10.23.2019

Kupagawa ni nini? Kupagawa hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Je, unajua una nafsi za aina gani? Je, una uwezo wa kuhisi nafsi yako? Unaweza kugusa nafsi yako? Je, unaweza kuhisi roho yako inafanya nini? Hujui, siyo? Kama unaweza kuhisi au kugusa kitu fulani kama hicho, basi ni roho mwingine aliye ndani yako akifanya kitu kwa nguvu—akikufanya utende na kusema vitu. Hilo ni jambo lililo nje yako, lisilo la asili kwako. Wale wenye pepo mbaya watakuwa na ufahamu wa kina wa hili.

kutoka katika “Ikiwa Una Ukweli au La Inaamua Kila kitu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Kama, wakati wa zama hizi, kutatokea mtu mwenye uwezo wa kuonyesha ishara na maajabu, na kutoa mapepo, kuponya wagonjwa, na kufanya miujiza mingi, na kama mtu huyu anadai kwamba yeye ni Yesu ambaye amekuja, basi hii itakuwa ni ghushi ya roho wachafu, na kumuiga Yesu. Kumbuka hili! Mungu Harudii kazi ile ile. Hatua ya kazi ya Yesu tayari imekwisha kamilika, na Mungu Hataichukua tena hatua hiyo ya kazi.
kutoka katika “Kuijua Kazi ya Mungu Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ikiwa katika siku za mwisho “Mungu” sawa na Yesu Angeonekana, Ambaye Anaponya wagonjwa, Anafukuza mapepo na Anayesulubiwa kwa ajili ya wanadamu, “Mungu” huyo, japo Analingana na maelezo ya Mungu katika Biblia, na rahisi kwa mwanadamu kukubali, Hangeweza, katika kiini chake, kuwa mwili uliovaliwa na Roho wa Mungu, bali na roho mwovu.
kutoka katika “Kiini cha Mwili Ulio na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuna wengine ambao wamepagawa na roho wachafu na wanalia kwa kusisitiza wakisema, “Mimi ni Mungu!” Lakini mwishowe, hufichuliwa, kwani wanafanya kazi kwa niaba ya kiumbe asiyefaa. Wanawakilisha Shetani na Roho Mtakatifu hajali kuwahusu hata kidogo. Hata ujiinue vipi, ama kwa nguvu kivipi, wewe bado ni kiumbe aliyeumbwa na wewe unamilikiwa na Shetani. … Huwezi kutengeneza njia ya enzi mpya, na huwezi kuhitimisha enzi nzee na huwezi kukaribisha enzi mpya ama kufanya kazi mpya. Kwa hivyo, huwezi kuitwa Mungu!
kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Watu waliopagawa na mashetani ni wale ambao wameingiliwa na kudhibitiwa na pepo wabaya. Onyesho kuu ni kuwa na maradhi ya saikolojia, au kutokuwa na akili timamu nyakati nyingine, kupoteza kabisa mantiki ya kawaida. Wanamwamini Mungu lakini hawawezi kukubali ukweli na wanaweza tu kuvuruga. Hii ndiyo maana, ingawa wanamwamini Mungu, hawawezi kuokolewa na lazima waondolewe. Wengi wa watu ambao wamepagawa na pepo wabaya ni vikaragosi wa Shetani na huvuruga kazi ya Mungu. Kuna maonyesho kumi makuu kama yafuatayo:
1. Wale wote wanaojifanya kuwa Mungu au Kristo wamepagawa na pepo wabaya.
2. Wale wote wanaojifanya kuwa na roho za malaika wamepagawa na pepo wabaya.
3. Wale wote wanaojifanya kuwa Mungu mwingine mwenye mwili wamepagawa na pepo wabaya.
4. Wale wote wanaosema kwamba maneno ya Mungu ni yao wenyewe au ambao wanawafanya wengine wachukulie maneno yao kama maneno ya Mungu wamepagawa na pepo wabaya.
5. Wale wote wanaojifanya kutumiwa na Roho Mtakatifu ili kuwafanya wengine wawafuate na kuwatii wamepagawa na pepo wabaya.
6. Wale wote wanaozungumza kwa ndimi mara nyingi, wanaofafanua ndimi na wanaweza kuona kila aina za maono ya miujiza, au ambao mara nyingi wanaonyesha dhambi za wengine wamepagawa na pepo wabaya.
7. Wale wote ambao mara nyingi husikia sauti za mwujiza za pepo au milio ya pepo au ambao mara nyingi huona mazimwi, na wale wote ambao kwa dhahiri ni wenye akili punguani wamepagawa na pepo wabaya.
8. Wale wote ambao wamepoteza fikira ya kawaida ya binadamu, wanaozungumza kwa maneno yenye kichaa mara kwa mara, wanaojizungumzia mara nyingi, wanaozungumza upuuzi au wanaosema mara nyingi kwamba Mungu amewaagiza na kwamba Roho Mtakatifu amewagusa pia wamepagawa na pepo wabaya.
9. Wale wote ambao wana matukio ya tabia isiyo ya kawaida, wanaotenda kipuuzi, ambao wakati mwingine ni wajinga, na hawawezi kuzungumza na wengine kwa kawaida ni watu ambao wamepagawa na pepo wabaya. Wale wote ambao wanaainishwa kama wasenge ni aina ya watu ambao wamepagawa na mashetani na ni miongoni mwa wale ambao wataondolewa.
10. Watu wengine kwa desturi ni wa kawaida kabisa lakini, kwa kipindi cha miezi kadhaa au mwaka mmoja au miaka miwili, huenda wakachokozwa na kukuza ugonjwa wa akili. Wakati wa ugonjwa huo wako sawa tu na wale ambao wamepagawa na roho wabaya. Ingawa watu hawa ni wa kawaida wakati mwingine, pia wanaainishwa kama waliopagawa na mashetani. (Ikiwa mtu ana ugonjwa wa akili miaka mingi kabla lakini amekuwa sawa kwa miaka mingi baadaye, anaweza kuelewa na kukubali ukweli kama imani yake, na kupitia mabadiliko kiasi, hawezi kuainishwa kama aliyepagawa na pepo wabaya.) Mtu ambaye amepagawa na mashetani amemilikiwa na kudhibitiwa kikamilifu na Shetani, ni wa Shetani, na amelaaniwa.
kutoka katika “Ili Kufanya Kazi ya Kanisa Vizuri Mtu Lazima Aweze Kutambua Kati ya Aina Kadha za Watu” katika Kumbukumbu Zilizochaguliwa za Kihistoria za Mipangilio ya Kazi ya Kanisa la Mwenyezi Mungu
Kuna aina mbili tu za hali ambapo roho waovu humdanganya mwanadamu: Moja ni kazi isiyo ya kawaida ya roho waovu, na nyingine ni roho waovu waliopata mwili tena kama binadamu. Wale wanaopinga Mungu na ukweli kama vile pepo ambaye ni joka kuu jekundu pia ni roho waovu; wao ni wenye kudhuru kwa siri zaidi, wenye nia mbaya zaidi. Baadhi ya roho waovu hutawala miili ya watu wakati fulani katika maisha yao; roho wengine waovu ni kupata mwili tena kwa pepo. Ingawa kwa nje hakuna kazi isiyo ya kawaida ya roho waovu na huwezi kuona dalili yoyote ya umiliki na pepo, wao hupinga ukweli kwa mhemko; wao humkataa na kumpinga Mungu kwa hasira. Pepo waliopata mwili tena si wa mwujiza, bali ni wa kawaida. Hata hivyo, ni dhahiri shahiri kuwa wao ni adui wa ukweli. Joka kubwa jekundu ni la kundi la pepo waliopata mwili tena, na wanasiasa wote na wakuu wa nchi wanaompinga Mungu pia ni pepo waliozaliwa tena. Kusema kwamba wale tu ambao wana kazi ya roho waovu wamepagawa na pepo na wao wenyewe ni pepo waovu hakukubaliani na uhalisi. Baadhi ya roho waovu hujificha ndani zaidi na huwezi kuwatambua; wao ni wa kundi la pepo waliopata mwili tena.
kutoka katika “Maswali na majibu” katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha VIII

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni