’anywa mali yake yote na watoto wake wote, lakini hakujisujudia na kusema chochote ambacho kilikuwa dhambi dhidi ya Mungu kutokana na hayo. Alikuwa ameshinda majaribio ya Shetani, na alikuwa ameshinda rasilimali zake zote za dunia na watoto wake, na majaribio ya kupoteza mali yake ya dunia, hivi ni kusema kwamba aliweza kutii Mungu kuchukua na kutwaa kutoka kwake na akatoa shukrani na sifa kwa Mungu kwa sababu ya hayo. Hivyo ndivyo ulivyokuwa mwenendo wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Shetani, na huo ndio uliokuwa ushuhuda wa Ayubu wakati wa jaribio la kwanza la Mungu. Kwenye jaribio la pili, Shetani aliunyosha mbele mkono wake ili kumdhuru Ayubu, na ingawaje Ayubu alipitia maumivu yaliyokuwa makubwa zaidi kuliko yale aliyokuwa amepitia awali, bado ushuhuda wake ulikuwa wa kutosha wa kuacha watu wakiwa wameshangazwa. Alitumia ujasiri wake, imani yake, na utiifu kwa Mungu, pamoja na kumcha Mungu kwake, kwa mara nyingine tena kumshinda Shetani, na mwenendo wake na ushuhuda wake viliweza kwa mara nyingine tena kuidhinishwa na kupata kibali cha Mungu. Wakati wa majaribio haya, Ayubu alitumia mwenendo wake halisi kumtangazia Shetani kwamba maumivu ya mwili wake yasingebadilisha imani yake na utiifu wake kwa Mungu au kuchukua ule upendo wake kwa Mungu na kumcha Mungu; asingemuacha Mungu au kutupilia mbali utimilifu wake binafsi na unyofu kwa sababu alikuwa amekabiliwa na kifo. Bidii ya Ayubu ilimfanya Shetani mwoga, imani yake ilimuacha Shetani akiwa na dukuduku na kutetemeka, nguvu za vita vya maisha yake na kifo chake na Shetani viliweza kuzua chuki na dharau nyingi kwa Shetani, utimilifu na unyofu wake ulimuacha Shetani akiwa hana chochote zaidi cha kumfanya kiasi cha kwamba Shetani aliyaacha mashambulizi yake kwake na kukata tamaa na mashtaka yake dhidi ya Ayubu mbele ya Yehova Mungu. Hii ilimaanisha kwamba Ayubu alikuwa ameushinda ulimwengu, alikuwa ameushinda mwili wake, alikuwa amemshinda Shetani, na alikuwa ameshinda kifo; alikuwa kwa kweli na hakika binadamu aliyemilikiwa na Mungu. Wakati wa majaribio haya mawili, Ayubu alisimama imara katika ushuhuda wake, na kwa hakika aliishi kwa kudhihirisha utimilifu wake na unyofu, na akapanua upana wa kanuni zake za kuishi za kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Baada ya kupitia majaribio haya mawili, ndani ya Ayubu kulizaliwa uzoefu mwingi, na uzoefu huu ulimfanya yeye kuwa mwenye kimo na uzoefu zaidi, ilimfanya kuwa mwenye nguvu zaidi, na imani kubwa zaidi, na ilimfanya yeye kuwa na ujasiri zaidi kuhusu haki na ustahili wa uadilifu ambao yeye alishikilia kwa dhati. Majaribio ya Yehova Mungu kwa Ayubu yalimpa uelewa wa kina na hisia za wasiwasi wa Mungu kwa binadamu, na kumruhusu yeye kuhisi thamani ya upendo wa Mungu, ambapo vyote vinaelekezwa katika utiliaji maanani kwa na kuhusu upendo wa Mungu na vyote viliweza kuongezwa katika kumcha Mungu. Majaribio ya Yehova Mungu kumwondoa tu Ayubu kutoka Kwake, lakini pia yaliuleta moyo wake karibu na Mungu. Wakati maumivu yale ya mwili yaliyovumiliwa na Ayubu yalifikia kilele, wasiwasi aliouhisi kutoka kwa Yehova Mungu haukumpa chaguo lolote ila kuilaani siku yake ya kuzaliwa. Mwenendo kama huo haukuwa umepangiliwa mapema lakini ulikuwa ni ufunuo wa kiasili wa kutilia maanani na kumpenda Mungu kutoka ndani ya moyo wake, ulikuwa ni ufunuo wa kiasili uliotoka kwenye kutilia maanani na kumpenda Mungu kwake. Hivi ni kusema, kwa sababu alijichukia, na hakuwa na radhi na hakuweza kuvumilia kuona Mungu Akiteswa, hivyo kutilia maanani na upendo wake vilifika hali ya kutojijali. Wakati huu, Ayubu aliimarisha kuabudu kwake kwa muda mrefu na kutamani kwake kwa Mungu na upendo kwa Mungu hadi katika kiwango cha utiliaji maanani na upendo. Wakati huohuo, aliweza kupandisha imani na utiifu wake kwa Mungu na kumcha Mungu kwake hadi katika kiwango cha kutilia maanani na upendo. Hakujiruhusu kufanya chochote ambacho kingesababisha madhara kwa Mungu, hakujiruhusu mwenendo ambao ungemuumiza Mungu, na hakujiruhusu kuleta masikitiko, huzuni au hata kutokuwa na furaha kokote kwake Mungu kwa sababu zake mwenyewe. Katika Macho ya Mungu, ingawaje Ayubu alikuwa bado Ayubu wa hapo awali, imani, utiifu na kumcha Mungu kwake kulikuwa kumemletea Mungu utoshelezi kamilifu. Wakati huu, Mungu alitarajia Ayubu kuweza kutimiza, alikuwa amegeuka kuwa mtu aliyestahili kuitwa “mtimilifu na mnyofu” mbele ya macho ya Mungu. Vitendo vyake vya haki vilimruhusu yeye kumshinda Shetani na kuwa makini katika ushuhuda wake kwa Mungu. Hivyo, pia, matendo yake ya haki yalimfanya kuwa mtimilifu, na kuruhusu thamani ya maisha yake kuimarishwa, kuzidishwa zaidi kuliko awali, na kumfanya yeye kuwa mtu wa kwanza kutoweza kushambuliwa au kujaribiwa zaidi na Shetani. Kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishtakiwa na kujaribiwa na Shetani; kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alikabidhiwa Shetani; na kwa sababu Ayubu alikuwa mwenye haki, alishinda na kumlemea Shetani, na kuweza kusimama imara katika ushuhuda wake. Kuendelea mbele, Ayubu akawa binadamu wa kwanza ambaye hangewahi tena kukabidhiwa Shetani, kwa kweli alikuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na akaishi kwenye nuru, katika baraka za Mungu bila ya kupelelezwa au kuangamizwa na Shetani.… Alikuwa amekuwa binadamu wa kweli katika macho ya Mungu, alikuwa ameachiliwa huru. …
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unaweza kusema umeshashindwa, lakini unaweza kutii hata kufa? Unapaswa uwe na uwezo wa kufuata hadi mwisho kabisa bila kujali kama kuna matumaini yoyote, na hupaswi kupoteza imani kwa Mungu bila kujali mazingira. Mwishowe, unapaswa kutimiza hali mbili za ushuhuda: ushuhuda wa Ayubu—utii hata kifo—na ushuhuda wa Petro—upendo mkuu wa Mungu. Kwa upande mmoja, unapaswa kuwa kama Ayubu: Hakuwa na mali hata kidogo, na alisumbuliwa na maumivu ya mwili, lakini hakulikana jina la Yehova. Huu ulikuwa ushuhuda wa Ayubu. Petro aliweza kumpenda Mungu hadi kifo. Alipokufa—alipoangikwa msalabani—bado alimpenda Mungu; hakufikiria juu ya matarajio yake mwenyewe au kufuatilia mambo yaliyo makuu au fikra za anasa, na alitafuta tu kumpenda Mungu, na kutii mipango yote ya Mungu. Hicho ndicho kiwango unachopaswa kutimiza kabla hujahesabiwa kuwa na ushuhuda, kabla hujawa mtu ambaye amefanywa mkamilifu baada ya kushindwa.
kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushuhuda wa kweli ni nini hasa? Ushuhuda uliozungumziwa hapa una sehemu mbili: Moja ni ushuhuda kwa kuweza kushindwa, na ya pili ni ushuhuda kwa kuweza kufanywa mkamilifu (ambako, kwa kawaida, ni ushuhuda unaofuata majaribio makuu zaidi na majonzi ya siku za usoni). Kwa maneno mengine, ikiwa unaweza kusimama imara wakati wa majonzi na majaribio, basi umekuwa na hatua ya pili ya ushuhuda. Kilicho cha maana sana leo ni hatua ya kwanza ya ushuhuda: kuweza kusimama imara wakati wa kila namna ya majaribio ya kuadibu na hukumu. Huu ni ushuhuda kwa kushindwa. Hilo ni kwa sababu leo ni wakati wa ushindi. (Unapaswa kujua kwamba leo ni wakati wa kazi ya Mungu duniani; kazi kuu duniani ya Mungu aliyepata mwili ni matumizi ya hukumu na kuadibu kushinda hili kundi la watu duniani wanaomfuata Yeye.) Kama una uwezo wa kushuhudia kwa kushindwa au la hakutegemei tu kama unaweza kufuata hadi mwisho, lakini, la muhimu zaidi, kama, unapopitia kila hatua ya kazi ya Mungu, una uwezo wa ufahamu wa kweli wa kuadibu na hukumu katika kazi hii, na kama wewe kweli unaiona kazi hii yote. Si jambo ambalo utaweza kulimaliza kwa kubahatisha ikiwa utafuata hadi mwisho kabisa. Lazima uweze kuwa radhi kusalimu amri wakati wa kila namna ya kuadibu na hukumu, lazima uwe na uwezo wa ufahamu wa kweli wa kila hatua ya kazi upitiayo, na lazima uweze kupata ufahamu wa, na utiifu kwa tabia ya Mungu. Huu ni ushuhuda wa msingi wa kushindwa unaotakiwa kwako. Ushuhuda wa kushindwa kimsingi unahusu ufahamu wako wa kupata mwili kwa Mungu. Lenye maana sana, hatua hii ya ushuhuda ni kwa kupata mwili kwa Mungu. Haijalishi kile ambacho unafanya au kusema mbele ya watu wa ulimwengu au wale wanaotawala; kilicho na maana kuliko vyote ni kama unaweza kuyatii maneno yote kutoka kinywani mwa Mungu na kazi Yake yote. Kwa hivyo, hatua hii ya ushuhuda inaelekezwa kwa Shetani na maadui wote wa Mungu—pepo na wenye uadui ambao hawaamini kwamba Mungu atakuwa mwili mara ya pili na kuja kufanya hata kazi kubwa zaidi, na zaidi ya hayo, hawaamini katika ukweli wa kurudi kwa Mungu kwa mwili. Kwa maneno mengine, inaelekezwa kwa wapinga Kristo wote—maadui wote wasioamini katika kupata mwili kwa Mungu.
…………
Ushuhuda wa siku za mwisho ni ushuhuda kwa kama unaweza kufanywa mkamilifu au la—ambako ni kusema, ushuhuda wa mwisho ni kwamba, kwa kuwa umekubali maneno yote yatokayo kinywani mwa Mungu mwenye mwili, na kwa kuwa umekuja kupata ufahamu wa Mungu na kuwa na hakika kumhusu Yeye, unaishi kwa kudhihirisha maneno yote kutoka kinywani mwa Mungu, na kutimiza masharti ambayo Mungu anakwambia—mtindo wa Petro na imani ya Ayubu, kiasi kwamba unaweza kutii hadi kufa, kujitoa mwenyewe kabisa Kwake, na hatimaye kutimiza mfano wa mwanadamu ambao ni wa juu ya kiwango kilichowekwa—kinachomaanisha mfano wa mtu ambaye ameshindwa, ameadibiwa, amehukumiwa, na kufanywa mkamilifu. Huu ni ushuhuda unaopaswa kuwa na mtu ambaye hatimaye amefanywa mkamilifu.
kutoka katika “Utendaji (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuwa na ushahidi mkuu kwa Mungu hasa kunahusiana na ikiwa una ufahamu wa Mungu wa vitendo au la, na ikiwa unaweza au huwezi kutii mbele ya mtu huyu ambaye ni wa kawaida na kutii mpaka hata kifo. Ikiwa unamshuhudia Mungu kwa kweli kupitia utii huu, hiyo inamaanisha kuwa umepatwa na Mungu. Kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo, na kuwa bila malalamiko mbele Yake, kutohukumu, kutokashifu, kutokuwa na mawazo, na kutokuwa na makusudi mengine—kwa njia hii Mungu atapata utukufu. Utiifu mbele ya mtu wa kawaida ambaye anadharauliwa na mwanadamu na kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo bila mawazo yoyote—huu ni ushuhuda wa kweli. Uhakika ambao Mungu anataka watu waingie ndani ni kwamba unaweza kutii maneno Yake, unaweza kuweka maneno Yake katika matendo, kuweza kuinama mbele ya Mungu wa vitendo na kujua upotovu wako mwenyewe, kuweza kufungua moyo wako mbele Yake, na mwishowe kupatwa na Yeye kupitia maneno haya Yake. Mungu hupata utukufu wakati maneno haya yanakushinda na kukufanya uwe mtiifu kikamilifu Kwake; kwa njia hii Anamwaibisha Shetani na kukamilisha kazi Yake.
kutoka katika “Watu Wanaoweza Kuwa Watiifu Kabisa Kwa Utendaji wa Mungu Ndio Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu Atakapokuja, watu watafurahia enzi Yake na hasira Yake, lakini haijalishi maneno Yake yalivyo makali, Anakuja kuokoa na kukamilisha binadamu. Kama viumbe, watu wanapaswa watekeleze wajibu ambao wanafaa kufanya, na kusimama shahidi kwa Mungu katikati ya usafishaji. Katika kila jaribio wanapaswa washikilie ushahidi ambao wanapaswa washuhudie, na kushuhudia ushuhuda mkubwa kwa Mungu. Huyu ni mshindi. Haijalishi Mungu Anavyokuboresha, unabaki kuwa na imani kubwa na kutopoteza imani katika Mungu. Ufanye kile mwanadamu anafaa kufanya. Hiki ndicho Mungu Anahitaji kwa mwanadamu, na moyo wako unapaswa kuweza kurudi Kwake kikamilifu na kumwelekea katika kila wakati. Huyu ni mshindi. Wale wanaoitwa washindi na Mungu ni wale ambao bado wanaweza kusimama kama mashahidi, wakidumisha imani yao, na ibada yao kwa Mungu wanapokuwa chini ya ushawishi wa Shetani na kuzingirwa na Shetani, hiyo ni, wanapokuwa katika nguvu za giza. Kama bado unaweza kudumisha moyo wa utakaso na upendo wako wa kweli kwa Mungu kwa vyovyote vile, unasimama shahidi mbele ya Mungu, na hii ndio Mungu Anaita kuwa mshindi.
kutoka katika “Unapaswa Kudumisha Ibada Yako kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kila hatua ya kazi anayoifanya Mungu ndani ya watu, kwa nje inaonekana kama maingiliano kati ya watu, kana kwamba yalizaliwa kwa mipango ya wanadamu au kutokana na kuingilia kwa wanadamu. Ila kisirisiri, hatua ya kazi, na kila kitu kinachotendeka, ni pingamizi la Shetani kwa Mungu, na huhitaji watu kuwa imara katika ushuhuda wao kwa Mungu. Kwa mfano, tazama wakati Ayubu alijaribiwa: kisirisiri, Shetani alikuwa akiwekeana dau na Mungu, na kilichomtokea Ayubu kilikuwa ni matendo ya wanadamu, na kuingilia kwa wanadamu. Kuna pingamizi la Shetani kwa Mungu katika kila hatua ambayo Mungu anatenda ndani yenu—katika kila kitu kuna vita. Kwa mfano, ikiwa unawabagua ndugu na dada zako, utakuwa na maneno ambayo unataka kusema—maneno unayohisi huenda yasimpendeze Mungu—lakini usipoyasema, utahisi kutoridhika ndani, na kwa wakati huu vita vitazuka ndani yako: “Niseme au nisiseme?” Hivi ndivyo vita. Kwa hivyo, katika kila jambo unalopitia kuna vita, na wakati kuna vita ndani yako, kutokana na ushirikiano wako na kuteseka kwako, Mungu anafanya kazi ndani yako. Hatimaye unaweza kuliweka kando jambo lenyewe na ghadhabu yako inazimika. Hiyo ndiyo athari ya ushirika wako na Mungu. Kila kitu wafanyacho watu kinawahitaji kulipa gharama fulani katika juhudi zao. Bila taabu ya kweli, hawawezi kumridhisha Mungu, hata hawakaribii kumridhisha Mungu, na wanarusha tu maneno matupu! Je, haya maneno matupu yaweza kumridhisha Mungu? Wakati Mungu na Shetani wanapigana katika milki ya kiroho, utamridhishaje Mungu, na utasimamaje imara katika ushuhuda wako Kwake? Unapaswa kujua kuwa kila kitu unachokipitia ni majaribu makubwa na ndipo Mungu hukuhitaji kuwa na ushuhuda. Kwa nje yataonekana kama mambo madogo; lakini haya mambo yakitendeka huonyesha kama unampenda Mungu au la. Ikiwa unampenda, utaweza kusimama imara katika ushuhuda wako Kwake, na ikiwa hujaweka upendo Wake katika vitendo, hili linaonyesha kuwa wewe si Mtu ambaye anapenda kuuweka ukweli katika vitendo, kwamba huna ukweli, huna uzima, kuwa wewe ni makapi! Mambo huwatokea watu wakati Mungu anawataka wasimame imara katika ushuhuda wao Kwake. Hakuna kubwa lililokutendekea kwa sasa, na huna ushuhuda mkubwa, lakini kila chembe ya maisha yako ya kila siku inahusiana na ushuhuda kwa Mungu. Ikiwa utawavutia ndugu na dada zako, wanafamilia, na kila aliye karibu nawe; ikiwa siku moja wasioamini watakuja na wavutiwe na yote unenayo na utendayo, na kuona kuwa yote afanyayo Mungu ni ya ajabu, basi utakuwa umekuwa na ushuhuda. Ijapokuwa huna ufahamu na wewe si mwerevu sasa, kupitia kwa kufanywa mkamilifu na Mungu, unaweza kumridhisha na kuzingatia mapenzi Yake. Wengine wataona kazi Yake kubwa miongoni mwa wasio werevu. Watu huja kumjua Mungu na huwa washindi mbele ya Shetani na waaminifu kwa Mungu kwa kiwango fulani. Hakuna atakayekuwa na uthabiti kuliko hili kundi la watu. Huu utakuwa ushuhuda mkubwa zaidi.
kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili
Leo, unaweza kutafuta kufanywa kuwa mkamilifu au kutafuta mabadiliko katika ubinadamu wako wa nje na maendeleo katika ubora wa tabia yako, lakini muhimu kabisa ni kwamba unaweza kuelewa kwamba kila kitu ambacho Mungu anafanya leo kina maana na ni cha manufaa: Kinakuwezesha wewe ambaye unaishi katika nchi ya uchafu kuepuka uchafu na kuuondoa wote, kinakuwezesha kushinda ushawishi wa Shetani na kuacha nyuma ushawishi wa giza wa Shetani—na kwa kulenga vitu hivi, unakuwa umelindwa katika nchi hii ya uchafu. Mwishowe, utaambiwa utoe ushuhuda gani? Unaishi katika nchi ya uchafu lakini unaweza kuwa mtakatifu, na hutakuwa tena mchafu na mwenye najisi, unamilikiwa na Shetani, lakini unaachana na ushawishi wa Shetani, na humilikiwi au kunyanyaswa na Shetani, na unaishi mikononi mwa Mwenyezi. Huu ndio ushuhuda, na thibitisho la ushindi katika vita na Shetani. Unaweza kumwacha Shetani, unachoishi kwa kudhihirisha hakifichui Shetani, lakini ni kile ambacho Mungu alitaka mwanadamu afikie Alipomuumba mwanadamu: ubinadamu wa kawaida, urazini wa kawaida, umaizi wa kawaida, azimio la kawaida la kumpenda Mungu, na utii kwa Mungu. Huo ndio ushuhuda ambao kiumbe wa Mungu huwa nao. Unasema, “Tunaishi katika nchi ya uchafu, lakini kwa sababu ya ulinzi wa Mungu, kwa sababu ya uongozi Wake, na kwa sababu Ametushinda, tumejiondoa katika ushawishi wa Shetani. Kwamba tunaweza kutii leo pia ni matokeo ya kushindwa na Mungu, na sio kwa sababu sisi ni wema, au kwa sababu tunampenda Mungu kwa asili. Ni kwa sababu Mungu alituchagua, na kutujaalia, ndio tumeshindwa leo, tunaweza kuwa na ushuhuda Kwake, na tunaweza kumhudumia, kwa hiyo, pia, ni kwa sababu Alituchagua, na kutulinda, ndio tumechaguliwa na kutolewa katika miliki ya Shetani, na tunaweza kuachana na uchafu na kutakaswa katika nchi ya joka kuu jekundu.” Aidha, kile unachoishi kwa kudhihirisha nje kitaonyesha kwamba una ubinadamu wa kawaida, kuna urazini katika kile unachosema, na unaishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu wa kawaida. Watu wengine wanapowaona wasiweze kusema, “Je, hii siyo sura ya joka kuu jekundu? Matendo ya dada hayaonekani kuwa ni ya dada, matendo ya kaka hayaonekani kuwa ni ya kaka, na hawana staha yoyote ya watakatifu.” Hawapaswi kusema, “si ajabu Mungu alisema ni uzao wa Moabu, Alikuwa sahihi kabisa!” Ikiwa watu wanawatazama na kusema, “Ingawa Mungu alisema wewe ni uzao wa Moabu, kile unachokiishi kwa kudhihirisha kimethibitisha kwamba umeachana na ushawishi wa Shetani; ingawa mambo hayo bado yapo ndani yako, unaweza kuachana nayo,” basi hili linaonyesha kwamba umeshindwa kabisa. Wewe ambaye umeshindwa na kuokolewa utasema, “Ni kweli kwamba sisi ni uzao wa Moabu, lakini tumeokolewa na Mungu, na ingawa uzao wa Moabu ulikataliwa na kulaaniwa, na kupelekwa uhamishoni na Waisraeli miongoni mwa Mataifa, leo Mungu ametuokoa. Ni kweli kwamba sisi ni wapotovu kuliko watu wote—hili lilitamkwa na Mungu, huu ni ukweli, na haupingwi na mtu yeyote. Lakini leo tumeukwepa ushawishi huo. Tunawachukia sana mababu zetu, tupo radhi kuwageuzia migongo mababu zetu, kuwatelekeza kabisa na kutii mipango yote ya Mungu, kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, na kutimiza matakwa Yake kwetu, na kufikia ridhaa ya mapenzi ya Mungu. Moabu alimsaliti Mungu, hakutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, na alichukiwa na Mungu. Lakini tunapaswa kujali moyo wa Mungu, na leo, kwa kuwa tunaelewa mapenzi ya Mungu, hatuwezi kumsaliti Mungu, na tunapaswa kuwakana mababu zetu wa kale!”
kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Punde tu Mungu anapokuwa uzima katika watu, wanakuwa hawana uwezo wa kumwacha Mungu. Je, hili sio tukio la Mungu? Hakuna ushuhuda mkubwa kuliko huu! Mungu amefanya kazi hadi kiwango fulani; Amewataka watu kutoa huduma, na kuadibiwa, au kufa, na watu hawajarudi nyuma, ambalo linaonyesha kuwa watu hawa wameshindwa na Mungu. Watu ambao wana ukweli ni wale ambao, katika matukio wanayopitia ya kweli, wanaweza kusimama imara katika ushuhuda wao, kusimama imara katika nafasi zao, kusimama katika upande wa Mungu, bila kurudi nyuma, na ambao wanaweza kuwa na uhusiano wa kawaida na watu wanaompenda Mungu, wale ambao, mambo yakishawatokea, wanaweza kumtii Mungu kabisa, na wanaweza kumtii Mungu hadi kifo. Matendo na ufunuo wako katika maisha halisi ndio ushuhuda wa Mungu, ni kuishi kwa kudhihirisha maisha ya mwanadamu na ushuhuda wa Mungu, na huku ni kufurahia upendo wa Mungu; unapopitia hadi kiwango hiki, matukio unayopitia yatakuwa yamekuwa na athari.
kutoka katika “Wanaompenda Mungu Wataishi Milele Katika Mwangaza Wake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Tanbihi:
a. Nakala ya awali imeacha “katika maisha yake mwenyewe.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni