7.27.2019

Kuna tofauti ipi kati ya maneno ya watu wanaotumiwa na Mungu kote katika enzi zote ambayo yanakubaliana na ukweli na maneno ya Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

XII. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Kipengele cha Ukweli Kuhusu Wanawali Wenye Busara Wakiisikia Sauti ya Mungu

Kuna tofauti ipi kati ya maneno ya watu wanaotumiwa na Mungu kote katika enzi zote ambayo yanakubaliana na ukweli na maneno ya Mungu?


Maneno Husika ya Mungu:
Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu.
kutoka katika “Mafanikio au Kushindwa Kunategemea Njia Ambayo Mwanadamu Hutembea” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ukweli ndio halisi zaidi katika methali zote za maisha, na ni mkuu kabisa kuliko methali hizo miongoni mwa wanadamu wote. Kwa sababu ni matakwa ambayo Mungu anayataka kwa mwanadamu, na ni kazi ambayo inafanywa na Mungu mwenyewe, hivyo inaitwa methali ya maisha. Sio methali iliyoundwa kutoka katika kitu fulani, wala si nukuu maarufu kutoka kwa mtu maarufu; badala yake, ni matamshi kwa mwanadamu kutoka kwa Bwana wa mbingu na nchi na vitu vyote, na sio maneno fulani yaliyotolewa na mwanadamu, bali ni maisha asili ya Mungu. Na hivyo unaitwa ni methali ya juu kabisa kupita methali zote za maisha.
kutoka katika “Ni Wale tu Wanaomjua Mungu na Kazi Yake Ndio Wanaoweza Kumridhisha Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Unafaa kuelewa mawanda ya hakika ya ukweli na kuelewa kile kilicho nje ya mawanda ya ukweli.
Watu wakipata ufahamu kidogo na kuwa na uelewa kulingana na uzoefu wao kutoka kwa maneno ya ukweli, je hii inahesabika kama ukweli? Kwa kiwango cha juu zaidi inaweza kusemekana kwamba wana uelewa fulani wa ukweli. Maneno yote ya nuru ya Roho Mtakatifu hayawakilishi neno la Mungu, hayauwakilishi ukweli, na hayafungamani ukweli. Inaweza tu kusemwa kuwa watu hao wana uelewa fulani wa ukweli, na nuru ya Roho Mtakatifu. … Kila mtu anaweza kuupitia ukweli, lakini hali ya uzoefu wao itakuwa tofauti, na kile kila mtu hupata kutoka kwa ukweli huo sawa ni tofauti. Lakini hata baada ya kuweka pamoja uelewa wa kila mtu bado huwezi kueleza kikamilifu ukweli huu mmoja; ukweli ni wa kina zaidi namna hiyo. Mbona Ninasema kuwa vitu vyote ambavyo umevipata na uelewa wako wote, haviwezi kuwa mbadala wa ukweli? Ukishiriki uelewa wako na wengine, wanaweza kuutafakari kwa siku mbili ama tatu kisha watamaliza kuupitia, lakini mtu hawezi kupata uzoefu kamilifu wa ukweli hata kwa maisha yote, hata watu wote kwa pamoja hawawezi kupata uzoefu wa huo kabisa. Hivyo inaweza kuonekana kuwa ukweli ni mkubwa sana! Hakuna jinsi ya kutumia maneno ili kuueleza ukweli kikamilifu, ukweli ukiwekwa kwa lugha ya binadamu ni methali kwa mwanadamu; ubinadamu hauwezi kupata uzoefu wake kikamilifu, na ubinadamu lazima uishi kwa kuutegemea. Kipande cha ukweli kinaweza kuufanya ubinadamu mzima kuishi kwa maelfu ya miaka.
Ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake. Ukisema kwamba kuwa na uzoefu fulani kunamaanisha kuwa una ukweli, basi unaweza kuwakilisha tabia ya Mungu? Huwezi. Mtu anaweza kuwa na uzoefu fulani ama mwanga kuhusu kipengele fulani ama upande wa ukweli, lakini hawezi kuwatolea wengine milele, kwa hivyo mwanga wake sio ukweli; ni kiwango tu ambacho kinaweza kufikiwa na mtu. Ni uzoefu wa kufaa tu na ufahamu ambao mtu anafaa kuwa nao, ambao ni uzoefu wao wa utendaji wa ukweli. Mwanga huu, nuru na uelewa kwa msingi wa uzoefu hayatawahi kuwa mbadala wa ukweli; hata kama watu wote wamepata uzoefu wa sentensi moja ya ukweli kabisa, na wakiweka maneno hayo yote pamoja, hilo bado si mbadala wa ukweli huo mmoja. Kama ilivyosemwa zamani, “Nilifupisha hili kwa ajili ya dunia ya binadamu kwa kanuni: Miongoni mwa wanadamu hakuna yule anayenipenda Mimi.” Hii ni kauli ya ukweli, ni asili ya kweli ya maisha, ni kitu chenye cha maana sana, ni udhihirisho wa Mungu binafsi. Unaweza kuipitia. Ukiipitia kwa miaka mitatu utakuwa na uelewa usio na kina, ukiipitia kwa miaka minane utapata uelewa zaidi, lakini uelewa wako hautaweza kuwa mbadala wa kauli ya ukweli. Mtu mwingine akipata uzoefu wake kwa miaka miwili atakuwa na uelewa mdogo; akiupitia kwa miaka kumi atakuwa na uelewa wa juu, na akipata uzoefu kwa maisha yake yote atapata uelewa mkubwa zaidi, lakini mkiuweka uelewa wenu pamoja, haijalisha uelewa wa kiwango kipi, uzoefu wa kiwango kipi, ufahamu kiasi gani, mwanga wa kiasi kipi, ama mifano mingapi ambayo ninyi wawili mnayo, hayo yote hayawezi kuwa mbadala wa kauli hiyo. Ninamaanisha nini na hili? Namaanisha kwamba maisha ya mwanadamu daima yatakuwa maisha ya mwanadamu, na haijalishi uelewa wako unalingana vipi na ukweli, kulingana na maana ya Mungu, kulingana na nia za Mungu, hayataweza kamwe kuwa mbadala wa ukweli. Kusema kuwa watu wana ukweli kunamaanisha kuwa wana uhalisi fulani, kuwa wana uelewa fulani wa ukweli wa Mungu, kuwa wana kuingia wa kweli katika maneno ya Mungu, kuwa wana uzoefu fulani wa kweli na maneno ya Mungu, na kuwa wako katika njia sahihi katika imani yao kwa Mungu. Kauli moja tu ya Mungu inatosha mtu kupata uzoefu kwa maisha yake yote; hata kama watu wangekuwa na uzoefu wa maisha kadhaa ama wa milenia kadhaa, bado hawangeweza kuupitia ukweli kabisa. …
… Kama una uzoefu fulani na kipengele cha ukweli, je, hili linaweza kuuwakilisha ukweli? Haliwezi kuwakilisha ukweli kabisa. Kwa hivyo unaweza kunena ukweli kabisa? Je, unaweza kueleza ukweli kikamilifu? Huwezi kwa kweli. Unaweza kugundua tabia na asili ya Mungu kutoka kwa ukweli? Huwezi. Uzoefu wa kila mtu wa ukweli ni kipengele chake kimoja tu, sehemu moja, mtazamo mmoja; kupata uzoefu wake katika mawanda yako finyu huwezi kugusia ukweli wote. Maana ya ukweli inafichua asili ya kawaida ya binadamu. Uzoefu wako mdogo unajumuisha kiwango kipi? Chembe ya changarawe ufuoni, tone la maji baharini. Kwa hiyo, bila kujali jinsi ufahamu na hisi zako kutoka kwa uzoefu wako ni ya thamani, hata kama ni za thamani sana—haziwezi kuhesabika kama ukweli. Chanzo cha ukweli na maana ya ukweli ni pana sana. Hakuna kinachoweza kuupinga. … Hata hivyo, vitu ambavyo watu wanavyo, mwanga ambao watu wamepata, vinawafaa tu wao binafsi ama kwa wengine katika mawanda fulani, lakini havitafaa katika mawanda tofauti. Uzoefu wa mtu ni finyu sana haijalishi ni wa maana kiasi gani, na uzoefu wao hautawahi kufikia kamwe mawanda ya ukweli. Mwanga wa mtu, uelewa wa mtu, hauwezi kamwe kulinganishwa na ukweli.
kutoka katika “Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Njia za mwanadamu kutenda na maarifa yake ya ukweli yote yanatumika tu katika mawanda fulani. Huwezi kusema kwamba njia ambayo mwanadamu anaiendea ni matakwa ya Roho Mtakatifu kabisa, kwa sababu mwanadamu anaweza kupewa nuru na Roho Mtakatifu tu na hawezi kujazwa kikamilifu na Roho Mtakatifu. Vitu ambavyo mwanadamu anaweza kuvipitia vyote vipo ndani ya mawanda ya ubinadamu na haviwezi kuzidi mawanda ya fikira katika akili ya kawaida ya mwanadamu. Wale wote wenye maonyesho halisi wanapitia uzoefu ndani ya mawanda haya. Wanapoupitia ukweli, siku zote ni uzoefu wa maisha ya kawaida ya mwanadamu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu, sio kupitia uzoefu kwa namna ambayo inakengeuka kutoka kwa maisha ya kawaida ya mwanadamu. Wanapitia uzoefu wa ukweli ambao unatiwa nuru na Roho Mtakatifu katika msingi wa kuishi maisha yao ya kibinadamu. Aidha, ukweli huu unatofautiana kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine, na kina chake kinahusiana na hali ya mtu huyo. Mtu anaweza kusema kwamba njia anayoipitia ni maisha ya kawaida ya kibinadamu ya mwanadamu kufuatilia ukweli na kwamba hiyo ndiyo njia ambayo mtu wa kawaida ambaye amepata nuru ya Roho Mtakatifu anaipita. Huwezi kusema kwamba njia wanayoipitia ni njia ambayo inafuatwa na Roho Mtakatifu. Katika uzoefu wa kawaida wa binadamu, kwa sababu watu wanaoutafuta ukweli hawafanani, kazi ya Roho Mtakatifu pia haifanani. Aidha, kwa sababu mazingira wanayoyapitia na kiwango cha uzoefu wao havifanani, kwa sababu ya mchanganyiko wa akili na mawazo yao, uzoefu wao pia umechanganyika kwa kiwango tofauti. Kila mtu anaelewa ukweli kulingana na hali yake tofauti ya kibinafsi. Ufahamu wao wa maana halisi ya ukweli hauko kamili, na ni kipengele chake kimoja tu au vichache. Mawanda ambayo ukweli unaeleweka kwa mwanadamu siku zote umejikita katika hali tofauti tofauti za watu, na hivyo hazifanani. Kwa njia hii, maarifa yanayoonyesha ukweli ule ule na watu tofauti havifanani. Huu kusema, uzoefu wa mwanadamu siku zote una mipaka, na hauwezi kuwakilisha kikamilifu matakwa ya Roho Mtakatifu, na kazi ya mwanadamu haiwezi kuchukuliwa kama kazi ya Mungu, hata kama kile kinachoonyeshwa na mwanadamu kinafanana kwa karibu sana na mapenzi ya Mungu, hata kama uzoefu wa mwanadamu unakaribiana sana na kazi ya ukamilifu itakayofanywa na Roho Mtakatifu. Mwanadamu anaweza kuwa tu mtumishi wa Mungu, akifanya kazi ambayo Mungu amemwaminia. Mwanadamu anaweza kuonyesha maarifa tu chini ya nuru ya Roho Mtakatifu na ukweli alioupata kutokana na uzoefu wake binafsi. Mwanadamu hana sifa na hana vigezo vya kuwa njia ya Roho Mtakatifu. Hana uwezo wa kusema kuwa kazi ya mwanadamu ni kazi ya Mungu.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Ushirika wa mwanadamu unatofautiana na neno la Mungu. Kile ambacho mwanadamu hushiriki kinaeleza vile anavyotazama mambo na uzoefu wake, kinaonyesha kile wanachokiona na kupitia uzoefu kwa msingi wa kazi ya Mungu. Wajibu wao ni kutafuta, baada ya Mungu kufanya kazi au kuzungumza, kile wanachopaswa kufanya au kuingia kwacho, halafu kukiwasilisha kwa wafuasi. Hivyo, kazi ya mwanadamu inawakilisha kuingia au matendo yake. Bila shaka, kazi hiyo imechanganyika na masomo ya kibinadamu na uzoefu au mawazo ya kibinadamu. Haijalishi namna ambavyo Roho Mtakatifu anafanya kazi, ama Anavyomfanyia kazi mwanadamu au Mungu mwenye mwili, siku zote watenda kazi ndio wanaoonyesha vile walivyo. Ingawa ni Roho Mtakatifu ambaye hufanya kazi, kazi hiyo imejengwa katika msingi wa mwanadamu alivyo kiasili, kwa sababu Roho Mtakatifu hafanyi kazi pasipo msingi. Kwa maneno mengine, kazi haifanyiki pasipokuwa na kitu, lakini siku zote hufanyika kulingana na mazingira halisi na hali halisi. Ni kwa njia hii pekee ndiyo tabia ya mwanadamu inaweza kubadilishwa, kwamba mitazamo yake ya zamani na mawazo yake ya zamani yanaweza kubadilishwa. Kile ambacho mwanadamu huonyesha ni kile anachokiona, kupitia uzoefu na kukitafakari. Hata kama ni mafundisho au fikira, haya yote hufikiwa na fikira za mwanadamu. Bila kujali ukubwa wa kazi ya mwanadamu, haiwezi kuzidi mawanda ya uzoefu wa mwanadamu, kile ambacho mwanadamu huona, au kile ambacho mwanadamu anaweza kukitafakari au kuingia akilini mwake. Kile ambacho Mungu anaonyesha ndivyo hivyo Mungu Mwenyewe alivyo, na hii ni nje ya uwezo wa mwanadamu, yaani, nje ya uwezo wa kufikiri kwa mwanadamu. Anaonyesha kazi Yake ya kuwaongoza wanadamu wote, na hii haihusiani na undani wa uzoefu wa mwanadamu, badala yake inahusu usimamizi Wake. Mwanadamu anaonyesha uzoefu wake wakati Mungu anaonyesha nafsi Yake—nafsi hii ni tabia Yake ya asili na iko nje ya uwezo wa mwanadamu. Uzoefu wa mwanadamu ni kuona kwake na kupata maarifa kulingana na uonyeshaji wa Mungu wa nafsi Yake. Kuona kama huko na maarifa kama hayo yanaitwa asili ya mwanadamu. Yanaonyeshwa kwa msingi wa tabia asili ya mwanadamu na ubora wa tabia yake halisi; hivyo pia vinaitwa nafsi ya mwanadamu. Mwanadamu anaweza kushiriki kile anachokipitia na kukiona. Kile ambacho hajawahi kukipitia au kukiona au akili yake haiwezi kukifikia, yaani, vitu ambavyo havipo ndani yake, hawezi kuvishiriki. Ikiwa kile ambacho mwanadamu anakionyesha sio uzoefu wake, basi ni mawazo yake au mafundisho ya kidini. Kwa ufupi, hakuna ukweli wowote katika maneno yake. Kama hujawahi kukutana na maswala ya jamii, hutaweza kushiriki kwa uwazi kwenye mahusiano changamani katika jamii. Kama huna familia na watu wengine wanazungumza juu ya masuala ya familia, huwezi kuelewa kiasi kikubwa cha kile walichokuwa wakisema. Kwa hivyo, kile ambacho mwanadamu anakifanyia ushirika na kazi anayofanya vinawakilisha asili yake ya ndani.
kutoka katika “Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili
Nyaraka za Paulo za Agano Jipya ni nyaraka ambazo Paulo aliandika kwa ajili ya makanisa, na sio uvuvio wa Roho Mtakatifu, wala sio matamshi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu. Ni maneno tu ya kushawishi, faraja, na kutia moyo ambayo aliyaandika kwa ajili ya makanisa wakati wa kazi yake. Na hivyo pia, ni rekodi zaidi ya kazi na muda ya Paulo. Ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada wote katika Bwana, na zilikuwa ni kwa ajili ya kuwafanya kaka na dada wa makani yote ya wakati huo kufuata ushauri wake na kudumu siku zote katika njia zote za Bwana Yesu. … Yote aliyoyasema yale yaliyokuwa ni ya kuadilisha na mazuri kwa watu yalikuwa sahihi, lakini hayakuwa yanawakilisha matamshi ya Roho Mtakatifu, na hakuwa anamwakilisha Mungu. Ni uelewa mbaya kupita kiasi, na makufuru makubwa sana kwa watu kuchukulia rekodi za uzoefu wa mwanadamu na nyaraka za mwanadamu kama maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu kwa makanisa! Hiyo ni kweli kabisa tunapokuja katika nyaraka ambazo Paulo aliziandika kwa ajili ya makanisa, kwani nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya kaka na dada kulingana na mazingira na hali ya kila kanisa kwa wakati huo, na yalikuwa ni kwa ajili ya kuwashawishi kaka na dada katika Bwana, ili waweze kupokea neema ya Bwana Yesu. Nyaraka zake zilikuwa ni kwa ajili ya kuwaamsha kaka na dada wa wakati huo. Inaweza kusemwa kuwa huu ulikuwa ni mzigo wake mwenyewe, na pia ulikuwa ni mzigo aliopewa na Roho Mtakatifu; hata hivyo, alikuwa ni mtume aliyeyaongoza makanisa ya wakati huo, ambaye aliandika nyaraka kwa ajili ya makanisa na kuwashawishi, huo ulikuwa wajibu wake. Utambulisho wake ulikuwa tu ni mtume anayefanya kazi, na alikuwa ni mtume tu aliyetumwa na Mungu; hakuwa mtabiri, wala mtoa unabii. Kwa hivyo kwake, kazi yake mwenyewe na maisha ya kaka na dada yalikuwa na umuhimu mkubwa sana. Hivyo, asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu. Maneno yake hayakuwa maneno ya Roho Mtakatifu, wala yasingesemwa kuwa ni maneno ya Mungu, maana Paulo hakuwa chochote zaidi ya kiumbe wa Mungu, na hakika hakuwa Mungu aliyepata mwili. Utambulisho wake haukuwa sawa na ule wa Yesu. Maneno ya Yesu yalikuwa ni maneno ya Roho Mtakatifu, yalikuwa ni maneno ya Mungu, maana utambulisho wake ulikuwa ule wa Kristo—Mwana wa Mungu. Inawezekanaje Awe sawa na Paulo? Ikiwa watu wanaona nyaraka au maneno kama ya Paulo kama matamshi ya Roho Mtakatifu, na kuwaabudu kama Mungu, basi inaweza kusemwa tu kuwa ni watu wasiochagua kwa busara. Tukisema kwa ukali zaidi, haya sio makufuru? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na inawezekanaje watu wapigie magoti rekodi za nyaraka zake na maneno aliyoyazungumza kana kwamba yalikuwa ni kitabu kitakatifu, au kitabu cha mbinguni? Je, inawezekana maneno ya Mungu kutamkwa kwa kawaida na mwanadamu? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na hivyo, unasemaje—kwamba nyaraka alizoandika kwa ajili ya makanisa haziwezi kutiwa doa na mawazo yake mwenyewe? Inawezekanaje zisitiwe doa na mawazo ya kibinadamu? Aliandika nyaraka kwa ajili ya makanisa kulingana na uzoefu wake binafsi, na kiwango cha maisha yake binafsi. Kwa mfano, Paulo aliandika waraka kwa kanisa la Wagalatia ambao ulikuwa na maoni fulani, na Petro aliandika waraka mwingine, ambao ulikuwa na mtazamo mwingine. Ni upi kati ya hizo ulitoka kwa Roho Mtakatifu? Hakuna anayeweza kutoa jibu, hakika. Hivyo inaweza kusemwa tu kwamba wote wanawiwa na mzigo kwa makanisa, lakini barua zao zinawakilisha kimo chao, zinawakilisha vile wanavyowapatia na kuwasaidia kaka na dada, na vile wanavyowiwa na makanisa, na zinawakilisha tu kazi ya binadamu; hayakuwa ya Roho Mtakatifu kabisa. Ikiwa unasema kwamba nyaraka zake ni maneno ya Roho Mtakatifu, basi wewe ni mpumbavu, na unafanya makufuru! Nyaraka za Paulo na nyaraka nyingine za Agano Jipya ni sawa na kumbukumbu za viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni. Zipo sawa na vitabu vya Watchman Nee au uzoefu wa Lawrence, na kadhalika. Ni vile tu vitabu vya viongozi mashuhuri wa kiroho wa hivi karibuni havijajumuishwa katika Agano Jipya, lakini hulka ya watu hawa ni sawa: Kulikuwa na watu ambao walitumiwa na Roho Mtakatifu wakati fulani, na hawakuweza kumwakilisha Mungu moja kwa moja.
kutoka katika “Kuhusu Biblia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili
Neno la Mungu haliwezi kuzungumzwa kama neno la mwanadamu, sembuse neno la mwanadamu kuzungumzwa kama neno la Mungu. Mwanadamu anayetumiwa na Mungu siye Mungu mwenye mwili, na Mungu mwenye mwili siye mwanadamu anayetumiwa na Mungu; katika hili, kunayo tofauti kubwa sana. Pengine, baada ya kusoma maneno haya, hukubali kuwa ni maneno ya Mungu, na kuyakubali tu kama maneno ya mwanadamu ambaye amepewa nuru. Ikiwa hivyo, basi umepofushwa na ujinga. Maneno ya Mungu yatawezaje kuwa sawa na maneno ya mwanadamu ambaye amepewa nuru? Maneno ya Mungu mwenye mwili yanaanzisha enzi mpya, yanaongoza wanadamu wote, yanafichua mafumbo, na kumwonyesha mwanadamu mwelekeo mbele katika enzi mpya. Nuru anayoipata mwanadamu ni utendaji au elimu rahisi. Haiwezi kuelekeza binadamu wote kuingia enzi mpya au kufichua fumbo la Mungu Mwenyewe. Mungu, hata hivyo, ni Mungu, na mwanadamu ni mwanadamu. Mungu yuko na dutu ya Mungu, na mwanadamu yuko na dutu ya mwanadamu. Iwapo mwanadamu anachukulia maneno yanayonenwa na Mungu kama kupewa nuru tu na Roho Mtakatifu, na kuchukua maneno yaliyonenwa na mitume na manabii kama maneno yaliyonenwa na Mungu Mwenyewe, basi mwanadamu anakosea. Licha ya haya, hufai kamwe kubadili jambo sahihi liwe baya, ama kuzungumzia lililo juu kama la chini, au kuzungumzia jambo kubwa kama lisilo na kina; haijalishi ni nini, hupaswi kamwe kwa makusudi kupinga lile unalojua kuwa ni ukweli. Kila anayeamini kuwa kuna Mungu anapaswa kufikiri juu ya tatizo hili kwa msimamo ulio sahihi, na anapaswa kukubali kazi Yake mpya na maneno Yake kama kiumbe wa Mungu—la sivyo aondolewe na Mungu.
kutoka katika Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni