Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja ushuhuda. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliopangwa kwa tarehe ya hoja ushuhuda. Panga kwa uhusiano Onyesha machapisho yote

12.24.2019

Mungu hutegemeza nini uamuzi Wake wa mwisho wa mtu?

Maneno Husika ya Mungu:

Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, wala si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo yote ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya nyingine, na vilevile njia zao katika kunifuata, sifa zao asilia, na utendakazi wao wa mwisho. Kwa njia hii, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu na kila mmoja atakuwa wa aina yake kama Nilivyowaweka.

12.18.2019

Mungu huwaokoa watu gani? Yeye huwaondosha watu gani?

Maneno Husika ya Mungu:


Wale walio wa Shetani hawaelewi maneno ya Mungu, na wale walio wa Mungu wanaweza kusikia sauti ya Mungu. Wale wote wanaotambua na kuelewa maneno Ninayozungumza ni wale watakaookolewa, na kumshuhudia Mungu; wote wasioelewa maneno Ninayoyazungumza hawawezi kutoa ushuhuda kwa Mungu, na ni wale watakaoondolewa.

12.17.2019

Mungu Ndiye Nguvu ya Maisha Yangu


Video ya Kiswahili ya Ushuhuda wa Kikristo "Mungu Ndiye Nguvu ya Maisha Yangu" | Jinsi Wakristo Humtegemea Mungu Kushinda

Fang Jin ni Mkristo. Alikamatwa na serikali ya CCP kwenye mkusanyiko. Ili kumlazimisha kuwataja ndugu zake wa kike na kiume na kumsaliti Mungu, polisi walimnyima chakula, maji na usingizi kwa siku saba mchana na siku sita usiku, na kusababisha kila aina ya mateso ya kinyama juu yake: mapigo makali, kuning’inizwa, kuchuchumaa, kudhihakiwa na kufedheheshwa. Alikuwa amejaa majeraha na alipooza miguu.

12.14.2019

Matendo maovu ni yapi? Maonyesho ya matendo maovu ni yapi?

Maneno Husika ya Mungu:


Ni kiwango kipi ambacho kulingana nacho matendo ya mtu yanatathminiwa kuwa mema au mabaya? Inategemea na iwapo katika fikira, maonyesho, na matendo yako, una ushuhuda wa kutia ukweli katika vitendo na wa kuishi kwa kudhihirisha uhalisi wa ukweli au la. Ikiwa huna uhalisi huu au huishi kwa kudhihirisha hili, basi bila shaka wewe ni mtenda maovu.

12.13.2019

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu

Sauti ya Mungu | “Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu”


Umeme wa Mashariki, Kanisa la Mwenyezi Mungu lilianzishwa kwa sababu ya kuonekana na kazi ya Mwenyezi Mungu, ujio wa pili wa Bwana Yesu, Kristo wa siku za mwisho. Linashirikisha wale wote ambao wanaikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho na ambao wameshindwa na kuokolewa kwa maneno Yake. Liliasisiwa kikamilifu na Mwenyezi Mungu mwenyewe na linaongozwa naye kama Mchungaji. Kwa hakika halikuanzishwa na mtu. Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.

12.09.2019

Matendo mema ni nini? Maonyesho ya matendo mema ni yapi?

Maneno Husika ya Mungu:


Ukimiliki ukweli, unaweza kumfuata Mungu. Kama unaishi kwa kudhihirisha, unaweza kuwa onyesho la neno la Mungu. Kama unao uzima, unaweza kufurahia baraka ya Mungu. Ni wale tu walio na ukweli wanaweza kufurahia baraka ya Mungu. Mungu huhakikisha kwamba anawafidia wale wote wanaompenda kwa moyo wao wote pamoja na pia wanaovumilia magumu na mateso, na wala si kwa wale wanaojipenda tu na wamejipata kwenye mtego wa uwongo wa Shetani.

11.30.2019

Utamu katika Shida

 

 Swahili Christian Testimony Video "Utamu katika Shida" | Mungu Ndiye Nguvu Wangu


Han Lu ni kiongozi wa Kanisa la Mwenyezi Mungu katika China bara. Ameamini katika Mungu kwa zaidi ya muongo mmoja na amepitia kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho. Anaelewa baadhi ya ukweli na anajua kwamba ni kupitia tu Kristo wa siku za mwisho, Mwenyezi Mungu, ndiyo mwanadamu ataweza kuwekwa huru kutoka dhambini na kuishi maisha yenye maana.

11.24.2019

Maskani Yangu Yako Wapi



Wazazi wa Wenya walitengana alipokuwa na umri wa miaka miwili, na baada ya hapo aliishi na baba yake na mama wa kambo. Mamake wa kambo hakuweza kumvumilia na daima alikuwa akibishana na baba yake.

11.06.2019

Mwana wa Adamu Ameonekana



Wimbo wa Injili "Mwana wa Adamu Ameonekana" | Sifu Kurudi kwa Yesu Mwokozi | Watoto Wanacheza Ngoma


Kutoka Mashariki ya ulimwengu (Mashariki ... Mashariki ...),

mwale wa mwanga unatokea (mwanga ... mwanga ...),

ukiangaza njia yote kwenda magharibi.

Mwana wa Adamu ameshuka duniani.

11.05.2019

Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu


Sauti ya Mungu | “Wale Wanaomjua Mungu Pekee Ndio Wanaoweza Kuwa na Ushuhuda Kwa Mungu”


Tazama Zaidi:

Maonyesho ya Mungu | "Namna Petro Alivyopata Kumjua Yesu" | Only Those Who Know God Can Be Perfected

https://sw.godfootsteps.org/videos/how-peter-came-to-know-Jesus-word.html

11.01.2019

Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme



Wimbo wa Kuabudu | "Sifa kwa Maisha Mapya katika Ufalme" | Watu wa Mungu Humsifu na Kumwabudu Mungu


Tumesikia sauti ya Mungu na kurudi nyumbani Kwake.

Mikutanoni tunakula na kunywa maneno ya Mungu, tunahudhuria karamu.

Sisi tunaaga huzuni na vifungo vyetu, tunaishi maisha mapya.

Maneno ya Mungu yako nasi kila siku, tunastarehe ndani yake.

Tunapofungua mioyo yetu katika ushirika wa kweli, mioyo yetu inaangazwa sana.

10.28.2019

Wanawali wenye hekima ni nini? Wanawali wapumbavu ni nini?

 
    Maneno Husika ya Mungu:
    Zamani, watu wengine wamefanya utabiri kuhusu “mabikira watano wenye busara, mabikira watano wapumbavu”; ingawa utabiri huo si sahihi, si wenye makosa kabisa, kwa hiyo Naweza kuwapa ninyi maelezo fulani. Mabikira watano wenye busara na mabikira watano wapumbavu hakika hawawakilishi idadi ya watu, wala hawawakilishi watu wa aina moja mtawalia.

10.25.2019

Kuna tofauti zipi kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya pepo wabaya?

Maneno Husika ya Mungu:
Lazima uelewe ni mambo yapi yanatokana na Mungu ni mambo yapi yanatokana na Shetani. Mambo yanayotokana na Mungu hukusababisha kuwa wazi zaidi kuhusu maono, na hukusababisha kusogea karibu na karibu zaidi na Mungu, ukishiriki upendo na ndugu kwa bidii; unakuwa na uwezo wa kutilia maanani mzigo wa Mungu, na moyo wako umpendao Mungu haupungui; kuna njia mbele yako kuitembea.

10.24.2019

Kazi ya pepo wabaya ni nini? Kazi ya pepo wabaya hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia katindani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuwa na hali za kawaida mbele ya Mungu. Ambayo ni kusema, punde tu kuna kazi ya Shetani ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba.

10.23.2019

Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe.

10.21.2019

Kuna tofauti ipi kati ya mtumishi mwema na mtumishi muovu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu.

10.20.2019

Kuna tofauti ipi kati ya ngano na magugu?


Maneno Husika ya Mungu:
Kama Nilivyosema, Shetani amewatuma wale ambao wananifanyia huduma kuukatiza usimamizi Wangu; hawa watendaji huduma ni magugu, lakini ngano hairejelei wazaliwa wa kwanza, lakini badala yake wana wote na watu ambao si wazaliwa wa kwanza. Siku zote ngano itakuwa ngano, siku zote magugu yatakuwa magugu; hii ina maana kwamba asili ya wale wa Shetni haiwezi kubadilika kamwe. Kwa hiyo, kwa ufupi, wao wanabaki kama Shetani. Ngano inamaanisha wana na watu, kwa sababu kabla ya kuumbwa ulimwengu Niliwaongezea watu hawa sifa Yangu.

10.13.2019

Mpinga Kristo ni nini? Mpinga Kristo anaweza kutambuliwaje?


Maneno Husika ya Mungu:
Kwa wakati ambao Mungu bado hakuwa amegeuka mwili, kipimo cha iwapo mwanadamu alimpinga Mungu kilitegemea iwapo mwanadamu alimwabudu na kumheshimu Mungu aliye mbinguni asiyeonekana. Ufafanuzi wa upinzani kwa Mungu wakati huo haukuwa halisi, kwani mwanadamu wakati huo hangemwona Mungu wala kujua mfano wa Mungu ama jinsi Alivyofanya kazi na kuongea. Mwanadamu hakuwa na dhana za Mungu na alimwamini Mungu kwa njia isiyo dhahiri, kwani Hakuwa amejitokeza kwa mwanadamu.

10.12.2019

Kwa nini makanisa yanaweza kupotoka na kuwa dini?

Maneno Husika ya Mungu:

Kwa nini inasemekana kwamba vitendo vya walio katika makanisa ya kidini vimepitwa na wakati? Ni kwa kuwa wanayoyaweka katika vitendo ni tofauti na kazi ya leo. Katika Enzi ya Neema, walichotenda kilikuwa sahihi, ila kwa kuwa enzi yenyewe imepita na kazi ya Mungu kubadilika, vitendo vyao hatua kwa hatua vimepitwa na wakati. Vimeachwa nyuma na kazi mpya na mwangaza mpya. Ikiwa imesimama juu ya msingi wake asili, kazi ya Roho Mtakatifu imepiga hatua kadhaa kwa kina.

10.02.2019

Mtu anawezaje kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu?

Mtu anawezaje kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Watu wanaamini katika Mungu, wanampenda Mungu, na kumkidhi Mungu kwa kugusa Roho wa Mungu kwa moyo wao, hivyo kupata ridhaa ya Mungu; na wakati wanajihusisha na maneno ya Mungu kwa moyo wao, kwa hivyo wanasisimuliwa na Roho wa Mungu. Ikiwa unataka kufikia maisha ya kawaida ya kiroho na kuanzisha uhusiano wa kawaida na Mungu, lazima kwanza uutoe moyo wako kwa Mungu, na uuweke moyo wako uwe mtulivu mbele za Mungu.