Unashuhudia kuwa Bwana Yesu amekwisha kurudi kama Mwenyezi Mungu, kwamba Yeye huonyesha ukweli wote ambao utawawezesha watu kupata utakaso na kuokolewa, na kwamba sasa Anafanya kazi ya hukumu kuanzia na nyumba ya Mungu, lakini hatuthubutu kukubali hili. Hii ni kwa sababu wachungaji wa kidini na wazee wa kanisa mara nyingi hutufundisha kwamba maneno na kazi zote za Mungu zimeandikwa katika Biblia na hakuwezi kuwa na maneno mengine au kazi ya Mungu nje ya Biblia, na kwamba kila kitu kinachoipinga au kwenda zaidi ya Biblia ni uasi. Hatuwezi kulitambua tatizo hili, kwa hivyo tafadhali unaweza kutueleza kulihusu.
Jibu:
Aina hii ya mtazamo kutoka kwa jamii ya dini haitokani na neno la Mungu; ilikuja hasa kama matokeo ya kufasiriwa vibaya kwa Biblia. Biblia inashuhudia hatua mbili za kwanza za kazi ya Mungu; hii ni kweli. Hata hivyo, kiandikwacho katika Biblia kina mipaka, na ndani yake hamna maneno yote aliyoyanena Mungu katika hizo hatua mbili za kazi Yake na ushuhuda wote kuhusu kazi hiyo. Kutokana na kuachwa maneno na migogoro miongoni mwa wakusanyaji wa Biblia, baadhi ya utabiri wa manabii, uzoefu wa mitume na ushuhuda wao uliachwa nje; huu ni ukweli unaotambuliwa.