Maneno Husika ya Mungu:
Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa upinzani kwa Mungu wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu. Kwa hivyo, vile mwanadamu alivyomwamini Mungu katika mawazo yake, Mungu hakumlaumu mwanadamu ama kuulizia mengi kutoka kwa mwanadamu, kwani mwanadamu hangemwona Mungu hata kidogo. Mungu anapopata mwili na kuja kufanya kazi miongoni mwa wanadamu, wote wanamtazama Mungu na kusikia maneno Yake, na wote wanaona vitendo vya Mungu katika mwili. Wakati huo, dhana zote za mwanadamu zinafutwa na kubaki povu tu. Kwa wale wanaomwona Mungu anayejitokeza katika mwili, wote walio na utiifu ndani ya mioyo yao hawalaaniwi, ilhali wanaosimama dhidi Yake kimakusudi watachukuliwa kuwa wapinzani wa Mungu. Wanadamu kama hao ni maadui wa Kristo na ni maadui wanaosimama dhidi ya Mungu kimakusudi.
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Yeyote asiyemtambua Mungu ni adui; yaani, yeyote aliye ndani ama nje ya mkondo huu ambaye hamtambui Mungu aliyepata mwili ni adui wa Kristo! … Wale watu wanaomwamini Yesu tu na hawamwamini Mungu aliyepata mwili wakati wa siku za mwisho na wale wanaodai kwa maneno kumwamini Mungu aliyepata mwili lakini wanafanya maovu wote ni adui wa Kristo, sembuse wale watu wasiomwamini Mungu. Hawa watu wote wataangamizwa.
kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kama umemwamini Mungu kwa miaka mingi, lakini hujawahi kumtii ama kuyakubali maneno Yake, na badala yake umemwuliza Mungu anyenyekee kwako na kufuata dhana zako, basi wewe ni mtu mwasi zaidi ya wote, na wewe si muumini. Mtu kama huyu anawezaje kutii kazi na maneno ya Mungu ambayo hayafuati fikira za mwanadamu? Mtu mwasi zaidi ni yule anayemkataa na kumpinga Mungu makusudi. Yeye ni adui wa Mungu na ni mpinga Kristo. Mtu kama huyu daima anakuwa na mtazamo wa kikatili kwa kazi mpya ya Mungu, hajawahi kuonyesha nia hata ndogo ya kutii, na hajawahi kuonyesha utii ama kujinyenyekeza kwa furaha. Anajisifu mbele ya wengine na kamwe haonyeshi utii kwa mwingine. Mbele ya Mungu, anajiona kuwa hodari zaidi katika kuhubiri neno na mwenye ujuzi zaidi katika kufanya kazi kwa wengine. Kamwe hatupi “hazina” anazomiliki tayari, lakini anazichukua kama vitu vinavyorithiwa kwa familia vya kuabudiwa, vya kuhubiri kuhusu wengine, na huvitumia kuhutubia wale wapumbavu wanaomwabudu. Hakika kuna baadhi ya watu kama hawa kanisani. Inaweza kusemwa kwamba wao ni “mashujaa wasioshindwa,” kizazi baada ya kizazi kinachokaa kwa muda mfupi ndani ya nyumba ya Mungu. Wanachukua kuhubiri neno (mafundisho ya dini) kama wajibu wao wa juu zaidi. Mwaka baada ya mwaka na kizazi baada ya kizazi, wao huenenda kwa nguvu wakitekeleza wajibu wao “mtakatifu na usiokiukwa”. Hakuna anayethubutu kuwaguza na hakuna mtu hata mmoja anayethubutu kuwashutumu kwa uwazi. Wanakuwa “wafalme” katika nyumba ya Mungu, wakienea kote wakiwaonea wengine kutoka enzi hadi enzi. Hili kundi la mapepo linataka kuungana mikono na kuharibu kazi Yangu; Nawezaje kuwaruhusu ibilisi hawa waishio kuwepo mbele Yangu?
kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Fahamuni kuwa mnapinga kazi ya Mungu, ama mnatumia dhana zenu kupima kazi ya leo, kwa sababu hamjui kanuni za kazi ya Mungu, na kwa sababu hamchukulii kazi ya Roho Mtakatifu kwa makini kutosha. Upinzani wenu kwa Mungu na kuzuia kazi ya Roho Mtakatifu kumetokana na dhana zenu na upumbavu wenu wa kiasili. Si kwa sababu kazi ya Mungu si sawa, lakini ni kwa sababu mna tabia ya kiasili ya kutotii. Baada ya kupata imani yao katika Mungu, watu wengine hawawezi hata kusema kwa uhakika mwanadamu alikotoka, ilhali wanathubutu kuzungumza hadharani wakitathmini haki na makosa ya kazi ya Roho Mtakatifu. Na pia wanawakemea mitume ambao wana kazi mpya ya Roho Mtakatifu, wakitoa maoni huku wakizungumza kwa zamu; ubinadamu wao uko chini sana, na hawana hisia zozote. Je, si siku itawadia ambapo watu kama hawa watakataliwa na kazi ya Roho Mtakatifu, na kuchomwa katika moto wa kuzimu? Hawafahamu kazi ya Mungu, lakini badala yake wanakosoa kazi Yake, na pia wanajaribu kumwagiza Mungu jinsi atakavyofanya kazi. Je, ni kwa namna gani watu hawa wasio na busara watamjua Mungu? Mwanadamu huja kumjua Mungu wakati anapomtafuta na anapokuwa na uzoefu naye; si katika kumkosoa kwa ghafla ndipo anapokuja kumjua Mungu kwa kupitia kutiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kadiri maarifa ya watu kuhusu Mungu yanavyozidi kuwa sahihi, ndivyo upinzani wao Kwake unavyopungua. Kinyume na hayo, kadri watu wanavyomjua Mungu kwa kiasi kidogo, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano wa kumpinga. Dhana zako, ubinadamu wako wa zamani, na utu wako, tabia na maadili ndiyo “mtaji” ambao unampingia Mungu, na kadri unavyokuwa mpotovu, ama ulivyoshushwa heshima na ulivyo duni, ndivyo unavyozidi kuwa adui wa Mungu. Wale waliomilikiwa na dhana kali na wenye tabia ya unafiki wamo hata zaidi katika uadui wa Mungu mwenye mwili, na watu kama hawa ni wapinga Kristo.
kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Watu wengine wanaoamini katika Mungu daima wanafukuza ndoto zao, wanataka kuyafikia maisha ya Mungu daima, kuwa na maisha ya Mungu; je hili sio jambo hatari? Hili ni jambo hatari sana. Baada ya kufanya kazi kwa muda fulani watasema: “Wakati joka kuu jekundu litakapoanguka kutoka mamlakani lazima tushike madaraka kama wafalme, na kutawala juu ya miji mingi!” Kudhihirisha vitu hivi ni vibaya sana. Wale wasio na uzoefu ni wa kufaa kuzungumza kanuni na kujiingiza katika ndoto, ilhali wanajifikiria kuwa werevu sana, na kufikiria kuwa tayari wanacho kile wanachotaka kwa imani yao kwa Mungu; wao ni wafuasi wa Paulo, na njia wanayoitembea ni njia ya Paulo kabisa; watu hawa wote watakuwa wapinga Kristo na watapata adhabu kali sana.
kutoka katika “Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Unapomtendea Mungu kama mwanadamu, Mungu unayemwamini ni Mungu asiye yakini mbinguni, unamkataa kabisa Mungu mwenye mwili, na moyoni mwako, humtambui Mungu wa vitendo. Kwa wakati huu, wewe utakuwa umekuwa mpinga Kristo, na utakuwa umeanguka gizani. Kadiri unavyofanya madai mengi kutoka kwa Mungu, na kadiri unavyotoa sababu zaidi, ndivyo utakavyokuwa na dhana nyingi juu ya Mungu na ndivyo utakavyokuwa katika hatari zaidi. Unapodai mengi kutoka kwa Mungu, hili linathibitisha kwamba humtendei Mungu kama Mungu kabisa; utakuja kujiona mwenyewe kama Mungu polepole. Unapokuwa ukifanya kazi kanisani, utajitolea ushuhuda, na kusema: “Wakati mmoja Mungu alifanya hili au lile.” Utakachokuwa unamaanisha ni kwamba Mungu ni mdogo kwako. Utamtendea kwa dharau. Moyoni mwako hakutakuwa na uchaji wowote, sauti ya usemi wako itabadilika, tabia yako itakua yenye kiburi, na hatua kwa hatua utaishia kujiinua. Hiki ndicho kinachofanyika wakati watu wanaanguka, na husababishwa kabisa na kutofuatilia ukweli. Wote wanaoanguka wanajikuza na kujitolea ushuhuda wao wenyewe, wao huenda wakijisifu na kujitwalia zaidi, na hawajamweka Mungu moyoni hata kidogo. Je, mmepitia au kushuhudia chochote Ninachosema? Watu wengi hujitolea ushuhuda bila kukoma: Nimeteseka kwa njia hii na ile, nimefanya kazi hii na ile, Mungu amenitendea kwa njia hii na ile, hatimaye Akiniuliza nifanye hiki na kile; Ananifikiria kwa heshima hasa, na sasa niko namna hii na ile. Wanazungumza kwa sauti fulani, na kuchukua msimamo fulani. Hatimaye, watu wengine huishia kufikiri kwamba wao ni Mungu. Wanapofikia hatua hiyo, Roho Mtakatifu atakuwa amewaacha muda mrefu uliopita. Ingawa, kwa sasa, wanapuuzwa, na hawatimuliwi, hatima yao imewekwa, na kile wanachoweza kufanya ni kusubiri adhabu yao tu.
kutoka katika “Watu Wanafanya Madai Mengi Sana kwa Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Wale wanaosoma Biblia katika makanisa makubwa hukariri Biblia kila siku, lakini hakuna yeyote anayeelewa madhumuni ya kazi ya Mungu. Hakuna hata mmoja anayeweza kumwelewa Mungu; juu ya hayo, hakuna yeyote anayekubaliana na moyo wa Mungu. Wote hawana thamani, wanadamu waovu, kila mmoja akisimama juu kufundisha kuhusu Mungu. Ingawa wanalionyesha hadharani jina la Mungu, wanampinga kwa hiari. Ingawa wanajiita waumini wa Mungu, wao ni wale wanaokula mwili na kunywa damu ya mwanadamu. Wanadamu wote kama hao ni mashetani wanaoteketeza nafsi ya mwanadamu, pepo wakuu wanaowasumbua kimakusudi wanaojaribu kutembea katika njia iliyo sawa, na vizuizi vinavyozuia njia ya wanaomtafuta Mungu. Inagawa wao ni wenye “mwili imara,” wafuasi wao watajuaje kwamba wao ni wapinga Kristo wanaomwongoza mwanadamu katika upinzani kwa Mungu? Watajuaje kwamba hao ni mashetani hai wanaotafuta hasa nafsi za kuteketeza?
kutoka katika “Wote Wasiomjua Mungu Ndio Wanaompinga Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Ingawa kile wapinga Kristo wanashiriki kinaonekana kuwa maneno ya Mungu kwa nje, na wanashiriki ufahamu na uzoefu kiasi wa ukweli, haimaanishi kwamba wana nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, kwa sababu Roho Mtakatifu hawafanyii kazi. Hata hivyo, wanaweza kuyaiba maneno ya wengine ya uzoefu na ufahamu na kuyatumia kujificha na kujipamba. Wanaweza kuiba ufahamu wa wengine ambao unalingana kiasi na ukweli ili kuwadanganya watu, na wanaposikia maneno haya, wanafikiri, “Kile anachosema mtu huyu ni sahihi na kizuri. Kweli ana nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu.” Watu watampenda mno. Lakini ukweli ni kwamba yote haya yameibwa kutoka kwa wengine. Niambie, je, wanadamu wapotovu wanatumia hila hizi? Wanadamu wote wapotovu wanajua jinsi ya kuiba, jinsi ya kujisingizia, jinsi ya kujificha. Kuiba maneno ya mtu mwingine ni rahisi sana tu. Baada ya kusikiliza ushirika wa mtu mwingine, kwa siri wanaandika maneno yenye nguvu zaidi na mazuri zaidi, wanayaiga mara nyingi kama kasuku hadi wayakariri, na kisha wanaenda kuyawasiliana na wengine. Wakati mwingine wataenda pahali pamoja kuwasikiza wengine, kisha waende pengine kuzungumza. Wanafanya hili haraka sana kiasi kwamba kufumba kufumbua, wameyafanya kuwa yao. Wanayaeneza punde tu wanapoyapata. Watu wanaweza kufanya hili—hiyo ni habari inayojulikana na wote. Kwa kuwa wapinga Kristo wako kwenye njia isiyo sahihi na hawana kazi ya Roho Mtakatifu, haiwezekani kwa wao kuwa na ufahamu wa kweli wa neno la Mungu na ukweli. Hata hivyo, kuna baadhi ya watu wanaosikia mambo fulani ambayo mpinga Kristo ameyawasilisha na kuhisi kwamba yanapendeza mno, na kisha wanafikiri, “Je, hana kazi ya Roho Mtakatifu? Vinginevyo, angewezaje kuwa na ufahamu kama huo wa maneno ya Mungu na ukweli?” Fikira ya aina hii si sahihi, kwa sababu ukweli ni kwamba maneno kama hayo yanaweza kuibwa. Anaweza kuiga maneno ya wengine. Siku hizi, kuna wachungaji kadhaa katika dini wanaojichukulia maneno ya Mungu na ushirika wa nyumba ya Mungu. Baada ya kuyasoma, wanayahubiri kwa umati siku za Jumapili, na watu wanapoyasikia, wanafikiri, “Ee, hayo yalikuwa mahubiri mazuri sana. Wakati huu kweli yalikuwa na ukweli.” Kisha wote wanachanga kwa shauku, na kwa njia hii, riziki yao sasa imehakikishwa. Je, kuna wachungaji wengi kama hao katika dunia ya dini? Unapowaonyesha njia ya kweli, wanakataa kuikubali, lakini baada ya kuvipata vitabu kutoka kwa nyumba ya Mungu, wanavitumia kwa siri katika mahubiri yao. Wanavitumia kuchuma fedha, kuwadanganya watu na kujiinua. Wanachukua yale ambayo kwa dhahiri ni maneno ya Mungu na kuyadai kama maneno yao wenyewe, uzoefu na maarifa yao wenyewe. Hii ni mbinu ya kustahili dharau ya wapinga Kristo ya kuwadanganya wengine.
kutoka katika “Jinsi ya Kutambua Udanganyifu wa Kristo wa Uongo na Mpinga Kristo” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha II
Kwa ajili ya utambuzi wa pepo wanaompinga Kristo, mtu lazima awe na uwezo wa kubaini sifa saba za asili yao. Hii ni muhimu sana kwa kutambua waziwazi uso wa kweli wa kishetani wa pepo wa mpinga Kristo. Maelezo ya sifa saba za asili mbaya mno za wapinga Kristo yametolewa hapa chini:
Kwanza, wapinga Kristo wote ni wenye kiburi na majivuno; wao hukataa kumtii mtu yeyote, hujiinua tu wao wenyewe, na hushikilia njia zao wenyewe za kufanya mambo. Wao huwaangalia wengine kwa chuki, hawana nafasi yoyote kabisa ya Mungu mioyoni mwao, na kamwe hawana uchaji Mungu. Hakuna mtu yeyote katika makanisa anayeweza kuwafanya wapinga Kristo wakubaliane na mambo, na hakuna anayeweza kuwadhibiti. Viongozi na wafanyakazi katika ngazi zote za makanisa ni kama maadui kwao. Kwa mfano, wengine husema: “Mimi humtii Mungu pekee na wala si mtu mwingine yeyote.” Au husema: “Mimi humtii mtu fulani na fulani, lakini sitamtii mtu mwingine yeyote.” Na kadhalika. Inaweza kuonekana kutokana na hili kwamba watu kama hawa wote wana asili ya ibilisi Shetani, ambayo ndiyo maana sio ajabu kabisa kwamba wana uwezo wa kujitukuza, wameridhika na hawako tayari kuendelea mbele, na wana hamu kuu ya kushuhudia kwamba wao ni wazaliwa wa kwanza wa Mungu, wana Wake wapendwa. Watu waovu kama hawa wote huwa pepo halisi wanaompinga Kristo mara tu wanapoingia mamlakani. Kukataa kumtii mtu yeyote na kujitukuza—hiyo ndiyo sifa ya kwanza ya asili mbaya mno ya wapinga Kristo.
Pili, kwa kuwa wapinga Kristo wana asili kama Shetani, yaani, hawaupendi ukweli na hata huchukia na kupinga ukweli na pia kumpinga Mungu, wapinga Kristo kamwe hawachukulii kula na kunywa maneno ya Mungu kwa uzito. Hawajawahi kula au kunywa maneno ya Mungu kwa kweli, wala hawakubali maneno ya Mungu na ukweli. Kwa hivyo, hawana nuru au mwanga wa Roho Mtakatifu utokao kwa maneno ya Mungu, na aidha hawajui ukweli kuhusu upotovu wao kupitia kwa maneno ya Mungu kwa kweli. Kwa hiyo, pepo wanaompinga Kristo kamwe hawazungumzi juu ya kujijua, sembuse kujichambua au kujifichua, kama kwamba hawakuwa na upotovu. Hajawahi kuwa na ushirika juu ya maarifa ya kweli ya maneno ya Mungu na ukweli, na aidha hawawezi kushuhudia kazi ya Mungu na kile anacho na alicho. Yote wanayojua kufanya ni kujijenga na kujishuhudia. Wao huthubutu hata kushuhudia kwamba wao ni wazaliwa wa kwanza wa Mungu, wana wapendwa, na kwamba wamekamilishwa. Kwa kweli ni wa kuleta hizaya na wasio na haya kupita kiasi. Hii ni sifa ya pili ya asili mbaya mno ya wapinga Kristo.
Tatu, kwa kuwa kulingana na asili zao mbaya mno wapinga Kristo hawapendi ukweli na hata huchukia ukweli, hupinga ukweli na kumpinga Mungu, mtu kamwe hataona wapinga Kristo wakiweka ukweli katika vitendo. Pepo wanaompinga Kristo kamwe hawatendi ukweli, na maonyesho makuu ya hili ni yafuatayo: 1. Kamwe hawatii hukumu, kuadibu, majaribio na usafishaji wa Mungu; 2. Wao kamwe hawatii maneno ya Mungu au ukweli; 3. Kamwe hawaukubali ukweli; 4. Kamwe hawakubali kupogolewa na kushughulikiwa; 5. Kamwe hawamtii mtu yeyote ambaye anaweza kufanya ushirika na kuweka ukweli kwenye vitendo—hawamtii mtu yeyote; 6. Wao daima hunena kutoka kwa nafasi ya juu kuliko wengine au hata kutoka kwa nafasi ya Mungu, kila mara wao huwakaripia watu. Wao ni stadi katika kufasili vibaya maneno ya Mungu, kupotosha ukweli, kugeuza mema na mabaya, kurudisha mashtaka ya uongo, wakiwalaani wengine bila sababu na kuwahukumu kiholela. Mara nyingi wao hudanganya, huhukumu, hulaani, na kuwasingizia watu wengine. Aidha, wamejawa na shauku ya uadui kwa watu wa Mungu walioteuliwa. Hii kwa hivyo inathibitisha kuwa wapinga Kristo ni watu ambao hawawezi kamwe kutenda ukweli. Hii ni sifa ya tatu ya asili mbaya mno ya wapinga Kristo.
Nne, vitendo na tabia za wapinga Kristo vyote ni kwa ajili ya kupigania mamlaka na faida, na kufikia lengo la kuwadhibiti watu wa Mungu walioteuliwa na kuanzisha ufalme wao wenyewe wa kujitegemea. Wapinga Kristo hufuatilia tu hadhi na mamlaka na huabudu nguvu za kishetani kupita mipaka. Hadhi, mamlaka na pesa ni sanamu za wapinga Kristo na malengo wanayofuatilia. Hiki ni kiini cha asili ya wapinga Kristo. Vitu ambavyo wapinga Kristo wanapania na kufanya kazi kwa bidii kwa ajili yavyo ni hadhi na mamlaka pekee. Ikiwa kitu sio kwa ajili ya hadhi na mamlaka, hawatakifanya. Wako tayari kufanya chochote ambacho kitasaidia kupigania kwao hadhi na mamlaka. Kwa ajili ya kutafuta hadhi, hawatasita kuadhibu, kusingizia au kuwadhuru wengine kwa njia yoyote. Machoni pa wapinga Kristo, wakiwa na hadhi na mamlaka wanaweza kupata kila kitu, lakini kupoteza hadhi na mamlaka kunamaanisha kupoteza kila kitu. Hili ni onyesho zima la kiini cha asili mbaya mno ya joka kuu jekundu. Hii ni sifa ya nne ya asili mbaya mno ya wapinga Kristo.
Tano, kando na kupenda ufuatiliaji wa mamlaka na hadhi, wapinga Kristo hupenda kushirikiana na kujihusisha na watu wote waovu. Wao huvutiwa na mtu yeyote anayeshiriki tabia mbovu kama zao na wanaweza kuwahudumia; wanapenda na kushirikiana na yeyote anayewaabudu na kuwasifu mno. Wote waliotegwa na wapinga Kristo ni pepo na wanyama, wanyama wakatili. Pepo wanaompinga Kristo kamwe hawapendi kujihusisha na watu waaminifu ambao wanaitembea njia sahihi na kufuatilia ukweli. Kamwe hawapendi watu wema na wazuri, na hata wanaweza kugeuza ukweli na kubadilisha yaliyo sahihi kuwa makosa ili kudai kwamba watu waovu ni wazuri na watu wazuri ni waovu. Wao hufanya juu chini kutengeneza na kuadhibu, kukashifu kwa uovu, kuwahukumu wengine bila sababu, kuficha dhambi zao wenyewe kwa kumlaumu mtu mwingine, na kutenda bila mpango. Hii husababisha machafuko katika makanisa kila mahali. Huu hata ni ushahidi zaidi wa asili mbaya mno ya wapinga Kristo. Kile ambacho pepo wote wanaompinga Kristo wanakidharau zaidi ni watu wazuri wanaofuatilia ukweli, kuunga mkono kanuni, na wanaotambua haki. Wanachochukia zaidi ni watu ambao wana utambuzi juu yao, wanaochukia uovu, na walio na ukweli na ubinadamu. Ndiyo maana wapinga Kristo wanaweza kuwatesa, kuwasingizia na kuwadhuru watu wema pamoja na pia kuwapinga viongozi na wafanyakazi wa ngazi zote. Hii ni sifa ya tano ya asili mbaya mno ya wapinga Kristo.
Sita, pepo wote wanaompinga Kristo wana chuki kali mno kwa mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu, na wanapanga njama kuchukua nafasi yake. Wana ghadhabu na kichaa. Wanapoyaona makanisa yakitekeleza uchaguzi wa kidemokrasia na kuona watu wa Mungu walioteuliwa wakianza kuingia katika njia sahihi katika imani yao, wao huanza uzinduzi wa mashambulio kwa hasira, wakifanya kila linalowezekana kuvuruga uchaguzi wa kanisa. Wao hueneza kila aina za uwongo na uasi wa dini ili kuwapotosha watu wa Mungu walioteuliwa na mpaka kuwashambulia, kuwahukumu na kuwalaani viongozi na wafanyakazi wa ngazi zote katika nyumba ya Mungu kama bandia. Hii ni ili waweze kupanda kutoelewana kati ya watu wa Mungu walioteuliwa na viongozi na wafanyakazi wa ngazi zote. Kwa ajili ya kuwadanganya na kuwadhibiti watu wa Mungu walioteuliwa, bila haya wao hata huwafanya wengine wawapigie kura na kuwatii badala ya kuwachagua wale wanaofuatilia ukweli, kutii kazi ya Mungu kwa kweli na ambao wameingia katika uhalisi wa ukweli wawe viongozi na wafanyakazi wa ngazi yoyote. Hii inafanya malengo ya wapinga Kristo kuyatawala makanisa na kudhibiti watu wa Mungu walioteuliwa waziwazi. Tunaweza kufikia uamuzi kutokana na hili kuwa pepo wote wanaowapinga Kristo wana chuki hasa kwa mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu pamoja na viongozi na wafanyakazi wa ngazi zote katika nyumba ya Mungu. Hii hata zaidi inafichua nia za kudharauliwa za pepo wanaompinga Kristo, kuogopa zaidi ukweli kutawala katika nyumba ya Mungu na kuogopa zaidi wale wanaofuatilia ukweli kutawala katika nyumba ya Mungu. Hii ni kwa sababu siku ambayo ukweli na watu wanaofuatilia ukweli watatawala katika nyumba ya Mungu ni siku ambayo wapinga Kristo watakutana na mwisho wao. Bila shaka, kile ambacho pepo wanaompinga Kristo wanachukia zaidi ni mtu anayetumiwa na Roho Mtakatifu na viongozi na wafanyakazi wa ngazi zote wanaofuatilia ukweli. Hii ni sifa ya sita ya asili mbaya mno ya wapinga Kristo.
Saba, hakuna pepo wowote wanaompinga Kristo ambao hutubu kwa kweli bila kujali wanakumbana na ushinde wa kugandamiza au kukataliwa kupi, wala hawatajitafakari wenyewe ili kujijua. Huku baadhi ya pepo huenda wakamwaga machozi, haya si machozi ya toba lakini badala yake ni machozi ya kukosewa, ya kutotii, ya chuki. Hakika si machozi ya majuto au ya kuwa na deni. Hii ni kwa sababu wote ambao hawana dhamiri au mantiki ni pepo, na pepo wote hawana ubinadamu hata kidogo. Wote ni wa namna ya Shetani na hawataokolewa na Mungu kabisa. Pepo wote wanaompinga Kristo wana asili ya ibilisi Shetani na hawawezi kabisa kuokolewa, kwa hivyo hawatawahi kujijua na kutubu kwa kweli. Hawatakubali ukweli kamwe na kumtii Mungu kwa kweli. Hii ni sifa ya saba ya asili mbaya mno ya wapinga Kristo.
Sifa hizo saba zilizopo hapo juu ni picha kamili ya asili ya Shetani na asili ya pepo wanaompinga Kristo. Wale wote ambao wana sifa hizi saba za wapinga Kristo ni Shetani na ibilisi halisi. Wote ni makaragosi ya Shetani waliopata tena mwili kutoka kwa ibilisi....
kutoka katika “Wapinga Kristo Lazima Wafukuzwe kabisa ili Kumwasi na Kumshinda Shetani kwa Kweli” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni