Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo msalabani. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo msalabani. Onyesha machapisho yote

12.05.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)

Mwenyezi-Mungu, Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Umeme-wa-Mashariki
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)

Mwenyezi Mungu alisema, Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Jinsi ambavyo mwenendo wa mtu ama mwili wake unavyobadilika haiamui ikiwa ameshindwa. Badala yake, ni wakati ambapo fikira zako, utambuzi wako, na ufahamu wako unabadilika—yaani, ni wakati mielekeo yako yote ya kifikira inabadilika—ndipo huwa umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa. 

11.24.2017

Fumbo la Kupata Mwili (4)

        


Mwenyezi Mungu alisema, “Mnapaswa kujua kuhusu hadithi ya ndani na uumbaji wa Biblia. Ufahamu huu haushikiliwi na wale ambao hawajakubali kazi mpya ya Mungu. Wao hawajui. Waelezee mambo haya ya kiini, na hawatakuwa pamoja nawe wenye kushikilia sana elimu ya vitabuni na sheria kuhusu Biblia. Wao huchunguza kwa uthabiti kile ambacho kimetabiriwa: Kauli hii imeshatimia? Kauli ile imeshatimia? Kukubali kwao injili ni kwa mujibu wa Biblia; wao huhubiri injili kulingana na Biblia. Wao huyategemea maneno ya Biblia kumwamini Mungu; bila Biblia, wao hawatamwamini Mungu. 

11.04.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Mwenyezi Mungu, Yesu, Mungu

Maono ya Kazi ya Mungu (2)

Mwenyezi Mungu alisema, Enzi ya Neema ilihubiri injili ya toba, na alimradi mwanadamu aliamini, basi angeokolewa. Leo, badala ya wokovu kuna majadiliano tu ya ushindi na ukamilifu. Haisemwi katu kwamba mtu mmoja akiamini, familia yake yote itabarikiwa, au kwamba wokovu ni ya mara moja na kwa wote.