Mwenyezi Mungu alisema: Wanadamu kwa kupotoshwa sana na Shetani, hawajui kuwa kuna Mungu na wameacha kumwabudu Mungu. Adamu na Hawa walipoumbwa mwanzoni, utukufu wa Yehova na Ushuhuda wa Yehova daima vilikuwepo. Lakini baada ya kupotoshwa, mwanadamu alipoteza utukufu na ushuhuda kwa sababu kila mtu alimwasi Mungu na kuacha kumtukuza kabisa. Kazi ya sasa ya kushinda ni kuupata ushuhuda na utukufu wote, na kuwafanya wanadamu wote wamwabudu Mungu, ili kuwepo na ushuhuda miongoni mwa viumbe wote. Hili ndilo linapaswa kufanywa katika hatua hii ya kazi.
Kristo ni ukweli, njia, na uzima. Kondoo wa Mungu husikia sauti ya Mungu. Mradi unasoma maneno ya Mwenyezi Mungu, utaona kuwa Mungu ameonekana.
12.03.2017
12.01.2017
Jinsi ya Kumjua Mungu Duniani
Mwenyezi Mungu alisema: Nyinyi nyote mna furaha kupokea tuzo mbele ya Mungu na kutambuliwa na Mungu. Haya ni matakwa ya kila mtu baada ya yeye kuanza kuwa na imani kwa Mungu, kwani mwanadamu kwa moyo wake wote hutafuta mambo yaliyo juu na hakuna aliye tayari kubaki nyuma ya wengine. Hii ndiyo njia ya mwanadamu. Kwa sababu hii, wengi kati yenu wanajaribu daima kupata neema ya Mungu mbinguni, lakini kwa kweli, uaminifu wenu na uwazi kwa Mungu ni wa kiasi kidogo sana ukilinganishwa na uaminifu na uwazi wenu kwenu wenyewe. Mbona Nasema hivi? Kwa sababu Sikiri uaminifu wenu kwa Mungu kabisa, na zaidi Nakana kuwepo kwa Mungu ndani ya mioyo yenu. Hiyo ni kusema, Mungu mnayemwabudu, Mungu asiye dhahiri mnayempenda, hayupo kabisa. Kinachonifanya niseme haya kwa uhakika ni kwamba mko mbali sana na Mungu wa kweli.
11.30.2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Wafaa Kujua Namna Ambavyo Ubinadamu Wote Umeendelea Hadi Siku ya Leo
ndugu na dada |
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Wafaa Kujua Namna Ambavyo Ubinadamu Wote Umeendelea Hadi Siku ya Leo
Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu
kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana
na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu
imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya
ubinadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji.
11.29.2017
Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja
Mwenyezi Mungu alisema: Mwanzoni, Mungu alikuwa anapumzika. Hakukuwa na binadamu ama kitu chochote kingine duniani wakati huo, na Mungu hakuwa amefanya kazi yoyote ile. Mungu alianza tu kazi Yake ya usimamizi baada ya binadamu kuwepo na baada ya binadamu kupotoshwa.
11.28.2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Asili na Utambulisho wa Mwanadamu
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Asili na Utambulisho wa Mwanadamu
Mwenyezi Mungu alisema, Kwa kweli, hawajasikitika, na wamekuwa wakitazama kile ambacho kimefanywa kwa miaka elfu sita iliyopita mpaka leo, kwa kuwa Sikuwaacha. Badala yake, kwa sababu mababu zao walikula tunda kutoka kwa mti wa ujuzi wa mema na maovu lililotolewa na yule mwovu, waliniacha kwa ajili ya dhambi. Mema ni Yangu, wakati maovu ni ya yule mwovu ambaye hunihadaa kwa ajili ya dhambi.
Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote
Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote |
Mungu Ndiye Bwana wa Viumbe Vyote
Mwenyezi Mungu alisema: Hatua moja ya kazi ya enzi mbili za awali ilifanyika Israeli; nyingine ilifanyika Uyahudi. Kuzungumza kwa jumla, hakuna hatua ya kazi hii iliyotoka Israeli; zilikuwa ni hatua za kazi zilizofanywa miongoni mwa wateule wa mwanzo. Hivyo, kwa mtazamo wa Wanaisraeli, Yehova Mungu ni Mungu wa Wanaisraeli pekee.
11.26.2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maono ya Kazi ya Mungu (3)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maono ya Kazi ya Mungu (3)
Mwenyezi Mungu alisema, Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu.
Mwenyezi Mungu alisema, Mara ya kwanza Mungu alipopata mwili ilikuwa kupitia kutungwa mimba kwa Roho Mtakatifu, na ilihusiana na kazi Aliyokusudia kufanya. Jina la Yesu liliashiria mwanzo wa Enzi ya Neema. Wakati Yesu Alianza kufanya huduma Yake, Roho Mtakatifu Alianza kutoa ushuhuda kwa jina la Yesu, na jina la Yehova halikuzungumziwa tena, na badala yake Roho Mtakatifu Alianza kazi mpya hasa kwa jina la Yesu.
11.25.2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Kuhusu Maisha ya Kawaida ya Kiroho
Mwenyezi Mungu alisema, Muumini lazima awe na maisha ya kawaida ya kiroho huu ni msingi wa kupitia maneno ya Mungu na kuingia katika hali halisi. Sasa hivi, je, maombi yote, kule kuja karibu na Mungu, kuimba, kusifu, kutafakari, na kule kujaribu kuelewa maneno ya Mungu ambayo mnatenda yanafikia viwango vya maisha ya kawaida ya kiroho? Hakuna kati yenu aliye wazi sana juu ya hili.
11.24.2017
Fumbo la Kupata Mwili (4)
Mwenyezi Mungu alisema, “Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? Kauli ile imeshatimia? Kukubali kwao injili ni kwa mujibu wa Biblia; wao huhubiri injili kulingana na Biblia. Wao huyategemea maneno ya Biblia kumwamini Mungu; bila Biblia, wao hawatamwamini Mungu.
11.23.2017
Fumbo la Kupata Mwili (3)
Mwenyezi Mungu alisema: Wakati ambapo Mungu huitekeleza kazi Yake, Yeye haji
kujishughulisha katika ujenzi wowote au mabadiliko; Yeye huja kutimiza
huduma Yake. Kila wakati Anapopata mwili, ni kwa ajili tu ya kufanikisha
hatua ya kazi na kuifungua enzi mpya. Sasa ni Enzi ya Ufalme, na
mwanadamu ameingia katika zoezi la ufalme.
11.22.2017
Fumbo la Kupata Mwili (2)
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (2)
Mwenyezi Mungu alisema: Katika wakati ambapo Yesu Alifanya kazi Uyahudi, Aliifanya wazi, lakini sasa, Nazungumza na Kufanya kazi kati yenu kwa siri. Wasioamini hawana ufahamu wowote. Kazi Yangu kati yenu imetengwa kutoka kwa nyingine. Maneno haya, kuadibu huku na hukumu hii, vinajulikana tu kwako na sio mwingine.
11.21.2017
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Fumbo la Kupata Mwili (1)
Matamshi ya Mwenyezi Mungu: Katika Enzi ya Neema, Yohana alimwandalia Yesu njia. Hangeweza kufanya kazi ya Mungu Mwenyewe ila alitimiza tu kazi ya mwanadamu. Ingawa Yohana alikuwa mtangulizi wa Bwana; hangeweza kumwakilisha Mungu; alikuwa tu binadamu aliyetumiwa na Roho Mtakatifu. Kufuatia ubatizo wa Yesu, “Roho Mtakatifu alimshukia Yeye kwa mfano wa njiwa.” Kisha Akaanza kazi Yake, hivyo, Alianza kufanya huduma ya Kristo. Hiyo ndiyo maana Alichukua utambulisho wa Mungu, kwa sababu Alitoka Kwa Mungu.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)