10.31.2019

Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani



Wimbo wa Kwaya ya Injili | “Wimbo wa Ufalme: Ufalme Washuka Duniani” | Wimbo wa Kusifu na Kuabudu



Wimbo wa kusisimua wa ufalme umevuma, ukitangazia ulimwengu wote kuwasili kwa Mungu kati ya mwanadamu! Ufalme wa Mungu umefika! Watu wote washangilia, vitu vyote vyafurahi! Kila kitu mbinguni kote kina furaha tele. Mandhari haya yanayopendeza mno ya shangwe ni yapi?

10.30.2019

Ufalme wa Kristo Unapatikana Miongoni mwa Wanadamu



I

Mwenyezi Mungu mwenye mwili

Anaonekana katika siku za mwisho Mashariki,

kama tu vile jua la haki likichomoza;

mwanadamu ameona mwanga wa kweli ukionekana.

Mungu wa haki na mwenye uadhama, mwenye upendo na huruma

Anajificha kwa unyenyekevu miongoni mwa wanadamu,

Akitoa ukweli, kuzungumza na kufanya kazi.

10.28.2019

Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu



 Wimbo Mpya wa Kusifu na Kuabudu 2019 | “Jinsi Upendo wa Mungu kwa Mwanadamu Ulivyo Muhimu” | MV

Mandhari iliyochorwa katika Biblia “Amri ya Mungu kwa Adamu”
ni ya kugusa na yenye kutia moyo.
Ingawa hiyo picha ina Mungu na mtu tu,
uhusiano kati ya hao wawili ni wa ndani sana tunaanza kuhisi mshangao.

Wanawali wenye hekima ni nini? Wanawali wapumbavu ni nini?

 
    Maneno Husika ya Mungu:
    Zamani, watu wengine wamefanya utabiri kuhusu “mabikira watano wenye busara, mabikira watano wapumbavu”; ingawa utabiri huo si sahihi, si wenye makosa kabisa, kwa hiyo Naweza kuwapa ninyi maelezo fulani. Mabikira watano wenye busara na mabikira watano wapumbavu hakika hawawakilishi idadi ya watu, wala hawawakilishi watu wa aina moja mtawalia.

10.25.2019

Kwa nini Mungu hawaokoi wale wanaofanyiwa kazi na pepo wabaya na wale waliopagawa?

Kwa nini Mungu hawaokoi wale wanaofanyiwa kazi na pepo wabaya na wale waliopagawa?

Maneno Husika ya Mungu:
Wale ambao walipagawa na roho wabaya hapo zamani (tangu kuzaliwa) watafichuliwa sasa. Nitakufukuza nje! Je, bado unakumbuka yale ambayo Nimeyasema? Mimi—Mungu mtakatifu na Asiye na waa—Siishi katika hekalu chafu na la kuchukiza. Wale ambao walikuwa wamepagawa na roho wabaya wanajua wenyewe, na Sihitaji kufafanua. Sijakujaalia! Wewe ni Shetani mkongwe, ilhali unataka kupenya katika ufalme Wangu! Hasha!

Kuna tofauti zipi kati ya kazi ya Roho Mtakatifu na kazi ya pepo wabaya?

Maneno Husika ya Mungu:
Lazima uelewe ni mambo yapi yanatokana na Mungu ni mambo yapi yanatokana na Shetani. Mambo yanayotokana na Mungu hukusababisha kuwa wazi zaidi kuhusu maono, na hukusababisha kusogea karibu na karibu zaidi na Mungu, ukishiriki upendo na ndugu kwa bidii; unakuwa na uwezo wa kutilia maanani mzigo wa Mungu, na moyo wako umpendao Mungu haupungui; kuna njia mbele yako kuitembea.

10.24.2019

Kazi ya pepo wabaya ni nini? Kazi ya pepo wabaya hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Ni kazi ipi hutoka kwa Shetani? Katika kazi inayotoka kwa Shetani, maono ndani ya watu si yakini na ni dhahania, na hawana ubinadamu wa kawaida, motisha za vitendo vyao si sahihi, na ingawa wanataka kumpenda Mungu, daima kuna lawama ndani yao, na lawama hizi na fikira daima zinaingilia katindani yao, zikizuia kukua kwa maisha yao, na kuwasitisha kuwa na hali za kawaida mbele ya Mungu. Ambayo ni kusema, punde tu kuna kazi ya Shetani ndani ya watu, mioyo yao haiwezi kuwa kwa amani mbele ya Mungu, na hawajui cha kufanya, kuona mkutano kunawafanya kutaka kuhepa, na hawawezi kufumba macho yao wakati wengine wanaomba.

10.23.2019

Mtu anawezaje kupata kazi ya Roho Mtakatifu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu inabadilika kutoka siku hadi siku, ikipanda juu kwa kila hatua; ufunuo wa kesho unakuwa hata juu kuliko wa leo, hatua kwa hatua ukikwea hata juu zaidi. Hii ndiyo kazi anayotumia Mungu kumkamilisha mwanadamu. Iwapo mwanadamu hawezi kwenda sambamba, basi anaweza kuachwa nyuma wakati wowote. Kama mwanadamu hana moyo wa kutii, basi hawezi kufuata hadi mwisho. Enzi ya kale imepita; hii ni enzi mpya. Na katika enzi mpya, kazi mpya lazima ifanywe.

Kupagawa ni nini? Kupagawa hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Je, unajua una nafsi za aina gani? Je, una uwezo wa kuhisi nafsi yako? Unaweza kugusa nafsi yako? Je, unaweza kuhisi roho yako inafanya nini? Hujui, siyo? Kama unaweza kuhisi au kugusa kitu fulani kama hicho, basi ni roho mwingine aliye ndani yako akifanya kitu kwa nguvu—akikufanya utende na kusema vitu. Hilo ni jambo lililo nje yako, lisilo la asili kwako. Wale wenye pepo mbaya watakuwa na ufahamu wa kina wa hili.

10.22.2019

Kazi ya Roho Mtakatifu ni nini? Kazi ya Roho Mtakatifu hudhihirishwaje?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya Roho Mtakatifu ni aina ya mwongozo wa kimatendo na kupata nuru kwa hali nzuri. Haiwaruhusu watu kuwa baridi. Huwaletea faraja, huwapa imani na uamuzi na kuwawezesha kufuatilia kufanywa kamili na Mungu. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wanaweza kuingia kwa vitendo; wao si baridi wala hawalazimishwi, lakini ni wa kimatendo. Wakati Roho Mtakatifu hufanya kazi, watu wana faraja na wenye radhi, na wako tayari kutii, na wana furaha kujinyenyekeza, na hata ingawa wana maumivu na ni dhaifu ndani, wana uamuzi wa kushirikiana, wanateseka kwa furaha, wanaweza kutii, na hawajatiwa doa na mapenzi ya mwanadamu, hawajatiwa doa na fikira ya mwanadamu, na hakika hawajatiwa doa na tamaa na motisha za mwanadamu.

10.21.2019

Kuna tofauti ipi kati ya mtumishi mwema na mtumishi muovu?

Maneno Husika ya Mungu:
Kazi ya mtenda kazi mwenye sifa inaweza kuwaleta watu katika njia sahihi na kuwaruhusu kuzama kwa kina katika ukweli. Kazi anayofanya inaweza kuwaleta watu mbele ya Mungu. Aidha, kazi anayofanya inaweza kutofautiana kutoka kwa mtu hadi mtu mwingine na wala haifungwi na kanuni, inawapa watu uhuru. Aidha, wanaweza kukua katika uzima kwa taratibu, wakiendelea kukua na kuzama ndani kabisa katika ukweli. Kazi ya mtenda kazi asiyehitimu haifikii kiwango hiki; kazi yake ni ya kipumbavu.

10.20.2019

Kuna tofauti ipi kati ya ngano na magugu?


Maneno Husika ya Mungu:
Kama Nilivyosema, Shetani amewatuma wale ambao wananifanyia huduma kuukatiza usimamizi Wangu; hawa watendaji huduma ni magugu, lakini ngano hairejelei wazaliwa wa kwanza, lakini badala yake wana wote na watu ambao si wazaliwa wa kwanza. Siku zote ngano itakuwa ngano, siku zote magugu yatakuwa magugu; hii ina maana kwamba asili ya wale wa Shetni haiwezi kubadilika kamwe. Kwa hiyo, kwa ufupi, wao wanabaki kama Shetani. Ngano inamaanisha wana na watu, kwa sababu kabla ya kuumbwa ulimwengu Niliwaongezea watu hawa sifa Yangu.