1.19.2018

Sura ya 51. Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

Sura ya 51. Je Unajua Ukweli Hakika Ni Nini?
Mwenyezi Mungu alisema, Ninyi nyote mara nyingi mmepata uzoefu wa hali ya kuwa katika mkutano, na kuhisi kana kwamba huna chochote cha kuhubiri kuhusu—hatimaye unajilazimisha na unasema kitu cha juu juu. Unajua vizuri kuwa maneno haya ya juu juu ni kanuni, lakini unahubiri kuyahusu hata hivyo, na mwishowe unahisi kuwa huna shauku, na watu chini yako wanasikiliza na wanahisi kuwa yanachosha sana—je hilo halijafanyika? Kama inabidi ujilazimishe kuhubiri, basi kwa upande mmoja Roho Mtakatifu hatafanya kazi, na kwa upande huo mwingine, hakuna faida kwa watu. Kama hujapata uzoefu wa ukweli lakini bado unataka kuhubiri kuuhusu basi, haijalishi unachosema, hautahubiri kwa dhahiri—utakuwa tu unahubiri vitu vya juu juu. Unaweza kufikiri kuwa maneno unayonena yana nuru, lakini ni kanuni tu, sio uhalisi, na watu wanaosikiliza hawataweza kushika vitu vya kweli; wanaweza kuwa wanahisi kwamba unachosema ni ukweli wanapokisikiliza, lakini baadaye utasahaulika kabisa. Kama unachohubiri kuhusu sio hali halisi, hutaweza kuigusa mioyo ya watu; watakisahau hata kama wanataka kukumbuka, na hutaweza kuwasaidia. Ukikabaliana na hali ambapo unataka kuhubiri lakini unahisi huwezi kuhubiri kuhusu mambo kikamilifu, ambapo uko tu na maarifa fulani ya kikanuni lakini hujui chochote kuhusu mambo muhimu, na kama huwezi kujibu maswali muhimu ambayo watu wengine wanauliza, basi ni afadhali usihubiri hata kidogo. Kuna wakati pia ambapo utaanza kujadili mada katika mkutano, na unahisi kuwa una maarifa kwa kiasi fulani kuihusu, na unaweza kushiriki kuhusu baadhi ya vitu vya kweli. Lakini baada ya kuijadili kwa kina kifupi kila mtu anaielewa, na huna chochote unachoweza kuhubiri kwa kina zaidi. Kile ambacho wengine hawajui, unaweza kuwa hujui pia. Kwa hivyo usijilazimishe kuhubiri; kwa mbadala unaweza kumfanya kila mtu ashiriki kuhusu mada hiyo. Kama unafikiri kuwa ni kanuni, basi ni bure kuhubiri kuihusu, na haitawapa wengine ujenzi wa maadili; katika hali hii, haijalishi unachosema, Roho Mtakatifu hatafanya kazi Yake, na unapojilazimisha tu na kuhubiri unaweza kusema vitu vya kipumbavu na kupotoka, na unaweza kuwapotosha watu. Unaona kwamba wale walio chini hawawezi kupokea kikamilifu vitu vya ndani kiasi kwa muda mfupi, na hawezi kuvikumbuka kwa urahisi; watu wengi wana msingi duni na wana ubora wa tabia wa chini, ilhali bado wana haraka ya kukubali kanuni hizi zenye makosa, zinazodhibiti—kwa hakika haya maajabu! Lazima uweke maanani maalum kwa kipengele hiki. Watu ni bure, na wakati mwingine wametawaliwa na kiburi chao, wanajua vizuri sana kuwa wanahubiri kanuni, na wako wazi kuhusu hili, ilhali bado wanafikiria,[a]“Watu hawa walio chini wanaweza kukosa kugundua, lakini kwa ajili ya kuepuka aibu sitalitilia maanani hilo; ni muhimu kuonyesha uwezo unapohitajika!” Basi huko sio tu kuwapumbaza watu? Hii pia ni kutokuwa mwaminifu kwa Mungu! Kama wewe ni mtu ambaye anaelewa ukweli, basi utajilaumu. Huwezi kuhubiri jinsi hiyo tena, na mada inapasa kubadilishwa. Unaweza kushiriki kuhusu kitu ambacho una uzoefu nacho, ama pia unaweza kuzungumza kuhusu maarifa fulani uliyo nayo kuhusu ukweli; kama huwezi kuhubiri kwa wazi kuhusu jambo fulani, unaweza kushiriki badala yake! Sio vizuri kamwe kuwa na mtu mmoja tu anayehubiri kila wakati. Kwa sababu unakosa uzoefu, haijalishi una uwezo gani wa kufikiria na kuwaza kitu, unachozungumzia baada ya hayo yote ni kanuni tu, na ni kitu pia kinachopatikana katika dhana za binadamu. Vitu vile ambavyo ni vya ukweli lazima vipitiwe; bila kupata uzoefu hakuna anayeweza kuelewa kikamilifu kiini cha ukweli, wala hawawezi kueleza kwa wazi hali ya kupata uzoefu wa ukweli; lazima mtu awe na uzoefu na ukweli ili awe na kitu cha kuhubiri kuhusu. Kutokuwa na uzoefu haikubalikii; hata kama una uzoefu itakuwa katika eneo finyu, na unaweza kunena juu ya hali finyu, lakini huwezi kusema zaidi. Kama mkutano unazunguka kila mara kwa mada moja, ama mada mbili, basi baada ya kurudia kushiriki juu ya na mada hizi, kutakuwa na baadhi ya watu ambao wanaokuja kuelewa kidogo. Ama labda unapoanza kuhubiri, unafikiria kuwa unahubiri kwa njia ya vitendo, lakini watu walio chini bado hawaelewi kweli, kwa sababu hali yako ni hali yako, na hali za watu walio chini sio hasa sawa na zako. Zaidi ya hayo, unapitia hili kwa wakati huu, lakini watu walio chini hawayapitii mambo yayo hayo kwa wakati huu, kwa hivyo wanafikiria kuwa unachohubiri kuhusu hakifai kwao. Unafaa kufanya nini katika hali hiyo? Unafaa basi kuwauliza maswali fulani ili kuelewa hali zao. Waulize kile ambacho wangefanya wangekabiliwa na hali hii. Mtu anafaa kutenda vipi kulingana na ukweli? Kwa kushiriki kidogo kwa namna hii njia itafunguliwa, na watu wanaweza kuongozwa kwa mada, na kwa kushiriki zaidi utapata matokeo. Ingawa kila mmoja anasoma vitabu, baadhi yao watashika maana ya ukweli, wengine watajawa na kanuni, na wengine kujawa na upumbavu, kwa hivyo matokeo yatakuwa tofauti. Wale ambao wana uzoefu fulani wanaweza kunena juu ya vitu vya utendaji, wanaweza kunena kuhusu uelewa fulani wa vitendo wa ukweli, na ukweli huu ni ukweli kutoka kwa mtazamo wao. Lakini wakati wale bila uzoefu wanasoma maneno ya ukweli, watapokea maana fulani halisi, na wataweza kueleza baadhi ya vitu kuhusu maana ya juu juu ya ukweli, lakini maelezo yao hayahesabiki kama uelewa wa ukweli. Kunaweza kuwa na baadhi ya watu chini katika mkutano, wanaouliza, “Ni nini wanachofamya?” Mtu atajibu, “Wanatoa ukweli.” Hii haiwezi kusemwa. “Wanafanya hasa kazi ya uchungaji na utoaji wa ukweli.” Hilo haliwezi kusemekana pia. Inaweza tu kusemwa tu kuwa wanafanya kazi ya uchungaji katika kanisa, na kufanya kazi ya unyunyizaji; haiwezi kusemwa kuwa wanatoa ukweli. Hamuwezi kusema kuwa wale kati yenu wa kimo cha chini wanatoa ukweli kwa wengine; hamwezi katu kusema hivyo. Ni watu wangapi wanao ukweli? Na kimo cha chini cha mwanadamu wanaweza kusemekana kuwa wanatoa ukweli? Hata kama mtu ana uzoefu kiasi na uelewa kiasi wa ukweli, hawezi kusema kuwa anaweza kutoa ukweli; hawezi kabisa kusema hivyo. Kusema hivyo ni kupotea sana! Wale ambao wanafanya kazi ya uchungaji, wanaofanya kazi ya unyunyizaji moja kwa moja, na wale ambao hasa wanawajibika kwa kazi ya kuingia katika uzima kanisani hawaelewi ukweli ilhali wanajaribu kuutoa kwa wengine. Je huu sio ukinzani? Mtu anaweza kukuuliza, “Ukweli ni nini?” Na unaweza kusema, [b]“Ukweli ni neno la Mungu!” Hili ni jambo ambalo huwezi kuongea kwa wazi kulihusu bado. Kama bado huwezi kunena kwa wazi kuhusu vitu ambavyo viko mbele ya macho yako, basi hujahitimu kutolea wengine. Sasa hivi wale wanaofanya kama viongozi hawana uzoefu wa kweli wa maisha; kwa kiwango cha juu zaidi, wana ubora wa tabia kiasi, na uwezo bora wa kupokea maarifa kutoka katika vitabu, na wanaweza kujadili uelewa fulani, kutenda katika jukumu la mshenga kwa wengine, lakini huwezi kusema kuwa wanatoa ukweli. Watu wengine wana akili nzuri, na baada ya kusoma na kusikiliza zaidi wanaweza kupata uelewa fulani, na ingawa wanaweza kushiriki maarifa haya kidogo na watu walio chini, hili haliwezi kuitwa kutoa ukweli; hili linaweza tu kuitwa kushiriki uelewa fulani. Wala utoaji wa kitu kwa wengine hauwezi kusemekana kuwa kushiriki ukweli. Ni mtu wa aina gani anaweza kutoa ukweli? Inaweza kusemwa tu kuwa wanafanya kazi ya uchungaji katika kanisa na kutembelea kanisa. “Kutembelea kanisa” ina umuhimu kwake; hivyo ni, ndugu na dada wanakabiliwa na matatizo fulani, na wengine wana uwezo wa kupokea. Kwa njia ya ugumu huu, wanabeba mzigo, wanajaribu kulielewa, na wanapokea nuru kiasi kwa kufanya hivo kusaidia watu. Je kuwasaidia wengine kunaweza kuchukuliwa kama kuuelewa ukweli? Wataweza kuuelewa ukweli vizuri, ama kuwa na ukweli zaidi ya wengine? Huwezi kusema hivyo, kwani hiyo siyo hali. Kuwaruhusu baadhi ya watu kufanya kazi ya uchungaji kanisani ni ili kuwakuza tu; kwani wana ubora wa tabia kiasi, wana uwezo mdogo wa kupokea, na pia hali ya familia yao inafaa, basi wameruhusiwa kutenda. Kumpandisha mtu cheo haimaanishi kuwa anaweza kutoa ukweli, ni kuwa tu watu wanapobeba mzigo basi kwa kweli wanapitia kazi ya Roho Mtakatifu, wanaweza kuhubiri kuhusu mwanga na nuru, na wanaweza kupokea mwanga na nuru mbele ya wengine, lakini mwanga huu hauwakilishi ukweli. Unaona, baadhi vya vijitabu vilivyotolewa vina ushirika, na vingine vina maswali ya ukweli na majibu (kuuliza maswali na kutoa majibu[c] kwa msingi wa ukweli unaitwa “maswali na majibu ya ukweli”), na pia ushirika fulani, na kwa hali hii, huwezi kusema, “Tunautoa ukweli ili kuusoma.” Unafaa kuelewa mawanda hakika ya ukweli na sharti pia uelewe ni nini hakifungamani ukweli. Niambie, kama baadhi ya watu watapokea ufahamu kidogo na kuwa na uelewa kulingana na uzoefu wao kutoka kwa maneno ya ukweli, je hii inahesabika kama ukweli? Kwa kiwango cha juu zaidi tunaweza kusema kuwa wana uelewa fulani wa ukweli. Maneno yote ya nuru ya Roho Mtakatifu hayawakilishi neno la Mungu, hayauwakilishi ukweli, na hayafungamani ukweli. Inaweza tu kusemwa kuwa watu hao wana uelewa fulani wa ukweli, na nuru ya Roho Mtakatifu. Ukipata uelewa fulani kutoka kwa ukweli na kisha uutoe kwa wengine, hivyo ni, kutoa uelewa wako wa binafsi na uzoefu, bado huwezi kusema: “Njoo, nitakutolea ukweli.” Kuliita ushirika ni sawa, na maneno yako lazima yawe yanayofaa. Mbona tunasema hivyo? Kunayo mengi zaidi kwa hali hiyo kuliko hayo. Lazima uone hali hii kwa wazi, na sio tu kuiweka katika maneno kwa njia fulani na kuiacha vile; haya sio maneno. Watu wanapata vitu ambavyo wanapaswa wawe navyo kutoka kwa ukweli, lakini hivyo sio kusema kuwa wana ukweli, kuwa ni wa ukweli; katu hatuwezi kusema hivyo. Haijalishi ni kiwango gani utapata kutoka kwa ukweli, huwezi kusema una uzima, wala huwezi kusema kuwa wewe ni wa ukweli; huwezi kusema hivo kabisa. Umepata tu riziki fulani kutoka kwa ukweli, ustawishaji maisha yako, kukufanya uwe na baadhi ya vitu ndani yako ambavyo lazima uwe navyo ili kuamini katika Mungu, na kumridhisha Mungu. Mungu anawatolea watu kupitia kwa ukweli, kuwaruhusu watu kumridhisha Mungu na kufuata mapenzi ya Mungu kupitia katika ukweli, na mwishowe hata watu wakitimiza kabisa mapenzi ya Mungu, bado haiwezi kusemwa kuwa ni wa ukweli, kwa uchache zaidi haiwezi kusemwa kuwa wana ukweli kama maisha yao. Kama tungeweza kusema hivo, kama mwanadamu ana uzoefu na ukweli wote ambao Mungu anaonyesha, ana ulewa juu yake, na anaelewa kwa wazi kila ukweli, basi wanafaa kuwa wanaweza kueleza ukweli, basi mwanadamu hatakuwa Kristo? Hii inakuwa kanuni ya Mungu na mwanadamu, na ni kosa kubwa, kubwa zaidi! Kwa ufupi, watu wanafaa kuelewa kitu: Haijalishi jinsi unavyouelewa ukweli vizuri, haijalishi kiwango cha uzoefu wako, haijalishi wewe ni mtiifu kikamilifu kivipi kwa mipango ya Mungu, haijalishi kuingia kwa maisha kwako ni wa juu ama wenye kina vipi, maisha yako bado ni maisha ya mwanadamu, na mwanadamu kamwe hawezi kuwa Mungu; hii ni bila shaka, na watu lazima waielewe. Hata kama hatimaye utaushika ukweli wote kabisa, na unaweza kujiwasilisha kwa mipango ya Mungu, na umekuwa mtu aliyekamilishwa, bado huwezi kusema kuwa wewe ni wa ukweli, na hata zaidi huwezi kusema kuwa unaweza kuueleza ukweli; kila kitu kilichosemwa hapo awali kuhusu mwanadamu kuwa na maisha ya Kristo ndani yake pia kimekosea, na ni kitu tu kilichoongelewa tu mara moja. Sasa hivi hata kama watu hawasemi hivi, wanaweza kuwa na uelewa wa ukungu na usio wazi ndani yao, na baadhi ya watu wanaweza kufikiria: “Tumeupata ukweli, ukweli sasa uko ndani yetu, kwa hivyo tuna ukweli, ukweli umo ndani ya mioyo yetu, na tunaweza kuueleza.” Je, hili halijakosea pia? Kusema kama mtu ana ukweli ni kusema kama ana uzoefu na ukweli huu, kama ana uelewa wake, na kama anaweza kuutenda. Unaweza kuelewa inaposemwa hivyo. Kila mtu anaweza kuupitia ukweli, lakini hali ya uzoefu wao itakuwa tofauti, na kile kila mtu hupata kutoka kwa ukweli huo sawa ni tofauti. Lakini hata baada ya kuweka pamoja uelewa wa kila mtu bado huwezi kueleza kikamilifu ukweli huu mmoja; ukweli ni wa kina zaidi namna hiyo. Mbona Ninasema kuwa vitu vyote ambavyo umevipata na uelewa wako wote, haviwezi kuwa mbadala wa ukweli? Ukishiriki uelewa wako na wengine, wanaweza kuutafakari kwa siku mbili ama tatu kisha watamaliza kuupitia, lakini mtu hawezi kupata uzoefu kamilifu wa ukweli hata kwa maisha yote, hata watu wote kwa pamoja hawawezi kupata uzoefu wa huo kabisa. Hivyo inaweza kuonekana kuwa ukweli ni wenye kina sana, hakuna jinsi ya kutumia maneno ili kuueleza ukweli kikamilifu, ukweli ukiwekwa kwa lugha ya binadamu ni methali kwa mwanadamu; ubinadamu hauwezi kupata uzoefu wake kikamilifu, na ubinadamu lazima uishi kwa kuutegemea. Kipande cha ukweli kinaweza kuufanya ubinadamu mzima kuishi kwa maelfu ya miaka, na ukweli ni maisha ya Mungu Mwenyewe, ukiiwakilisha tabia Yake binafsi, ukiwakilisha dutu Yake binafsi, ukiwakilisha kila kitu ndani Yake. Ukisema una ukweli na kwamba kuwa na uzoefu fulani kunamaanisha kuwa una ukweli, basi unaweza kuwakilisha tabia ya Mungu? Huwezi. Unaona, mtu anaweza kuwa na uzoefu fulani ama mwanga kuhusu kipengele fulani ama upande wa ukweli, lakini hawezi kuwatolea wengine milele, kwa hivyo mwanga wake sio ukweli, ni kiwango tu ambacho mtu amefikia, uzoefu—uzoefu unaofaa—mtu anafaa kuwa nao, uelewa unaofaa, ambacho ni kipengele cha kweli cha uzoefu wa ukweli. Mwanga huu, nuru na uelewa kwa msingi wa uzoefu hayatawahi kuwa mbadala wa ukweli; hata kama watu wote wamepata uzoefu wa ukweli, nawakiweka maneno yao yote pamoja, haya hayawezi kuwa sawa na sentesi hiyo moja ya ukweli. Kama ilivyosemwa zamani, “Nilitunga methali nyingine: Miongoni mwa wanadamu hakuna yule anayenipenda Mimi.” Hii ni kauli ya ukweli, ni asili ya kweli ya maisha, ni kitu chenye cha maana sana, ni udhihirisho wa Mungu binafsi; hii ni kauli ya ukweli, unaweza kuipitia. Ukiipitia kwa miaka mitatu utakuwa na uelewa usio na kina, ukiipitia kwa miaka minane utapata uelewa zaidi, lakini uelewa wako hautaweza kuwa mbadala wa kauli ya ukweli! Mtu mwingine akipata uzoefu wake kwa miaka miwili atakuwa na uelewa mdogo; akiupitia kwa miaka kumi atukuwa na uelewa wa juu, na akipata uzoefu kwa maisha yake yote atapata uelewa mkubwa zaidi, lakini mkiuweka uelewa wenu pamoja, bado hautakuwa mbadala wa kauli ya ukweli. Haijalisha uelewa wa kiwango kipi, uzoefu wa kiwango kipi, ufahamu kiasi gani, mwanga wa kiasi kipi, ama mifano mingapi ambayo ninyi wawili mmechanganya pamoja, hayo yote hayawezi kuwa mbadala wa kauli hiyo. Ninamaanisha nini na hili? Kuwa tu maisha ya mwanadamu daima yatakuwa maisha ya mwanadamu, na haijalishi uelewa wako unalingana vipi na ukweli, kulingana na maana ya Mungu, kulingana na mahitaji ya Mungu, hayataweza kamwe kuwa mbadala wa ukweli. Kusema kuwa watu wana ukweli kunamaanisha kuwa wana uhalisi fulani, kuwa wana uelewa fulani wa ukweli wa Mungu, kuwa wana kuingia wa kweli katika maneno ya Mungu, kuwa wana uzoefu fulani wa kweli na maneno ya Mungu, na kuwa wako katika njia sahihi katika imani yao kwa Mungu. Kauli moja tu ya Mungu inatosha mtu kupata uzoefu kwa maisha yake yote, kupata uzoefu kwa maisha mengi, ama kwa maelfu kadhaa ya miaka; watu hawawezi kupata uzoefu kamili na nzima kuupitia ukweli kabisa. Kama umeelewa tu maneno ya juu juu kisha useme kuwa una ukweli, je si hilo halina msingi? Kauli zingine sio makosa tu, lakini jambo muhimu ni kuwa watu hawana uelewa sahihi. Mara nyingine watu wanafikiri kuwa wana ukweli, na kuwa hilo ni jambo la ajabu! Wanapopata mwanga mdogo, saa zingine hali zao zinaboreshwa na wanaweza kushiriki jambo la kutoa nuru, wanajiridhisha wenyewe, wanakuwa na hamu kubwa ya chakula na kinywaji, na wamefanikiwa kwa mambo yote; kwa jinsi hii wanafikiria kwamba wana ukweli. Je wana ukweli? Watu walio na ukweli wanaweza kuanguka chini wakati wowote na popote? Watu wanapokuwa na ukweli, watawezaje bado kumkataa Mungu na kumsaliti Mungu? Ukidai kuwa una ukweli, na hilo linathibitisha kuwa ndani yako kuna uzima wa Kristo, basi hilo ni jambo baya sana! Basi umekuwa Bwana. Hii ni kauli ya upumbavu, na inaamuliwa kikamilifu na watu; inafungamana na dhana na mawazo ya binadamu, na siyo hali ya kushikika na Mungu.
Wakati watu wanaelewa ukweli, na kuishi na ukweli kama maisha, hili linaashiria maisha gani? Ni maisha ambayo watu wanaishi wakilitegemea neno la Mungu. Watu wanapokuwa na uzima huo ndani yao, basi maisha yao yanaishiwa kulingana na ukweli, maisha yao yanaishiwa katika eneo la ukweli, maisha yao yamejawa na uelewa wa ukweli, na uzoefu wa ukweli, kuwa kwa msingi huu na kutoenda nje ya mawanda hayo— hayo ndiyo maisha yanayorejelewa. Watu wanautegemea ukweli kama maisha yao, na kuishi maisha yao kulingana na ukweli. Si kwamba wakati watu wanautegemea ukweli kama maisha yao basi wana maisha ya ukweli; si kusema pia kuwa kama una ukweli kama maisha unakuwa ukweli, na maisha yako ndani yanakuwa maisha ya ukweli. Mwishowe maisha yako bado ni maisha ya mwanadamu. Unaweza kuishi ukiyategemea maneno ya Mungu, uwe na uelewa fulani wa ukweli, na kuelewa kwa kiwango cha juu, na uelewa huu hauwezi kuchukuliwa kutoka kwako; unapata uzoefu na kuelewa kikamilifu, unahisi kuwa vitu hivi ni vizuri, ni vya thamani sana, na unakuja kuvikubali kama msingi wa maisha yako, na unaishi ukitegemea vitu hivi, basi hakuna anayeweza kubadilisha hayo, haya ni maisha yako. Maisha yako yana vitu hivi tu, yana uelewa pekee, uzoefu, na ufahamu wa ukweli; haijalishi utakachofanya utakuwa unaishi kwa kutegemea vitu hivi, na haijalishi utakachofanya hutaenda zaidi ya mawanda haya, hutaenda zaidi ya mipaka hii; hayo yatakuwa maisha yako, na kusudi la mwisho la kazi ya Mungu ni kwamba watu watakuwa na maisha ya aina hii. Kama Mungu Mwenyewe binafsi Alikamilisha kikundi cha Miungu wakubwa na Miungu wadogo, je huo haungekuwa machafuko? Hata hivyo, hilo ni jambo lisilowezekana, ni jambo la upumbavu, ni dhana ya upumbavu kutoka kwa binadamu, na sio jambo linalowezekana. Mungu Anaweza tu kuwaumba watu, Mungu hawezi kumuumba Mungu; Mungu Anaweza tu kupata mwili kama mfano wa mwili, lakini haimaanishi kuwa Alimuumba Mungu. Mungu hakujiumba Mwenyewe, Yeye ana dutu Yake binafsi, ambayo haitabadilika kamwe. Hakujiumba Mwenyewe, Anaweza tu kuumba watu na kuumba vitu vingine.
Kama una uzoefu fulani na maneno ya Mungu, na unaishi kwa kutegemea uelewa wako wa ukweli, basi neno la Mungu linakuwa maisha yako. Huwezi kusema kuwa ukweli ni maisha yako, kuwa unachoeleza ni ukweli; kama unafikiria hivyo, basi umekosea. Kama una uzoefu fulani na kipengele cha ukweli, je, hili linaweza kuuwakilisha ukweli? Haliwezi kuwakilisha ukweli kabisa. Kwa hivyo unaweza kunena ukweli kabisa? Kwa uchache zaidi unaweza kuunena kabisa. Unaweza kugundua na kuona tabia ya Mungu kutoka kwa ukweli? Huwezi kuiona. Unaweza kugundua kiini cha Mungu? Huwezi kugundua. Uzoefu wa kila mtu wa ukweli ni kipengele chake kimoja tu, sehemu moja, mtazamo mmoja; kupata uzoefu wake katika mawanda yako finyu huwezi kugusia ukweli wote. Maana asili ya ukweli inayoelezwa—chanzo hicho—inafichua asili ya kawaida ya binadamu. Uzoefu wako mdogo unajumuisha kiwango kipi? Chembe ya changarawe ufuoni, tone la maji baharini. Kwa hivyo, hata kama unahisi kuwa uelewa uliopata kutoka kwa uzoefu ni wa thamani, ama unahisi hata kuwa ni wa thamani kabisa, kabisa—huo hauwezi kuhesabika kama ukweli. Chanzo cha ukweli, na maana ya ukweli, inachukua eneo kubwa kabisa! Hakuna kinachoweza kuipinga. Watu wengine husema pia, “Je uzoefu wangu hautapingwa kamwe?” Bila shaka, hali yako ya ukweli ambayo umeipata kutoka kwa uzoefu itawezaje kupingwa? Ukweli unaweza kuwa maisha yako katika mazingira yoyote, unaweza kukupa njia, na unaweza kukuruhusu kuishi. Vitu ambavyo watu wanavyo, mwanga wa watu, viinawafaa tu wao binafsi ama kwa wengine katika mawanda fulani, lakini havitafaa katika mawanda tofauti. Uzoefu wa mtu ni finyu sana haijalishi ni wa maana kiasi gani, na uzoefu wao hautawahi kufikia kamwe mawanda ya ukweli. Mwanga wa mtu, uelewa wa mtu, hauwezi kamwe kulinganishwa na ukweli.
Watu wanapokuwa na uzoefu fulani na ukweli, wakielewa baadhi ya nia za Mungu, na kuwa na uelewa fulani wa Mungu, watu wanapopitia mabadiliko fulani, na wanapokuwa watakatifu na wasafi kiasi, inaweza bado kusemwa kuwa ni watu, kuwa ni watu wa kawaida kabisa ambao Mungu anataka kupata. Wewe ni mtu wa aina gani? Watu wengine wanasema, “Mimi ni mtu aliye na ukweli.” Haifai kusema hivyo. Unaweza tu kusema: “Mimi ni mtu ambaye ameharibiwa na Shetani, kisha nikapata kupitia kuadibu kwa Mungu, hukumu, na wokovu, na hatimaye nimekuja kupata uzoefu fulani na uelewa wa ukweli na wa maneno ya Mungu; Mimi ni mtu tu ambaye ameokolewa na Mungu.” Ukisema: “Mimi ni mtu ambaye ana ukweli. Nimepata uzoefu wa neno lote la Mungu, na ninalielewa lote. Maana ya kila neno la Mungu, kwa muktadha upi, na katika hali gani lilinenwa, nayajua yote. Je hii haimanishi kuwa na ukweli?” basi utakuwa umekosea tena. Unaweza kuwa na uzoefu fulani na maneno ya Mungu, na kupata mwanga kutoka kwayo, lakini huwezi kusema wewe ni mtu ambaye ana ukweli. Wale wanaoelewa tu kanuni fulani, na wanaweza kuhubiri kanuni fulani wanaweza kusema vile hata kwa kwa kiwango cha chini. Watu wanapokuja mbele ya Mungu, na kuja mbele ya ukweli, wanafaa kusimama katika nafasi gani? Watu ni nini, hata hivyo? Ni nini hasa maisha ambayo watu wanayo ndani yao? Maisha ya Mungu ni nini? Watu wanafaa kuelewa hili vema kabisa. Watu pia wanafaa kuelewa muundo na kiini chao. Watu wengine wanafikiri kuwa wana ukweli baada ya kupata uzoefu wa siku chache za kazi ya Mungu, na hao ni watu wenye kiburi sana, hao ni watu wasio na busara yoyote. Kila mtu anafaa kuchambua suala la aina hii, ili aweze kujielewa mwenyewe, kuuelewa ubinadamu, mwanadamu ni nini kwa kweli na, baada ya kukamilishwa, wataweza kufika kiwango kipi, kauli zipi, vyeo vipi, ni majina yapi yanafaa—watu wanafaa kujua vitu hivi na sio tu kujiingiza katika ndoto kila wakati. Kuwa mtu, ni afadhali kupotoka ukiwa upande wa ukweli, kwani huu una msingi zaidi. Watu wengine wanaoamini katika Mungu daima wanafukuza ndoto zao, wanataka kuyafikia maisha ya Mungu daima, kuwa na maisha ya Mungu; je hili sio jambo hatari? Hili ni jambo hatari sana. Baada ya kufanya kazi kwa muda kidogo watahubiri: “Wakati joka kuu jekundu litakapoanguka kutoka mamlakani lazima tushike madaraka kama wafalme, na kutawala juu ya miji mingi!” Kudhihirisha vitu hivi ni vibaya sana. Wale wasio na uzoefu wanahubiri kwa urahisi kuhusu kanuni, wanajiingiza katika ndoto, wanajifikiria kuwa werevu sana, na kufikiria kuwa tayari wanacho kile wanachotaka kwa imani yao kwa Mungu; wao ni wafuasi wa Paulo, na njia wanayoitembea ni njia ya Paulo kabisa; watu hawa wote watakuwa wapinga kristo na watapata adhabu kali sana.
Tanbihi :
a. Nakala asili inaacha “ilhali bado wanafikiria.”
b. Nakala asili inaacha “Na unaweza kusema.”
c. Nakala asili inaacha “na kutoa majibu.”

kutoka kwa Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni