Sauti Yangu inatoka kama radi, ikitia nuru roboduara zote nne na dunia nzima, na katikati ya radi na umeme, binadamu wanaangushwa chini. Hakuna mwanadamu aliyewahi kusimama imara katikati ya radi na umeme: Wanadamu wengi wanaogopa sana kuja kwa mwangaza Wangu na hawajui cha kufanya. Wakati mwangaza hafifu unaanza kuonekana Mashariki, watu wengi, wakiongozwa na huu mng’ao dhaifu, wanaamshwa mara moja kutoka kwa njozi zao. Lakini, hakuna aliyewahi kutambua kwamba siku imewadia mwangaza Wangu unaposhuka duniani. Wanadamu wengi wanashtuliwa na ujio wa ghafla wa mwangaza; baadhi yao, kwa macho ya kuvutiwa ya dadisi, wanaangalia mwendo wa mwangaza na kutoka upande upi unasongea; ama wengine wanasimama tayari wakitazama mwangaza, ili waweze kuelewa wazi zaidi palipotoka mwangaza.
Iwe ilivyo, kuna yeyote aliyewahi kugundua thamani ya mwangaza wa leo? Kuna yeyote aliyewahi kufahamu ajabu ya mwangaza huu? Wanadamu wengi wamechanganyikiwa tu; wamejeruhiwa machoni na kutupwa chini matopeni na mwangaza. Mtu anaweza kusema kwamba, chini ya mwangaza huu usiokuwa na ufasili, dunia imefunikwa na vurugu, ikifanya mtazamo wa kusikitisha usiovumilika ambao, ukichunguzwa kwa kina, unamtesa mtu na huzuni nyingi. Kutoka hapa, mtu anaelewa kwamba, wakati mwangaza una nguvu kabisa, hali ya dunia itakuwa kwamba haiwezi kumruhusu mwanadamu kusimama mbele Yangu. Binadamu uko katika mng’ao wa mwangaza; tena, binadamu uko katika wokovu wa mwangaza lakini kwa wakati huo huo pia chini ya majeraha yanayotokana na mwangaza: Kuna yeyote asiye chini ya mapigo yanayoua ya mwangaza? Kuna yeyote anayeweza kutoroka kuchoma kwa mwangaza? Nimetembea kote duniani, kutawanya mbegu za Roho Wangu, ili binadamu wote duniani kwa sababu hii wataongozwa nami. Kutoka kwa urefu wa juu wa mbingu, Naangalia chini kwa dunia yote, Nikitazama matukio ya ajabu na yasiyo ya kawaida ya viumbe wa dunia. Sehemu ya juu ya bahari inaonekana kuteswa na mshtuko wa tetemeko la ardhi: Ndege wa bahari wanaruka hapa na pale, wakitafuta samaki wa kumeza. Wakati huo huo, hii haijulikani chini ya bahari, ambayo hali ya sehemu ya juu haiwezi kabisa kuzindua fahamu, kwa sababu chini ya bahari kutulia kama mbingu ya tatu: Hapa viumbe vilivyo hai vikubwa na vidogo vinaishi pamoja kwa amani, bila kushiriki katika “migogoro ya mdomo na ulimi” hata mara moja. Miongoni mwa matukio ya ajabu na ya kichekesho, binadamu ndio unaoona ni vigumu sana kuniridhisha. Hii ni kwa sababu hadhi Niliyompa mwanadamu ni ya juu sana, na hivyo tamaa yake ni kubwa mno, na ndani ya macho yake daima kuna kiwango cha uasi. Ndani ya nidhamu Yangu kwa mwanadamu, ndani ya hukumu Yangu kwake, kumekuwa na mengi yenye maumivu, mengi yaliyo na huruma, lakini kwa mambo haya mwanadamu hana habari hata kidogo. Sijawahi kumshughulikia mwanadamu yeyote kwa ukali: Nimepeana tu marekebisho mwafaka, wakati mwanadamu hajatii, na tu, wakati mwanadamu amekuwa mdhaifu, Nimetoa msaada mwafaka. Lakini, wakati binadamu unaendelea kujitenga nami na zaidi ya hayo unatumia mipango danganyifu ya Shetani kuasi dhidi Yangu, Nitamwangamiza mwanadamu mara moja, Nikiwaacha wanadamu bila nafasi ya kufanya maonyesho makuu ya ujuzi wao mbele Yangu, ili wasiweze tena kujigamba na madoido na hali, wakionea wengine, duniani.
Natumia mamlaka Yangu duniani, Nikidhihirisha kazi Yangu yote. Yote yaliyo katika kazi Yangu yanajitokeza duniani; mwanadamu hajawahi, duniani, kuweza kuufahamu mwendo Wangu mbinguni, wala kutafakari kabisa mizunguko na njia za Roho Wangu. Wanadamu wengi wanaelewa tu maelezo madogo yaliyo nje ya roho, bila kuweza kuelewa hali halisi ya roho. Matakwa Yangu kwa binadamu hayatoki kwa Mimi wa mbinguni Nisiye dhahiri, ama kwa Mimi wa dunia Nisiyekadiriwa: Natoa matakwa ya kufaa kulingana na kimo cha mwanadamu. Sijawahi kumweka yeyote kwa matatizo, wala Sijawahi “kukamua damu ya mtu yeyote” ili kujiridhisha: Inaweza kuwa kwamba matakwa Yangu yamezuiwa na masharti haya pekee? Kwa viumbe lukuki duniani, ni yupi asiyetii tabia za maneno yaliyo mdomoni Mwangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa, wanaokuja mbele Yangu, hajachomwa kabisa kupitia maneno Yangu na moto Wangu unaochoma? Ni yupi kati ya viumbe hawa anayethubutu kujigamba mbele Yangu? Ni yupi kati ya viumbe hawa hainami mbele Yangu? Mimi ni Mungu anayelazimisha tu ukimya kwa viumbe? Kwa mambo lukuki katika uumbaji, Nachagua yale yanaoridhisha nia Yangu; kwa wanadamu lukuki, Nawachagua wale wanaotunza roho Yangu. Nachagua bora zaidi kwa nyota zote, hivyo Naongeza mwangaza hafifu kwa ufalme Wangu. Natembea duniani, Nikitawanya harufu Yangu nzuri kila mahali, nami Naacha umbo Langu kila mahali. Kila pahali panatingika kwa mvumo wa sauti Yangu. Watu kila mahali wanadumu kwa hamu ya mambo waliyozea ya urembo wa mandhari ya jana, kwani binadamu wote wanakumbuka siku za nyuma …
kutoka katika Neno la Mungu Sura ya 17
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni