Unashuhudia kuwa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Neno Laonekana katika Mwili ni maneno ya Mungu Mwenyewe, lakini tunaamini kuwa ni maneno ya mtu aliyepatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, Kile ningependa kufuatilia ni, ni nini hasa tofauti kati ya maneno yanayoonyeshwa na Mungu mwenye mwili na maneno yaliyosemwa na mtu ambaye amepatiwa nuru na Roho Mtakatifu?
Jibu:
Yote ambayo Mwenyezi Mungu huonyesha ni ukweli, na Neno Laonekana katika Mwili kwa kweli ni matamshi ya Mwenyezi Mungu, ambaye ni kuja kwa mara ya pili kwa Bwana Yesu. Wote walio na moyo na roho watakikubali kikamilifu baada ya kuona neno Lake, watambue kwamba ni sauti ya Mungu, na kusujudu mbele ya Mungu. Hata hivyo, bado kuna baadhi ya watu wanaoamini kwamba maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni maneno tu yaliyoandikwa na mwanadamu aliyetiwa msukumo na Roho Mtakatifu, na hawaamini ni neno halisi la Mungu. Hili linaonyesha kwamba imani yetu kwa Mungu haimaanishi kumjua Mungu, kwamba hatuwezi kubainisha neno la Mungu kutoka kwa maneno ya mwanadamu, na kwamba zaidi ya hayo, hatuwezi kubainisha dhahiri maneno yanayokubaliana na ukweli kutoka kwa ukweli halisi.