9.13.2019

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanashikilia maneno ya Paulo katika Biblia: “Andiko lote limetolewa kwa msukumo wa Mungu” (2 Timotheo 3:16), wakiamini kwamba kila kitu katika Biblia ni maneno ya Mungu. Lakini unasema kwamba maneno ya Biblia si maneno ya Mungu kabisa, kwa hiyo haya yote yanamaanisha nini?

Wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanashikilia maneno ya Paulo katika Biblia: “Andiko lote limetolewa kwa msukumo wa Mungu” (2 Timotheo 3:16), wakiamini kwamba kila kitu katika Biblia ni maneno ya Mungu. Lakini unasema kwamba maneno ya Biblia si maneno ya Mungu kabisa, kwa hiyo haya yote yanamaanisha nini?

Jibu:
Kuanzia, tunahitaji kuelewa jinsi Biblia ilipata umbo, na wakati ilitungwa. Kitabu asili cha Biblia kinahusu Agano la Kale. Waisraeli, yaani, Wayahudi, waliliita Agano la Kale Andiko pekee. Na kisha, katika Enzi ya Neema, Bwana Yesu alifanya hatua ya kazi ya ukombozi. Zaidi ya miaka mia tatu baada ya Bwana, viongozi wa kanisa wa wakati huo walikuja pamoja kufanya mkutano. Waliamini kwamba siku za mwisho zilikuwa zikikaribia na kwamba maneno ambayo Bwana Yesu alikuwa amenena, na nyaraka ambazo wanafunzi walikuwa wameandika, zinapaswa kujumuishwa pamoja kuunda kitabu sawa na Agano la Kale, na kutumiwa makanisa kila mahali. Kwa njia hii maandishi yangehifadhiwa vizuri na maisha ya makanisa yangewekwa kwa njia sahihi. Kwa hivyo, walichambua na kuleta pamoja maandishi yote ya mitume na wanafunzi wa Bwana Yesu na hatimaye, baada ya kufanya utafiti, waliamua uteuzi wa vipande ishirini na saba vya maandishi kuwa sheria rasmi ya Agano Jipya. Kufuatia hiyo waliunganisha kazi ishirini na saba ya sheria rasmi ya Agano Jipya na Agano la Kale kuwa maudhui kamili ya Biblia. Huu ndio msingi wa kutungwa kwa kitabu kizima cha Agano Jipya na Kale. Kuna wengine wanaoamini kwamba andiko lote linatiwa msukumo na Mungu; hasa, Paulo wakati huo alisema: “Andiko lote limetolewa kwa msukumo wa Mungu.” Kuna ukweli kwa maneno haya. Wakati huo ambapo yalisemwa, hakukuwa na Agano Jipya kwa kuwa Agano Jipya halikuwa limekuwa kitabu na bado lilikuwa barua zilizofunguka. Katika aina hii ya usuli, maneno ya Paulo hata hivyo yalikuwa yanahusu nini? Bila shaka, yalikuwa yanahusu Agano la Kale. Kwa hivyo, kauli ya Paulo katika Timotheo 2 kwamba “Andiko lote limetolewa kwa msukumo wa Mungu” inalengwa kwa Agano la Kale kwa sababu Agano Jipya bado halikuwa limekuwa kitabu wakati huo lakini lilikuwa barua kadhaa zilizofunguka katika utunzaji wa kila kanisa. Huu ni ukweli na hivyo kile Paulo alichosema hakika hakihusu Agano Jipya. Hata hivyo, watu wa siku za mwisho walichukua “andiko” aliyozungumzia Paulo kumaanisha maandiko kamili ya Agano la kale na Jipya. Hii inaenda dhidi ya ukweli wakati huo na kuenda kinyume na kile ambacho Paulo alisema wakati huo. Kwa hivyo, haipatani na ukweli na inakuja chini ya ufafanuzi wenye ubaguzi na wenye makosa. Kando na hili, ikisemwa kwamba Agano la Kale limetolewa kwa msukumo wa Mungu, je hili lina maana? Je “kutolewa kwa msukumo na Mungu” kunawakilisha nini? Tunaita nini “kutolewa kwa msukumo”? Katika Enzi ya Sheria ya Agano la Kale, Musa alikuwa kiongozi wa Waisraeli na mhubiri aliyewekwa na Mungu, yaani, mtu aliyewaongoza watu wa Israeli kutoka Misri, na kupitisha sheria za Mungu. Kazi ya Enzi ya Sheria ilifanywa na Mungu kupitia Musa. Musa alikuwa na mamlaka zaidi kueleza Agano la Kale na wengine hawakuwa na sifa hii. Haya, katika Vitabu Vitano vya Musa, je, alisema kwamba kile alichoandika kilitolewa kwa msukumo wa Mungu? Kwanza, Musa hakusema hili; pili, manabii hao wote ambao Mungu alitumia katika enzi ya Agano la Kale, hakuna kati yao wanaonekana kuwa waliongea kwa njia hii. Kwa manabii wakuu zaidi, Isaya, Danieli, na Ezekieli, je, kuna yeyote kati yao alisema maneno haya? La. Sentensi “Kila andiko, limetolewa kwa msukumo wa Mungu” ilisemwa baadaye tu na Paulo, na hivyo haiwezi kuchukuliwa kikamilifu kuwa ushahidi. Iwapo Mungu angesema kwamba Agano la Kale chote kilitolewa kwa msukumo wa Mungu, ingempasa kunena kupitia kwa manabii lakini hili halionekani katika maneno ya manabii. Iwapo Musa angeweza kuchukua mtazamo huu, angesema hivyo, lakini hakuna maneno kama hayo katika kile alichosema Musa. Hii ndiyo aina ya ufahamu ambao tunapaswa kuwa nao kuhusu kutungwa kwa Biblia na muundo wake. Hili linaweza kusemwa kuwa maelezo ya ndani ya Biblia ambayo yanaturuhusu kujua jinsi Biblia iliundwa hata hivyo, nani aliiandika, na nani alifanya rekodi yake. Biblia ilikuwa na waandishi idadi kadhaa ambao walishiriki ufahamu wa pamoja na mtazamo wa pamoja. Ni wangapi kati yao walisema kwamba yote inatolewa kwa msukumo wa Mungu? Ni Paulo pekee. Je, kile ambacho Paulo alisema wakati huo, kwamba andiko lote lilitolewa kwa msukumo wa Mungu, kilifafanuliwaje mamia ya miaka baadaye? Agano la Kale na Jipya yote yanatolewa kwa msukumo wa Mungu. Je, si ufafanuzi kama huo ni usioaminika na usioaminisha?
Baada ya kuonekana kwa Agano Jipya na muungano wake na Agano la Kale, kwa kusoma maneno ya Paulo watu waliamini kwamba “andiko” katika maneno ya Paulo lilijumuisha Agano la Kale na Agano Jipya. Iwapo Paulo bado angekuwa hai, na angesikia maelezo kama hayo na warithi wake, angeanza mara moja kuyabisha. akitamka: “Nilichosema wakati huo kilikuwa kinahusu Agano la Kale, hakikujumuisha Agano Jipya.” Kando na hili, nafasi ya Paulo ingekuwa ipi, au kwa kuongezea wale wote kama Paulo na wengine walioandika nyaraka za Agano Jipya, iwapo wangeona watu katika vikundi vya siku za mwisho wakichukulia nyaraka ambazo walikuwa wameandika kana kwamba zilikuwa neno la Mungu? Je, wangeweza kukubali jambo hili? Wangesema nini? Wangesema: “Ee jamani, haya ni masumbuko. Mmetenda kosa kubwa na mmefanya uasi. Sisi sote ni ndugu, kile ambacho tumesema hakiwakilishi neno la Mungu. Vipofu mlioje, mbona mmechukua maneno yetu kuwa neno la Mungu?” Wangeshangaa, siyo? Paulo na Petro hawakuandika nyaraka mara moja baada ya kupaa kwa Bwana Yesu. Ilikuwa miaka thelathini baada ya Bwana Yesu kupaa ndipo nyaraka zao zilionekana moja baada ya nyingine, na waliandika nyaraka kwa urasmi tu baada ya kuhubiri kwa miaka ishirini au thelathini. Baada ya barua hizi ambazo walikuwa wameandika kutumwa kwa makanisa, je, ndugu katika makanisa walizionaje? Je, wangesema “Aa, hii ni sauti ya Mungu, hili ni neno la Mungu!”? Je, wangesema hili? Wangesema: “Aa, hii ni barua kutoka kwa Ndugu Petro, angalia, anachoandika kwa barua hii ni kizuri kwa kweli, kwa kweli kinarekebisha maadili,” “Aa, hii ni barua kutoka kwa Ndugu Paulo,” “Hii ni barua kutoka kwa Barnaba,” “Hii ni barua kutoka kwa Mathayo.” … Wakati huo je, wengine wangechukulia nyaraka hizi kutoka kwa wanafunzi kuwa neno la Mungu? Asilimia mia moja la, hawangezichukulia hivyo, kwa sababu Petro, Matayo na wale wanafunzi wengine hawakuwahi kusema kwamba walikuwa Mungu, wala hawakuwahi kusema kwamba walikuwa Mungu mwenye mwili. Wote walikubali kwamba walikuwa waumini katika Bwana Yesu, kwamba walikuwa wanafunzi wa Bwana Yesu. Kwa hivyo, ndugu wa makanisa wakati huo pia waliwaona kama ndugu na kuchukulia barua zao na kile walichosema kuwa maneno ya ndugu, mawasiliano ya ndugu, na kushuhudia kwa ndugu, ambayo ni sahihi kabisa na pia yanapatana na usuli wa historia. Hata hivyo, watu leo huchukulia maneno ya wanafunzi hawa kuwa neno la Mungu, na kuyataja hapohapo na neno la Mungu; je, hii si kuenda dhidi ya ukweli wa historia ya wakati huo? Watu leo na macho yao yakiwa yamefunguliwa wazi wanathubutu kuenda dhidi ya ukweli wa historia na kuchukua maneno ya watu hawa kuwa neno la Mungu bila kuhisi wamekosea. Iwapo mtu angefunua ukweli huu, bado wangejitetea, na kutaja maneno ya Biblia katika utetezi wao. Je, kuna msingi wowote wa maneno hayo? Yanahusu nini? Unayaelewa? Kuna maneno kwa maana hii katika barua za wanafunzi: Petro alitaja kwamba maneno, nyaraka, za Ndugu Paulo zilikuwa zimetiwa nuru na Mungu, na Roho Mtakatifu, na zilikuwa na kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini Petro hakusema kwamba maneno ya Paulo yalikuwa neno la Mungu. Petro hakusema kwamba maneno ya Paulo yalitolewa kwa msukumo wa Roho Mtakatifu na kwamba lazima yachukuliwe kuwa neno la Mungu, la sivyo ulikuwa umekosea. Paulo pia hakuthubutu kusema kwamba maneno yake yalifichuliwa na Mungu, kwamba yalitolewa kwa msukumo wa Mungu. Paulo wala Petro hawakuthubutu kutoa ushuhuda kwamba kile walichosema wao wenyewe kilikuwa neno la Mungu, hivyo, waumini katika siku za mwisho wanawezaje kuchukulia maneno yao kama neno la Mungu? Wanatenda kosa lipi? Je, ungesema kwamba wakalimani wa maandiko katika ulimwengu mzima wa dini wameyaelewa sawasawa au la? Kukabili kosa kubwa la upuuzi kama hilo, hawalifahamu, hawalielewi na hawawezi kuliona. Watu hawa wenyewe hawana ukweli na hawawezi kubaini vitu; hata hivyo, watu wengine wanawaabudu kijinga. Imani ya watu katika Mungu ni kuamini mwanadamu bila kufikiri, wataamini chochote watakachoambiwa waamini. Watu wa kidini ni wa ushirikina kuhusu Biblia, wanaiabudu, kuiweka juu ya Mungu, wakifikiri kwamba Biblia inamwakilisha Mungu, na yote yanapaswa kuwa kulingana na Biblia. Wana imani ya ushirikina na ibada kama hiyo kuhusu Biblia. Je hii si tabia ya upuuzi? Watu wanashikiliaje imani ya ushirikina kuhusu Biblia? Wanafanya hivyo wakati hawaitendei kwa mujibu wa ukweli wa historia. Hawafuatilii ukweli kwa kweli na kuitendea Biblia kulingana na nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, lakini badala yake wanaabudu watu mashuhuri kiujinga, na bila kujali nani alisema nini wanachukulia yote kuwa ukweli, na kuyakubali yote, na kuyatumia yote bila kuchagua kwa busara. Je, Paulo alikuwa bila kosa? Kile alichosema kilikuwa sahihi? Alikuwa pia mwanadamu, inawezekanaje mwanadamu kukosa najisi? Kwa hivyo, si makosa kwamba katika Enzi ya Neema watu waliunganisha pamoja barua za wanafunzi na neno la Mungu na kuyafumbana pamoja na neno la Mungu? Maneno ya Mungu katika Biblia ni neno la Mungu, ilhali kile kinachosemwa na mwanadamu ni neno la mwanadamu. Ni maneno yapi katika Biblia ni neno la Mungu? Tunapaswa kuyatambua. Yote ambayo yalisemwa na Yehova Mungu Mwenyewe, kile Yehova Mungu alimwagiza Musa kusema, kile ambacho Yehova Mungu aliwaagiza manabii kusema, kile ambacho manabii waliombwa kuwasilisha, na pia kile Bwana Yesu Mwenyewe alisema, haya pekee ndio neno la kweli la Mungu. Je, umeona kitu katika maneno ya manabii ambacho hasa ni ya ishara? Yanasema “Hivyo alisema Yehova,” “Hii ndiyo Yehova anasema,” hayasemi “Hivyo nasema mimi Danieli (mimi Isaya).” Maneno haya yanaweka wazi kwa watu kwamba manabii walikuwa wakiiga maneno asili ya Mungu. Kwa hivyo, maneno yote asili ya Mungu ambayo yaliwasilishwa na manabii ni neno la kweli la Mungu, yote ambayo yalirekodiwa kuwa yalisemwa na Yehova Mungu Mwenyewe ni neno la kweli la Mungu, yote ambayo yalirekodiwa na wanafunzi kuwa yalisemwa na Bwana Yesu Mwenyewe ni neno la Mungu. Kuna sehemu moja tu ya Biblia ambayo ni neno la kweli la Mungu na kando na hiyo, kila kitu walichosema wanafunzi na vitu ambavyo watumishi wa Mungu walirekodi ni kushuhudia kwa wanadamu. Punde tu tunapozungumza kuhusu kushuhudia kwa wanadamu, kuna shida. Wakati mwingine kile wanachosema si kamili, si thabiti, kinakosa vitu; kwa hivyo, katika kazi Yake ya siku za mwisho Mungu anasema kwamba wakati huo kulikuwa na ukweli wa aina hii, na ilikuwa hivyo wakati huo, na lazima Afanye nyongeza fulani. Kwa mfano, hali za Paulo zilikuwa hivi na vile, hali za Petro zilikuwa hivi na vile; Mungu huongeza hizi kaika kazi Yake ya siku za mwisho. Kwa hivyo, tunaweza kuona kutoka kwa hili kwamba chochote ambacho mwanadamu amesema hakifuatani kikamilifu na usuli wenye kweli. Mungu anafichua suala hili katika kazi Yake ya siku za mwisho.
kutoka katika Ushirika kutoka kwa Aliye Juu
Kwa sababu katika nyaraka Paulo alisema wakati mmoja kwamba kila andiko limetolewa kwa kutiwa msukumo na Mungu, baadaye, jamii za dini zilianza kukiwekea mipaka kila kitu kiandikwacho katika Biblia kama kilichotolewa kwa kutiwa msukumo na Mungu, na kilicho maneno ya Mungu. Alichokisema Paulo hakikuwa na msingi, kwa sababu Mungu hakuishuhudia Biblia kwa njia hii kamwe, wala Bwana Yesu hakusema kamwe kwamba Biblia ilitolewa kwa kutiwa msukumo na yake Mungu na ilikuwa neno la Mungu hasa. Ushuhuda wa Paulo kuhusu Biblia ulitegemea tu maarifa yake binafsi juu ya Biblia; hakuwa akizungumza hasa kwa niaba ya Mungu. Roho Mtakatifu na Mungu mwenye mwili pekee ndio wanajua siri ya kile Biblia inahusu, na wanadamu wenye kuumbwa hawajaweza kuifahamu kabisa. Huu ni ukweli. Bwana Yesu alisema tu kwamba Biblia ni ushuhuda wa Mungu; Hakusema yote iliongozwa kwa pumzi yake Mungu na ilikuwa neno la Mungu. Wala Roho Mtakatifu hakutoa kamwe ushuhuda kama huo wa Biblia kwa mtu yeyote. Hivyo, alichokisema Paulo hakikuwa na msingi. Hakuwa akizungumza kwa niaba ya Mungu, sembuse Roho Mtakatifu. Yaliyomo ndani ya Biblia yote ni kumbukumbu za matukio halisi na ushuhuda wa uzoefu unaohusiana na kazi ya Mungu, zilizoandikwa na watu waliomhudumia Yeye. Hakuna sura yoyote iliyoandikwa na Mungu Mwenyewe; waandishi wake walikuwa hasa wakiliwasilisha neno la Mungu au wakiuelezea uzoefu na ufahamu wao wenyewe, wakipewa nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu, ili kushuhudia jina na kazi ya Mungu. Huu ni ukweli. Ingawa matukio ya mitume yaliyoandikwa na nyaraka zilipewa nuru na Roho Mtakatifu, haziwakilishi neno la Mungu, kwa sababu Roho Mtakatifu anamwangaza, Anampa nuru, na kumwongoza kila mtu kulingana na hali yake binafsi ili aweze kuufikia ufahamu wa ukweli na kupata maarifa ya Mungu. Haya ndiyo matokeo ya kazi ya Roho Mtakatifu. Hivyo, kupata nuru na mwangaza huu unaoletwa na kazi ya Roho Mtakatifu haulingani na neno la Mungu; matamshi ya Mungu yanawakilisha tabia ya maisha ya Mungu na yote yanabeba asili ya ukweli wa tabia ya maisha Yake. Hakuna sentensi itamkwayo na Mungu inayoweza kupitiwa na wanadamu kabisa, kwa sababu matamshi Yake yana asili ipitayo kiasi ya ukweli kwetu ili kuishi kwa kudhihirisha ndani ya uzoefu wenye mipaka ya maisha ya mara moja tu. Kwa sababu hii, haidhuru watu wanavyoufahamu ukweli au wanavyomjua Mungu, hawataweza kuonyesha neno Lake kamwe. Inavyoonekana, kupata nuru na mwangaza wa Roho Mtakatifu unawapa tu wanadamu nuru na mwongozo fulani ambao kupitia huo wanaufahamu ukweli; licha ya jinsi uzoefu na ushuhuda wao unavyoweza kuwa mwingi, haya hayapaswi hata kutajwa papo hapo na matamshi ya Mungu. Kwa sababu asili ya wanadamu na asili ya Mungu ni tofauti kama usiku na mchana, wanadamu hawataweza kulionyesha neno la Mungu kamwe; Kristo pekee aliyepewa asili ya utakatifu wa Mungu ndiye Anayeweza kufanya hivyo. Manabii wanaweza tu kuliwasilisha neno la Mungu; hata watu ambao wanatumiwa na Roho Mtakatifu wanaweza tu kuuzungumzia uzoefu na kile wao wenyewe wamekishuhudia. Wanadamu wanaweza tu kuelezea kulingana na asili yao, kuishi kwao kulingana na, kwa zamu, kunaamua ushuhuda wao. Mungu anamiliki asili ya utakatifu, hivyo, kwa kawaida Analionyesha neno Lake; sisi binadamu tuna asili yetu ya utu, hivyo kile tunachokionyesha ni kwa kawaida kimetegemezwa kwa uzoefu wetu na kile ambacho tumekishuhudia. Hii ikiwa hali, mbali na sehemu zinazowasilishwa na wanadamu ambazo ni neno la Mungu, bila shaka mengineyo ni masimulizi ya uzoefu na ufahamu wa wanadamu. Ingawa haya yanaweza kukubaliana na ukweli, hayawezi kabisa kulinganishwa na neno la Mungu, kwa kuwa asili ya wanadamu ni tofauti sana na ile ya Mungu. Kwa hiyo, tunapoisoma Biblia, tunapaswa kutofautisha dhahiri kati ya sehemu zilizo na neno la Mungu na zile zinazosemwa na wanadamu. Ni katika njia hii tu ndipo tunapoweza kuishughulikia Biblia ifaavyo na kwa njia ambayo inapatana na mapenzi ya Mungu. Isitoshe, jamii ya dini inapodai kwamba kila kitu kiandikwacho ndani ya Biblia ni neno la Mungu, hili halipatani na ukweli wa historia wa wakati. Kwa mfano, katika Enzi ya Neema, Roho Mtakatifu hajatoa ushuhuda kamwe Akisema kwamba nyaraka na ushuhuda ulioandikwa na mitume ni andiko lililotolewa kwa kutiwa msukumo na Mungu. Aidha, mitume wenyewe hawakusema kamwe kwamba kile walichokiandika kilitolewa kwa kutiwa msukumo na Mungu; wala hawangethubutu kudai kwamba kilikuwa neno la Mungu halisi. Nyaraka zilizotumwa kwa makanisa wakati huo zote zilionekana kuwa nyaraka zilizoandikwa na ndugu wa kimitume; hakuna yeyote hasa aliyesema kwamba, zilikuwa neno la Mungu lililotolewa kwa pumzi yake Mungu. Huu ulikuwa ukweli wakati huo. Je, si ukweli tena siku hizi? Sasa, katika siku za mwisho, watu wanaosisitiza kwamba nyaraka ni neno la Mungu wanaenda kinyume cha ukweli wa historia! Katika Enzi ya Sheria, watumishi na manabii wa Mungu hawakusema kwamba maneno yao yalikuwa maandiko yaliyotolewa kwa kutiwa msukumo na Mungu, wala kwamba yalikuwa neno la Mungu. Kuhusu vitabu walivyoviandika, bila shaka huenda Waisraeli wa wakati huo wangekuwa wameviona kama vilivyoandikwa na watumishi wa Mungu au manabii. Kando na hayo maneno ya Mungu waliyoyawasilisha, mengineyo yangeweza kuainishwa kama kumbukumbu za kazi ya Mungu. Kama Waisraeli hawakushuhudia kamwe kwamba vitabu vilivyoandikwa na watumishi na manabii hawa vyote vilikuwa maandiko yaliyotolewa kwa kutiwa msukumo na Mungu na matamshi, basi wanadamu wanaoishi miaka elfu mbili baadaye wanawezaje kwenda kinyume cha ukweli wa historia wa wakati huo? Watu wanawezaje kusisitiza waziwazi kwamba maneno ya Biblia yaliyoandikwa na wanadamu hakika ni neno la Mungu halisi? Hii si kwa mujibu wa ukweli wa historia! Ushirikina na uabudu sanamu ambayo kwa hayo watu katika siku za mwisho wanaiona Biblia yanafahamika hasa kutoka kwa dhana na mawazo ya wanadamu; hayana msingi kabisa katika neno la Mungu. Desturi hii miongoni mwa jamii ya dini ya kuifuata Biblia bila kufikiria ni ya kupotosha, na inampinga Mungu. Hivi ndivyo nguvu ya mpinga Kristo huwapotosha na kuwatatanisha watu kujiunga na ushirikina na ibada za uongo za Biblia. Hili limesababisha madhehebu mengi kuundwa tayari, yakiyaingiza maisha ya kanisa na kuingia kwa watu katika ghasia na kusababisha matokeo mengi hasi. Kuhusu jambo hili, watu wote wanapaswa kutafakari kujihusu, kutambua kinachoendelea, na kutafuta ukweli ili kulitatua tatizo hili na kuepuka kupotoka kutoka kwa njia sahihi.
kutoka katika “Wale Ambao Hawawezi Kumjua Kristo kama Ukweli, Njia na Uzima Hawataingia Kamwe Katika Ufalme wa Mbinguni” katika Mkusanyiko wa Mahubiri—Ruzuku ya Maisha
Wengi wa ulimwengu wa kidini wanategemea maneno ya Paulo kuwa “Andiko lote limetolewa kwa msukumo wa Mungu” (2 Timotheo 3:16), kwa kubainisha kuwa kila kitu katika Biblia ni neno la Mungu, na kuwa mradi tu mtu ashikilie Biblia atachukuliwa juu katika ufalme wa mbinguni. Hasa katika siku za mwisho, waumini wengi katika Bwana bado wanaamini katika hili. Lakini wazo hili linapatana na ukweli? Je, Bwana Yesu aliwahi kusema “Andiko lote limetolewa kwa msukumo wa Mungu”? Je, Roho Mtakatifu alisema hili? Hapana! Hili lilisemwa na Paulo. Waumini wengi wanatumia maneno haya kutoka kwa Paulo kama msingi wa imani yao kuwa kila neno katika Biblia lilifunuliwa na Mungu na ni neno la Mungu. Je, si hilo ni kosa kubwa? Watu wengine pia wanaamini kuwa hata kama limezungumzwa na mwanadamu, ni neno la Mungu mradi tu limerekodiwa katika Biblia. Je, si maoni kama hayo ni ya uongo na ya upumbavu? Waumini katika Bwana wanapaswa wote kuwa wazi kabisa kuwa Biblia ni ushuhuda wa Mungu tu na kumbukumbu inayohifadhi kazi ya Mungu. Uumbaji wa Biblia uliwekwa kimsingi na kazi ya Mungu ya wokovu wa mwanadamu. Kila hatua ya kazi ya Mungu imejaa vita kati ya Mungu na nguvu za uovu wa Shetani, hiyo ndiyo maana neno la Mungu sio kitu pekee kilichorekodiwa katika Biblia, kwa kuwa kuna maneno pia kutoka watu mbalimbali na hata Shetani. Huu ni ukweli wazi. Je, ni hoja iliyo na utetezi kusema kuwa kila neno la Biblia ni neno la Mungu? Si hii ni kupotosha ukweli na kuchanganya nyeusi na nyeupe? Watu wanawezaje kukuza bado imani yenye makosa kama hii? Mbona wasiongee kulingana na ukweli? Yeyote ambaye amesoma Biblia anajua kuwa Biblia iko na mazungumzo kati ya Mungu na Musa, kati ya Mungu na Ayubu, kati ya Mungu na wateule Wake, na kati ya Mungu na Shetani. Basi maneno yaliyozungumzwa na mtu ambaye Mungu anazungumza naye litakuwa neno la Mungu? Si huo ni upumbavu sana? Kwa hivyo, msemo kuwa “Kila andiko, limetolewa kwa msukumo wa Mungu na ni neno la Mungu” hauwezi kwa urahisi kuwa na utetezi! Watu wengine wapumbavu wamesisitiza kiholela kuwa neno la mwanadamu katika Biblia ni neno la Mungu. Hili linakinzana na ukweli kabisa. Hii linampaka Mungu doa kabisa, kukufuru Mungu, na kwa uzito linaikasirisha tabia ya Mungu! Maneno ya Mungu ni maneno ya Mungu, maneno ya mwanadamu ni maneno ya mwanadamu, na maneno ya Shetani ni maneno ya Shetani. Mbona watu huyachanganya? Maneno ya Mungu daima yatakuwa ndiyo ukweli. Maneno ya mwanadamu hayawezi kuwa ukweli kamwe na sanasana yanaweza tu kufuata ukweli. Maneno ya Shetani daima yatakuwa udanganyifu na uongo. Hata yakitamkwa mara elfu kumi, bado yatakuwa uongo na udanganyifu! Watu wenye hekima wanapaswa kukubali ukweli huu. Ni watu wapumbavu tu ndio watashikilia mitazamo ya uongo.
Tutakuwa dhahiri hata zaidi katika suala hili baada ya kukisoma kifungu kingine cha maneno ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu anasema, “Leo, watu wanaamini kwamba Biblia ni Mungu, na kwamba Mungu ni Biblia. Na hivyo pia, wanaamini kwamba maneno yote ya Biblia ni maneno pekee ambayo Mungu alizungumza, na kwamba yote yalizungumzwa na Mungu. Wale wanaomwamini Mungu hata wanafikia hatua ya kufikiri kwamba ingawa vitabu vyote sitini na sita vya Agano la Kale na Agano Jipya viliandikwa na watu, vyote viliandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na ni rekodi ya matamshi ya Roho Mtakatifu. Hii ni tafsiri ya watu yenye makosa, na haiafikiani kabisa na kweli. Kimsingi, mbali na vitabu vya unabii, sehemu kubwa ya Agano la Kale ni rekodi ya kihistoria. Baadhi ya nyaraka za Agano Jipya zinatokana na uzoefu wa watu, na baadhi zinatokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu; nyaraka za Paulo, kwa mfano, zilitokana na kazi ya mwanadamu, zote zilitokana na kupatiwa nuru na Roho Mtakatifu, na ziliandikwa kwa ajili ya makanisa, yalikuwa ni maneno ya kushawishi na kutia moyo kwa kaka na dada wa makanisa. Hayakuwa maneno yaliyozungumzwa na Roho Mtakatifu—Paulo asingeweza kuzungumza kwa niaba ya Roho Mtakatifu, na wala hakuwa nabii, sembuse kuona maono ambayo Yohana aliona. Nyaraka zake ziliandikwa kwa ajili ya makanisa ya Efeso, Filadefia, Galatia, na makanisa mengineyo. Na hivyo, nyaraka za Paulo za Agano Jipya ni nyaraka ambazo Paulo aliandika kwa ajili ya makanisa, na sio uvuvio wa Roho Mtakatifu, wala sio matamshi ya moja kwa moja ya Roho Mtakatifu. … Ikiwa watu wanaona nyaraka au maneno kama ya Paulo kama matamshi ya Roho Mtakatifu, na kuwaabudu kama Mungu, basi inaweza kusemwa tu kuwa ni watu wasiochagua kwa busara. Tukisema kwa ukali zaidi, haya sio makufuru? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu? Na inawezekanaje watu wapigie magoti rekodi za nyaraka zake na maneno aliyoyazungumza kana kwamba yalikuwa ni kitabu kitakatifu, au kitabu cha mbinguni? Je, inawezekana maneno ya Mungu kutamkwa kwa kawaida na mwanadamu? Inawezekanaje mwanadamu azungumze kwa niaba ya Mungu?” (“Kuhusu Biblia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Si kila kitu katika Biblia ni rekodi ya maneno aliyoyasema Mungu. Kimsingi Biblia inaandika hatua mbili za awali za kazi ya Mungu, ambapo sehemu moja ni rekodi ya utabiri wa kale wa manabii, na sehemu nyingine ni uzoefu na maarifa yaliyoandikwa na watu waliotumiwa na Mungu katika enzi zote. Uzoefu wa kibinadamu umetiwa doa na maoni na maarifa ya kibinadamu, kitu ambacho hakiepukiki. Katika vitabu vingi vya Biblia kuna dhana nyingi za kibinadamu, upendelevu wa binadamu, na ufasiri wa ajabu wa binadamu. Ni kweli, maneno mengi ni matokeo ya kupatiwa nuru na kuangaziwa na Roho Mtakatifu, na ni tafsiri sahihi—lakini haiwezi kusemwa kuwa ni udhihirishaji sahihi kabisa wa ukweli” (“Kuhusu Biblia (3)” katika Neno Laonekana katika Mwili).
Baada ya kusoma maneno ya Mwenyezi Mungu, wote tunaweza kuona Biblia haijatolewa kabisa kwa ufunuo wa Mungu, yote sio neno la Mungu. Na kuhusu sehemu zipi za Biblia ni neno la Mungu na zipi ni maneno ya binadamu, wale walio na jicho la kutambua wanaweza kutambua mara moja. Kwani jina la mwandishi limeandikwa kwa uwazi kwa kila maandiko ya Biblia, na pia imeandikwa kwa uwazi sehemu zipi za Biblia zina maneno ya Mungu. Hivyo itakuwaje kwamba bila kufumba jicho, watu wanaendelea kuchukua maneno ya mwanadamu na ya Shetani kama yale ya Mungu? Je, hii ni njia ya haki ya kunena? Kama waumini wa Bwana wanasisitiza kudai kuwa maneno ya binadamu yalivyo katika Biblia ni kwa kweli maneno ya Mungu, mnafikiria Mungu atahisi vipi? Je, hii ni haki kwa Mungu? Je, huku sio kumkashifu, kumdunisha na kumkufuru Mungu? Uzito wa neno la mwanadamu katika macho ya Mungu ni upi? Mbona tusichukue muda kufikiria? Neno la mwanadamu litaweza kulingana na lile la Mungu vipi? Kiini cha mwanadamu na kile cha Mungu vina tofauti kubwa, kwa hivyo kwa hakika maneno ya mwanadamu na yale ya Mungu yanatengana hata zaidi. Kama, kwa kupitia kupata nuru na kuangaza kwa Roho Mtakatifu, neno la mwanadamu linaweza kulingana na ukweli, haya tayari ni mafanikio makubwa. Kama neno la mwanadamu halielekezwi na kazi ya Roho Mtakatifu, je sio udanganyifu na uongo? Kama waumini wa Mungu hawawezi kuona haya, basi nasikitika hao ni wajinga na wapumbavu sana! Siku hizi, dunia nzima ya kidini inachukua maneno ya binadamu katika Biblia kama yale ya Mungu. Hii inaonyesha kuwa hakuna yeyote katika dunia ya kidini anayemjua Mungu kweli. Viongozi wengi wa dunia ya kidini ni Mafarisayo wanafiki. Wale wanaomjua Mungu kwa kweli hawawezi kamwe kuamini kuwa Biblia yote inatolewa kwa ufunuo wa Mungu na yote ni neno la Mungu. Kwa hakika hawawezi kuabudu kwa upofu Biblia na hata kuichukulia Biblia kama Mungu. Imeshikiliwa kwa upana katika dunia ya kidini kuwa Biblia yote ilitolewa kwa ufunuo wa Mungu na ni neno la Mungu, na kwamba Biblia inaweza kumwakilisha Mungu. Hili ni wazo la uwongo wa kipumbavu sana katika dunia yote ya kidini. Sasa tunaweza naona hili wazi.
kutoka katika Maswali na Majibu Bora zaidi Kuhusu Injili ya Ufalme

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni