59. Uzoefu wa Kutenda Ukweli
Hengxin Jiji la Zhuzhou, Mkoa wa Hunan
Sio muda mrefu mno uliopita, nilisikia "Ushirika na Kuhubiri Kuhusu Kuingia kwa Maisha," jambo ambalo lilinielekeza kuelewa kwamba ni wale tu wanaotenda ukweli wanaoweza kupata ukweli na hatimaye kuwa wale ambao wanaomiliki ukweli na ubinadamu hivyo kupata kibali cha Mungu. Kuanzia hapo kwendelea, kwa makusudi nilifanya jitihada za kuunyima mwili wangu na kutenda ukweli katika maisha yangu ya kila siku.
Wakati fulani baadaye, nilitambua kwa furaha kwamba ningeweza kutenda ukweli kiasi. Kwa mfano, siku za nyuma niliogopa kuonyesha upande wangu mwovu kwa wengine. Sasa kwa makusudi nilikuwa wazi na ndugu wa kiume na wa kike, nikichangua tabia yangu potovu. Kabla, wakati nilipopogolewa na kushughulikiwa, ningetoa udhuru na kukwepa wajibu. Sasa nilifanya jitihada makusudi kujikana badala ya kujaribu kuhalalisha tabia yangu mbaya. Katika siku za nyuma, nilipopata msuguano na wenzangu kazini, nilikuwa na mawazo finyu, uchwara na wa kuelekea kununa. Sasa nilipokabiliwa na hali hizo ningeunyima mwili wangu na kutumia stahamaha na subira na wengine. … Kila wakati nilipofikiria maendeleo yangu katika kutenda ukweli, ningejihisi kuwa na furaha mno. Nilidhani kuwa uwezo wangu wa kutenda ukweli kiasi ulimaanisha kwamba nilikuwa mweledi halisi wa ukweli. Kwa njia hii, bila kujua nikawa mwenye maringo na wa kujipongeza.
Siku moja, nilikuwa nikisomasoma “Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo” na nikapata kwa kibahati maneno yafuatayo ya Mungu: "Watu wengine husema: Ninahisi kuwa nina uwezo wa kuweka ukweli fulani katika matendo sasa, sio kwamba siwezi kuweka ukweli wowote katika matendo. Katika mazingira mengine, ninaweza kufanya mambo kulingana na ukweli, ambako kumaanisha nahesabika kama mtu anayeweka ukweli katika matendo, na nahesabika kama mtu mwenye ukweli. Kwa kweli, kinyume na hali za zamani, au kinyume na wakati ulipomwamini Mungu mara ya kwanza, kuna mabadiliko machache. Katika siku za nyuma, hukuelewa chochote, na hukujua ukweli ulikuwa nini au tabia potovu ilikuwa nini. Sasa unajua mambo fulani na unaweza kuwa na matendo fulani mazuri, lakini hii ni sehemu ndogo tu ya mabadiliko hayo; sio mabadiliko ya tabia yako kwa kweli, kwa sababu huwezi kutekeleza ukweli mkomavu na wa kina ambao unahusisha asili yako. Tofauti na siku zako zilizopita, kwa kweli una mabadiliko fulani, lakini mabadiliko haya ni mabadiliko machache tu ya ubinadamu wako, na yakilinganishwa na hali ya juu ya ukweli, wewe bado uko mbali sana na lengo. Hii ni kusema kwamba hujafikia lengo wakati unaweka ukweli katika matendo.” Baada ya kusoma maneno haya, sikuweza kujizuia kushtuka. Yote ambayo nimefanikisha yalikuwa ni tabia chache nzuri? Bado niko mbali na kutenda ukweli kwa uhalisi? Je, nini basi, nilifikiri, inamaanisha kutenda ukweli kwa uhalisi? Nilianza kuchunguza jibu halisi la swali hili. Baadaye, katika ushirika wa mwanadamu, niliona maneno yafuatayo: "Wale ambao kwa shauku hutenda ukweli wanaweza kumudu gharama na wako tayari kuzikubali shida zinazohusika. Kwa dhahiri, mioyo yao imejaa furaha na raha. Wale ambao wako tayari kutenda ukweli hawatawahi kufanya kitu tu kwa namna isiyo ya dhati kamwe kwa sababu hawafanyi tu kwa sababu ya monyesho. Dhamiri na sababu wanazomiliki kama wanadamu wa kawaida huwalazimisha kutenda sehemu yao kama viumbe wa Mungu. Kwao, kutenda ukweli ndicho kiini cha kuwa binadamu; ni sifa ambayo yule aliye na ubinadamu wa kawaida anapaswa kumiliki" ("Ukweli Lazima Utendwe Kwa Moyo" katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo na Viongozi na Wafanyakazi wa Kanisa). Baada ya kusoma hili, hatimaye nilielewa: Wataalamu halisi wa ukweli wanaweza kutenda ukweli kwa sababu wanaelewa kusudi la kufanya hivyo. Wao hujua kwamba kutenda ukweli ndiyo maana ya kuwa binadamu, sifa ambyao wanadamu wanapaswa kuwa nayo. Kwa hiyo, hawafanyi hivyo kwa maonyesho; huwa wanauona kama wajibu wao. Wako tayari kuvumilia shida na kulipa gharama; hawana malengo ya kibinafsi na tamaa. Lakini nilitendaje ukweli? Wakati nikifichua tabia zangu potovu, huenda nilikuwa wazi na kuzifunua kwa ndugu zangu wa kiume na wa kike, lakini katika moyo wangu nilikuwa nikifikiria, "Mnaona jinsi ninavyotenda ukweli? Ninaweza kuweka wazi tabia zangu potovu. Hilo linanifanya kuwa bora kuliko ninyi, naam?" Wakati nilipopogolewa na kushughulikiwa, naweza kuwa sikutoa udhuru kwa sauti, lakini ndani nilikuwa nikisema "Ona? Huwa sitoi udhuru tena. Nimekuwa mzuri sana. Labda ninastahili kama mtu ambaye yuko tayari kuukubali ukweli sasa, naam?" Wakati nilipokuwa na msuguano na wenzangu kazini, huenda kwamba nilijaribu kwa makusudi kujizuia mwenyewe na kuepuka mlipuko wowote, lakini moyoni mwangu nilikuwa nikifikiria, "Mnaona? Mimi si kama nilivyokuwa kabla, kuwa uchwara na mwenye mawazo finyu. Nimebadilika, naam?" … Wakati nilipofikiri jinsi nilivyokuwa nikitenda ukweli, hatimaye niligundua kuwa sikuwa kwa kweli natenda ukweli. Nilikuwa nimejaa nia zangu na tamaa zangu. Nilikuwa nikilifanya kwa sababu ya maonyesho. Nilitaka watu wengine kunipenda na kunisifu. Ningewezaje kusema kwamba nilikuwa nikitenda ukweli kwa sababu nilielewa umuhimu wake? Nilikuwa nikifanyaje hili ili kumridhisha Mungu wangu? Nilikuwa nikifanya hili ili kujiridhisha na kujionyesha kwa wengine. Nilikuwa nikimshutumu na kumlaghai Mungu. Kwa uhalisi, nilikuwa nausaliti ukweli. Kanuni yangu inayodaiwa kuwa "kutenda ukweli" ilikuwa tu kufuata desturi. Lilikuwa ni zoezi la kizuizi, kukoma kwa tabia fulani mbaya. Lilikuwa tu badiliko la nje. Nilikuwa na bado niko mbali sana na kufikia viwango vinavyotakiwa kwa mweledi wa ukweli. Hata hivyo, sio tu kuwa nilifikiri kwa kujipujua kwamba nilikuwa mweledi wa ukweli, hata nilikuja kuwa wa kujipongeza kama matokeo. Tabia yangu ilikuwa kweli iliyovuka mpaka!
Mungu, asante kwa nuru Yako na mwongozo Wako. Asante kwa kunionyeshea kwamba sikuwa mweledi wa kweli wa ukweli na kwamba utekelezaji wangu wa ukweli haukufikia viwango Vyako. Kuanzia siku hii kwendelea, niko tayari kuchunguza nia zangu mwenyewe na kushikilia viwango vinavyohitajiwa kutenda ukweli. Nitajioondolea uchafu na kuwa mweledi wa ukweli.
kutoka kwa Ushuhuda wa Kuipitia Hukumu ya Kristo
Yaliyopendekezwa: Kuhusu Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni