Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu-kupata-mwili. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Mungu-kupata-mwili. Onyesha machapisho yote

3.17.2019

Ni zipi tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu?

Ni zipi tofauti muhimu kati ya Mungu mwenye mwili na hao watu ambao hutumiwa na Mungu?


Aya za Biblia za Kurejelea:

"Mimi nawabatiza na maji ili mtubu. Lakini yule ajaye baada ya mimi ni mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye sistahili kuvichukua viatu vyake. Atawabatiza na Roho Mtakatifu, na moto" (MT 3:11).

Maneno Husika ya Mungu:

Kristo ni mwili uliovishwa na Roho wa Mungu. Mwili huu ni tofauti na wa mwanadamu yeyote aliye wa nyama. Tofauti hii ni kwa sababu Kristo sio wa mwili na damu bali ni mwili wa Roho. Anao ubinadamu wa kawaida na uungu kamili. Uungu Wake haujamilikiwa na mwanadamu yeyote. Ubinadamu Wake wa kawaida unaendeleza shughuli Zake zote za kawaida katika mwili, wakati uungu Wake unafanya kazi ya Mungu Mwenyewe.  

11.21.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (1)


  Matamshi ya Mwenyezi Mungu: Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, “Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa.” Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu.