12.18.2019

Mungu huwaokoa watu gani? Yeye huwaondosha watu gani?

Maneno Husika ya Mungu:


Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa.

kutoka katika “Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Walio hai ni wale ambao roho zao zimezaliwa upya, wale wanaojua kumtii Mungu, na ambao ni watii kwa Mungu. Wanao ukweli, na ushuhuda, na ni watu wa aina hii tu ndio wanaompendeza Mungu katika nyumba Yake. Mungu anawaokoa wale ambao wanaweza kuwa hai tena, ambao wanaweza kuuona wokovu wa Mungu, ambao wanaweza kuwa watii kwa Mungu, na wapo tayari kumtafuta Mungu. Anawaokoa wanaomwamini Mungu aliyepata mwili, na wanaamini katika kuonekana Kwake. Baadhi ya watu wanaweza kuwa hai tena, na baadhi hawawezi; inategemea na asili yao kama inaweza kuokolewa au la. Watu wengi wamesikia sana kuhusu maneno ya Mungu lakini bado hawaelewi mapenzi ya Mungu, wameyasikia maneno mengi sana ya Mungu lakini bado hawawezi kuyaweka katika vitendo, hawawezi kuishi kwa kudhihirisha ukweli wowote na pia kwa kukusudia kabisa wanaingilia kazi ya Mungu. Hawawezi kufanya kazi yoyote kwa ajili ya Mungu, hawawezi kujitolea chochote Kwake, na pia wanatumia kwa siri pesa za kanisa, na kula katika nyumba ya Mungu bure. Watu hawa ni wafu, na hawataokolewa. Mungu anawaokoa wale ambao wapo katika kazi Yake. Lakini kuna sehemu ya watu hao ambao hawawezi kupokea wokovu Wake; ni idadi ndogo tu ndiyo inaweza kupokea wokovu Wake, maana watu wengi ni wafu sana, ni wafu sana kiasi kwamba hawawezi kuokolewa, wameharibiwa kabisa na Shetani, na kwa asili, wamekuwa hatari sana. Wala idadi ndogo hiyo ya watu haikuweza kumtii Mungu kikamilifu. Hawakuwa wale ambao walikuwa waaminifu kabisa kwa Mungu tangu mwanzo, au wale ambao walikuwa na upendo wa hali ya juu kabisa kwa Mungu toka mwanzo; badala yake, wamekuwa watiifu kwa Mungu kwa sababu ya kazi Yake ya ushindi, wanamwona Mungu kwa sababu ya upendo wake mkuu, kuna mabadiliko katika tabia zao kwa sababu ya tabia ya Mungu ya haki, na wanamjua Mungu kwa sababu ya kazi Yake, ambayo ni halisi na ya kawaida.

kutoka katika “Je, Umekuwa Hai Tena?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Mungu siku zote amewakamilisha wote wanaomhudumia. Hawatupilii mbali kwa urahisi tu. Kama tu utakubali kwa kweli hukumu na kuadibu kwa neno la Mungu, kama unaweza kuweka pembeni matendo yako na sheria za kidini za kale, na kukoma kutumia fikira za kale za kidini kama kipimo cha neno la Mungu hii leo, ni hapo tu ndipo kutakuwa na mustakabali kwako. Lakini kama utashikilia vitu vya kale, kama bado unavithamini, basi huwezi kupata wokovu. Mungu hawatambui watu kama hao.

kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini Lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale wanaomwamini Mungu kwa kweli ni wale walio tayari kuweka neno la Mungu kwenye matendo, na ni wale walio radhi kutenda ukweli. Wale wanaoweza kwa kweli kuwa shahidi kwa Mungu pia ni wale walio radhi kuweka neno Lake kwenye matendo, na ni wale ambao kwa kweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wanaotumia hila na wale wanaotenda yasio haki wote ni watu wasiokuwa na ukweli na wote huleta aibu kwa Mungu. Wale walio kanisani wanaohusika na mabishano ni vibaraka wa Shetani, na ni mfano mwema wa Shetani. Mtu wa aina hii ni mwovu sana. Wale wasio na ufahamu na wasio na uwezo wa kusimama upande wa ukweli wanahifadhi nia mbovu na kufifisha ukweli. Watu hawa hata zaidi ni waakilishi kamili wa Shetani; wamepita hali ya ukombozi na ni wazi mno kuwa wao wote ni vitu vya kuondolewa. Wale wasiotenda ukweli hawapaswi kuruhusiwa kusalia katika familia ya Mungu, wala wale wanaobomoa kanisa kwa makusudi. Lakini sasa Sifanyi kazi ya kufukuza. Watafichuliwa tu na kuondolewa mwishoni. Hakuna kazi nyingine ya bure itakayofanywa kwa watu hawa; wale walio wa Shetani hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, ilhali wale wanaotafuta ukweli wanaweza kusimama upande wa ukweli. Wale wasiotenda ukweli hawastahili kusikia njia ya kweli na hawastahili kuwa na ushuhuda kwa ukweli. Kimsingi ukweli si kwa ajili ya masikio yao lakini badala yake unazungumzwa kwa ajili ya masikio ya wale wanaoutenda. Kabla ya mwisho wa kila mtu kufichuliwa, wale wanaovuruga kanisa na kukatiza kazi kwanza wataachwa upande moja. Pindi kazi itakapokamilika, watu hawa watafunuliwa mmoja baada ya mwingine kabla ya kuondolewa. Wakati wa kutoa ukweli, Siwatilii maanani kwa sasa. Ukweli wote unapofichuliwa kwa mwanadamu watu hao wanapasa kuondolewa, kwa kuwa huo pia utakuwa wakati ambapo watu wataainishwa kulingana na aina yao. Kwa sababu ya werevu wao mdogo, wale wasio na ufahamu watakuja kuangamia mikononi mwa watu waovu na watapotoshwa na watu waovu na watashindwa kurudi. Watu hawa wanapasa kushughulikiwa kwa njia hii, kwa kuwa hawaupendi ukweli, kwa sababu hawana uwezo wa kusimama upande wa ukweli, kwa sababu wanawafuata watu waovu, wanawaunga mkono watu waovu, na kwa sababu wanashirikiana na watu waovu na kumuasi Mungu. Wanajua vema kuwa watu hao waovu wananururisha uovu lakini wanafanya mioyo yao kuwa migumu na kuwafuata, wakienda kinyume na ukweli. Je, watu hawa wasiotenda ukweli lakini wanaofanya mambo ya uharibifu na ya chukizo wote si wanafanya maovu? Ingawa kuna wale miongoni mwao ambao wanajipa mtindo wenyewe kama “wafalme” na wale wanaofuata msururu nyuma yao, je, asili yao ya kuasi Mungu si ni sawa yote? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu hawaokoi? Je, wanaweza kutoa sababu gani kuwa Mungu si mwenye haki? Je, si ni uovu wao wenyewe ambao umewaangamiza? Je, si ni uasi wao ambao utawavuta hadi jahanamu? Wale wanaotenda ukweli mwishowe wataokolewa na kufanywa wakamilifu kwa kupitia ukweli. Wale wasiotenda ukweli mwishowe watakaribisha maangamizi kwa kupitia ukweli. Hii ndio miisho inayowasubiri wale wanaotenda ukweli na wale wasioutenda.

kutoka katika “Onyo kwa Wale Wasiotenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Natazama kutoka kwenye kiti cha enzi. Naangalia kwa kina ndani ya mioyo ya watu. Naokoa wale ambao wana hamu na Mimi kwa bidii, na Ninawaonea huruma. Nitawaokoa katika umilele wanaonipenda mioyoni mwao zaidi ya mengine yote, wale ambao wanaelewa mapenzi Yangu, na wanaonifuata hadi mwisho wa njia! Mkono Wangu utawashikilia kwa usalama ili wasikabiliwe na tukio hili na wasikutane na madhara.

kutoka katika “Sura ya 35” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Baadhi hutenda kwa ustaarabu na huonekana hasa “wenye tabia nzuri” mbele ya Mungu, na bado wanakuwa waasi na wasiozuiliwa mbele ya Roho Mtakatifu. Je, mnaweza kumhesabu binadamu kama huyu miongoni mwa safu ya waaminifu? Kama wewe ni mnafiki na mmoja ambaye ni stadi katika kutangamana, basi Nasema kwamba bila shaka wewe ni mmoja ambaye humchezea Mungu. Kama maneno yako yamejaa visingizio na udhibitisho usio na thamani, basi Nasema kwamba wewe ndiwe ambaye huko radhi kabisa kuweka ukweli katika matendo. Kama wewe una siri nyingi usizotaka kutoa, na kama huko radhi kabisa kuweka wazi siri zako—yaani, ugumu wako—kwa wengine ili uweze kutafuta njia ya mwangaza, basi Ninasema kwamba wewe ni mmoja ambaye hatapokea wokovu kwa urahisi na ambaye hataweza kuibuka kutoka gizani kwa urahisi. Kama kutafuta njia ya ukweli kunakufurahisha vyema, basi wewe ni yule anayeishi kila mara katika mwangaza. Kama wewe unafurahia kuwa mtoa huduma katika nyumba ya Mungu, ukifanya kazi kwa bidii na kwa makini bila kuonekana, siku zote ukitoa na katu hupokei, basi Nasema kwamba wewe ni mtakatifu mwaminifu, kwani hutafuti tuzo na unakuwa tu binadamu mwaminifu. Kama uko radhi kuwa wazi, kama uko radhi kutoa kila kitu ulichonacho, kama una uwezo wa kujitolea maisha yako kwa ajili ya Mungu na kuwa shahidi, kama wewe ni mwaminifu hadi kwa kiwango ambapo unajua tu kumridhisha Mungu na si kujifikiria au kuchukua chochote kwa ajili yako, basi Nasema kwamba watu kama hao ndio wanaostawishwa na mwangaza na wataishi milele katika ufalme.

kutoka katika “Maonyo Matatu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu wengine wanaondoka wakati kitu kilicho kibaya kinawafikia, na wanashindwa kusimama baada ya kila pingamizi. Watu hawa wote ni wapumbavu ambao hawapendi ukweli, na watakosa kupata ukweli hata wakiishi maisha yao yote kwa imani. Watu wapumbavu kama hao watawezaje kufuata hadi mwisho? Watu werevu na wale ambao kwa kweli wana ubora wa ndani na wanaelewa masuala ya kiroho ni watafutaji wa ukweli, na mara nane kwa kumi pengine wanaweza kupata ufunuo kiasi, funzo, kupata nuru na maendeleo. Kitu kama hicho kinapofanyika kwa mpumbavu asiyeelewa masuala ya kiroho, mara kumi, hatapata faida yoyote ya maisha hata mara moja, hatafanya mabadiliko hata mara moja na hataelewa asili yake hata mara moja. Anaanguka mara kumi, anajikwaa mara kumi, lakini bado hazinduki wala hatafuti ukweli kutafuta kiini cha shida. Bila kujali jinsi mtu wa aina hii huenda akasikiza mahubiri, hatawahi kuelewa ukweli—ameshindwa tu. Kila wakati anapojikwaa anahitaji mtu mwingine kumsaidia kusimama tena, kumbembeleza. Asipobembelezwa au kusaidiwa, hatainuka tena kabisa. Kila wakati kinapofanyika, kuna hatari ya kuanguka, na kila wakati kuna hatari ya yeye kudhoofika. Je, huu sio mwisho kwake? Je, bado kuna sababu zozote kwa watu hawa wasio na manufaa kuokolewa? Wokovu wa Mungu kwa binadamu ni wokovu kwa wale wanaopenda ukweli. Ni wokovu kwa wale wenye dhamira na azimio, wale wanaotamani ukweli na haki. Kusema mtu ana azimio kunamaanisha kuwa anataka sana haki, uzuri na ukweli, na kuwa ana dhamiri. Mungu hufanya kazi ndani ya watu hawa ili waweze kuelewa na kupata ukweli, ili upotovu wao uweze kutakaswa na tabia ya maisha yao iweze kubadilishwa. Ikiwa ndani yako hakuna upendo wa ukweli ama hamu ya haki na mwanga, basi wakati wowote unapokumbana na uovu, hutakuwa na hiari ya kutupa mbali vitu viovu ama azimio la kupitia shida, na kama dhamiri yako ni yenye ganzi, welekevu wako wa kupokea ukweli pia ni wenye ganzi, huko makini kwa ukweli ama vitu vinavyofanyika, huwezi kutofautisha chochote, na huna uwezo wa kushughulikia ama kutatua mambo, basi hakuna njia ya kuokolewa. Mtu wa haina hii hana chochote cha kumpendekeza, hana chochote cha thamani cha kufanya kazi nacho. Hajibu bila kujali jinsi Mungu Anavyonena kwa wazi ama kwa dhahiri kuhusu ukweli, kana kwamba amekufa tayari. Je, haijafika mwisho kwake? Yeyote aliye na pumzi anaweza kuokolewa kwa upumuaji bandia. Lakini kama amekufa tayari na roho yake imeondoka, basi upumuaji bandia hautafanya lolote. Kitu kinapokufika, unanywea, na huwi na ushuhuda wowote, kwa hivyo huwezi kuokolewa kamwe na utakuwa umefika mwisho.

kutoka katika “Watu Waliochanganyikiwa Hawawezi Kuokolewa” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Wanadamu kama hawa hawaelewi kazi mpya lakini wamejawa na fikira zisizokoma. Hawafanyi chochote kanisani; badala yake, wanachochea na kusambaza uhasi kila pahali, hata kushiriki katika kila namna ya utovu wa nidhamu na vurugu kanisani, na hivyo kuwarusha wale wasiobagua katika vurugu na machafuko. Haya ibilisi wanaoishi, hawa mapepo mabaya wanapaswa kuondoka kanisani haraka iwezekanavyo, kanisa lisije likaharibiwa kwa sababu yako. Labda huogopi kazi ya leo, lakini huogopi adhabu ya haki ya kesho? Kuna idadi kubwa ya watu kanisani ambao ni vimelea, na pia kuna idadi kubwa ya mbwa mwitu wanaotafuta kuvuruga kazi ya kawaida ya Mungu. Vitu hivi vyote ni mapepo yaliyotumwa na Ibilisi, ni mbwa mwitu wakali wanaotafuta kuwala kondoo wasio na hatia. Iwapo wanadamu kama hawa hawatafukuzwa, basi wanakuwa vimelea kwa kanisa na nondo wanaokula sadaka. Hawa mabuu wenye kudharauliwa wajinga, duni, na wenye kuchukiza wataadhibiwa siku moja karibuni!

kutoka katika “Wale Wanaomtii Mungu kwa Moyo wa Kweli Hakika Watapatwa na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Wale ambao wanafikiri tu juu ya miili yao na wanapenda starehe, wale ambao imani yao ni tata, wale wanaoshiriki katika tiba ya uchawi na usihiri, wale ambao ni wazinzi, na waliovaa matambara na wasio sawa, wale wanaoiba dhabihu kwa Yehova na mali Yake, wale ambao wanapenda rushwa, wale wanaoota kwa uzembe kwenda mbinguni, wale ambao wana kiburi na wenye majivuno, na wanajitahidi tu kwa ajili ya umaarufu wa kibinafsi na utajiri, wale ambao hueneza maneno yasiyofaa, wale wanaomkufuru Mungu Mwenyewe, wale ambao hawafanyi lolote ila kumhukumu na kumkashifu Mungu Mwenyewe, wale wanaokusanyika na wengine na kujaribu kujitegemea, wale wanaojitukuza juu zaidi kuliko Mungu, wale wanaume na wanawake wapuuzi, na wanaume na wanawake wenye umri wa kati na wazee ambao wametegwa katika uovu, wanaume na wanawake wanaofurahia umaarufu wa kibinafsi na utajiri na kufuata hadhi ya kibinafsi kati ya watu wengine, wale watu wasio na toba ambao wamenaswa katika dhambi—je, si wao wote hawawezi kuokolewa? Ufisadi, hali ya kuwa mwenye dhambi, tiba ya uchawi, usihiri, mwenendo chafu, na maneno mafidhuli hufanya fujo kati yenu, maneno ya kweli na uhai hukanyagwa kati yenu, na lugha takatifu inanajisiwa kati yenu. Ninyi Mataifa, mliojawa na uchafu na kutotii! Mtaishia wapi? Je, wale wanaopenda mwili, ambao wanafanya matendo maovu ya mwili, na ambao wametegwa katika uasherati wanawezaje kuthubutu kuendelea kuishi? Je, hujui kwamba watu kama nyinyi ni mabuu ambao hawawezi kuokolewa? Ni nini kinachowapa sifa inayostahili ya kudai hili na lile? Hadi leo, hakujakuwa na mabadiliko hata kidogo kwa wale ambao hawapendi ukweli na wanapenda tu mwili—hivyo watu hawa wanaweza kuokolewaje? Hata leo, wale ambao hawapendi njia ya uzima, ambao hawamtukuzi Mungu na kumshuhudia Yeye, ambao hupanga njama kwa ajili ya hali yao wenyewe, ambao wanajisifu wenyewe sana—je, wao bado si sawa? Iko wapi thamani ya kuwaokoa? Kama mnaweza kuokolewa hakutegemei jinsi ulivyo na sifa za kustahili, au ni umefanya kazi kwa miaka ngapi, sembuse idadi ya sifa ambazo unazo. Kunategemea na ikiwa kumekuwa na matokeo yoyote katika kufuatilia kwako. Unapaswa kujua kwamba wale ambao wameokolewa ni miti ambayo huzaa matunda, si miti ambayo ina majani ya kustawi sana na maua mengi lakini haizai matunda. Hata kama umetumia miaka mingi kuzurura mitaani, ina maana gani? Ushahidi wako uko wapi? Uchaji wako kwa Mungu ni mdogo sana kuliko upendo wako wa wewe na hamu zako za tamaa—mtu kama huyu si mpotovu? Ungewezaje kuwa mfano na kielelezo cha wokovu? Asili yako haibadiliki, wewe ni muasi sana, huwezi kuokolewa! Watu kama hao hawataondolewa? Je, wakati ambapo kazi Yangu inamalizika si wakati ambapo siku yako ya mwisho itakuja? Nimefanya kazi nyingi sana na kusema maneno mengi kati yenu—ni kiasi gani cha hayo kilichoingia ndani ya masikio yenu? Ni kiasi gani cha hayo ambacho mmewahi kutii? Wakati kazi Yangu itaisha ndio pia utakuwa wakati unapoacha kunipinga na kusimama dhidi Yangu. Wakati wa kazi Yangu, daima nyinyi hutenda dhidi Yangu, hamyatii maneno Yangu kamwe. Ninafanya kazi Yangu, na wewe unafanya kazi yako mwenyewe, unatengeneza ufalme wako mdogo mwenyewe—nyinyi kundi la mbweha na mbwa, kila kitu mnachofanya ni dhidi Yangu! Nyinyi daima mnajaribu kuwaleta wale wanaowapenda tu katika kumbatio lenu—uko wapi uchaji wenu? Kila kitu mnachofanya ni kidanganyifu! Hamna utii au uchaji, kila kitu mnachofanya ni udanganyifu na cha kukufuru! Je, watu kama hao wanaweza kuokolewa? Wanaume zinzi, wa kiasherati daima hutaka kuwavuta kwao wale makahaba wabembe kwa ajili ya raha yao wenyewe. Sitawaokoa mapepo wenye uasherati kama hao, Nawachukia ninyi mapepo wachafu, uasherati wenu na kupiga bemba kwenu kumewatumbukiza kuzimu—mna nini cha kusema kujihusu? Ninyi pepo mchafu na roho wabaya ni waovu sana! Nyinyi ni wa kuchukiza! Takataka kama nyinyi mnawezaje kuokolewa? Je, wale waliotegwa katika dhambi bado wanaweza kuokolewa? Ukweli huu, njia hii, na maisha haya hayapendezi kwenu; mnavutiwa na dhambi, pesa, hadhi, umaarufu na faida, ridhaa za mwili, maumbile mazuri ya wanaume na ubembe wa wanawake. Ni nini kinachowapa sifa zinazostahili kuingia katika ufalme Wangu? Taswira yenu ni kubwa zaidi kuliko Mungu, hali yenu ni ya juu zaidi kuliko Mungu, kutosema chochote cha sifa yenu kati ya wanadamu—mmekuwa sanamu ambayo watu wanaabudu. Je, hamjabadilika kuwa malaika mkuu? Wakati mwisho wa watu unafichuliwa, ambao pia ni wakati kazi ya wokovu inafikia kikomo, wengi wenu mtakuwa maiti ya maiti ambayo haiwezi kuokolewa na lazima muondolewe.

kutoka katika “Utendaji (7)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Watu ambao baadaye watasalimika kupitia pumziko wote watakuwa wamevumilia siku ya dhiki na pia kumshuhudia Mungu; wote watakuwa watu ambao wamefanya jukumu lao na wana nia ya kumtii Mungu. Wanaotaka tu kutumia fursa kufanya huduma ili kuepuka kutenda ukweli hawataweza kubaki. Mungu ana viwango sahihi vya mipangilio ya matokeo ya kila mtu; Hafanyi tu maamuzi haya kulingana na maneno na mwenendo wa mtu, wala Hayafanyi kulingana na tabia zao wakati wa kipindi kimoja cha muda. Hakika Hatakuwa na huruma na mwenendo wowote mbaya wa mtu kwa sababu ya huduma ya mtu ya zamani kwa Mungu, wala Hatamnusuru mtu kutokana na kifo kwa sababu ya gharama kwa Mungu ya mara moja. Hakuna anayeweza kuepuka adhabu ya uovu wake, na hakuna anayeweza kuficha tabia zake mbovu na hivyo kuepuka adhabu ya maangamizi. Kama mtu anaweza kweli kufanya jukumu lake, basi inamaanisha kwamba ni mwaminifu milele kwa Mungu na hatafuti tuzo, bila kujali iwapo anapokea baraka ama bahati mbaya. Kama watu wana uaminifu kwa Mungu waonapo baraka lakini wanapoteza uaminifu wao wasipoweza kuona baraka na mwishowe bado wasiweze kumshuhudia Mungu na bado wasiweze kufanya jukumu lao kama wapasavyo, hawa watu waliomhudumia Mungu wakati mmoja kwa uaminifu bado wataangamizwa. Kwa ufupi, watu waovu hawawezi kuishi milele, wala hawawezi kuingia rahani; watu wenye haki tu ndio mabwana wa pumziko.

kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni