Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi ya Roho Mtakatifu. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Kazi ya Roho Mtakatifu. Onyesha machapisho yote

11.30.2019

Kuna tofauti zipi kati ya mabadiliko ya tabia na tabia nzuri?

Maneno Husika ya Mungu:

Mabadiliko katika tabia hasa huhusu mabadiliko katika asili ya watu. Mambo ya asili ya mtu hayawezi kuonekana kutoka kwa mienendo ya nje; yanahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuwepo kwao. Yanahusisha moja kwa moja maadili ya mtu katika maisha, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi yake, na kiini chake.

11.28.2019

Mabadiliko ya tabia hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:

Ikiwa tabia yako inaweza kubadilika au la inategemea na ikiwa unaweza kuendelea na maneno halisi ya Roho Mtakatifu au la na una ufahamu wa kweli. Hili ni tofauti na kile mlichoelewa awali. Kile ulichoelewa kuhusu mabadiliko katika tabia awali kilikuwa kwamba wewe, ambaye ni rahisi kuhukumu, kupitia kwa kufundishwa nidhamu na Mungu huzungumzi ovyo ovyo tena. Lakini hii ni hali moja tu ya mabadiliko, na hivi sasa suala muhimu zaidi ni kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu.