Maneno Husika ya Mungu:
Huu ndio wakati Ninapoamua mwisho wa kila mtu, wala si hatua ambapo nilianza kumfinyanga mwanadamu. Mimi huandika maneno na matendo yote ya kila mtu katika kitabu Changu, moja baada ya nyingine, na vilevile njia zao katika kunifuata, sifa zao asilia, na utendakazi wao wa mwisho. Kwa njia hii, hakuna mtu yeyote atakayeepuka mkono Wangu na kila mmoja atakuwa wa aina yake kama Nilivyowaweka.
Ninaamua hatima ya kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu.
Ninaamua hatima ya kila mwanadamu si kwa kuzingatia umri, ukubwa, kiwango cha mateso, sembuse kiwango ambacho kwacho anavuta huruma, bali ni kwa kuangalia kama ana ukweli. Hakuna chaguo lingine ila hili tu. Ni sharti mjue kwamba wale wote ambao hawafuati mapenzi ya Mungu wataadhibiwa. Huu ndio ukweli usiobadilika. Kwa hivyo, wale wote wanaoadhibiwa wanaadhibiwa kwa ajili ya haki ya Mungu na kama malipo kwa ajili ya vitendo vyao vingi viovu.
kutoka katika “Unapaswa Kutayarisha Matendo Mema ya Kutosha kwa ajili ya Hatima Yako” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kabla ya binadamu kuingia rahani, iwapo kila aina ya mtu ataadhibiwa ama kutuzwa kutaamuliwa kulingana na iwapo wanatafuta ukweli, iwapo wanamjua Mungu, iwapo wanaweza kumtii Mungu anayeonekana. Waliomhudumia Mungu anayeonekana lakini bado hawamjui wala kumtii hawana ukweli. Watu hawa ni watenda maovu, na watenda maovu bila shaka wataadhibiwa; zaidi ya hapo, wataadhibiwa kulingana na mienendo yao mibovu. Mungu ni wa mwanadamu kumwamini, na pia Anastahili utii wa mwanadamu. Wale wanaomwamini tu Mungu asiye yakini na asiyeonekana ni wale wasiomwamini Mungu; zaidi ya hapo, hawawezi kumtii Mungu. Kama hawa watu bado hawawezi kumwamini Mungu anayeonekana wakati kazi Yake ya ushindi inakamilika, na pia wanaendelea kutomtii na kumpinga Mungu anayeonekana katika mwili, hawa wanaoamini isiyo yakini bila shaka, wataangamizwa. Ni kama ilivyo na wale miongoni mwenu—yeyote anayemtambua Mungu Aliyepata mwili kwa maneno lakini bado hatendi ukweli wa utii kwa Mungu Aliyepata mwili hatimaye ataondolewa na kuangamizwa, na yeyote anayemtambua Mungu anayeonekana na pia kula na kunywa ukweli ulioonyeshwa na Mungu anayeonekana lakini bado anamtafuta Mungu asiye yakini na asiyeonekana pia yeye ataangamizwa baadaye. Hakuna hata mmoja wa watu hawa anayeweza kubaki hadi wakati wa pumziko baada ya kazi ya Mungu kukamilika; hakuwezi kuwa yeyote kama watu hawa atakayebakia hadi wakati wa pumziko. Watu wenye pepo ni wale wasiotenda ukweli; asili yao ni ile inayompinga na kutomtii Mungu, na hawana nia hata kidogo za kumtii Mungu. Watu wote kama hao wataangamizwa.
kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Katika kazi ya Mungu ya siku za mwisho, Anaamua matokeo ya watu kutokana na utendaji wao, lakini huu utendaji ni upi? Je, unaujua? Nyinyi mnaweza kufikiri kwamba hili linarejelea tabia ya watu iliyopotoka ikijionyesha kazini mwao, lakini halimaanishi lile. Utendaji huu unanena kuhusu ikiwa unaweza kuweka ukweli kwenye vitendo au la na ikiwa unaweza kusalia mwaminifu unapotenda wajibu wako au la, na vilevile mtazamo wako wa kumwamini Mungu, msimamo wako kwa Mungu, uamuzi wako wa kuteseka kwa ajili ya ugumu, mtazamo wako kwa kukubali hukumu na kupogolewa, kiwango chako cha mabadiliko na idadi ya dhambi kubwa. Haya yote yanachangia katika utendaji wako. Utendaji huu haumaanishi kiwango cha mwisho cha kufichua tabia yako iliyopotoshwa, lakini badala yake umefanikiwa kwa kiasi gani katika imani yako kwa Mungu.
kutoka katika “Maana Ndani ya Mungu Kuamua Matokeo ya Watu Kupitia Utendaji Wao” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo
Nimewatafuta wengi duniani wawe wafuasi Wangu. Kati ya hawa wafuasi wote, kuna wale wanaohudumu kama makuhani, wale wanaoongoza, wanaojumuisha wana, wanaojumuisha watu, na wale wanaotoa huduma. Nawagawa katika makundi haya tofauti kwa msingi wa uaminifu wanaonionyesha. Wakati wanadamu wote wameainishwa kulingana na aina zao, yaani, asili ya kila aina ya mwanadamu inapowekwa wazi, basi Nitamhesabu kila mwanadamu miongoni mwa aina yake kamili na kuweka kila aina katika nafasi yake kamili ili Nikamilishe lengo Langu la ukombozi wa mwanadamu.
kutoka katika “Wengi Wanaitwa, Lakini Wachache Wanachaguliwa” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu hutumia majaribio kuanzisha matokeo ya binadamu. Kunavyo viwango viwili vya kutumia katika majaribio yanayoasisi matokeo ya binadamu: Kiwango cha kwanza ni idadi ya majaribio ambayo watu hao wanapitia, na kiwango cha pili ni matokeo ya watu hawa katika majaribu haya. Ni viashirio hivi viwili vinavyoasisi matokeo ya binadamu.
kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wakati Mungu anataka kuumiliki moyo wa mtu, Atawapa majaribio mengi. Kwenye majaribio haya, kama Mungu hatauchukua moyo wa mtu huyu, wala Haoni kama mtu huyu anao mwelekeo wowote—hivi ni kusema Havioni vitu ambavyo mtu huyu anapitia au anafanya mambo kwa njia ambayo ni ya kumcha Mungu, na Haoni mwelekeo au suluhisho ambalo linajiepusha na maovu kutoka kwa mtu huyu. Kama hivi ndivyo ilivyo, basi baada ya majaribio mengi, subira ya Mungu kwa mtu huyu binafsi itaondolewa, na Hatamvumilia mtu huyu tena. Hataweza kuwapa watu kama hawa majaribio, na Hataweza tena kuwashughulikia. Basi hiyo inamaanisha kwamba matokeo ya mtu huyu ni yapi? Inamaanisha kwamba hawatakuwa na matokeo. Yawezekana kwamba mtu huyu hajafanya maovu yoyote. Yawezekana pia kwamba watu hawa hawajafanya chochote cha kukatiza au kutatiza. Yawezekana kuwa watu hawa hawajampinga Mungu waziwazi. Hata hivyo, moyo wa mtu huyu umefichwa kutoka kwa Mungu. Hawajawahi kuwa na mwelekeo na mtazamo wazi kwa Mungu, na Mungu hawezi kuona waziwazi kwamba moyo wake amekabidhiwa Yeye, na Yeye Hawezi kuona waziwazi kwamba mtu huyu anatafuta kumcha Mungu na kujiepusha na maovu. Mungu hana subira tena kwa watu hawa, Hatawagharamia tena, Hatatoa tena rehema Yake kwao, na Hatawafanyia kazi wao tena. Maisha ya imani ya mtu huyu katika Mungu tayari hayapo tena. Hii ni kwa sababu katika majaribio yote mengi ambayo Mungu amempa mtu huyu, Mungu hajapata matokeo Anayotaka.
kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Kunao msemo ambao mnafaa kutilia maanani. Ninasadiki msemo huu ni muhimu sana, kwa sababu kwangu Mimi unakuja akilini mara nyingi kila siku. Kwa nini hivyo? Kwa sababu kila wakati Ninapokumbana na mtu, kila wakati Ninaposikia hadithi ya mtu, kila wakati Ninaposikia kile alichopitia mtu au ushuhuda wake wa kusadiki Mungu, siku zote Ninatumia msemo huu kuweza kupima kama mtu huyu binafsi ni mtu wa aina ambayo Mungu anataka au la, mtu wa aina ambayo Mungu anapenda. Hivyo msemo huu ni upi, basi? … Msemo ni “tembea katika njia ya Mungu: mche Mungu na kuepuka maovu.” Je, huoni kwamba kauli hii ni rahisi kupindukia? Ilhali ingawa msemo huu unaweza kuwa rahisi, mtu ambaye anao uelewa wa ndani na wa kweli wa msemo huu atahisi kwamba ni wenye uzito mkubwa; kwamba unao thamani nyingi ya kutenda; kwamba ni lugha ya uzima iliyo na uhalisia wa ukweli; ambayo ni lengo la maishani katika kulenga wale wanaotafuta kutosheleza Mungu; na hiyo ni njia ya maisha marefu itakayofuatwa na mtu yeyote anayejali nia za Mungu. … Kwa nini Nikauzungumzia msemo huu? Licha ya mtazamo wenu, au kile mtakachofikiria, lazima Nizungumzie msemo huu kwa sababu unafaa ajabu namna ambavyo Mungu huasisi matokeo ya binadamu. Bila kujali kama uelewa wenu wa sasa wa msemo huu upo, namna mnavyouchukulia, bado Nitawaeleza: Kama mtu anaweza kuutenda msemo huu kwa njia bora na kutimiza kiwango cha kumcha Mungu na kujiepusha na maovu, basi atahakikishiwa kuishi kisha atahakikishiwa kuwa mtu mwenye matokeo mazuri. Kama huwezi kutimiza kiwango kilichowekwa wazi katika msemo huu, basi inaweza kusemekana kwamba matokeo yako hayajulikani. Hivyo basi Ninaongea kwenu kuhusu msemo huu kwa matayarisho yenu ya kiakili, na ili mjue ni kiwango aina gani ambacho Mungu anatumia kuwapima.
kutoka katika “Namna ya Kujua Tabia ya Mungu na Matokeo ya Kazi Yake” katika Neno Laonekana katika Mwili
Asili ya kila mtu inaamua iwapo ataangamizwa; hii inaamuliwa kulingana na asili iliyofichuliwa na mienendo yao na kutafuta kwao ukweli. Miongoni mwa watu wanaofanya kazi sawa na pia kufanya kiasi sawa cha kazi, wale ambao asili yao ni nzuri na wanaomiliki ukweli ni watu wanaoweza kubaki, lakini wale ambao asili yao ya ubinadamu ni mbovu na wasiomtii Mungu anayeonekana ni wale watakaoangamizwa. Kazi ama maneno yoyote ya Mungu yanayoelekezwa kwa hatima ya binadamu yanahusiana na binadamu ipasavyo kulingana na asili ya kila mtu; hakutakuwa na ajali yoyote, na hakika hakutakuwa na kosa hata kidogo. Mtu anapofanya kazi tu ndipo hisia za binadamu ama maana itachanganywa ndani. Kazi anayofanya Mungu ndiyo inayofaa zaidi; hakika Hataleta madai ya uongo dhidi ya kiumbe yeyote.
kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Chanzo: Kanisa la Mwenyezi Mungu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni