Unashuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu mwenye mwili ambaye kwa sasa anafanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Lakini wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanasema kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu kwa kweli ni kazi ya mwanadamu, na pia watu wengi ambao hawamwamini Bwana Yesu wanasema kuwa Ukristo ni imani katika mtu. Bado hatuwezi kutambua hasa ni nini tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, hivyo tafadhali shiriki hili kwa ajili yetu.
Jibu:
Kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu bila shaka ni tofauti. Tukichunguza kwa makini sote tutaweza kuliona. Kwa mfano, tukiangalia matamshi na kazi ya Bwana Yesu na kisha tuangalie maneno na kazi ya mitume, tunaweza kusema kuwa tofauti ni wazi kabisa. Kila neno lililotamkwa na Bwana Yesu ni ukweli na lina mamlaka, na linaweza kufunua mafumbo mengi. Haya yote ni mambo ambayo mwanadamu kamwe hawezi kufanya. Hiyo ndio maana kuna watu wengi sana wanaomfuata Bwana Yesu, ilhali kazi ya mitume inaweza tu kueneza injili, kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na kutoa kwa kanisa. Matokeo ni machache sana. Tofauti katika ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu ni wazi sana. Basi, ni kwa nini watu hawawezi kuitambua? Sababu ni nini? Ni kwa sababu wanadamu wapotovu hawajui Mungu na hawana ukweli wowote.