Mwenyezi Mungu alisema: Wakati ambapo Mungu huitekeleza kazi Yake, Yeye haji
kujishughulisha katika ujenzi wowote au mabadiliko; Yeye huja kutimiza
huduma Yake. Kila wakati Anapopata mwili, ni kwa ajili tu ya kufanikisha
hatua ya kazi na kuifungua enzi mpya. Sasa ni Enzi ya Ufalme, na
mwanadamu ameingia katika zoezi la ufalme.
Hatua hii ya kazi si kazi ya
mwanadamu au ya kumfanya mwanadamu mkamilifu kwa kiasi fulani; ni
kuimaliza sehemu ya kazi ya Mungu. Kazi Yake si kazi ya mwanadamu na si
kumfanya mwanadamu mkamilifu kwa kiasi fulani kabla ya kuondoka duniani;
ni kutimiza huduma Yake kwa ukamilifu na kuimaliza kazi ambayo Anapaswa
kuifanya, ambayo ni kutengeneza mipango ya kufaa ya kazi Yake duniani,
na hivyo kupata kutukuka. Kazi ya Mungu mwenye mwili ni tofauti na ile
ya wale wanaotumiwa na Roho Mtakatifu.Mungu anapofanya kazi Yake
duniani, Yeye anajali kutimilika kwa huduma Yake pekee Yake.Na kwa
mambo mengine yasiyohusiana na huduma Yake, Yeye kimatendo
hajishughulishi hata kidogo, hata kwa kiwango cha kuzipa mgongo shughuli
hizo. Yeye hufanya tu kazi Anayopaswa kufanya, na hajishughulishi na
kazi ambayo mwanadamu anapaswa kufanya. Kazi Anayofanya ni ile tu
inahusiana na enzi Aliyomo na huduma Anayopaswa kukamilisha, kana kwamba
mambo mengine yote si jukumu Lake. Yeye hajijazi na maarifa ya kawaida
kuhusu jinsi ya kuishi kama mwanadamu, na Hajifunzi mahusiano ya jamii
au mambo yoyote ambayo mwanadamu anaelewa. Hajishughulishi kamwe na
mambo ambayo mwanadamu anapaswa kujua na Anafanya tu kitu ambacho ni
jukumu Lake. Kwa hivyo, mwanadamu anavyoona, Mungu mwenye mwili ni
“mwenye upungufu” katika mambo mengi mno, hata kwa kiasi kwamba Anavipa
mgongo vingi ambavyo mwanadamu anapaswa kuwa navyo, na kwamba hana
ufahamu wa mambo kama hayo. Mambo kama ufahamu wa maisha ya kawaida, na
vile vile kanuni za tabia na kuhusiana na wengine huonekana kuwa zisizo
na umuhimu wowote Kwake. Hata hivyo, huwezi kuona kutoka kwa Mungu
mwenye mwili tabia zozote zisizo za kawaida. Hiyo ni kusema, Uanadamu
Wake unadumisha maisha Yake kama mwanadamu wa kawaida na fikira za
kawaida za ubongo Wake, na kumpa uwezo wa kutofautisha kati ya mazuri na
mabaya. Hata hivyo, Hajajazwa na kingine chochote, yote ambayo ni ya
wanadamu (walioumbwa) pekee. Mungu anapata mwili ili kukamilisha huduma
Yake pekee. Kazi Yake inaelekezwa kwa enzi nzima na sio kwa my binafsi
au mahali fulani. Kazi Yake inaelekezwa kwa ulimwengu mzima. Huu ndio
mwelekeo wa kazi Yake na kanuni Anayofuata katika kazi Yake. Hii haiwezi
kubadilishwa na yeyote, na mwanadamu hawezi kuhusika kwa sehemu yoyote.
Kila wakati ambapo Mungu hupata mwili, Yeye huja pamoja na kazi ya enzi
hiyo, na sio dhamira ya kuishi ubavuni mwa mwanadamu kwa miaka
ishirini, thelathini, arobaini, au hata miaka sabini, themanini ili
waweze kuelewa bora zaidi na kupata utambuzi Kwake. Hakuna haja ya hilo!
Kufanya hivyo hakungeweza katu kuzidisha ufahamu ambao mwanadamu anao
wa tabia ya asili ya Mungu; badala yake, kungeongeza tu kwa fikira zao
na kufanya fikira na mawazo ya mwanadamu yawe kuukuu. Na kwa hiyo nyote
mnapaswa kuelewa hasa ni nini kazi ya Mungu aliyepata mwili. Yawezekana
kwamba hamyaelewi maneno Yangu: “Siji kuyapitia maisha ya mwanadamu wa
kawaida”? Je, mmesahau maneno: “Mungu haji duniani kuishi maisha ya
mwanadamu wa kawaida”? Hamlielewi kusudi la Mungu kupata mwili, wala
hamjui maana ya “Mungu angekujaje duniani na dhamira ya kuyapitia maisha
ya kiumbe aliyeumbwa”? Mungu anakuja tu duniani kukamilisha kazi Yake,
na kwa hivyo Kazi Yake duniani ni ya muda mfupi. Haji duniani na nia ya
Roho wa Mungu kukuza mwili Wake kuwa mkuu wa kipekee wa kanisa. Mungu
anapokuja duniani, ni Neno ambalo linageuka kuwa mwili; mwanadamu, hata
hivyo, hajui kuhusu kazi Yake na analazimisha makusudi kama hayo juu
Yake. Lakini nyote mnapaswa kufahamu kuwa Mungu ni Neno lililogeuka kuwa
mwili, na sio mwili uliokuzwa na Roho wa Mungu ili kusimamia nafasi ya
Mungu kwa ufupi. Mungu Mwenyewe hakuzwi, ila ni Neno kugeuka mwili, na
leo hii Anatekeleza kazi Yake kirasmi miongoni mwenu. Nyote mwajua na
kukubali kwamba kupata mwili kwa Mungu ni ukweli, lakini mnajidai kuwa
na ufahamu ambao kwa kweli hamna. Ninyi hamthamini kabisa kazi ya Mungu
aliyepata mwili au umuhimu na kiini cha Yeye kupata mwili, na husimulia
kwa urahisi tu maneno ambayo hunenwa na wengine. Je, unaamini kwamba
Mungu aliyepata mwili ni kama unavyodhani.
Mungu hugeuka mwili ili
tu Aiongoze enzi na Aanzishe kazi mpya. Lazima muelewe hoja hii. Hii ni
tofauti kabisa na kazi ya mwanadamu, na mawili haya hayawezi
kuzungumzwa kwa pamoja. Mwanadamu anahitaji muda mrefu wa kukuzwa na
kufanywa mkamilifu kabla mwanadamu aweze kutumiwa kutekeleza kazi, na
uanadamu wa hali ya juu unahitajika. Mwanadamu hapaswi kudumisha hali
yake ya uanadamu wa kawaida tu, bali pia mwanadamu zaidi ya hapo lazima
aelewe kanuni nyingi na sheria za tabia kabla ya mengine, na zaidi ya
hayo lazima ajifunze zaidi kuhusu hekima na maadili ya mwanadamu. Haya
ndiyo mwanadamu lazima kujengwa nayo. Hata hivyo, hivi sivyo ilivo na
Mungu mwenye mwili, kwa maana kazi Yake haimwakilishi mwanadamu na wala
si ya binadamu; bali ni dhihirisho la moja kwa moja la hali Yake na
utekelezi wa moja kwa moja wa kazi Anayopaswa kufanya. (Kwa kawaida,
kazi Yake hufanyika wakati inapaswa kufanyika, na sio tu wakati wowote
kiholela. Badala Yake, kazi Yake hufanyika wakati ambapo ni wakati wa
kukamilisha huduma Yake). Yeye hajihusishi katika maisha ya mwanadamu
wala katika kazi ya mwanadamu, hiyo inamaanisha, uanadamu Wake haujengwi
na yoyote kati ya haya (lakini hili haliathiri kazi Yake). Anatimiza
huduma Yake tu ikiwa wakati umewadia wa kufanya hivyo; haijalishi hali
Aliyomo, Yeye huendelea mbele na kazi Anayopaswa kufanya. Haijalishi
mwanadamu anajua nini kumhusu, au maoni ya mwanadamu kumhusu, kazi Yake
haiathiriki. Hii ni kama tu vile Yesu Alivyofanya kazi Yake; hakuna
Aliyejua Yeye ni nani, lakini Aliendelea tu mbele na kazi Yake. Mambo
haya hayakumuathiri katika utendaji wa kazi Yake Aliyopaswa kufanya. Kwa
hivyo, Hakukiri au kutangaza kuwa Yeye ni nani, na Yeye Alimfanya
mwanadamu Amfuate tu. Kwa kawaida, huu haukuwa tu uvumilivu wa Mungu;
ilikuwa ni njia ambayo Yesu Anafanya kazi katika mwili. Angeweza tu
kufanya kazi kwa namna hii, kwani mwanadamu hangeweza kumtambua Yesu kwa
jicho la kawaida. Na hata kama mwanadamu angeweza, mwanadamu hangeweza
kusaidia katika kazi Yake. Zaidi ya hayo, hakugeuka mwili ili mwanadamu
apate kujua mwili huu Wake; ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya kazi Yake na
kukamilisha huduma Yake. Kwa sababu hii, hakutilia maanani hali ya
kufanya Ajulikane. Alipokamilisha kazi Aliyopaswa kufanya, utambulisho
Wake na hadhi Yake vilijulikana wazi kwa mwanadamu. Mungu mwenye mwili
hukaa kimya na hafanyi matangazo yoyote. Yeye hajishughulishi na
mwanadamu au vile mwanadamu anaendelea katika kumfuata, na yeye husonga
tu mbele katika kutimiza huduma Yake na kufanya kazi Anayopaswa kufanya.
Hakuna Anayeweza kusimama mbele ya njia ya kazi Yake. Wakati muda
unawadia wa kazi Yake kukamilika, ni muhimu kazi hiyo ikamilike na
kufikishwa kikomo. Hakuna anayeweza kusema vinginevyo. Baada tu ya Yeye
kuondoka kutoka kwa mwanadamu baada ya kukamilisha kazi Yake ndipo
mwanadamu ataelewa kazi Anayofanya, ingawa hataifahamu kikamilifu. Na
itachukua muda mrefu ndipo mwanadamu aelewe nia Yake Alipofanya kazi
hiyo mara ya kwanza. Kwa maneno mengine, kazi ya enzi ambapo Mungu
anageuka mwili imegawanywa katika sehemu mbili. Sehemu moja ni kupitia
katika kazi na maneno ya Mungu mwenye mwili Mwenyewe. Pindi tu huduma ya
mwili Wake imetimika kikamilifu, sehemu nyingine ya kazi inatakiwa
kutekelezwa na Roho Mtakatifu; basi utakuwa wakati wa mwanadamu kutimiza
wajibu wake, kwa maana Mungu ameshafungua njia tayari, na lazima
itembelewe na mwanadamu mwenyewe. Hiyo ni kusema, Mungu anageuka kuwa
mwili ili kutekeleza sehemu moja ya kazi Yake, na inaendelezwa kwa
urithi na Roho Mtakatifu na vile vile wale watu wanaotumiwa na Roho
Mtakatifu. Kwa hivyo mwanadamu anapaswa kujua kazi ya msingi inayopaswa
kutekelezwa na Mungu mwenye mwili katika hatua hii ya kazi. Mwanadamu
lazima aelewe hasa umuhimu wa Mungu kugeuka kuwa mwili na kazi
Anayopaswa kufanya, badala ya kumuuliza Mungu ni nini kinachotakiwa kwa
mwanadamu. Haya ni makosa ya mwanadamu, na vile vile fikira, na zaidi ya
hayo, ni kutotii kwake.
Mungu anakuwa mwili bila nia ya kumfanya
mwanadamu apate kuujua mwili Wake, ama kukubali mwanadamu kutofautisha
tofauti kati ya mwili wa Mungu mwenye mwili na ule wa mwanadamu; Mungu
hapati mwili ili kufunza mwanadamu uwezo wa utambuzi, na zaidi nia ya
mwanadamu kumwabudu Mungu mwenye mwili, ambayo kupitia kwayo atapata
utukufu mkuu. Hakuna kati ya haya yaliyo mapenzi ya Mungu ya awali ya
Mungu kuwa mwili. Mungu hawi mwili ili kulaani mwanadamu, kufichua
mwanadamu akipenda, ama kufanya vitu kuwa vigumu kwa mwanadamu. Hakuna
kati ya hayo lililo penzi la awali la Mungu. Kila wakati ambapo Mungu
anakuwa mwili, ni kazi isiyo na budi. Ni kwa ajili ya kazi Yake kuu na
usimamizi Wake mkuu ndio maana Anafanya hivyo, na si kwa sababu ambazo
mwanadamu anafikiria. Mungu anakuja tu duniani Anavyohitajika na kazi
Yake, na kila wakati ikiwa lazima. Haji duniani Akiwa na nia ya
kuzurura, ila kutekeleza kazi ambayo Anapaswaa kufanya. Mbona basi
Ajipatie kazi hii ya umbinguni na kujiweka katika hatari kubwa kufanya
kazi hii? Mungu anakuwa mwili tu inapobidi, na kila wakati ikiwa na
umuhimu wa kipekee. Kama ingekuwa tu kwa sababu ya kumfanya mwanadamu
amuangalie na kufungua macho yao, basi kwa uhakika kabisa, hangekuja
kati ya wanadamu kwa kubembeleza. Anakuja duniani kwa usimamizi Wake na
kazi Yake kuu, na kuwa na uwezo wa kutwaa wanadamu zaidi. Anakuja
kuwakilisha enzi na kumshinda Shetani, na ni katika mwili ndimo Anakuja
kumshinda Shetani. Zaidi, Anakuja kuwaongoza binadamu wote katika maisha
yao. Haya yote yanahusu uongozi Wake, na ni kazi inayohusu ulimwengu
wote. Mungu angekuwa mwili ili tu kumruhusu mwanadamu kuja kuujua mwili
Wake na kuyafungua macho ya mwanadamu, basi mbona Hangesafiri kwa kila
taifa? Je hili sio jambo la wepesi zaidi? Lakini hakufanya hivyo, badala
yake, Akachagua mahali palipofaa pa kuishi na kuanza kazi Aliyopaswa
kufanya. Mwili huu pekee ni wa umuhimu mkuu. Anawakilisha enzi nzima, na
Anatekeleza kazi ya enzi nzima; Analeta enzi ya zamani kufika tamati na
kuikaribisha mpya. Haya yote ni mambo muhimu yanayohusu usimamizi wa
Mungu, na ni umuhimu wa hatua ya kazi iliyotekelezwa na Mungu kuja
duniani. Wakati ambapo Yesu alikuja duniani, Alizungumza tu maneno kiasi
na kutekeleza kazi kiasi; Hakujishughulisha na maisha ya mwanadamu, na
Aliondoka baada ya kumaliza kazi Yake. Baada ya Mimi kumaliza kuzungumza
na kuyapokeza maneno Yangu kwenu siku hii, nanyi nyote mkishayaelewa,
basi hatua hii ya kazi itakuwa imemalizika, haijalishi maisha yenu
yatakuwa vipi. Katika siku za usoni, lazima kuwe na wale wa kuendeleza
hatua hii ya kazi na kufanya kazi kwa mujibu wa maneno haya duniani;
kisha kazi ya mwanadamu na ujenzi wa mwanadamu utaanza. Lakini sasa, ni
kazi ya Mungu tu kutimiza huduma Yake na kumaliza hatua ya kazi. Mungu
hufanya kazi kwa njia isiyo sawa na ya mwanadamu. Mwanadamu hupenda
mikusanyiko na mabaraza, na huthamini sana utaratibu. Mungu huchukia
sana mikusanyiko na mikutano ya mwanadamu. Mungu huzungumza na kunena na
mwanadamu visivyo rasmi; hii ni kazi ya Mungu, ambayo ni iliyokombolewa
isivyo kawaida na pia hukuweka wewe huru. Hata hivyo, Nachukia zaidi
kukusanyika nanyi, na Mimi siwezi kuzoea maisha yaliyoshurutishwa sana
kama yenu. Mimi huziona sheria kuwa za kuchukiza sana; hizo humzuia
mwanadamu kiasi cha kumfanya mwanadamu aogope kuanza kutenda, aogope
kuzungumza, na aogope kuimba, na macho yake hukodolewa kwako moja kwa
moja. Nachukia zaidi namna yenu ya mkusanyiko na mikusanyiko mikubwa.
Sitamani kabisa kukusanyika nanyi kwa njia hii, kwani niia hii ya kuishi
humfanya mtu ahisi amewekewa mipaka. Kwa sababu mnafuata utaratibu
mwingi sana na sheria nyingi sana, kuwaruhusu ninyi kuongoza
kungewaelekeza watu wote kwa sheria. Mwanadamu hangekuwa na njia ya
kuziacha sheria chini ya uongozi wenu, na badala yake maana ya udini
ingekuwa kali sana milele, na desturi za mwanadamu kuongezeka kwa idadi
kubwa zaidi. Wanadamu wengine huendelea kuzungumza na kunena wakati
ambapo wanakusanyika na hawahisi uchovu kamwe, ihali wengine wanaweza
kuendelea kunena kwa siku nyingi. Hii yote inafikiriwa kuwa mikusanyiko
mikubwa na mikutano ya mwanadamu; haina uhusiano wowote na kula na
kunywa, na kufurahia, au na maisha ambayo roho huwekwa huru. Hii yote ni
mikutano! Mikutano yenu ya mfanyakazi mshiriki, na vilevile mikusanyiko
mikubwa na midogo, yote inanichukiza Mimi, na Sijawahi kuwa na hamu
nayo. Hii ni kanuni ambayo Nafanyia kazi; Siko radhi kuhubiri wakati wa
mikusanyiko, wala Siko radhi kutangaza chochote kwa watu wote, sembuse
kuitisha mkutano wa ninyi nyote kwa siku chache za mkutano maalumu.
Sioni likiwa la kupendeza kwenu nyote kukusanyika pamoja kwa kufaa;
Nachukia kabisa kuwaona ninyi mkiishi ndani ya mipaka ya utaratibu
wowote, aidha, Siko radhi kushiriki katika utaratibu wenu wowote kama
huo. Kadri mnavyofanya hivyo, ndivyo Ninavyoiona kuwa ya kuchukiza
zaidi. Sina hamu hata kidogo na utaratibu na sheria zenu; haijalishi
mnavifanya kwa jinsi nzuri iliyoje, Nayaona yote kuwa ya kuchukiza. Sio
kwamba mipango yenu ni isiyofaa au kwamba ninyi ni duni sana; ni kwamba
Nachukia sana mwenendo wenu wa kuishi, na zaidi ya hayo, Mimi siwezi
kuuzoea. Ninyi hamwelewi kabisa kazi Ninayotaka kufanya. Kipindi hicho,
wakati ambapo Yesu alitekeleza kazi Yake mahali fulani na kisha
Akamaliza kuhubiri mahubiri, Angewaongoza wanafunzi Wake na kuondoka
katika mji huo. Aliwaongoza wanafunzi Wake kujadiliana wenyewe kwa
wenyewe, na kuondoka kati ya umma; Alifanya kazi kila mara kwa njia
hiyo. Aliondoka kati ya wanadamu, na kuwaongoza wanafunzi wake wachache
wapendwa kwenda juu ya milima, kuzungumza nao kuhusu njia walizopaswa
kuelewa. Kazi Yake kati ya umma ya jumla ilikuwa nadra. Kulingana na
kile mnachotaka kutoka Kwake, Mungu aliyepata mwili hapaswi kuwa na
maisha ya mwanadamu wa kawaida; lazima Aitekeleze kazi Yake, na lazima
Azungumze, kama Anaketi, Anasimama, au kutembea. Lazima Afanya kazi
nyakati zote na Hawezi kukoma “kukimiba”, la sivyo Anazembea katika
majukumu Yake. Je, mahitaji haya ya mwanadamu ni kwa mujibu wa akili ya
mwanadamu? Uadilifu wenu uko wapi? Je, hamtaki mengi kupita kiasi? Kazi
Yangu inahitaji kuchunguzwa na wewe? Je, Nakuhitaji wewe kuangalia
Ninapotimiza huduma Yangu? Najua vizuri kazi Ninayopaswa kufanya na
wakati ambapo Napaswa kuifanya; Sihitaji kuingilia kutoka kwa wengine.
Labda inaweza kuonekana kwako kana kwamba Sijafanya mengi, lakini
kufikia wakati huo kazi Yangu tayari imefika mwisho. Chukueni mfano wa
maneno ya Yesu katika Injili Nne. Hayo vilevile hayakuwa na mipaka?
Wakati huo, Yesu aliingia katika sinagogi na kuhubiri mahubiri; Alikuwa
ameimaliza katika muda usio zaidi ya dakika kadhaa. Baada ya Yeye
kumaliza kunena, Aliwaongoza wanafunzi Wake ndani ya mashua na Akaondoka
bila maelezo yoyote. Sanasana, wale waliokuwa ndani ya sinagogi
walijadiliana miongoni mwao wenyewe, na jambo hilo halikumhusu Yesu
tena. Mungu alitekeleza tu kazi ambayo Alipaswa kuifanya, na sio zaidi.
Siku hizi, wengi huniomba Ninene na kuzungumza mengi zaidi, kwa masaa
kadhaa kwa siku. Kama mwonavyo, yule anenaye pekee ndiye Mungu, sio
vinginevyo. Ninyi nyote ni vipofu! Nyote ni katili! Nyote ni vitu
visivyojua visivyo na hisi! Mna fikira nyingi sana! Madai yenu hupita
mipaka! Ninyi ni wasio na utu! Hamwelewi kabisa Mungu ni nini! Ninyi
huamini kwamba wazungumzaji na wasemi wote ni Mungu, kwamba yeyote
ambaye yuko radhi kuwapa ninyi maneno ni baba yenu. Niambieni, je, ninyi
nyote mlio na maumbo yaliyoumbwa vizuri na sura “ya ajabu” bado mna
hata sehemu kidogo ya hisi? Je, mnajua sasa jua la mbinguni! Kila mmoja
wenu ni kama maofisa wapotovu na wenye uchoyo, kwa hiyo mwawezaje kuona
maana? Mwawezaje kutambua kati ya mema na mabaya? Nimewapa ninyi mengi
sana, lakini ni wangapi miongoni mwenu wamezingatia? Nani anaweza
kulipata kwa ukamilifu? Ninyi hamjui ni nani alifungua njia ambayo kwayo
mnatembea siku hii, kwa hiyo ninyi huendelea kunidai Mimi, mkifanya
madai yasiyo na maana kutoka Kwangu. Je, nyuso zenu hazijabadilika kwa
sababu ya aibu? Sijazungumza mengi? Je, Sijafanya mengi? Ni nani
miongoni mwenu anaweza kweli kuyatunza maneno Yangu kama hazina? Ninyi
hunisifu mno katika kuwepo Kwangu, lakini hudanganya na kulaghai bila
Mimi kujua! Matendo yenu ni yenye kustahili dharau sana na ya kuchukiza!
Najua kwamba ninyi huniambia Mimi nizungumze na kufanya kazi ili muweze
kushibisha macho yenu na kupanua uzoefu wenu tu, sio kuyageuza maisha
yenu. Ni mangapi ambayo Nimenena kwenu tayari? Maisha yenu yangekuwa
yamebadilika kitambo sana, kwa hiyo mbona mnaendelea kurudia hali mbaya
leo? Yaweza kuwa kwamba maneno Yangu yameibwa kutoka kwenu kwa hivyo
hamkuyapokea? Kusema kweli, Sitamani kusema zaidi kwa walioharibika
tabia namna hivyo kama ninyi. Haileti manufaa! Siko radhi kufanya kazi
isiyoleta manufaa hivyo! Ninya mnataka tu kupanua uzoefu wenu au
kuyashibisha macho yenu, sio kupata uzima! Nyote mnajidanganya wenyewe!
Nawauliza, ni mangapi kati ya yale Niliyowazungumzia ana kwa ana
yametiwa katika vitendo na ninyi? Yote mfanyayo ni ulaghai wa
kudanganya! Nachukia sana wale miongoni mwenu wanaofurahia kutazama, na
Nauona udadisi wenu kuwa wa kuchukiza kabisa. Kama hamko hapa kuitafuta
njia ya kweli au kuwa na kiu ya ukweli, basi ninyi ni wale Ninaowachukia
sana! Najua kwamba ninyi hunisikiliza tu ili kuridhisha udadisi wenu au
kutimiza mojawapo ya shauku yenu. Hamna wazo la kutafuta kuweko kwa
ukweli au kuchunguza kuingia katika njia sahihi ya uzima; matakwa haya
hayako miongoni mwenu kabisa. Ninyi humchukulia tu Mungu kuwa mtu
anayechezewa wa kuchunguza na kustahi. Moyo wenu unaotafuta uzima ni
mdogo sana, ilhali shauku yenu ya udadisi sio! Kuzungumza kwa watu kama
hao kuhusu njia ya uzima ni kimsingi kuzungumza na kitu kisichokuwepo;
ingekuwa heri kutozungumza! Hebu Niwaambie! Kama mnatazamia tu kuijaza
tupu iliyo ndani ya moyo wenu, basi heri msije Kwangu! Mnapaswa
kuyalenga maisha yenu! Msijidanganye! Heri msichukulie udadisi wenu kama
msingi wa ufuatiliaji wenu wa maisha, au kuutumia kama kisingizio cha
kuniomba Mimi kuzungumza na ninyi. Huu wote ni ulaghai, ambao kwao ninyi
ni mabingwa! Nakuuliza tena: Ni kiasi gani cha yale ambayo Nimekwambia
uingie ndani umefanya kwa kweli? Je, wajua yote ambayo Nimenena kwako?
Umetia katika vitendo yote ambayo Nimenena kwako.
Kazi ya kila
enzi huanzishwa na Mungu Mwenyewe, lakini unapaswa kujua kwamba licha ya
kazi yoyote ya Mungu, Yeye haji kuanzisha muungano au kufanya mikutano
yoyote halisi au kuanzisha makundi ya aina yoyote kwa ajili yenu. Yeye
huja tu kufanya kazi Anayopaswa kufanya. Kazi Yake haizuiliwi na
mwanadamu yeyote. Yeye hufanya kazi Yake vile Anavyopenda; haijalishi
kile mwanadamu anajua au kufikiri, Yeye hutilia maanani katika
kukutekeleza kazi Yake. Tangu kuumbwa kwa dunia, kumekuwa na hatua tatu
za kazi; kutoka kwa Yehova mpaka kwa Yesu, na kutoka kwa Enzi ya Sheria
mpaka kwa Enzi ya Neema, Mungu hajawahi kuitisha mkutano halisi kwa
mwanadamu, wala hajawahi kuwakusanya wanadamu wote pamoja kufanya
mkutano halisi wa ulimwengu ili kupanua kazi Yake. Yeye hufanya tu kazi
ya mwanzo wa enzi nzima wakati muda na wakati na mahali uko sawa, na
kupitia kwa hili Anaikaribisha enzi ili kuwaongoza wanadamu katika
maisha yao. Mikutano halisi ni mikutano ya wanadamu; kuwakusanya watu
pamoja kusherehekea siku kuu katika kazi za mwanadamu. Mungu
hasherehekei siku kuu na, zaidi ya hayo, Anachukizwa nazo; Yeye haitishi
mikutano halisi na zaidi ya hayo Anachukizwa nayo. Sasa lazima uelewe
ni nini hasa kazi ya Mungu mwenye mwili!
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Kujua zaidi Kanisa la Mwenyezi Mungu, Umeme wa Mashariki
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni