Ulishuhudia kuwa Bwana amerejea na hufanya kazi Yake ya hukumu akianza kwa nyumba ya Mungu katika siku za mwisho. Hili linaonekana kuwa tofauti na hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe katika Kitabu cha Ufunuo. Kile watu wengi katika dini wanachofikiria ni kwamba hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe imelenga wasioamini walio wa pepo Shetani. Bwana atakapokuja, waumini watachukuliwa kwenda mbinguni, na kisha Atatuma maafa kuwaangamiza wasioamini. Hiyo ndiyo hukumu mbele ya kiti cha enzi kikubwa cheupe. Unashuhudia mwanzo wa hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, lakini hatujaona Mungu akileta maafa kuwaangamiza wasioamini. Basi inawezaje kuwa hukumu ya kiti cha enzi kikubwa cheupe?
Jibu:
Wale wote ambao wanaelewa Biblia wanajua kuwa hukumu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi iliyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo ni maono ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Mwenyezi Mungu mwenye mwili Alikuja kuonyesha ukweli na kufanya kazi Yake katika siku za mwisho, Akianza kuwatakasa na kuwaokoa binadamu potovu. Hii inamaanisha hukumu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi imeanza tayari. Hukumu lazima ianzie kutoka nyumba ya Mungu. Mungu kwanza Ataunda kikundi cha washindi kabla ya maafa. Kisha, Mungu ataleta chini maafa makubwa na kuanza kuyazawadia mazuri na kuadhibu maovu, hadi hii enzi ya uovu iangamizwe. Hukumu ya Mungu ya kiti kikubwa cheupe cha enzi katika siku za mwisho basi itakamilika kabisa.