Unashuhudia kuwa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Neno Laonekana katika Mwili ni maneno ya Mungu Mwenyewe, lakini tunaamini kuwa ni maneno ya mtu aliyepatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, Kile ningependa kufuatilia ni, ni nini hasa tofauti kati ya maneno yanayoonyeshwa na Mungu mwenye mwili na maneno yaliyosemwa na mtu ambaye amepatiwa nuru na Roho Mtakatifu?
Jibu:
Yote ambayo Mwenyezi Mungu huonyesha ni ukweli, na Neno Laonekana katika Mwili kwa kweli ni matamshi ya Mwenyezi Mungu, ambaye ni kuja kwa mara ya pili kwa Bwana Yesu. Wote walio na moyo na roho watakikubali kikamilifu baada ya kuona neno Lake, watambue kwamba ni sauti ya Mungu, na kusujudu mbele ya Mungu. Hata hivyo, bado kuna baadhi ya watu wanaoamini kwamba maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni maneno tu yaliyoandikwa na mwanadamu aliyetiwa msukumo na Roho Mtakatifu, na hawaamini ni neno halisi la Mungu. Hili linaonyesha kwamba imani yetu kwa Mungu haimaanishi kumjua Mungu, kwamba hatuwezi kubainisha neno la Mungu kutoka kwa maneno ya mwanadamu, na kwamba zaidi ya hayo, hatuwezi kubainisha dhahiri maneno yanayokubaliana na ukweli kutoka kwa ukweli halisi.
Kwa kweli, kuna tofauti dhahiri kabisa kati ya maneno yanayokubaliana na ukweli na ukweli halisi. Neno la Mungu ni ukweli, na hakuna mtu anayeweza kukana jambo hilo, lakini maneno ya mwanadamu, kama inawezekana, yanakubaliana tu na ukweli. Iwapo mtu angelinganisha maneno ya mwanadamu yanayokubaliana na ukweli kwa neno la Mungu, kweli hakungekuwa na tofauti? Kweli hangeweza kuona tofauti? Mtu anaweza kusemwa kuwa ana ukweli kama hajapitia neno la Mungu na kuwa na maarifa ya neno Lake? Mtu akizungumza maneno yanayokubaliana na ukweli, je, hili linamaanisha kwamba anauonyesha ukweli? Watakatifu wa enzi za zamani walisema mambo mengi yanayokubaliana na ukweli; je, maneno hayo yanaweza kujadiliwa kwa usawa na ukweli unaoonyeshwa na Mungu? Wale wanaouelewa ukweli kwa kweli na kuutambua ukweli wanaweza kuona kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya maneno yanayokubaliana na ukweli na ukweli wenyewe. Ni wale tu wasiouelewa ukweli, au wanaokosa kuutambua, ambao wanaunganisha mambo hayo mawili. Ili tubainishe maneno yanayokubaliana na ukweli kutoka kwa ukweli, lazima tuelewe ukweli ni nini hasa. Sisi tulio na imani katika Bwana tumesoma maneno Yake mengi, tunakiri hayo mamlaka na uwezo wa maneno Yake, na pia tunaweza kuhisi kwamba neno la Bwana tu ni ukweli. Hatutawahi kupitia ukweli kikamilifu, na bila kujali kiwango cha uzoefu ama ufahamu tulio nao kuhusu ukweli, hatungeweza kuthubutu kamwe kusema kwamba tunao ukweli kikamilifu au tunao ufahamu wa kweli kuhusu Mungu. Ndani ya jamii ya kidini, kuna wachungaji na wazee wengi wanaothubutu kuifafanua Biblia, lakini hawathubutu kulifafanua neno la Mungu watakavyo. Hakuna yeyote kati ya wanadamu anayethubutu kusema kwamba analielewa neno la Mungu, na hakuna anayethubutu kusema kwamba anauelewa ukweli. Hii linaonyesha kwamba kiini cha ukweli ni chenye kina sana, na kinaweza kuonyeshwa na Mungu pekee. Mwanadamu anapopitia kazi ya Mungu, anaweza tu kutimiza kiwango fulani cha ufahamu wa ukweli, kuingia katika sehemu ya uhalisi wake, na kusema mambo machache yanayokubaliana na ukweli, jambo ambalo ni zuri kadri ya matarajio ya mtu. Hata hivyo, hawezi kamwe kumiliki au kuonyesha ukweli. Huu ni ukweli. Katika enzi za zamani, watakatifu walisema mambo mengi yanaokubaliana na ukweli, lakini hakuna mtu ambaye angethubutu kusema kwamba maneno hayo ni ukweli. Ukweli ni nini basi, hasa? Ukweli unaonyeshwa na Mungu, na Kristo pekee ndiye ukweli, njia, na uzima. Kila kitu ambacho Mungu husema ni ukweli, kila kitu ambacho Mungu husema kinawakilisha tabia Yake na chote Alicho na Alicho nacho, na maneno Yake yamejaa uweza na hekima Yake. Mungu alitumia maneno Yake kuumba mbingu, nchi, na vitu vyote, na Mungu hutumia maneno Yake kwa ajili ya kazi Yake kuelekea wokovu wa wanadamu; kupitia maneno ya Mungu vitu vyote vinatimizwa. Watu wote ambao wamepitia kazi ya Mungu wanaweza kuona uwezo na kudura ya maneno ya Mungu, jambo ambalo linathibitisha kwamba Mungu pekee ndiye Anayeweza kuuonyesha ukweli. Uwezo wa ukweli na asili yake ya milele haviwezi kueleweka kwa wanadamu, ukweli pekee ndio wa milele, na unaishi pamoja kwa amani na Mungu. Ni wa kudumu na usiobadilika. Wanadamu wakiupata ukweli kama uzima, basi wamepata uzima wa kudumu. Umuhimu wa Mungu kumpa mwanadamu ukweli ili mwanadamu aweze kuupata ukweli kama uzima ni mkubwa sana. Ni jinsi Mwenyezi Mungu anavyosema, “Ukweli ukiwekwa kwa lugha ya binadamu ni methali kwa mwanadamu; ubinadamu hauwezi kupata uzoefu wake kikamilifu, na ubinadamu lazima uishi kwa kuutegemea. Kipande cha ukweli kinaweza kuufanya ubinadamu mzima kuishi kwa maelfu ya miaka.
“Ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake” (“Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo).
“Ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha” (“Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu” (“Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Kwa nini haiwezi kusemwa kwamba maneno ya mwanadamu ambayo yanakubaliana na ukweli ni ukweli? Kwa sababu maneno ya mwanadamu yanayokubaliana na ukweli yanawakilisha uzoefu na maarifa yake kuhusu ukweli tu, na ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu hufanya kazi ili kuwaelimisha watu na kuwaongoza kwa ufahamu wa polepole kuhusu ukweli na kuingia katika uhalisi wake, kulingana na kimo halisi cha kiroho cha watu wakati huo. Kila wakati Roho Mtakatifu anapowaelimisha watu, jambo hili linawapa ufahamu kiasi tu kuhusu mwanga wa ukweli na maarifa kidogo tu kuhusu uhalisi wa ukweli. Roho Mtakatifu hangewahi kutoa kiini kamili cha ukweli kwa mwanadamu kwa hatua moja, kwa sababu mwanadamu hangeweza kukitimiza na hangeweza kukipitia. Kile mwanadamu anachosema kinachokubaliana na ukweli ni ufahamu na uzoefu wa ukweli wa juu juu na finyu sana, na kiko mbali na kiini cha ukweli. Hiki kiko chini ya wastani sana na kiwango cha ukweli, kwa hiyo hakiwezi kusemwa kuwa ni ukweli. Hata kama kile ambacho mwanadamu anasema kinatiwa msukumo na nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu na kinakubaliana kikamilifu na ukweli, ni kwa ajili tu ya ujenzi wa maadili na manufaa ya mwanadamu, lakini hakiwezi kuwa uzima wa mwanadamu, wakati ukweli unaweza kuwa uzima wa milele wa mwanadamu. Hii ni kwa sababu mwanadamu hawezi kamwe kupitia kiini cha ukweli kikamilifu, na hawezi kamwe kuishi kwa kudhihirisha mfano wa ukweli. Mwanadamu anaweza tu kuishi kwa kudhihirisha sehemu ndogo ya mfano wa ukweli, jambo ambalo ni zuri sana. Ukweli unaweza kuwa uzima wa mwanadamu milele na unaweza kumpa mwanadamu uzima wa kudumu, lakini wakati ambapo wanadamu wanasema maneno yanayokubaliana na ukweli, ni mbinu ya muda mfupi tu ya kusaidia ujenzi wao wa maadili, na matokeo ambayo yanayo yanadumu kwa kipindi cha muda tu, kwa hiyo maneno kama hayo hayawezi kuwa uzima wa kudumu wa mwanadamu. Hii ndiyo tofauti halisi kati ya maneno yanayokubaliana na ukweli na ukweli wenyewe. Kutokana na hili, tunaweza kuona kwamba hata kama usemi wa mwanadamu unatiwa nuru na Roho Mtakatifu na hata kama unakubaliana na ukweli, bado hauwezi kusemwa kuwa ni ukweli. Huu ni ukweli, na wale walio na uzoefu wa maisha wanaweza kujifunza na kuhisi hivi.
kutoka katika Majibu kwa Maswali ya Tamthilia
Iwapo tutofautishe kati ya usemi wa mwanadamu unaolingana na ukweli na maneno yaliyoonyeshwa na Mungu katika mwili, lazima kwanza tuelewe kwamba Mungu ana kiini kitakatifu cha Mungu na mwanadamu ana kiini cha binadamu. Neno la Mungu ni ufunuo wa maisha ya Mungu na ni onyesho la tabia ya Mungu, wakati maneno ya mwanadamu hufichua kiini cha binadamu. Ni maonyesho ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu pekee ndiyo ukweli, na maonyesho hayo pekee ni neno la Mungu. Hii ni kwa sababu kiini cha maisha ya Mungu ni cha pekee na hakimilikiwi na mwanadamu yeyote. Hata hivyo, watu wanaotumiwa na Mungu na watu walio na kazi ya Roho Mtakatifu wanaweza kusema maneno yanayolingana na ukweli na yanayoweza kuwaadilisha wengine. Hili linatokana na nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu na pia kutoka kwa uzoefu wa mwanadamu na ufahamu wa ukweli katika neno la Mungu. Hata hivyo, hili si onyesho la moja kwa moja la Roho Mtakatifu, hivyo si neno la Mungu.
Mwenyezi Mungu anasema, “Kwa kweli, Ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha” (“Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Unafaa kuelewa mawanda ya hakika ya ukweli na kuelewa kile kilicho nje ya mawanda ya ukweli.
“Watu wakipata ufahamu kidogo na kuwa na uelewa kulingana na uzoefu wao kutoka kwa maneno ya ukweli, je hii inahesabika kama ukweli? Kwa kiwango cha juu zaidi inaweza kusemekana kwamba wana uelewa fulani wa ukweli. Maneno yote ya nuru ya Roho Mtakatifu hayawakilishi neno la Mungu, hayauwakilishi ukweli, na hayafungamani ukweli. Inaweza tu kusemwa kuwa watu hao wana uelewa fulani wa ukweli, na nuru ya Roho Mtakatifu. … Kila mtu anaweza kuupitia ukweli, lakini hali ya uzoefu wao itakuwa tofauti, na kile kila mtu hupata kutoka kwa ukweli huo sawa ni tofauti. Lakini hata baada ya kuweka pamoja uelewa wa kila mtu bado huwezi kueleza kikamilifu ukweli huu mmoja; ukweli ni wa kina zaidi namna hiyo. Mbona Ninasema kuwa vitu vyote ambavyo umevipata na uelewa wako wote, haviwezi kuwa mbadala wa ukweli? Ukishiriki uelewa wako na wengine, wanaweza kuutafakari kwa siku mbili ama tatu kisha watamaliza kuupitia, lakini mtu hawezi kupata uzoefu kamilifu wa ukweli hata kwa maisha yote, hata watu wote kwa pamoja hawawezi kupata uzoefu wa huo kabisa. Hivyo inaweza kuonekana kuwa ukweli ni mkubwa sana! Hakuna jinsi ya kutumia maneno ili kuueleza ukweli kikamilifu, ukweli ukiwekwa kwa lugha ya binadamu ni methali kwa mwanadamu; ubinadamu hauwezi kupata uzoefu wake kikamilifu, na ubinadamu lazima uishi kwa kuutegemea. Kipande cha ukweli kinaweza kuufanya ubinadamu mzima kuishi kwa maelfu ya miaka.
“Ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake. Ukisema kwamba kuwa na uzoefu fulani kunamaanisha kuwa una ukweli, basi unaweza kuwakilisha tabia ya Mungu? Huwezi. Mtu anaweza kuwa na uzoefu fulani ama mwanga kuhusu kipengele fulani ama upande wa ukweli, lakini hawezi kuwatolea wengine milele, kwa hivyo mwanga wake sio ukweli; ni kiwango tu ambacho kinaweza kufikiwa na mtu. Ni uzoefu wa kufaa tu na ufahamu ambao mtu anafaa kuwa nao, ambao ni uzoefu wao wa utendaji wa ukweli. Mwanga huu, nuru na uelewa kwa msingi wa uzoefu hayatawahi kuwa mbadala wa ukweli; hata kama watu wote wamepata uzoefu wa sentensi moja ya ukweli kabisa, na wakiweka maneno hayo yote pamoja, hilo bado si mbadala wa ukweli huo mmoja. … Ninamaanisha nini na hili? Namaanisha kwamba maisha ya mwanadamu daima yatakuwa maisha ya mwanadamu, na haijalishi uelewa wako unalingana vipi na ukweli, kulingana na maana ya Mungu, kulingana na nia za Mungu, hayataweza kamwe kuwa mbadala wa ukweli. Kusema kuwa watu wana ukweli kunamaanisha kuwa wana uhalisi fulani, kuwa wana uelewa fulani wa ukweli wa Mungu, kuwa wana kuingia wa kweli katika maneno ya Mungu, kuwa wana uzoefu fulani wa kweli na maneno ya Mungu, na kuwa wako katika njia sahihi katika imani yao kwa Mungu. Kauli moja tu ya Mungu inatosha mtu kupata uzoefu kwa maisha yake yote; hata kama watu wangekuwa na uzoefu wa maisha kadhaa ama wa milenia kadhaa, bado hawangeweza kuupitia ukweli kabisa” (“Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo).
Kuhusu tofauti kati ya maneno ya mwanadamu yanayolingana na ukweli na neno la Mungu, maneno ya Mwenyezi Mungu yanatoa maelezo ya wazi kabisa: Ukweli unatoka kwa Mungu, unaonyeshwa kupitia Kristo, na pia ni onyesho la moja kwa moja la Roho Mtakatifu, na kila kitu Mungu husema ni ukweli. Ukweli ndio uhai hasa wa Mungu Mwenyewe, ni onyesho la tabia ya haki ya Mungu, ni ufunuo wa kila ambacho Mungu anacho na alicho, ni uhalisi wa mambo mema, na unawakilisha kiini cha maisha binafsi ya Mungu. Hata hivyo, watu wanaotumiwa na Mungu na watu walio na kazi ya roho Mtakatifu wanaweza kusema maneno yanayolingana na ukweli. Hili linatoka kwa nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, na pia kutoka kwa uzoefu wa mwanadamu wa, na ufahamu wa ukweli katika neno la Mungu. Maneno haya yanayolingana na ukweli yanawakilisha uzoefu wa Mungu na ufahamu. Hayo ni uhalisi wa ukweli ambao mwanadamu amefanikisha uingiaji kwao, na ni matokeo ya kazi ya Mungu. Haijalishi jinsi ufahamu wa mwanadamu wa ukweli ulivyo wa kina au wa juu, au jinsi anavyomjua Mungu vyema, kila kitu kinachosemwa na binadamu hufichua kiini cha maisha yake ya binadamu. Kwa sababu maneno yanayozungumzwa na mwanadamu ambayo yanalingana na ukweli ni mbali sana na kina cha kiini cha ukweli, kile ambacho mwanadamu anasema hakiwezi kuitwa ukweli. Kuna tofauti za asili na kubwa kati ya maneno ambayo yanalingana na ukweli na ukweli halisi. Neno la Mungu ni ukweli, ni kiini cha maisha ya Mungu, hivyo neno la Mungu ni la milele na halibadiliki. Ni kama tu alivyosema Bwana Yesu: “Mbingu na dunia zitapita: bali maneno yangu hayatapita hata milele” (Luka 21:33). Mwenyezi Mungu pia anasema, “Maneno yangu ndio ukweli usiobadilika milele” (“Mnapaswa Kuzingatia Matendo Yenu” katika Neno Laonekana katika Mwili). Hii ni sawa sana na Amri Kumi zilizotangazwa rasmi na Mungu katika Enzi ya Sheria: Ingawa maelfu ya miaka imepita, bado zinashikwa na wanadamu leo. Hili ni kwa sababu neno la Mungu ni ukweli, ni uhalisi wa mambo mema, linaweza kustahimili majaribu ya wakati, na litasimama milele na milele. Hata hivyo, kwa sababu maneno ya wanadamu si ukweli, hayatadumu milele. Tunaweza kuona kutoka kwa uendeleaji wa historia ya binadamu, iwe ni katika mawanda ya utafiti wa kisayansi na sheria, au katika nadharia za sosiolojia, ambazo kwa muda mfupi maneno ya mwanadamu yanapinduliwa au kuachwa, auhata yanapitwa na wakati kufumba kufumbua. Hata kama maneno ambayo mwanadamu anasema yanalingana na ukweli, yanaweza tu kutusaidia sisi, kutupa riziki, na kutufadhili kwa muda mfupi. Hayawezi kuwa maisha yetu. Mbona tunasemwa kwamba maneno ya mwanadamu hayawezi kuwa maisha ya mwanadamu? Kwa sababu huku neno la mwanadamu likiweza kulingana na ukweli, ni uzoefu na ufahamu wa mwanadamu tu wa neno la Mungu na liko mbali sana na kiini cha ukweli na haliwezi hata kidogo kuwakilisha ukweli, wala haliwezi kuwa na matokeo ya kuwa maisha ya mwanadamu ambayo ukweli unaweza; linaweza kutusaidia kwa muda mfupi tu na kutupa ujenzi wa maadili na ufadhili, hivyo hiyo ndio maana neno la mwanadamu linalolingana na ukweli si ukweli, na haliwezi kuwa maisha ya mwanadamu. Hivyo kwa nini maneno ya Mungu pekee ndiyo yanaweza kuwa maisha ya mwanadamu? Kwa sababu neno la Mungu ni ukweli na ni uhalisi wa mambo mema, sisi binadamu hatuwezi kulipitia kikamilifu kamwe, na kila ukweli hauwezi kuisha kwa sisi binadamu. Hata kama tungepitia milele, bado hatungelithubutu kusema kwamba tunamiliki ukweli au tumepata ukweli kikamilifu. Huu ni ukweli. Aidha, ukweli unaweza kuwatakasa wanadamu, kuwaokoa wanadamu, na kuwakamilisha wanadamu. Kwa kuutegemea ukweli kuishi, tunaweza kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu wa kweli, kuishi kwa kudhihirisha sura ya ukweli, na hivyo tunaweza kupata kumjua Mungu, kumtii Mungu, kumwabudu Mungu, na kulingana na Mungu, ambayo ilikuwa nia ya Mungu alipowaumba binadamu mwanzoni. Kama tu inavyosema Biblia, “Na tumuumbe mwanadamu katika sura yetu, kwa mfanano wetu” (Mwanzo 1:26). Nia ya Mungu katika kuwaumba wanadamu haikuwa kuwapa wanadamu mwili tu, lakini kimsingi ilikuwa kuwapa wanadamu maisha mapya. Maisha haya mapya ni neno la Mungu, ambalo ni ukweli. Ukweli unapokuwa maisha yetu, unapokuwa uhalisi wa maisha yetu, ambapo ni wakati tunaishi kwa kudhihirisha mfano wa ukweli, na kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mwanadamu halisi, basi tutakuwa tumekamilisha nia ya Mungu katika kuwaumba wanadamu. Kwa hivyo, tunasema kwamba neno la Mungu pekee na ukweli pekee ndivyo vinavyoweza kuwa maisha ya milele ya mwanadamu. Hata ingawa watu wanaotumiwa na Mungu wanaweza kuwa na uzoefu fulani na ufahamu wa neno la Mungu, na wanaweza kuwa na uwezo wa kusema mambo fulani yanayolingana na ukweli, haya ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu. Ni wokovu wa Mungu na Mungu kumkamilisha mwanadamu. Maneno ya watu wanaotumiwa na Mungu yanayolingana na ukweli au ufahamu wao wa kweli wa Mungu haumaanishi kwamba wanamiliki kiini cha ukweli, wala hauwakilishi kumiliki maisha ya Mungu. Badala yake, unaonyesha tu kwamba wamepata ukweli na kwamba ukweli umekuwa uhalisi wa maisha yao. Hii ni kwa sababu mwanadamu si ukweli na hawezi kuthubutu kusema kwamba hakika anamiliki ukweli. Kwa hivyo, bila kujali ni kiasi kipi maneno ya mwanadamu yanalingana na ukweli, au ni kiasi gani yanaweza kutuadilisha, hayawezi kusemwa kuwa ukweli, na aidha hayo si neno la Mungu.
kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme
Kama tunataka kujua kwa nini maneno yanayokubaliana na ukweli yaliyonenwa na wanadamu ambao Mungu huwatumia si ukweli, ni lazima kwanza tuelewe kuhusu “ukweli” ni nini kwa kweli. Katika historia nzima, hakuna mtu aliyewahi kujua kwa hakika ukweli ni nini. Bwana Yesu alipokuja katika ulimwengu huu katika Enzi ya Neema, Yeye alisema, “Mimi ndiye njia, ukweli na uhai” (Yohana 14:6). Bado hakuna yeyote aliyeelewa maana halisi ya “ukweli.” Ni pale tu ambapo Kristo wa siku za mwisho—Mwenyezi Mungu—anapokuja ndipo mafumbo ya “ukweli” yanafichuliwa kikamilifu kwa wanadamu.
Hebu tuangalie kile ambacho Mwenyezi Mungu anasema kuhusu hili: “Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu” (“Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha” (“Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Ukweli ukiwekwa kwa lugha ya binadamu ni methali kwa mwanadamu; ubinadamu hauwezi kupata uzoefu wake kikamilifu, na ubinadamu lazima uishi kwa kuutegemea. Kipande cha ukweli kinaweza kuufanya ubinadamu mzima kuishi kwa maelfu ya miaka.
“Ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake” (“Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo).
Kutoka katika maneno ya Mwenyezi Mungu, tunaweza kuona: Ukweli unatoka kwa Mungu, na unatoka katika maonyesho ya Kristo. Hiyo ni kusema, maneno yote yaliyonenwa na Mungu ni ukweli. Hii ni kwa sababu ukweli ni kiini cha uzima wa Mungu, tabia ya Mungu, kile ambacho Mungu anacho na alicho, na uhalisi wa mambo yote chanya. Ukweli ni wa milele na hautabadilika kamwe. Maneno ya Mungu yana mamlaka na nguvu. Yanaweza kumtakasa, kumwokoa na kumkamilisha mwanadamu, na yanaweza kuwa uzima wa milele wa mwanadamu. Hivyo, maneno yote yaliyonenwa na Mungu ni ukweli. Kazi, ufunuo, na kile Anachoamuru yote ni ukweli. Kile ambacho Mungu anaamuru au kumwagiza mwanadamu kuendeleza na kutii, na yote Anayotaka kwa mwanadamu na anayomwamuru mwanadamu kuishi kwa kuyadhihirisha ni ukweli, uhalisi wa mambo yote chanya. Na hivyo, kuna ukweli unaopatikana katika kila neno ambalo Mungu ananena. Katika kila hatua ya kazi Yake, Mungu ameonyesha ukweli mwingi. Maisha ya thamani ambayo Mungu anatupatia sisi wanadamu yamo ndani ya huu ukweli.
Yote ambayo Mungu anaonyesha wakati wa kazi ya kupata Kwake mwili mara mbili ni ukweli. Ni kama tu maneno ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema: Maneno Yake yaliwezesha wanadamu kushuhudia tabia ya Mungu, upendo Wake, na kiini kitakatifu. Yote haya ni ukweli wa thamani unaotusaidia kumjua Mungu. Upendo, uvumilivu, na msamaha wa Bwana Yesu kwa wanadamu, pamoja na matakwa Yake kwa wanadamu wampende Mungu kwa mioyo, roho na akili zao zote, kuwapenda majirani zao kama wanavyojipenda wenyewe, kuwa nuru ya ulimwengu na chumvi ya dunia, yote haya ni mambo chanya. Haya ni ukweli. Pia ni uhalisi wa maisha ambao tunatakiwa kuumiliki. Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, amekuja na Yeye anaonyesha ukweli wote wa kuhukumu, kutakasa, na kuwakamilisha wanadamu. Ukweli huu ni uhalisi wa maisha ambayo mwanadamu lazima afikie kuumiliki katika Enzi ya Ufalme. Kristo wa siku za mwisho anamfichulia mwanadamu tabia ya Mungu ya haki, uadhama, ghadhabu na kutovumilia kosa. Yeye anafunua mafumbo ya mpango wa usimamizi wa Mungu wa kuwaokoa wanadamu, mafumbo ya hatua tatu za kazi za Mungu, kiini na ukweli wa ndani wa kila hatua ya kazi Yake, pamoja na fumbo la kupata Kwake mwili, jinsi Mungu anavyofanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho, na ufalme wa Kristo ni nini. Anafunua jinsi Mungu anavyofichua miisho ya kila mmoja, na jinsi Mungu anavyouzawadi wema na kuuadhibu uovu. Anafichua maana ya haki ya Mungu, maana ya utakatifu wa Mungu na maana ya kiishara ya tabia ya Mungu, kupendezwa, hasira, majonzi, na furaha Yake. Anafichua kilicho cha haki na kilicho kiovu, kilicho chanya na kilicho hasi, na asili na ukweli wa upotovu wa mwanadamu unaosababishwa na Shetani. Mwenyezi Mungu anamwonyesha mwanadamu jinsi ya kumcha Mungu na kuepuka maovu, maisha ya kweli ni nini na jinsi ya kuishi kwa maana, na kadhalika. Mwenyezi Mungu ameshafichua ukweli na mafumbo haya yote kwa mwanadamu ili aje ajue na kuelewa, ili kwamba wamche Mungu na kuepuka maovu, amtii na kumwabudu Mungu. Ukweli wa Mwenyezi Mungu ni njia ya uzima wa milele ambayo binadamu anastahili kuimiliki. Wale wanaokumbatia ukweli wote wa Mungu na kuishi kwa kuufuata watapata uzima wa milele. Ilhali wale wanaokataa kukubali ukweli wowote hakika wataangamia. Hivyo, ukweli wote ambao Mwenyezi Mungu anaonyesha katika siku za mwisho ni kazi ya Mungu ya kuhitimisha enzi na kuanzisha enzi mpya katika siku za mwisho. Wanadamu wanaotumiwa na Mungu ni wale ambao Mungu anawaokoa na kuwakamilisha. Wajibu wao katika kazi ya Mungu ni kushirikiana na kazi ya Mungu na kuwaongoza watu wateule wa Mungu. Na hivyo, maneno yoyote wanayozungumza ambayo yanakubaliana na ukweli ni matunda ya kazi ya Roho Mtakatifu. Ingawa maneno haya yana faida kwa watu, hatuwezi kuyaita ukweli; hatuwezi kuyachukulia kama neno la Mungu kwa sababu maneno ya wanadamu yanatoka katika maarifa na uzoefu wao wa ukweli, na yanaweza tu kuwakilisha mtazamo, mawazo na ufahamu wa kibinadamu, na lazima yatafifilizwa na taka za kibinadamu. Aidha, maarifa na uzoefu wa mwanadamu kuhusu ukweli vina kikomo. Haijalishi anaingia katika uhalisi wa ukweli kwa kiasi gani, bado hawezi kusemwa ni mfano halisi wa ukweli, wala hawezi kusemwa anaishi kulingana na ukweli kikamilifu. Hivyo, hata kama alionyesha kiasi kidogo cha uhalisi wa ukweli alioishi kwa kuudhihirisha, maneno yake yanakubaliana tu na ukweli. Ni lazima yasiwekwe katika kiwango sawa na ukweli wenyewe. Ni maneno ya Mungu mwenye mwili tu ndiyo ukweli. Hiyo ni kusema, ni Mungu tu aliye na kiini cha ukweli, na Mungu tu ndiye ukweli. Haijalishi ni kwa miaka mingapi tumemwamini Mungu, daima sisi ni wachanga mbele za Mungu. Hatuwezi kamwe kuishi kwa kudhihirisha mfano wa Mungu. Na hivyo, maneno ya wanadamu ambao Mungu huwatumia au wanadamu walio na kazi ya Roho Mtakatifu yanaweza kuchukuliwa tu kama maneno yanayokubaliana na ukweli. Hatuwezi kuyachukulia kama ukweli wenyewe. Huu ni ukweli usiopingika. Tunapoita maneno ya mwanadamu ukweli, tunampinga na kumkufuru Mungu!
kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni