Bwana Yesu alitundikwa msalabani kama sadaka ya dhambi kwa mwanadamu, na hivyo akitukomboa kutoka kwa dhambi. Tukipotea kutoka kwa Bwana Yesu na kumwamini Mwenyezi Mungu, si huu utakuwa usaliti wa Bwana Yesu? Si huu utakuwa uasi?
Jibu:
Katika siku za mwisho sasa, wakati ambapo Mungu amefanya kazi mpya na kuchukua jina jipya, tunamsaliti Mungu au tunaenda mwendo sawa na kazi ya Mungu? tulipoliacha jina la Yesu na kukubali jina la Mwenyezi Mungu? Mungu anapoanzisha kazi mpya, mwanadamu anaweza tu kuokolewa kwa kuenda mwendo sawa na kazi ya Mungu. Hii ni kweli. Tunaweza kuona kutoka kwa neno la Mwenyezi Mungu, sababu ya Mungu kuchukua jina “Mwenyezi Mungu” ilihusiana na kazi inayofanywa katika siku za mwisho na tabia inayoonyeshwa na Mungu. Mwenyezi Mungu asema, “Mungu Anapopata mwili mara hii, kazi Yake ni kuonyesha tabia Yake, kimsingi kupitia kuadibu na hukumu.
Akitumia haya kama msingi, Analeta ukweli zaidi kwa mwanadamu, kuonyesha njia zaidi za matendo, na hivyo Hufikia lengo Lake la kumshinda mwanadamu na kumwokoa mwanadamu kutokana na tabia yake potovu. Hili ndilo liko katika kazi ya Mungu katika Enzi ya Ufalme” (Dibaji ya Neno Laonekana katika Mwili). Kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni kuhukumu na kuadibu watu wapotovu, kuweka watu katika aina zao na kumaliza enzi. Kwa sababu ya ukombozi wa Bwana Yesu, dhambi zetu ziliwasamehewa. Lakini bila shaka, hatujajitenga kabisa na dhambi. Tabia zetu zote bado ni zenye kiburi, ubinafsi, tamaa, udanganyifu na uovu. Tumenaswa katika mzunguko mwovu wa kutenda dhambi wakati wa mchana na kutubu usiku, tukitegemea neema kwa ajili ya wokovu. Hivyo, ili kutuokoa kabisa, Mungu anaongea katika siku za mwisho na tabia Yake yenye haki, uadhama na isiyokosewa, na kufanya kazi Yake mpya ya hukumu, kuadibu, kushinda na kumtakasa mwanadamu, Akituletea kabisa enzi mpya—Enzi ya Ufalme. Hatua ya kazi iliyofanywa na Mungu katika siku za mwisho haionyeshi miujiza. Kila kitu kinatimizwa na maneno. Dhambi, uasi na udhalimu wa mwanadamu vinahukumiwa na kuadibiwa na neno la Mungu, hivyo kumtakasa kabisa mwanadamu na kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, ambayo kwayo tunaweza kuona kuwa Mungu ni Mwenye kudura na busara. Mungu hakika ni Mwenyezi Mungu Mwenyewe. Ni Mungu aliyeumba vitu vyote na hutawala kila kitu! Kwa hivyo watu wanamsujudia Mungu na kumwabudu Mungu. Wakati huo huo, jina “Mwenyezi Mungu” hutumiwa ili kumaliza kabisa juhudi za vita vya miaka elfu sita dhidi ya Shetani.
Kazi ya Mungu ya hukumu na kuadibu katika siku za mwisho pia ni kazi ya kuchambua wanadamu kulingana na aina zao wenyewe. Hii inatimiza unabii wa 1 Petro 4:17, “Kwa maana muda umekuja ambao lazima hukumu ianze katika nyumba ya Mungu.” Hii pia inatimiza unabii wa kutofautisha kondoo na mbuzi, ngano na magugu na mtumishi nzuri na mtumishi mbaya. Hii ni kazi ambayo Mungu hufanya katika siku za mwisho. Tutalielewa baada ya kusoma vifungu kadhaa vya neno la Mungu.
“Kazi ya siku za mwisho ni kutenganisha vitu vyote kulingana na jinsi yavyo, kuhitimisha mpango wa usimamizi wa Mungu, kwa maana muda u karibu na siku ya Mungu imewadia. Mungu huwaleta wote ambao wameingia katika ufalme Wake, yaani, wale wote ambao wamekuwa waaminifu Kwake mpaka mwisho, katika enzi ya Mungu Mwenyewe. Hata hivyo, kabla ya kuja kwa enzi ya Mungu Mwenyewe, kazi Atakayofanya Mungu si kutazama matendo ya mwanadamu wala kuchunguza maisha ya wanadamu, ila ni kuhukumu uasi wake, kwa maana Mungu atawatakasa wale wote wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi. Wale wote ambao wamefuata nyayo za Mungu mpaka siku hii ni wale ambao wamekuja mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na kwa hivyo, watu wote wanaokubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha utakaso wa Mungu. Kwa maneno mengine, wale wote wanaoikubali kazi ya Mungu katika awamu yake ya mwisho ni chombo cha hukumu ya Mungu.
“‘Hukumu’ katika maneno yaliyonenwa awali—hukumu itaanza na nyumba ya Mungu—inarejelea hukumu ambayo Mungu anatoa leo kwa wale wanaokuja mbele ya kiti Chake cha enzi katika siku za mwisho” (“Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Ni kwa njia ya kuadibu na hukumu ndipo mwisho wa mambo yote yatafunuliwa. Mwanadamu huonyesha tu ukweli ulio ndani yake anapoadibiwa na kuhukumiwa. Mabaya yataekwa na mabaya, mema na mema, na wanadamu watabainishwa kulingana na aina. Kupitia kuadibu na hukumu, mwisho wa mambo yote utafichuliwa, ili mabaya yaadhibiwe na mazuri yatunukiwe zawadi, na watu wote watakuwa wakunyenyekea chini ya utawala wa Mungu. Kazi hii yote inapaswa kutimizwa kupitia kuadibu kwa haki adhibu na hukumu. Kwa sababu upotovu wa mwanadamu umefika upeo wake na uasi wake umekua mbaya mno, ni haki ya tabia ya Mungu tu, ambayo hasa ni ya kuadibu na hukumu, na imefichuliwa kwa kipindi cha siku za mwisho, inayoweza kubadilisha na kukamilisha mwanadamu. Ni tabia hii pekee ambayo itafichua maovu na hivyo kuwaadhibu watu wote dhalimu. Kwa hivyo, tabia kama hii imejazwa umuhimu wa wakati, na ufunuo na maonyesho ya tabia yake ni kwa ajili ya kazi ya kila enzi mpya. Mungu hafichui tabia yake kiholela na bila umuhimu. Kama, wakati wa mwisho wa mwanadamu umefichuliwa katika kipindi cha siku za mwisho, Mungu bado anamfadhili binadamu kwa huruma na upendo usioisha, kama yeye bado ni wa kupenda mwanadamu, na kumkabili hukumu ya haki, bali anamwonyesha stahamala, uvumilivu, na msamaha, kama bado Yeye anamsamehe mwanadamu bila kujali ubaya wa makosa anayofanya, bila hukumu yoyote ya haki, basi kungekuwepo na mwisho wa usimamizi wa Mungu? Ni wakati gani tabia kama hii itaweza kuwaongoza wanadamu katika hatima inayofaa? Chukua, kwa mfano, hakimu ambaye daima ni mwenye upendo, mwenye roho safi na mpole. Anawapenda watu bila kujali dhambi wanazozifanya, na ni mwenye upendo na stahamala kwa watu bila kujali hao ni nani. Kisha ni lini ambapo ataweza kufikia uamuzi wa haki? Katika siku za mwisho, ni hukumu ya haki tu inaweza kubainisha mwanadamu na kuleta mwanadamu katika utawala mpya. Kwa njia hii, enzi nzima inafikishwa mwisho kupitia kwa tabia ya Mungu iliyo ya haki ya hukumu na kuadibu” (“Maono ya Kazi ya Mungu (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili). Neno la Mungu linatuambia waziwazi kwamba kazi ya msingi ya Mungu katika siku za mwisho ni kuainisha vitu vyote kulingana na aina zao. Pia ni kazi ya kumhukumu na kumwadibu mwanadamu kwa neno, kuhukumu dhambi ya mwanadamu na kuadibu uasi wa mwanadamu na udhalimu, kumgeuza kabisa mwanadamu na kumfanya mwanadamu awe mkamilifu. Wote wanaokubali na kutii kazi ya Mungu katika siku za mwisho ni walengwa wa hukumu na utakaso wa Mungu. Hukumu ya haki ya Mungu pekee ndiyo inaweza kumwokoa mwanadamu, kumkamilisha mwanadamu na kumleta katika ufalme mpya. Na Mwokozi Yesu mwenye upendo na huruma alifanya tu kazi ya kusamehe dhambi ya mwanadamu. Hakuwa afanye kazi ya kumtakasa na kumbadilisha mtu, sembuse kuchambua watu kulingana na aina zao. Kwa hivyo, kwa kukubali tu kazi ya hukumu na adhabu ya neno la Mwenyezi Mungu, kwa kuheshimu jina la Mwenyezi Mungu kama lililo kuu, ndiyo mwanadamu anaweza kupokea wokovu kamili wa Mungu. Tukilitetea jina la Bwana Yesu lakini tulikatae jina la Mwenyezi Mungu, hatutapokea ukweli na wokovu kwa wanadamu kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho.
kutoka katika Majibu kwa Maswali ya Tamthilia
Mwenyezi Mungu ni Yehova Mungu, aliyetoa sheria ili kuongoza maisha ya watu, na Yeye ndiye Bwana Yesu aliyesulubiwa msalabani ili kukomboa wanadamu. Kazi ya hukumu iliyofanywa na Mwenyezi Mungu, kazi ya ukombozi iliyofanywa na Bwana Yesu, na kazi ya sheria iliyofanywa na Yehova Mungu—hii yote ilifanywa na Mungu mmoja. Mungu anamuokoa mwanadamu kwa hatua moja kila wakati, kulingana na mpango Wake, na mahitaji ya mwanadamu.
Basi kukubali jina la Mwenyezi Mungu sio kukosa shukrani kwa Bwana Yesu, au kumsaliti, lakini ni kufuata nyayo za Mwanakondoo, kushika njia ya Mungu, na kumfuata kwa uaminifu. Mungu anakubali hili, kama ilivyoandikwa katika Ufunuo 14:4, “Hao ndio wale wanaomfuata Mwanakondoo popote aendapo. Hawa walikombolewa kutoka miongoni mwa wanadamu, wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na Mwanakondoo.” Wote wanaoshikilia jina la Yesu na kukataa kukubali Mwenye Mungu hakika watakuwa wasaliti wa Mungu, na Atawaangamiza. Kama ilivyokuwa wakati Mungu alipokuja kufanya kazi na jina la Yesu, wanafunzi wote waliokubali kazi mpya ya Mungu na kumfuata Bwana Yesu hawakuwa wanaacha njia ya kweli au kumsaliti Yehova Mungu. Badala yake, walikuwa wanafuata nyayo za Mungu, na ni wao tu walikuwa waaminifu kwa Mungu. Mafarisayo walioamini kuwa walikuwa waaminifu kwa Yehova Mungu walishikilia jina Lake, na kukataa Bwana Yesu. Kwa hivyo, hawakukosa tu kusifiwa na Yehova Mungu, bali pia walielekezewa laana na adhabu ya Mungu. Hivyo tunapaswa kujifunza somo kutokana na kufeli kwa Mafarisayo, tukubali jina la Mwenyezi Mungu na tufuate nyayo za Mungu. Hii ndio njia pekee ya kupata wokovu wa Mungu.
kutoka katika Majibu kwa Maswali ya Tamthilia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni