9.21.2019

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wana elimu dhabiti ya Biblia, kuieleza Biblia kinaganaga mara kwa mara kwa watu wakiwafanya washikilie Biblia, kwa hiyo kuieleza Biblia kinaganaga na kuiinua kwa kweli ni kumshuhudia na kumtukuza Bwana? Kwa nini inasemwa kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa ni Mafarisayo wa uongo? Bado hatuwezi kulielewa jambo hili, kwa hiyo unaweza kutujibu hili tafadhali?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, Biblia

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wana elimu dhabiti ya Biblia, kuieleza Biblia kinaganaga mara kwa mara kwa watu wakiwafanya washikilie Biblia, kwa hiyo kuieleza Biblia kinaganaga na kuiinua kwa kweli ni kumshuhudia na kumtukuza Bwana? Kwa nini inasemwa kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa ni Mafarisayo wa uongo? Bado hatuwezi kulielewa jambo hili, kwa hiyo unaweza kutujibu hili tafadhali?

Jibu:
Kwa watu, kueleza Biblia hakupaswi kuwa makosa, lakini wakati huo huo kama kueleza Biblia, kile wanachofanya hasa ni vitendo ambavyo vinavyopinga Mungu. Hawa ni watu wa aina gani? Je, si Mafarisayo wanafiki? Je, si wao ni wapinga Kristo wanaompinga Mungu? Kueleza Biblia ni kumpinga Mungu vipi? Kwa nini ni kumhukumu Mungu? Hata kuwasiliana kwa njia hii bado kuna watu ambao hawaelewi na bado wanadhani kuwa kuieleza Biblia ni kumwinua na kumshuhudia Mungu. Makuhani wakuu wa Kiyahudi, waandishi na Mafarisayo wakati huo wote walikuwa wasomi wa maandiko na wataalamu ambao mara nyingi walieleza maandiko kwa watu.

9.20.2019

Wakati huo, wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, Mafarisayo Wayahudi walimkana na kumhukumu Yeye vikali na kumtundika msalabani. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anapokuja kufanya kazi Yake, wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa pia wanamkana Yeye vikali na kumhukumu Yeye, wakimtundika Mungu msalabani tena. Kwa nini Mafarisayo Wayahudi na wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa huuchukia ukweli hivyo na kumpinga vikali Kristo kwa njia hii? Ni nini hasa kiini chao cha asili?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

Kila mtu anayeamini katika Bwana anajua Mafarisayo waliompinga Bwana Yesu, lakini mzizi, asili ya kweli ya upinzani wao ilikuwa nini? Unaweza kusema kwamba katika historia ya dini ya miaka 2,000, hakuna mtu aliyeelewa jibu la swali hili. Ingawa kulaani kwa Bwana Yesu kwa Mafarisayo kuliandikwa katika Agano Jipya, hakuna mtu ambaye ameweza kumaizi asili ya Mafarisayo. Mwenyezi Mungu anapowasili katika siku za mwisho, Anafichua jibu la kweli kwa swali hili. Hebu tusome maneno ya Mwenyezi Mungu, “Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima.

9.19.2019

Mafarisayo mara kwa mara waliielezaBiblia kinaganaga kwa watu katika masinagogi, wakionekana kuwa wacha Mungu na wenye huruma, na kwa dhahiri hawakuonekana kufanya kitu chochote kinyume cha sheria. Kwa nini Mafarisayo walilaaniwa na Bwana Yesu? Unafiki wao ulidhihirishwaje? Kwa nini husemekana kwamba wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa hutembea njia sawa na Mafarisayo wanafiki?

Watu wanaoamini katika Bwana wanajua kwamba Bwana Yesu kweli aliwachukia Mafarisayo na aliwalaani na kutamka dhiki saba juu yao. Hii ina maana sana katika kuruhusu waumini katika Bwana kutambua Mafarisayo wanafiki, kujitenga na utumwa na udhibiti wao na kupata wokovu wa Mungu. Hata hivyo, ni aibu. Waumini wengi hawawezi kutambua kiini cha unafiki wa Mafarisayo. Hata hawaelewi ni kwa nini Bwana Yesu aliwachukia na kuwalaani Mafarisayo sana. Leo tutazugumza kidogo kuhusu matatizo haya. Mafarisayo mara nyingi waliwafafanulia wengine Biblia katika sinagogi.

9.18.2019

Unashuhudia kuwa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Neno Laonekana katika Mwili ni maneno ya Mungu Mwenyewe, lakini tunaamini kuwa ni maneno ya mtu aliyepatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, Kile ningependa kufuatilia ni, ni nini hasa tofauti kati ya maneno yanayoonyeshwa na Mungu mwenye mwili na maneno yaliyosemwa na mtu ambaye amepatiwa nuru na Roho Mtakatifu?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Kanisa

Unashuhudia kuwa maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika Neno Laonekana katika Mwili ni maneno ya Mungu Mwenyewe, lakini tunaamini kuwa ni maneno ya mtu aliyepatiwa nuru na Roho Mtakatifu. Kwa hiyo, Kile ningependa kufuatilia ni, ni nini hasa tofauti kati ya maneno yanayoonyeshwa na Mungu mwenye mwili na maneno yaliyosemwa na mtu ambaye amepatiwa nuru na Roho Mtakatifu?

Jibu:
Yote ambayo Mwenyezi Mungu huonyesha ni ukweli, na Neno Laonekana katika Mwili kwa kweli ni matamshi ya Mwenyezi Mungu, ambaye ni kuja kwa mara ya pili kwa Bwana Yesu. Wote walio na moyo na roho watakikubali kikamilifu baada ya kuona neno Lake, watambue kwamba ni sauti ya Mungu, na kusujudu mbele ya Mungu. Hata hivyo, bado kuna baadhi ya watu wanaoamini kwamba maneno yaliyoonyeshwa na Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho ni maneno tu yaliyoandikwa na mwanadamu aliyetiwa msukumo na Roho Mtakatifu, na hawaamini ni neno halisi la Mungu. Hili linaonyesha kwamba imani yetu kwa Mungu haimaanishi kumjua Mungu, kwamba hatuwezi kubainisha neno la Mungu kutoka kwa maneno ya mwanadamu, na kwamba zaidi ya hayo, hatuwezi kubainisha dhahiri maneno yanayokubaliana na ukweli kutoka kwa ukweli halisi.

9.17.2019

Unashuhudia kwamba Bwana Yesu amekwisha kurudi kama Mwenyezi Mungu mwenye mwili, ambaye huonyesha ukweli wote ambao humtakasa na kumwokoa wanadamu na ambaye hufanya kazi ya hukumu akianzia na familia ya Mungu, hivyo tunafaa kutambuaje sauti ya Mungu na tunafaa kuthibitishaje kwamba Mwenyezi Mungu ndiye hasa Yesu aliyerudi?

Swali ni la umuhimu mkubwa sana. Kukubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho, na kutazama kuonekana kwa Mungu, lazima tujue jinsi ya kutambua sauti ya Mungu. Kwa Kweli, kutambua sauti ya Mungu kumaanisha kufahamu maneno na matamshi ya Mungu, na kufahamu zile sifa bainifu za maneno ya Muumba. Bila kujali kama maneno ya Mungu aliyepata mwili, au matamshi ya Roho wa Mungu, yote ni maneno yaliyonenwa na Mungu kwa mwanadamu kutoka juu sana. Sauti na sifa bainifu ya maneno ya Mungu ni namna hiyo. Hapa, mamlaka na utambulisho ya Mungu vimebainishwa kwa dhahiri. Hii, inaweza kusemwa, ni njia ya pekee ambayo Muumba hunena. Matamshi ya Mungu kila wakati Yeye huwa mwili bila shaka hufikia maeneo mengi.

9.16.2019

Kwa miaka elfu mbili, imani ya mwanadamu katika Bwana imekuwa imetegemezwa Biblia, na kuja kwa Bwana Yesu hakukuikanusha Biblia ya Agano la Kale. Baada ya Mwenyezi Mungu kufanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho, kila mtu anayemkubali Mwenyezi Mungu atalenga kula na kunywa maneno ya Mwenyezi Mungu na aitasoma Biblia mara chache tena. Kile ninachopenda kufuatilia ni, baada ya mtu kuikubali kazi ya Mwenyezi Mungu katika siku za mwisho, ni mtazamo gani sahihi hasa mtu anafaa kuwa nao kwa Biblia, na mtu anafaa kuitumia kwa jinsi gani? Imani ya mtu katika Mungu inafaa itegemezwe nini ili mtu aitembee njia ya imani katika Mungu na kupata wokovu wa Mungu?

Biblia ni kumbukumbu halisi ya hatua za kwanza mbili za kazi ya Mungu. Kwa maneno mengine, ni ushuhuda wa hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu, ambazo zinahitimisha uongozi na ukombozi wa wanadamu baada ya kuumbwa kwa mbingu na dunia na vitu vyote, pamoja na wanadamu. Kutokana na kuisoma Biblia, kila mmoja anaweza kuona jinsi Mungu aliwaongoza wanadamu wakati wa Enzi ya Sheria na kuwafundisha kuishi mbele Zake na kumwabudu Yeye. Tunaweza kuona pia jinsi Mungu aliwakomboa wanadamu wakati wa Enzi ya Neema na kuwasamehe dhambi zao zote zilizopita huku akiwapa amani, furaha, na kila aina ya neema. Watu hawawezi tu kuona kwamba Mungu alikuwa amewaumba wanadamu, bali pia kwamba Yeye alikuwa amewaongoza kwa uthabiti na halafu akawakomboa.

9.15.2019

Biblia ni ushahidi wa kazi ya Mungu; ni kwa kusoma Biblia pekee ndiyo wale wanaomwamini Bwana wanaweza kutambua kwamba Mungu aliumba mbingu na dunia na vitu vyote na kuona matendo ya ajabu ya Mungu, ukuu Wake na uweza. Katika Biblia kuna maneno mengi ya Mungu na ushuhuda mwingi wa uzoefu wa mwanadamu; inaweza kuyakimu maisha ya mwanadamu na kuwa na manufaa sana kwa mwanadamu, hivyo kile ninachopenda kufuatilia ni, kwa kweli tunaweza kupata uzima wa milele kwa kusoma Biblia? Kweli hakuna njia ya uzima wa milele katika Biblia?

Kupitia kusoma Biblia tunakuja kuelewa kuwa Mungu ni Muumba wa vitu vyote na tunaanza kutambua matendo Yake ya ajabu. Hii ni kwa sababu Biblia ni ushuhuda wa hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu. Ni rekodi ya maneno na kazi ya Mungu na ushuhuda wa mwanadamu katika Enzi ya Sheria na Enzi ya Neema. Kwa hivyo, Biblia ni muhimu sana kwa imani yetu. Fikiria kuihusu, kama sio Biblia, mwanadamu angewezaje kuelewa neno la Bwana na kumjua Bwana? Ni kwa njia nyingine ipi ndiyo mwanadamu angeshuhudia matendo ya Mungu na kuanza kukuza imani ya kweli kwa Mungu? Mwanadamu asiposoma Biblia, ni kwa njia nyingine ipi ataweza kushuhudia ushuhuda wa kweli wa watakatifu wote katika enzi zote wakimtii Mungu? Kwa hivyo, kusoma Biblia ni muhimu kwa utendaji wa imani, na muumini yeyote wa Mungu hafai kupotoka kutoka kwa Biblia. Unaweza kusema, yeyote anayepotoka kutoka kwa Biblia hawezi kuamini katika Bwana.

9.14.2019

Biblia ni kanuni ya Ukristo na wale wanaomwamini Bwana wamefanya hivyo kwa mujibu wa Biblia kwa miaka elfu mbili. Aidha, watu wengi katika ulimwengu wa kidini wanaamini kwamba Biblia inamwakilisha Bwana, imani hiyo katika Bwana ni imani katika Biblia, na imani katika Biblia ni imani katika Bwana, na kwamba mtu akipotea kutoka kwa Biblia basi hawezi kuitwa muumini. Tafadhali hebu niulize kama kumwamini Bwana kwa njia hii au la kunakubaliana na mapenzi ya Bwana?

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki, siku za mwisho

Biblia ni kanuni ya Ukristo na wale wanaomwamini Bwana wamefanya hivyo kwa mujibu wa Biblia kwa miaka elfu mbili. Aidha, watu wengi katika ulimwengu wa kidini wanaamini kwamba Biblia inamwakilisha Bwana, imani hiyo katika Bwana ni imani katika Biblia, na imani katika Biblia ni imani katika Bwana, na kwamba mtu akipotea kutoka kwa Biblia basi hawezi kuitwa muumini. Tafadhali hebu niulize kama kumwamini Bwana kwa njia hii au la kunakubaliana na mapenzi ya Bwana?

Jibu:
Wengi wanaamini kuwa Biblia inamwakilisha Bwana, inamwakilisha Mungu na kwamba imani katika Bwana inamaanisha imani katika Biblia, imani katika Biblia ni sawa na imani katika Bwana. Watu wanaweka hali sawa kwa Biblia kama wanavyofanya kwa Mungu. Kuna pia wale ambao wanatambua Biblia bila kumtambua Mungu. Wanaichukulia Biblia kama kuu, na hata kujitahidi kuifanya Biblia ichukue nafasi ya Mungu. Kuna hata viongozi wa kidini ambao wanatambua Biblia bila kumtambua Kristo, na kudai kuwa wale wanaohubiri kurejea kwa mara ya pili kwa Bwana kuwa waasi wa dini. Ni nini hasa ndio suala hapa? Ni dhahiri, dunia ya kidini imezama hadi kiwango cha kuitambua Biblia pekee na kukosa kuamini katika kurejea kwa Bwana—hakuna kuwaokoa wao.

9.13.2019

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanashikilia maneno ya Paulo katika Biblia: “Andiko lote limetolewa kwa msukumo wa Mungu” (2 Timotheo 3:16), wakiamini kwamba kila kitu katika Biblia ni maneno ya Mungu. Lakini unasema kwamba maneno ya Biblia si maneno ya Mungu kabisa, kwa hiyo haya yote yanamaanisha nini?

Kuanzia, tunahitaji kuelewa jinsi Biblia ilipata umbo, na wakati ilitungwa. Kitabu asili cha Biblia kinahusu Agano la Kale. Waisraeli, yaani, Wayahudi, waliliita Agano la Kale Andiko pekee. Na kisha, katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya hatua ya kazi ya ukombozi. Zaidi ya miaka mia tatu baada ya Bwana, viongozi wa kanisa wa wakati huo walikuja pamoja kufanya mkutano. Waliamini kwamba siku za mwisho zilikuwa zikikaribia na kwamba maneno ambayo Bwana Yesu alikuwa amenena, na nyaraka ambazo wanafunzi walikuwa wameandika, zinapaswa kujumuishwa pamoja kuunda kitabu sawa na Agano la Kale, na kutumiwa makanisa kila mahali.

9.12.2019

Unashuhudia kuwa Bwana Yesu amekwisha kurudi kama Mwenyezi Mungu, kwamba Yeye huonyesha ukweli wote ambao utawawezesha watu kupata utakaso na kuokolewa, na kwamba sasa Anafanya kazi ya hukumu kuanzia na nyumba ya Mungu, lakini hatuthubutu kukubali hili. Hii ni kwa sababu wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa mara nyingi hutufundisha kwamba maneno na kazi zote za Mungu zimeandikwa katika Biblia na hakuwezi kuwa na maneno mengine au kazi ya Mungu nje ya Biblia, na kwamba kila kitu kinachoipinga au kwenda zaidi ya Biblia ni uasi. Hatuwezi kulitambua tatizo hili, kwa hivyo tafadhali unaweza kutueleza kulihusu.

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,maombi

Aina hii ya mtazamo kutoka kwa jamii ya dini haitokani na neno la Mungu; ilikuja hasa kama matokeo ya kufasiriwa vibaya kwa Biblia. Biblia inashuhudia hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu; hii ni kweli. Hata hivyo, kiandikwacho katika Biblia kina mipaka, na ndani yake hamna maneno yote aliyoyanena Mungu katika hizo hatua mbili za kazi Yake na ushuhuda wote kuhusu kazi hiyo. Kutokana na kuachwa maneno na migogoro miongoni mwa wakusanyaji wa Biblia, baadhi ya utabiri wa manabii, uzoefu wa mitume na ushuhuda wao uliachwa nje; huu ni ukweli unaotambuliwa.

9.11.2019

Unashuhudia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu mwenye mwili ambaye kwa sasa anafanya kazi Yake ya hukumu katika siku za mwisho. Lakini wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanasema kwamba kazi ya Mwenyezi Mungu kwa kweli ni kazi ya mwanadamu, na pia watu wengi ambao hawamwamini Bwana Yesu wanasema kuwa Ukristo ni imani katika mtu. Bado hatuwezi kutambua hasa ni nini tofauti kati ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu, hivyo tafadhali shiriki hili kwa ajili yetu.

Kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu bila shaka ni tofauti. Tukichunguza kwa makini sote tutaweza kuliona. Kwa mfano, tukiangalia matamshi na kazi ya Bwana Yesu na kisha tuangalie maneno na kazi ya mitume, tunaweza kusema kuwa tofauti ni wazi kabisa. Kila neno lililotamkwa na Bwana Yesu ni ukweli na lina mamlaka, na linaweza kufunua mafumbo mengi. Haya yote ni mambo ambayo mwanadamu kamwe hawezi kufanya. Hiyo ndio maana kuna watu wengi sana wanaomfuata Bwana Yesu, ilhali kazi ya mitume inaweza tu kueneza injili, kuwa na ushuhuda kwa Mungu, na kutoa kwa kanisa. Matokeo ni machache sana. Tofauti katika ya kazi ya Mungu na kazi ya mwanadamu ni wazi sana. Basi, ni kwa nini watu hawawezi kuitambua? Sababu ni nini? Ni kwa sababu wanadamu wapotovu hawajui Mungu na hawana ukweli wowote.

9.10.2019

Bwana Yesu alisema: “Ila yeyote akunywaye maji ambaye nitampa hatawahi kuwa na kiu; lakini maji hayo ambayo nitampa yatakuwa chemichemi ya maji ambayo yanachipuka katika uhai wa daima” (Yohana 4:14). Watu wengi wanafikiri kwamba Bwana Yesu tayari ametupa njia ya uzima wa milele, lakini nimeyasoma maneno haya ya Mwenyezi Mungu: “Ni Kristo wa Siku za Mwisho Pekee Ndiye Anayeweza Kumpa Mwanadamu Njia ya Uzima wa Milele.” Haya yote yanahusu nini? Kwa nini yanasema kwamba ni Kristo tu wa siku za mwisho anayeweza kumpa mtu njia ya uzima wa milele?

Kuhusu kile njia ya uzima wa milele kilicho kwa kweli, tunapaswa kwanza kujua inapotoka. Sisi sote tunajua kwamba Mungu alipokuwa mwili, Alitoa ushuhuda kwamba Yeye ndiye kweli, njia, na uzima. Huu ni ushahidi wa kutosha kwamba Kristo pekee ndiye Anayeweza kuonyesha njia ya uzima wa milele. Kwa kuwa Kristo ndiye kuonekana kwa Mungu mwenye mwili, kwa kuwa Yeye ndiye Roho wa Mungu aliyejivika mwili, hiyo ina maana kwamba kiini cha Kristo ni kiini cha Mungu, na kwamba Kristo Mwenyewe ndiye kweli, njia, na uzima. Kwa hivyo, Kristo anaweza kuonyesha ukweli na kutekeleza kazi ya kuwakomboa na kuwaokoa wanadamu. Hii ni ya hakika. Bila kujali Mungu anakuwa mwili katika enzi gani, kiini cha Kristo hakiwezi kubadilika kamwe. Bwana Yesu ni Mungu Mwenyewe katika mwili.