4.01.2019

Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe" (Official Video)


Sauti na maneno ya Roho Mtakatifu | "Waovu Lazima Waadhibiwe" (Official Video)


Mimi ni Mungu wa vitendo Mwenyewe; Sifanyi ishara za ajabu na maajabu, lakini kila pahali hujaa kazi Zangu za ajabu. Njia iliyoko mbele itakuwa angavu mno. Ufunuo Wangu wa kila hatua ndio njia Ninayowaonyesha, mpango Wangu wa usimamizi. Hiyo ni kusema, baadaye ufunuo utakuwa mwingi zaidi na wazi zaidi. Hata katika Ufalme wa Milenia, katika siku zijazo zisizo mbali sana, ni lazima mwendelee kulingana na ufunuo Wangu na mwendo Wangu.  Yote yamechukua umbo, yote yameandaliwa, waliobarikiwa wana baraka za milele zinazowasubiri; wale waliopigwa wana kuadibu kwa milele kunakowasubiri. Siri Zangu ni nyingi sana kwenu, yale ambayo Kwangu ni maneno rahisi zaidi yaweza yakawa magumu sana kwenu; kwa hiyo, Nasema zaidi na zaidi, kwa sababu ninyi huelewa kidogo sana, na mnahitaji Nieleze neno kwa neno, lakini msiwe na wasiwasi mwingi, Nitawanenea kulingana na kazi Yangu.

      Tufuate: Neno la Mungu | "Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni