Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ukweli na Mafundisho ya Dini. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Ukweli na Mafundisho ya Dini. Onyesha machapisho yote

11.30.2019

Kuna tofauti zipi kati ya mabadiliko ya tabia na tabia nzuri?

Maneno Husika ya Mungu:

Mabadiliko katika tabia hasa huhusu mabadiliko katika asili ya watu. Mambo ya asili ya mtu hayawezi kuonekana kutoka kwa mienendo ya nje; yanahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuwepo kwao. Yanahusisha moja kwa moja maadili ya mtu katika maisha, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi yake, na kiini chake.