8.19.2019

Unyakuo ni lazima utegemezwe maneno ya Mungu na sio dhana na mawazo ya mwanadamu

Kanisa la Mwenyezi Mungu,Umeme wa Mashariki,Biblia

XX. Ni Lazima Mtu Ashiriki kwa Dhahiri Unyakuo ni nini na Maana Halisi ya Kuinuliwa Mbele ya Kiti cha Enzi cha Mungu

Unyakuo ni lazima utegemezwe maneno ya Mungu na sio dhana na mawazo ya mwanadamu

Aya za Biblia za Kurejelea:
Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako ufike, Mapenzi yako yafanywe duniani, kama ilivyo mbinguni” (Mathayo 6:9-10).
Na mimi Yohana nikauona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukija chini kutoka kwa Mungu mbinguni…. Tazama, hema takatifu la Mungu liko pamoja nao watu, na yeye atakaa pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Na yeye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao, na kuwa Mungu wao” (Ufunuo 21:2-3).
Falme za ulimwengu zimekuwa falme za Bwana wetu, na za Kristo wake; na yeye atatawala milele na milele” (Ufunuo 11:15).
Na hakuna mwanadamu amepaa hadi mbinguni, isipokuwa yeye ambaye alishuka chini kutoka mbinguni, ambaye ni Mwana wa Adamu aliye mbinguni” (Yohana 3:13).
Maneno Husika ya Mungu:
“Kunyakuliwa” si kuchukuliwa kutoka mahali pa chini kwenda mahali pa juu jinsi watu wanavyofikiria. Hili ni kosa kubwa sana. Kunyakuliwa kunarejelea kujaaliwa Kwangu na kuchagua. Kunawalenga wale wote ambao Nimewaamua kabla na kuwachagua. … Hili halilingani kabisa na mawazo ya watu. Wale walio na sehemu katika nyumba Yangu katika siku zijazo wote ni watu ambao wamenyakuliwa mbele Yangu. Hii ni kweli kabisa, haibadiliki kamwe, na haiwezi kukataliwa na mtu yeyote. Hili ni jibu la mapigo dhidi ya Shetani. Mtu yeyote Niliyemwamua kabla atanyakuliwa mbele Yangu.
kutoka katika “Sura ya 104” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili
Kuingia rahani hakumaanishi kwamba mambo yote yatakoma kusonga, ama kwamba mambo yote yatakoma kuendelea, wala hakumaanishi kwamba Mungu atakoma kufanya kazi ama mwanadamu atakoma kuishi. Ishara ya kuingia rahani ni kama hii: Shetani ameangamizwa; wale watu waovu wanaomuunga mkono Shetani kwa kufanya maovu wameadhibiwa na kuondolewa; nguvu zote za uhasama kwa Mungu zimekoma kuwepo. Mungu kuingia rahani kunamaanisha kwamba Hatafanya tena kazi Yake ya wokovu wa binadamu. Binadamu kuingia rahani kunamaanisha kwamba binadamu wote wataishi ndani ya mwangaza wa Mungu na chini ya baraka Zake; hakutakuwa na upotovu wowote wa Shetani, wala maovu yoyote kutokea. Binadamu wataishi kama kawaida duniani, na wataishi chini ya ulinzi wa Mungu. Mungu na mwanadamu waingiapo rahani pamoja, kutamaanisha kwamba binadamu wameokolewa na kwamba Shetani ameangamizwa, kwamba kazi ya Mungu miongoni mwa mwanadamu imemalizika kabisa. Mungu hataendelea tena kufanya kazi miongoni mwa mwanadamu, na mwanadamu hataendelea tena kumilikiwa na Shetani. Kwa hivyo, Mungu hatakuwa shughulini tena, na mwanadamu hatakimbiakimbia tena; Mungu na mwanadamu wataingia rahani wakati huo huo. Mungu atarudia nafasi yake ya awali, na kila mtu atarudia nafasi yake husika. Hizi ndizo hatima ambazo Mungu na mwanadamu wataishi ndani kwa utaratibu huu baada ya mwisho wa usimamizi wote wa Mungu. Mungu ana hatima ya Mungu na mwanadamu ana hatima ya mwanadamu. Apumzikapo, Mungu ataendelea kuwaongoza binadamu wote kwa maisha yao duniani. Akiwa kwa mwangaza wa Mungu, mwanadamu atamwabudu Mungu wa kweli aliye mbinguni. … Binadamu wanapoingia rahani, kunamaanisha kwamba mwanadamu amekuwa kiumbe halisi; binadamu watamwabudu Mungu wakiwa duniani na kuwa na maisha ya kawaida ya wanadamu. Watu hawatakuwa tena wasiomtii Mungu ama kumpinga Mungu; watarudia maisha asili ya Adamu na Hawa. Haya ndiyo maisha na hatima binafsi ya Mungu na binadamu baada ya kuingia rahani. Kushindwa kwa Shetani ni mwelekeo usioepukika katika vita kati ya Mungu na Shetani. Kwa njia hii, kuingia kwa Mungu rahani baada ya kukamilika kwa kazi Yake ya usimamizi na wokovu kamili wa mwanadamu na kuingia rahani pia kunakuwa mielekeo isiyoepukika. Pahali pa pumziko pa mwanadamu ni duniani, na pahali pa Mungu pa pumziko ni mbinguni. Wakati mwanadamu anamwabudu Mungu katika pumziko, ataishi duniani, na wakati Mungu anaongoza sehemu iliyobaki ya binadamu katika pumziko…. Baada ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, Shetani hatakuweko tena, na kama Shetani, wale watu waovu pia hawatakuweko tena. Kabla ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani, wale watu waovu waliomtesa Mungu wakati mmoja duniani na adui waliokuwa hawamtii duniani watakuwa tayari wameangamizwa; watakuwa wameangamizwa na majanga makubwa ya siku za mwisho. Baada ya hao watu waovu kuangamizwa kabisa, dunia haitajua tena unyanyasaji wa Shetani. Binadamu watapata wokovu kamili, na hapo tu ndipo kazi ya Mungu itaisha kabisa. Haya ndiyo masharti ya Mungu na mwanadamu kuingia rahani.
kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Mungu aliumba binadamu na Akawaweka duniani, ambao Amewaongoza mpaka siku ya leo. Kisha Akaokoa binadamu na kuhudumu kama sadaka ya dhambi kwa binadamu. Mwishowe lazima bado ashinde binadamu, aokoe binadamu kabisa na kuwarejesha kwa mfano wao wa awali. Hii ndiyo kazi Amekuwa akifanya kutoka mwanzo hadi mwisho—kurejesha mwanadamu kwa sura yake halisi na kwa mfano wake wa awali. Ataanzisha ufalme Wake na kurejesha mfano wa awali wa mwanadamu, kumaanisha kwamba Atarejesha mamlaka Yake duniani na kurejesha mamlaka Yake miongoni mwa viumbe vyote. … Kurudisha mamlaka Yake kunamaanisha kumfanya mwanadamu amwabudu na kumfanya mwanadamu amtii; kunamaanisha kwamba Atamfanya mwanadamu aishi kwa sababu Yake na kufanya adui zake waangamie kwa sababu ya mamlaka Yake; kunamaanisha kwamba Atafanya kila sehemu Yake kuendelea miongoni mwa binadamu na bila upinzani wowote wa mwanadamu. Ufalme Anaotaka kuanzisha ni ufalme Wake Mwenyewe. Binadamu Anaotaka ni wale wanaomwabudu, wale wanaomtii kabisa na wana utukufu Wake. Asipookoa binadamu wapotovu, maana ya uumbaji Wake wa mwanadamu hautakuwa chochote; Hatakuwa na mamlaka yoyote miongoni mwa mwanadamu, na ufalme Wake hautaweza kuweko tena duniani. Asipoangamiza wale adui wasiomtii, Hataweza kupata utukufu Wake wote, wala Hataweza kuanzisha ufalme Wake duniani. Hizi ndizo ishara za ukamilishaji wa kazi Yake na ishara za ukamilishaji wa utimilifu Wake mkubwa; kuangamiza kabisa wale miongoni mwa binadamu wasiomtii, na kuwaleta wale waliokamilika rahani. Wakati binadamu wamerejeshwa katika mfano wake wa awali, wakati binadamu wanaweza kutimiza kazi yao husika, kuwa na nafasi zao wenyewe na kutii mipango yote ya Mungu, Mungu atakuwa amepata kundi la watu duniani wanaomwabudu, na Atakuwa pia Ameanzisha ufalme duniani unaomwabudu. Atakuwa na ushindi wa milele duniani, na wale wanaompinga wataangamia milele. Hii itarejesha nia Yake ya asili ya kumuumba mwanadamu; itarejesha nia Yake ya kuumba vitu vyote, na pia itarejesha mamlaka Yake duniani, mamlaka Yake miongoni mwa vitu vyote na mamlaka yake miongoni mwa adui Zake. Hizi ni ishara za ushindi Wake wote. Tangu sasa na kwendelea binadamu wataingia katika raha na kuingia katika maisha yafuatayo njia sahihi. Mungu pia ataingia katika raha ya milele na mwanadamu na kuingia katika maisha ya milele yanayoshirikisha Mungu na mwanadamu. Uchafu na kutotii duniani vitatoweka, na pia maombolezo duniani. Wote walio duniani wanaompinga Mungu hawatakuweko. Mungu na wale Aliowaokoa pekee ndio watabaki; viumbe Wake tu ndio watabaki.
kutoka katika “Mungu na Mwanadamu Wataingia Rahani Pamoja” katika Neno Laonekana katika Mwili
Wanadamu, wakitawaliwa na tabia yao ya kishetani, wanahodhi tamaa na hamu kiasi ndani yao, ambayo imejificha ndani ya ubinadamu wao. Yaani, wanadamu hawataki kamwe kubaki ardhini; wanashinda wakitaka kupaa hewani. Je, hewani ni mahali pa mtu kuishi? Huko ni mahali pa Shetani, sio mahali pa wanadamu. Wakati wa kuumba wanadamu, Mungu aliwaweka ardhini ili maisha yako ya kila siku yaweze kuwa ya kawaida na mitindo ya maisha yako iwe yenye nidhamu, na ili uweze kujifunza ujuzi wa kawaida kuhusu jinsi ya kuwa binadamu, na kujifunza jinsi ya kuishi maisha yako na jinsi ya kumwabudu Mungu. Mungu hakukupa mabawa; Hakukuruhusu ukae juu angani. Wale walio na mabawa ni ndege, na wale wanaozurura kote hewani ni Shetani na roho wabaya na pepo wachafu. Wao sio wanadamu!
kutoka katika “Masharti Matano Ambayo Watu Wanayo Kabla ya Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Kumwamini Mungu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

  Masomo yanayohusiana Asili na Maendeleo ya Kanisa la Mwenyezi Mungu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni