ndugu na dada |
Kanisa la Mwenyezi Mungu|Wafaa Kujua Namna Ambavyo Ubinadamu Wote Umeendelea Hadi Siku ya Leo
Uzima wa kazi ya miaka 6,000 yote umebadilika kwa utaratibu
kuambatana na nyakati. Mabadiliko katika kazi hii kumefanyika kulingana
na hali zinazozunguka ulimwengu mzima. Kazi ya usimamizi ya Mungu
imebadilika tu kwa utaratibu kulingana na mitindo ya kimaendeleo ya
ubinadamu kwa ujumla; haikuwa imepangwa tayari mwanzoni mwa uumbaji.
Kabla ya ulimwengu kuumbwa, au punde tu baada ya kuumbwa kwake, Yehova
hakuwa amepanga bado awamu ya kwanza ya kazi, ile ya sheria; awamu ya
pili ya kazi, ile ya neema; au awamu ya tatu ya kazi, ile ya kushinda,
ambapo Angefanya kazi kwanza miongoni mwa kundi la watu—baadhi ya vizazi
vya Moabu, na kuanzia hapa Angeweza kushinda ulimwengu mzima.
Hakuyaongea maneno haya baada ya kuumba ulimwengu; Hakuyaongea maneno
haya baada ya Moabu, wala hata kabla ya Lutu. Kazi yake yote ilifanywa
bila kupangwa.Hivi ndivyo hasa kazi Yake nzima ya usimamizi ya miaka
elfu sita imeendelea; kwa vyovyote vile, Hakuwa ameandika mpango kama
huo kama Chati ya Muhtasari wa Maendeleo ya Ubinadamu kabla ya kuumba
ulimwengu. Katika kazi ya Mungu, Anaeleza moja kwa moja Yeye ni nani;
Hachemshi bongo kuunda mpango. Bila shaka, manabii wengi wameongelea
unabii mwingi, lakini bado haiwezi kusemekana kwamba kazi ya Mungu siku
zote imekuwa ya upangaji mpango wa dhati; unabii ulitolewa kulingana na
kazi halisi ya Mungu. Kazi zake zote ni kazi halisi zaidi. Hutekeleza
kazi Yake kulingana na maendeleo ya nyakati, na Anatekeleza kazi Yake
nyingi zaidi halisi kulingana na mabadiliko ya mambo Kwake Yeye,
kutekeleza kazi ni sawa na kutoa dawa kwa ugonjwa; Anafanya uangalizi
wakati akifanya kazi Yake; Anafanya kazi kulingana na uangalizi Wake.
Katika kila awamu ya kazi Yake, Anaweza kuelezea hekima Yake tosha na
kuelezea uwezo Wake tosha; Anafichua hekima Yake tosha na mamlaka Yake
tosha kulingana na kazi ya enzi hiyo husika na kuruhusu watu wowote wale
waliorudishwa na Yeye wakati wa enzi hizo kuweza kuiona tabia Yake
nzima. Anawaruzuku watu na kutekeleza kazi Anayofaa kufanya kulingana na
kazi ambayo lazima ifanywe katika enzi husika; Anawaruzuku watu
kulingana na kiwango ambacho Shetani amewapotosha. Ilikuwa ni njia hii
wakati Yehova aliweza kuwaumba mwanzo Adamu na Hawa ili kuwaruhusu
kumdhihirisha Mungu katika nchi na kuwa na mashahidi wa Mungu miongoni
mwa uumbaji, lakini Hawa alitenda dhambi baada ya kujaribiwa na nyoka;
Adamu alifanya vivyo hivyo, na kwa pamoja wakiwa kwenye bustani wakalila
tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Na hivyo basi, Yehova alikuwa
na kazi ya ziada ya kutenda miongoni mwao. Aliuona uchi wao na kuifunika
mili yao kwa nguo ziliyotengenezwa kutoka kwenye ngozi za wanyama.
Kufuatia haya, Alimwambia Adamu Kwa sababu umesikiliza sauti ya mkeo, na
umekula kutoka kwenye mti, ambao Nilikuamuru, Nikisema, usile kutoka
kwenye mti huu: mchanga umelaaniwa kwa sababu yako…mpaka urudi
mchangani; kwa kuwa ulitolewa ardhini: kwa kuwa wewe ni vumbi, na
mavumbini utarudi.” Kwa mwanamke Akasema, “Nitazidisha mara dufu uchungu
wako na kupata kwako watoto; kwa uchungu utazaa wana; na tamaa yako
itakuwa kwa mumeo, na yeye atatawala juu yako.” Kuanzia hapo aliwafukuza
kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuwafanya kuishi nje ya bustani, kama
vile binadamu wa kisasa afanyavyo sasa nchini. Wakati Mungu alipomwumba
mwanadamu mwanzoni kabisa, Hakupanga kumfanya binadamu kujaribiwa na
nyoka baada ya kuumbwa na kisha kuwalaani binadamu na nyoka. Kwa hakika
hakuwa na mpango wa aina hii; ilikuwa tu maendeleo ya mambo yaliyompa
kazi hii mpya miongoni mwa uumbaji Wake. Baada ya Yehova kutekeleza kazi
Yake miongoni mwa Adamu na Hawa kwenye ardhi, ubinadamu uliendelea
kuimarika kwa miaka elfu kadhaa mpaka “Mungu akaona ya kwamba maovu ya
mwanadamu ni makubwa duniani, na kuwa kila wazo la fikira za moyo wake
ni ubaya tu siku zote. Na ikamghairi BWANA kuwa alikuwa amemuumba
mwanadamu duniani, na ikamhuzunisha moyoni. … Lakini Nuhu akapata neema
katika macho ya BWANA.” Wakati huu Yehova alikuwa na kazi mpya zaidi,
kwa ajili ubinadamu Aliouumba ulikuwa umezidisha dhambi baada ya
kujaribiwa na nyoka. Kwa mujibu wa hali hizi, Yehova aliichagua familia
ya Nuhu miongoni mwa watu hawa na kuwanusuru, na kutekeleza kazi Yake ya
kuuangamiza ulimwengu kwa gharika. Ubinadamu umeendelea kukua kwa njia
hii mpaka siku ya leo, ukiendelea kupotoka pakubwa, na wakati maendeleo
ya ubinadamu yafikapo kilele, utakuwa ndio mwisho wa ubinadamu. Kuanzia
mwanzo kabisa hadi mwisho wa ulimwengu, ukweli wa ndani wa kazi Yake
siku zote umekuwa hivi. Itakuwa sawa na namna ambavyo binadamu
atakavyoainisha kulingana na aina yake; mbali na kila mtu anayeamuliwa
kabla kwa kategoria inayowafaa mwanzoni kabisa, watu wanawekwa kwenye
kategoria kwa utaratibu baada ya kupitia mchakato wa maendeleo.
Mwishowe, yeyote ambaye hawezi kuokolewa kwa uzima atarudishwa kwa
“mababu zake.” Hamna kati ya kazi za Mungu miongoni mwa ubinadamu
iliyokuwa tayari imetayarishwa wakati wa uumbaji wa ulimwengu; badala
yake, ilikuwa ni maendeleo ya mambo yaliyomruhusu Mungu kutekeleza kazi
Yake hatua kwa hatua kwa uhalisia zaidi na kwa kimatendo zaidi miongoni
mwa ubinadamu. Hivi ni kama ambavyo Yehova Mungu hakumwumba nyoka ili
kumjaribu mwanamke. Haukuwa mpango Wake mahususi, wala halikuwa jambo
ambalo alikuwa ameliamulia kimakusudi awali; mtu anaweza kusema kwamba
hali hii haikutarajiwa. Hivyo basi ilikuwa ni kwa sababu ya haya ndiyo
Yehova aliwatimua Adamu na Hawa kutoka kwenye Bustani ya Edeni na kuapa
kutowahi kumwumba binadamu tena. Lakini hekima ya Mungu inagunduliwa tu
na watu kwenye msingi huu, kama tu ile hoja Niliyotaja awali. “Hekima
Yangu hutumika kutokana na njama za Shetani.” Haikujalisha ni vipi
ambavyo ubinadamu ulizidi kupotoka au vipi nyoka alivyowajaribu, Yehova
bado alikuwa na hekima Yake; kwa hivyo, Amekuwa Akijihusisha katika kazi
mpya tangu Alipouumba ulimwengu, na hamna hatua zozote za kazi hii
zimewahi kurudiwa. Shetani ameendelea kutekeleza njama zake; ubinadamu
umekuwa ukipotoshwa siku zote na Shetani, na Yehova Mungu pia ameendelea
kutekeleza kazi Yake ya hekima siku zote. Hajawahi kushindwa, na
Hajawahi kusita kufanya kazi Yake kuanzia uumbaji wa ulimwengu mpaka
sasa. Baada ya ulimwengu kupotoshwa na Shetani, Aliendelea siku zote
kufanya kazi miongoni mwa watu ili kumshinda adui Wake anayepotosha
ubinadamu. Vita hivi vitaendelea kuanzia mwanzo hadi mwisho wa
ulimwengu. Kwa kufanya kazi hii yote, Hajauruhusu tu ubinadamu, ambao
umepotoshwa na Shetani, kupokea wokovu Wake mkubwa, lakini pia
ameuruhusu kuiona hekima Yake, uweza na mamlaka, na hatimaye Atauruhusu
ubinadamu kuiona tabia Yake ya haki—huku Akiwaadhibu wenye maovu na
kuwatuza wenye wema. Amepigana na Shetani hadi siku hii ya leo na
Hajawahi kushindwa, kwani Yeye ni Mungu mwenye hekima, na hekima Yake
hutumika kutokana na njama za Shetani. Na kwa hivyo basi mbali na
kufanya tu kila kitu mbinguni kunyenyekea kwa mamlaka Yake; pia Hufanya
kila kitu nchini kupumzika chini ya kigonda Chake, na pia Huwafanya wale
watenda maovu wanaoshambulia na kunyanyasa ubinadamu kujipata katika
kuadibu Kwake. Matokeo yote ya kazi yanaletwa kutokana na hekima Yake.
Alikuwa hajawahi kufichua hekima Yake kabla ya uwepo wa ubinadamu, kwani
Hakuwa na maadui kule mbinguni, juu ya nchi, au kwenye ulimwengu kwa
ujumla, na hakukuwa na nguvu za giza zilizoshambulia chochote katika
maumbile. Baada ya malaika mkuu kumsaliti Yeye, Aliuumba ubinadamu
kwenye nchi, na ilikuwa ni kwa sababu ya ubinadamu ndiyo Alianza rasmi
vita Vyake vya milenia nzima dhidi ya Shetani, malaika mkuu, vita
ambavyo vilizidi kushamiri kwa kila hatua iliyopigwa. Uweza Wake na
hekima vinapatikana katika kila mojawapo ya awamu hizi. Ni katika muda
huu tu ndipo kila kitu kule mbinguni na nchini huweza kushuhudia hekima
ya Mungu, uweza Wake, na hasa uhalisi wa Mungu. Angali anatekeleza kazi
Yake kwa njia ile ya kihalisi leo; aidha, Anapoendelea kutekeleza kazi
Yake anafichua pia uweza Wake na hekima Yake; Anawaruhusu kuona ule
ukweli wa ndani katika kila awamu ya kazi, kuweza kuona hasa ni vipi
unaweza kuelezea ule uweza wa Mungu na hasa ni vipi unavyoweza kuelezea
ule uhalisia wa Mungu.
Je, watu hawaamini kwamba ilipangwa awali
kabla ya uumbaji kwamba Yuda angeweza kumwuza Yesu? Kwa hakika, Roho
Mtakatifu alikuwa amepanga haya kulingana na uhalisia wakati huo.
Ilifanyika tu kwamba kulikuwepo mtu kwa jina la Yuda ambaye siku zote
angebadhiri fedha. Hivyo basi alichaguliwa kutekeleza wajibu huu na kuwa
mwenye huduma katika njia hii. Huu ni mfano halisi wa kutumia
rasilimali za mahali palepale. Yesu hakujua hili kwanza; Alilijua hili
tu Yuda alipolifichuliwa baadaye. Kama mtu mwingine angeweza kutekeleza
wajibu huu, basi mtu mwingine angeweza kufanya hivi badala ya Yuda. Kile
ambacho kiliamuliwa awali kiliweza hasa kufanywa wakati mmoja na Roho
Mtakatifu. Kazi ya Roho Mtakatifu siku zote inafanywa kwa hiari; wakati
wowote Anapopanga kazi Yake, Roho Mtakatifu ataitekeleza. Kwa nini
sikuzote Nasema kwamba kazi ya Roho Mtakatifu ni ya uhalisi? Kwamba siku
zote ni mpya na haijawahi kuwa zee, na siku zote inakuwa na uhai zaidi?
Kazi ya Mungu ilikuwa bado haijawahi kupangwa wakati ulimwengu
ulipoumbwa; hivi sivyo kamwe ilivyofanyika! Kila hatua ya kazi hufikia
athari yake bora kwa wakati wake mwafaka, nazo haziingiliani kati. Kunao
wakati mwingi ambapo mipango katika akili zako hazilingani kamwe na
kazi ya hivi punde ya Roho Mtakatifu. Kazi Yake si rahisi kama
wanavyofikiria watu, wala si ngumu kama watu wengi wanavyofikiria;
inajumuisha kuwaruzuku watu wakati wowote na mahali popote kulingana na
mahitaji yao ya sasa. Hakuna aliye wazi zaidi kuhusu kiini halisi cha
watu kama Yeye, na ni kwa sababu hii mahususi ndiposa hakuna kinachoweza
kufaa mahitaji ya kihalisi ya watu kama vile ambavyo kazi Yake
inavyofanya. Hivyo basi, kutoka katika mtazamo wa kibinadamu, kazi Yake
ilipangiwa milenia kadha mbele. Anavyofanya kazi miongoni mwenu sasa,
kulingana na hali yenu, Yeye pia Anafanya kazi na kuongea wakati wowote
na mahali popote. Wakati watu wako katika hali fulani, Yeye huongea
maneno hayo ambayo hasa ndiyo wanayohitaji ndani yao. Ni kama hatua ya
kwanza ya kazi Yake ya nyakati za kuadibu. Baada ya nyakati za kuadibu,
watu walionyesha tabia fulani, walikuwa na mienendo ya kuasi katika njia
fulani, hali fulani nzuri ziliibuka, hali fulani mbaya pia ziliibuka,
na mipaka ya juu ya hali hii ya ubaya ikafikia kiwango fulani. Mungu
alifanya kazi Yake kutokana na mambo haya yote, na hivyo basi Alichukua
haya yote ili kuweza kutimiza athari bora zaidi kwa ajili ya kazi Yake.
Anatekeleza tu kazi Yake ya kuruzuku miongoni mwa watu kulingana na hali
zao za sasa. Yeye Hutekeleza kila hatua ya kazi Yake kulingana na hali
halisi za watu. Uumbaji wote umo mikononi Mwake; Angekosa kuujua? Kwa
mujibu wa hali za watu, Mungu hutekeleza hatua inayofuata ya kazi
inayofaa kufanywa, wakati na mahali popote. Kazi hii haikupangwa maelfu
ya miaka kabla; hii ni dhana ya kibinadamu tu! Yeye hufanya kazi kwa
kadri Anavyoangalia athari ya kazi Yake, na kazi Yake inaendelea kuwa ya
kina na kukuzwa; kwa kadri Anavyoendelea kuangalia matokeo ya kazi
Yake, ndipo Anapotekeleza hatua inayofuata ya kazi Yake. Yeye hutumia
mambo mengi ili kuingia kwenye mpito hatua kwa hatua na kufanya kazi
Yake mpya kuonekana na watu baada ya muda. Aina hii ya kazi inaweza
kuruzuku mahitaji ya watu, kwani Mungu anawajua watu vizuri mno. Hivi
ndivyo Anavyotekeleza kazi Yake kutoka mbinguni. Vilevile, Mungu mwenye
mwili anafanya kazi Yake kwa njia iyo hiyo, Akipangilia kulingana na
uhalisia na utendakazi miongoni mwa ubinadamu. Hakuna yoyote kati ya
kazi Zake iliyopangwa kabla ya ulimwengu kuumbwa, wala kupangwa kwa
umakinifu kabla ya wakati. Miaka 2,000 baada ya ulimwengu kuumbwa,
Yehova aliona ubinadamu ulikuwa umepotoka sana kiasi cha kwamba
Alikitumia kinywa cha nabii Isaya kutabiri kwamba baada ya Enzi ya
Sheria kukamilika, Angetekeleza kazi Yake ya kuukomboa ubinadamu katika
Enzi ya Neema. Huu ulikuwa mpango wa Yehova, bila shaka, lakini mpango
huu uliweza pia kufanywa kulingana na hali ambazo Aliangalia wakati huo;
bila shaka Yeye hakuufikiria mara moja baada ya kumwumba Mwanadamu.
Isaya alitabiri tu, lakini Yehova hakuandaa matayarisho mara moja wakati
wa Enzi ya Sheria; badala yake, Alianza kazi hii katika mwanzo wa Enzi
ya Neema, wakati mjumbe alipojitokeza katika ndoto ya Yusufu na kumpa
yeye nuru, wakimwambia kwamba Mungu angekuwa mwili, na hivyo kazi Yake
ya kupata mwili ikaanza. Mungu hakujitayarishia kazi Yake ya kuwa mwili
baada ya kuumba ulimwengu, kama watu wanavyofikiria; jambo hili
liliamuliwa tu kulingana na kiwango cha maendeleo ya ubinadamu na hadhi
ya vita Vyake na Shetani.
Wakati Mungu anapokuwa mwili, Roho Wake
anamwingia binadamu; kwa maneno mengine, Roho wa Mungu anauvaa mwili.
Anafanya kazi Yake nchini, na badala ya kuleta naye hatua mbalimbali
zilizozuiliwa kazi hii haina mipaka kamwe. Kazi ambayo Roho Mtakatifu
hufanya katika mwili bado inaamuliwa na athari ya kazi Yake, na Yeye
hutumia mambo haya kuamua urefu wa muda ambao Atafanya kazi akiwa mwili.
Roho Mtakatifu hufichua moja kwa moja kila hatua ya kazi Yake; Yeye
huchunguza kazi Yake anapozidi kuendelea; si jambo ambalo linazidi
maumbile kiasi cha kupanua ile mipaka ya kufikiriwa na binadamu. Hii ni
kama kazi Yehova katika kuumba mbingu na nchi na vitu vyote; Aliweza
kupanga na kufanya kazi wakati huo huo Alitenga nuru kutoka kwenye giza,
na asubuhi pamoja na jioni vyote vikawa—hii ilichukua siku moja. Siku
ya pili Aliumba mbingu, ambayo pia ilichukua siku moja na kisha Akaiumba
nchi, bahari na viumbe vilivyojaa ndani, pia ikichukua siku nyingine
moja. Hali hii iliendelea hivyo hadi siku ya sita, wakati Mungu
alipomwumba binadamu na kumwacha asimamie viumbe hivi vyote juu ya nchi,
mpaka siku ya saba, alipokuwa amemaliza kuumba viumbe vyote, na
akapumzika. Mungu Alibariki siku ya saba na kuitenga kuwa siku takatifu.
Aliiamulia siku hii takatifu baada ya kuviumba viumbe vyote, na wala si
kabla ya kuviumba. Kazi hii iliweza pia kutekeleza kwa hiari; kabla ya
kuviumba viumbe vyote, Hakuamua kuumba ulimwengu kwa siku sita na kuamua
kupumzika siku ya saba; hoja hizi haziko hivi kamwe. Hakusema hivyo,
wala Hakupanga hivi. Kwa vyovyote vile Hakusema kwamba uumbaji wa viumbe
vyote ungekamilishwa katika siku ya sita na kwamba Angepumzika siku ya
saba; badala yake, Aliumba kulingana na kile kilichokuwa kikionekana
kizuri Kwake. Punde Alipomaliza kuumba kila kitu, tayari ilikuwa ni siku
ya sita. Kama ingekuwa ni siku ya tano alipomaliza kuumba kila kitu,
Angepangilia basi siku ya sita kuwa siku takatifu; hata hivyo, Alimaliza
kuumba kila kitu katika siku ya sita, na hivyo basi siku ya saba ikawa
siku takatifu, ambayo imepangiwa kuwa hivyo hadi siku ya leo. Hivyo
basi, kazi Yake ya sasa inatekelezwa kwa njia sawa na hiyo. Yeye huongea
na kuwaruzuku kulingana na hali zenu. Yaani, Roho huongea na kufanya
kazi kulingana na hali za watu; Roho huangalia kila kitu na kufanya kazi
wakati wowote na mahali popote. Kile Ninachofanya, kwa mfano, kuwawekea
na kuwapatia bila kiwazo ni kile mnachohitaji. Ndiyo maana Nasema
kwamba hakuna kazi Yangu iliyo tofauti na uhalisia; yote ni halisi,
kwani nyinyi nyote mnajua ya kwamba “Roho wa Mungu hulinda vyote.” Kama
haya yote yalikuwa yameamuliwa kabla ya wakati, huoni kwamba mambo
yangekuwa yamekwisha amuliwa? Unafikiri kwamba Mungu alifanya kazi kwa
milenia nzima sita na kisha awali kupangilia ubinadamu kuwa mwasi,
wapingaji, waongo na wasio aminifu, kama kuwa na mwili, tabia za
kishetani zilizopotoka, ashiki za macho na kujihusisha kwao kwa mambo
yasiyofaa. Haya yote hayakupangwa awali, lakini yalitokana na upotovu wa
kishetani. Baadhi watasema, “Shetani naye hakuwa ndani ya mashiko ya
Mungu? Mungu naye alikuwa amepanga awali kwamba Shetani angepotosha
binadamu kwa njia hii, na baada ya hapo akatekeleza kazi Yake miongoni
mwa binadamu.” Je, Mungu angepanga awali Shetani hasa ili kuupotosha
ubinadamu? Anayo hamu mno ya kuuruhusu ubinadamu kuishi maisha ya
kawaida na kibinadamu; Angenyanyasa maisha ya ubinadamu? Basi kumshinda
Shetani na kuokoa ubinadamu si kungekuwa jitihada za bure bilashi? Je,
uasi wa binadamu ungeamuliwa vipi kabla? Ulitokana na kunyanyaswa na
Shetani kwa hali halisi; ungepangwa vipi awali na Mungu? Shetani aliye
ndani ya mashiko ya Mungu ambaye mnamwelewa na Shetani ndani ya mashiko
ya Mungu ambaye Ninamzungumzia ni tofauti sana. Kulingana na kauli zenu
kwamba “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake,” Shetani
asingemsaliti Yeye. Je, wewe hujasema kwamba Mungu ni mwenyezi? Maarifa
yenu ni ya kidhahania mno na hayaambatani na uhalisia; hayaeleweki wala
hayana urazini na hayafanyi kazi! Mungu ni mwenyezi; huu si uwongo
kamwe. Malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa sababu Mungu alimpa sehemu ya
mamlaka awali. Bila shaka, tukio hili halikutarajiwa, kama vile Hawa
kukabiliwa na jaribio la nyoka. Hata hivyo, bila kujali ni vipi ambavyo
Shetani hutekeleza usaliti wake, tofauti na Mungu, yeye si mwenyezi.
Kama vile mlivyosema, Shetani ni mwenye nguvu; haijalishi ni nini
atafanya, mamlaka ya Mungu humshinda siku zote. Hii ndiyo maana ya kweli
katika ule msemo “Mungu ni mwenyezi, na Shetani yumo mikononi Mwake.”
Hivyo basi, vita Vyake na Shetani lazima vitekelezwe hatua moja baada ya
nyingine; aidha, Yeye hupanga kazi Yake katika kuitikia ujanja wa
Shetani. Hivi ni kusema, kulingana na enzi, Anawaokoa watu na kufichua
hekima na uweza Wake. Vilevile, kazi katika siku za mwisho haikuamuliwa
awali kabla ya enzi ya Neema; haikuamuliwa awali katika mpangilio
unaofuatana kama huu: Kwanza, fanya tabia ya nje ya binadamu kubadilika;
pili, fanya binadamu kupokea kuadibu na majaribio yake; tatu, fanya
binadamu kupitia kifo; nne, fanya binadamu kupitia zile nyakati za
kumpenda Mungu na kuelezea uamuzi wa kiumbe kilichoumbwa; tano, fanya
binadamu kuyaona mapenzi ya Mungu na kujua Mungu kabisa, kisha
kumkamilisha binadamu. Hakupanga mambo haya wakati wa Enzi ya Neema;
badala yake, Alianza kupanga mambo haya katika enzi ya sasa. Shetani
yumo kazini, kama vile alivyo Mungu. Shetani huonyesha tabia yake
potovu, huku naye Mungu huongea moja kwa moja na kufichua baadhi ya
mambo muhimu. Hii ndiyo kazi inayofanywa leo, na hii ndiyo kanuni sawa
inayofanya kazi na iliyotumika kwenye siku za kale baada ya ulimwengu
kuumbwa.
Kwanza Mungu alimwumba Adamu na Hawa, na pia Alimwumba
nyoka. Miongoni mwa mambo haya yote, nyoka ndiye aliyekuwa mwenye sumu
zaidi; mwili wake ulikuwa na sumu, na Shetani aliitumia sumu hiyo ili
kufaidika. Ni nyoka aliyemjaribu Hawa hadi akatenda dhambi. Adamu
alitenda dhambi baada ya Hawa kutenda, na wawili hawa waliweza
kutofautisha kati ya mema na maovu. Kama Yehova Alikuwa Amejua kwamba
nyoka angemjaribu Hawa, na kwamba Hawa angemjaribu Adamu, kwa nini
Akawaweka wote pale katika bustani? Kama Aliweza kutabiri mambo haya
kwa, nini Akamwumba nyoka na kumweka ndani ya Bustani ya Edeni? Kwa nini
Bustani ya Edeni ilikuwa na tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya?
Alinuia wao walile hilo tunda? Wakati Yehova alipokuja, Adamu wala Hawa
hawakuthubutu kumkabili Yeye, na ulikuwa tu wakati huu ambapo Yehova
alijua kwamba walikuwa wamelila tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya
na kujipata katika ujanja wa yule nyoka. Hatimaye Alimlaani nyoka, na
Akamlaani Adamu na Hawa. Yehova hakuwa na habari wakati wawili hawa
walipolila tunda lile la mti. Ubinadamu ulipotoka hadi kufikia kiwango
cha kuwa na uovu na uasherati wa kimapenzi, hadi kufikia awamu ya mambo
haya yote waliyoyahifadhi katika mioyo yao yakawa maovu na yasiyo ya
haki; yote yalikuwa machafu. Yehova hivyo basi alijutia kwa kuumba
ubinadamu. Baadaye Alitekeleza kazi Yake ya kuharibu ulimwengu kwa
gharika, ambayo Nuhu na watoto wake wa kiume walinusurika. Baadhi ya
mambo kwa hakika hayajaendelea na kuzidi maumbile ya kawaida kama vile
watu wanavyoweza kufikiria. Baadhi wanauliza: Kwa sababu Mungu alijua
malaika mkuu angemsaliti Yeye, kwa nini alimwumba? Hizi ndizo hoja:
Wakati nchi haikuwepo, malaika mkuu ndiye aliyekuwa malaika mkuu zaidi
mbinguni. Alikuwa na mamlaka juu ya malaika wote kule mbinguni; haya
ndiyo yaliyokuwa mamlaka ambayo Mungu alimpa. Kando na Mungu, ndiye
aliyekuwa malaika mkubwa zaidi mbinguni. Wakati Mungu alipouumba
ubinadamu baadaye, malaika mkuu alitekeleza usaliti mkuu zaidi dhidi ya
Mungu nchini. Nasema kwamba alimsaliti Mungu kwa sababu alitaka
kuusimamia ubinadamu na kumzidi Mungu katika mamlaka. Ni malaika mkuu
ambaye alijaribu Hawa hadi akatenda dhambi; alifanya hivyo kwa sababu
alipenda kuanzisha ufalme wake nchini na kuufanya ubinadamu kumsaliti
Mungu na kumtii badala yake. Aliona kwamba kulikuwa na vitu vingi
ambavyo vilimtii; malaika walimtii sawa na vile ambavyo watu walivyomtii
duniani. Ndege na wanyama, miti, misitu, milima, mito na viumbe vyote
vilivyo nchini vilikuwa katika utunzaji wa binadamu—yaani, Adamu na
Hawa—huku nao Adamu na Hawa wakimtii. Malaika mkuu hivyo basi alitamani
kuzidi mamlaka ya Mungu na kumsaliti Mungu. Baadaye aliwaongoza malaika
wengi kumsaliti Mungu, ambao baadaye walikuja kuwa pepo wachafu
mbalimbali. Je, huoni kwamba maendeleo ya binadamu hadi siku ya leo
yamesababishwa na upotoshaji wa malaika mkuu? Ubinadamu upo tu namna
ulivyo leo kwa sababu malaika mkuu alimsaliti Mungu na kuupotosha
ubinadamu. Kazi hii ya hatua kwa hatua haipo popote pale karibu na
dhahania na nyepesi kama vile watu wanavyofikiria. Shetani alitekeleza
usaliti wake kwa sababu fulani. Watu hawawezi kufahamu kitu chepesi kama
hicho. Kwa nini Mungu akaiumba mbingu na nchi na viumbe vyote, na pia
kumwumba Shetani? Kwa sababu Mungu anamdharau Shetani sana, naye Shetani
ni adui Wake, kwa nini akamwumba Shetani? Kwa kumwumba Shetani, hakuwa
anamwumba adui? Mungu kwa hakika hakuumba adui; badala yake, Alimwumba
malaika, na baadaye malaika akamsaliti Yeye. Hadhi yake ilikuwa kubwa
mno kiasi cha kwamba alitaka kumsaliti Mungu. Mtu anaweza kusema kwamba
hali hii ilikuwa ya sadfa, lakini ulikuwa pia mtindo usiokwepeka. Ni
sawa na vile ambavyo mtu atakufa akiwa na umri fulani bila uwezo wa
kuzuia hali hiyo; mambo yamefikia tayari katika awamu fulani. Kunao hata
baadhi ya wale wa kipumbavu wanaosema: Kwa sababu Shetani ni adui Yako,
kwa nini Ukamwumba? Kwani hukujua kuwa malaika huyu mkuu angekusaliti
Wewe? Kwani Huwezi kukazia macho kutoka kwa milele moja hadi nyingine?
Kwani Wewe huijui asili yake? Kwa sababu ulijua waziwazi kuwa
angekusaliti Wewe, basi kwa nini ukamfanya kuwa malaika mkuu? Hata kama
mtu atapuuza suala la usaliti wake, aliweza bado kuwaongoza malaika
wengi na akashuka hadi kwa ulimwengu wa binadamu wasiodumu ili
kuupotosha ubinadamu; hadi siku ya leo umeshindwa kukamilisha mpango
Wako wa usimamizi wa miaka elfu sita. Hayo ni kweli? Je, huoni kwamba
unajiweka kwenye matatizo mengi zaidi kuliko inavyohitajika? Wengine
bado husema: Kama Shetani asingeupotosha ubinadamu hadi siku ya leo,
Mungu asingeuokoa ubinadamu kwa njia hii. Katika mfano huu, hekima na
uweza wa Mungu vyote vingekuwa havionekani; hekima Yake ingewezaje
kujionyesha? Hivyo basi Mungu alikiumba kizazi cha binadamu kwa minajili
ya Shetani; katika siku za usoni, Mungu angefichua uweza
Wake—vinginevyo, binadamu angewezaje kugundua hekima Yake? Kama binadamu
asingempinga Yeye na kuchukua hatua ya kumwasi Yeye, isingehitajika kwa
vitendo Vyake kujionyesha. Kama uumbaji wote ungemwabudu Yeye na kumtii
Yeye, Asingekuwa na kazi ya kufanya. Hali hii nayo ni mbali zaidi na
uhalisia wa mambo, kwani hakuna uchafu wowote kuhusu Mungu, na hivyo
basi Hawezi kuumba uchafu. Yeye hufichua tu vitendo Vyake ili kuweza
kushinda adui Wake, ili kuokoa ubinadamu, ambao aliuumba, ili kuyashinda
mapepo na Shetani, ambao wanamchukia, wanamsaliti Yeye na wanampinga
Yeye, ambao walikuwa katika utawala Wake na walimilikiwa na Yeye mwanzo
kabisa; Anataka kuwashinda hawa mapepo na katika kufanya hivyo kuufichua
uweza Wake kwa viumbe vyote. Ubinadamu na viumbe vyote vilivyomo nchini
sasa hivi vimemilikiwa na Shetani na katika utawala wa waovu. Mungu
anataka kuvifichua vitendo Vyake kwa viumbe vyote ili watu waweze kumjua
Yeye, na hivyo kuishia kumshinda Shetani na kuangamiza kabisa adui
Zake. Uzima wa kazi hii unakamilishwa kupitia kwa ufichuzi wa vitendo
Vyake. Viumbe Vyake vyote vimemilikiwa na Shetani, na hivyo basi
Anapenda kuufichua uweza Wake kwa viumbe hivyo, kwa hivyo kumshinda
Shetani. Kama Shetani asingekuwepo, Asingehitaji kuvifichua matendo Yake
Kama usingekuwa unyanyasaji wa Shetani, angeuumba ubinadamu na
kuuongoza kuishi katika Bustani ya Edeni. Kwa nini Hakuwahi kufichua
vitendo Vyake vyote kwa malaika au malaika mkuu kabla ya kusalitiwa na
Shetani? Kama malaika na malaika mkuu wangalimjua Yeye, na pia kumtii
Yeye pale mwanzoni, basi Asingewahi kutekeleza vile vitendo vya kazi
visivyo na maana. Kwa sababu ya uwepo wa Shetani na mapepo, watu
humpinga na wanajazwa hadi pomoni na tabia ya uasi, na hivyo basi Mungu
angependa kufichua vitendo Vyake. Kwa sababu Angependa kupigana vita na
Shetani, lazima Atumie mamlaka Yake kumshinda Shetani na kutumia vitendo
Vyake vyote kumshinda Shetani; kwa njia hii, kazi Yake ya wokovu
Anayotekeleza miongoni mwa ubinadamu itawafanya watu waone hekima na
uwezo Wake. Kazi anayofanya Mungu leo ni yenye maana na haifanani kwa
vyovyote vile na ile baadhi watu wanayoisema: “Je, kazi hii Unayofanya
haihitilafiani? Je, huu mfuatano wa kazi si mazoezi ya kujitatiza Wewe
tu? Ulimwumba Shetani, kisha baadaye ukamruhusu Akakusaliti na kukupinga
Wewe. Uliuumba ubinadamu, na kisha ukamkabidhi Shetani, na Ukaruhusu
Adamu na Hawa kujaribiwa. Kwa sababu uliyafanya mambo haya yote
kimakusudi, kwa nini Unauchukia ubinadamu? Kwa nini Unachukia Shetani?
Mambo haya si ya kujitungia Wewe? Ni nini kipo cha Wewe kuchukia?” Watu
wengi wa kipumbavu watasema hayo. Wanatamani kumpenda Mungu, lakini
mioyoni mwao wanalalamika kumhusu Mungu—ukinzani jinsi gani! Wewe
huelewi ukweli, unazo fikira nyingi sana za kimiujiza, na pia unadai
kwamba hili ni kosa la Mungu—wewe ni mpumbavu kiasi kipi! Ni wewe
unayecheza na ukweli; si kosa la Mungu! Baadhi ya watu wataweza hata
kulalamika na kulalamika: Ni wewe uliyemwumba Shetani, na ni Wewe
uliyempa Shetani ubinadamu. Ubinadamu unamiliki tabia ya kishetani;
badala ya kuusamehe, Unauchukia kwa kiwango fulani. Mwanzo Uliupenda
ubinadamu kwa kiwango fulani. Ulimtimua Shetani hadi ulimwenguni mwa
binadamu, na sasa Unauchukia ubinadamu. Ni wewe unayeuchukia na kuupenda
ubinadamu—maelezo ya kauli hii ni yapi? Je, huu si ukinzani?? Bila
kujali ni vipi mnavyoangalia suala hili, hivi ndivyo ilivyofanyika
mbinguni; malaika mkuu alimsaliti Mungu kwa njia hii, nao ubinadamu
ukapotoshwa kwa njia hii, na ukaendelea mpaka leo kwa njia hii. Bila
kujali ni vipi mnavyopangilia kauli hizi, hii ndiyo hadithi yote. Hata
hivyo, lazima muelewe kwamba Mungu anaifanya kazi ya leo ili kuwaokoa
nyinyi, na ili kumshinda Shetani.
Kwa sababu malaika hasa alikuwa
mnyonge na hakumiliki uwezo wowote, angekuwa mwenye kiburi kama angepewa
mamlaka, hasa malaika mkuu, ambaye hadhi yake ilikuwa ya juu zaidi
kuliko ile ya wale malaika wengine. Malaika mkuu alikuwa ndiye mfalme wa
malaika wote. Aliwaongoza mamilioni ya malaika, na kwa usimamizi wa
Yehova mamlaka yake yalizidi yale ya malaika yeyote mwingine. Alitaka
kufanya hivi na vile, na kuwaongoza malaika hadi ulimwenguni mwa
binadamu ili kuutawala ulimwengu. Mungu alisema kwamba Yeye huutawala
ulimwengu; malaika mkuu akasema kwamba ulimwengu ulikuwa wake wa
kutawala, na kuanzia hapo akamsaliti Mungu. Mbinguni, Mungu alikuwa
ameuumba ulimwengu mwingine. Malaika mkuu akataka kuutawala ulimwengu
huu na pia kushuka chini kwenye himaya ya binadamu. Je, Mungu
angemruhusu kufanya hivi? Hivyo basi, Alimtimua hadi chini na akawa
angani. Tangu hapo alipoupotosha ubinadamu, Mungu amefanya vita dhidi
yake ili kuukoa ubinadamu; Ametumia milenia hizi sita kumshinda. Dhana
yenu ya Mwenyezi Mungu hailingani na kazi ambayo Mungu anatekeleza sasa;
haifanyi kazi katika kutenda na ni ya upumbavu ajabu! Kwa hakika, Mungu
alitangaza malaika mkuu kuwa adui Yake baada tu ya malaika mkuu
kumsaliti Yeye. Ilikuwa kutokana tu na kusaliti kwake Mungu ndiposa
aliudhalilisha ubinadamu baada ya kuwasili katika ulimwengu wa
ubinadamu, na ilikuwa kwa sababu hii ndiposa ubinadamu uliendelea hadi
kiwango hiki. Kufuatia haya, Mungu alikula kiapo na Shetani:
Nitakushinda wewe na kuuokoa ubinadamu, uumbaji Wangu. Shetani
hakushawishika wakati wa mwanzo na akasema, ni nini kwa hakika
unachoweza kunifanyia mimi? Wewe unaweza kunifukuza hadi katika anga
kweli? Wewe unaweza kwa kweli kunishinda mimi? Baada ya Mungu kumtimua
hadi angani, Hakumtilia maanani tena na kisha Alianza kuuokoa ubinadamu
na kufanya kazi Yake mwenyewe, licha ya unyanyasaji ulioendelea kutoka
kwa Shetani. Kila kitu ambacho Shetani angeweza kufanya kilitokana na
nguvu alizopewa na Mungu; alichukua vitu hivi pamoja naye hadi angani na
amevihifadhi vitu hivi hadi leo. Mungu alimtimua hadi angani lakini
hakuchukua mamlaka yake, na hivyo basi aliendelea kuupotosha ubinadamu.
Mungu, kwa mkono mwingine, Alianza kuuokoa ubinadamu, ambao Shetani
alikuwa amepotosha baada ya kuumbwa kwao. Mungu hakufichua vitendo Vyake
wakati akiwa mbinguni; hata hivyo, kabla ya kuiumba dunia, Aliwaruhusu
watu kuviona vitendo Vyake katika ulimwengu Aliouumba mbinguni na hivyo
kuwaongoza watu juu mbinguni. Aliwapa hekima na busara, na kuwaongoza
watu hao kuishi kwenye ulimwengu huo. Kiasili, hakuna kati yenu ambaye
amewahi kusikia haya awali. Baadaye, baada ya Mungu kuumba ubinadamu,
malaika mkuu alianza kuupotosha ubinadamu; duniani, ubinadamu wote
ulikuwa katika fujo. Ulikuwa ni wakati huu tu ambapo Alianza vita Vyake
dhidi ya Shetani, na ulikuwa ni katika wakati huu tu ambapo watu waliona
vitendo Vyake. Mwanzo vitendo Vyake vilifichwa kutoka kwa ubinadamu.
Baada ya Shetani kutimuliwa hadi angani, alijishughulisha na masuala
yake, naye Mungu akajishughulisha Mwenyewe na kazi Yake binafsi, mara
kwa mara Akifanya vita dhidi ya Shetani, kila wakati mpaka siku za
mwisho. Sasa ndio wakati ambao Shetani anafaa kuangamizwa. Mwanzoni
Mungu alimpa mamlaka, na baadaye Mungu alimtimua hadi angani, lakini
Shetani alibaki mwasi. Baadaye, alipofika nchini, aliupotosha ubinadamu,
lakini Mungu alikuwa kwa hakika ulimwenguni akiusimamia ubinadamu.
Mungu hutumia usimamizi Wake wa watu kumshinda Shetani. Kwa kuwapotosha
watu, Shetani huleta hutamatisha hatima ya watu na kuinyanyasa kazi ya
Mungu. Kwa upande mwingine, kazi ya Mungu ndiyo wokovu wa ubinadamu. Ni
hatua gani ya kazi yenyewe ya Mungu ambayo hainuii kuuokoa ubinadamu? Ni
hatua gani hainuii kutakasa watu, ili kuwafanya kuwa wenye haki na
kuwafanya kuishi kwa njia ambayo huunda taswira inayoweza kupendwa?
Shetani, hata hivyo, hafanyi hivi. Yeye huupotosha ubinadamu; siku zote
anatekeleza kazi zake za kuupotosha ubinadamu kote ulimwenguni. Bila
shaka, Mungu pia hufanya kazi Yake. Hamtilii maanani Shetani. Haijalishi
ni mamlaka kiasi kipi Shetani anayo, mamlaka yake bado yalitoka kwa
Mungu; Mungu kwa hakika hakumpa mamlaka Yake yote tu, na hivyo basi
haijalishi ni nini afanyacho Shetani, hawezi kuzidi Mungu na siku zote
huwa kwenye udhibiti wa Mungu. Mungu hakufichua vitendo Vyake vyovyote
akiwa mbinguni. Alimpa Shetani kiwango kidogo tu cha mamlaka ili
kumruhusu kutekeleza udhibiti wake dhidi ya malaika. Hivyo basi,
haijalishi ni nini hufanya, hawezi kuzidi mamlaka ya Mungu kwa sababu
mamlaka ambayo Mungu alimpa awali ni finyu. Huku Mungu akifanya kazi,
Shetani hunyanyasa. Katika siku za mwisho, atamaliza unyanyasaji wake;
vilevile, kazi ya Mungu itakamilika, na aina ya mtu ambaye Mungu
angependa kumkamilisha atakuwa amekamilika. Mungu huwaelekeza watu kwa
njia nzuri; maisha Yake ni maji yenye uzima, yasiyopimika na yasiyo na
mipaka. Shetani amepotosha binadamu hadi kiwango fulani; hatimaye, yale
maji hai ya uzima yatamkamilisha binadamu, na haitawezekana kwa Shetani
kuingilia kati na kutekeleza kazi yake. Hivyo basi, Mungu ataweza
kuwapata kabisa watu wake. Shetani angali anakataa kukubali haya sasa;
siku zote hupambana na Mungu, lakini Mungu hamtilii maanani. Amesema,
Nitakuwa mshindi dhidi ya nguvu zote za giza za Shetani na dhidi ya
ushawishi wote wa giza. Hii ndiyo kazi ambayo lazima ifanywe kwa mwili,
na ndiyo pia maana ya kupata mwili kwa Yesu Kristo. Ni kukamilisha awamu
ya kazi ya kumshinda Shetani katika siku za mwisho, kuondoa vitu vyote
vinavyomilikiwa na Shetani. Ushindi wa Mungu dhidi ya Shetani ni mtindo
usioepukika! Shetani kwa hakika alishindwa kitambo sana. Wakati injili
ilipoanza kuenezwa kote nchini mwa joka kubwa jekundu, yaani, wakati
Mungu mwenye mwili alipoanza kufanya kazi na kazi hii ikafanywa
kuendelea, Shetani aliweza kushindwa kabisa, kwani kupata mwili wa
Kristo kulimaanisha kumshinda Shetani. Shetani aliona kwamba Mungu
alikuwa kwa mara nyingine tena amekuwa mwili na alikuwa ameanza
kutekeleza kazi Yake, na akaona kwamba hakuna nguvu ambazo zingeweza
kukomesha kazi hii. Hivyo basi, alipigwa na bumbuazi alipoona kazi hii
na hakuthubutu kufanya kazi yoyote nyingine zaidi. Kwanza Shetani
alifikiria kwamba pia alimiliki hekima nyingi, na akaingilia kati na
kunyanyasa kazi ya Mungu; hata hivyo, hakutarajia kwamba Mungu alikuwa
kwa mara nyingine tena amekuwa mwili, na kwamba katika kazi Yake, Mungu
alikuwa ametumia uasi Wake kuhudumu kama ufunuo na hukumu kwa ubinadamu;
na hivyo basi kushinda ubinadamu na kumshinda Shetani. Mungu ni mwerevu
kumshinda, na kazi Yake inamzidi Shetani. Hivyo basi, Niliwahi kutaja
awali kwamba: Kazi Ninayoifanya inatekelezwa kutokana na ujanja wa
Shetani. Mwishowe Nitafichua uweza Wangu na hali ya kutoweza kwa
Shetani. Wakati Mungu anapofanya kazi Yake, Shetani anamfuata unyo kwa
unyo kutoka nyuma mpaka mwishowe anaangamizwa—hatajua hata
kilichomgonga! Ataweza kutambua tu ukweli baada ya kuvunjwa na
kupondwapondwa; na wakati huo atakuwa tayari amechomwa kwenye ziwa la
moto. Hatakuwa ameshawishika kabisa wakati huo? Kwani hatakuwa na njama
zozote zingine za kutumia!
Ni kazi hii ya kihalisi ya hatua kwa
hatua ambayo mara nyingi inalemea moyo wa Mungu kwa huzuni ya binadamu,
ili vita Vyake na Shetani vimedumu kwa sasa miaka 6,000. Hivyo basi
Mungu alisema hivi: Sitawahi tena kuumba ubinadamu, wala kuwahi tena
kuwapa malaika mamlaka. Kuanzia hapo, wakati malaika walipokuja kazini
duniani, walimfuata tu Mungu ili kufanya kazi fulani. Hakuwahi kuwapatia
malaika mamlaka. Je, malaika ambao Waisraeli waliwaona walitekeleza
vipi kazi yao? Walijifichua katika ndoto na kupitisha maneno ya Yehova.
Wakati Yesu alipofufuka siku tatu baada ya kusulubishwa, ni malaika ndio
waliolisukuma jiwe kando; Roho wa Mungu hakufanya kazi hii yeye
binafsi. Malaika waliweza kufanya tu kazi ya aina hii; waliweza kuwa na
wajibu wa usaidizi na hawakuwa na mamlaka, kwani Mungu hatawahi tena
kuwapatia mamlaka. Baada ya kufanya kazi kwa muda fulani, watu ambao
Mungu alitumia hapa duniani walichukua nafasi ya Mungu na kusema, Nataka
kuzidi ulimwengu! Nataka kusimama kwenye mbingu ya tatu! Tunataka
hatamu za nguvu ya ukuu! Wangekuwa na kiburi baada ya siku kadhaa za
kazi; walitaka nguvu ya ukuu duniani, walitaka kuanzisha taifa jingine,
walitaka vitu vyote katika utawala wao na walitaka kusimama katika
mbingu ya tatu. Je, kwani hujui kwamba wewe ni binadamu tu unayetumiwa
na Mungu? Unawezaje kupaa hadi kwenye mbingu ya tatu? Mungu huja duniani
kufanya kazi, kimyakimya na bila ya kujitangaza, na Huondoka kimyakimya
baada ya kukamilisha kazi Yake. Hajitangazi kama vile binadamu
wanavyofanya, lakini badala yake Anatekeleza kwa kiuhalisia kazi Yake.
Wala haingii kanisani na kujitangaza, Nitawamaliza nyinyi nyote!
Nitawalaani na kuwaadibu! Anatekeleza tu kazi Yake binafsi, na kuondoka
mara Anapomaliza. Wale wachungaji wa kidini wanaowaponya wagonjwa na
kupunga mapepo, wanawasomea wengine kutoka kwenye madhabahu, na kutoa
hotuba ndefu na zenye makuu na kuzungumzia masuala yasiyo ya kihalisi,
wana kiburi hadi moyoni! Wao ni vizazi vya malaika mkuu!
Baada ya
kutekeleza kazi Yake ya miaka 6,000 hadi leo, Mungu tayari amefichua
vitendo Vyake vingi, kimsingi kumshinda Shetani na kuuokoa ubinadamu
wote. Anatumia fursa hii kuruhusu kila kitu mbinguni, kila kitu kilicho
duniani, kila kitu kinachopatikana baharini pamoja na kila kifaa cha
mwisho ambacho Mungu aliumba ulimwenguni kuweza kuona uweza wa Mungu na
kushuhudia vitendo vyote vya Mungu. Huchukua fursa ya kumshinda Shetani
ili kufichua vitendo Vyake kwa ubinadamu na kuwaruhusu watu kuweza
kumsifu Yeye na kuitukuza hekima Yake kwa kumshinda Shetani. Kila kitu
nchini, mbinguni na ndani ya bahari humletea utukufu, huusifu uweza
Wake, kinasifu vitendo Vyake vyote na kutamka kwa sauti jina Lake
takatifu. Hii ni ithibati ya ushindi Wake dhidi ya Shetani; hii ni
ithibati ya Yeye kumshinda Shetani; na la muhimu zaidi, ni ithibati ya
wokovu Wake kwa ubinadamu. Uumbaji wote wa Mungu humletea utukufu,
humsifu Yeye kwa kumshinda adui Wake na kurudi kwa ushindi na humsifu
Yeye kama Mfalme mkubwa mwenye ushindi. Kusudio lake si kumshinda
Shetani tu, na hivyo basi kazi Yake imeendelea kwa miaka 6,000. Anatumia
kushindwa kwa Shetani kuuokoa ubinadamu; Anakutumia kushindwa kwa
Shetani kufichua vitendo Vyake vyote na kufichua utukufu Wake wote.
Atapata utukufu, na umati wote wa malaika utaweza pia kushuhudia utukufu
Wake wote. Wajumbe walio mbinguni, wanadamu walio nchini na uumbaji
wote ulio nchini utauona utukufu wa Muumba. Hii ndiyo kazi Aifanyayo.
Viumbe vyake kule mbinguni na nchini wote utauona utukufu Wake, na
atarudi kwa vifijo na nderemo baada ya kumshinda Shetani kabisa na
kuruhusu binadamu kumsifu Yeye. Ataweza hivyo basi kutimiza kwa ufanisi
vipengele hivi viwili. Mwishowe ubinadamu wote utashindwa na Yeye, na
atamwondoa yeyote yule anayepinga au kuasi, hivi ni kusema, Atawaondoa
wale wote wanaomilikiwa na Shetani. Unaviona vitendo hivi vyote vya
Mungu sasa, ilhali ungali unapinga na unakuwa mwasi na hutaki
kunyenyekea; unayahifadhi mambo mengi ndani yako na unafanya utakacho;
unafuata ashiki zako, na kile upendacho—huu ni uasi; huu ni upingaji.
Kusadiki Mungu ambako kunatekelezwa kwa ajili ya mwili, kwa ajili ya
ashiki za mtu, na kwa ajili ya kile anachopenda mtu, kwa ajili ya
ulimwengu, na kwa ajili ya Shetani ni kuchafu; ni upinzani na uasi.
Kunazo aina zote tofauti za kusadiki sasa: Baadhi hutafuta hifadhi dhidi
ya janga, na wengine hutafuta kupokea baraka, huku baadhi wakitamani
kuelewa mafumbo na bado wengine hujaribu kupata pesa. Hiyo yote ni
mifumo ya upinzani; hiyo yote ni kukufuru! Kusema kwamba mtu anapinga au
anaasi—huku si kwa mujibu wa mambo haya? Watu wengi sasa hivi
wanalalamika, wanatamka manung'uniko au kutoa hukumu. Mambo haya yote
yanafanywa na waovu; wao ni binadamu wapinzani na waasi; watu kama hao
wamemilikiwa na kujawa na Shetani. Watu ambao Mungu huwapata ni wale
wanaonyenyekea Kwake kabisa, wale waliopotoshwa na Shetani lakini
kuokolewa na kushindwa na kazi Yake sasa, wale waliovumilia majaribu na
hatimaye wamepokelewa kabisa na Mungu na hawaishi tena katika utawala wa
Shetani na wamevunja minyororo ya udhalimu,, walio radhi kuishi kwa
kudhihirisha utakatifu —hawa ndio watu watakatifu zaidi; hawa ndio wale
watakatifu. Kama matendo yako ya sasa hayalingani na sehemu moja ya
mahitaji ya Mungu utaondolewa. Hii haipingiki. Kila kitu kinafanywa
kulingana na leo; ingawa Amekuamulia awali na kukuchagua wewe, hatua
zako leo bado zitaamua matokeo yako. Kama huwezi kuendelea kwa mwendo
sawa sasa, utaondolewa. Kama huwezi kuendelea kwa mwendo sawa sasa, hata
unawezaje kutumaini [a] kuendelea kwa mwendo sawa baadaye?
Vile sasa muujiza mkubwa kama huo umekufanyikia wewe, bado huamini. Hebu
Niambie, utamwamini vipi baadaye wakati Atakapomaliza kazi Yake na
Hafanyi tena kazi kama hiyo? Wakati huo itakuwa vigumu zaidi kwako wewe
kumfuata Yeye! Baadaye Mungu atategemea mwelekeo na maarifa yako katika
kazi ya Mungu kuwa mwili na kile ulichopitia wewe ili kuamua kama wewe
ni mwenye dhambi au mwenye haki, au kuamua kama wewe ndiwe uliyefanywa
kuwa mtimilifu ama wewe ni yule aliyeondolewa. Lazima uweze kuona wazi
sasa. Roho Mtakatifu hufanya kazi hivyo: Yeye huamua matokeo yako
kulingana na tabia yako leo. Nani huongea maneno ya leo? Nani hufanya
kazi ya leo? Nani huamua kama utaondolewa leo? Nani huamua kukufanya
kuwa mtimilifu? Hivi sivyo Ninavyofanya Mimi mwenyewe? Mimi Ndimi
ninayeongea maneno haya; Mimi Ndimi ninayetekeleza kazi hii. Kulaani,
kuadibu na kuhukumu watu vyote ni sehemu ya kazi Yangu mimi binafsi.
Hatimaye, kukuondoa kutakuwa pia kazi Yangu binafsi. Yote ni kazi Yangu
binafsi! Kukufanya kuwa mtimilifu ni shughuli Yangu binafsi, na
kukuruhusu kufurahia baraka ni shughuli Yangu binafsi pia. Hii yote ni
kazi Yangu binafsi. Matokeo yako hayakuamuliwa awali na Yehova;
yanaamuliwa leo na Mungu wa leo. Yanaamuliwa sasa; hayakuamuliwa kabla
ya ulimwengu kuumbwa. Baadhi ya watu wapumbavu husema, Pengine kuna
jambo mbaya na macho Yako, na Hunioni mimi kama vile Unavyofaa kuniona.
Hatimaye mtaona namna Roho atakavyoonyesha kila kitu! Yesu kwanza
Alimchagua Yuda kama mwanafunzi Wake. Watu hufikiria kwamba Yesu alikuwa
amefanya kosa kwa kumchagua yeye. Angewezaje kumchagua mwanafunzi
ambaye angemsaliti? Mwanzo Yuda hakuwa na nia ya kumsaliti Yesu. Hili
jambo lilifanyika tu baadaye. Wakati huo Yesu alikuwa amemchukua Yuda
kwa upendo; Alimfanya mwanamume huyo kumfuata Yeye na kumfanya
kuwajibikia masuala yao ya kifedha. Kama Angejua kwamba Yuda angebadhiri
pesa, Asingemwacha kusimamia pesa hizo. Mtu anaweza kusema kwamba Yesu
hakujua mwanzo kwamba mwanamume huyu alikuwa asiye mwaminifu na
mdanganyifu, na kwamba aliwadanganya ndugu zake. Baadaye Yuda
alipokwisha kumfuata kwa muda fulani, Yesu alimwona akiwadanganya ndugu
zake na akidanganya Mungu. Watu waligundua pia kwamba siku zote
angetumia pesa kutoka kwenye mfuko wa fedha na kisha wakamwambia Yesu.
Yesu alipata habari tu kuhusu haya yote wakati huu. Kwa sababu Yesu
alikuwa atekeleze kazi ya kusulubishwa na Alihitaji mtu wa kumsaliti
Yeye, na Yuda alitokea tu kuwa mhusika mzuri wa wajibu huu, Yesu
akasema, kutakuwepo miongoni mwenu ambaye atanisaliti Mimi. Mwana wa
adamu atatumia usaliti huu kuweza kusulubishwa na baada ya siku tatu
atafufuka. Wakati huo Yesu hakuchagua hasa Yuda ili aweze kumsaliti
Yeye; kinyume cha mambo ni kwamba, Alipenda kwamba Yuda awe mwanafunzi
mtiifu. Kwa mshangao Wake, Yuda aligeuka kuwa mlafi na mwenye sifa mbaya
aliyemsaliti Bwana, na akatumia hali hii kumchagua Yuda kwa kazi hii.
Kama wanafunzi wote kumi na wawili wa Yesu wangekuwa watiifu, na hakuna
mtu kama Yuda angekuwa miongoni mwao, yule mtu wa kumsaliti Yesu
angekuwa hatimaye mtu kutoka nje ya wale wanafunzi. Hata hivyo, wakati
huo ilifanyika tu kwamba kulikuwa na mmoja miongoni mwao aliyefurahia
kuchukua hongo—Yuda. Yesu kwa hivyo basi alimtumia mwanamume huyu
kukamilisha kazi Yake. Jambo hili liweje rahisi hivyo! Yesu hakuliamua
awali mwanzoni mwa kazi Yake; alifanya tu uamuzi huu punde tu mambo
yalipoimarika hadi hatua fulani. Huu ulikuwa ni uamuzi wa Yesu, yaani,
uamuzi wa Roho wa Mungu Mwenyewe. Wakati huo ni Yesu aliyemchagua Yuda;
wakati Yuda alipomsaliti Yesu baadaye, haya yalikuwa ni matendo ya Roho
Mtakatifu ili kuhudumu hatima Zake mwenyewe; ilikuwa ni kazi ya Roho
Mtakatifu wakati huo. Wakati Yesu alipomchagua Yuda, Hakuwa na wazo
lolote kwamba Angemsaliti. Alijua tu kwamba alikuwa Yuda Iskariote.
Matokeo yenu yanaamuliwa pia kulingana na kiwango chenu cha kunyenyekea
leo na kulingana na kiwango chenu cha ukuzi wa maisha, na wala si
kulingana na wazo miongoni mwa dhana za binadamu kwamba “ilikuwa
imepangiwa awali katika uumbaji wa ulimwengu.” Lazima uelewe mambo haya
waziwazi. Kazi hii nzima haitekelezwi kulingana na kufikiria kwako.
kutoka kwa Neno Laonekana Katika Mwili
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni