Maneno Husika ya Mungu:
Mabadiliko katika tabia hasa huhusu mabadiliko katika asili ya watu. Mambo ya asili ya mtu hayawezi kuonekana kutoka kwa mienendo ya nje; yanahusisha moja kwa moja thamani na umuhimu wa kuwepo kwao. Yanahusisha moja kwa moja maadili ya mtu katika maisha, mambo yaliyo ndani kabisa ya nafsi yake, na kiini chake.
Mtu ambaye hawezi kukubali ukweli hatakuwa na mabadiliko katika hali hizi.Ni kwa kupitia kazi ya Mungu pekee, kuingia kikamilifu katika ukweli, kubadili maadili na mitazamo yake kuhusu kuwepo na maisha, kulinganisha msoni yake na ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zake zinaweza kusemekana zimebadilika. Huenda ukaonekana kufanya juhudi fulani, unaweza ukawa thabiti unapokabiliwa na shida, huenda ukaweza kutekeleza utaratibu wa kazi kutoka walio juu, au huenda ukaweza kwenda popote unapoambiwa kwenda, lakini haya ni mabadiliko madogo tu katika mienendo yako, na hayatoshi kujumuisha mabadiliko katika tabia yako. Huenda ukaweza kukimbia katika njia nyingi, kuvumilia shida nyingi na kustahamili fedheha kuu; huenda ukajihisi karibu sana na Mungu, na Roho Mtakatifu anaweza kukufanyia kazi fulani. Hata hivyo, Mungu anapokuomba ufanye jambo fulani ambalo halipatani na fikira zako, huenda bado usitii, lakini utafute visababu, na kuasi na kumpinga Mungu, hata kufikia kiwango cha wewe kumhakiki Mungu na kumpinga Yeye. Hili ni tatizo kubwa! Hili linaonyesha kwamba bado una asili inayompinga Mungu na kwamba hujapitia mabadiliko yoyote kabisa.
Mtu ambaye hawezi kukubali ukweli hatakuwa na mabadiliko katika hali hizi.Ni kwa kupitia kazi ya Mungu pekee, kuingia kikamilifu katika ukweli, kubadili maadili na mitazamo yake kuhusu kuwepo na maisha, kulinganisha msoni yake na ya Mungu, na kuwa na uwezo wa kutii na kujitoa kabisa kwa Mungu ndio tabia zake zinaweza kusemekana zimebadilika. Huenda ukaonekana kufanya juhudi fulani, unaweza ukawa thabiti unapokabiliwa na shida, huenda ukaweza kutekeleza utaratibu wa kazi kutoka walio juu, au huenda ukaweza kwenda popote unapoambiwa kwenda, lakini haya ni mabadiliko madogo tu katika mienendo yako, na hayatoshi kujumuisha mabadiliko katika tabia yako. Huenda ukaweza kukimbia katika njia nyingi, kuvumilia shida nyingi na kustahamili fedheha kuu; huenda ukajihisi karibu sana na Mungu, na Roho Mtakatifu anaweza kukufanyia kazi fulani. Hata hivyo, Mungu anapokuomba ufanye jambo fulani ambalo halipatani na fikira zako, huenda bado usitii, lakini utafute visababu, na kuasi na kumpinga Mungu, hata kufikia kiwango cha wewe kumhakiki Mungu na kumpinga Yeye. Hili ni tatizo kubwa! Hili linaonyesha kwamba bado una asili inayompinga Mungu na kwamba hujapitia mabadiliko yoyote kabisa.
kutoka katika “Unachopaswa Kujua Kuhusu Kuigeuza Tabia Yako” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Mnafahamu nini kuhusu mabadiliko katika tabia? Asili za mabadiliko katika tabia na mabadiliko katika mwenendo ni tofauti, na mabadiliko katika matendo pia ni tofauti—yote ni tofauti kwa asili. Watu wengi wanaweka mkazo maalum kwa tabia katika imani yao kwa Mungu, hivyo mabadiliko yanatokea katika mienendo yao. Baada ya kumwamini Mungu, wanakoma kubishana na wengine, wanakoma kupigana na watu na kuwatukana, wanakoma kuvuta sigara na kunywa pombe, hawaibi mali yoyote ya umma—hata iwe msumari ama kipande cha mbao—nao hawathubutu kuwashitaki watu wanapopata hasara ama wakikosewa. Bila shaka, baadhi ya mabadiliko yanatokea katika mienendo yao. Kwa sababu, baada ya kumwamini Mungu, kuikubali njia ya kweli kunawafanya kuhisi vizuri zaidi, na kwa sababu pia wameionja neema ya kazi ya Roho Mtakatifu, wanakuwa na bidii hasa, na hata hakuna kitu chochote ambacho hawawezi kutelekeza ama kufanya. Ilhali baada ya kuamini kwa miaka mitatu, mitano, kumi ama thelathini—kwa sababu hakujakuwa na mabadiliko katika tabia ya maisha yao, mwishowe wanarudia njia zao mbaya za awali, kiburi na majivuno yao vinakua, nao wanaanza kugombania mamlaka na faida, wanatamani pesa za kanisa, wanafanya chochote kwa maslahi yao, wanatamani vyeo na starehe, nao wanakuwa wanyonyaji wa nyumba ya Mungu. Viongozi wengi, hasa, wameachwa. Na ukweli huu unathibitisha nini? Mabadiliko katika tabia tu hayawezi kudumu. Kama hakuna mabadiliko katika tabia ya maisha ya watu, basi siku moja upande wao wa uovu utajionyesha. Kwa sababu kiini cha mabadiliko katika mienendo yao ni bidii, pamoja na kazi ya Roho Mtakatifu wakati huo, ni rahisi sana kwao kuwa na bidii, ama kuonyesha ukarimu kwa muda. Kama wasioamini wanavyosema, “kufanya tendo moja zuri ni rahisi, kilicho kigumu ni kufanya matendo mazuri maishani.” Watu hawana uwezo wa kufanya matendo mazuri katika maisha yao yote. Mienendo yao inaongozwa na maisha hayo; maisha yao yalivyo, ndivyo mwenendo wao ulivyo, na kile tu kinachofichuliwa kwa asili kinawakilisha maisha hayo, na asili ya mtu. Vitu vilivyo vya bandia haviwezi kudumu. Mungu anapofanya kazi ili kumwokoa mwanadamu, si kwa ajili ya kumpamba mwanadamu kwa mwenendo mzuri—kazi ya Mungu ni kwa ajili ya kubadilisha tabia za watu, kuwafanya wazaliwe na kuwa watu wapya. Hivyo, hukumu ya Mungu, kuadibu, majaribu, na usafishaji wa mwanadamu vyote ni kwa ajili ya kuibadilisha tabia yake, ili aweze kutimiza utii na uaminifu kamili kwa Mungu, na kumwabudu Mungu kwa kawaida. Hili ndilo lengo la kazi ya Mungu. Kuwa na tabia nzuri si sawa na kumtii Mungu, hasa si sawa na kulingana na Kristo. Mabadiliko katika tabia yanategemea mafundisho, na kuzaliwa na juhudi—hayategemei maarifa ya kweli kumhusu Mungu, ama juu ya ukweli, hasa hayategemei uongozi wa Roho Mtakatifu. Ingawa kuna nyakati ambapo baadhi ya yale watu wanayofanya yanaongozwa na Roho Mtakatifu, haya si maonyesho ya maisha, sembuse kuwa sawa na kumjua Mungu; haijalishi mienendo ya mtu ni mizuri kiasi gani, haithibitishi kwamba anamtii Mungu, ama kwamba anauweka ukweli katika matendo. Mabadiliko ya tabia ni udanganyifu wa muda, ni udhihirisho wa bidii, nayo si maonyesho ya maisha hayo. …
Watu wanaweza kuwa na tabia nzuri, lakini hiyo haimaanishi kuwa wako na ukweli. Bidii ya watu inaweza tu kuwafanya wazingatie mafundisho na kufuata kanuni; watu wasio na ukweli hawana namna ya kutatua shida halisi, na mafundisho hayawezi kushikilia nafasi ya ukweli. Wale ambao wamepitia mabadiliko katika tabia zao ni tofauti. Wana ukweli ndani yao, wanatambua masuala yote, wanajua jinsi ya kutenda kulingana na mapenzi ya Mungu, jinsi ya kutenda kulingana na kanuni za ukweli, jinsi ya kutenda ili kumridhisha Mungu, nao wanaelewa asili ya upotovu wanaoufichua. Mawazo na dhana zao wenyewe vinapofichuliwa, wanaweza kutambua na kuunyima mwili. Hivi ndivyo mabadiliko katika tabia yanavyoonyeshwa. Kitu cha muhimu kuhusu mabadiliko katika tabia ni kwamba yana ukweli na uwazi, na unapotekeleza mambo, yanauweka ukweli katika matendo kwa usahihi wa karibu na upotovu wao hauonekani mara nyingi.
kutoka katika “Tofauti Kati ya Mabadiliko ya Nje na Mabadiliko katika Tabia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Wale wasio na ukweli hawajakuwa na mabadiliko katika tabia hata kidogo. Hiyo si kusema kwamba mtu aliyekomaa katika ubinadamu wake lazima atakuwa na mabadiliko katika tabia; labda hufanyika wakati baadhi ya sumu za kishetani katika asili ya mtu zinabadilika kwa sababu ya maarifa yao kuhusu Mungu na ufahamu wao wa ukweli. Hiyo ni kusema, sumu hizo zinatakaswa na ukweli unaoonyeshwa na Mungu unaanza kustawi ndani ya mtu huyo, unakuwa maisha yake, nao unakuwa msingi wa kuwepo kwake. Hapo tu ndipo anakuwa mtu mpya, na hivyo tabia yake inabadilika. Hivi si kusema kwamba tabia yake ya nje ni ya upole kuliko hapo awali, kuwa alikuwa na kiburi lakini sasa maneno yake ni ya busara, kwamba hakuwa anamsikiza mtu yeyote lakini sasa anaweza kuwasikiza wengine—mabadiliko haya ya nje hayawezi kusemwa kuwa ni mabadiliko katika tabia. Bila shaka mabadiliko katika tabia yanajumuisha hali hizi, lakini jambo lililo muhimu zaidi ni kuwa maisha yake ya ndani yamebadilika. Ukweli unaoonyeshwa na Mungu unakuwa maisha yake hasa, baadhi ya sumu za kishetani zilizo ndani zimetolewa, mtazamo wa mtu huyo umebadilika kabisa, na hakuna chochote kati ya hali hizo kinachokubaliana yale ya dunia. Anaona waziwazi njama na sumu za joka kubwa jekundu; amefahamu kiini cha kweli cha maisha. Kwa hivyo maadili ya maisha yake yamebadilika—hili ndilo badiliko la muhimu zaidi na kiini cha mabadiliko katika tabia.
Watu waliishi awali kwa msingi gani? Watu wote wanaishi kwa ajili yao wenyewe. Kila mtu na wake—hii ndiyo jumla ya asili ya mwanadamu. Kumwamini Mungu kunafanywa kwa ajili ya mtu binafsi, na kupata baraka ni hivyo hata zaidi. Kutelekeza mambo, kujitumia kwa ajili ya Mungu, na kuwa mwaminifu kwa Mungu—haya yote yanafanywa kwa ajili ya mtu binafsi. Kwa jumla, yote ni kwa ajili ya kujipatia baraka. Katika dunia, kila kitu ni kwa ajili ya faida ya kibinafsi. Kumwamini Mungu ni kwa ajili ya kupata baraka, nako ni kwa ajili ya kupata baraka ndipo mtu huacha kila kitu, na mtu anaweza kustahimili mateso mengi ili apate baraka. Haya yote ni ushahidi wa kutegemea nadharia wa asili ya upotovu ya mwanadamu. Hata hivyo, wale walio na mabadiliko katika tabia wako tofauti. Wanahisi kwamba watu wanafaa kuishi ili kumridhisha Mungu, kutimiza wajibu wao vizuri, na kuishi maisha yenye maana, ili hata watakapokufa, watahisi kuridhika na hawatakuwa na majuto yoyote—hawatakuwa wameishi bure. Kwamba watu wanaweza kumwabudu, kumtii na kumridhisha Mungu ni msingi wa kuwa mtu na huu ndio wajibu wao kulingana na kanuni zisizobadilika za mbinguni na dunia. Vinginevyo, hawangestahili kuitwa binadamu; maisha yao yangekuwa matupu na yasiyo na maana. Kutokana na kufananisha hali hizi mbili, tunaona kuwa ile ya mwisho ni mtu ambaye tabia yake imebadilika, na kwa sababu tabia ya maisha yake ilibadilika, bila shaka mtazamo wa maisha umebadilika. Akiwa na maadili tofauti, hatawahi tena kuishi kwa ajili yake mwenyewe, na imani yake kwa Mungu haitawahi tena kuwa kwa ajili ya kujipatia baraka. Ataweza kusema, “Baada ya kumjua Mungu, kifo ni nini kwangu? Kumjua Mungu kumenifanya niishi maisha yaliyo na maana. Sijaishi bure na sitakufa nikiwa na majuto—sina malalamishi.” Je, huu si mtazamo uliobadilika wa maisha? Kwa hiyo, chanzo kikuu cha mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu ni kuwa na ukweli kwa ndani, na kuwa na maarifa kuhusu Mungu; mtazamo wa mtu wa maisha unabadilika, na maadili ni tofauti na awali. Mabadiliko yanaanza kutoka ndani, na kutoka kwa maisha ya mtu; kwa kweli si tu mabadiliko ya nje. Baadhi ya waumini wapya, baada ya kumwamini Mungu, wameiacha dunia ya kilimwengu; wanapokumbana na wasioamini wana machache ya kusema, na ni vigumu sana kwao kuwasiliana na jamaa na marafiki wao wasioamini. Wasioamini wanasema, “Mtu huyu amebadilika.” Kwa hiyo anafikiria, “Tabia yangu imebadilika kweli—wasioamini wanasema nimebadilika.” Kwa kweli, tabia yake imebadilika kweli? Haya ni mabadiliko ya nje tu. Hakujakuwa na mabadiliko katika maisha yake, na asili yake ya kishetani inabaki imara ndani yake, haijaguswa hata kidogo. Wakati mwingine, watu wanashikwa na ari kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu; baadhi ya mabadiliko ya nje yanatokea, nao wanatenda vitendo vizuri vichache. Lakini hii si sawa na mabadiliko katika tabia. Huna ukweli, mtazamo wako kuhusu mambo haujabadilika, hata hauko tofauti na ule wa wasioamini, na maadili na mtazamo wako kuhusu maisha havijabadilika. Hata huna moyo unaomcha Mungu, ambao angalau unafaa kuwa nao. Hakuna kitu ambacho kinaweza kuwa mbali na mabadiliko katika tabia yako.
kutoka katika “Tofauti Kati ya Mabadiliko ya Nje na Mabadiliko katika Tabia” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Madondoo ya Mahubiri na Ushirika kwa ajili ya Marejeo:
Katika ulimwengu wa kidini, kuna wacha Mungu wengi, wao husema, “Tumebadilika kwa sababu ya imani yetu katika Bwana Yesu. Tunaweza kujitahidi kwa ajili ya Bwana, kutenda kazi, kuvumilia gerezani kwa ajili ya Bwana, na hatulikatai jina Lake mbele yawengine. Tunaweza kuyatenda mambo mengi mema, kufadhili, kuchanga na kuwasaidia maskini. Haya ni mabadilikomakubwa! Tumebadilika, ndiyo sababu tunafaa kumngojea Bwana ili atulete katika ufalme wa mbinguni.” Je, mnafikiria nini juu ya maneno haya? Je, mna ufahamu wowote ijapo kwa maneno haya? Je, kutakaswa kunamaanisha nini? Je, unafikiria kwamba kama tabia yako imebadilika na unatenda matendo mema basi umetakaswa? Mtu mwingine husema, “Nimeacha kila kitu.” Hata Nimeiacha kazi yangu ulimwenguni, familia yangu na tamaa za mwili ili kujitahidi kwa ajili ya Mungu. Je, hii ni sawa na kutakaswa? Ingawa umeyatenda haya yote, huu si ushahidi thabiti kwamba umetakaswa. Hivyo, jambo muhimu ni lipi? Je, ni katika kipengele kipi unaweza kupata kutakaswa kunakoweza kuchukuliwa kama kutakaswa halisi? Kutakaswa kwa tabia ya kishetani ambayo humpinga Mungu. Sasa, udhihirisho wa tabia ya kishetani ambao humpinga Mungu ni upi? Je, udhihirisho ulio wazi zaidi ni upi? Kiburi cha mtu, majivuno, haki ya kibinafsi, na kujidai mwenyewe, pamoja na upotovu, hila, kusema uongo, udanganyifu na unafiki. Wakati mambo haya si sehemu ya mtu tena, basi kwa kweli ametakaswa. Kuna madhihirisho 12. Acheni tulitazame kila mojawapo ya haya madhihirisho 12: mtu mwenyewe kujiona kuwa mwenye kuheshimika zaidi; kuwaruhusu wale ambao hunitiiMimi kustawi na wale ambao hunipinga Mimikuangamia; kufikiria tu kuwa Mungu ndiye mkuu zaidi kukushinda, kutomnyenyekea mtuyeyote, kutowajali wengine; kufanyiza ufalme wa kibinafsi mara tu unapokuwa na uwezo; kutaka kuwa mtawala wa pekee na mjua yote na kuyaamua mambo wewe mwenyewe. Huu udhihirisho wote ni tabia za kishetani. Tabia hizi za kishetani lazima zitakaswe kabla ya mtu kuyapitia mabadiliko katika tabia ya maisha yake. Mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu ni kuzaliwa upya kwa sababu kiini chake kimebadilika. Awali, wakati alipopewa uwezo, aliweza kuunda ufalme wa kibinafsi. Sasa, wakati anapopewa uwezo, yeye humhudumia Mungu, humshuhudia Mungu na huwa mtumishi wa wateule wa Mungu. Je, haya siyo mabadiliko halisi? Awali, aliringa mwenyewe katika hali zote na aliwataka watu wengine wamheshimu na kumwabudu. Sasa, yeye humshuhudia Mungu kila mahali, hajishughulishi tena. Bila kujali wanavyonishughulikia watu, ni vyema. Bila kujali watu wanasema nini juu yangu, ni vyema. Sijali. Ninataka tu kumtukuza sana Mungu, kumshuhudia Mungu, kuwasaidia wengine wapate ufahamu wa Mungu, na kuwasaidia wengine watii mbele za uwepo wa Mungu. Je, haya si mabadiliko katika tabia ya maisha? “Nitawashughulikia ndugu kwa upendo. Nitawahurumia wengine katika hali zote. Katika mambo yote, sitajifikiria, nitawafikiria tu wengine. Nitawasaidia wengine kuyastawisha maisha yao na kuyatimiza majukumu yangu. Nitawasaidia wengine kuupata ukweli na kuufahamu ukweli. Hii ndio maana ya kuwapenda watu, kuwapenda wengine kama mwenyewe! Kumhusu Shetani, unaweza kumtambua, kuwa na kanuni, kuwa na mipaka naye na kuyafunua maovu ya Shetani kabisa ili wateule wa Mungu wasipatwe na madhara yake. Huku ni kuwalinda wateule wa Mungu, na huku ni kuwapenda wengine zaidi kama mwenyewe. Zaidi ya hayo, unapaswa kukipenda ambacho Mungu hukipenda na kukichukia ambacho Mungu hukichukia. Je, basi, Mungu hukichukia nini? Yeye huwachukia wapinga Kristo, pepo waovu, na watu waovu. Hilo linamaanisha kuwa sisi pia tunapaswa kuwachukia wapinga Kristo, pepo waovu na watu waovu. Lazima tusimame upande wa Mungu. Hatuwezi kupatana nao. Mungu huwapenda wale ambao Yeye hutaka kuwaokoa na kuwabariki. Kuhusu watu hawa, lazima tuwajibike, tuwashughulikie kwa upendo, tuwasaidie, tuwaelekeze, tuwakimu na kuwahimili wao. Je, haya si mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu? Zaidi ya hayo, wakati umetenda dhambi au makosa fulani, au umetelekeza kanuni katika kulitenda jambo fulani, unaweza kukubali ukosoaji wa ndugu, kukaripia, kushughulikia na kupogoa; unaweza kuyapokea mambo haya yote kutoka kwa Mungu, usiwe na kinyongo, na uutafute ukweli ili kuusuluhisha upotovu wako. Je, haya si mabadiliko katika tabia yako ya maisha? Ndio, ni mabadiliko. …
Je, mabadiliko katika mwenendo ambao unazungumziwa katika ulimwengu wa kidini huwakilisha mabadiliko katika tabia ya maisha? (Hapana, hauwezi.) Kwa nini mabadiliko katika mwenendo wa mtu hayawezi kuwakilisha mabadiliko katika tabia yake ya maisha? Sababu muhimu ni kuwa bado anampinga Mungu. Unaweza kuyaona hayo kwa nje, Mafarisayo walikuwa wacha Mungu sana, waliomba, waliyaelezea maandiko na walizifuata kanuni za sheria vizuri sana. Ingeweza kusemwa kwamba kwa nje, hawakufedheheka. Watu hawakuweza kuyaona makosa. Hata hivyo, kwa nini bado waliweza kumpinga na kumshutumu Kristo? Je, hili linaonyesha nini? Hawakuwa na ukweli na hawakumjua Mungu. Kwa nje, walikuwa wazuri sana, lakini hawakuwa na ukweli, hii ndiyo sababu waliweza kumpimga Mungu. Kama walikuwa wazuri sana kwa nje, kwa nini hili halichukuliwi kama mabadiliko katika tabia ya maisha? Hii ni kwa sababu bado walikuwa wenye kiburi, wenye majivuno na hasa wenye unyoofu. Waliyaamini maarifa yao, nadharia na ufahamu wa maandiko. Waliamini kwamba walifahamu kila kitu na kwamba walikuwa bora kuliko watu wengine. Hii ndiyo sababu wakati ulimwengu wa kidini unasikia kwamba Kristo wa siku za mwisho ameuelezea ukweli wote, wanamshutumu Yeye ingawa wanajua kwamba ni ukweli.
kutoka katika Mahubiri na Ushirika Kuhusu Kuingia Katika Maisha, Juzuu ya 138
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni