Wewe hushuhudia kuwa Mungu Mwenyezi huonyesha ukweli na hufanya kazi Yake ya hukumu ya siku za mwisho. Nadhani kuwa imani yetu katika Bwana Yesu na kukubali kazi ya Roho Mtakatifu inamaanisha kuwa tayari tumepitia kazi ya Mungu ya hukumu. Hapa kuna maneno ya Bwana Yesu kama ushahidi: “Nisipoenda, Mfariji hatakuja kwenu; lakini nikiondoka, nitamtuma kwenu. Na wakati atakuja, ataushutumu ulimwengu kuhusu dhambi, na kuhusu haki, na kuhusu hukumu” (Yohana 16:7-8). Tunaamini kwamba, ingawa kazi ya Bwana Yesu ilikuwa kazi ya ukombozi, baada ya kupaa mbinguni na siku ya Pentekoste, Roho Mtakatifu alishuka na kufanya kazi kwa wanadamu: “… ataushutumu ulimwengu kuhusu dhambi, na kuhusu haki, na kuhusu hukumu.” Inafaa kuwa kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho, kwa hiyo ninachopenda kukifuatilia ni, ni nini hasa tofauti kati ya kazi ya hukumu katika siku za mwisho zinazofanywa na Mwenyezi Mungu na kazi ya Bwana Yesu?
Jibu:
Kwa kuwa mnatambua aliyofanya Bwana Yesu ilikuwa kazi ya ukombozi, na njia aliyoleta ni: “Tubuni: kwa kuwa ufalme wa mbinguni u karibu” (Mathayo 4:17), basi mlikuwa na msingi gani kuamua kwamba Roho Mtakatifu alikuja katika Pentekoste kufanya kazi ya hukumu katika siku za mwisho? Mlitumia tu msingi wa neno la Bwana Yesu ambalo lilisema, “Nisipoenda, Mfariji hatakuja kwenu; lakini nikiondoka, nitamtuma kwenu. Na wakati atakuja, ataushutumu ulimwengu kuhusu dhambi, na kuhusu haki, na kuhusu hukumu” (Yohana 16:7-8), mnathubutu kuwa na uhakika kwamba kazi iliyofanywa na Roho Mtakatifu ilikuwa kazi ya hukumu katika siku za mwisho, kuna msingi wowote kulingana na neno la Mungu? Je, Bwana Yesu alisema “Roho Mtakatifu amekuja.
Anayofanya ni kazi ya hukumu ya siku za mwisho”? Bwana Yesu hakuwa amewahi kusema hayo. Bwana Yesu alisema dhahiri, “Na iwapo mtu yeyote atayasikia maneno yangu, na asiyaamini, Mimi sitamhukumu: kwa kuwa mimi sikuja ili niihukumu dunia, bali kuiokoa dunia. Yeye ambaye ananikataa mimi, na hayakubali maneno yangu, ana yule ambaye anamhukumu: neno hilo ambalo nimelisema, ndilo hilo ambalo litamhukumu katika siku ya mwisho” (Yohana 12:47-48). Bwana Yesu alifanya wazi kabisa kwamba kile alichofanya sio kazi ya hukumu. Bwana Yesu ataonyesha tu ukweli unaohusu kufanya kazi ya hukumu wakati Atakaporudi katika siku za mwisho. Ili kuwa na uhakika, si sawa kwa watu wengine kutaja kazi ya Roho Mtakatifu katika Enzi ya Neema kama kazi ya hukumu ya Mungu. Kwa kawaida, tunahitaji usisimuaji, nuru, na mwangaza wa Roho Mtakatifu ili tupate ukiri na toba ya dhambi ya kweli. Hata hivyo, kukiri na kutubu mbele ya Bwana kwa machozi machungu, ni matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu, ambayo ni tofauti kabisa na kazi ya Mungu ya hukumu katika siku za mwisho. Hebu tusikie vifungu viwili vya neno la Mwenyezi Mungu na tutaelewa kazi ya hukumu ni nini.
Mwenyezi Mungu asema, “Ikifika kwa neno ‘hukumu,’ utawaza juu ya maneno ambayo Yehova alizungumza kila mahali na pia maneno ya kukaripia ambayo Yesu aliwaambia Mafarisayo. Ingawa maneno haya ni yenye ukali, sio hukumu ya Mungu kwa mwanadamu; maneno tu ambayo yamezungumzwa na Mungu katika mazingira tofauti, yaani, mandhari tofauti, maneno haya ni tofauti kabisa na yale maneno anayonena Kristo wakati Anamhukumu mwanadamu siku za mwisho. Katika siku za mwisho, Kristo anatumia ukweli tofauti kumfunza mwanadamu, kufichua kiini cha mwanadamu, na kuchangua maneno na matendo yake. Maneno haya yanajumuisha ukweli mbalimbali, kama vile wajibu wa mwanadamu, jinsi mwanadamu anavyofaa kumtii Mungu, jinsi mwanadamu anavyopaswa kuwa mwaminifu kwa Mungu, jinsi mwanadamu anavyostahili kuishi kwa kudhihirisha ubinadamu wa kawaida, na pia hekima na tabia ya Mungu, na kadhalika. Maneno haya yote yanalenga nafsi ya mwanadamu na tabia yake potovu. Hasa, maneno hayo yanayofichua vile mwanadamu humkataa Mungu kwa dharau yanazungumzwa kuhusiana na vile mwanadamu alivyo mfano halisi wa Shetani na nguvu ya adui dhidi ya Mungu. Mungu anapofanya kazi Yake ya hukumu, Haiweki wazi asili ya mwanadamu kwa maneno machache tu; Anafunua, kushughulikia na kupogoa kwa muda mrefu. Mbinu hizi za ufunuo, kushughulika, na kupogoa haziwezi kubadilishwa na maneno ya kawaida, ila kwa ukweli ambao mwanadamu hana hata kidogo. Mbinu kama hizi pekee ndizo huchukuliwa kama hukumu; ni kwa kupitia kwa hukumu ya aina hii pekee ndio mwanadamu anaweza kutiishwa na kushawishiwa kabisa kujisalimisha kwa Mungu, na zaidi ya hayo kupata ufahamu kamili wa Mungu. Kile ambacho kazi ya hukumu humletea mwanadamu ni ufahamu wa uso halisi wa Mungu na ukweli kuhusu uasi wake mwenyewe. Kazi ya hukumu humruhusu mwanadamu kupata ufahamu zaidi wa mapenzi ya Mungu, wa makusudi ya kazi ya Mungu, na wa mafumbo yasiyoweza kueleweka kwa mwanadamu. Pia inamruhusu mwanadamu kutambua na kujua asili yake potovu na asili ya upotovu wake, na pia kugundua ubaya wa mwanadamu. Matokeo haya yote huletwa na kazi ya hukumu, kwa maana asili ya kazi ya aina hii hasa ni kazi ya kuweka wazi ukweli, njia, na uhai wa Mungu kwa wale wote walio na imani ndani Mwake. Kazi hii ni kazi ya hukumu inayofanywa na Mungu” (“Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili).
“Kazi ya hukumu ni kazi ya Mungu Mwenyewe, kwa hivyo lazima ifanywe na Mungu Mwenyewe kwa kawaida; haiwezi kufanywa na mwanadamu kwa niaba Yake. Kwa sababu hukumu ni kumshinda mwanadamu kupitia ukweli, hakuna shaka kuwa Mungu bado Anaonekana kama kiumbe aliyepata mwili kufanya kazi hii miongoni mwa wanadamu. Hiyo ni kumaanisha, wakati wa siku za mwisho, Kristo atautumia ukweli kuwafunza wanadamu duniani kote na kufanya ukweli wote ujulikane kwao. Hii ni kazi ya hukumu ya Mungu” (“Kristo Hufanya Kazi ya Hukumu kwa Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Kazi ya hukumu ya Mungu ni fumbo. Bila ya ufunuo wa Mungu, hakuna mtu anayeweza kuibaini—na huu ni ukweli. Mwenyezi Mungu ameeleza waziwazi hukumu ni nini na matokeo ya kazi ya hukumu. Baada ya kuyasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, tunafahamu zaidi kuhusu kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho ni kutakasa kabisa na kuwaokoa wanadamu. Sio tu kusema maneno machache ya kukaripia au kulaani kwa mtu. Wala maonyesho ya vifungu vichache vya maneno haya hayawezi kuwaweka watu huru kutoka utumwani mwa dhambi ili kupokea utakaso na wokovu wa Mungu. Mungu anahitaji kuonyesha maneno ya kutosha kuelezea vipengele vyote vya ukweli ambavyo wanadamu waliopotoka wanapaswa kuelewa na kuingia ili kupokea utakaso na wokovu, na kufunua mafumbo yote ya mpango Wake wa usimamizi kwa wanadamu. Hii ni mamia, hata maelfu ya mara, zaidi ya maneno yaliyoonyeshwa na Bwana Yesu katika Enzi ya Neema. Kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho inalenga kuonyesha ukweli na neno la hukumu, kuhukumu na kufunua asili ya mtu ya kishetani ambayo inampinga na kumdharau Mungu, na ukweli wa upotovu wa mtu na Shetani, ikifichua kabisa tabia takatifu, ya haki na isiyokosewa ya Mungu. Vipengele vyote vya ukweli kuhusu nia ya Mungu na matakwa ya wanadamu, ni aina gani ya watu watapokea wokovu au adhabu, na kadhalika, vinafichuliwa kwetu. Kwa kupitia kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho, tunaelewa kusudi la mpango wa usimamizi wa Mungu. Tunaweza kutofautisha kati ya mambo mazuri na mabaya, na kuona wazi uso wa kipepo wa Shetani ambaye humpinga Mungu kwa kichaa. Tunabaini ukweli wa kupotoshwa kwa kina kwa mwanadamu na Shetani na kutambua asili yetu ya Shetani ambayo inakataa na kumsaliti Mungu. Kuhusiana na tabia ya haki, yenye kudura, na hekima ya Mungu na yote kuhusu mali ya Mungu na nafsi, tunapata ufahamu kiasi wa kweli na kuzaa moyo wa kumwogopa Mungu. Tunaanguka chini kwa aibu, tukihisi kuwa hatukustahili kuishi mbele ya Mungu. Tunajidharau na kujinyima, hatua kwa hatua tunajitenga na mbano wa dhambi, kuishi kwa kudhihirisha mfano wa mtu halisi na kuwa na hofu ya kweli na utiifu kwa Mungu. Haya ni matokeo ya kupitia kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho. Ni kazi ya aina hii tu ndiyo kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho.
Hebu basi tuangalie Enzi ya Neema. Bwana Yesu alifanya tu kazi ya ukombozi na kuhubiri njia ya toba, Akionyesha tu pande za tabia ya Mungu yenye huruma na upendo kwa mwanadamu. Ingawa Bwana Yesu pia alisema baadhi ya maneno ya kumhukumu mtu, kuwashutumu na kuwatukana Mafarisayo, haya hayakuwa malengo ya kazi Yake. Bwana Yesu alifanya tu kazi ya ukombozi ambayo ililenga juu ya msamaha wa dhambi, kufundisha toba na kutoa neema. Haikuwa kazi iliyozingatia juu ya kuhukumu na kutakasa dhambi za mwanadamu. Hivyo kazi ya Bwana Yesu ilizunguka tu kazi ya ukombozi na Alionyesha maneno machache ambayo yaliwafundisha watu jinsi ya kutubu na kuungama dhambi, jinsi ya kuwa wanyenyekevu na wenye subira, jinsi ya kubatizwa, kubeba msalaba, kuteseka, nk. Kwa kuamini katika Bwana, tunahitaji tu kufuata neno la Bwana kukiri na kutubu, basi dhambi zetu zingesamehewa. Hatungetiwa hatia tena na sheria na kuhukumiwa kifo. Tungekuwa wenye sifa ya kumwomba Mungu na kufurahia neema na baraka za Mungu. Haya yalikuwa matokeo yaliyofanikishwa na kazi ya ukombozi wa Mungu katika Enzi ya Neema, ambayo yalikuwa tofauti kabisa na yale ya kazi ya hukumu katika siku za mwisho. Hata hivyo, watu wengine wanaamini kwamba, kwa kupitia kazi ya Roho Mtakatifu katika Enzi ya Neema na kupokea nuru, kemeo na nidhamu ya Roho Mtakatifu, kwa kuwa na kwa kuomba kwa machozi, kuungama dhambi, na kuwa na mwenendo mzuri, ni uzoefu wa hukumu ya Mungu na kupata utakaso. Nawauliza basi, tunajua kiini cha dhambi zetu wenyewe? Je, tunajua kiini cha asili yetu ya kishetani ambayo inampinga Mungu? Je, tunajua ukweli kuhusu upotovu wa kina wa mwanadamu? Je, tunaona waziwazi kiini cha Shetani? Je, tunajua tabia ya haki ya Mungu, yenye uadhama na isiyokosewa? Je, tumejitenga kwa kweli na kwa muunganisho na udhibiti wa dhambi? Je, tabia yetu ya kishetani imetakaswa? Je, tumekuwa wenye heshima na utiifu kwa Mungu? Ikiwa hatujatimiza haya, tunawezaje kusemekana kuwa tumepitia hukumu na kupata utakaso wa Mungu? Je, mmeelewa jinsi nilivyowasiliana? Kazi ya Bwana Yesu katika Enzi ya Neema haikuwa kazi ya hukumu. Kazi ya Mwenyezi Mungu katika Enzi ya Ufalme ni kazi ya hukumu ya Mungu katika siku za mwisho.
kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni