XVII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Jinsi ya Kutambua Kati ya Uhalisi wa Ukweli na Maarifa ya Biblia na Mafundisho
Ukweli ni nini? Maarifa ya Biblia na mafundisho ni nini?
Aya za Biblia za Kurejelea:
“Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu” (Yohana1:1).
“Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, aliyejawa neema na ukweli” (Yohana 1:14).
“Mimi ndiye njia, ukweli na uhai” (Yohana 14:6).
“Watakase kupitia kwa ukweli wako: neno lako ni ukweli” (Yohana 17:17).
“Akajibu na kuwaambia, Isaya ametabiri vizuri kuhusu ninyi wazandiki, jinsi ilivyoandikwa, Watu hawa wananiheshimu kwa midomo yao, bali mioyo yao iko mbali na mimi. Hata hivyo, wananiabudu bure, wakifundisha mafundisho ambayo ni amri za wanadamu. Kwa kuiweka kando amri ya Mungu, mnashikilia desturi ya wanadamu, kama kuosha vyungu na vikombe: nanyi mnafanya mambo mengine mengi kama haya.Naye akawaambia, Mnakataa kabisa amri ya Mungu, ili mweze kuizingatia desturi yenu wenyewe. … Mkilisababisha neno la Mungu lisiwe na athari yoyote kupitia desturi yenu, ambayo mmepokea: na mambo mengine kama haya mnayoyafanya” (Marko 7:6-9, 13).
Maneno Husika ya Mungu:
Mungu ndiye ukweli, njia na uzima.
kutoka katika “Kuonekana kwa Mungu Kumeleta Enzi Mpya” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ukweli ukiwekwa kwa lugha ya binadamu ni methali kwa mwanadamu; ubinadamu hauwezi kupata uzoefu wake kikamilifu, na ubinadamu lazima uishi kwa kuutegemea. Kipande cha ukweli kinaweza kuufanya ubinadamu mzima kuishi kwa maelfu ya miaka.
Ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake.
kutoka katika “Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Ukweli si wa kifomyula, wala si sheria. Haujakufa—ni maisha, ni kitu kilicho na uhai, na ni kanuni ambayo lazima kiumbe kifuate na kanuni ambayo lazima mwanadamu awe nayo katika maisha yake. Hiki ni kitu ambacho lazima uelewe zaidi kutoka kwa uzoefu. Haijalishi ni katika awamu gani ambayo umeifikia katika uzoefu wako, huwezi kutenganishwa na neno la Mungu au ukweli, na kile unachoelewa kuhusu tabia ya Mungu na kile unachojua kuhusu kile Alicho nacho Mungu na kile Alicho ni vitu ambavyo vimeonyeshwa vyote katika maneno ya Mungu; vimeungana kabisa na ule ukweli. Tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho vyenyewe ni ukweli; ukweli ni dhihirisho halisi la tabia ya Mungu na kile Alicho nacho na kile Alicho. Unafanya kile Mungu Alicho nacho na kile Alicho kuwa thabiti na kukionyesha waziwazi; unakuonyesha moja kwa moja kile ambacho Mungu anapenda, kile ambacho Hapendi, kile Anachokutaka ufanye na kile ambacho Hakuruhusu ufanye, ni watu wapi Anaowadharau na ni watu wapi Anaowafurahia. Katika ule ukweli ambao Mungu anaonyesha watu wanaweza kuona furaha, hasira, huzuni, na shangwe Yake, pamoja na kiini Chake—huu ndio ufichuzi wa tabia Yake.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha.
kutoka katika “Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kila kitu ambacho Mungu anafanya ni ukweli na maisha. Ukweli kwa mwanadamu ni kitu ambacho hawawezi kukosa katika maisha yao, kitu ambacho hawawezi kuishi bila; unaweza pia kusema kwamba ndicho kitu kikuu zaidi. Ingawa huwezi kukiangalia au kukigusa, umuhimu wake kwako hauwezi kupuuzwa; ndicho kitu cha pekee kinachoweza kukuletea pumziko moyoni mwako.
kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe III” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ukweli huu ni tabia ya maisha ya ubinadamu wa kawaida, ni sawa na kusema, kile ambacho Mungu alitaka kwa mwanadamu alipomuumba hapo mwanzo, yaani, ubinadamu wote wa kawaida (ikiwa ni pamoja na hisia za kibinadamu, umaizi, hekima, na maarifa ya msingi ya kuwa mwanadamu).
kutoka katika “Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengi hawaelewi kwa nini wanapaswa kumwamini Mungu, wala jinsi ya kumwamini Mungu, na hawafanyi chochote zaidi ya kutafuta kiupofu dondoo ili kufasiri sura za Biblia. Hawajawahi kufuata mwelekeo wa kazi ya Roho Mtakatifu; muda wote huo, hawajafanya chochote, bali kujifunza na kuchunguza Biblia kwa papara, na hakuna hata mmoja ambaye amepata kazi mpya ya Roho Mtakatifu nje ya Biblia, hakuna ambaye amewahi kujitenga na Biblia, wala kuthubutu kujitenga na Biblia. Watu wamejifunza Biblia kwa miaka yote hii, wamekuja na maelezo mengi sana, na kufanya kazi kubwa sana, pia wana maoni mengi tofauti kuhusu Biblia, ambayo yamekuwa ni mdahalo usiokwisha, kiasi kwamba ziadi ya madhehebu elfu mbili yameanzishwa hadi leo. Wote wanataka kutafuta ufafanuzi maalumu, au siri za kina zaidi katika Biblia, wanataka kuichunguza, na kuipata katika usuli wa kazi ya Yehova katika Israeli, au usuli wa kazi ya Yesu katika Yudea, au siri nyingi zaidi ambazo hakuna yeyote anayejua.
kutoka katika “Kuhusu Biblia (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kila siku wao hutafuta dalili Yangu katika Biblia, na kupata vifungu “vinavyofaa” hapa na pale wanavyovisoma bila kukoma, na ambavyo wao hukariri kama maandiko. Hawajui jinsi ya kulingana na Mimi, hawajui maana ya kuwa katika uadui na Mimi, na wanasoma tu maandiko kwa upofu. Wao huzuia ndani ya Biblia na Mungu asiye yakini ambaye hawajawahi kumwona, na hawana uwezo wa kumwona, na wao huitoa tu na kuiangazia wakati wao wa ziada. Wao wanaamini kuwepo Kwangu tu ndani ya eneo la Biblia. Kwa fikira zao, Mimi ni sawa na Biblia; bila Biblia Mimi sipo, na bila Mimi hakuna Biblia. Wao hawatilii maanani kuwepo Kwangu au matendo, lakini badala yake hujishughulisha na umakini mno na maalum kwa kila neno la Maandiko, na wengi wao hata huamini kwamba Mimi sipaswi kufanya jambo lolote Nipendalo kufanya ila tu kama lilitabiriwa na Maandiko. Wao hutia umuhimu mwingi sana kwa Maandiko. Inaweza kusemwa kwamba wao huona maneno na maonyesho yakiwa muhimu mno, kwa kiasi kwamba wao hutumia mistari ya Biblia kupima kila neno Ninalolisema, na kunilaani Mimi. Wanalotafuta si njia ya uwiano na Mimi, au njia ya uwiano na ukweli, lakini njia ya uwiano na maneno ya Biblia, na wanaamini kwamba chochote ambacho hakiambatani na Biblia, bila ubaguzi, si kazi Yangu. Je, si watu wa namna hiyo ni wazawa watiifu wa Mafarisayo?
kutoka katika “Unapaswa Kutafuta Njia ya Uwiano na Kristo” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine hufanya kazi na kuhubiri na, ingawa kwa juu juu inaonekana kana kwamba wanashiriki kuhusu neno la Mungu, yote wanayozungumza kuhusu ni maana sisisi ya neno la Mungu, lakini hakuna kitu halisi kinachotajwa. Mahubiri yao ni kama mafundisho kutoka kwa kitabu cha kiada cha lugha; maneno ya Mungu yanapangwa kitu kimoja baada ya kingine, kipengele baada ya kipengele, na baada ya wao kumaliza kila mtu huwasifu, kwa kusema: “Mtu huyu ana uhalisi. Alihubiri vizuri sana na kwa maelezo ya kina sana.” Baada ya wao kumaliza kuhubiri, wanawaambia wengine wayaweke yote pamoja na kuyatuma kwa kila mtu. Matendo yao yanakuwa kuwadanganya wengine na yote wanayohubiri ni uongo. Kwa juu juu, inaonekana kana kwamba wanahubiri neno la Mungu tu na linaonekana kulingana na ukweli. Lakini kwa utambuzi ulio makini zaidi, utaona kwamba ni maandishi na mafundisho tu na fikira za uongo pamoja na mawazo na mawazo kiasi ya binadamu na vile vile sehemu fulani zinazomwekea Mungu mipaka. Je, kuhubiri kwa namna hii hakuingilii kazi ya Mungu? Ni huduma inayompinga Mungu.
kutoka katika “Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kutoa kwenu “muhtasari kuhusu ukweli” hakufanywi ili watu wapate maisha au kupata mabadiliko katika tabia zao kutoka kwa ukweli. Badala yake, ni ili watu wawe weledi wa maarifa na mafundisho fulani kutoka katika ukweli. Wao huonekana kuelewa lengo la kazi ya Mungu, wakati kwa kweli wamekuwa weledi wa baadhi ya maneno na mafundisho tu. Hawaelewi maana iliyokusudiwa ya ukweli; si tofauti na kusomea theolojia au kusoma Biblia. Unakusanya vitabu hivi au vifaa hivyo, na kisha kuwa na kipengele hiki cha mafundisho au kipengele kile cha ujuzi. Wao ni wasemaji wa kiwango cha juu wa mafundisho—lakini ni nini kinachofanyika wanapomaliza kunena? Watu basi hawana uwezo wa kupitia, hawana ufahamu wa kazi ya Mungu, wala hawajifahamu. Mwishowe, yote ambayo watakuwa wamepata ni virai na kanuni, na wanaweza kuzungumza juu ya mambo hayo machache pekee. Mungu angefanya jambo jipya, je, ungeweza kulinganisha mafundisho yote unayojua na hilo? Kwa hiyo, hayo mambo yako ni kanuni tu na wewe unawafanya watu wajifunze theolojia tu, kutowaruhusu kupitia neno la Mungu au ukweli. Vitabu hivyo ambavyo watu hukusanya vinaweza kuwaleta katika theolojia na maarifa tu, katika virai na katika kanuni na mila. Haviwezi kuwaleta watu mbele ya Mungu au kuwaruhusu kuuelewa ukweli au mapenzi ya Mungu. Unafikiri kwamba wanapouliza swali baada ya swali, kisha kuyajibu, na muhtasari na ufupisho kuandikwa, basi ndugu zako wataweza kuyaelewa kwa urahisi. Unafikiri kwamba mbali na kuwa rahisi kukumbuka, masuala haya ni wazi mara moja, na kwamba hii ni njia nzuri sana ya kufanya vitu. Lakini kile wanachokielewa siyo maana halisi iliyokusudiwa ya ukweli na hakilingani na uhalisi—ni maneno na mafundisho tu. … Kufanya hivi ni kuwaongoza watu kuelewa na kuwa weledi wa maarifa. Wewe huwaleta wengine katika mafundisho ya kidini, na kuwafanya wamfuate na kumwamini Mungu ndani ya mafundisho ya dini. Je, huko si kuwa sawa tu na Paulo? Ninyi hufikiri kwamba kupata weledi wa maarifa ya ukweli ni muhimu hasa, na kwamba kukariri mafungu ya maneno ya Mungu, kuzungumza kuhusu mafundisho na kugundua virai ndani ya maneno ya Mungu yote ni muhimu sana, lakini jinsi watu wanavyoelewa neno la Mungu si muhimu hata kidogo. Kwa hiyo, siku zote ninyi hutaka kuweka katika mfumo vitu hivi ili watu wote washirikiane, wakisema mambo sawa, na kuzungumza kuhusu mafundisho, ili wawe na maarifa sawa na kutii kanuni sawa—hili ndilo lengo lenu. Ninyi kufanya hili kunaonekana kuwa kwa ajili ya watu kupata ufahamu, wakati kinyume chake hamjui kwamba hili linawaleta watu katikati ya kanuni ambazo ziko nje ya ukweli wa maneno ya Mungu.
kutoka katika “Bila Ukweli Ni Rahisi Kumkosea Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kupata ufahamu wa kweli kuhusu maana halisi katika neno la Mungu sio jambo rahisi. Usifikiri tu kwamba ikiwa unaweza kutafsiri maana halisi ya maneno ya Mungu, na kila mtu akisema ni vizuri na kukupa hongera inahesabika kama kuelewa, neno la Mungu. Hilo si sawa na kuelewa neno la Mungu. Ikiwa umepata nuru kiasi kutoka ndani ya neno la Mungu na umefahamu umuhimu wa kweli wa neno la Mungu, ikiwa unaweza kueleza mapenzi ya Mungu ni yapi ndani ya maneno hayo na yatafanikisha nini hatimaye, punde haya yote yanaeleweka hilo linahesabika kama kuwa na kiwango fulani cha ufahamu wa neno la Mungu. Hivyo, kuelewa neno la Mungu si jambo rahisi kabisa. Kwa sababu tu unaweza kutoa maelezo ya madoido ya maandishi ya neno la Mungu haimaanishi kuwa unalielewa. Bila kujali vile unavyoweza kueleza maandishi ya neno la Mungu bado ni mawazo na jinsi ya kufikiria kwa mwanadamu—ni bure! … Ukieleza hili kwa uhalisi au kutoka kwa fikira au mawazo yako mwenyewe, basi ufahamu wako si wa kweli bila kujali jinsi unavyoweza kueleza kwa umbuji. Inawezekana kwamba wewe hata unaweza hata kutoka maana nje ya muktadha na kueleza neno la Mungu vibaya, na hilo ni la taabu hata zaidi. Hivyo, ukweli kimsingi unapatikana kwa kupokea nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu kupitia kujua neno la Mungu. Kuelewa maana halisi ya neno Lake au kuweza kulieleza hakuhesabiki kama kupata ukweli. Kama ungehitaji tu kueleza maandishi ya neno Lake, basi kungekuwa na haja gani ya kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu? Katika hali hiyo ungehitaji kuwa na kiwango fulani cha masomo, na wale ambao hawajasoma wangekuwa kwenye hatari kabisa. Kazi ya Mungu si kitu ambacho kinaweza kufahamika na akili ya mwanadamu. Ufahamu wa kweli wa neno la Mungu unategemea hasa kupata nuru kutoka kwa Roho Mtakatifu; hii ni namna ya kuupata ukweli.
kutoka katika “Ni Kwa Kufuatilia Ukweli Tu Ndiyo Unaweza Kupata Mabadiliko Katika Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kama mmesoma sana neno la Mungu lakini mnaelewa tu maana ya maandishi na hamna maarifa ya kwanza ya neno la Mungu kupitia uzoefu wenu wa vitendo, hamtajua neno la Mungu. Ili mradi unahusika, neno la Mungu si maisha, lakini barua bila uhai. Na kama unaamini tu barua bila uhai, huwezi kufahamu kiini cha neno la Mungu, wala kuelewa mapenzi Yake. Wakati tu unapitia neno Lake katika uzoefu wako halisi ndio maana ya kiroho ya neno la Mungu itafunguka yenyewe kwako, na ni katika uzoefu tu ambapo unaweza kufahamu maana ya kiroho ya ukweli mwingi, na ni kwa kupitia tu uzoefu ndio unaweza kufungua mafumbo ya neno la Mungu. Usipoliweka katika vitendo, basi haijalishi jinsi neno Lake lilivyo wazi, jambo pekee ambalo umefahamu ukashikilia ni barua tupu na mafundisho, ambayo yamekuwa kanuni za dini kwako. Si hili ndilo Mafarisayo walifanya? Kama mtatenda na kupitia neno la Mungu, linakuwa vitendo kwenu; msipotafuta kulitenda, basi neno la Mungu kwenu ni kidogo zaidi ya hadithi ya mbingu ya tatu. …
… Watu wengi wameridhika na kuelewa tu maandiko ya neno la Mungu na kuzingatia katika kujiandaa wenyewe na mafundisho bila kupitia kina chake katika vitendo; si hiyo ni njia ya Mafarisayo? Jinsi gani kirai “Neno la Mungu ni uzima” kikawa ukweli kwao, basi? Wakati tu mtu anatenda neno la Mungu ndio maisha yake yanaweza kweli kuchanua; maisha hayawezi kukua tu kwa kusoma neno Lake. Kama ni imani yako ya kwamba kuelewa neno la Mungu ni kila kinachohitajika kuwa na maisha, kuwa na kimo, basi kuelewa kwako ni potovu. Kuelea kwa kweli neno la Mungu hutokea wakati unatenda ukweli, na ni lazima uelewe ya kwamba “ni kwa kutenda tu ukweli kunaweza kueleweka siku zote.”
kutoka katika “Tendeni Ukweli Mara Mnapouelewa” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama hujapata uzoefu wa ukweli lakini bado unataka kuhubiri kuuhusu basi, haijalishi unachosema, hautahubiri kwa dhahiri—utakuwa tu unahubiri vitu vya juu juu. Unaweza kufikiri kuwa maneno unayonena yana nuru, lakini ni kanuni tu, sio uhalisi, na watu wanaosikiliza hawataweza kushika vitu vya kweli; wanaweza kuwa wanahisi kwamba unachosema ni ukweli wanapokisikiliza, lakini baadaye utasahaulika kabisa. Kama unachohubiri kuhusu sio hali halisi, hutaweza kuigusa mioyo ya watu; watakisahau hata kama wanataka kukikumbuka, na hutaweza kuwasaidia.
kutoka katika “Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni