Wakati huo, wakati Bwana Yesu alikuja kufanya kazi Yake, Mafarisayo Wayahudi walimkana na kumhukumu Yeye vikali na kumtundika msalabani. Mwenyezi Mungu wa siku za mwisho anapokuja kufanya kazi Yake, wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa pia wanamkana Yeye vikali na kumhukumu Yeye, wakimtundika Mungu msalabani tena. Kwa nini Mafarisayo Wayahudi na wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa huuchukia ukweli hivyo na kumpinga vikali Kristo kwa njia hii? Ni nini hasa kiini chao cha asili?
Jibu:
Kila mtu anayeamini katika Bwana anajua Mafarisayo waliompinga Bwana Yesu, lakini mzizi, asili ya kweli ya upinzani wao ilikuwa nini? Unaweza kusema kwamba katika historia ya dini ya miaka 2,000, hakuna mtu aliyeelewa jibu la swali hili. Ingawa kulaani kwa Bwana Yesu kwa Mafarisayo kuliandikwa katika Agano Jipya, hakuna mtu ambaye ameweza kumaizi asili ya Mafarisayo. Mwenyezi Mungu anapowasili katika siku za mwisho, Anafichua jibu la kweli kwa swali hili. Hebu tusome maneno ya Mwenyezi Mungu, “Je, mngependa kujua kiini cha sababu ya Mafarisayo kumpinga Yesu? Je, mnataka kujua dutu ya Mafarisayo? Walikuwa wamejawa na mawazo makuu kuhusu Masiha. Kilicho zaidi, waliamini tu kuwa Masiha angekuja, ilhali hawakutafuta ukweli wa uzima.