Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Tatu
Mwenyezi Mungu alisema, “Kuongezea, miongoni mwa vitu vyote, iwe ni wanyama, mimea, au kila aina ya nyasi, Mungu aliumba pia baadhi ya mimea ambayo ni muhimu kwa kutatua madhara au magonjwa kwa mwili wa mwanadamu. Utafanya nini, kwa mfano, ukichomeka? Je, unaweza kuosha kwa maji? Je, unaweza kutafuta kitambaa na kufunika mahali hapo? Huenda pakajaa usaha au kuambukizwa kwa njia hiyo. Utafanya nini, kwa mfano, ukiungua kwa bahati na moto au na maji moto? Unaweza kumimina maji juu yake? Kwa mfano, ukipata homa, upate mafua, upate majeraha kutokana na kazi ya viungo, maradhi ya tumbo kutokana na kula kitu kibaya, au kupata magonjwa fulani kwa sababu ya mienendo ya maisha au masuala ya hisia, kama vile magonjwa ya mishipa ya damu, hali za kisaikolojia au magonjwa ya ogani zilizo ndani ya mwili—kuna mimea inayolingana ya kutibu haya yote.