3.23.2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Tatu


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Tatu


Mwenyezi Mungu alisema, “Kuongezea, miongoni mwa vitu vyote, iwe ni wanyama, mimea, au kila aina ya nyasi, Mungu aliumba pia baadhi ya mimea ambayo ni muhimu kwa kutatua madhara au magonjwa kwa mwili wa mwanadamu. Utafanya nini, kwa mfano, ukichomeka? Je, unaweza kuosha kwa maji? Je, unaweza kutafuta kitambaa na kufunika mahali hapo? Huenda pakajaa usaha au kuambukizwa kwa njia hiyo. Utafanya nini, kwa mfano, ukiungua kwa bahati na moto au na maji moto? Unaweza kumimina maji juu yake? Kwa mfano, ukipata homa, upate mafua, upate majeraha kutokana na kazi ya viungo, maradhi ya tumbo kutokana na kula kitu kibaya, au kupata magonjwa fulani kwa sababu ya mienendo ya maisha au masuala ya hisia, kama vile magonjwa ya mishipa ya damu, hali za kisaikolojia au magonjwa ya ogani zilizo ndani ya mwili—kuna mimea inayolingana ya kutibu haya yote. Kuna mimea inayoendeleza mzunguko wa damu kuondoa ukwamaji, kutuliza maumivu, kukomesha kutokwa na damu, kutia ganzi, kuwasaidia watu kupata tena ngozi ya kawaida, kuondoa ukwamaji wa damu mwilini, na kuondoa sumu mwilini. Kwa ufupi, yote inaweza kutumiwa katika maisha ya kila siku. Ni ya kufaa watu na imetayarishwa na Mungu kwa ajili ya mwili wa mwanadamu iwapo inahitajika. Baadhi ya hiyo iliruhusiwa na Mungu kugunduliwa bila uangalifu na mwanadamu, ilhali mingine iligunduliwa kutoka kwa vitu fulani maalum au na watu fulani waliotayarishwa na Mungu. Baada ya ugunduzi wao, wanadamu wangeipitisha kwa wengine, na halafu watu wengi wangejua kuihusu. Kwa njia hii, uumbaji wa Mungu wa mimea hii unakuwa na thamani na maana. Kwa ufupi, vitu hivi vyote vinatoka kwa Mungu na vilitayarishwa na kupandwa Alipowaumbia wanadamu mazingira ya kuishi. Vitu hivi vyote ni muhimu sana. Je, fikira Zake Mungu zilifikiriwa vizuri sana kuliko za wanadamu? Unapoona yote ambayo Mungu amefanya, unaweza kuhisi upande wa Mungu wa vitendo? Mungu alifanya kazi katika siri. Kabla ya mwanadamu kuingia katika ulimwengu huu, kabla ya kukutana na wanadamu hawa, Mungu alikuwa tayari ameviumba vitu hivi vyote. Kila kitu alichofanya kilikuwa kwa ajili ya wanadamu, kwa ajili ya kuendelea kuishi kwao, na kwa ajili ya kufikiria juu ya kuwepo kwa wanadamu, ili wanadamu waweze kuishi kwa furaha katika ulimwengu huu yakinifu wa ufahari na wingi ambao Mungu aliwatayarishia, bila kuwa na wasiwasi kuhusu chakula au nguo, na bila kukosa chochote. Wanadamu wanaendelea kuzaa na kuendelea kuishi katika mazingira hayo.”

Kuna chochote ambacho Mungu hufanya, bila kujali iwapo kitu hicho ni kikubwa au kidogo, kisicho na thamani au maana? Kila kitu Afanyacho kina thamani na maana. Tujadili hili kutoka kwa swali ambalo watu mara nyingi hulizungumzia. Watu wengi huuliza: Ni kipi kilitangulia, kuku au yai? (Kuku.) Je, utajibuje hili? Kuku alitangulia, hilo ni hakika! Kwa nini kuku alitangulia? Kwa nini yai halingetangulia? Je, kuku haanguliwi kutoka kwa yai? Mayai huangua kuku, kuku huatamiza mayai. Baada ya kuatamiza mayai kwa siku 21, kuku huangua. Kisha kuku huyo hutaga mayai, na kuku huanguliwa tena kutoka kwa mayai. Hivyo kuku alitangulia au yai lilitangulia? Mnajibu "kuku" kwa uhakika. Kwa nini? (Biblia inasema Mungu aliumba ndege na wanyama wa mwitu.) Hiyo ina msingi katika Biblia. Ninataka mzungumze kuhusu maarifa yenu wenyewe kuona iwapo mna maarifa ya kweli ya matendo ya Mungu. Je, mna hakika kuhusu jibu lenu au la? (Kwa sababu vitu vyote vilivyoumbwa na Mungu vinaimarishana na kuzuiana, na kutegemeana vyenyewe. Mungu aliumba kuku, anayeweza kutaga mayai, na kuku anahitaji kuatamiza mayai. Kuna haja hiyo na hali ya utendaji.) Baadhi ya ndugu na dada walicheka. Mbona msizungumze kuhusu jambo hilo? (Mungu aliumba kuku, halafu akampa uwezo wa kuzaa uhai—uwezo wa kuatamiza mayai, na uwezo wa kufanya maisha yaendelee.) Maelezo haya yanakaribia ukweli. Je, ndugu au dada wengine wana maoni? Zungumza kwa huru na kuwasiliana. Hii ni nyumba ya Mungu. Ni kanisa. Ikiwa mna kitu cha kusema, semeni. (Hivi ndivyo ninavyofikiria: Mungu aliumba vitu vyote, na kila kitu alichoumba ni kizuri na kamili. Kuku ni kiumbe hai na ana kazi ya kuzaa na kuatamiza mayai. Hili ni kamili. Kwa hiyo, kuku alitangulia, na kisha yai. Hiyo ndiyo taratibu.) Hili ni hakika. Si fumbo la maana sana, lakini watu wa dunia huliona kuwa la maana sana na hutumia falsafa kwa utoaji hoja. Mwishowe, bado huwa hawana hitimisho. Jambo hili ni kama tu watu kutojua kwamba kuku aliumbwa na Mungu. Watu hawajui kanuni hii, wala hawana uhakika kuhusu iwapo yai au kuku anapaswa kutangulia. Hawajui ni nini kinapaswa kutangulia, hivyo kila mara wao hushindwa kupata jibu. Ni kawaida kabisa kwamba kuku alitangulia. Ikiwa yai lingetangulia kabla ya kuku, basi hiyo haingekuwa kawaida! Bila shaka kuku alitangulia. Hiki ni kitu rahisi sana. Hakiwahitaji nyinyi kuwa wenye maarifa mengi. Mungu aliumba hivi vyote. Kusudi lake la mwanzo lilikuwa ni mwanadamu kuvifurahia. Kuku akiwepo tu yai litakuja kwa kawaida. Je, hilo si dhahiri? Ikiwa yai lingeumbwa kwanza, je, halingehitaji kuku kuliatamiza? Kuumba kuku moja kwa moja ni rahisi kabisa. Kuku angeweza kutaga mayai na pia kuatamiza vifaranga wadogo, huku mwanadamu akiweza kula kuku pia. Je, hilo si la kufaa zaidi. Vile Mungu afanyavyo mambo ni kwa maneno machache ya wazi na sio kwa usumbufu. Yai linatoka wapi? Linatoka kwa kuku. Hakuna yai bila kuku. Alichoumba Mungu ni kiumbe chenye uhai! Wanadamu ni wa upuuzi na wa dhihaka, kila mara wanajitatanisha katika mambo haya rahisi, na mwishowe hata wanafikia kifungu kizima cha hoja za uwongo. Hayo ni ya kitoto! Uhusiano kati ya yai na kuku ni dhahiri: Kuku alitangulia. Hayo ndiyo maelezo sahihi kabisa, njia sahihi kabisa ya kulielewa, na jibu sahihi kabisa. Hii ni ya kweli.


kutoka kwa Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni