11.15.2017

1. Kutazama Kuonekana kwa Mungu katika Hukumu na Kuadibu Kwake

Mwenyezi Mungu, Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki

Sehemu ya Kwanza
Kama mamia ya mamilioni ya wafuasi wengine wa Bwana Yesu Kristo, tunafuata sheria na amri za Biblia, kufurahia neema tele ya Bwana Yesu Kristo, na kukusanyika pamoja, kuomba, kusifu, na kuhudumu kwa jina la Bwana Yesu Kristo - na haya yote sisi hufanya chini ya utunzaji na ulinzi wa Bwana. Mara nyingi, sisi huwa dhaifu, na mara nyingi sisi huwa wenye nguvu. Tunaamini kwamba matendo yetu yote yanaambatana na mafundisho ya Bwana. Na basi, ni dhahiri shahiri kwamba sisi pia tunajiamini kutembelea njia ya kutii mapenzi ya Baba aliye mbinguni. 
Tunatamani kurudi kwake Bwana Yesu, ujaji tukufu wa Bwana Yesu, kwa mwisho wa maisha yetu hapa duniani, kwa kuonekana kwa ufalme, na kwa kila kitu kama ilivyotabiriwa katika Kitabu cha Ufunuo: Bwana anafika, na analeta maafa, na kuwazawadia walio wema na kuwaadhibu walio waovu, na anawachukua wale wote wanaomfuata na kukaribisha kurudi Kwake angani kumlaki. Kila wakati tunawaza kuhusu haya, hatuna budi ila kujawa na hisia. Tunashukuru kwa kuwa tulizaliwa nyakati za mwisho na tuna bahati ya kutosha ya kushuhudia kuja kwake Bwana. Ingawa tumepitia mateso, yote ni kwa ajili ya malipo ya “utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi sana”; hii ni baraka iliyoje! Hamu hii yote na neema inayopewa na Bwana mara kwa mara hutufanya kuingia kwenye maombi, na hutuleta pamoja kila mara. Labda mwaka ujao, labda kesho, au labda hata mapema wakati mwanadamu hatarajii, Bwana atarejea ghafla, na atatokea kati ya kundi la watu ambao wamekuwa wakimsubiri kwa umakinifu. Sote tunashindana kati yetu, hakuna anayetaka kubaki nyuma, ili kuwa kundi la kwanza la kutazama kuonekana kwa Bwana, na kuwa mmoja ya wale watakaochukuliwa kwenda mbinguni. Tumetoa kila kitu, bila kujali gharama, kwa ajili ya kuwadia kwa siku hii. Baadhi yetu wameacha kazi zao, wengine wameachana na familia zao, wengine kukana ndoa zao, na baadhi yao hata wamepeana akiba zao zote. Ni upendo usio na ubinafsi wa aina gani huu! Uaminifu na utiifu kama huu lazima uwe unashinda ule wa watakatifu wa nyakati za zamani! Kwa kuwa Bwana anavyompa neema yeyote yule ambaye Yeye anataka, na kumrehemu yeyote ambaye Yeye anataka, kujitolea kwetu na matumizi yetu, na matumizi yetu, tunaamini, tayari yametazamika machoni pake. Kwa hivyo, pia, sala zetu za dhati zimefikia masikio Yake, na tunaamini kuwa Bwana atatuzawadia kwa ajili ya kujitolea kwetu. Aidha, Mungu aliturehemu kabla hajauumba ulimwengu, na hakuna atakayenyakua baraka na ahadi Zake kutoka kwetu. Sote tunapanga kuhusu siku za usoni, na kupuuza kwamba kujitolea kwetu na kugharamia ni mambo tunayoweza kutumia ili kuchukuliwa kwenda mbinguni kukutana na Bwana. Pia, bila kusita hata kidogo, sisi tunajiweka kwenye kiti cha enzi cha siku za baadaye, tukitawala mataifa na watu wote kwa jumla, ama tunatawala kama wafalme. Yote haya, sisi huchukulia kama jambo la lazima, kama kitu kinachotarajiwa.
Tunadharau wale wote walio kinyume na Bwana Yesu; na mwishowe, wote wataangamizwa. Nani aliwaambia wasiamini kwamba Bwana Yesu ni Mwokozi? Bila shaka, kuna wakati tunajifunza kutoka kwa Bwana Yesu na tunakuwa na huruma kwa dunia, kwa kuwa hawaelewi, na tunapaswa kuwa wavumilivu na kuwasamehe. Kila kitu tufanyacho ni kwa mujibu wa mafundisho ya Biblia, kwani kila kitu ambacho hakifuatani na Biblia ni uzushi, na madhehebu maovu. Imani kama hiyo imehifadhiwa ndani ya akili zetu. Mola wetu yumo katika Biblia, na tusipoondoka kwenye Biblia basi hatutaondoka kwa Bwana; tukitii kanuni yake, basi tutaokolewa. Sisi husaidiana na kuchochea kila mmoja wetu, na kila wakati tunapokusanyika pamoja ni matumaini yetu kwamba kila kitu tunachosema na kutenda kinaambatana na matakwa ya Bwana na kuwa kinaweza kukubaliwa na Bwana. Licha ya uhasama mkubwa ulioko kwenye mazingira yetu, mioyo yetu imejaa furaha. Tunapowaza kuhusu baraka hizi tunazoweza kupata kwa urahisi, je, kuna kitu ambacho hatuwezi kukiacha? Je, kuna kitu ambacho hatuwezi kutengana nacho? Yote haya ni thabiti, na haya yote yanatazamwa na macho ya Mungu. Sisi, walio wachache na maskini ambao tumeinuliwa kutoka jaani, ni sawa na wafuasi wa Bwana Yesu wa kawaida: Tunaota kuhusu kuchukuliwa kwenda mbinguni, na kubarikiwa, na kutawala mataifa yote. Upotovu wetu umeanikwa peupe machoni pa Mungu, na tamaa zetu na uchoyo zinahukumiwa machoni pa Mungu. Bado, yote haya hutokea bila ajabu, yenye mantiki, na hakuna hata mmoja kati yetu ambaye hushangaa kama hamu yetu ni ya haki, wala hamna kati yetu ambaye anashuku usahihi wa yote yale ambayo sisi tunashikilia. Nani anayeweza kujua mapenzi ya Mungu? Hatujui jinsi ya kutafuta, au kuchunguza, au hata kujishughulisha na njia ambayo mwanadamu hupitia. Kwa maana sisi hujali tu kuhusu kama tutaweza kuchukuliwa kwenda mbinguni, kama tunaweza kubarikiwa, kama kuna pahali tumetengewa kwa ufalme wa mbinguni, na kama sisi tutaweza kupata mgawo wa maji ya uzima wa mto wa maisha na matunda ya mti wa uzima. Je, sisi hatumwamini Bwana, na je, sisi sio wafuasi wake Bwana, kwa ajili ya kupata vitu hivi? Dhambi zetu zimesamehewa, tumetubu dhambi zetu, tumekunywa kikombe cha mvinyo ambao ni mchungu, na tumeweka msalaba migongoni mwetu. Nani anayeweza kusema kuwa gharama ambayo tumelipia haitakubalika na Bwana? Nani anayeweza kusema kuwa hatujatayarisha mafuta yanayotosha? Hatutaki kuwa kama wale bikira wapumbavu, ama kama wale ambao wameachwa. Aidha, tunaomba kila wakati, na kumwomba Bwana atuepushe kutokana na kudanganywa na Kristo wa uongo, kwa maana imeandikwa kwenye Biblia kuwa “Basi iwapo mtu yeyote atawaambia, Tazama, Kristo yupo hapa, au yuko pale; msiamini hili. Kwa maana watatokea makristo wa uongo, na manabii wa uongo, nao watatoa ishara kubwa na maajabu; ili kwamba, ikiwezekana, watawadanganya walio wateule zaidi. (Matayo 24: 23-24). Sisi sote tumeweka mistari hii ya biblia kwenye kumbukumbu, tunazijua aya hizi toka mbele mpaka nyuma, na tunaziona kama hazina ya thamani, kama maisha, na kama vitambulisho vyetu vya wokovu wetu na kuchukuliwa kwenda mbinguni kwetu….
Kwa maelfu za miaka, wanaoishi wamefariki, wakichukua tamaa zao na ndoto zao, na hakuna anayejua kwa ukweli iwapo wameenda kwa ufalme wa mbinguni. Wafu wanarudi, na wamesahau hadithi zote zilizotokea wakati mmoja, na bado wanafuata mafundisho na njia za babu zetu. Kwa hivyo, miaka inavyopita na siku zinavyosonga, hakuna anayejua iwapo Bwana Yesu, Mungu wetu, kwa kweli hukubali yote tunayoyafanya. Kwa urahisi, tunangojea matokeo na kubashiri kuhusu yale yote ambayo yatatokea. Bado Mungu yu kimya siku zote, na hajawahi kutuonekania, wala kusema nasi. Na kwa hivyo, kwa hiari yetu tunahukumu mapenzi ya Mungu na tabia kwa mujibu wa Biblia na ishara. Sisi tumezoea kimya cha Mungu; tumekuwa na mazoea ya kupima haki na makosa ya tabia zetu kutumia njia zetu za mawazo: tumekuwa na mazoea ya kutumia elimu yetu, dhana, na maadili yetu na kuyafanya yachukue nafasi ya matakwa ya Mungu kwetu sisi; tumekuwa na mazoea ya kufurahia neema ya Mungu; tumekuwa na mazoea ya Mungu kutoa msaada wakati sisi tunahitaji msaada huo; tumekuwa na mazoea ya kunyosha mikono yetu kwa Mungu ili tupate mambo yote, na kumuagiza Mungu; na pia tumekuwa na mazoea ya kufuata mafundisho ya dini, bila kutilia maanani jinsi Roho Mtakatifu hutuongoza; zaidi ya hayo, tumekuwa na mazoea ya siku ambazo sisi ni bwana zetu wenyewe. Tunamwamini Mungu wa namna hii, ambaye hatujawahi kukutana naye. Maswali kama namna tabia Yake ilivyo, utu wake na mali yake, mfano wake, kama tutamjua ama hatutamjua wakati atakaporudi, na kadhalika—haya yote hayana umuhimu. Jambo muhimu ni kuwa Yeye yumo mioyoni mwetu, na kuwa tunamsubiri, na kuwa tunaweza kufikiria jinsi Alivyo. Tunathamini imani yetu, na kuthamini hali yetu ya kiroho. Tunaona kila kitu ni kama samadi, na kukanyaga mambo yote kwa nyayo zetu. Kwa sababu sisi ni wafuasi wa Bwana mwenye utukufu, bila kujali jinsi safari yetu ilivyo ndefu na ngumu, bila kujali shida na hatari inayotukumba, hakuna kitu kitakachosimamisha nyayo tunapomfuata Bwana. “Mto wa maji safi ya uzima, wenye kung’aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo. Na katika kila upande wa ule mto, ulikuwapo ule mti wa uzima, unaozaa matunda aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi: Na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa. Wala hapatakuwa na laana tena: Lakini kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo kitakuwa ndani yake; na watumwa wake watamtumikia: Nao watauona uso wake; na jina lake litakuwa katika vipaji vya nyuso zao. Na hapatakuwa na usiku pale; wala hawahitaji mshumaa, wala nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwapa nuru: nao watatawala milele hata na milele (Ufunuo wa Yohana 22:1-5). Kila wakati sisi hukariri maneno hayo, mioyo yetu hujawa na furaha isiyo na kifani na maridhio pia, na machozi hutiririka kutoka machoni mwetu. Shukrani ni kwa Bwana kwa kutuchagua, shukrani ni kwa Bwana kwa neema Yake. Mara mia sasa, yeye ametupa uzima wa milele kwa ulimwengu ujao, na kama angetuuliza tufe sasa, tungetii amri hiyo bila kusita hata kidogo. Bwana! Tafadhali njoo hivi karibuni! Usikawie hata dakika moja tena, kwa kuwa sisi tunakutamani na tumeacha kila kitu kwa ajili yako.
Mungu amenyamaza, na kamwe hawajawahi kujionyesha kwetu, ilhali kazi Yake haijawahi kusimamishwa. Yeye huangalia nchi zote, na huamuru vitu vyote, na kuona maneno yote na matendo yote ya mwanadamu. Usimamizi wake hufanywa hatua kwa hatua na kulingana na mpango wake. Usimamizi wake huendelea kimya kimya, bila madhara ilhali nyayo zake, daima hukaribia binadamu, na kiti chake cha hukumu kimeenezwa katika ulimwengu kwa kasi ya umeme, mara moja kikifuatwa na mshuko wa kiti chake cha enzi kati yetu. Ni tukio la adhimu jinsi gani hilo, yaani, tukio hilo ni uwakilishaji wa mandhari kwa makini na wa kuonyesha Mungu ni mkuu. Kama njiwa na kama simba anayenguruma, Roho anawasili kati yetu sisi sote. Yeye ni mwenye hekima, Yeye ni mwenye haki na wa adhimu, Yeye huwasili kati yetu kwa ukimya, na huwasili na mamlaka akiwa amejazwa na upendo na huruma. Hakuna mtu anayefahamu kuja Kwake, hakuna mtu anayekaribisha kuwasili kwake, na zaidi ya hayo, hakuna mwanadamu ambaye anajua chote atakachokifanya Yeye. Maisha ya mwanadamu inabaki ilivyo bila kubadilika; moyo wake hauna tofauti, na siku zinapita kama kawaida. Mungu anaishi kati yetu kama mtu wa kawaida, kama mfuasi asiye na maana na pia kama muumini wa kawaida. Ana shughuli Zake Mwenyewe, malengo Yake mwenyewe, na vile vile, ana uungu usiomilikiwa na binadamu wa kawaida. Hakuna mtu ambaye ameona kuwepo kwa uungu Wake, na hakuna mtu ambaye ametambua tofauti ya kiini Chake na kile cha binadamu. Sisi huishi pamoja Naye, bila mipaka au kuogopa, kwa kuwa sisi humwona tu kama muumini wa kawaida asiye na maana. Yeye huona matukio yetu yote, na fikra na mawazo yetu yote yanaanikwa wazi mbele Yake. Hakuna mtu ambaye hutilia maanani uwepo Wake, hamna aliye na mawazo yoyote ya kazi Yake, na zaidi ya hayo, hakuna mtu ana tuhuma yoyote kuhusu Yeye ni nani. Sisi huendelea na kazi yetu tu, kana kwamba Yeye hahusiani nasi….
Kwa bahati, Roho Mtakatifu huonyesha kifungu cha maneno “kupitia” Kwake, na ingawa inaonekana ni jambo lisilotarajiwa, tunatambua kuwa huo ni usemi wa Mungu, na tunakubali kwa urahisi kutoka kwa Mungu. Hii ni kwa sababu, bila kujali ni nani anayeonyesha maneno haya, ilimradi yanatoka kwa Roho Mtakatifu tunapaswa kuyakubali, na hivyo hatuwezi kuyakana. Matamshi yajayo yanaweza kuwa kupitia kwangu, au kwako, ama yanaweza kupitia yeye. Bila kujali ni nani, yote ni neema ya Mungu. Ilhali bila kujali mtu ni nani, hatufai kumwabudu, kwa kuwa bila kuzingatia chochote kingine, hawezi kuwa Mungu; hatuwezi kwa njia yoyote kumchagua mtu wa kawaida kama huyu, kuwa ndiye Mungu wetu. Mungu wetu ni mkubwa na mwenye kuheshimika; anawezaje kuwakilishwa na binadamu wa kawaida asiye na umuhimu? Zaidi ya hayo, sisi wote tunasubiri ujaji wa Mungu kuturudisha kwa ufalme wa mbinguni, na kwa hivyo mwanadamu asiye na umuhimu mkubwa anawezaje kuhitimu kufanya kazi ngumu kama hiyo? Bwana akirudi tena, ni lazima iwe juu ya wingu jeupe, linaloonekana na wote. Huo utakuwa wa adhimu namna gani! Itakuwaje Awe amejificha kwa ukimya kati ya kundi la watu wa kawaida? ……
                                                                           Kutoka kwa Kuhusu Sisi
Tufuate Kanisa la Mwenyezi Mungu 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni