3.29.2019

Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?

 Ni jinsi gani Mungu anayepata mwili ili kufanya kazi ya hukumu huimaliza imani ya wanadamu katika Mungu asiye yakini na enzi ya giza ya utawala wa Shetani?


Aya za Biblia za Kurejelea:

"Na itatimia katika siku za mwisho, kwamba mlima wa nyumba ya Yehova utawekwa imara juu ya milima, na utainuliwa juu zaidi ya vilima; na mataifa yote yatamiminika kwenda kwake. Na watu wengi wataenda na kusema, Njoo, na hebu twende juu ya mlima wa Yehova, kwa nyumba ya Mungu wa Yakobo; na atatufunza kuhusu njia zake, nasi tutatembea kwa njia zake: kwani sheria itatoka Zayuni, na neno la Mungu litatoka Yerusalemu. 

3.28.2019

Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God


Wimbo wa Kuabudu | "Tabia ya Haki ya Mungu ni ya Pekee" | How to Know God


Mungu huonyesha tabia Yake ya haki kupitia mbinu na kanuni za kipekee,
haidhibitiwi na watu, matukio au vitu.
Na hakuna awezaye kubadili dhana au mawazo Yake,
au kumshawishi Ajaribu njia tofauti.
Hii ndiyo asili ya kipekee ya tabia ya haki ya Muumba!
Tabia Yake ya haki!

3.27.2019

Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?

 Jinsi ya kuelewa kwamba Kristo ndiye ukweli, njia, na uzima?


Aya za Biblia za Kurejelea:

"Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu. Hivyo ndivyo alivyokuwa mwanzoni na Mungu" (YN. 1:1-2).

"Na Neno alifanywa kuwa mwili, na akakaa kati yetu, (nasi tukautazama utukufu wake, utukufu kama ule wa Mwana wa pekee aliyezaliwa na Baba,) aliyejawa neema na ukweli" (YN. 1:14).

"Mimi ndiye njia, ukweli na uhai: hakuna mwanadamu ayaje kwa Baba, bali kwa njia yangu" (YN. 14:6).

"Maneno ninayoongea kwenu ni roho, na ni uhai" (YN. 6:63).

Maneno Husika ya Mungu:

Ukweli unatoka katika ulimwengu wa mwanadamu, na bado ukweli katika mwanadamu unapitishwa na Kristo. Unaanzia kwa Kristo, yaani, kutoka kwa Mungu mwenyewe, na hauwezi kufikiwa na mwanadamu.

3.26.2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”


Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Kazi ya Kueneza Injili Ni Kazi ya Kuokoa Binadamu Pia”


Watu wote wanahitaji kuelewa kusudio la kazi Yangu ulimwenguni, yaani, lengo la mwisho la kazi Yangu na ni kiwango kipi ambacho lazima Nitimize katika kazi hii kabla inaweza kukamilika. Kama, baada ya kutembea na Mimi hadi leo, watu hawaelewi kazi Yangu inahusu nini, basi hawajakuwa wakitembea na Mimi bure? Watu wanaonifuata Mimi wanafaa kujua mapenzi Yangu. Nimekuwa nikifanya kazi ulimwenguni kwa maelfu ya miaka, na hadi leo ningali nafanya kazi Yangu vivyo hivyo sasa. Ingawa kunavyo vipengele vingi hasa vilivyojumuishwa katika kazi Yangu, kusudio la kazi hii linabakia lilelile.

3.25.2019

Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kwili kwa Mungu hukamilish umuhimu wa kupata mwili?

Kwa nini husemwa kuwa kupata mwili kwili kwa Mungu hukamilish umuhimu wa kupata mwili?


Aya za Biblia za Kurejelea:

"Kwa hiyo Kristo alitolewa mara moja kuzichukua dhambi za wengi; na kwa wale wamtazamiao ataonekana mara ya pili bila dhambi kwa wokovu" (EBR 9:28).

"Mwanzoni kulikuwa na Neno, na Neno alikuwa na Mungu, na Neno alikuwa Mungu" (YN. 1:1).

Maneno Husika ya Mungu:

Kupata mwili mara ya kwanza kulikuwa kumkomboa mwanadamu kutoka katika dhambi kupitia mwili wa Yesu, hivyo, Aliokoa mwanadamu kutoka kwa msalaba, lakini tabia potovu ya kishetani ilibaki ndani ya mwanadamu. Kupata mwili mara ya pili si kwa ajili ya kuhudumu tena kama sadaka ya dhambi ila ni kuwaokoa kamilifu wale waliokombolewa kutoka kwa dhambi. Hii inafanyika ili wale waliosamehewa wakombolewe kutoka kwa dhambi zao, na kufanywa safi kabisa, na kupata mabadiliko ya tabia, hivyo kujikwamua kutoka kwa ushawishi wa Shetani wa giza na kurudi mbele za kiti cha enzi cha Mungu. Hivyo tu ndivyo mwanadamu ataweza kutakaswa kikamilifu. Mungu Alianza kazi ya wokovu katika Enzi ya Neema baada ya Enzi ya Sheria kufika mwisho. 

3.24.2019

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”

Maneno ya Roho Mtakatifu kwa makanisa | “Mwokozi Amerudi Tayari Juu ya ‘Wingu Jeupe’”


Mwenyezi Mungu anasema, “Tangu Yesu aondoke, wafuasi waliomfuata, na watakatifu wote waliookolewa kwa sababu ya jina Lake, wamekuwa wakimtamani mno na kumngoja. Wale wote waliookolewa kwa neema ya Yesu Kristo katika Enzi ya Neema wamekuwa wakiitamani siku hiyo ya furaha katika siku za mwisho, wakati ambapo Yesu Mwokozi atawasili juu ya wingu jeupe na kuonekana kati ya mwanadamu. Bila shaka, haya pia ni mapenzi ya pamoja ya wale wote wanaolikubali jina la Yesu Mwokozi leo. Ulimwenguni kote, wale wote wanaojua kuhusu wokovu wa Yesu Mwokozi wamekuwa wakingoja kwa hamu kurejea kwa ghafla kwa Yesu Kristo, ili kutimiza maneno ya Yesu akiwa duniani: “Nitarejea jinsi Nilivyoondoka”.

Kwa nini husemwa kuwa wanadamu wapotovu wanahitaji zaidi wokovu wa Mungu aliyepata mwili?

Kwa nini husemwa kuwa wanadamu wapotovu wanahitaji zaidi wokovu wa Mungu aliyepata mwili?


(Fungu Lililochaguliwa la Neno la Mungu)

Mwanadamu Aliyeanguka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii kabisa kwamba mwili wa mwanadamu umeharibiwa ndio maana Mungu akamfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mhusika wa uharibifu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, Mungu ni lazima Awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi.

3.23.2019

Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Tatu


Matamshi ya Mungu | “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee VIII Mungu ni Chanzo cha Uhai kwa Vitu Vyote (II)” Sehemu ya Tatu


Mwenyezi Mungu alisema, “Kuongezea, miongoni mwa vitu vyote, iwe ni wanyama, mimea, au kila aina ya nyasi, Mungu aliumba pia baadhi ya mimea ambayo ni muhimu kwa kutatua madhara au magonjwa kwa mwili wa mwanadamu. Utafanya nini, kwa mfano, ukichomeka? Je, unaweza kuosha kwa maji? Je, unaweza kutafuta kitambaa na kufunika mahali hapo? Huenda pakajaa usaha au kuambukizwa kwa njia hiyo. Utafanya nini, kwa mfano, ukiungua kwa bahati na moto au na maji moto? Unaweza kumimina maji juu yake? Kwa mfano, ukipata homa, upate mafua, upate majeraha kutokana na kazi ya viungo, maradhi ya tumbo kutokana na kula kitu kibaya, au kupata magonjwa fulani kwa sababu ya mienendo ya maisha au masuala ya hisia, kama vile magonjwa ya mishipa ya damu, hali za kisaikolojia au magonjwa ya ogani zilizo ndani ya mwili—kuna mimea inayolingana ya kutibu haya yote.

3.22.2019

Mungu Anashuka na Hukumu

Mungu Anashuka na Hukumu

I

Anapokuja chini katika taifa la joka kuu jekundu,

Mungu anageuka kuutazama ulimwengu na unaanza kutingika.

Je, kuna mahali popote ambapo hapatapata hukumu Yake?

Ama kuishi katika janga Analotoa?

Kila mahali Aendapo anamwaga mbegu ya janga,

lakini kupitia kwayo Anatoa wokovu na kuonyesha upendo Wake.

Mungu anatamani kuwafanya watu zaidi kumjua, kumwona na kumheshimu.

3.21.2019

Maneno ya Roho Mtakatifu | “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia”


Maneno ya Roho Mtakatifu | “Utakapouona Mwili wa Kiroho wa Yesu Ndio Utakuwa Wakati Mungu Ametengeneza Upya Mbingu na Dunia”


Mwenyezi Mungu anasema, “Watu wengi wanaweza kukosa kujali kuhusu kile Ninachosema, lakini bado Nataka kumwambia kila anayeitwa mtakatifu wa Mungu anayemfuata Yesu kwamba, mtakapoona Yesu Akishuka kutoka juu mbinguni juu ya wingu jeupe kwa macho yenu wenyewe, huu ndio utakuwa mwonekano wa umma wa Jua la haki.

3.20.2019

Matamshi ya Mungu | Sura ya 22 na 23

Leo, wote wako tayari kuelewa mapenzi ya Mungu na kujua tabia ya Mungu, lakini hakuna anayejua kwa nini hawezi kufuata matamanio yake, hajui kwa nini moyo wake daima humsaliti, na kwa nini hawezi kutimiza kile anachotaka. Kwa hiyo, yeye anakabiliwa tena na hali mbaya ya kukata tamaa, lakini pia anaogopa. Asiweze kuonyesha hisia hizi zinazopingana, anaweza tu kuonyesha huzuni na kuendelea kujiuliza: Je, inaweza kuwa Mungu hajanipa nuru? Inaweza kuwa Mungu ameniacha kwa siri? Pengine wengine wote wako sawa, na Mungu amewapa wote nuru isipokuwa mimi. 

3.19.2019

Matamshi ya Mungu | “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” Sehemu ya Kwanza



Hivyo, muda mfupi uliopita nyote mmesikia hadithi ya Ibrahimu. Alichaguliwa na Mungu baada ya gharika kuuangamiza ulimwengu, jina lake lilikuwa Ibrahimu, na alipokuwa na miaka mia moja, na mke wake Sara akiwa na umri wa miaka tisini, ahadi ya Mungu ilimjia. Mungu alimwahidi nini? Mungu alimwahidi kile ambacho kinarejelewa katika Maandiko: “Na mimi nitambariki yeye, na pia nitakupa mwana kutoka kwake.” Ni maelezo yapi yalitangulia ahadi ya Mungu ya kumpa mtoto? Maandiko yanaelezea yafuatayo: “Kisha Ibrahimu akaanguka chini kifudifudi, na kucheka, na akasema moyoni, Je, mtoto atazaliwa kwa mtu mwenye umri wa miaka mia moja? naye Sara, aliye na umri wa miaka tisini, atazaa?” Kwa maneno mengine wanandoa hawa wazee walikuwa na umri mwingi sana wa kupata watoto.