3.26.2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”


Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”


Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile. Kwa mfano, ingawa Nimejazwa na hukumu na adabu kwa binadamu, kila ninachofanya bado ni kwa ajili ya kumwokoa binadamu, kwa ajili ya kueneza injili Yangu kwa njia bora zaidi na kupanua zaidi kazi Yangu miongoni mwa Mataifa baada ya binadamu kufanywa kuwa kamili. Kwa hiyo leo, katika wakati ambapo watu wengi tayari wametamauka pakubwa, Naendelea na kazi Yangu, Nikiendeleza kazi ambayo lazima Nifanye ili kuhukumu na kuadibu binadamu. Licha ya ukweli kwamba binadamu amechoshwa na kile Ninachosema na licha ya ukweli kwamba hana tamanio la kujali kuhusu kazi Yangu, Ningali natekeleza wajibu Wangu kwa sababu kusudio la kazi Yangu halijabadilika na mpango Wangu asilia hautabadilika. Kazi ya hukumu Yangu ni kumfanya binadamu anitii Mimi kwa njia bora zaidi, na kazi ya kuadibu Kwangu ni kuruhusu binadamu awe na mabadiliko bora zaidi. Ingawa kile Ninachofanya ni kwa minajili ya usimamizi Wangu, Sijawahi kufanya chochote ambacho hakikufaidi binadamu. Hiyo ndiyo maana Nataka kufanya mataifa yote nje ya Israeli kuwa matiifu tu kama Waisraeli na kuwabadilisha kuwa binadamu halisi, ili Niwe na mahali pa usalama katika nchi zilizo nje ya Israeli. Huu ndio usimamizi Wangu; ndiyo kazi Ninayotimiza katika nchi za Mataifa. Hata sasa, watu wengi bado hawauelewi usimamizi Wangu kwa sababu hawajautilia maanani, badala yake wanafikiria tu kuhusu mustakabali na hatima zao. Haijalishi ni nini Ninachosema, watu hawajali kazi Yangu, badala yake wanalenga tu hatima zao za baadaye. Mambo yakiendelea kwa namna hii, kazi Yangu itapanuliwa vipi? Injili Yangu itaenezwa vipi kotekote ulimwenguni? Lazima mjue kwamba wakati kazi Yangu inapanuka, Nitawatawanya, Nitawaadhibu kama vile tu Yehova alivyoyaadhibu makabila ya Israeli. Haya yote yatafanywa ili injili Yangu iweze kuenea kotekote kwenye ulimwengu mzima, ili kazi Yangu iweze kuenezwa kwa Mataifa, ili kwamba jina Langu litukuzwe na watu wazima na watoto kwa pamoja na jina Langu takatifu litatukuzwa katika vinywa vya watu kutoka makabila na mataifa yote. Ili kwamba katika enzi hii ya mwisho jina Langu litatukuzwa miongoni mwa Mataifa, kwamba matendo Yangu yataonekana na mataifa mengine na wataniita Mwenyezi kwa sababu ya matendo Yangu, na kwamba maneno Yangu yatatimika karibuni. Nitawafanya watu wote wajue kwamba Mimi siye tu Mungu wa Waisraeli, lakini Mimi ni Mungu wa Mataifa yote, hata mataifa yale Niliyoyalaani. Nitawafanya watu wote waone kwamba Mimi ndimi Mungu wa viumbe vyote. Hii ndiyo kazi Yangu kubwa zaidi, kusudio la mpango wa kazi Yangu katika siku za mwisho, na kazi ya pekee kutimizwa katika siku za mwisho.

Kazi ambayo Nimekuwa nikisimamia kwa maelfu ya miaka inafichuliwa kabisa tu kwa binadamu katika siku za mwisho. Ni sasa tu ndipo Nimelifumbua fumbo kamili la usimamizi Wangu kwa mwanadamu. Binadamu anajua kusudio la kazi Yangu na zaidi ya yote anapata uelewa wa mafumbo Yangu yote. Na Nimemwambia binadamu kila kitu kuhusu hatima ambayo amekuwa akijali kuhusu. Tayari Nimemfichulia binadamu mafumbo yote yaliyofichwa kwa zaidi ya miaka 5,900. Yehova ni nani? Masiha ni nani? Yesu ni nani? Mnafaa kuyajua haya yote. Mabadiliko makubwa ya kazi Yangu yamo katika majina haya. Je, mmeelewa haya? Jina Langu takatifu linafaa kutangazwa vipi? Jina Langu linafaa kuenezwaje katika taifa lolote ambalo limeniita kwa jina Langu lolote? Kazi Yangu tayari imeanza kupanuka, na Nitaeneza ukamilifu wake katika mataifa yote. Kwa sababu kazi Yangu imetekelezwa ndani yenu, Nitawapiga kama vile Yehova alivyowapiga wale wachungaji wa nyumba ya Daudi kule Israeli, na kuwasababisha kutawanyika miongoni mwa mataifa yote. Kwani katika siku za mwisho, Nitapondaponda mataifa yote kuwa vipande vidogo vidogo na kusababisha watu wao kuenezwa upya. Nitakaporudi tena, mataifa yatakuwa tayari yamegawanywa kwa mipaka iliyowekwa na mwako wa moto Wangu utakaokuwa ukichoma. Katika wakati huo, Nitajionyesha upya kwa binadamu kama jua linalochoma, Nikijionyesha kwao hadharani kwa taswira ya yule Aliye Mtakatifu ambaye hawajawahi kumwona, Nikitembea miongoni mwa mataifa yote, kama vile tu Mimi, Yehova, Nilivyotembea miongoni mwa makabila ya Wayahudi. Kuanzia hapo kuendelea, Nitawaongoza watu huku wakiishi ulimwenguni. Hakika watauona utukufu Wangu hapo na hakika wataona pia nguzo ya wingu hewani ili uwaongoze, kwani Nitaonekana katika sehemu takatifu. Binadamu ataiona siku Yangu ya haki na pia maonyesho Yangu ya utukufu. Hilo litafanyika Nitakapoutawala ulimwengu mzima na kuwaleta wana wengi katika utukufu. Kila pahali duniani, watu watainama, nalo hema Langu takatifu litaundwa miongoni mwao juu ya mwamba wa kazi ambayo Natekeleza sasa. Watu watanihudumia pia hekaluni. Madhabahu, yaliyojaa mambo machafu na ya kuchukiza, Nitayavunjavunja vipandevipande na Nitajenga upya mengine. Madhabahu matakatifu yatarundikwa wanakondoo na ndama waliozaliwa karibuni. Nitaangusha hekalu lililopo leo na kujenga jingine upya. Hekalu lililopo sasa na lililojaa watu wenye chuki litaporomoka na lile Nitakalojenga litajaa watumishi watiifu Kwangu. Kwa mara nyingine watasimama na kunihudumia Mimi kwa utukufu wa hekalu Langu. Kwa hakika mtaiona siku ambayo Nitapokea utukufu mkuu na hakika mtaiona siku ambayo Nitaliangusha hekalu na kujenga lingine upya. Pia, hakika mtaona siku ya kuletwa kwa hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu. Huku Nikilibomoa hekalu, ndivyo Nitakavyoleta hema Langu takatifu hapa ulimwenguni mwa binadamu; itakuwa kama vile tu ambavyo watu wanavyoniona Nikishuka. Baada ya kuangamiza mataifa yote, Nitayakusanya pamoja upya, Nikilijenga hekalu Langu na kuandaa madhabahu Yangu, ili wote waweze kutoa kafara zao Kwangu, kunihudumia Mimi hapo, na kujitolea kwa uaminifu katika kazi Yangu kwenye mataifa mengineyo. Itafanywa namna tu ambavyo wana wa Israeli wanavyofanya sasa, na joho la kuhani na taji la mfalme, utukufu Wangu, Yehova, ukiwa miongoni mwao na uadhama Wangu ukivinjari juu yao na ukiwa nao. Kazi Yangu katika Mataifa itatekelezwa pia katika njia hiyo. Kama vile kazi Yangu kule Israeli ilivyokuwa, ndivyo kazi Yangu katika Mataifa itakavyokuwa kwa sababu Nitaongeza kazi Yangu kule Israeli na kuieneza katika mataifa yale mengine.


kutoka katika Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia

 Sikiliza Nyimbo: Ngurumo Saba Zatoa Sauti - Zikitabiri Kuwa Injili ya Ufalme Itaenea Kote Ulimwenguni


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni