7.31.2018

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno

Sura ya 4 Ukweli wa Kazi ya Mungu ya Siku za Mwisho

Umuhimu wa Kazi ya Mungu ya Maneno

Maneno Husika ya Mungu:
Katika Enzi ya Ufalme, Mungu anatumia neno ili kukaribisha enzi mpya, ili kubadilisha mbinu za kazi Yake, na kuweza kufanya kazi katika enzi nzima. Hii ndiyo kanuni ambayo kwayo Mungu hufanya kazi katika Enzi ya Neno. Alikuwa mwili ili kuweza kuzungumza kutoka mitazamo tofauti, kumwezesha binadamu kumwona Mungu kwa kweli, ambaye ni Neno linaloonekana katika mwili, na hekima Yake na maajabu. Kazi kama hiyo inafanywa ili kwa njia bora zaidi kutimiza shabaha za kumshinda binadamu, kumkamilisha binadamu, na kumwondoa binadamu. Hii ndiyo maana ya kweli ya kutumia neno ili kufanya kazi katika Enzi ya Neno.

7.30.2018

Tamko la Hamsini

Tamko la Hamsini

Mwenyezi Mungu alisema, Makanisa yote na watakatifu wote wanapaswa kutafakari kuhusu siku zilizopita na kutumainia siku za usoni: Ni mangapi kati ya matendo yenu ya zamani ndiyo yanayostahili, na ni mangapi kati yao yalishiriki katika ujenzi wa ufalme? Usiwe mtu mwenye kujifanya kujua kila kitu! Unapaswa kuona wazi dosari zako na unafaa kuelewa hali zako mwenyewe. Najua kwamba hakuna yeyote kati yenu yuko tayari kuweka jitihada yoyote na kugharimika muda wowote kuhusu hili, kwa hivyo hamuwezi kupata ujuzi wowote. Mnaharibu muda wenu wote katika kula, kunywa na kustarehe.

7.28.2018

Mungu Anapata Mwili ili Tu Kumshinda Shetani na Kuwaokoa Binadamu

Mungu Anapata Mwili ili Tu Kumshinda Shetani na Kuwaokoa Binadamu

I
Wakati wa kupata mwili huku kwa Mungu duniani,
Anafanya kazi Yake miongoni mwa wanadamu.
Kazi hii yote ina kusudi moja—kumshinda ibilisi Shetani.
Atamshinda Shetani kupitia kumshinda mwanadamu,
pia kupitia kukufanya mkamilifu. 

7.27.2018

Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Kwa Nini Yasemekana Kwamba Kuzijua Awamu Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kujua Mungu?

(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)
Kujua Hatua Tatu za Kazi ya Mungu Ndiyo Njia ya Kumjua Mungu
Kazi ya kumsimamia mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu, na ina maana kuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu imegawanywa katika hatua tatu. Hatua hizi tatu hazihusishi kazi ya kuuumba ulimwengu, ila ni hatua tatu za kazi ya Enzi ya Sheria, Enzi ya Neema, na Enzi ya Ufalme. Kazi ya kuiumba dunia ilikuwa kazi ya kusababisha uwepo wa wanadamu wote. Haikuwa kazi ya kumwokoa mwanadamu, na haina uhusiano na kazi ya kumwokoa mwanadamu, kwa kuwa dunia ilipoumbwa mwanadamu hakuwa amepotoshwa na Shetani, na hivyo hakukuwa na haja ya kutekeleza kazi ya kumwokoa mwanadamu. Kazi ya kumwokoa mwanadamu ilianza tu baada ya mwanadamu kupotoshwa na Shetani, na kwa hivyo kazi ya kumsimamia mwanadamu pia ilianza tu punde mwanadamu alipopotoshwa.

7.26.2018

Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia


Swahili Gospel Full Movie "Fichua Siri Kuhusu Biblia" | Kufichua Hadithi ya Kweli ya Biblia


    Feng Jiahui na wazazi wake waliamini katika Bwana tangu alipokuwa mdogo. Alipokuwa na umri wa miaka 18 aliingia katika shule ya seminari, na katika miaka yake ya 30 akawa mhubiri katika kanisa la nyumba huko Shanxi, Uchina. Kwa miaka mingi, Feng Jiahui alidumisha imani madhubuti ya kuwa Biblia ilitiwa msukumo na Mungu, na kwamba lazima tuamini katika Mungu kwa mujibu wa Biblia. Aliamini kuwa hakukuwa na maneno yaliyonenwa na Mungu nje ya Biblia, na kwamba kuondoka kutoka kwa Biblia kutakuwa uzushi.

7.25.2018

Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Uhusiano Kati ya Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Maneno Husika ya Mungu:
Kutoka kwa kazi ya Yehova mpaka ile ya Yesu, na kutoka kwa kazi ya Yesu hadi kwa kazi iliyoko kwa awamu hii ya sasa, awamu hizi tatu zinajumlisha upana wote wa usimamizi wa Mungu, na zote ni kazi za Roho mmoja. Kutoka Alipoumba ulimwengu, Mungu Amekuwa Akisimamia wanadamu. Yeye ndiye Mwanzo na ndiye Mwisho; Yeye ndiye wa Kwanza na wa Mwisho, na Yeye ndiye mwanzilishi wa enzi na Yeye ndiye huleta enzi kwenye kikomo. Awamu tatu za kazi, katika enzi tofauti na maeneo mbalimbali, hakika yanafanywa na Roho mmoja. Wote ambao wanatenganisha awamu hizi tatu wanampinga Mungu.

7.24.2018

Mabadiliko ya Mtu Aliyeanguka

Ushuhuda-wa-Kuipitia-Hukumu-ya-Kristo, Kanisa, Yesu, Roho Mtakatifu

 Mabadiliko ya Mtu Aliyeanguka

Tong Xin    Mkoa wa Fujian
Nilizaliwa vijijini. Nilitoka kwa nasaba ya wakulima wanyenyekevu na zaidi ya hayo familia yetu ilikuwa na watu wachache, kwa hiyo mara nyingi tulikuwa tunadhulumiwa. Nilipokuwa na umri wa miaka 13, kulikuwa na mtoto aliyepigwa na mtu fulani kutoka nje ya kijiji chetu. Wanakijiji walimlaumu kwa uongo baba yangu kwa kuchochea hilo na wakasema walitaka kupekua nyumba yetu na kuchukua ngawira mali yetu, kuchukua nguruwe wetu na hata kumpiga baba yangu.

7.23.2018

Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Kusudio na Umuhimu wa Kila Mojawapo ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu.

Maneno Husika ya Mungu:

Kazi ambayo Yehova alifanya kwa Waisraeli ilianzisha mahali pa Mungu pa asili miongoni mwa binadamu, ambapo pia palikuwa pahali patakatifu ambapo Alikuwapo. Aliwekea kazi Yake mipaka kwa watu wa Israeli. Mwanzoni, Hakufanya kazi nje ya Israeli; badala yake, Aliwachagua watu Aliowaona kuwa wa kufaa ili kuzuia eneo la kazi Yake. Israeli ni mahali ambapo Mungu aliwaumba Adamu na Hawa, na kutoka katika mavumbi ya mahali hapo Yehova alimuumba mwanadamu; mahali hapa pakawa kituo cha kazi Yake duniani. Waisraeli, ambao walikuwa wa ukoo wa Nuhu na pia wa ukoo wa Adamu, walikuwa msingi wa kibinadamu wa kazi ya Yehova duniani.

7.22.2018

2018 Best African Worship Song "Miaka Elfu Mbili ya Kungoja" | Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu

2018 Best African Worship Song "Miaka Elfu Mbili ya Kungoja" | Karibu Kurudi kwa Bwana Yesu


Utambulisho

Kwamba Mungu amekuwa mwili
hutikisa ulimwengu wa kidini,
inavuruga utaratibu wa kidini,
na inakoroga roho za wale
wanaongoja kuonekana kwa Mungu.

Tamko la Kwanza

Tamko la Kwanza

Mwenyezi Mungu alisema, Je, wale wanaoshuhudia maneno Yangu huyakubali kwa kweli? Je, mnanijua kwa kweli? Mmejifunza utiifu kweli? Ninyi hutumia rasilimali kwa ajili Yangu kwa uaminifu? Mmekuwa na ushuhuda thabiti, usiokubali kushindwa Kwangu mlipokabiliwa na joka kuu jekundu? Je, moyo wenu wa ibada hulifedhehesha kweli joka kuu jekundu? Ni kupitia tu kwa jaribio la maneno Yangu ndipo Naweza kutimiza lengo Langu la kulitakasa kanisa na kuwachagua wale wanaonipenda Mimi kweli.

7.21.2018

Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu.

Sura ya 3 Ukweli Kuhusu Awamu Tatu za Kazi ya Mungu

Nia ya Awamu Tatu za Kazi ya Mungu.

Maneno Husika ya Mungu:

Mpango Wangu mzima wa usimamizi, mpango ambao una urefu wa miaka elfu sita, unashirikisha hatua tatu, au enzi tatu: Enzi ya Sheria mwanzoni; Enzi ya Neema (ambayo pia ni Enzi ya Ukombozi); na katika siku za mwisho, Enzi ya Ufalme. Kazi Yangu katika enzi hizi tatu hutofautiana katika maudhui kulingana na asili ya kila enzi, lakini katika kila hatua huambatana na mahitaji ya mwanadamu—au, kwa usahihi zaidi, inafanywa kulingana na ujanja ambao Shetani hutumia katika vita Vyangu dhidi yake. Madhumuni ya Kazi Yangu ni kumshinda Shetani, ili kudhihirisha hekima Yangu na kudura, kufichua ujanja wote wa Shetani na hivyo kuokoa wanadamu wote, wanaoishi chini ya miliki yake.

7.20.2018

Nilifurahia karamu kubwa

Umeme wa Mashariki, Mungu, Kristo, wokovu

Nilifurahia karamu kubwa

Xinwei    Mkoa wa Zhejiang
Juni 25 na 26 zilikuwa siku zisizohaulika. Eneo letu la Zhejiang lilipata tukio kubwa, viongozi wengi na wafanyakazi wa eneo wakiwa wamekamatwa na joka kubwa jekundu. Ni wachache wetu tu tuliokimbia bila kuumia na, mioyo yetu ikiwa imejaa shukrani, tulikula kiapo cha siri kwa Mungu: kushirikiana vizuri na kazi iliyokuwa ifuate. Kufuatia hilo tulianza kazi yenye msisimko na shughuli nyingi ya kushughulika na matokeo.

7.19.2018

Ni Nini Maana ya “Kumkosea Mungu”

Ni Nini Maana ya “Kumkosea Mungu

Ukilibadilisha au kulikanganya neno la Mungu Mwenyewe, basi hiyo ni sawa na uasi wa Mungu, kukufuru dhidi Yake na usaliti. Hii ni sawa tu na malaika mkuu kusema:"Mungu, Unaweza kuumba mbingu na ardhi na vitu vyote na Unaweza kufanya miujiza, lakini pia mimi ninaweza. Unapanda juu kwenye kiti cha enzi, na hivyo hivyo mimi pia napanda. Unatawala mataifa yote, Ninatawala mataifa yote pia. Wewe ulimuumba mwanadamu ilhali mimi ninawatawala!" Je, hii si ya hali sawa? Wengine wana mtazamo fidhuli kuhusu mipangilio ya kazi kutoka juu.

7.18.2018

Mungu Ameonekana Mashariki mwa Dunia na Utukufu

 Mungu Ameonekana Mashariki mwa Dunia na Utukufu

Mungu anafanya kazi ulimwenguni kote.
Kelele za radi ya Mashariki hazipungui,
Zikitikisa madhehebu na makundi yote.
Ni sauti ya Mungu iliyoleta vyote wakati wa sasa.
Ni sauti Yake ndiyo itashinda kila kitu.
Wanaanguka katika mtiririko huu, na kumtii Yeye.
Mungu ameshachukua utukufu kutoka duniani kitambo,

7.17.2018

Trela ya Filamu "Yule Anayeshikilia Ukuu juu ya Kila Kitu" | Ushuhuda wa Nguvu ya Mungu


Trela ya Filamu "Yule Anayeshikilia Ukuu juu ya Kila Kitu" | Ushuhuda wa Nguvu ya Mungu

    Trela ya Filamu "Yule Anayeshikilia Ukuu juu ya Kila Kitu" | Ushuhuda wa Nguvu ya Th Mungu roughout the vast universe, all celestial bodies move precisely within their own orbits. Under the heavens, mountains, rivers, and lakes all have their boundaries, and all creatures live and reproduce throughout the four seasons in accordance with the laws of life…. This is all so exquisitely designed—is there a Mighty One ruling and arranging all this? Since coming into this world crying we have begun playing different roles in life.

Sura ya 15. Kutoka katika Siasa Isiyo na Kadri hadi Kutafuta kuwa Msaliaji

Kanisa la Mwenyezi Mungu,ukweli,upendo wa Mungu

Sura ya 15. Kutoka katika Siasa Isiyo na Kadri hadi Kutafuta kuwa Msaliaji

1. Uhamaji wa Watu kuelekea kwenye Siasa Isiyo na Kadri
Je, nyote mmekuwa mkitafuta nini hivi karibuni? Je, imekuwa mabadiliko ya tabia na kuwa na ushuhuda wa Mungu? Haijakuwa hiyo! Nawaona watu wengi tena wakitafuta kufa kwa ajili ya Mungu ili kumuaibisha Shetani. Je, mnasubiri tu kuadhibiwa badala ya kupanga kutenda ukweli ama kutafuta kubadilishwa kwa tabia, kulipiza upendo wa Mungu? Baada ya kusoma “Usaliti (1) “na “Usaliti (2), “watu walikuwa na mipango ya kufa.

7.16.2018

Sura ya 16. Imani Tatu katika Mungu wa Vitendo

Sura ya 16. Imani Tatu katika Mungu wa Vitendo

Ndani ya familia ya Mungu, kuna imani kadhaa tofauti katika Mungu; imani hizi tofauti lazima zitambulishwe ili kuona wewe ni wa gani.
Na imani ya aina ya kwanza, ambayo pia ni aina bora zaidi, mtu huyo ana uwezo wa kuyaamini maneno ya Mungu katika vitu vyote; ana uwezo wa kukubali ufichuzi wote wa Mungu, ushugulikiaji, na upogoaji; yeye ni mwagalifu kwa mapenzi ya Mungu, hupenda, ni mwaminifu kwa, na humwabudu Mungu, na ako tayari kutenda ukweli. Imani kama hiyo huzaa maisha, na inawezesha mtu kupata mabadiliko katika tabia na kupatwa na Mungu.

7.15.2018

Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mwenyezi Mungu,siku za mwisho

Sura ya 2 Ukweli wa Majina ya Mungu

Kwa Nini Mungu Hutajwa Majina, na Jina Moja Linaweza Kuwakilisha Uzima wa Mungu?

Maneno Husika ya Mungu:
Je, Jina la Yesu “Mungu pamoja nasi,” linaweza kuwakilisha tabia ya Mungu kwa ukamilifu wake? Je, linaweza kueleza Mungu kwa ukamilifu? Kama mwanadamu atasema ya kwamba Mungu Ataitwa tu Yesu, na hawezi kuwa na jina lingine kwa sababu Mungu hawezi kubadilisha tabia yake, basi maneno hayo ni kufuru! Je, unaamini kwamba jina la Yesu, Mungu pamoja nasi, linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu? Mungu Anaweza kuitwa majina mengi, lakini baina ya majina haya mengi, hamna moja ambalo linaweza kujumlisha yote ambayo Mungu Anamiliki, na hamna jina moja ambalo linaweza kumwakilisha Mungu kikamilifu. Na hivyo Mungu Ana majina mengi, lakini majina haya mengi hayawezi kuelezea tabia ya Mungu kikamilifu, kwa kuwa tabia ya Mungu ni tajiri sana, na inapita maarifa ya mwanadamu.

7.14.2018

24. Hakuna Anayeweza Kufanya Kazi Badala Yake

24. Hakuna Anayeweza Kufanya Kazi Badala Yake

Kazi ya Mungu hufanywa na Mungu Mwenyewe.
Ni Yeye ndiye Anayeianzisha kazi Yake, na ni Yeye anayeikamilisha.
Ni Yeye anayeipanga kazi.
Ni yeye ndiye anayeisimamia, na zaidi kuifanikisha kazi hiyo.

7.13.2018

3. Wokovu Unawezekana Tu Kupitia Imani kwa Mwenyezi Mungu.

3. Wokovu Unawezekana Tu Kupitia Imani kwa Mwenyezi Mungu.

Maneno Husika ya Mungu:   
Yesu Alipokuja katika ulimwengu wa mwanadamu, Alileta Enzi ya Neema na Akatamatisha Enzi ya Sheria. Wakati wa siku za mwisho, Mungu kwa mara nyingine Alipata mwili, na Alipopata mwili mara hii, Alikamilisha Enzi ya Neema na Akaleta Enzi ya Ufalme. Wale wote wanaokubali kupata mwili kwa Mungu kwa mara ya pili wataongozwa mpaka Enzi ya Ufalme, na wataweza kukubali kibinafsi uongozi wa Mungu. Hata ingawa Yesu Alifanya kazi nyingi miongoni mwa wanadamu, Yeye Alimaliza tu ukombozi wa wanadamu wote na akawa sadaka ya dhambi ya mwanadamu, na Hakumwondolea mwanadamu tabia yake yote ya upotovu. Kumwokoa mwanadamu kikamilifu kutokana na ushawishi wa Shetani hakukumlazimu Yesu kuchukua dhambi zote za mwanadamu kama sadaka ya dhambi tu, lakini pia kulimlazimu Mungu kufanya kazi kubwa zaidi ili kumwondolea mwanadamu tabia yake kikamilifu, ambayo imepotoshwa na Shetani.

7.12.2018

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Sura ya 59. Namna ya Kumridhisha Mungu katikati ya Majaribu

Ninaibua maswali machache kwa tafakari yenu: Tangu mara ya mwisho tuliposema kwamba kutakuwa na miaka saba mingine ya majaribu makubwa, iwe ni kwa dhiki au majanga, je, mmegundua kusudi la Mungu kupitia kwa hayo? Ni asili gani ya binadamu mnaweza kuona katika mijibizo na mitazamo ya watu kwa miaka hii saba ya majaribu? Hili litachanganuliwa vipi? Fikirieni hilo.

7.11.2018

Sura ya 13. Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao

Umeme wa Mashariki,Kristo,hukumu

Sura ya 13. Maana ya Utendaji wa Watu Kuamua Matokeo Yao

1. Hakuna Ambaye Angeokolewa iwapo Mungu Angeangalia Tu Maonyesho ya Asili ya Watu
Kwa sasa, utendaji wa watu unaamua matokeo yao, lakini huu utendaji ni upi? Je, unaujua? Nyinyi mnaweza kufikiri kwamba hili linarejelea tabia ya watu iliyopotoka ikijionyesha kazini mwao, lakini halimaanishi lile.

7.10.2018

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Kiini cha Mwili Ulio na Mungu

Mwenyezi Mungu alisema, Mungu mwenye mwili wa kwanza Aliishi duniani kwa miaka thelathini na tatu na nusu, lakini Alitekeleza huduma Yake kwa miaka mitatu na nusu pekee ya hiyo miaka yote. Kipindi Alichofanya kazi na kabla Aanze kazi Yake, Alikuwa na ubinadamu wa kawaida. Aliishi na ubinadamu Wake wa kawaida kwa miaka thelathini na tatu na nusu. Katika miaka yote mitatu na nusu ya mwisho Alijifichua kuwa Mungu mwenye mwili.

7.09.2018

38. Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mungu,Kristo

38. Siri Niliyoishikilia kwa Kina Ndani ya Moyo Wangu

Wuzhi    Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong
Katika majira ya kuchipua ya mwaka wa 2006, nilinyang'anywa cheo changu kama kiongozi na nikarudishwa nilikotoka kwa sababu nilifikiriwa kuwa "bwana ndiyo" sana. Niliporejea mara ya kwanza, nilitumbukia ndani ya kikalibu cha mateso na maumivu makubwa. Sikuwahi kufikiri kwamba baada ya miaka mingi ya uongozi mambo yangeharibika kwa sababu ya kuwa "bwana ndiyo."

Kazi na Kuingia (10)

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Yesu, upendo wa Mungu

Kazi na Kuingia (10)

Kwa wanadamu kuendelea mbele kiasi hiki ni hali isiyo na kigezo. Kazi ya Mungu na kuingia kwa mwanadamu vinaendelea bega kwa bega, na hivyo kazi ya Mungu, pia, ni tukio kubwa lisilo na kifani. Kuingia kwa mwanadamu hadi sasa ni ajabu ambayo kamwe haijawahi kufikiriwa na mwanadamu.

7.08.2018

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia”

Uchaguzi Kutoka katika Mafungu Kumi ya Neno la Mungu juu ya “Kazi na Kuingia”

1. Tangu watu waanze kukanyaga njia sahihi ya maisha, kumekuwa na mambo mengi ambayo bado hayajaeleweka vizuri. Bado wapo kwenye mkanganyiko kabisa kuhusu kazi ya Mungu, na kuhusu kiasi gani cha kazi wanapaswa kufanya. Hii, kwa upande mmoja, ni kwa sababu ya kuwa na uelekeo tofauti wa uzoefu wao na mipaka katika uwezo wao wa kupokea; kwa upande mwingine, ni kwa sababu kazi ya Mungu bado haijawaleta watu katika hatua hii. Kwa hiyo, kila mtu anapata utata kuhusu masuala mengi ya kiroho.

20. Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

20. Ni Nani Anayejua Moyo wa Kutunza wa Mungu?

Qingxin    Mji wa Zhengzhou, Mkoa wa Henan
Kuhusu kipengele cha ukweli cha "Mungu ni mwenye haki ", siku zote nilikuwa na ufahamu wa upuuzi kwa kiasi fulani. Nilidhani kuwa almradi mtu fulani hufichua upotovu katika kazi yake au hufanya makosa ambayo huiharibu kazi ya kanisa, mtu huyo atakabiliwa na rada, au kupoteza kazi yake au aathiriwe na adhabu.

7.07.2018

13. Kuelewa Mapenzi ya Mungu Katikati ya Matatizo

Umeme wa Mashariki,Mungu,Injili

13. Kuelewa Mapenzi ya Mungu Katikati ya Matatizo

Xiao Rui    Mji wa Panzhihua, Mkoa wa Sichuan
Nilipokuwa nikihubiri injili nilikutana na viongozi wa madhehebu ambao walisema uongo ili kupinga na kuvuruga, na kuwaita polisi. Hili lilisababisha wale niliokuwa nikihubiria kutothubutu kuwasiliana nasi, na wale ambao walikuwa tu wameikubali injili kutoweza kuwa na imani katika kazi ya Mungu. Nilipofanya kazi kwa bidii sana lakini matokeo yalikuwa duni, nilifikiri: kazi ya Kiinjili ni ngumu sana kutekeleza.

7.06.2018

Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu

Epuka Ushawishi wa Giza na Upatwe na Mungu

Ushawishi wa giza ni utumwa wa Shetani, ni ushawishi wa Shetani, na ni ushawishi ambao una hali ya kifo.
Baada ya kumwomba Mungu kwa dhati, unaelekeza moyo wako kwa Mungu kikamilifu, katika hatua hii, moyo wako unasongezwa na Roho wa Mungu, uko tayari kujitoa mwenyewe kikamilifu, na katika wakati huu, umeepuka ushawishi wa giza. Kama yote ambayo mtu anafanya yanampendeza Mungu na anapatana na matakwa ya Mungu, basi yeye ni mtu ambaye anaishi ndani ya maneno ya Mungu, yeye ni mtu anayeishi chini ya uangalizi na ulinzi wa Mungu.

12. Wakati wa Uzoefu Mmoja Niliona Ulinzi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, ushuhuda

12. Wakati wa Uzoefu Mmoja Niliona Ulinzi wa Mungu

Yongxin, Jiji la Yibin, Mkoa wa Sichuan
Hatukuwahi kumwamini Mungu kabla. Mnamo mwaka wa 2005, tukitiwa moyo na Mungu, mume wangu, baba mkwe wangu, mjomba wangu, na mimi wote tuliikubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho. Baada ya muda mfupi, kanisa lilinipangia kufanya wajibu wa kuhifadhi vitabu. Baadaye, nyumba yetu ilishika moto, na wakati wa moto huu tulipokea ulinzi wa Mungu wa ajabu. Mungu kwa hakika ni mwenyezi!

7.05.2018

51. Nilipitia Wokovu wa Mungu

Umeme wa Mashariki, Mungu, Injili

51. Nilipitia Wokovu wa Mungu

Cheng Hao    Mji wa Yongzhou, Mkoa wa Hunan
Kwa neema ya Mungu, mimi na mke wangu tulipandishwa vyeo hadi kwa timu ya injili ya pili ili kutimiza wajibu wetu. Muda mfupi uliopita, mke wangu alipandishwa cheo kuwa mkurugenzi wa timu, huku mimi, kutokana na kiburi changu mwenyewe na utukutu wangu, nilipoteza kazi ya Roho Mtakatifu na kupelekwa nyumbani kutafakari juu ya matendo yangu.

30. Tafakuri kuhusu Kubadilishwa

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki, Kanisa

30. Tafakuri kuhusu Kubadilishwa

Yi Ran    Mji wa Laiwu , Mkoa wa Shandong
Wakati fulani awali, kwa sababu yangu kutoelewa kanuni iliyotumiwa na kanisa ya masahihisho ya wafanyakazi wa kanisa, wakati kanisa lilibadilisha kiongozi, dhana iliibuka ndani yangu. Kutoka kwa kile nilichoweza kuona, dada aliyebadilishwa alikuwa mzuri sana kwa kupokea na kushirikiana ukweli, na aliweza kuwa wazi juu ya maonyesho yake ya upotovu.

7.04.2018

9. Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Kanisa,Mungu,

9. Katikati ya Maafa Niliona Ulinzi wa Mungu

Zhang Min, Beijing
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mvua ilianza kunyesha sana asubuhi. Kufikia wakati wa adhuhuri wakati nilipaswa kwenda kwa mkutano, niliona mvua ilikuwa nzito sana kiasi kwamba sikutaka kwenda. Lakini ulikuwa mara moja tu kwa wiki, kama singeenda singekuwa na njia yoyote ya kufanya kazi yangu ya kanisa. Chochote kilichokuwako kikiendelea nje, bado ilinipasa nishiriki nao. Nilipofikiria hayo, niliharakisha kwenda kwa mkutano.

8. Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Mungu,Injili

8. Mungu Aliilinda Familia Yetu Wakati wa Maafa

Wang Lan, Beijing
Mnamo Julai 21, mwaka wa 2012, mafuriko makubwa zaidi tangu miaka sitini yalipitia kijijini mwetu kwa nguvu mno. Maafa yalianguka kutoka mbinguni, maji ya mafuriko yalichanganya matope na mawe na kuharibu kijiji chote. Nyumba nyingi  ziliharibiwa na maji na maporomoko ya matope. Baada ya saa kumi na moja alasiri hiyo, mvua ilikuwa ikinyesha kwa nguvu sana.

7.03.2018

13. Kama Tu Binadamu Watamwabudu Mungu wa Kweli Ndiyo Wataweza Kuwa na Jaala Nzuri

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Mungu

13. Kama Tu Binadamu Watamwabudu Mungu wa Kweli Ndiyo Wataweza Kuwa na Jaala Nzuri

Mungu aliumba dunia hii. Aliumba binadamu.
Alikuwa mjenzi wa utamaduni wa zamani wa Ugiriki na ustaarabu wa binadamu.
Mungu tu ndiye Anayefariji, Anayefariji binadamu huyu.
Mungu pekee ndiye Anayejali kuhusu binadamu huyu mchana na usiku.
Kukua kwa binadamu na kuendelea 
hakutenganishwi na mamlaka ya Mungu, mamlaka kuu ya Mungu.
Historia na siku za baadaye za binadamu
zinahusiana sana na mpango wa Mungu, mpango wa Mungu. 

3. Ujana Uliotumiwa Bila Majuto

Umeme wa Mashariki, siku za mwisho, upendo wa Mungu

3. Ujana Uliotumiwa Bila Majuto

Xiaowen, Chongqing
"Upendo ni hisia safi, safi bila ya dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vikwazo au umbali. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Ukipenda hudanganyi, kunung'unika, kutelekeza, kutarajia kupata malipo" ("Upendo safi bila Dosari" katika Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya). Wimbo huu wa neno la Mungu siku moja ulinisaidia kupitia maumivu ya maisha ya muda mrefu yaliorefuka bure gerezani ambao ulidumu miaka 7 na miezi 4.

7.02.2018

28. Vigezo vya Mtu Mwema Kwa Dhati

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,

28. Vigezo vya Mtu Mwema Kwa Dhati

Moran   Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong
Tangu nilipokuwa mtoto, siku zote nilishikiza umuhimu mkubwa kwa jinsi watu wengine walivyoniona na ukadiriaji wao kwangu. Ili niweze kupata sifa kutoka kwawengine kwa kila kitu nilichokifanya, sikubishana na yeyote asilani wakati wowote kitu chochote kilichoibuka, ili kuepuka kuharibu picha nzuri watu wengine walikuwa nayo kwangu. Baada ya kuikubali kazi ya Mungu katika siku za mwisho, niliendelea kwa njia hii, nikizingatia kwa kila njia iwezekanayo picha nzuri ambayo ndugu zangu wa kiume na wa kike walikuwa nayo kwangu.

Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Mbili

Ufafanuzi wa Tamko la Arubaini na Mbili

Sijui kama watu wameona mabadiliko yoyote katika tamko la leo. Huenda watu wengine wameona kidogo, lakini hawathubutu kusema kwa kweli. Labda wengine hawajatambua chochote.

7.01.2018

73. Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo?

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Yesu, siku za mwisho

73. Kwa Nini Nimetembea Njia ya Mafarisayo?

Suxing Mkoa wa Shanxi
Mimi ni mtu mwenye kiburi na majivuno, na cheo kimekuwa udhaifu wangu. Kwa miaka mingi, nimefungwa na sifa na cheo na sijaweza kujiweka huru kutoka kwazo. Mara kwa mara nimepandishwa cheo na kubadilishwa na mtu mwingine; nimekuwa na vizuizi vingi katika cheo changu na nimekumbwa na matuta mengi njiani. Baada ya miaka mingi ya kushughulikiwa na kusafishwa, nilihisi kwamba sikuwa nachukulia cheo changu kwa uzito.

7. Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu

Kanisa la Mwenyezi Mungu, Mungu, upendo wa Mungu

7. Katikati ya Maafa Niliiona Tabia ya Haki ya Mungu

Li Jing, Beijing
7 Agosti, mwaka wa 2012
Siku hiyo, ilianza kunyesha asubuhi. Nilikwenda kwa mkutano nyumbani mwa ndugu mmoja, wakati mvua ilipoendelea kuongezeka zaidi na zaidi kwa uzito. Kufikia alasiri ilikuwa ikinyesha kana kwamba ilitoka mbinguni moja kwa moja. Wakati tulipomaliza mkutano wetu, mvua ilikuwa imeingia katika ua wa ndugu yangu, lakini kwa sababu nilikuwa na wasiwasi juu ya familia yangu, nilijitahidi kwenda nyumbani. Nusu ya barabara huko, baadhi ya watu waliokimbia hatari waliniambia, "Je, si wewe unatoroka, bado unakwenda nyumbani?" Nilipofika nyumbani, mtoto wangu aliniuliza, "Je, mafuriko hayakukuzoa?" Ni hapo tu nilipojua kwamba sikuwa na Mungu moyoni mwangu.