Bwana Yesu alikuwa Mungu mwenye mwili na hakuna yeyote anaweza kukanusha hili. Sasa unashuhudia kwamba Mwenyezi Mungu ni Bwana Yesu aliyerudi katika mwili, lakini wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa wanasema kuwa kile unachoamini ni mtu tu, wanasema kuwa umedanganywa, na hatuwezi kulielewa jambo hili. Wakati huo Bwana Yesu alipokuwa mwili na kuja kufanya kazi ya ukombozi, Mafarisayo Wayahudi pia walisema kuwa Bwana Yesu alikuwa mtu tu, wakisema kwamba mtu yeyote aliyemwamini Yeye alikuwa akidanganywa. Kwa hiyo, tungependa kufuatilia kipengele hiki cha ukweli kuhusu kupata mwili. Kupata mwili ni nini hasa? Na ni nini asili ya kupata mwili? Tafadhali shiriki hili kwa ajili yetu.
Jibu:
Imani yenu katika Bwana Yesu kama kupata mwili kwa Mungu si uwongo. Lakini mbona mnamwamini Bwana Yesu? Je, kweli mnamfikiria Bwana Yesu kuwa ni Mungu? Mnamwamini Bwana Yesu kwa sababu ya kile kilichorekodiwa katika Biblia na kwa sababu ya kazi ya Roho Mtakatifu. Lakini haijalishi mnachosema, ikiwa hamjamwona Bwana Yesu uso kwa uso, je, mwaweza kuthubutu kusema kwamba mnamjua Bwana Yesu? Katika imani yenu kwa Bwana, mnarudia tu maneno ya Petro, aliyesema kwamba Bwana Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu aishiye, lakini je, mnaamini kwamba Bwana Yesu ni dhihirisho la Mungu, ni Mungu Mwenyewe? Mnathubutu kusema kwamba mnatambua kiini kitakatifu cha Bwana Yesu? Mnathubutu kuahidi kwamba kama Bwana Yesu angekuja tena akionyesha ukweli, mngetambua sauti Yake? Imani yenu kwa Bwana Yesu si chochote ila imani katika maneno haya mawili “Bwana Yesu.”