Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yesu-Mwokozi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Yesu-Mwokozi. Onyesha machapisho yote

12.05.2017

Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)

Mwenyezi-Mungu, Kanisa-la-Mwenyezi-Mungu, Umeme-wa-Mashariki
Kanisa la Mwenyezi Mungu | Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Kushinda (3)

Mwenyezi Mungu alisema, Matokeo ya kutimizwa kutoka kwa kazi ya kushinda kimsingi ni kwa ajili ya mwili wa mwanadamu kuacha kuasi, yaani, ili fikira za mwanadamu zipate ufahamu mpya wa Mungu, moyo wake umtii Mungu kabisa, na aamue kuwa wa Mungu. Jinsi ambavyo mwenendo wa mtu ama mwili wake unavyobadilika haiamui ikiwa ameshindwa. Badala yake, ni wakati ambapo fikira zako, utambuzi wako, na ufahamu wako unabadilika—yaani, ni wakati mielekeo yako yote ya kifikira inabadilika—ndipo huwa umeshindwa na Mungu. Ukiamua kutii na kupata fikira mpya, pale ambapo huingizi mawazo na nia zako katika maneno na kazi ya Mungu, na wakati ubongo wako unaweza kufikiri kwa njia ya kawaida, yaani, unapoweza kujitolea kwa Mungu kwa moyo wako wote—huyu ni mtu aliyeshindwa kabisa.